You are on page 1of 5

 Karibu Umoja wa Mataifa Русский Español Português

SW 

Habari za UN

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KABRASHA LA SAUTI  SAJILI 

Nchi zaidi ya 20 kukabiliwa na


njaa kali, hatua za haraka
zahitajika kuepusha
baa:WFP/FAO Ripoti

© WFP/Arete/Damilola Onafuwa | Mtoto wa miezi 7 akipimwa utapiamlo katika kituo cha afya cha
jimbo la Yobe nchini Nigeria

23 Machi 2021 Msaada wa Kibinadamu

Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa


imeonya kwamba katika nchi zaidi ya 20 duniani tatizo la njaa
litaongezeka kwa kiasi kikubwa na kutoa wito wa hatua za haraka
ili kuepusha janga kubwa zaidi na hatari ya baa la njaa.

Ripoti hiyo ya mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la mpango wa chakula


duniani WFP na la chakula na kilimo FAO iliyopewa jina “ maeneo yenye
njaa” imesema katikia miezi ijayo bila msaada wa wa dharura haraka
maisha ya mamilioni ya watu yatakuwa hatarini hasa nchini Yemen, Sudani
Kusini na Kaskazini mwa Nigeria ambazo zinashika nafasi ya juu ya orodha
hiyo zikikabiliwa na viwango vya juu vya njaa hivi sasa huku familia katika
baadhi ya maeneo nchini Sudan Kusini na Yemen tayari ziko au zitakuwa
hatarini kwa njaa kali na vifo.

Masshirika hayo yameongeza kuwa ingawa idadi kubwa yan chi


zilizoathirika ziko Afrika , njaa kali inatarajiwa kuongezeka katika kanda
nyingi duniani kuanzia Afghanistan barani Asia, Syria na Lebanon Mashariki
ya Kati hadi Haiti Amerika ya Kusini na Caribbea.

Kukimbizana na wakati
Mashirika hayo yamesema zaidi ya watu milioni 34 ulimwenguni tayari
wanakabiliwa na viwango vya dharura vya njaa kali, ikimaanisha kuwa ni
hatua kidogo tu kuwa baa la njaa.
“Kiwango cha mateso kinatisha. Na ni jukumu letu sote kuchukua hatua
sasa na kuchukua hatua haraka kuokoa maisha, kulinda maisha na kuzuia
hali kuwa mbaya zaidi ", amesema Mkurugenzi Mkuu wa FAO Qu
Dongyu.
“Katika kanda nyingi, msimu wa kupanda ndio umeanza tu au uko karibu
kuanza. Lazima tukimbizane na wakati na tusiruhusu fursa hii ya kulinda,
kuleta utulivu na hata kuongeza uzalishaji wa chakula wa ndani, kuteleza. ”
WFP/Kiyori Ueno | Sekina Hassen (kulia) na wenzake wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya
Udassa Repi wakinywa ui. Hupata huduma hii kila asubuhi kutokana na msaada wa WFP na hivyo
wanaweza kuzingatia masomo badala ya kushinda njaa.

Janga linalojitokeza
Kuna sababu kadhaa zinazochangia kuongezeka kwa ukosefu wa uhakika
wa chakula, na mataifa yanakabiliwa na moja au mchanganyiko wa chachu
muhimu ambayo ni pamoja na mizozo, janga la COVID-19, mabadiliko ya
tabianchi na milipuko ya nzige.

Pia kuongezeka kwa changamoto za kuwafikia watu wenye mahitaji ya


kibinadamu ni wasiwasi mwingine. “Tunashuhudia msiba ukitokea mbele
ya macho yetu. Njaa inayochangiwa na mizozo, nakuchochewa na majanga
ya hali ya mabadiliko ya tabianchi na janga la COVID-19 inabisha hodi
kwenye mlangoni kwa mamilioni ya familia”, amesema David Beasley,
Mkurugenzi Mtendaji wa WFP.

Vipaumbele vitatu vya haraka


Kwa mujibu wa ripoti hiyo Bwana Beasley ameongeza kuwa "Tunahitaji kwa
dharura vitu vitatu ili kuzuia mamilioni ya watu kufa kwa njaa: Mosi,
mapigano yanapaswa kukomeshwa, pili lazima turuhusiwe kufikia jamii
zilizo katika mazingira magumu na kutoa msaada wa kuokoa maisha, na
tatu zaidi ya yote tunahitaji wafadhili kuongeza dola bilioni 5.5 ambazo
tunaziomba kwa ajili ya mwaka huu. ”
Fedha hizo zitatumika kwa msaada wa chakula cha kibinadamu, usaidizi
wa kugawa pesa taslimu na hatua zingine za dharura za kusaidia kuokoa
maisha, kulingana na ombi lililozinduliwa mapema mwezi huu na mashirika
mawili ya Umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo pia inapendekeza hatua muhimu katika kila "eneo lenye njaa"
kushughulikia mahitaji ya sasa na ya baadaye, kama kuongeza chakula na
msaada wa lishe, kutoa mbegu zinazostahimili ukame, kukarabati
miundombinu ya uvunaji wa maji na kuanzisha miradi ya pesa-kwa-kazi.

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani


bofya hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila
wakati zinapochapishwa jisajili hapa.

♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati


wowote popote ulipo.

♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter

NJAA WFP FAO NIGERIA YEMEN


SUDAN KUSINI COVID-19

TAARIFA ZIHUSIANAZO

Hatua za haraka zahitajika kuepusha baa la


njaa katika nchi nne:WFP/FAO

Zaidi ya watu milioni 820 wanakabiliwa na


njaa kote duniani - SOFI

Idadi ya waliokuwa na njaa 2018 ilipungua


ingawa idadi ya nchi imeongezeka - ripoti

MAKTABA  MSEMAJI WA UN 
KATIBU MKUU  TUPATE 

A-Z SITE INDEX HAKIMILIKI

MASWALI YA MARA KWA MARA

TAHADHARI YA UDANGANYIFU NOTISI BINAFSI

KANUNI ZA MATUMIZI

    CHANGIA

You might also like