You are on page 1of 16

Sauti ya Waislamu

Safari ya Hijja Hijiria 1433

Waislamu kumiminika Kidongo Chekundu leo


Balozi Marekani ajitetea, serikali haihusiki

ISSN 0856 - 3861 Na. 1035 Dhuul-Qaad 1434, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 20, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs

Uandikishaji unaendelea. Gharama za Hijja ni kama Hijja iliyopita mwaka jana, USD 3850. Tarehe za safari ni 19 Oktoba, 2012 na kurudi tarehe 11 Novemba, 2012. Wahi kujiandikisha sasa. Kumhijia mtu ni $900. Semina zitaanza Oktoba 7-16, 2012 Kwa mawasiliano: +255 22 2181577, +25 22 2182370, 0754 498888, 0786383820, 0754 261910 E-mail: tmht@live.com, info@hajjtrusttz.org Website: wwwhajjtrusttz.org

Kizaazaa Baraza la Mitihani Uk. 4


DKT. Shukuru Kawambwa

Siasa za Janjawidi Wakatoliki amri bado zipo Zanzibar wasalim wa Obama Libya Nusura yawakute ya Balozi
Yaliyojiri katika uchaguzi mdogo Bububu, Zanzibar hivi karibuni. Habari Uk. 3

Dr. Kawambwa, Ndalichako kuzua balaa Ya Taharir Square, sensa kuhamia NECTA Makachero, waandishi wana agenda gani?

Uchaguzi bado wa kingunguri, KMKM Ndio walioipiga mweleka CUF Bububu

Waislam Sumbawanga wafanya kazi ya Polisi Waliosusia sensa Rukwa wanusurika kifungo

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Tangazo
AN-NUUR

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012

AN-NUUR

MAONI YETU

Si kosa la kibindamu Ni makusudi, hujuma


Usiri huu wa nini? Muda wote huu wa nini
Kilichofanyika katika Baraza la Mitihani Tanzania, sio kosa la kibinadamu kama Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi anavyodai. Sana tunaweza kusema ni blanda. Ni uzembe usio vumilika. Lakini wakati mwingine tunalazimika kushawishika pia kukubaliana na hoja za Waislamu mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika na kugundulika kuwa madai yao hayana ukweli. Tu n a c h o s h a w i s h i k a kukubaliana nao ni yale madai kuwa huenda hata haya makosa ya kibindamu ambayo sisi tunasema kuwa ni uzembe na blanda, husababishwa na ukweli kwamba Baraza limekosa sura ya kitaifa kutokana na aina ya watu na mioyo yao katika kutenda kazi. Kwamba huongozwa na imani zao za Kikristo. Katika moja ya mambo yaliyozungumzwa katika moja ya vikao vya viongozi wa taasisi za Kiislamu, iliarifiwa kuwa mahali wanapochinjiwa watoto wa Kiislamu na wengine kupewa nafasi ya kutesa ni katika ile kamati ya siri ya kutunuku. Ikadaiwa kuwa utaratibu wa kutunuku imekuwa jambo la siri lisilo na kanuni wala mwongozo, lisilofahamika hata kwa waratibu wa masomo. Kwamba kamati hiyo imekuwa ikifanya mambo kienyeji kiasi kwamba hakuna mfanano katika muachano katika nafasi baina ya Madaraja. Na kwamba inaweza ikaweka utaratibu ambao wana uhakika watoto wa Kiislamu watafeli katika somo la Maarifa ya Uislamu (O Level) na Islamic Knowledge (A Level). Mfano unatolewa kuwa inawezekana wakaweka kuwa kiwango cha ufaulu wa alama A kikaanzia labda 90 wakati katika masomo mengine ni 75 au hata 85. Na katika madaraja ya chini, yaani D, E, S na F wakaweka pia alama za juu na Class Interval kubwa ya kutoka F kwenda S ili kuhakikisha kuwa hata mtoto akiomba rufaa lazima afeli tu. Katika utaratibu huu, mwanafunzi wa Islamic Knowledge akipata 37 anaweza kuangukia F wakati katika masomo mengine ni D au E na akipata 54 akaambulia D wakati katika masomo mengine hiyo ni C inayokimbilia B. Hii maana yake ni kuwa watoto wa Kiislamu wanaofanya somo la Maarifa ya Uislamu kwa kidato cha nne na Islamic Knowledge kwa kidato cha sita, wanalazimishwa kufeli na kuwekewa mazingira magumu ya kupata A na B. Kama madai haya ni kweli au la, sisi tunadhani hapa ndipo inapoonekana mantiki ya madai ya Waislamu kufanyika uchunguzi wa kina. Labda tuulize: baada ya mitihani kusahihishwa na wasahihishaji kutoa alama stahiki, muda wa mwezi mpaka miezi miwili ambayo Kamati ya Kutunuku ya NECTA inakaa na matokeo hayo kabla ya kutoa matokeo rasmi, inafanya nini? Kama iliwezekana serikali kuweka jopo la kuteuwa watoto wa kwenda kidato cha tano ambao hukata majina ya watoto wa Kiislamu kama ilivyodaiwa na mashuhuda wa hujuma hiyo, je, kipi k i t a w a f a n y a Wa i s l a m u wasiwe na wasiwasi kwamba Kamati ya kutunuku ya Wakristo watupu inazifanya shule za seminari za Kikristo zitese bila kujali kuwa kwa kufanya hivyo inawafanya wanafunzi wengine wa Kitanzania walio wengi kuteseka?

