You are on page 1of 35

1

UTANGULIZI

Kwanza kabisa namshukuru Mungu Kwa kuniwezesha kuandika kitabu hiki chenye kumsaidia mtu
yoyote kuweza kujiandalia aina ya chakula akipendacho Kwa msaada wa maelekezo yaliyo kwenye
kitabu hiki.

Pia namshukuru mama yangu mzazi Magreth Mhagama,mashabiki na wadau wote wa instagram
katika page ya jifunze kupika,familia yangu, marafiki, na wadau mbalimbali kuweza kuchangia kwa
namna moja ama nyingine kukamilisha kitabu hiki cha toleo la pili.

Bila kusahau hoteli, migahawa, watu na wapishi mbalimbali kuweza kutoa mchango mkubwa wa
kutoa mbinu na siri mbalimbali za kuhusu vyakula, vitafunwa na vinywaji mbalimbali.
Mashabiki wote wa instagram ambao ndio mmekua nguzo kubwa ya kunipa moyo kuendelea na kazi
hii ya kutoa huduma ya maandalizi ya vyakula kwa jamii nawashukuru mno.

Kwa makundi mengine mengi siwezi kuwataja kwa mmoja mmoja kwa sababu ya uwingi
nawashukuru sana kwa mchango wenu mkubwa sana mliojitoa kufanikisha kitabu hiki na
kuwashukuru kwa kusema asante na Mungu awabariki sana.

Natumaini mtafurahia hili toleo la pili huku matoleo mengine yakifuata baada ya hili na Mungu
awabariki sana.

Mawasiliano:

Instagram; Jifunze_kupika

2
YALIYOMO
1.DAGAA LA KUKAANGA NA KABICH (cabbage) .........................................................................4
2.VILEJA VYA TENDE........................................................................................................................4
3.WALI WA NAZI NA MAHARAGE ..................................................................................................5
4.COCONUT CAKE (cake ya nazi).......................................................................................................6
5.KUKU MZIMA WA KUOKA............................................................................................................7
6.MEAT SACK (VIFURUSHI VYA NYAMA) ....................................................................................8
7.KASHATA ZA KOROSHO ...............................................................................................................9
8.PILAU YA SAMAKI (TUNA) .........................................................................................................10
9.SAMAKI WA KUPAKA ..................................................................................................................11
10.VIAZI /POTATOES ZA ROAST ...................................................................................................12
11.MKATE WA MAYAI.....................................................................................................................13
12.KABABU ZA NYAMA..................................................................................................................15
13.SIMPLE RICE ................................................................................................................................16
14.KUKU NA ROAST LA UKWAJU .................................................................................................17
15.FRUIT CUSTARD..........................................................................................................................18
16.PILAU YA KUKU (NYEUPE).......................................................................................................19
17.KUKU WA TOMATO KETCHUP ( tomato sauce) .......................................................................20
18.NYAMA .........................................................................................................................................21
19.VILEJA VYA NJUGU....................................................................................................................22
20.EGG CHOP .....................................................................................................................................23
21.PWEZA ...........................................................................................................................................24
22.DOUGHNUTS(donaz) ....................................................................................................................25
23.MANGO AND STRAWBERRIES JELLY.....................................................................................26
24.NYAMA NA KABICH ...................................................................................................................27
25.VIAZI/MBATATA ..............................................................................................................................28
26.NDIZI ZA KUKAANGA (PLANTAINS) ......................................................................................29
27.CHICKEN BREAD.........................................................................................................................30
28.PIZZA AINA YA KWANZA .........................................................................................................32
29.PIZZA AINA YA PILI....................................................................................................................33
30.JUICE YA EMBE, PASSION, NANASI NA NDIZI......................................................................34

3
1.DAGAA LA KUKAANGA NA KABICH (cabbage)
MAHITAJI
Madagaa mabichi 1/2 kg
Kabich (cabbage) 1/2 (likate kate)
Nyanya tomatoes 3-4 kubwa
Carrots 1-2 (kata vipande vidogo vidogo)
Chumvi kiasi
Mafuta ya kupikia

MATAYARISHO

Safisha dagaa na uchuje maji yote halafu ukaange ikiiva na kukauka weka pembeni.kata nyanya
(tomatoes )ukipenda toa maganda. Weka sufuria kwenye jiko tia mafuta ya kupikia vijiko 3 vya
chakula (tblsp). Kaanga nyanya kwa dakika kama 2 zilainike tu.

Weka kabich na carrots na chumvi kwenye nyanya, kaanga mpaka iwe kavu. Ikiwa kavu kaanga kwa
dakika kama 1. Halafu changanya na dangaa zilizokaangwa.onja kama kila kitu kiko sawa tayari kwa
kuliwa na wali au ugali.

2.VILEJA VYA TENDE


MAHITAJI
unga wa ngano 1 1/4 cups
Mayai 3
Siagi(butter) 1/2 cup
Sukari iliosagwa (castor sugar/icing sugar) 1/2 cup
Corn starch(corn flour) 1 cup
Custod 3/4 cup
Nazi chicha (desicated coconut) kiasi

4
Arki vanilla 1 tsp
Nido (milk powder) 3tbsp
Baking powder 3/4 tsp
Samli (ghee) 1 tbsp
Tende kiasi
Ufuta 1 tbsp
Samli 1 tsp
Chocolate (kama ukiamua)

JINSI YA KUTENGENEZA

Chukua tende itowe kokwa itie samli 1tsp na ufuta uivuruge mpaka ichanganyike vizuri ifanye
vidonge vidogo vidogo iweke pembeni (au unaweza kuchukua tende uitowe kokwa kisha uweke
kipande cha chocolate kati).
Kwenye chombo saga sukari na siagi na samli 1 tbps kwa hand mixer mpaka ilainike vizuri tia viini
vya mayai (egg york) yote matatu weka ute (egg white) pembeni endelea kusaga kidogo mpaka
yachanganyike tia custod powder ,corn starch, decicated coconut 1 tbsp, nido ,arki na baking powder
endelea kusaga zaidi kidogo kisha tia unga kidogo kidogo uwe unachanganya kwa mkono mpaka uwe
donge liwe soft (kama limekua soft kabla hujaumaliza unga si lazima uingie wote unga ukiwa mwingi
sana vitakua vigumu).
Fanya vidonge vidogo vidogo viwe na shape ya yai kati tia kidonge cha tende uloitengeneza, kisha tia
kimoja kimoja kwenye ute wa yai kitowe kitie nazi (decicated coconut) kama unavyoona picha weka
kwenye treya choma kwa oven 160°c kwa dakika 15.

