You are on page 1of 5

BIASHARA YA KUSINDIKA MAHINDI

🔴UTANGULIZI

Biashara hii ni miongoni mwa biashara zenye uhitaji wa mtaji wa wastani kuianzisha kwani
huhitaji utengenezaji wa kiwanda kidogo kwa shughuli za uchakataji, upakiaji na usambazaji wa
bidhaa. pia ni miongoni mwa biashara zitoazo faida kubwa na ya haraka.

💚matumizi ya unga wa mahindi

➡Hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile ugali, uji, togwa na vyakula vya watoto.

➡Pia huchanganywa na shayiri na kutengeneza vinywaji kama vile bia.

🔴ORODHA YA BEI ZA MASHINE ZA KUKOBOA & KUSAGA MAHINDI

Bei za mashine hutofautiana kulingana na aina ya kinu kinachotumika na uwezo wa mashine


kusaga kiasi cha mahindi kwa saa.
VINU VYA KUSAGA;

👉Saizi25 - 1,800,000 KG250 kwa saa, MOTA hp10.

👉Saizi50 - 2,800,000 KG500 kwa saa.MOTA hp20.

👉Saizi75 - 3,500,000 KG750 kwa saa,MOTA hp30.

👉Saizi100 - 4,000,000 KG1,000 kwa saa.MOTA hp40.

VINU VYA KUKOBOA;

👉Rola2 - 2,800,000 KG500 kwa saa, MOTA hp20.

👉Rola3 - 3,500,000 KG750 kwa saa, MOTA hp30.

👉Rola4 - 4,000,000 KG1,000 kwa saa, MOTA hp40.

(Pia vinavyotumia mafuta kwa ajili ya watu wa vijijini vipo.Tupo Vingunguti Estate, nyerere
road.+255 716 811 838 ).
🔴JINSI YA KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA

Kuna aina mbili za unga wa mahindi:-


1- Unga wa mahindi yasiyokobolewa (Dona)
2- Unga wamahindi yaliyokobolewa (Sembe)

💚VIFAA-- • Mashine ya kukoboa

• Mashine ya kusaga
• Ungo
• Debe
• Mifuko
• Chekeche ya nafaka
1.KUSINDIKA MAHINDI KUPATA UNGA WA DONA

👉JINSI YA KUSINDIKA

➡Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,
ungo au sinia.

➡Osha mahindi yako kwa maji safi na salama

➡Anika kwenye chekeche safi ili yakauke

➡Saga mahindi kupata unga

➡Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni, makaratasi yasiyopitisha


unyevu kisha hifadhi katika sehemu safi na kavu.
2.UNGA WA MAHINDI YALIYOKOBOLEWA (SEMBE)

👉JINSI YA KUSINDIKA

➡ Pepeta na pembua mahindi ili kuondoa vumbi na takataka nyingine kwa kutumia chekeche,
ungo au sinia

➡Koboa na saga

➡Fungasha kwenye mifuko safi na kavu ya pamba, plastiki/nailoni na ya karatasi isiyopitisha


unyevu.
➡Hifadhi kwenye sehemu safi na kavu

🔴MAKADIRIO YA FAIDA

Ukishaweka mashine na zana zote kuchakata mahindi.

👉Debe moja la mahindi hutoa kilo 20 had 24 za unga.

👉 Gunia la kilo kg100 lina debe tano (5) = kilo 100 hadi kilo 120 za unga.

👉 Kikawaida mahindi huuzwa kati ya sh.45,000 had sh.67,000 kutegemeana na mazingira husika.

👉 Na unga bei ya kawaida kilo ni sh.1200

👉 So. gunia (kilo 100 --> 120) litakupa wastani wa sh.120,000 --> 144,000.

KWA GUNIA MOJA LA MAHINDI UTAPATA WASTANI WA FAIDA SH.80,000 HADI


100,000.

🔴KUMBUKA

Isajili.bidhaa yako kwa mamlaka.husika na lipia sido upate kutengenezewa vifungashio kwajili
ya bidhaa yako.
Imetayarishwa na Mwl. Aloyce Kandonga
Follow instagram: sed20.19
#SED4LYF
by @sharak

Man Ngege
Hakuna vitu vya kuweka kwenye unga ili kuongeza ubora
48w
Reply
Mayanga Mahugija
Nategemea mwezi huu kununua Kinu sb50 na Mota HP 40 no shilingi ngapi 0719767780
3y
Reply
Daniel Patrick
Mwl Aloyce kunakitu umekosea naomba kurekebishwa kama nitakua nimesema uongo. Gunia la
kilo mia za mahindi haziwezi kutoa kilo 100 achana na 120 uliyo andika. Debe moja la mahindi
kina kilo 16-18 inategemea na mbegu husika. ukikoboa gunia la kilo 100 unapata unga kilo 68-
73 inategemea na kinu cha kukoboa. Hivyo basi kwenye kila gunia toa gharama za usafiri na
mifuko, umeme , wafanyakazi kuna faida ya 7000 tu
3y
Reply
Real Profesa Ndyamukama
Nataka nifungue mradi huu ifikapo mapema January 2021

You might also like