You are on page 1of 29

KUCHUNGUZA ATHARI NA SABABU ZA UTUMIZI WA DAWA ZA KULEVYA MIONGONI MWA

WANAFUNZI WA SHULE ZA

BRENDA CHELIMO CHESANG.

UTAFITI HUU UMEWASILISHWA ILI KUTIMIZA MASHARI ILI KUTUNUKIWA SHAHADA YA UALIMU
KATIKA CHUO KIKUU CHA TURKANA,2022.

UTHIBITISHO

Atakayetia sahihi yake hapa chini atadhibitisha kuwa atasoma utafiti uliofanywa kuchunguza athari
na sababu za utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi wa shule za upli na
atapendekeza ikubaliwe na chou kikuu cha Turkana kwa ajili ya kutimiza sehemu ya masharti ya
kutunukiwa shahada ya elimu ya chou kikuu cha Turkana.
Mhariri;Naomi chepkemoi.

(msimamizi)

Tareha

HATILINZI
Haki zote zimehifadhiwa.Hairuhusiwi kuiga,kunakili,kutafsiri,kuhifadhi kwa mfano wowote ule au
kutoa hata sehemu kidogo ya kazi hii kwa njia yoyote ile ila kwa niaba ya mwandishi au kwa niaba ya
chuo kikuu kishirikishi cha Turkana.

TAMKO

Mimi Brenda Chelimo ,ninaapa kwamba utafiti huu ni kazi yangu halisi na haijawahi kuwasilishwa
katika chuo kingine kwa ajili ya kutunukiwa shahada yayote ile ya masomo.

Sahihi

Tarehe
TABARUKU

Ninapenda kuitabaruku utafiti huu kwa wazazi wangu wapendwa Fred Chesang na Hellen Andiema
Chelagat na ndugu zangu Shadrack Jovial Kiptoo na Pauline Cherop.

Pia ninaitabaruku kwa wanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Turkana na wanafunzi wenzangu
wa Kiswahili katika chuo kikuu chaTurkana.
SHUKRANI

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Maulana kwa uhai,uwezo na afya katika kipindi chote cha
masomo na utafiti huu.Ashukuriwe kwani yeye ndiye muweza yote.

Shukrani zangu za dhati kwa msimamizi wangu Bi.Naumi Chepkemoi kwa kuisimamia kazi hii tangu
mwanzo.

Kwa njia ya shukrani tu ningependa kukumbuka mijadala ya kina kirefu niliyoyafanya na Dkt.Evelyne
Kanus,Bw.Edward Lokidor na Bw.Simon Ekiru.Kwa hakika mijadala hii imenipa upeo mpana na
uwanda nilikuwa nikushughulikia.

Shukrani nyingine zinawaelekea wasimamizi wa elimu katika kaunti ya Turkana,kwa kunisaidia na


kuniruhusu kuvitumia vifaa na kuvitafiti sehemu Fulani katika eneo hilo.
IKISIRI

Mada ya utafiti huu ni kuchunguza athari na sababu za utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa
wanafunzi wa shule za upili.

Utafiti huu utafanywa katika eneo la Turkana Mashariki katika shule la wasichana ya Turkana.

Utafiti huu umebaini kuwa wanafunzi wa shule za upili haswa wa kidato cha pili na tatu ndio wenye
uraibu wa matumizi za dawa za kulevya kwa wingi bila kujali athari zake.Tutachunguza kwa kina
sababu zinazowapelekea kufanya hivyo ikiwa miongoni mwa;ilhamu ya kutaka kujua au kuvionja na
pia kutumwa kuvinunua,matangazo yanayopendeza na kuiga kutoka kwa watu wengine.
YALIYOMO

UTHIBITISHO………………………………………………………………………………………………………………………………2

HATIMILIKI…………………………………………………………………………………………………………………………………3

TAMKO………………………………………………………………………………………………………………………………………4

TABARUKU……………………………………………………………………………………………………………………………….5

SHUKRANI……………………………………………………………………………………………………………………………….6

IKISIRI………………………………………………………………………………………………………………………………………7

YALIYOMO……………………………………………………………………………………………………………………………….8
SURA YA KWANZA

1.0 Utangulizi………………………………………………………………………………………………………..11
1.1 Usuli wa mada……………………………………………………………………………………………11
1.2 Tamko la utafiti…………………………………………………………………………………………11
1.3 1Malengo ya utafiti……………………………………………………………………………………….11
1.4 Lengo la utafiti………………………………………………………………………………………………..12
1.5 Malengo ya utafiti………………………………………………………………………………………….12
1.6 Maswali ya utafiti…………………………………………………………………………………………12
1.7 Nadharia tete……………………………………………………………………………………………………..12
1.8 Umuhimu wa utafiti………………………………………………………………………………………………12
1.9 Vikwazo vya utafiti………………………………………………………………………………………………13

1.10 Vifaa vya utafiti……………………………………………………………………………………………………13

1. 11 Hitimisho………………………………………………………………………………………………………………13

SURA YA PILI

2.0 Mapitio ya kazi tangulizi…………………………………………………………………………………………………..14

2.1 Utangulizi………………………………………………………………………………………………………………………14

2.2 Kazi za kijumla zinazoshughulikia swala la dawa za kulevya…………………………………………………14

2.3 Kazi mahususi zinazochunguza suala la dawa za kulevya……………………………………………………14

2.4 Kiunzi cha nadharia……………………………………………………………………………………………………………15

2.4.1 Nadharia ya mguso……………………………………………………………………………………………………………15

2.4.2 Nadharia ya utegemezi………………………………………………………………………………………………………15

2.5 Hitimisho……………………………………………………………………………………………………………………………
15…

SURA YA TATU

3.0 Utangulizi………………………………………………………………………………………………………………………………16
3.1 Mbinu za utafiti……………………………………………………………………………………………………………………16