3.WALI WA NAZI NA MAHARAGE

MAHITAJI
mchele vikombe 2
Mafuta ya kupikia 2 tblsp
Chumvi kiasi
Maharage yalochemshwa 1/2 kikombe (siolazima maharage)
Tui la nazi vikombe 5 ( kikombe ulopimia mchele ndio upimie tui)

MATAYARISHO

5
Osha mchele uroweke kwa nusu saa.kwenye sufuria tia tui la nazi chumvi na mafuta. Weka kwenye
jiko moto mkubwa, mpaka lichemke. Usiende mbali lisije kumwagika.
Likiaza kuchemka tia mchele changanya, acha uive karibu ya kukauka maji tia maharage. Changanya
mpaka chini kwenye dish wali usiunguwe.

Ukikauka either utie kwenye oven or ufunike uwache na moto mdogo mdogo sana uzidi kukauka na
kuiva vizuri.halafu tayari kwa kuliwa.

4.COCONUT CAKE (cake ya nazi)


MAHITAJI:
Siagi 250gm
Sukari ilosagwa 250gm
Unga wa ngano 300gm
Mayai 4
tui la nazi 1/2 kikombe
Baking powder 1 1/2 tsp
vanilla kijiko 1 tsp
Sukari ilosagwa 2 tblsp
Whipping cream kikopo kimoja
Nazi ya machicha kikombe 1

MATAYARISHO:

Saga siagi na sukari kwa mashine (hand mixer) mpaka ilainike iwe kama cream (dakika 10) , tia yai
moja moja na saga kila yai lisagike vizuri.
Tia bakingpowder , arki na tui la nazi, saga kidogo kisha zima mashine.

Chekecha unga mara tatu (ukiuchekecha mara 3 unafanya cake iwe laini zaidi). Mimina unga nusu
kwenye siagi ilosagwa changanya kwa mwiko ukisha kuchanganyika tia unga ulobaki.
Changanya vizuri. Tia kwenye tray na choma kwenye oven nyuzi joto 150 au moto wa kati. Mpaka
cake iive .
Itoe na iache ipoe kabisa iwe baridi. Chukuwa zile chicha nusu zitie kwenye frying pan ilokuwa kavu

6
weka juu ya jiko zi roast mpaka ziwe golden colour. Ziache zipoe kisha changanya na zile chicha
zilobaki nyeupe hivi utapata rangi mbili kama hapo kwenye cake yetu.

Tia whipping cream kwenye bakuli pamoja na sukari ilosagwa, mix kwa mashine au kwa mkono
mpaka iwe crem nzito.toa cake weka kwenye sahani ikate pembeni kama unapenda ipakae ile cream
cake yote halafu weka chicha juu ya cream tayari kwa kuliwa .

5.KUKU MZIMA WA KUOKA


MAHITAJI
Kuku mzima 1 (me nimetoa ngozi pia unaweza kumfanya na ngozi yake kama unapenda)
Tandoori masala 1tbsp
Bizari ya manjano 1tsp
Bizari nzima powder 1 tsp (cummin powder)
Curry powder 1tbs
Black papper 1tbs
Chilli powder size unopenda
Olive oil 1 tbsp (au mafuta yoyote)
Yogurt 4 tbsp
Ndimu size unopenda
Kitunguu thom 1 tsp (garlic)
Tangawizi 1 tsp (gigger)

JINSI YA KUTENGENEZA

Changanya vitu vyako vyote kwenye kibakuli.muweke kuku wako kwenye sahani fanya kumchana
chana baadhi ya sehemu kwa kisu ili upitishe spice mpaka ndani. Sasa anze kumpaka huo
mchanganyiko kwa mkono usisahau kupitisha mchanganyiko mpaka ndani sehemu ulozichana kwa
kisu.

7
Ukisha kuhakikisha kuku wote kaenea mchanganyiko wako vizuri sana mfunike kwa foil au kitu
chochote umuache aloane kwa muda wa masaa 3 au hata zaidi sio mbaya.

Ukimaliza paka mafuta trey yako ya kuchomea muweke kuku wako na rojo lake lote.washa oven yako
moto 180 mchome ukiona anapiga rangi sana juu punguza moto umuache mpaka aive vizuri unaweza
kumuangalia kama kashaiva mpaka ndani kwa kupenyeza kisu unafanya kama unamnyambua hivi
kidogo.akisha iva mtoe kwenye oven weka kwenye sahani yako tayarisha salad kama unapenda.

6.MEAT SACK (VIFURUSHI VYA NYAMA)


MAHITAJI
nyama ya kusaga 1/4
Njegere 1/2 kikombe
Bizari nzima ( cumin ) 1 tsp
Chumvi kiasi
Pilipili manga 1 tsp
Kitunguu maji 1 kikubwa (chopped)
Tangawizi mbichi 1 tsp
Kitunguu thaum 1
Butter iloyayushwa 2 tblsp
Sambusa pastry zilokaa square.

MATAYARISHO

Chemsha nyama pamoja na tangawizi , chumvi, pilipili manga, kitunguu thoum na bizari nzima tia na
maji nusu kikombe.iache mpaka iive ikiwa karibu ya kukauka maji tia njegere na vitunguu maji.acha
ikauke iwe kavu kabisa kisha weka pembeni ipoe.

Chukua tray pakaa butter kisha chukua pastry kata squre kunja (ile butter iliyoyayushwa inatumika
hapa kwenye kukunja) ukisha kunja zipange kwenye tray. Zitie kwenye oven (bake ) mpaka ziwe

8
golden colour tayari kwa kuliwa.

