You are on page 1of 3

Chimbuko la Qur-an

Imani ya Uislam huchukulia tukio lile la pangoni kama ufunguo wa imani yao na kimsingi ndiyo tukio la
kwanza ambalo kwalo kitabu kitukufu cha umma huo (Qur an) kilianza kupatikana kwa tendo la mtume
Muhammad kukaririshwa kifungu cha aya za sura ya 96 isemayo Soma kwa jina la Mola wako
aliyeumba…..mafunuo hayo Muhamaad aliyakariri kwa nguvu zote na ndiyo yanayotajwa katika Uislam
kama sura ya kwanza kushuka ingawa haijawekwa mwanzoni mwa kitabu cha Qur an, pia tukio hilo
hutajwa kutokea usiku wenye nguvu wa mwezi wa Ramadhani (Lailatulqadir).

Mfumo wa mafunuo yake ya mbele.

Baada ya tukio hilo la pangoni inadaiwa kuwa Muhammad aliendelea kupokea mafunuo mengine zaidi
ambapo mfumo wa upekeaji wa mafunuo hayo ulikuwa kama ifuatavyo:-

Pindi kukiwa na jambo linalotatiza akili za wafuasi wa Muhammad na kuhitajika ufumbuzi toka kwa
mtume mwenyewe au ikiwa mfuasi mmojawapo ana hoja yeyote inayohitaji majibu toka kwa
Muhammad mwenyewe ndipo mtume Muhammad alionekana kupatwa na hali ya kushangaza
inayoelezwa katika kitabu kimoja wapo cha hadithi ya mtume na ndipo maono yake hujitokeza. nukuu:-

Sahihi Bukhary vol 2 hadithi no 610, chapter (16)

To wash the perfume thrice of the clothes (of hram). Narrated Safwan bin Yali said to umar “ show me
the prophet when he is being inspired divinely.” While the prophet was at Jirana (in the company of his
companions) a person came and asked, O Allahs Apostle! What is your verdict regarding that person
who assumes Ihram for “Umra and is scented with perfume

Kuosha vazi la Ihram na kufukiza na manukato (Pafyumu). Imesimuliwa na Safwan bin Yali alimwambia
Umar nionyeshe(nijulishe)pindi mtume anapopata uvuvio mtakatifu.” Pindi mtume alipokuwa eneo la
Jirana (katikati ya waambata wafuasi wake ) mtu mmoja alikuja na kuuliza, Ewe mtume wa Allah ! nini
hukumu yako kuhusiana na mtu aliye vaa Ihram katika ibada ya “umra na vazi hilo likiwa limepuliziwa
manukato Pafyumu.?

Kitabu hiki kinaeleza kuwa baada ya swali hilo mtume Muhammad alionekana kubadilika rangi ya sura
yake kuwa nyekundu na kuanza kukoroma ambapo baada ya tukio hilo wafuasi wake walimfunika kwa
kitambaa na ndipo inadaiwa kuwa Muhammad huanza kupokea mafunuo yake na baadae kuwataka
wafuasi wake kueleza walichomsikia akitamka. Hivyo ndivyo mafunuo ya Muhammad yalivyo patikana.
Uhifadhi wa mafunuo ya Qur-an

Katika kipindi cha awali cha mafunuo hayo ya Muhammad hapakuwa na uwezekano wa kuandikwa kwa
mafunuo hayo kutokana na kile kinachoelezwa katika kitabu cha:-

Maisha ya Muhammad uk no 8 kfg F Kujifunza Kwake paragrafu 1.

(nukuu), Habari ya kusoma haijakuwa katika Hijaz; kwahivyo Mtume aliondokea kama Makureshi
wengine, bila ya kujua kuandika wala kusoma kilichoandikwa. Hajakuwako Kureshi yeyote aliyekuwa
akijua kuandika wala kusoma wakati huo, elimu yao ilikuwa ni ya kujifundisha mambo yanayohusu
maisha yao ya kibedui, kama vile vita, kutunga mashairi ya kusifu ushujaa wao………….