3.2 Mbinu za kukusanya data …………………………………………………………………………….16


3.2.1Dodosi……………………………………………………………………………………………………………16

3.2.2 Hojaji……………………………………………………………………………………………………………16

3.2.3 Usaili au mahojiano………………………………………………………………………………………17

3.3 Data ya awali………………………………………………………………………………………………..17

3.4 Sampuli nan jia za usampulishaji……………………………………………………………………18

3.4.1 Kundi lengwa…………………………………………………………………………………………………18

3.4.2 Uteuzi wa sampuli…………………………………………………………………………………………18

3.5 Mkabala wa utafiti……………………………………………………………………………………………18

3.6 Vifaa vya utafiti…………………………………………………………………………………………………18

3.7 Eneo la utafiti………………………………………………………………………………………………………19

3.8 Hitimisho………………………………………………………………………………………………………………19

SURA YA NNE

4.0 Uwasilishaji,uchambuzi na mijadala za data ya utafiti………………………………………………20

4.1 Utangulizi………………………………………………………………………………………………………………20

4. 2 Idadi kamili ya wanafunzi wanaotumia dawa za kulevya katika shule ya wasichana ya


Turkana………………………………………………………………………………………………………………………………20

4.3 Tamko la serikali na shirika la afya mkoani…………………………………………………………………20

4. 4 Maoni ya taasisi mbalimbali………………………………………………………………………………………21

4.4.1 Maoni ya vituo vya afya………………………………………………………………………………………………21

4.4.2 Chama cha walimu……………………………………………………………………………………………………..21

4.5 Mapendekezo…………………………………………………………………………………………………………………21

4.6 Hitimisho…………………………………………………………………………………………………………………………21

SURA YA TANO

5.0 Muhtasari,hitimisho,na mapendekezo………………………………………………………………………………22


5.1 Utangulizi………………………………………………………………………………………………………………………………22

5.1.1 Kueleza mbinu ambazo wanafunzi hupata dawa……………………………………………………………………22

5.1.2 Madhara za dawa za kulevya kwa wanafunzi…………………………………………………………………………22

5.1.3 Kuchanganua idadi ya walioathirika………………………………………………………………………………………23

5.2 Hitimisho…………………………………………………………………………………………………………………………………23

5.3 Mapendekezo…………………………………………………………………………………………………………………………24

5.3.1 mapendekezo kwa wanafunzi………………………………………………………………………………………………24

5.3.2 mapendekezo kwa walimu na walimu wakuu………………………………………………………………………24

5.3.3 mapendekezo kwa wazazi…………………………………………………………………………………………………….24

5.3.4 mapendekezo kwa serikali…………………………………………………………………………………………………….25


SURA A KWANZA

1.0 UTANGULIZI

1.1 Usuli wa mada

Sura hii ya kwanza inaeleza kuhusu uwanja wa tatizo ,tatizo la utafiti,malengo ya utafiti,nadharia ya
utafiti na hitimisho.Katika sura hii ,nitachunguza athari na sababu za utumizi wa dawa za kulevya
miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili .Imebainika kuwa ili kijana yeyote ahisi kuwa ana sehemu
au kuwafanana wengine katika jumuiya ya vijana wenzake ,aghalabu huishia kujiingiza matumizi ya
dawa za dawa za kulevya kwa jino na ukucha .Taasisi za elimu ndizo ambazo zimegeuka lindi la
matumizi ya dawa za kulevya.

Ni idadi au asilimia kidogo sana ya vijana ndio huweza kujiepusha na utumiaji huu wa dawa wa
kulevya na kuendelea na masomo yao vyema na hatimaye kufua dafu,ilhali wengine huathirika
vibaya sana na hivyo kukosa kuendeleza masomo yao na hata wakaathirika kiafya.

Tatizo hilo ndilo linalinifanya kufanya utafiti katika kuona ni jinsi gani vijana watafahamishwa ili
waweze kuepuka na utumiaji wa dawa za kulevya .Hili linaweza kuafikiwa ikiwa wataelekezwa
athari na madhara za dawa za kulevya.

1.2 Tamko la utafiti

Tatio la utafiti huu ni kuchunguza sababu zinazochangia wanafnzi kutumia dawa za kulevya na mbinu
za kuziepuka na pia kufahamu athari za dawa hizi.Nitachunguza na kufafanua matatizo
yanayowakumba vijana haswa wa kidato cha pili na tatu.
Nitajadili na kueleza mbinu tofauti zitakazotumiwa ili kusaidia wanafunzi kuepuka na madhara hayo
na utumizi wa dawa hizi za kulevya haswa pombe na bangi.

1.3 Malengo ya utafiti

Katika utafiti huu ,malengo yatagawika au kugawanywa katika ;lemgo kuu na lengo mahususi

1.4 Lengo kuu

Lengo kuu la utafiti huu ni kuchanguza athari za dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi.

Sababu zinazowapelekea wanafunzi kutumia dawa za kulevya.

1.5 Malengo mahususi

-Kuchunguza jinsi wanafunzi wa shule za upili haswa zile za bweni kupata dawa hizi za kulevya
wakiwa humu shuleni.