7.KASHATA ZA KOROSHO
MAHITAJI
Korosho (cashews) 1 cup
Nido 2 tbsp
Maji (water) 5tbsp
Sukari 1/2 cup
Hiliki (cadamon powder) 1/4 tbsp
Samli 1 tsp

JINSI YA KUTENGEZA

Zisage korosho kwa blender ziwe unga zichanganye na hiliki na nido ziweke pembeni.Weka kikaango
kwenye moto wa kiasi (au chombo chochote ambacho kitafaaa) tia sukari na maji ikoroge ili sukari
iyayuke mpaka ifanye mapovu ,usiiache mpaka ikaanza kunata, tia unga wako wa korosho uikoroge
uwe unaiponda ponda ili isiwe na madonge, ikoroge mpaka uone inaanza kua haigandi kwenye chuma
kisha endelea kukoroga wakati ipo kwenye moto kwa dakika 1, kisha itie kwenye sahani uloipaka
samli kidogo ili isigande.
Iache ipoe mpaka uwe unaweza kuikamata, uikande kama chapati (itakua kama unga wa chapati
ulokandwa).Ipake samli kwenye sehemu yako unayokandia chapati (kama unatumia kibao au kwenye
meza unaweza kuweka baking paper) weka donge lako lieneze vizuri kwenye rolling pin (pia ipake
samli isigande) kisha zikate size unayotaka kama unavyoona kwenye picha.Ziache zipoe enjoy kwa

9
coffee (Unaweza ku double ingredients ukapata nyingi zaidi).

8.PILAU YA SAMAKI (TUNA)


MAHITAJI YA SAMAKI
Samaki vipande 5 (unaweza kufanya idadi unayopenda)
Kitunguu thom 1tsp (garlic)
Tangawizi 1tsp ( gigger)
Bizari nzima powder 1tsp (cummin powder)
Pilipili manga powder 1 tsp( black papper)
Chilli powder unayopenda
Mafuta
Chumvi ya size
Ndimu ya size

MAHITAJI YA PILAU
Mchele 2 mug (mug cup/kwa jina lingine kombe kubwa)
Vitunguu maji 7 medium size (chopped)
Bizari nzima powder 1 tsp
Bizari nzima 1 tbsp (whole cummin)
Masala ya pilau 1 tsp
Karafuu chembe 5
Mbatata 3 medium size zikate mara mbili kila moja
Mafuta 8 tbsp
Chumvi ya size
Hiliki powder 1 tsp (cardamom powder)
Maji 2 1/2 mug ( yawe yamoto)
Mdalasini vijiti 3

MATAYARISHO

10
Kwanza osha mchele wako vizuri loweka na maji.Mchanganye samaki wako na vitu vyote isipokuwa
mafuta mueke pembeni.Sasa kaanga vitunguu vyako mpaka viwe brown colour viweke pembeni
Kaanga mbatata zako weka pembeni pia kaanga samaki wako waeke pembeni.

Kwenye fraying pan tupu weka bizari nzima ( whole cummin) zichome bila kutia mafuta mpaka zipige
rangi kidogo toa weka pembeni.

Sasa tenga sufuria yako kwenye moto weka mafuta yako 8 tbsp yakipata moto kidogo weka spice zako
zote zikaange kidogo hakikisha zisiungue kama sekunde20,weka whole cummin yako uloichoma
chota vitunguu ulivokaanga kama 2 tbsp weka ndani yake changanya tumia akili vitu visiungue.

Weka maji yako zile mug 2 1/2 yawe teyari yamoto weka chumvi ya kiasi chako.Sasa acha yachemke
tena vizuri mwaga maji mchele wako mimina changanya vizuri mpaka maji yote yakauke funika na
foil au ufuniko weka kwenye oven moto 140 mpaka uive.

Toa pilau yako pakuwa kwenye trey au bakuli kigodo kidogo huku unauchanganya na vitunguu vyako
ulivokaanga ukimaliza weka samaki wako juu na mbatata zako ufunike vizuri kama kwa dakika
10.Sasa weka kwenye sahani yako tayari kwa kuliwa na salad, kachumbari, au pilipili.

9.SAMAKI WA KUPAKA
MAHITAJI
Samaki 1 (mkubwa kiasi)
Tangawizi 1 tsp
Kitunguu saumu (darlic) 1tsp
Chumvi kiasi
Ndimu 2 tbsp

11
Bizari nzima (cumin powder)
Pilipili (chilli) kiasi
Mafuta 2tbsp (For coconut sauce)
Tui la nazi zito(coconut milk) 1 mug
Tungule/nyanya (tomatoes) nusu
Kitunguu maji nusu
Kitunguu saumu (garlic) 1 tsp Ukwaju
(tamarind paste) 3tbsp Tungule ya
kibati (tomato puree) 1 tsp Chumvi
kiasi
Ndimu (lemon juice) kiasi
Bizari nzima (cumin powder) 1tsp
Mafuta 3tsp
Bizari manjano (termeric powder) 1tsp

JINSI YA KUTENGENEZA

Msafishe samaki na umueke mipasuo juu (ili akolee vizuri) kisha mchanganye na vitu vyake
nilivyoviweka kwenye mahitaji , mueke kwa saa moja aingie spices vizuri.Weka kwenye blender
tomato, kitunguu, garlic, tomato puree na cumin usage mpaka visagike vizuri.
Weka mafuta kwenye chombo weka kwenye moto yakipata tia hivyo vitu ulivovisaga kwa blender
vikaange kidogo kisha weka tui la nazi na bizari na manjano chumvi kiasi na ukwaju ukoroge ili tui
lisikatike likianza kua zito kidogo weka ndimu uonje chumvi (usisahau kua samaki ana chumvi pia
hivyo weka kwa kiasi) hapo usiache mpaka likawa zito sana sababu ukilitoa kwenye moto litazidi kua
zito, epua weka pembeni.
Mchome samaki wako pande zote mbili kwa joto 200°c mpaka apige rangi juu asiungue (utatumia
dakika 10 mpaka 15 kuchoma kila upande wa samaki inategemea na ukubwa wa samaki)
Ukimaliza kumchoma mueke kwenye trey umtie ile sauce ya nazi kila upande mchome tena kwa
dakika 5 kila upande (weka sauce kidogo pembeni kwa ajili ya kula na wali au mkate).