Qur an 62:2

Yeye ndiye aliyemleta Mtume katika watu wasiyojua kusoma,anayetokana na wao, awasomee Aya zake
na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na hikima…

Qur an 7:157

Ambao wanamfuata Mtume, Nabii aliye Ummy (asiyejua kusoma wala kuandika, na juu ya hivi
atafundisha mafundisho hayo ya ajabu ya Uislam)…….

Kadri ya ushahidi huo wa kitabu hicho cha Maisha ya Muhammad kilichoandikwa na mwanazuoni
mtafsiri wa Qur an pamoja na aya hizo za kitabu cha Qur an yenyewe tunaona kumbe sababu iliyofanya
mafunuo hayo yasiandikwe ni kutokana na ukweli kuwa wakati huo jamii ya Waarabu waliomzunguka
Muhammad hawakuwa na uwezo wa kusoma wala kuandika.

Hivyo kutokana na sababu hiyo mfumo wa kuhifadhi Qur an ulikuwa ni wa kukariri kichwani na
kuhifadhi, na wale waliokuwa na uwezo huo walitambuliwa kwa jina maalumu la Maafidhi au Muhfadhin
walitembea wakiwa wamehifadhi mafunuo hayo katika vifua vyao.

Kuweka Qur an katika maandishi


Mbali na mfumo huo wa kukariri uliotumika kipindi fulani tangu kuanza kwa mafunuo ya Muhammad,
kitabu cha maisha ya Muhammad kinatoa maelezo juu ya hatua ya pili ya uhifadhi wa mafunuo hayo
mara baada ya kupatika kwa ukombozi wa kielemu kwa jamii ya Waarabu:-

Maisha ya Muhammad uk no 8 kfg F Kujifunza Kwake paragrafu 2. By al Farsy

Mtu wa awali aliyejifundisha kusoma na kuandika katika maji wa Makka alikuwa Bwana Harb bin
Humayya-babu yake Bwana Muawiya. Alijifunza kwa watu wa Yaman, nay eye akaja kuwafundisha
waliotaka katika mji wa Makka. Wakati mtume walipopata utume walikuwako watu 6 tu katika Makka
waliokuwa wakijua kuandika. Katika hao 4 waliingia katika Uislam. Na ndiyo wakawa waandikaji “Wahyi
(aya za Qur-an). Watu hao walikuwa ni Sayyidna Abubakar, Sayyidna Umar, Sayyidna Uthman na
Sayyidna Ali.

Hadi kifo cha Muhammad, jumaatatu mwezi 12 Mfunguo sita mwaka wa 11 AH-8 june 632, akiwa na
umri wa miaka 63 (Maisha ya Muhammad uk 81, paragrafu 5) Qur an haikuwa imekusanywa wala
kuwekwa kwenye mfumo wa kitabu kimoja bali mafunuo ya Qur an yalikuwa katika maeneo mbalimbali
kama vile:-

Vichwani mwa watu (Maafidhi).

Majani ya mitende

Ngozi za wanyama nk

Lakini baada ya kifo hicho cha Muhammad wazo la kukusanywa kwa mafunuo hayo lilikuja kupitia kwa
mmoja wa wafuasi mstari wa mbele wa Muhammad ajulikanae kwa jina la Sayyidina Umar kuwa sasa
wangepaswa kukusanya mafunuo hayo na kuyaweka pamoja kwa kile kilichoonekana kuwa baadhi ya
wafuasi wa Muhammad waliokariri mafunuo hayo walikuwa wanakufa vitani:-

(Nukuu) Mkweli Mwaminifu/ Katika maneno ya Bwana wa Mitume (SAW) Uk no 18 By Sheikh Said
Moosa Mohammed Al Kindy (Mada) Iwekeni katika sura (Fulani) hivi na hivi.

You might also like