-Kuainisha madhara wanayopokea wanafunzi hawa haswa kwa kutotimiza malengo yao pale shuleni
ya kufanya vyema kwenye mtihani yao.

-Kuonyesha idadi kamili ya wanafunzi walioathirika na matumizi haya ya dawa za kulevya na


kuonyesha jinsi walivyoathirika.

1.6 Maswali ya utafiti

Dawa za kulevya zimechangia vipi katika kutokufaulu kwa wanafunzi?

Je,madhara ya dawa ya kulevya ni yepi?

Dawa hizi za kulevya ina manufaa gani kwa wanaotumia na faida zake ni zipi?

1.7 Nadharia tete

Kulingana na Enon (1995) anaeleza kuwa nadharia tete ni mabunio ya matokeo tarajiwa ya utafiti
unaokusudiwa kufanywa.

Utafiti huu unaongozwa na nadharia tete zifuatazo;

-Athari na madhara ya dawa ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi.

-Sababu zinazochangia katika kutumia dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi.


1.8 Umuhimu wa utafiti

Utafiti huu una umuhimu ufuatao;

-Kusaidia katika kutafuta mikakati na mbinu maalum itakayosaidia katika kupunguza matumizi ya
dawa za kulevya shuleni.

-Kuwafahamisha wanafunzi athari za kutumia dawa za kulevya ikiewemo ;kutofanya vyema


masomoni,kuwadhuru kiafya na huenda wakapata madhara baadaye.

-Kusaidia kuendeleza tafiti nyingine katika wilaya ya Tuukana haswa miongoni mwa shule za upili
kama vile shule ya wasichana ya Lodwa na zingine.

1.9 Vikwazo vya utafiti

Katika utafiti huu kuna baadhi ya vikwazo mbalimbali ambazo nitakumbana nazo katika ukusanyaji
wa taarifa zake;

Utafiti unakumbwa na shida ya usafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine ikizingatiwa kuwa shule hii
ya wasichana ya Turkana imo katika sehemu inayokumbwa na shida ya usafiri barabara zikiwa katika
hali isiyopendeza.
SURA YA PILI

2.0 Mapitio ya kazi tangulizi

2.1 utanguliz

Mapitio ya kazi tangulizi ni usomaji wa vitabu vilivyoandikwa kuhusu mada ninayoifanyia utafiti.

Katika utafiti huu nitapitia kazi tangulizi ambazo zinazungumzia juu ya matumizi na athari ya dawa
za kulevya ,miongoni mwa wanafunzi.

Hii ni kuniwzesha kubainisha pengo la kiutafiti ambao ndilo haswa nitakalotafiti .Nitaanza na kazi
tangulizi ambazo zilichunguza sababu na athari za dawa za kulevya.

2.2 Mapitio ya kazi tangulizi

Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka wa 1957 wanasema kuwa matumizi ya dawa ya
kulevya ni hali ya ulevi wa muda au kila mara unaotokana na matumizi ya mara kwa
mara.Wanasisitiza kuwa hali hii huweza kuwa utegemezi ambayo huwa vigumu kufanya bila
matumizi ya dawa hizi.

Wanaeleza kuwa ni nadra sana kupata hali ambapo kitu chochote kinachoingizwa mwilini
kitashindwa kuwasababisha baadhi ya watu kuathirika na msisimko wa kuridhika au kufurahia,kwa
namna inayowashawishi kuendeleza matumizi yake hadi kufikia kiwango cha matumizi
mabaya.Yaani kutumia kupita kiasi au kutumia zaidi ya inavyohitajika.

Wanasayansi na waandishi wengine ,kuruhusudhana ya matumizi ya dawa za kulevya kujumuisha


watu ambao si watumiaji dawa za kulevya ,kulingana na ufafanuzi wa shirika la Marekani la Tiba za
ulevi.
Fafanuzi za miaka ya 1957 na1964 za matumizi ya dawa za kulevya,utegemezi,na utumiaji mbaya
umeendelea kudumu hadi sasa katika vitabu vya kiutabibu.Inafaa kukumbukwa kuwa mwongozo
utambuzi wa takwimu (DSM-IV-TR) kwa sasa(2006) unatoa vigezo maalum vya kufafanulia matumizi
mabaya ya utegemezi

(DSM-IV-TR) hutumia istilahi utegemezi wa vileo badala ya matumizi ya vileo miongoni mwa
wanafunzi,ambao ni uigaji mbaya wa mkondo wa vileo ,unaosababisha kuathirika vibaya kiafya au
dhiki ,kama ionekanavyo na vigezo vitatu au zaidi vilivyopendekezwa,kuanzia Watoto katika kipindi
kimoja cha miezi 12.Ufafanuzi huu pia huweza kutumika kwa dawa za kulevya zenye ishara ndogo au
zisizoonekana za kimwili,baada ya kuacha kwa mfano bangi.

Kwa hivyo nakubaliana na mawazo ya wataalamu kuwa utumizi wa dawa za kulevya huweza kuzua
utegemezi miongoni mwa wanafunzi au watumizi na kuwa vigumu kuyaacha .

Madhara yake huweza kuwa za kiafya n ahata za kisaikolojia.

2.3 Nadharia

Nadharia ni mwongozo uliondaliwa kwa ajili ya kuwezesha shughuli fulani kufanikiwa kama
ilivyokusudiwa. Kwa mfano, katika kufanya utafiti wake ili kufanya afanikiwe vizuri na aaminike.

