You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA


MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA
MAZINGIRA-NEMC
Katika kikao kilichoitishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Mb), tarehe 24 Januari
2016, mjini Dodoma kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la
Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama
ifuatavyo:
1.
Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda Mkoani
Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa
wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na
kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC
wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:
a.

Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,

b.

Wakili Heche Suguta Manchare - Mwanasheria Daraja la II

c.

Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa Mazingira

Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia.


2.
Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo
makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa
Baraza. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya
apewe barua ya onyo kali la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa
watumishi wa Baraza.

3.
NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia
utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi
zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu
yaliyoko kwa mujibu wa Sheria. Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe.
Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili
kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi
wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.

4.
Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki
moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo: Anwani ya barua
pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote
mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa ama chochote na
watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa
mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.

5.
Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya
Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC ipitie upya orodha ya
wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote
ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha
taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na
kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.

6.
Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC
kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
08.01.2016

You might also like