10.VIAZI /POTATOES ZA ROAST


MAHITAJI
viazi ulaya (potatoes) 1/2 kg Bizari
ya njano (turmeric) 2 tsp Bizari
nzima (cumin powder) 1 tsp
Pilipili manga (black pepper) 1tsp
Tangawizi mbichi (fresh ginger) 1 tsp
Kitunguu thaum (garlic) 1tsp

12
Kitunguu maji (onion) 2 vikubwa. (Chopped)
Chumvi (salt) kiasi
Limau (lemon)
Mafuta ya kupikia (cooking oil)
Maji glass 1-2
Majani Giligilani (coriander leave) ukipenda

MATAYARISHO

Kaanga vitunguu mpaka viwe vyekundu (kumbuka vitunguu ukivitoa kwenye mafuta vinaendelea
kuiva) kwaiyo viweke pembeni.

Menya viazi halafu kata size ndogo ndogo.Osha na maji kisha kausha ziwe kavu.Zichanganye na
bizari, pilipili manga, tangawizi, kitunguu thaum na bizari nzima, mix vizuri. Weka mafuta (tumia
mafuta ulokaangia vitunguu) vijiko 4 vya kulia kwenye sufuria, halafu weka kwenye moto yakipata
moto tia viazi ulivochanganya na spices.

Pika kwa dakika 2 uwe unakoroga visigande. Halafu tia maji glass moja kubwa. Acha vichemke kwa
moto wa kati usifunike. Maji yakishakukauka tizama kama vimeiva tia vitunguu vilivyokaangwa.
Kama havijaiva ongeza maji nusu glass au maji unayo ona yataivisha. Halafu tia vitunguu,Mix vizuri
acha kwenye jiko na moto mdogo mdogo kwa dakika 2 weka chumvi na limau. Onja kama kila kitu
kiko sawa tayari kwa kuliwa na wali, ugali, chapati au mkate.

11.MKATE WA MAYAI
MAHITAJI
mayai 5
Unga wa ngano 300 gm
Sukari 200 gm/ 1/4 kg
Hiliki 1/2 tsp

13
Baking powder 2 tsp

MATAYARISHO

Changanya unga na baking powder halafu chunga/chekecha mara tatu.Weka pembeni.


Pakaa butter kwenye tray halafu tia unga mkavu izungushe tray ili unga ugande mule kwenye butter.
Halafu mwaga unga ulobaki hii inafanya mkate usigande kisha Weka pembeni.

Piga mayai sukari na hiliki, kama unatumia mashine full speed kwa dakika 5 mpaka 10.
Kama unatumia mkono piga mpaka mayai yawe mapovu na yawe mara 4 yake Yavimbe.

Mayai yakiwa tayari zima machine tia unga nusu mix kwa mwiko wa mbao au plastic, ukichanganya
changanya kidogo kidogo ( folding) kama kwa mfano unaogopa yale mayai yasijirudi.
Halafu malizia na nusu ya unga wako changanya kidogo kidogo (usikoroge kama unapika uji). Usijali
ukiona kama kuna vidonge viwili au vitatu vya unga utaondoka ukipambia.

Ikiwa umechanganyika mimina kwenye tray weka kwenye cooker kati moto wa kati. Ukiiva tayari
kwa kuliwa

14
12.KABABU ZA NYAMA
MAHITAJI
Nyama ya kusaga 1/2 kilo
Tangawizi mbichi ilosagwa 1 tsp (gigger)
Kitunguu thomu kilosagwa 1tps ( garlic)
Bizari nzima powder 1/2 tsp (cummin powder)
Bread crumbs 2 tbsp (chenga za mkate)
Pilipili ya kuwasha 1 au size unopenda mwenyeo ( isage)
Mafuta ya kuchomea
Chumvi kiasi
Pilipili manga 1/2 tsp (black papper)
Kitunguu maji 1 kidogo ( chopped km cha sambusa)
Yai 1

JINSI YA KUTENGENEZA

Osha nyama yako vizuri ichuje maji yote ichanganye na vitu vyote isipokuwa mafuta na yai iache
kama nusu saa.
Sasa fanya katika shape yako kisha weka mafuta yako yapate moto vizuuri .piga yai lako kwenye
kibakuli chovya nyama yako na yai choma mpaka zipige rangi vizuri toa weka kwenye sahani uloweka

15
kitchen tissue zijichuje mafuta.panga kwenye sahani yako tayari kwa kuliwa.

13.SIMPLE RICE
MAHITAJI
mchele kikombe 1
Mafuta kijiko cha kulia 2
Chumvi kiasi
maji kikombe 1 na 1/2 mpaka viwili inategemea na mchele utakao tumia, lakini kwa basmat rice
kimoja na nusu kinatosha. Hakikisha kikombe utakachopimia mchele ndio utumie kupimia maji.

MATAYARISHO

16
Uoshe mchele mpaka maji yawe safi.Tia mchele kwenye dish pamoja na maji na chumvi. Tia chumvi
kidogo kidogo kila ukiweka chumvi mix hakikisha chumvi imeyayuka halafu onja kama iko sawa
kabla hujaongeza. Ikiwa kidogo ongeza kama ni nyingi mwaga maji weka mengine.

Ikishakuwa chumvi iko sawa weka mafuta halafu mix vizuri.Weka juu ya jiko na moto mkubwa
funika uache uchemke kwa dakika 2 kisha mix tena.acha mpaka ukaribie kukauka ufunuwe ukoroge
usije kuganda na kuungua.

Ikisha kauka unaweza kutia kwenye oven ikakauka au punguza moto uwe mdogo sana funika mpaka
ikauke vizuri na iive. Tayari kwa kuliwa.

14.KUKU NA ROAST LA UKWAJU


MAHITAJI
Kuku 1 (alokatwa vipande vya size)
Ukwaju mbivu 1/4 kg
Tomato ketchup (tomato sauce) 4 tblsp
Sukari 1tblsp
Chumvi kiasi
Tangawizi 1tsp
Pilipili manga 1 tsp
Kitunguu thaum 1 tsp
Nazi ya chicha (desiccated) 2 tblsp
Ufuta (sesame seeds) 1 tblsp
Giligilani ya kusaga 1 tsp
Bizari nzima ( cumin) 1 tsp
Nyanya tomatoes 2 kubwa (chopped)
Mafuta ya kupikia 5 tblsp

17
MATAYARISHO

Chemsha ukwaju uchuje upate juice nzito nusu kikombe.Changanya hiyo juice ya ukwaju ulopata na
tomato ketchup, chumvi, nazi, sukari, kitunguu thoum, tangawizi, pilipili manga, bizari nzima,
giligilani na ufuta. Changaya vizuri halafu mtie kuku mchanganye mpaka achanganyike vizuri. Mueke
upande akolee kwa nusu saa.