Utafiti huu utaongozwa na nadharia ya mguso na utegemezi.

2.3.1 Nadharia ya mguso

Nadharia hii inaeleza kuwa mtu anapohusishwa kwa ukaribu na dawa za kulevya au na mtu
anayezitumia dawa hizi pia huenda akapata mhilamu wa kujaribu kuvitumia. Hii pia hutokana na hali
ya wazazi kuwatuma Watoto kuwanunulia dawa hizi.

Wanapotazama televisheni na kuona Habari zinazovutia na kupendeza huweza kufurahishwa na


hivyo kuwapelekea kutaka kuvitumia.

2.3.2 Nadharia ya utegemezi

Shirika la afya duniani (WHO) kuhusu dawa zinazosababisha utegemezi wa kulevya walifafanua
utegemezi kwa vileo na uzoevu kama sehemu ya matumizi mabaya za dawa za kulevya.

Matumizi ya dawa za kulevya ni hali ya ulevi wa muda au kila mara unaotokana na matumizi ya mara
kwa mara ya dawa (asili au sanisi) sifa zake ni Pamoja na;
i. Utashi mkubwa au uhitaji wa kuendelea kutumia dawa za kulevya na kuitafuta kwa njia
yoyote ile.
ii. Utegemezi wa kiakili
iii. Tabia ya kuongeza kiwango.

Neno utegemezi wa dawa za kulevya, hatimaye hutumika kama kategoria ambayo ianaweza
kujumuisha wale watu ambao, chini ya DSM IV , wanaweza kutambuliwa kama wategemezi wa vileo
au watumiaji wa vileo hivi vibaya (DSM-IV }

2.4 Hitimisho

Mapitio kuhusiana na mada ya utafiti yalibainisha kwamba, kazi za kutumia au utumizi wa dawa za
kulevya, zinaweza kuwekwa kwa makundi mawili sababu zinazochagia utmuzi na athari
zinazottokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Ilibainika kuwa hali ya kuwa na mgusano au kukaribiana na dawa hizi huchangia pakubwa. Pia
hutegemezi wa dawa hizi hutokana na kuvitumia mara kwa mara.

Katika sura ifuatayo, utafiti wa awali na mbinu za utafiti zitashughulikiwa ili kubaini jinsi utafiti wa
awali ulivyofinikishwa.

Aidha, mbinu zilizotumika katika utafiti kamili, uchanganuzi wa dawa na matatizo yatajadiliwa kwa
uketo.
.

SURA YA TATU

3.0 MBINU ZA UTAFITI

3.1 Utangulizi

Mbinu za utafiti ni kama kanuni au sheria ambazo zitatumiwa kutuelekeza au kufuatwa katika hatua
za hutafiti wa kitaalamu ili kufanya utafiti huu huweze kuaminiwa. Katika utafiti huu data
zitakusanywa kutoka kwa wanafunzi pamoja na waalimu wa wilaya ya Turkana haswa shule ya
wasichana ya Turkana.

3.2 Mbinu za kukusanya data

Ukusanyaji wa data utafanywa katika wiliya ya Turkana ,mkoa wa Turkana mashiriki katika shule ya
wasichana ya Turkana.

Nitawashirikisha wafuatao; mimi kama mtafiti, waalimu wa shule hiyo, wazazi wa wanafunzi na
wanafunzi wa kidato cha pili na wa tatu.

Nitatumia mbinu ya hojaji na dodoso katika kukusanya data kwa kuwa ni mbinu rahisi na huweza
kuchukua muda mfupi wahojiwa huweza kujibu maswali bila uoga wa kujulikana.

Mbinu hii pia huweza kutupa taarifa kamili.

3.3 Data ya awali

Nitakusanya data kutoka kwa kiongozi wa Afya anayewakilisha vijana na pia wakuu wa elimu. Utafiti
huu utafanyika tarehe 18/08/2022 hadi 25/09/2022. Katika shule ya wasichana ya Turkana.

Shule hii iliteuliwa kwa sababu iliweza kuripoti idadi kubwa ya wanaotumia mihadharati.
Madhumuni ya utafiti huu ni kufanyia majaribu mbinu za utafiti uliokuwa umependekezwa
kutumika.

3.4 Dodoso

Utafiti huu utakuwa wa aina mbili .Dodoso la aina ya kwanza itakuwa na maswali 10 za walimu
katika shule ya Turkana na pia miongoni mwa viongozi wa wilaya.
Dodoso la pili litaandaliwa kwa ajili ya wanafunzi katika shule ya upili ya Turkana.

3.5 Hojaji

Haya ni maswali yanayoandaliwa au yanayohusiana na suala linalotafitiwa ambayo mimi kama


mtafiti hutoa kwa miniajili ya kuibua,majibu,maoni,mtazamo na mikabala mahususi kuhusu mada ya
utafiti.

Nitaanza na maswali rahisi kisha yale magumu .Katika hojaji hizi aina ya kwanza ni hojaji funge nay a
pili ni maswali wazi.

Maswali wazi itawapa nafasi ya kujieleza kulingana na maswali ya mtafiti.

Mbinu hii ya kukusanya data itasaidia katika kupata maswali yanayokusudiwa kwa kuwa

-huweza kukusanya data kutoka kwa kundi kubwa.

-data zake huchanganuliwa kwa urahisi

-ina usuli wa majibu

-inatumia wakati mfupi sana haswa maswali yap apo.

