You are on page 1of 4

Maziwa ya mama ni muhimu kwa ajili ya ukuaji wa mtoto kiakili na kimwili.

Mtoto anatakiwa
kunyonya kama kawaida na kupata chakula cha nyongeza.

Zingatia:

 Vyombo vya mtoto visafishwe kwa Maji safi na sabuni.


 Chakula kinaweza kuchanganywa na maziwa ya mama kidogo baada ya kuandaliwa.
 Vyakula vipikwe kwa mvuke au kuchemshwa kiasi na kupondwapondwa au kusagwa.
 Ili kupata mchanganyiko mzito changanya na:
 maziwa ya mama
 supu
 Tui la nazi, maziwa ya almond,soya n.k
 Maziwa ya kopo
 Ni muhimu kabla ya kuandaa chakula cha mtoto au kumlisha mtu anawe mikono kwa maji safi yanayotiririka na
sabuni. Kumbuka kumnawisha mtoto pia.
 Mtoto asikabwe wakati wa kula, alishwe kwa upendo na taratibu ikibidi imba nyimbo.
 Ni muhimu kumbadilishia mtoto ladha, rangi na aina ya chakula angalau baada ya siku 2.

JJ Breastfeeding STORE
Mtoto asipatiwe:
 Mayai mabichi, asali, juisi ya matunda, chai, kahawa, soda, juisi ya kiwandani, keki, biskuti na crips.
 Maziwa ya ng’ombe mpaka atimize mwaka mmoja.
 Tumia kwa kiasi kidogo vitu hivi au epuka: chumvi, sukari na siagi (hii mpaka mtoto atimize mwaka 1) kwenye
chakula cha mtoto.

Mlo wa Kwanza (mfano: asubuhi saa nne) wakati wa kusaga au kumlisha tumia maziwa ya mama
Option 1: Uji wa nafaka moja, maziwa, mafuta au siagi , karoti iliyosagwa ikalainika au boga , rojo ya tunda au tende
Option 2: Uji wa nafaka moja, yai, mafuta au siagi , mboga za majani, rojo ya tunda.
Option 3: Boga hususani butternut mnaita bogalishe, mafuta au siagi , njegele
Option 4: uji wa nafaka moja, mdalasini kidogo, maziwa unaweza kuongeza ndizi mbivu au rojo ya embe uji ukiiva.
Option 5: supu ya kuku, minofu ya kuku, carrot, njegere pika halafu saga kwa pamoja
Option 6: Maharage marefu ya kijani, karoti na boga au butternut au apple na mafuta au siagi

Mlo wa pili (jioni labda saa kumi)


Anaweza kupewa tunda lililopondwa au kusagwa bila kuweka maji unaweza kuchanganya na maziwa ya mama kama ndizi
mbivu, parachichi, embe n.k
Au
unaweza kumpatia mlo wowote kati ya nliyoorodhesha hapo juu.

JJ Breastfeeding STORE
Mapendekezo kuhusu ulishaji wa mtoto vyakula vya nyongeza miezi 6-8

Umri wa mtoto Idadi ya milo Kiasi Uzito na ulaini Aina za vyakula Ulishaji
kwa siku wa chakula shirikishi

Miezi 6 Anakula mara 2 Vijiko 2 – 3 vya Kiwe kizito Anza na Mtoto atahitaji
chakula kila mlo kisichomwagika kwa mchanganyiko muda wa kuzoea
urahisi kutoka katika wa vyakula kula vyakula
kijiko vichache. vingine
Zingatia makundi
ya chakula.

Samaki na
nyama anza
kumpa wiki ya 2.
Miezi 7-9 Milo 2- 3 kwa Mlishe mtoto Mlishe mtoto Mlishe mtoto Mlishe mtoto kwa
siku na asusa nusu (1/2) ya chakula kizito chakula upendo na
mara 1-2 kwa kikombe kila mlo kilichopondwa mchanganyiko usimlazimishe.
siku huku (Kikombe1=mililita pondwa katika umri kilichoandaliwa
akiendelea 250) wa miezi 8 mtoto kutoka katika Chakula kivutie
kunyonyeshwa anaweza kula makundi matano na vyombo vya
chakula hicho ya vyakula. kuvutia.

MAJI: Mtoto atumie nusu kikombe mpaka kikombe kimoja kwa siku. Maji anywe kwenye kikombe wakati wa kula
tu.

JJ Breastfeeding STORE
Chakula kilaini lakini kizito Chakula anachoweza kushika

Mlishe kwa upendo Mpatie maji kwenye kikombe

JJ Breastfeeding STORE

You might also like