Weka dish kwenye jiko tia mafuta yakipata moto kaanga nyanya tomatoes kwa dakika 3 halafu tia
kuku pamoja na marinade (ile sauce ya ukwaju uloroekea). Mix vizuri halafu funika punguza moto
acha kuku aive. Usisahau kukoroga ili asiungue.Kuku akisha kuiva onja kama kila kitu kiko sawa
Tayari kwa kuliwa na wali, ugali, chapati ama maandazi.

15.FRUIT CUSTARD
MAHITAJI
maziwa ya maji kikombe kikubwa (mug) 1
Custard powder 2 tblsp
Sukari 3 tsp
Hiliki ilosagwa 1/2tsp
Fruits unazopenda mwenyewe, mimi nimeweka green grapes, mango na redcurrants.

MATAYARISHO

Changanya maziwa, sukari, hiliki na custard powder, mix mpaka custard powder iyayuke yote.Weka
kwenye dish halafu weka kwenye jiko moto wa kati huku unakoroga mpaka iwe nzito ( Koroga mpaka
chini isigande). Itizame ikiwa nzito sana ongeza maziwa na ikiwa nyepesi sana ongeza custard
powder. Inatakiwa iwe kama uji lakini kila ikipowa inakuwa nzito. Onja kama kila kitu kiko sawa.

Zima moto weka pembeni wacha ipowe halafu iweke kwenye friji.Ikiwa tayari unataka kula, kata

18
fruits zako vipande vidogo vidogo weka kwenye glass au kibakuli halafu mimina custard juu yake.

16.PILAU YA KUKU (NYEUPE)


MAHITAJI:
Mchele 1 1/4 mug
Kuku nusu
Mafuta 1/2 cup
Kitunguu maji 1 na nusu (midium)
Siagi 1 tsp
Tangawizi 1 tsp
Kitunguu saumu(garlic) 1 tsp
Bizari nzima (cumin seeds) 1tbsp
Mdalasini mzima 4 (cinammon)
Pilipili manga nzima (black papper) 1 tsp
Chumvi kiasi
Hiliki nzima(cadamon) 4
Hiliki ya unga 1/2 tsp
Viazi potetoes 2 (zikate mara mbili)

JUNSI YA KUTENGENEZA

Kosha mchele vizuri na uuroweke kwa saa moja.Mkate kuku vipande umchemshe na
tangawizi,chumvi na garlic akichemka mbakishe na supu iwe 1 1/2 mug (kama kuku mlaini
usimchemshe sana).
Kata kitunguu maji kama cha sambusa (chopped) weka mafuta na siagi kwenye dishi yakipata moto
kaanga vitunguu mpaka vilainike visipige rangi weka mbatata kaanga kidogo tia viungo vyote kanga
kidogo sana uhakikishe vitunguu havipigi rangi mtie kuku wako umchanganye kidogo kisha tia supu
uonje chumvi vizuri chumvi ikolee zaidi .

19
Supu ikichemka weka mchele wako weka moto wa size upike wali mpaka ukauke (uwe unaukoroga
usigande chini).
Kisha utie kwenye oven uuchome kwa 15 minutes (unaweza kuufunika ili usiungue juu).toa ukikauka
vizuri enjoy na salad.

17.KUKU WA TOMATO KETCHUP ( tomato sauce)

MAHITAJI
Kuku 1 (ila mimi nimetumia chicken's wings)
Plain yogurt (maziwa mgando/ mtindi) kikombe 1
Tangawizi ilosagwa 1ts
Kitunguu thaum 1 tsp
Pilipili manga 1 tsp
Rangi nyekundu (food colour) 1/ 2 tsp
Gilgilani ilosagwa 1 tsp
Tandoori masala 1 tsp.
Chumvi kiasi
Ndim au limau 1
Pilipili sauce (ile ya kula na chips) kiasi
Tomato ketchup/ tomato sauce (ile ya kula na chips 1/2 kikombe

MATAYARISHO

Msafishe kuku mkate size unayopenda kisha muache ajichuje maji awe mkavu.Kwenye bakuli kubwa
changanya yoghurt, pilipili manga, kitunguu thoum, tangawizi, Tanduri masala, rangi nyekundu na

20
giligilani usiweke chumvi. Mix vizuri halafu mtie kuku umchanganye na huo mchanganyiko mpaka
akolee.Kisha muweke kwenye friji usiku mzima au masaa 5.

Akisha kukolea mtowe kwenye friji, mtie chumvi halafu muache mpaka awe na joto lakawaida la
chumba.Halafu mchome kwa grill au makaa.

Akisha kuiva bado akiwa wamoto Mix tomato sauce, maji vijiko 2 vya kulia, ndim au limau na chilli
sauce pamoja mimina kwenye kuku mchanganye vizuri onja kama kila kitu kiko sawa Tayari kwa
kuliwa yaani ni mtamu utakula kama ile style ya wa Nigeria yaani mpaka mfupa utautafuna .

18.NYAMA
MAHITAJI:
Nyama kilo kasorobo (stek)
Pilipili hoho (mix capsicum) 1
Kitungu maji nusu (sliced)
Chumvi kiasi
Soy sauce / soya sauce1tbsp
Ndimu (lemon juice) 1 tbsp
Bizari nzima (cumin seeds) 1 tbsp
Pilipili manga nzima(black paper) 1tsp
Mafuta 3tbsp
Kitunguu Thomu (garlic paste) 1 tsp
Tangawizi 1tsp
Kotmiri/gilgilani (coriander) 1tbsp
Corn starch 1 tsp

JINSI YA KUTENGENEZA

Ikate nyama vipande vidogo vidogo itie tangawizi, garlic, chumvi, soya sauce , pilipili manga na
cumin (zitwange pamoja) uichemshe nyama yako mpaka iive kabla haijakauka vizuri tia ndimu na
corn starch (itie maji kidogo) tia na mafuta 2 tbsp iwache ikaangike kidogo weka pembeni.