3.3.2 Usaili au mahojiano

Ni mbinu ya kutumia maswali ya ana kwa ana au moja kwa moja kwa mbinu ya majibizano.Huweza
kuwa baina ya mtu na mtu na kikundi .

Mahojiano yaweza kuwa ya ana kwa ana kama vile mtafiti na mtafitiwa .

Pia huweza kuendelezwa kwa njia ya simu.

Katika utafiti huu nitatumia mahojiano ya ana kwa ana baina ya mtafitiwa mmoja mmoja .Maswali
yataandaliwa na pia mwongozo wao.Kinasa sauti kitatumika kurekodi majibu ya watafitiwa ili
kuhifadhi kumbukumbu.Pia ninahitaji daftari ili kuepuka utepetevu iwapo kinasa sauti kitakua na
hitilafu.

Faida ya mbinu hii ni kuwa huchukua muda mfupi.

Humpa mtafitiwa muda wa kueleza na kutoa ufafanuzi wa hoja zake.

Mtafiti huweza kutoa maswali ya ziada kuliko yale yaliyoandaliwa.

3.3 Data msingi


Data msingi ni data ambazo zinapatikana moja kwa moja kutoka kwa mtafitiwa .

Kulingana na utafiti huu,nitatumia data msingi kwa upana zaidi .

Nitakusanya data za msingi kutoka kwenye eneo linalokaribu na shule hii,eneo ya Loima ili kuweza
kuelewa mtazamo wake kuhusu jambo hilo.

Pia nitawatembelea watafitiwa ambao ni wanafunzi ili kupata taarifa nitakazo tegemea kuendeleza
utafiti huu.

3.4 Sampuli nan jia ya usampulishaji

3.4.1 Kundi lengwa

Hili ni kundi ambalo mtafiti anakusudia kupata habari kutoka kwao.Hii ni kundi wakilishi kutoka
katika jamii hiyo pana ninayoshughulika nayo,nitazingatia uteuzi sampuli wa mtabakisho katika
hatua ya kwanza ,kufanya hivi,kutaniwezesha kupata vijisehemu vilipo kundi wakilishi.Kwa muktadha
huu,vijisehemu hivi vitajumuisha idara zote za kiakademia zinazopatikana katika shule hiyo.

Hatua itakayofuatia katika uteuzi wa sampuli itakuwa uteuzi wa sampuli kimaksudi .Hatua hii
itaniwezesha kupata walengwa binafsi ili kuwahoji.Kwa sababu ya wingi wao,nitateua tu walengwa
sita kutoka kila idara na skuli huku nikizingatia usawa wa jinsia miongoni mwa walimu.

3.4.2 Uteuzi wa sampli

Ili kupata kundi wakilishi ,kutoka kwa jamii pana la wanafunzi na walimu ,nitatumia sehemu tu ya
wanafunzi mle shuleni ,wanafunzi mle shuleni wakiwa zaidi y amia saba ,wanafunzi kumi tu ndio
watakaotumika.

Mbinu ya usampulishaji wa kukusudia na wa idadi isiyo kamili itatumika.

Hatua itakayotumika zaidi katika uteuzi wa sampuli itakuwa uteuzi sampuli kimaksudi .Mtindo huu
utaniwezesha kupata walengwa binafsi ili kuwahoji.

3.5 Mkabala wa utafiti

Kuna mikabala miwili mikuu ,ule wa kiidadi na wa kimaelezo (au usio wa kiidadi) mkabala wa kiidadi
hutumia rekodi na taarifa na kuchanganuliwa kwa kutumia takwimu,mkabala usio wa kiidadi ni
mbinu ya kuchunguza data ambayo mtafiti hueleza na kufafanua data zake kwa kutumia maele

Katika utafiti huu nitatumia mkabala wa kimaelezo kwa sababu utafiti huu hulenga jinsi mambo
yalivyo pasipo kubadili.
3.6 Vifaa vya utafiti

Hivi ni vile vyombo vitakavyotumika katika kukusanya data kuhusu mada inayotafitiwa.hivi ni kama
vile vitabu vya kunakili habari muhimu,kalamu,kinasa sauti cha kurekodi habari muhimu wakati wa
mahojiano.

Kutahitajika vifaa vya ziada ili kuepuka utepetevu ikiwa vifaa hivi vitaharibika au kupata hitilafu
wakati wa kukusanya data.

3.7 Eneo la utafiti

Utafiti huu umefanywa katika nchini Kenya,katika kaunti ya Turkana,eneo la Turkana mashariki ,eneo
ndogo ya Loima.Katika shule ya wasichana ya Turkana.

3.8 Hitimisho

Utafiti wa awali ulikuwa dira itakayo msaidia mtafiti kusanifu mbinu za kutumia katika utafiti
kamili.Aidha ,utamsaidia kuelewa hali halisi ya nyanjani na aina za data ambayo angekusanya wakati
wa utafiti kamili.

Utafiti kamili utafanywa nyanjani ,utafanya katika eneo la Turkana,Mashariki .mbinu za ukusanyaji
data ni mahojiano,dodosi,hojaji na sampuli.

Data itakayopatikana kutokana na utafiti huu utachanganuliwa kwa maelezo,matumizi ya vijalizo vya
kuchunguza maneno Pamoja na kutumia kigezo cha asilimia.
SURA YA NNE

4..0 UWASILISHAJI, UCHAMBUZI NA MIJADALA YA DATA.