Na Bakari Mwakangwale

Waislamu kumiminika Kidongo Chekundu leo


vikali lamu hiyo, wametaka kutimuliwa balozi wa Marekani mjini Doha na kufungwa vituo vya kijeshi vya Washington nchini humo. Wa a n d a m a n a j i h a o wamepiga nara za kuilaani Marekani na siasa zake za chuki dhidi ya Uislamu. Wakati huo huo, habari kutoka Kabul mji mkuu wa Afghanistan zinasema kuwa, maelfu kwa maelfu ya wanachuo wa mji huo wameandamana juzi na kulaani lamu hiyo ya Kimarekani. Mjini London Uingereza nako, Waislamu na wapenda haki wamefanya mkusanyiko mkubwa na kuonyesha hasira zao dhidi ya filamu hiyo ambayo imewakasirisha Waislamu kote ulimwenguni. Nchini Iran pia miji mbalimbali imeshuhudia maandamano na mikusanyiko ya kulaani lamu hiyo. Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya kidini walikusanyika katika vyuo vyao na kulaani filamu hiyo, huku wakitoa

WAISLAMU jijini Dar es Salaam leo wanatarajiwa kukusanyika katika viwanja vya wazi vya Kidongo Chekundu baada ya mshuko wa swala ya Ijumaa kupinga vikali lamu inayo ukashifu Uislamu na kumdhalilisha kiongozi wa Umma, Mtume Muhammad (SAW). Waislamu Tanzania tunapinga lamu hiyo ambayo maudhui yake ni kashfa kwa Uislamu, alisema Katibu wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda. Ponda amesema, filamu hiyo ni uchokozi wa makusudi kwa Waislamu Duniani kote. Katika mkutano huo, Masheikh wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu watatoa majumuisho na ya vikao vilivyokuwa vikifanyika katika Misikiti mbalimbali jijini kufuatia tukio hilo, ambapo kwa pamoja watalaani kitendo hicho cha kumdhalilisha Mtukufu wa Daraja (s w a). Uongozi wa Jumuia na Taasisi za Kiislamu nchini pia umewataka Waislamu kutochoka kumtetea Mtume wa Allah hivyo kuwataka kuhudhuria katika viwanja vya wazi Kidongo Chekundu, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, ili ulimwengu ushuhudie umma wa Kiislamu Tanzania ukipaza sauti kuwalaani watengezaji wa lamu hiyo. Wa k a t i h u o h u o , maandamano ya kulaani filamu hiyo inayomvunjia heshima mbora wa viumbe Mtume Muhammad (saw), yameendelea kushuhudiwa katika kila kona ya dunia. Maandamano sasa yamevuka mipaka ya ulimwengu wa Kiislamu na sasa yanashuhudiwa hata katika nchi za Ulaya. Mjini Paris, Ufaransa usalama umeimarishwa katika ubalozi wa Marekani mjini humo baada ya kushuhudiwa maandamano makubwa ya kulaani lamu hiyo. Vikosi vya usalama nchini humo vimewekwa katika barabara zote zinazoelekea katika ubalozi huo mjini Paris. Nchini Qatar wananchi Waislamu wa nchi hiyo wameandamana Jumatatu ambapo sambamba na kulaani

wito wa kuchukuliwa hatua kali dhidi ya wahusika. Maandamano kama hayo yameshuhudiwa pia katika nchi za Somalia, Algeria, Tunisia, Sudan, Libya, Ubelgiji, Palestina na Lebanon. Nchi nyingine ambazo nako kumefanyika maandamano ni Yemen, Pakistan, Iraq na Misri. Katika hatua nyingine, Ubalozi wa Marekani nchini nao umetoa tamko lake la kupongeza wito wa Rais Jakaya Kikwete na Viongozi wa Dini ya Kiislamu kuhimiza utulivu na majadiliano ya amani baada ya kukashiwa Waislamu katika lamu hiyo. Tamko hilo linapongeza kauli iliyotolewa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Tanzania kwa kulaani kushambuliwa kwa wanadiplomasia wa Kimarekani huko Libya na vitendo vingine vilivyo kinyume na imani za kidini, Inaendelea Uk. 4

UBUNGO55105, Tel: 2450069, 0754 260241 ISLAMIC HIGH SCHOOL P.O. Box
Fax: 2450822 Dar es Salaam E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

Shule ya Kiislamu ya Ubungo (Ubungo Islamic High School) inatangaza PROGRAMU maalum ya maandalizi ya kujiandaa na Kidato cha Kwanza 2013 kwa wanafunzi Waislamu. Programu hii itaanza tarehe 15/09/2012 hadi tarehe 10/12/2012 Jumatatu hadi Jumamosi saa 3:00 asubuhi hadi saa 8:30 mchana. Masomo yatakayofundishwa katika programu hii ni: 1. Elimu ya Dini ya Kiislamu 2. English Language 3. Arabic Language 4. Mathematics 6. Introduction to Computer Ni programu maalumu ya miezi mitatu (15/09/20212 hadi 10/12/2012) Ada ya masomo kwa programu yote ni Tshs 50,000/= inalipwa yote mwanzoni mwa programu. Fomu za kujiunga zinapatikana Shuleni - BURE Kwa mawasiliano zaidi: 0714 888557, 0659 204013, 0717 295107 MLETE MWANAO APATE ELIMU BORA NA MALEZI MEMA YA KIISLAMU Wabillah Tawfiiq MKUU WA SHULE

