You are on page 1of 2

Ta ifa Founda tion Primary Sc hool (Eng lish Medium)

Mshangano, Songea Municipal


P.O. Box 226 , SONGEA.
| www.taifa.ac.tz | info@taifa.ac.tz | 0752546874 | 0752400400 |
SCHOOL VISION: Eradication of poverty, SCHOOL MOTTO: Hard working, co-operation, SCHOOL MISSION: Education we get should
diseases and ignorance through Education. peace and love to everybody. liberate us and useful to the community.

Mzazi/ Mlezi wa:

Maelezo haya yanahusu utaratibu wa kujiunga au kuendelea na masomo katika shule yetu ya
Awali na Msingi TAIFA FOUNDATION PRE AND PRIMARY SCHOOL mwaka 2023. Shule
itafunguliwa tarehe 9 January 2023.
1. MWONGOZO WA MALIPO
Malipo ya lazima kwa wanafunzi wote yameainishwa na kufafanuliwa katika jedwali hapo chini.
Malipo haya yameainishwa katika ngazi ya madarasa:
DARASA
SHULE YA TATU,
KWANZA NNE NA MAELEZO
AWALI TANO NA
NA PILI SABA
SITA
Karo ya Shule 470,000.00 500,000.00 550,000.00 550,000.00
Chakula 300,000.00 330,000.00 330,000.00 330,000.00
Mitihani ya Ndani na
15,000.00 15,000.00 35,000.00 50,000.00
ya Nje
Viandikwa 30,000.00 30,000.00 30,000.00 30,000.00
Vitabu vya kiada (TET) 50,000.00 70,000.00 70,000.00 70,000.00
Cavendish Day (PTA) 20,000.00 20,000.00 20,000.00 20,000.00
Kulipwa shuleni baada ya
Mahafali - - -
makubaliano na PTA
UMITASHUMTA 5,000.00 5,000.00 5,000.00 5,000.00
School Diary 20,000.00 20,000.00 20,000.00 20,000.00
Tahadhari ya Afya 10,000.00 10,000.00 10,000.00 10,000.00
JUMLA 920,000.00 1,000,000.00 1,070,000.00 1,085,000.00

2. AWAMU ZA MALIPO
Malipo hayo yatafanyika kwa awamu tatu kama ifuatavyo:
Awamu ya Awamu ya Awamu ya JUMLA
Januari Aprili Julai
Shule ya Awali 320,000.00 300,000.00 300,000.00 920,000.00
Darasa la Kwanza na Pili 350,000.00 300,000.00 350,000.00 1,000,000.00
Darasa la Tatu, Tano na Sita 360,000.00 360,000.00 350,000.00 1,070,000.00
Darasa la Nne na Saba 420,000.00 440,000.00 225,000.00 1,085,000.00

Malipo yafanyike kwenye akaunti ya shule:


JINA LA BENKI: NMB
JINA LA AKAUNTI: TAIFA FOUNDATION SECONDARY SCHOOL
NAMBA YA AKAUNTI: 23710002251

3. MALIPO KWA WAKATI


Malipo yote ya ada na michango mingine ya shule ni lazima yalipwe kwa wakati kama
ilivyoelekezwa ili kuepusha usumbufu kwa mtoto na shule na pia kutuwezesha kukamilisha
mipango ya uendeshaji wa shule.

1
Ta ifa Founda tion Primary Sc hool (Eng lish Medium)
Mshangano, Songea Municipal
P.O. Box 226 , SONGEA.
| www.taifa.ac.tz | info@taifa.ac.tz | 0752546874 | 0752400400 |
SCHOOL VISION: Eradication of poverty, SCHOOL MOTTO: Hard working, co-operation, SCHOOL MISSION: Education we get should
diseases and ignorance through Education. peace and love to everybody. liberate us and useful to the community.

Jina la mwanafunzi na darasa lake liandikwe kwenye pay–in–slip (fomu ya kuweka fedha) na
iletwe na mzazi shuleni na iwapo atatumwa mtoto basi mzazi ahakikishe ana kopi ya slipu hiyo.
Ofisi zitakuwa wazi kuanzia tarehe 2 Januari 2023.
4. MAAGIZO YA KITAALUMA
(i) Kila mwanafunzi atapewa vitabu vyote vya kiada kwa masomo yote. Mzazi atatakiwa
kushirikiana nasi kuhakikisha vitabu hivyo vinatumika ipasavyo na kutunzwa. Vitabu hivyo
vitapatikana shuleni.
(ii) Pamoja na vitabu, wanafunzi wa Awali ya Kwanza na ya Pili (PPI & PPII), watapewa
penseli, kalamu za rangi, crayons, vitabu-picha, abakusi, kichongeo na kifutio shuleni.
(iii) Wanafunzi wa kuanzia darasa la III hadi darasa la VII watatakiwa kuwa na peni, rula,
penseli, kichongeo, ufutio na mkebe (Mathematical set).
(iv) Kila mwanafunzi anatakiwa kuja na rimu moja (bunda moja la karatasi) ya A4 isipokuwa
wanafunzi wa Darasa la Nne na la Saba watakaotakiwa kuja na rimu mbili (bunda mbili
za karatasi) moja Januari na nyingine Aprili.

5. HUDUMA YA HOSTELI
Shule inatoa huduma ya Hosteli inayoambatana na usafiri iliyopo eneo la Mkuzo. Watoto walio
katika madarasa ya mitihani, hasa darasa la Saba wanashauriwa kuishi hosteli. Shule ina
utaratibu wa kuendesha masomo rekebishi (remedial) kwa wanafunzi wa hosteli kwa muda wa
ziada. Maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa Hosteli yapo kwenye kijarida kinachopatikana shuleni.
6. HUDUMA YA USAFIRI
Shule inatoa huduma ya usafiri kwa wanaohitaji. Maelezo yahusuyo huduma ya USAFIRI
yanapatikana katika kipeperushi tofauti kinachopatikana shuleni.
7. MATUMIZI YA LUGHA
Lugha ya mawasiliano, kujifunzia na kufundishia shuleni ni kiingereza. Hivyo mwanafunzi
anatakiwa kutumia lugha ya kiingereza muda wote na si vinginevyo.
8. MAVAZI
Uniform za Shule
Wazazi watakuwa na uhuru wa kuwanunulia wanafunzi sare za shule. Sampuli za aina na rangi
ya sare za shule zinapatikana shuleni.
Sare za Michezo
Gharama za sare (Tshirt na Tracksuit) hazitalipwa benki hivyo mzazi atatakiwa kuja na malipo
haya moja kwa moja (cash) shuleni na kuonana na wahusika.
9. HUDUMA YA CHAKULA
Chakula kinatolewa shuleni kwa wanafunzi wote. Huduma ya chakula siyo ya hiyari na kila mtoto
anatakiwa kupata milo miwili ya chakula hapa shuleni. Shule hairuhusu wafanya bishara
ndogondogo za chakula katika eneo lake na hivyo mtoto asipewe fedha kwa ajili ya kununua
chakula akiwa shuleni.

Shule imeazimia kutoa huduma ya ziada ya uji kwa watoto wa AWALI kabla masomo kuanza
baada ya kuona kuwa baadhi ya watoto wetu huwahi kuja kabla kupata huduma hiyo nyumbani.
Huduma hii haitaambatana na malipo ya ziada.

You might also like