21
Kwenye frying pan weka 1 tbsp mafuta ukaange kitunguu na capsicum zikipiga rangi kidogo
zichanganye kwenye nyama tia kotmiri juu,enjoy na nan bread au wali.

19.VILEJA VYA NJUGU


MAHITAJI

Siagi 3/4 cup


Unga 2 1/4 cup
Sukari 3/4 cup
Custord 2 tbsp
Jam ya size
Maziwa ya unga 2 tbsp (milk powder)
Baking powder 1/2 tsp
Mayai 3
Vanila 1 tsp
Njugu zilosagwa 1/4 cup ( zichome kwanza)

JINSI YA KUTENGENEZA
Kwenye bakuli weka sukari na siagi saga kwa mashine (hand mixer) mpaka vilainike viwe kama
cream.Weka viini vya mayai, ( ute utakuja kutumia baadae) saga tena vizuri Weka custord, baking
powder vanila na unga wa maziwa saga tena.Sasa weka unga wako kidogo kidogo huku unachanganya
kwa mkono mpaka upate donge.acha donge lako litulie kama dakika 10.

Kata unga wako vidonge vidogo vidogo.ukimaliza kufanya unga wote sasa vipake ute wa yai juu
baadae chukua kimoja kimoja kigaragize kwenye njugu zilosagwa ule upande ulopaka ute wa yai tu
kisha panga kwenye trey ya kuchomea ulopaka siagi au mafuta ukimaliza kufanya hivo vyote tumia
kidole chako cha shahada kufanya kitobo na uweke jam kwa kutumia kijiko kidogo.Choma kwenye
oven moto 150 c kwa dakika 15 -17 vikiwa tayari toa subiri vipoe kidogo weka kwenye sahani na

22
enjoy kwa juice, soda, chai ama coffe.

20.EGG CHOP
MAHITAJI
Mbatata (potatoes, viazi) 7 medium size
Siagi 1/2 tsp ( butter)
Milk 1/2 tsp
Kitunguu thom ( garlic) 1 tsp
Tangawizi (ginger) 1 tsp
Mafuta ya kuchomea kiasi
Chumvi kiasi
Ndimu kiasi
Mayai 6
Unga wa sembe kiasi
Pilipili ya kuwasha unayopenda

JINSI YA KUTENGENEZA
Chemsha mayai yako 4 yaki iva toa maganda weka pembeni.Menya mbatata zako kata vipande vya
size kosha vizuri zichemshe, zikiwiva mwaga maji yote weka kwenye bakuli wakati zikiwa zamoto
weka maziwa, na siagi ziponde kwa mwiko vizuri.

Weka vitu vyako vyote vilobaki kwenye mbatata zako isipokuwa yale mayai 2 yalobaki, unga wa
sembe na mafuta.Changanya vizuri onja chumvi na ndimu kama ipo sawa.Sasa chota mbatata zako
tandaza kwenye kiganja weka yai moja lifunike na mbatata vizuri utapata donge la duwara lenye yai
ndani.

Fanya hivo na mayai mengine ulochemsha ukimaliza yote chukua moja moja garagaza kwenye unga
wa sembe weka pembeni.Sasa weka mafuta yako yapate moto vizuri piga yale mayai yako 2 yalobaki
kwenye kibakuli.

Chukua donge lako moja moja ulokuwa ushatia unga wa sembe lichovye kwenye yai vizuri lienee
kisha tia kwenye mafuta yamoto acha kwa dakika 1 au 2 geuza upande wa pili acha pia kwa dakika

23
kama hizo litoe weka kwenye sahani uloweka kitchen tissue ijichuje mafuta Fanya hivo mpaka
umalize zote kisha acha zipoe na ukate katikati.

21.PWEZA
MAHITAJI
pweza 1 mkubwa
Kitunguu thaum ( garlic) 1tsp
Tangawizi 1 tsp
Pilipili manga 1 tsp
Limau au ndim 1
Pilipili mbuzi 1 ukipenda
Mafuta ya kupikia

MATAYARISHO

Msafishe na umkate vipande vikubwa vikubwa pweza wako. Mchuje maji yote.Weka pweza kwenye
dish pamoja na kitunguu thaum, tangawizi, pilipili manga na pilipili mbuzi.Weka kwenye kuka acha
achemke na maji yake, usiweke maji hata kidogo, mpaka aive vizuri.
Mtoe kwenye dish chuja maji.Weka mafuta kwenye frying pan kwa moto wakati mkaange pweza kwa
dakika kama 5 au mpaka uridhike na rangi yake.Muweke kwenye sahani mkamulie limao au ndimu

24
tayari kwa kuliwa.

22.DOUGHNUTS(donaz)
MAHITAJI:
Unga wa ngano 2 cups
Hamira 2 tsp
Sukari 4 tbsp
Siagi(butter) 2 1/2 tbsp (melted)
Nido 2 tbsp (si lazima)
Vanilla 1tsp
Maji (warm) 2 tbsp
Yai 1
Milk (warm) 3/4 mug

For glazing:
Icing sugar 1 cup
Milk 2tbsp warm
Chocolate
Siagi 1 tsp

JINSI YA KUTENGENEZA

25
Weka hamira chombo kidogo itie maji 2tbsp acha pembeni , kwenye bakuli weka unga,sukari,nido na
vanilla changanya kisha weka hamira na siagi uchanganye mpaka ichanganyike vizuri ,tia yai kwenye
chombo ulipige kidogo ulitie uchanganye.
Kisha weka maziwa kidogo kidogo huku unakanda mpaka uchanganyike vizuri (maziwa si lazima
yote) unga wako unatakiwa uwe donge lakini liwe laini(soft) lisiwe kavu sana (ikiwa unga umeloa
sana tia unga kidogo kisha paka mafuta mkono wako uendelee kuukanda mpaka uwe soft).uache
uumuke mpaka uwe double size ukiumuka uchanganye tena.
Kata shape ya donaz.weka tena ziumuke kisha choma kwa mafuta ya moto wa size (medium
heat).Ukizitoa ziache zipoe kisha unaweza kuziglaze.

