Professional Documents
Culture Documents
Makao makuu yako Tabora Mjini. Eneo la mkoa ni 76,151 km mnamo 34,698 km (46%) ni hifadhi ya misitu, 17,122 km (22%) ni hifadhi ya wanyama. Wakazi walio wengi ni wakulima na wafugaji. Jumla ya wakazi ilikuwa watu 1,717,908 (mw. 2002).
Ramani ya Mkoa wa Tabora Kulikuwa na wilaya 6 (idadi ya wakazi kwa mabano): Tabora Mjini (188,808), Nzega (417,097), Igunga (325,547), Uyui (282,272), Urambo (370,796), Sikonge (133,388). Mnamo Machi 2012 ilianzishwa pia wilaya ya Kaliua. Tabora haina barabara za lami. Kuna njia ya reli ya kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma kwa upande moja na kwenda Mwanza kwa upande mwingine. Jina la Urambo humkumbuka Mtemi Mirambo aliyekuwa mtwala muhimu wa Wanyamwezi kabla ya kuingia kwa ukoloni. Wenyeji wa Tabora ni hasa Wanyamwezi.