Maandalizi ya Kidato cha Kwanza 2013

3
Na Mwandishi Wetu
PAMOJA na kuwepo kwa inayoitwa serikali ya umoja wa kitaifa, bado hali ya uchaguzi imebaki ileile ya kijanjaweed ambapo matokeo hayategemei kura za wapiga kura halali. Yaliyojiri katika uchaguzi mdogo wa Bububu, ni ushahidi tosha kuwa suala la demokrasia na uchaguzi ulio huru na wa haki, bado ni ndoto za mbali katika siasa za Zanzibar. Kwa kiasi kikubwa na katika hali iliyo wazi, kilichoitwa ushindi wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hili, kumechangiwa na kutumika kwa vyombo vya dola, KMKM, Polisi pamoja na wapiga kura mamluki waliopitishwa na kulindwa na wana usalama hao. Toka kabla ya kuka siku ya uchaguzi, kulikuwa na uvumi kwamba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ingeshirikiana na baadhi ya viongozi wa CCM na vikosi vya ulinzi pamoja na Polisi kuhujumu na kuvuruga upigaji kura kwa lengo la kusaidia CCM ishinde. Haikuwa kicho, bali kwa kujiamini kabisa, wanausalama walikuwa wakipitisha watu waliotambulika kuwa mamluki, wakawalinda na kuhakikisha kuwa wanapiga kura. Kwa upande mwingine, Polisi na KMKM walitumika kuwasambaratisha vijana wa CUF ambao walikuwa wamejizatiti kuweka ulinzi kuhakikisha kuwa hakuna mamluki anayepiga kura. Kusambaratishwa kwa vijana hao kulirahisisha zoezi la kuleta mamluki hutoka majimbo ambapo CCM ina nguvu. Ubaya wa mambo ni kuwa askari wanapofanya kazi waliyotumwa ya kuipatia CCM ushindi katika uchaguzi, hawatizami hata sura wala kujali kauli ya kiongozi wa serikali, hasa akiwa kutoka upande wa CUF. Mfano ni katika uchaguzi huu ambapo, baadhi ya mawaziri wa serikali kutoka CUF walikuwa wakijitahidi kuwapa nasaha polisi waache kazi ya kupitisha wapiga kura mamluki, lakini hakuna polisi aliyewajali. Katika baadhi ya maeneo, wakati wananchi wakiwa wamedhibitiwa na askari wanapiga kelele huyo siye, KMKM wanawapitisha. Hivyo ndivyo ilivyokuwa Bububu wala halikuwa jambo la kicho. Ilikuwa ni ile kufanya kwa jeuri kama kusema tunafanya mtafanya nini? Shuhuda mmoja wa hili anasema kuwa ameshuhudia magari mawili kwa nyakati tofauti moja canter limebeba watu linaingiya likiongozwa na gari la jeshi ambapo waliokuwemo hawakupekuliwa hata kutazamwa vitambulisho vyao huku wananchi wanapiga kelele hao sio. Lakini wapi. Wakapita wakapiga kura wakilindwa na askari. Shuhuda mwingine anasema kuwa pale Kibweni KMKM

Siasa za Janjawidi bado zipo Zanzibar


ilikuwa kama pana karamu vespa na baiskeli nyingi watu wengi walivaa kiraia hasa wanawake na kila wakati gari likitoka na baadhi yao kuelekea vituoni. Hawa bila wasiwasi wakipiga kura kama sehemu ya mkakati kwamba ni watu wa Bububu na wana vitambulisho halali. Hii ndiyo hali ilivyokuwa katika uchaguzi wa Bububu. Ni hali inayokatisha tamaa kwa mwananchi wa kawaida ambaye bado ana ndoto kuwa kuna uchaguzi wa haki na huru na kwamba kura yake ndiyo itakayoamua nani mshindi. Mwandishi mmoja katika maoni yake katika mtandao anasema kuwa hakuna anayeweza kubisha kwamba sasa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imejaribiwa na imefeli majaribu hayo. (kwamba) Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu ulikuwa ni mtihani uliokuwa ndani ya mtihani. Mtihani wa kwanza ni kwamba ulitakiwa upime kiwango cha ukubalifu wa Ajenda ya Zanzibar. Akiendelea akasema kuwa mtihani wa pili ulikuwa upime kiwango cha utendaji na ufanyaji kazi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar na kwa hili

Habari

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21- 27, 2012


kuwa ndio kipimo cha kushinda na kushindwa kwa vyama vilivyoingia kwenye uchaguzi. Nachukulia suala zima kwenye mizani ya Umoja ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na Mustakabali wa Ajenda ya Zanzibar. Je, ndio tuseme kuwa tumefeli na wahafidhina wakisaidiwa pakubwa na Tanganyika ndio walioshinda? Pengine falsafa na mantiki iliyo katika swali hili ndiyo inabidi kila Mzanzibari ajiulize, kipi kinatawala katika kufanya mambo yetu, Uzanzibari au maslahi binafsi yanayotumiwa na maadui wa Zanzibar kuidhoosha Zanzibar? Swali hili hili inabidi pia tujiulize, katika kutaka serikali ya muungano katika sura ya mkataba au muundo huu uliopo hivi sasa, masilahi ya Zanzibar yapo wapi zaidi?