JINSI YA KUTENGENEZA GLAZING

Weka icing sugar kwenye chombo uichanganye na 2 tbsp vya maziwa (warm) mpaka iwe soft na nzito
kidogo kisha weka donaz yako moja moja ukiitowa weka pembeni.Kwa chocolate glazing chukua
chocolate moja tia siagi yayusha kwa microwave kisha weka donazyako moja moja weka pembeni
igande.Kama unapenda unaweza kuzipamba pia.

23.MANGO AND STRAWBERRIES JELLY


MAHITAJI
embe mbivu (ripe mango) 1
Strawberries 4 kubwa
Rangi nyekundu ( food colour) 1/2 tsp
Sukari 4 tblsp
Vegetable jelly powder 2 packs
Kibakuli cha kigae

26
MATAYARISHO

Saga embe kwa blender mpaka iwe laini kama unahitaji kuchuja basi chuja, tia kwenye dish ambalo
unaweza kupasha moto baadae weka sukari vijiko 2 mix halafu weka pembeni.Weka strawberries
kwenye dish na rangi nyekundu na sukari ilobaki kisha Pika mpaka ziwe laini.

Zisage kwa blender halafu rudisha kwenye dish.Chukuwa maji ya moto sana nusu kikombe changanya
na jelly packet 1 koroga mpaka iyayuke. Halafu mix na embe,Kisha mimina nusu kwenye kibakuli
weka kwenye friji.

Ikisha kuganda fanya kama ulivyofanya kwa embe changanya strawberries na jell. Kisha mimina nusu
juu ya lile embe liloganda.Rudisha kwenye friji,Ikiganda itoe. Lile embe lilobaki kama limeganda
lipashe moto kidogo litakuwa liquid tena halafu mimina kwenye kibakuli. Rudisha kwenye friji. Acha
igande malizia na strawberry ilobaki.Weka kwenye friji kwa masaa 3 tayari kwa kuliwa .

24.NYAMA NA KABICH
MAHITAJI YA NYAMA
nyama 1/2 kg
Zucchini or bilingani 1
Nyanya tomatoes 2 kubwa
Mafuta ya kupikia 3 tblsp
Kitunguu maji ( chopped )
Tangawizi (ilosagwa) 1ts
Kitunguu thaum (garlic)1tsp
Pilipili boga/ pilipili hoho 1/2
Maggi/ kidonge cha supu (roweka na maji ya moto kikombe 1)
All purpose seasoning 1 tsp sio lazima kama huna.

MAHITAJI YA KABICH
KABICH 1/2 likate jembamba jembamba
Carrot 1 kubwa ipare

27
Kitunguu thaum 1 tsp
Siagi (butter) 2 tblsp

MATAYARISHO

Kata nyama vipande vidogo vidogo.Kaanga vitunguu maji kwenye dish mpaka viwe vyekundu. Tia
nyama mix halafu ifunike acha iive kwa maji yake wenyewe. Ikikaribia kukauka tia nyanya tomatoes,
zucchini, pilipili hoho, tangawizi na kitunguu thaum.

Koroga mpaka vichanganyike vizuri acha vichemke kwa dakika 5. Weka maggi na all purpose
seasoning kama unayo, ongeza na maji nusu kikombe. Funika acha ziive Kwa moto wa kati Mpaka
iwe nzito. Lakini uwe unakoroga ili isigande.Onja kama inahitaji chumvi Halafu weka pembeni.

KABICH MATAYARISHO

Weka dish kwenye jiko tia siagi,Kisha tia kitunguu thaum mix kwa dakika 1 weka kabich na carrots
mix mpaka ichanganyike vizuri. Pika kwa dakika 3 Onja chumvi.Kama kila kitu kiko sawa tayari kwa
kuliwa na ugali.
Angalizo: Unaweza kupika vitu vyote hivi bila kutia chumvi. Siagi, magi na all purpose seasoning
vyote hivi vina chumvi kwa hiyo onja kabla hujaongeza.

25.VIAZI/MBATATA

MAHITAJI
Mbatata 10 medium size (potatoes, viazi)
Mafuta 1/4kikombe (tea cup)
Tomato chopped 3 tbsp or(two medium size fresh tomatoes)
Tomato puree 2 1/2 tbsp
Ukwaju kiasi
Rangi nyekundu kiasi
Chumvi kiasi

JINSI YA KUPIKA

28
Kwanza roweka ukwaju wako na maji yamoto ukilainika chuja upate rojo zito la size, Menya mbatata
zako kata vipande vya size kosha vizuuri ziweke kwenye moto na maji zichemshe mpaka ziive bila
kuvurugika (zinachukua kama dakika 10 kwa moto wa juu makisio) zikiiva chuja maji yote weka
pembeni.

Sufuria hiyo hiyo weka mafuta yakipata moto weka tomato chopped kaanga mpaka ilainike weka
nyanya changanya vizuri weka rangi yako uloitia maji kidogo kama 2 tbsp acha vichemke kama
dakika moja.

Sasa weka rojo lako la ukwaju na chumvi acha vichemke pamoja kwa dakika 1 nyengine onja chumvi
na ukali size yako unayopenda, ukiona ukali hautoshi unaweza kuengeza hata ndimu.Sasa mimina
mbatata zako ulochemsha changanya vizuri kwa uangalifu bila kuvuruga mpaka uone mbatata zote
zimeenea mchanganyiko na zimepiga rangi vizuri ( usizikaushe urojo wote).Hapo sasa weka kwenye
sahani yako au bakuli tayari kwa kuliwa na pilipili kama unapenda.

26.NDIZI ZA KUKAANGA (PLANTAINS)


MAHITAJI
ndizi mbizu (ripe plantains) 3
Mafuta ya kupikia (cooking oil) 5 tblsp
Chumvi kidogo (pinch of salt)

MATAYARISHO
zioshe ndizi na maganda yake kisha zikate size unayopenda (zikate na maganda yake ndio zinakatika
vizuri). Ukimaliza kuzikata ndio unazimenya, ziweke kwenye bakuli weka chumvi mix kidogo.Weka

29
frying pan kwenye jiko, tia mafuta ukiona kidogo ongeza lakini yasiwe mengi yakafunika ndizi wakati
wa kukaanga.Zikaange pande zote mbili usiziache sana zinaiva mara moja.