4.1 Utangulizi

Data zilizokusanywa kwa kupitia mbinu mbalimbali zilichambuliwa na kuchanganuliwa kwa makini
sana.

Data hizo ziliwekwa katika asilimia ili kurahisisha usomaji wa maudhui yatokanayo na
uchambuzi,data zilizokusanywa zinakusudia kujibu mada ya utafiti,tatizo la utafiti,nia kuu,
maudhumuni ya utafiti,na maswali ya utafiti.

Katika sura hii nimewasilisha nilichokipata shuleni ,miongoni mwa walimu,wazazi na wilaya ya elimu
mkoani.

4.2 Idadi kamili ya wanafunzi wanaotumia dawa za kulevya

Katika shule ya wasichana ya Turkana matokeo yalikuwa kama yafuatayo;

-Idadi kamili ya wanafunzi wote ni 768 ambayo ni asilimia 100.

Shule hii ina mikondo minne katika kila kidato,ambayo ni mashariki,magharibi,kati na kusini kuanzia
kidato cha kwanza hadi cha nne.

Wanafunzi wakiwa 48 katika kila mkondo.

Katika asilimia yote ,ilibainika kuwa wale waliokuwa wameacha shule na wengine kufukuzwa
kutokana na mienendo mibaya ni asilimia nane ambayo ni wanafunzi 61.

Katika kidato cha pili mashariki ilikuwa na asilimia kubwa ya visa vya utovu wa nidhamu na kubakiwa
wanafunzi 30 ambayo ni asilimia 66 huku asilimia 34wakiwa waliopatikana na visa vya utovu wa
nidhamu.

4.3 Tamko la serikali

Baaada yakutembelea ofisi mbalimbali za serikali ilibainika kuwa idadi kubwa ya watafiti walikuwa
wamewasilisha hoja saw ana hio wakiwa jumla ya 14, ilibainika kuwa tatizo hili liliwakumba
wanafunzi wengi na kuwa chanzo cha matokeo mbaya. Asilimia 4 walisema kuwa baadhi ya dawa
zilikuwa na manufaa kwa wanafunzi kwani iliondoa uchovu lakini asilimia 96 ilipinga madai hayo na
kuunga kuondolewa kwa dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi.

Wakuu wa mikoa,walimu na hata Waziri wa elimu aliweza kupendekeza kuwa


-wanafunzi wafanyiwe msasa na kupimwa kabla ya kuingia shuleni

-Atakaye patikana na dawa za kulevya achukuliwe hatua kali.

-Wanafunzi watengewe muda wa kufanya mazoezi.

-Walimu na wafanyakazi wote watengewe nafasi shuleni.

4.4 Maoni ya taasisi mbalimb ali

4.4.1 Vituo vya afya

Wanafunzi wote wahakikishe kuwa vipimo kamili na sahihi zinachukuliwa katika vituo vya afya
vinavyotambulika na kupewa ripoti kamili kuhusiana na afya yao.

Taarifa hizi waziwasilishe shuleni kabla ya kuruhusiwa kuingia shuleni.

4.4.2 Chama cha walimu

Walimu wote walishauriwa kuhakikisha kuwa wanazifuata kanuni zinazowaongoza ‘Code of conduct’
na kujitenga na visa vyovyote vitakavyowapelekea kuadhibiwa.

Walihitajika kuwaongoza wanafunzi katika njia zinazohitajika.

Mwalimu yeyote ambaye angepatikana na hatia yoyote atahudumia kifungu cha miaka kadhaa
gerezani.

4.5 Mapendekezo

Kutokana na utafiti huu,mtafiti ninapendekeza kuwa dawa za kulevya ziondolewe na kupigwa


marufuku miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili na hatua kali kuchukuliwa kwa yeyote
atakayepatikana na hatia yoyote.

4.6 Hitimisho

Sura hii imefanya uwasilishaji wa data na kutambua kuwa visa vya matumizi ya dawa vinaongezeka
kila kuchao na kusababisha kudorora kwa matokeo ya wanafunzi.Kinachosikitisha ni kuwa wanafunzi
na baadhi ya walimu wanashuhudia visa hivi lakini hawafanyi lolote ila wanadhani kuwa ina manufaa
kwa masoma yao.

Baadhi ya walimu huwasaidia wanafunzi katika kuvipata bidhaa hivi.Ni jukumu letu sasa kwa
ushirikiano kuhakikisha kuwa jambo hili linafika kikomo katika taasisi zote za elimu.Sura inayofuata

muhtasari,hitimisho na mapendekezo.
SURA YA TANO

5.0 MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO.

5.1 Utangulizi

Sura hii inafanya muhtasari,hitimisho na mapendekezo ya utafiti mzima.Utafiti huu unakusudia


kutoka majibu kuhusu maswala yafuatayo;

-kueleza mbinu ambazo wanafunzi haswa wale wa shule za bweni huweza kupata dawa hizi za
kulevya wakiwa mle shule ndani.

-kuainisha madhara wanayopokea wanafunzi hawa haswa kwa kutotimiza malengo yao pale shuleni.

-kuorodhesha idadi kamili ya wanafunzi walioathirika katika shule ya wasichana ya Turkana kutoka
na madhara ya dawa za kulevya.