AN-NUUR

Masikini Zanzibar
Inatoka Uk. 16 alihoji mmoja wa Wananchi wa Bububu akiwaambia waandishi wa habari, ingawa hatimaye mtu huyo aliishia kwa kisago cha Wanamaji hao. Wapo katika wapasha habari walioeleza kwamba kulikuwapo na rundo la mamluki kutoka majimbo mengine ya ngambo

la pili suala kubwa lilikuwa ni je kwa kiasi gani serikali hiyo ni moja panapohusika dhana ya Maridhiano na Mustakabali wa Zanzibar. Akitoa maoni yake akasema: Kwangu, na naamini kwa wengine wengi, suala kamwe halikuwa kushinda na kushindwa kwa CUF ama CCM. Njia za kila mmoja wao kukia kwenye ushindi huo, zilipaswa kuakisi kwenye majibu ya masuali mawili ya juu, ambayo nayaita kuwa ni mtihani ndani ya mtihani. Sichukulii, kwa hivyo, matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar

na vijijini, yakiwamo Majimbo ya Kwamtipura, Bumbwini, Kiembesamaki, Magogoni, na janjaweed kutoka Chumbuni, ambao walikuwa na Vipande vya Kupiga kura, wakavalishwa Sare za KMKM, na hatimaye wakapiga kura isivyo halali katika Kituo cha SUZA A na SUZA B ambavyo vilikuwapo kwa ajili ya Wapiga kura wa Shehia za Sharifu Msa na Kibweni. Nadhani hayo ndiyo waliyokuja nayo akina Balozi na Makada wa CCM sare mpya na vipande vya kura, alisema kijana Said Mwalimu ambaye pia ni moja ya wananchi wa Jimbo la Bububu, waliokuwapo kujaribu kuwabainisha Mamluki ambao pia walidaiwa kutegesha katika Maskani ya Beit el Ras, jirani kabisa na Mlango wa kuingia SUZA na Kituo kidogo cha Polisi, hali ambayo ililalamikiwa kuibua vurumai za kila mara siku ya Uchaguzi. Wakati hayo yakiendelea, Msafara Mkubwa wa Aina yake wa Magari ya Jeshi la wananchi wa Tanzania, yaliyojaa Askari waliovalia sare na wenye silaha, na pia canter lililowabeba mamluki, wakiongozwa na Gari aina ya Land Rover lenye Nambari 2609 JW 97, ambao moja kwa moja waliingia katika Vituo vya Kupiga kura vya SUZA A na SUZA B, wakatekeleza zoezi hilo kwa haraka na bila ya pingamizi ya aina yeyote. Hilo halikuwa siri kwani hata baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Zanzibar, lilitendeka machoni kwao, usoni pia mwa

vyombo vya habari. Huo ni wakati ambao pia Wandishi wa Habari walipokea kipigo, kupokwa vifaa na vitendea kazi, na kutishiwa uhai wao, ambao ni pamoja na Bw. Munir Zakaria wa Channel 10, na Bw. Ahmed Omar, Mawandishi wa Kujitegemea. Piga wale tumia branco..ua angalau watu kumi na tano kisha na wewe ujitwange risasi ujimalize, hayo ni maneno kutoka moja ya Makamanda Watoa order wa Kikosi Maalumu cha Kuzuiya Magendo, KMKM, ambaye akitoa amri kwa wafuasi wake walipokuwa wakitekeleza mashambulizi katika maeneo ya Vituo vya Kupiga kura vya Shule za Msingi na Sekondari za Bububu, ambapo wakipiga kura Wananchi wa Shehia za Bububu na Mwanyanya. Mashambulizi hayo yalikuja kufuatia madai kuwa miongoni mwa Askari wa KMKM walichomwa kisu na pia kujeruhiwa na kuporwa fedha zao, pale wananchi walipojaribu kuwazuiya wasiende kupiga kura katika Vituo hivyo, kwa madai kuwa huenda walidhaniwa kuwa miongoni mwa wapiga kura mamluki. Licha ya majeraha makubwa, vipigo vikali, udhalilishaji ukiwamo wa kuwaweka baadhi ya watu kubaki uchi wa mnyama, kijana Abdulla dulla alifariki dunia baada ya kupigwa risasi sehemu za paja, na Mohamed Omar Mmanga, wote wakaazi wa Bububu, kulazwa Hospitali ya Alrahma, Mjini Unguja, baada ya kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa Askari wa KMKM. Wengine waliowekwa rumande kwa zaidi ya masaa 72 katika Kituo cha Polisi cha Ngambo, Wilaya ya Magharibi Unguja, baada pia ya kusota katika selo za KMKM kwa zaidi ya masaa 12, ni pamoja na Mohamed Ali Amour, Omar Bakar Faki, Khalef Mohamed Juma (17), Mohamed Yussuf Ali, Khamis Ruweikh

