You are on page 1of 7

BAMIA

njia nyengine kataka bamia, viazi kata vipande vidogo vidogo na biriga ya pia vipande vidogo vdgoo..
kaanga kwa mafuta mingi toa weka kando zijichuje mafuta. kaanga kitunguu nyanya weka pilipil
ukipenda na tomato paste kidog weka maji kiduchu viivee vikikauka weka vile ulivyokaangaa mix vizur
enjoy

Viungo vya mishkaki

Mpenzi wangu nimefurahi sana kuwa unapenda vyakula vyetu vya kipemba

Uzile

Mdasili

Garam masala

Tandori masala

Zananjiro

Paprika

Corianda poda

Pilipili manga

Chumvi

Na ndimu

Maggie cube

Wali wa mchaichai na iliki jaman chefs jaribuni hii mlete mrejesho so tasty 😋

Nimechemsha maji na mchaichai yalipochemka nikachuja maji halafu nikakaanga kitunguu maji , nikatia
iliki na yale maji ya mchaichai nikaweka chumvi na mchele wangu.
SIRI YA MAPISHI YA HALF CAKE TAMU SANA

MAHITAJI

1.Unga wa ngano kilo moja

2.Sukari kikombe kimoja

3.Baking powder kijiko kimoja na nusu cha chai

4.Baking soda nusu kijiko cha chai

5.Hiriki ya unga robo kijiko cha chai

6.Maziwa fresh kikombe kimoja (ukihitaji)

7.Siagi vijiko 3 vya chakula au mafuta ya kupikia vijiko vitatu vya chakula

8.Vanilla kijiko kimoja cha chai (ukihitaji)

9.Mayai mawili (ukihitaji)

10.Chumvi kijiko kimoja na nusu cha chai

11.Maji ya uvuguvugu
12.Mafuta ya kupikia

MAPISHI

1.Katika beseni au bakuli kubwa mimina unga wa ngano,sukari,chumvi,hiriki,baking powder,baking soda,


kisha changanya vizuri.

2.Tengeneza kama shimo katika unga wa ngano kisha mimina siagi,mimina maziwa mimina vanilla na
mimina ute wa yai kisha changanya vizuri na unga.

3.Anza kukanda unga wa ngano kwa maji ya uvuguvugu hadi uwe mgumu mgumu lakini sio sana na
usinate kwenye chombo wala kwenye mikono.Ngano ya half keki haitakiwi kuwa laini kama ya maandazi

4.Tengeneza duara kubwa kisha lipake mafuta na paka mafuta kwa pembeni katika chombo cha
kukandia.

5.Funika ngano kwa muda wa dakika 40 hadi saa 1

6.Funua ngano kisha ikate katika madonge makubwa kiasi kama kabichi dogo

7.Sukuma madonge hayo kama chapati nene kiasi kisha anza kukata vipande vya half cake.

8.Weka kikaango katika moto wa wastani kisha kaanga half keki zako hadi ziwe na rangi ya kahawia kwa
nje, na geuza upande wa pili.

9.Toa half keki katika kikaango kisha ziweke katika chujio au tissue ili zichuje mafuta.
10.Half keki zipo tayari

Andaa chai yako ya maziwa na half keki kisha jionee tofauti.

KUKU WA KUKAANGWA

MAHITAJI

1.Kuku mzima au aliyekatwa katwa

2.Paste ya kitunguu na tangawizi - (Vitunguu saum na tangawizi vilivyosagwa):- Kijiko kimoja cha chakula

3.Pilipili ya unga kiasi kidogo

4.Manjano kijiko kimoja cha chai

5.Limao kubwa kipande

6.Pilipilimanga kijiko kimoja cha chai

7.Garam masala au biryani masala au chicken masala kijiko kimoja cha chai

8.Manjano kijiko kimoja cha chai


9.Mtindi kijiko kimoja cha chakula

10.Corn flour vijiko vitatu vya chakula (Utaweka kama unahitaji kuku atafunike kama kaukau)

11.Chumvi kiasi

MAPISHI

1.Hakikisha vipande vya kuku vimekauka maji

2.Chukua bakuli la plastiki au la glass kisha mimina viungo vyote kasoro chumvi na limao

3.Changanya viungo ulivyomimina kwenye bakuli

4.Kamulia limao kwenye mchanganyiko wa viungo kisha changanya vizuri

5.Mimina vipande vya kuku kwenye bakuli kisha changanya vizuri na viungo vyote

6.Funika bakuli kisha acha kuku kwa muda wa saa 1, au weka bakuli katika fridge kwa muda wa saa 2

7.Funua kisha mimina chumvi na changanya tena acha kwa dakika 5

8.Weka kikaango jikoni kisha mimina mafuta ya kupikia acha yapate moto kiasi
9.Anza kukaanga vipande vya kuku au kuku mzima hadi rangi ibadirike iwe ya kahawia

(Muda wa kukaanga ni kama dakika 8 kwa kila mkaango wa vipande vibichi)

10.Weka vipande vya kuku katika chujio au sinia lenye tissue ili kuchuja mafuta

11.Katakata vitunguu viweke juu ya vipande vya kuku au majani ya giligilani ili kuongeza harufu nzuri

Karibu,Niadd kama friend kwa recipes mbalimbali

Unachukuwa

Unga

Chumvi

Hamira kidogo

Baking powder kidogo

Sukari kidogo

Blueband vijiko 2

Unakanada na maji

Nyama ya kusaga

Nyama

Chumvi

Pilipili
Pilipili manga

Kitungu saumu unasaga

Kitungu maji unakata vidogo vidogo

Na carrot

Na pilipili boga

Unachoma kwenye oven kama huna ovrn hata ukikanga inakuwa nzuri tu

You might also like