Ufafanuzi wa maelezo haya ni kama yafuatayo;

5.1.1 kueleza mbinu ambazo wanafunzi huweza kupata dawa za kulevya wakiwa shuleni

Kulingana na utafiti huu ,ilibainika kuwa wanafunzi wengi ya bweni ndio waliopatikana wakitumia
dawa hizi za kulevya ilhali huwa shuleni mchana kutwa na usiku kucha huku wakiwa chini ya ulinzi
mkali wa walimu na walinzi wa shule.Iliweza kubainika kuwa miongoni mwa wanafunzi hawa
waliweza kupata dawa kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa mle shuleni na huku wakiwauzia kwa
bei isiyo ghali huku wanafunzi wakichukua kwa wingi sana.

Iliweza kuorodheshwa baadhi ya walimu waliwapa wanafunzi ruhusa bila ya kujua walipokuwa
wakielekea ,hivyo wanafunzi walionekana wakizurura kule mitaani na haswa kwenye vibanda
vilivyodhaniwa kuuza dawa za kulevya.

Kulegezwa kwa sheria inayowazuia wanafunzi kuingia shuleni na bidhaa vya kila aina watokapo
nyumbani na baada ya tamasha tofauti nje ya shule kulichangia dawa kuletwa shuleni.
Iliweza kubainika kuwa wageni haswa wazazi,Rafiki na jamaa za wanafunzi waliruhusiwa
kuwatembelea wanafunzi wakati wowote na bila kuchunguzwa kabla kuingia shulei,jambo hili pia
ilichangia kuwepo kwa dawa miongoni mwa wanafunzi.

5.1.2 Madhara ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi

Baada ya kuendeleza utafiti huu iliweza kubainika kuwa wanafunzi wengi walikuwa wakidhibitisha
taabia Fulani ambazo ziliashiria kubadilika kwa hali ya kawaida ya wanafunzi wakiwa darasani na
hata katika kushirikiana na wanafunzi wenzao na hata walimu.

Wanafunzi wengi walionekana kutotia makini katika masomo yao darasani na kutumia muda mwingi
wakisinzia wakiwa darasani,kutokamilisha mijarabu yao waliyopewa na wanafunzi,wengi wakakosa
heshima na hata kutaka kupigana na walimu.

Matokeo katika mijarabu na hata mitihani yalikuwa hayapendezi.

Visa vya wanafunzi kuwaibia wengine viliongezeka ili waweze kupata fedha vya kununua dawa za
kulevya.

Wanafunzi wengine walitoroka shuleni na kuacha masomo kwa kukata tamaa ya masomo kwa
kutokufanya vyema masomoni.

5.1.3 KUchanganua idadi ya wanafunzi waliweza kuathirika na madhara ya dawa za kulevya

Ilibainika kuwa katika asilimia mia moja ya wanafunzi darasani asilimia kumi tu ndio ilibainika
kutotumia dawa za kulevya.

Wanafunzi waliweza kutoa sababu tofauti za kutumia dawa za kulevya,wengine wakisema kuwa
iliwasaidia kupunguza usingizi ili waweze kupata muda wa kutosha wa kusoma.

Wengine walisema kuwa dawa zilikuwa na manufaa kwa kuwa iliwasaidia kuweza kusahau shida zao
za nyumbani kwa mfano ukosefu wa mahitaji tofauti na kuweza kujihisi vyema.

5.2 Hitimisho

Utafiti uliweza kutambua kuwa asilimia ya wanafunzi katika shule ya upili waliweza kutumia dawa
hizi za kulevya aidha kwa kutaka au kwa kulazimishwa na mazingira yao kwa mfano;

-kazi ngumu na nyingi za shuleni zinazowafanya kutaka wakati wa kuweza kukamilisha kazi
wanazopewa na walimu na hivyo kutaka dawa ya kuwazuia kupata usingizi.

-kuiga tabia za wanafunzi wengine wanaowazunguka na hata wazazi wao.


Utafiti uliweza kutambua kuwa wazazi Pamoja na walimu walikuwa na zoezi kubwa ya kuhakikisha
kuwa wanafunzi wanazuiliwa na kujiingiza na uraibu wa aina hii na kuhakikisha kuwa
wanachunguzwa kila mara wakiwa shuleni na hata nyumbani.

Wanafunzi walitambulika kuwa walikuwa na dhana kuwa dawa hizi zilikuwa na manufaa katika
masomo yao ambayo hawakuweza kuzingatia madhara ya dawa hizi za dawa za kulevya.

Wanafunzi wangefundishwa madhara ya dawa hizi za kulevya na kuwasaidia wale waliokuwa


wameathirika kuepuka au kuweza kurekebisha tabia zao na kuweza kufanya vyema katika masomo
yao bila kuhitaji kutumia dawa hizi za kulevya.

Ili kuweza kusaidia kuhakikisha kuwa tabia au uraibu wa dawa hizi zinaafikiwa kulihitaji kushirikiana
kwa taasisi mbalimbali na hata katika viwango vya mtu binafsi.

Tatizo hizi zilitambulika kuwa ni tatizo iliyozikumba shule nyingi kwenye taifa nzima na hata nchi za
kigeni na hivyo mapendekezo kutolewa ili kushughulikia swala hili kwa ushirika.

5.3 Mapendekezo

Kutokana na matokeo ya utafiti huu,mapendekezo yalitolewa kwa makundi yafuatazo;

5.3.1 Kwa wanafunzi binafsi

Wanafunzi waweze kutambua madhara ya dawa za kulevya na kuelewa kuwa manufaa ni chache na
za muda

sana.

Wanafunzi waweze kujitenga na vikundi ambavyo vinatishia tabia zao.