Khamis, na Juma Omar Juma (44); kabla ya kuporwa simu zao za mkononi na pia kabla ya kupelekwa Mahakama ya Mkoa, wakishitakiwa kwa tuhuma za Makosa ya Kuwashambulia na Kuwajeruhi Askari. Kwa ujumla mazingira hayo na mengineyo huenda ndiyo yaliyopelekea baadhi ya Viongozi, Waangalizi wakiwamo wa Jumuiya ya Maimamu ya Zanzibar, na pia Wananchi, kuamini kwamba Bububu ni Jimbo la mgogoro kutokana na kitendo cha wananchi kupandikiziwa Muwakilishi wa Majeshi, kinyume na utaratibu wa uchaguzi wa Kisheria na wa kidemokrasia.

Aidha katika Taarifa ya Viongozi wa CUF, imeongezwa kuwa jamii, umma wa wananchi, na kila mwenye busara, wote wanaelewa kwamba uchaguzi na mchakato mzima wa Uwakilishi katika Vyombo vya Kutunga Sheria, katika zama hizi za Demokrasia na Utawala Bora, hasa katika nchi inayofuata mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hauwezi kufanyika wala kukubalika katika hali hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Chama cha Wananchi, CUF, hakiamini kwamba uliofanyika ni uchaguzi, bali ni uchafuzi uliolenga kupandikiza, Muwakilishi wa Majeshi, Muwakilishi wa Tume, na pia chaguo la Chama tawala, pasi na kuridhia maamuzi ya Wananchi wenyewe wa Bububu, hata ikibidi kwa mabavu, mtutu wa bunduki, na nguvu za ziada za Dola. Wakati huo huo Chama cha CUF kinalaani kitendo ha kushambuliwa, kupigwa, na kujeruhiwa vibaya kwa Mbunge wake wa Jimbo la Mtoni, Unguja, Bw. Faki Haji Makame. Laana hizo zimekuja kupitia Kikao cha Waandishi wa Habari, kilichofanyika juzi, ambapo Kiongozi huyo pia alikuwapo, katika Ukumbi wa CUF, Vuga,

Mjini Unguja. Walinipiga vijana wa CCM baada ya kunifukuza mbele ya Naibu Katibu Mkuu wao Vuai Ali Vuai ambaye nilimsalimia kabla hakuitikia akanambia nimezuiya watu wake wasipige kura na nitakiona na papo hapo ndipo yaliponikuta hayo hadi Polisi wa Kituo cha Bububu ambao walikuwa kama mita mia mbili waliponiona wakaja wakaniokoa, alisema kwa simanzi Mbunge huyo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tukio hilo lilitokea mchana wa Jumapili ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu, jirani na Maeneo ya Tawi la CCM Bububu, ambapo si mbali na Kituo cha Polisi Bububu. Uchaguzi huo uliodaiwa kujaa vurugu na hujuma ulikuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Muwakilishi wa Jimbo hilo , Marehemu Salum Amour Mtondoo, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu, kufuatia shinikizo la damu. Pamoja na yote, huku Wa n a n c h i w a B u b u b u wakikaririwa wakisema bado hawajafikia hatua ya kupata Muwakilishi wao kihalali, na kwamba wamebambikiziwa Muwakilishi wa Majeshi, wamesema wao kama Waislamu wanabaki na msimamo wa kuvunja fungamano la kushirikiana na Majeshi na Vikosi vyote vilivyowahujumu, wakiwamo askari wa KMKM. Sisi hatutashikamana nao tena kwa lolote na hata hiyo Hospitali yao Waislamu hawataitumia tena kwani wametufanyia uadui hatuna imani nao asilan abadan , alisema Maalim Ali Omar, Mkaazi wa Kibweni. Mwananchi huyo ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni Mwalimu, akikazia msimamo huo alisema, siye bwana tunataka Muwakilishi wa kutetea Maslahi ya Zanzibar na wala siyo haya mapandikizi.