27.CHICKEN BREAD

MAHITAJI (For chicken fillings):


Kuku nusu
Ndimu (lemon juice) 3 tbsp
Chumvi kiasi
Bizari nzima (cummin powder) 1tsp
Bizari manjano(tumeric) 1/4 tsp
Pilipili manga (black papper powder)
Pilipi hoho (mix capsicum) nusu
Kitunguu maji 1(small chopped)
Soya source 2tsp
Thomu 1 tsp
Tangawizi 1tsp
Carrot 1 chopped
Siagi 1tbsp
Kotmiri(coriander) zilokatwa
(For dough)
Unga wa ngano 2 1/2 cups

30
Hamira 1 tbsp
Nido (milk powder) 2 tbps
Chumvi kiasi
Sukari 1 tsp
Maziwa 3/4 mug (warm)
Siagi (butter) 3tbsp warm
Yai 1 (lipige na maziwa 1tsp)
Ufuta (si lazima)

JINS YA KUPIKA

Mkate kuku umchemshe na chumvi,ndimu,garlic,tangawizi, cumin,black paper,soya source na bizari


mpaka achemke vizuri mtoe mifupa yote umnyambue kwa mkono awe mdogo mdogo.

Weka siagi kwenye sufuria ulotoa kuku ikipata moto weka vitunguu vikaange mpaka vilainike tia
pilipili hoho(ukipata kuchanganya za kila rangi ndo nzuri) na carrot kaanga vizuri kisha muingize
kuku wako umponde kwa mwiko kidogo umchanganye vizuri kisha weka coriandor mueke pembeni.

Changanya unga na hamira,chumvi,sukari,nido na siagi 2tbps uchanganye vizuri mpaka ichanganyike


weka maziwa kidogo kidogo huku unaukanda mpaka ulainike uwe donge uwache uumuke kwa nusu
saa.

Kata vidonge vidogo vidogo usukume kwa rolling pin ufanye shape kama hiyo kwenywe picha upake
siagi juu kidogo ukate kama kwenye pic weka kuku wako kati uusuke kwa kupishana ipange kwenye
trey uache uumuke kidogo.Lipake yai juu na ufuta uchome kwa oven 160°c kwa 18-20min au mpaka
upige rangi vizuri ukiitoa kwenye oven ipake siagi juu.

31
28.PIZZA AINA YA KWANZA
MAHITAJI
Unga wa ngano 1/2 kg/ 500 gm
(Huu unafanya pizza 2)
Hamira 2 tsp
Sukari 1tblsp
Chumvi kiasi
maji kiasi
Extra virgin olive oil 2 tblsp (mafuta ya alizeti/ mafuta ya zaitun)

MAHITAJI YA VITU VYA KUWEKA JUU YA PIZZA


cheese 1/2 kg/500 gm, kwa pizza zote mbili. (Ipare )
hapa unaweza kuweka unachopenda mwenyewe mimi nimeweka:
Black olives
Sausage 1 nimeikata
Sweetcorns
Vipande vya kuku
Pilipili

MATAYARISHO

Loweka hamira pamoja na sukari mpaka iumuke kisha Weka unga kwenye bakuli kisha tia chumvi,
olive oil changanya vizuri kisha weka hamira iloumuka.

Changanya halafu weka maji kidogo kudogo mpaka unga wako ushikane uwe mlaini. Yaani usikupe
tabu kuukanda.Ukande kwa dakika 10.Upakae mafuta juu uweke kwenye bakuli ufunike uache
uumuke kabisa.

Ukisha kuumuka ukande tena kidogo halafu ugawe sehemu mbili. Chukua tray si lazima iwe ya duara
ukiona itagandisha pakaa siagi. Weka unga wako nusu kwenye tray utandaze sawa sawa mpaka uwe
shape ya ile tray.

Ukisha kukaa sawa weka tomato sauce ulitengeneza kabla, tumia kijiko usiweke yote kwa
pamoja.Tandaza sauce yako juu ya ule unga wacha nafasi pembeni kama kwenye picha hapo juu.

Kisha weka cheese juu yake weka vitu vyako vilokatwa (toppings) kwa kutumia mkono vi didimize
chini (press down) kidogo kidogo.

32
Halafu choma kwenye oven kwa moto wa kati. Iweke kati kati kwenye cooker. Ikiiva ikate.

29.PIZZA AINA YA PILI


MAHITAJI
Nyanya (tomatoes) 3 size ya kati
Kitunguu thaum (garlic) vipunje 4-5 usivisage
Kitunguu maji 1
Tangawizi mbichi kipande usiisage
Tomatoes puree 1 tblsp
Mix herbs zilokauka (sio lazima ) 1 tsp (zinapatikana supermarket)
Chumvi kiasi.

MATAYARISHO

Nyanya usizikate zifanye alama ya ''X'' kwa kisu halafu ziweke kwenye dish pamoja na kitunguu maji
(kilokatwa sehemu 4 tu), kitunguu thaum na tangawizi tia na maji nusu kikombe. Funika weka kwenye
jiko acha viive.

Ukiona maji yamebakia kidogo weka nyanya acha kwenye jiko kwa dakika moja. Zima moto acha
vipoe kabisa.Vikisha kupoa toa maganda ya nyanya (tomatoes) halafu weka vitu vyote kwenye
blender usiweke maji. (Inatakiwa iwe nzito) Saga vizuri.Weka sauce yako kwenye kibakuli changanya

33
na chumvi na mix herbs. Halafu iweke pembeni.

30.JUICE YA EMBE, PASSION, NANASI NA NDIZI

MAHITAJI
embe mbivu 1 kubwa
Nanasi 1 size ya kati
Passion fruit 2
Banana (ndizi mbivu) 2
Sukari kiasi
Maji (yalochemshwa au ya kununuwa) kiasi

MATAYARISHO

Menya embe lisage kama halina nyuzi huna haja ya kulichuja.Menya nanasi likate halafu lisage
uchuje. Zitoe kokwa kwenye passions sizage na zichuje.

Changanya embe, passion na nanasi pamoja tia sukari na maji size onja kama kila kitu kiko sawa.
Weka kwenye friji iwe baridi. Ikifika time ya kunywa kata banana vipande vidogo vidogo weka

34
kwenye juice.

/ .1 (
) '"( )

35

You might also like