Professional Documents
Culture Documents
Umuhimuwakusajilimadalalibyrahmamagimba
Umuhimuwakusajilimadalalibyrahmamagimba
KUSAJILI
MAWAKALA WA
MILKI
(MADALALI)
KWA
MAENDELEO YA
SEKTA YA MILKI
NCHINI
SEKTA YA MILKI NCHINI TANZANIA
Sekta ya milki ni msingi wa maendeleo ya taifa letu, ikigusa maisha ya kila raia.
Sekta hii inaumuhimu katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania, ikichangia kwa kiasi kikubwa kwenye Pato la Taifa
kwa takribani Shilingi Trilioni 2.9 mwaka 2021 kulingana na takwimu, na pia imetoa fursa za ajira kwa watanzania.
Miaka ya hivi karibuni, sekta hii imekua kwa haraka ikiongozwa na mambo kama vile utandawazi, ongezeko la idadi ya
watu, na uwekezaji mkubwa katika miundombinu na miradi ya maendeleo inayovutia wawekezaji wa ndani na wa
kigeni.