Kizaazaa Baraza la Mitihani


Dr. Kawambwa, Ndalichako kuzua balaa Ya Taharir Square, sensa kuhamia NECTA Makachero, waandishi wana agenda gani? Au wanataka kuuwa watu walete ya Uamsho?
watoto wa kuendelea na elimu ya sekondari na A Level, zimejaa Wakristo, wakikaa wanajikuta wapo peke yao na hapo ndio hufanya kazi kwa kuangalia Ukristo na Wakristo. Sasa Waziri aseme, atuambie, Kamati yake imegundua nini? Ni kweli au sio, na kama ni kweli wale watoto wa Kiislamu walioporwa nafasi zao, anawalipaje? Alihoji na kuongeza akisema kuwa, Waislamu walisema kuwa dhulma na hujuma zote hizo hufanyika kwa sababu walioshikilia nafasi muhimu na nyeti katika Baraza ni Wakristo watupu. Wakataka uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe ili kulipa sura ya kitaifa Baraza hilo. Ile hoja kwamba Baraza halifanyi kazi kwa kutizama dini haina maana tena maana tayari ishaonekana Muislamu anafaulu na jina lake linakatwa, wanaoamua nani aende sekondari au High School wanasukumwa na dini zao, alisema. Kwa upande mwingine katika vikao vinavyoendelea kujadili namna ya kuliweka sawa Baraza, imetolewa ile hoja inayobebwa na shutuma kuwa huenda Baraza wakati mwingine linawafelisha watoto wa Kitanzania kwa makusudi ili kuendelea kuonyesha kuwa shule za Kanisa zinafanya vizuri. Somo la hesabu linatajwa kuwa ni tatizo la kitaifa, masomo kama kemia yanajulikana kuwa watoto hawafanyi sana vizuri, kipi kinafanya kiwango cha ufaulu cha hesabu (Advance Maths) kiwe cha juu sana kupita hata Kiswahili na historia? Wa n a o u l i z a s w a l i h i l i wanadai kuwa zipo tuhuma kuwa japo watoto hawafanyi vizuri sana katika somo la hesabu, lakini kufeli kwao kumekuwa kukisababishwa na njama za kutaka shule za Kanisa zionekane kutesa kila mwaka. Wa n a o l e t a m a d a i h a y a wanasema kuwa huenda kuna shule hazifaulu kihalali, sasa ikitokea wototo wote wana A au A na B tu, inabidi yafanyike maarifa kupandisha alama za ufaulu (Cut Off Score) ili angalau na C na D ziwepo. Hata hivyo, kama hivyo ndivyo inavyofanyika, hali hiyo itawafanya watoto wengine kufeli sana. Tuhuma zilizopo ni kuwa uchezeaji huu wa alama ya mwanzo (Cut Off Score) ama kupandhishwa au kushushwa kila mwaka na kati ya somo na

Habari

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012

AN-NUUR

Na Mwandishi Wetu
HUENDA kile kizaazaa kilichoikumba Idara ya Takwimu katika sensa mwaka huu kikahamia Baraza la M i t i h a n i l a Ta n z a n i a (NECTA). Hatua hiyo inakuja ikilenga kutafuta haki na kulifanya Baraza hilo litimize wajibu wake kwa taifa kuliko hivi sasa ambapo linashutumiwa kukiuka maadili ya kazi zake. Hata hivyo, bado haijafahamika ni hatua za aina gani zitachukuliwa na lugha gani itatumika itakayoeleweka kwamba Wa i s l a m u wamechoshwa na kile walichodai NECTA kukosa sifa ya kitaifa na badala yake kuonekana kama chombo cha kuendeleza upendeleo na ubaguzi katika elimu nchini. Mkakati huo unakuja kufuatia hatua ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa kupuuza madai ya Waislamu na badala yake kutoa maelezo pungufu yanayolenga kuendeleza mfumo uliopo. Waziri anasema kwa Islamic Knowledge kosa lilikuwa la kibinadamu, lakini hoja yetu ya msingi ni kuwa hata haya makosa ya kibinadamu huenda yanachochewa na ukweli kwamba NECTA imekuwa kama kitengo cha Kanisa toka ianzishwe, inaajiri mchungaji wa kuangalia masilahi ya watoto wa Kikristo, lakini haitaki kuweka mtaalamu wa somo la Maarifa ya Uislamu. Sasa atuambie Waziri Kawambwa, hiyo Kamati yake inasema nini kuhusu hoja kuwa toka Baraza liundwe lina sura ya Kikristo? Anasema nini kuhusu kuajiri mchungaji? Anasema nini kuhusu yale madai kuwa nafasi za watoto wa Kiislamu waliopasi zilichwa wakapewa akina John? Anahoji mjumbe mmoja akiongea na mwandishi baada ya kutoka katika kikao kilichojadili hatua za kuchukua baada ya kutolewa taarifa ya Waziri. Mjumbe huyo ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe gazetini anasema kuwa risala ya Waislamu kwa Waziri ilikuwa wazi, iliorodhesha baadhi ya majina ya watoto wa Kiislamu ambao walipasi na kuchaguliwa kwenda sekondari lakini majina yao wakapewa watoto wa Kikristo. Amesema, haya yaliwezekana kwa sababu toka NECTA mpaka Kamati na Majopo ya kuteuwa

