You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI


MAREKEBISHO YA TANGAZO LA AJIRA
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania linatangaza nafasi za Ajira kwa
mwaka wa fedha 2015/2016 kwa vijana waliosomea ujuzi/fani, cheti na
stashahada toka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na wahitimu wa
kidato cha sita na nne kati ya mwaka 2009 hadi 2014 waliohudhuria na
kufaulu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Waombaji wa kazi
watume barua za maombi kabla ya tarehe 17 Julai, 2015 kwa anuani
ifuatayo:
Kamishna Jenerali,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
S.L.P 5821,
DAR ES SALAAM.
1.

SAJINI WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI (SERGEANT OF FIRE AND


RESCUE) Nafasi 200.
Mwombaji awe amehitimu na kupata cheti cha mtihani wa kidato
cha sita kati ya mwaka 2009 hadi 2014.
Sifa za ziada:Mwenye Stashahada ya Habari na Mawasiliano, Utunzaji wa
Kumbukumbu, Ugavi na Ununuzi, Sheria, Katibu Muhtasi, Uhasibu
na Uuguzi;

au awe na cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la I

katika moja ya fani ya Umakenika, Ufundi Bomba, Ufundi Umeme


wa Majengo, Ufundi Umeme wa Magari, Wachora Ramani, Fundi
Rangi wa Magari, Uchomeleaji, Ufundi Uashi, Mtaalam wa mazoezi
ya viungo, Ufundi Mitambo, Kada za Afya na Ufundi Seremala.
1

2. KONSTEBO WA ZIMAMOTO NA UOKOAJI (FIRE CONSTABLE)


Nafasi 803.
Mwombaji awe amehitimu na kupata cheti cha mtihani wa kidato
cha nne kati ya mwaka 2009 hadi 2014.
Sifa za ziada:
Mwenye cheti katika fani ya Habari na Mawasiliano, Utunzaji wa
Kumbukumbu, Zimamoto na Uokoaji, Ugavi na Ununuzi, Katibu
Muhtasi, Uhasibu na Uuguzi;

au awe na cheti cha majaribio ya

ufundi Daraja la I katika moja ya fani ya Umakenika, Ufundi Bomba,


Ufundi Umeme wa Majengo, Ufundi Umeme wa Magari, Wachora
Ramani, Uchomeleaji, Ufundi Uashi, Mtaalam wa mazoezi ya
viungo, Ufundi Mitambo, Kada za Afya, na Ufundi Seremala.

MASHARTI MUHIMU KWA MWOMBAJI:


Mwombaji ni lazima awe amepitia na kuhitimu mafunzo ya
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Waombaji wote wawe wamehitimu kidato cha sita na nne kati
ya mwaka 2009 hadi 2014.
Mwombaji ambatanishe vivuli vya vyeti vyote yaani cheti cha
kuzaliwa,

kuhitimu

elimu

ya

sekondari,

cheti/vyeti

vya

taaluma na cheti cha kumaliza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),


(CV) ikiwa na majina ya wadhamini watatu na anwani zao na
picha

mbili

ndogo

za

(passpot

size),

hati

haitakubaliwa.
Mwombaji aandike kazi aliyoomba juu ya bahasha.

ya

kiapo

SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe Raia wa Tanzania.
Mwombaji wa nafasi ya Sajini awe na umri usiopungua miaka
18 na usiozidi miaka 30 na kwa nafasi ya konstebo umri
usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 28.
Mwombaji asiwe na kumbukumbu za kutenda uhalifu.
Mwombaji awe na urefu usiopungua sentimenta 155.
Mwombaji awe hajawahi kuajiriwa na Idara nyingine Serikalini.
Barua zote za maombi zitumwe kwa njia ya Posta.
Mwombaji awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji.
Mwombaji

awe

tayari

kufanya

kazi

mahali

popote

atakapopangiwa ndani ya Nchi.


Angalizo:

Waombaji

Tangazo la Ajira

wote

waliotuma

maombi

kwenye

la awali wasitume tena, maombi yao

yatashughulikiwa.

Imetolewa na
Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (T)
DAR ES SALAAM.

You might also like