Wanafunzi waweze kutumia wakati wao vyema ili kuweza kukamilisha kazi zote kwa wakati ufaao.

5.3.2 Kwa walimu wakuu na walimu wote .

Walimu wakuu waweze kuwachunguza wanafunzi vyema kabla ya kuingia shuleni na sheria kali za
kuwazuia kuingia shuleni wakati wowote ule kutoka kwa wazazi au jamaa.

Walimu waweze kutambua tabia zisizo za kawaida na kuchukua hatua .

Sheria zitolewe na mwalimu ili kuwazuia wafanyakazi shuleni kuwauzia wanafunzi bidhaa yoyote ile
shuleni.
5.3.3 Kwa wazazi

Wazazi waweze kuwachunguza Watoto wao vyema wakiwa nyumbani na wanapoenda shuleni.

Waweze kuepuka na matumizi ya dawa hizi kwa kuwa wanafunzi huweza kuiga tabia hizi.

5.3.4 Kwa serikali.

Serikali iweze kutoa sheria ili kuweza kuzuia wanafunzi kuuziwa dawa za kulevya na yeyote
yule,yule atakaye patikana na makosa ya kuwauzia wanafunzi dawa za kulevya atapigwa adhabu kali
au kufungwa kwa muda mrefu na kutumikia kifungu.

5.4 Mapendekezo kwa tafiti zijazo

Tafiti zijazo zinapendekezwa kushughulikia sababu na madhara ya dawa za kulevya miongoni mwa
wanafunzi wa vyuo vikuu na njia mwafaka za kuhakikisha kuwa suluhisho linapatikana katika
kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi hawatumii tena dawa za kulevya na kuendeleza
uchunguzi huu kwa jamii nzima,kwa kuwahamasisha watu wote.

MAREJELEO

-DSM-IV&DSM-IV-TR; Utegemezi wa vilewevu .Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-09-27.Ikiwemo


mnamo 2010-11-06.

-Boobs G,Kreeks MJ (2007). ‘Stress,dsyregulationof drug pathways,and transition to drug


dependa’ce'AM J Psychiatrist.

‘-Fafanuzi kuhusiana na matumizi ya Opiodi kwa kutibu ya matumizi,2001. Chuo cha Marekani ya
kutibu maumivu,Chama cha maumivu cha marekani.
-Nils Bejerot katika Nadharia za matumizi mabaya ya dawa za kulevya ,baadhi ya mitazamoya kisasa
9 Mei 2009 at Weyback machine ,ukurasa wa 246-255,NIDA,198

-Kalivas PW,Volkow ND(2005) ‘THE Neural basis of addiction;a pathology motivation and choice.

-The science behind drug use and addiction Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-11-0

-Mikabala ya matibabu kwa utegemezi wa dawa za

Kulevya 17 oktoba 2010 at Weyback Machine Taasisi ya dawa za kulevya.

KIAMBATANISHI

HOJAJI

1.Jina la shule……………………………………………………………………………………………………

2.Eneo la shule……………………………………………………………………………………………………

3.Mwaka wa utafiti…………………………………………………………………………………………….

4.Tarehe ya utafiti………………………………………………………………………………………………..

Katika maswali yanayofuatia jibu la au ndio

(kwa walimu na mwalimu mkuu)

(a) Je,unadhani kuwa dawa za kulevya yana madhara yoyote kwa matokeo ya wanafunzi?
(b) Je unazitambua dalili za utumiaji wa dawa za kulevya?.....
(c) Unatambua kuwa ni jukumu lako kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanya vizuri katika
masomo yao?
(d) Umewahi kuzitambua dalili zozote za utumizi wa dawa za kulevya unapokuwa darasani?
(e) Je ,kuna uwezekano kuwa wanafunzi wana zitumia dawa za kulevya?
(f) Kama viongozi wa wanafunzi,tutashirikiana kupata mbinu za kuwarekebisha wanafunzi?
(kwa maswali yanafuata toa maelezo panapohitajika)
(g) Ni nini haswa chanzo cha matokeo mabaya miongoni mwa
wanafunzi?..............................................................................................................
(h) Eleza baadhi ya dalili za utumizi wa dawa za
kulevya………………………………………………………………………………………………..
(i) Fafanua mienendo ambazo hazipendezi miongoni mwa
wanafunzi……………………………………………..
(j) Kama walimu ni juhudi gani tunazotia kuhakikisha kuwa tunaangamiza matumizi ya dawa
hizi…………………………………………………………………………………..

(maswali kwa wanafunzi)

(a) Je,wazifahamu dawa za kulevya?


(b) Umewahi kuvitumia dawa za kulevya?
(c) Kuna uwezekano wa kuvipata dawa hizi shuleni?
(d) Kuna manufaa yoyote ya dawa hizi?
(e) Je,wazitambua madhara yake?

Katika maswali yanayofuata utahitajika kutoa maelezo mafupi


(f) Ni kweli kuwa kazi mnazopewa ni nyingi na hampati muda wakutosha kudurusu?Toa
ufafanuzi…………………………………………………………………………………………
(g) Kuna ulinzi wa kutozha shuleni au la?ni vitu vipi unaeza kuingia navyo shuleni?
(h) Ni mbinu zipi unaweza kuvipata dawa za kulevya shuleni na kwa bei gani?
(i) Unakubaliana kuwa kuna matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa wanafunzi?Dalili
zake ni zipi?......................................................................................................................
(j) Maoni yako ni yepi kwa wanafunzi wengine?

You might also like