Waislamu kumiminika viwanja vya Kidongo Chekundu leo


Inatoka Uk. 2 huku wakihimiza kuwepo kwa utulivu na majadliano ya amani. Katika sehemu ya taarifa ya ubalozi huo, imenukuliwa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Rodham Clinton siku ya Ijumaa, Septemba 14, 2012, iliyosema kuwa Serikali ya Marekani haihusiki kwa vyovyote vile na lamu ya udhalilishaji inayosambazwa katika mtandao wa internet, ambayo ndiyo imesababisha maandamano katika nchi mbalimbali. Ilieleza kuwa Marekani inapinga na kulaani maudhui ya filamu hiyo yasiyo na chembe ya heshima na ujumbe wake wa kuudhi na kuleta chuki. Baada ya hapo taarifa hiyo ya ubalozi ikaendelea na kumbukumbu mbalimbali za misaada iliyotolewa na Marekani kwa Tanzania kuonyesha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Taifa hilo na Tanzania kwa watu wa imani zote. Marekani na Tanzania ni nchi zenye hazina kubwa ya kuheshimu uhuru wa dini na watu wake wa dini mbalimbali kuvumiliana. Ubalozi wetu jijini Dar es Salaam una fahari kubwa kushirikiana na viongozi wa dini zote. Programu za kujenga maelewano, na mabadilishano ya kitamaduni na kielimu na Watanzania wa imani zote, ikiwemo Waislamu, ni jambo linalopewa kipaumbele cha juu na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania. Programu zetu za kusaidia maendeleo zinatuwezesha kufanyakazi na viongozi wa kidini, mashirika ya kiraia na sekta binafsi na kusaidia jitihada zao za kujenga mustakabali Mwema kwa Watanzania wote. Kwa mfano, kwa kupitia Millennium Challenge Corporation (MCC), serikali ya Marekani inafadhili mradi wa kupeleka Zanzibar umeme wa megawati 100 kupitia nyaya zinazolazwa baharini ili kuboresha upatikanaji wa umeme visiwani humo. Kwa kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) mradi wa kutokomeza Malaria visiwani Zanzibar umepunguza kwa kiwango kikubwa matukio ya ugonjwa huo Zanzibar. Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) umekuwa ukiendesha programu mbalimbali za kukabiliana na VVU/ UKIMWI zinazookoa Maisha ya maelfu ya watu nchini Tanzania. Hali kadhalika, Mpango wa kusaidia kilimo na usalama wa chakula unaoendeshwa na USAID (Feed the Future) unafadhili shughuli mbalimbali za kilimo na kiuchumi zinazolenga kuinua ubora wa Maisha wa Watanzania wote - ambao miongoni mwao Waislamu ni sehemu kubwa. Ikiendelea ripoti ya Balozi ikasema, Katika kujenga na kuimarisha mahusiano

somo na katika utaratibu ambao ni siri kubwa, haufanywi kwa masilahi ya wadau wote wa NECTA, bali kwa masilahi ya shule zinazotakiwa kutesa ili zisiteseke. Yapo madai pia wakati mwingine Cut Off Score ya somo kama la Maarifa ya Uislamu (O Level) na Islamic Knowledge hupandishwa bila kufuata kanuni zozote za kitaalamu kwa lengo la kufelisha watoto wanaochukua somo hilo. Wa n a o l e t a m a d a i h a y a wanasema kuwa lengo la mkakati huu ni katika sura mbili: Moja kuwakatisha tamaa watoto wa Kiislamu kuchukua somo hilo

na pili kushusha kiwango chao cha ufaulu. Tumejadili hili na tumesema hizi ni shutuma nzito ambazo hamna namna Baraza linaweza kujisafisha, ila kwa kufanyika uchunguzi huru sio hiki kiinimacho cha Waziri Kawambwa na ndio maana Waislamu walipendekeza katika Risala yao kuwa uchunguzi uhusishe masomo mengine, maeneo mengine katika utendaji wa NECTA na utizame nyuma kwa uchache miaka mitano. Amesema Mjumbe huyo wa kikao cha Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Habari za ndani za kikao hicho zinafahamisha kuwa Waislamu watalikamata suala hili mpaka wahakikishe kuwa wanalipa Baraza heshma na hadhi linaostahiki. Pamoja na mipango mingine, huenda ule utaratibu waliotumia Misri wa Tahrir Square ukafanyika nchi nzima mpaka ukweli ujulikane na hatua za kurekebisha hali zichukuliwe. Wa k a t i h u o h u o , w a t u

wamekuwa wakihoji nini agenda ya makachero na baadhi ya Vyombo vya Habari kupalilia kinachodaiwa uvamizi wa Bakwata na kumngoa Mufti wa Baraza hilo. Kinachoonekana katika suala hili ni kana kwamba vyombo hivyo vinawachochea Waislamu kumvamia Mufti wa Bakwata. Hawa inavyoonekana wana agenda ya kuuwa watu, waharibu mali na kisha wawasingizie Waislamu ili wapate sababu ya kufanya hujuma kama Bush anavyosingizia vita dhidi ya ugaidi kuendesha Vita ya Msalaba (Crusade) Amesema muumini mmoja akitoa maoni yake. Hawa wanataka wachochee Waislamu waingie mitaani kisha wapandikize vijana wao katili wasio na muhali wala kuona vibaya wafanye hujuma ipatikane sababu ya Crusade itakayowarejesha nyuma Waislamu miaka 30, ameongeza muumini huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ustadh Haji.

baina ya watu wa nchi hizi mbili, Ubalozi wa Marekani umekuwa ukiwakaribisha vijana wa Kiislamu katika maktaba yake kuu na katika maktaba ndogo (American Corners) zilizopo Unguja, Pemba na Mwanza. Aidha, Ubalozi umekuwa ukiendesha programu mbalimbali za kuwafikia Watanzania huko waliko (outreach programs) na kuwa na majadiliano nao yaliyo wazi. Mfuko wa Balozi wa Marekani wa Kuhifadhi Amali za Kitamaduni (The Ambassadors Fund for Cultural Preservation) umekuwa ukitupa fursa ya kuonyesha jinsi Marekani inavyoheshimu na kuthamini hazina ya kipekee ya kitamaduni na kihistoria ya Tanzania. Toka mwaka 2002, Watu wa Marekani wametoa jumla ya Dola za Kimarekani 1,090,000 katika kusaidia hazina za kiutamaduni na kihistoria za Tanzania, ikiwa ni pamoja na Miskiti ya Kizimkazi na Micheweni huko Zanzibar na magofu ya Kilwa Kisiwani. Hali kadhalika, Watu wa Marekani wametoa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 49 kuchangia mradi wa matumizi ya teknolojia ya kisasa ya habari katika kufundishia mashuleni (Tanzania 21st Century Education Program -TZ21) unaotekelezwa huko Zanzibar na Mtwara kupitia USAID. Hiyo ni sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa Septemba 18 mwaka huu.

Sudan yakataa askari wa Marekani


KHARTOUM Serikali ya Sudan imepinga o m b i l a M a re k a n i l a kutaka kutumwa nchini humo askari maalumu kwa ajili ya kulinda ubalozi wake mjini Khartoum kufuatia kukithiri maandamano ya kulaani filamu inayomvunjia heshima Mtukufu Mtume Muhammad (saw). Shirika la Habari la Sudan (Suna) limeandika ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi hiyo kuwa, serikali ya Khartoum inapinga ombi la Marekani la kutaka kutumwa nchini Sudan askari maalumu kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika ubalozi wake mjini Khartoum, baada ya kuongezeka malalamiko ya jamii ya kimataifa hususan Waislamu kote duniani dhidi ya kuvunjiwa heshima matukufu ya dini ya Kiislamu kunakofanywa na Marekani na Israel. Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Ali Karti, amesema Sudan yenyewe inaweza kulinda ofisi za wawakilishi wa kidiplomasia, hivyo serikali ya Khartoum haioni umuhimu wa kutumwa askari wa Marekani nchini humo. Hivi karibuni Washington ilipeleka askari 300 mjini sanaa Yemen kwa sababu hiyo hiyo, hali iliyozidisha hasira za wananchi na baadhi ya viongozi wa serikali walioitaja kuwa ni uvamizi dhidi ya nchi yao. Yemen nako wamepinga vikali kuingia nchini humo wanajeshi wa Marekani kwa kisingizio hicho hicho cha kulinda wanadiplomasia. Baada ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani kutangaza habari ya kutumwa wanajeshi wa nchi hiyo huko Yemen kwa ajili ya kuulinda ubalozi wa Marekani nchini humo, Bunge na baadhi ya wakuu wa vyama na wananchi wa Yemen wamepinga vikali hatua hiyo na kusisitiza kuwa wanajeshi hao wanapaswa kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo. Wi z a r a y a U l i n z i y a Marekani siku kadhaa zilizopita ilitangaza taarifa ya kutumwa huko Yemen wanajeshi 150 wa nchi hiyo kwa kile walichokiita kuwa ni eti kwa ajili ya kuulinda ubalozi wa nchi hiyo huko Sanaa baada ya kusambaa maandamano ya wananchi dhidi ya lamu inayoyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu iliyotengenezwa huko Marekani, ambayo imezusha hasira kubwa za Waislamu kote duniani. Bunge la Yemen limepinga kuweko wanajeshi hao wa Marekani nchini humo na kuitaka serikali ya Washington kuwaondoa mara moja askari wake iliowatuma huko Sanaa mji mkuu wa Yemen. Bunge la Yemen limesema kuweko vikosi vya kigeni nchini humo hakukubaliki kwa hali yoyote ile na kuitaka serikali ya nchi hiyo kutekeleza majukumu yake ya kudhamini usalama wa mabalozi na wanadiplomasia wa kigeni. Wa k a t i h u o h u o , maandamano ya kulaani filamu inayomvunjia heshima mbora wa viumbe Mtume Muhammad (saw) yameendelea kushuhudiwa katika kila kona ya dunia. Maandamano sasa yamevuka mipaka ya ulimwengu wa Kiislamu na sasa yanashuhudiwa hata katika nchi za Ulaya. Mjini Paris, Ufaransa usalama umeimarishwa katika ubalozi wa Marekani mjini humo baada ya kushuhudiwa maandamano makubwa ya kulaani lamu hiyo. Vikosi vya usalama nchini humo vimewekwa katika barabara zote zinazoelekea katika ubalozi huo mjini Paris. Nchini Qatar wananchi Waislamu wa nchi hiyo wameandamana Jumatatu ambapo sambamba na kulaani vikali filamu hiyo, wametaka kutimuliwa balozi wa Marekani mjini Doha na kufungwa vituo vya kijeshi vya Washington nchini humo. Wa a n d a m a n a j i h a o wamepiga nara za kuilaani Marekani na siasa zake za chuki dhidi ya Uislamu. Wakati huo huo, habari kutoka Kabul mji mkuu wa Afghanistan zinasema kuwa, maelfu kwa maelfu ya wanachuo wa mji huo wameandamana juzi na kulaani filamu hiyo ya Kimarekani ambayo inamtusi na kumvunjia heshima Bwana Mtume (saw). Mjini London Uingereza nako, Waislamu na wapenda haki wamefanya mkusanyiko mkubwa na kuonyesha hasira zao dhidi ya filamu hiyo ya kishenzi ambayo imewakasirisha Waislamu kote ulimwenguni. Nchini Iran pia miji

Habari za Kimataifa

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21- 27, 2012

AN-NUUR

Iran yaongeza zawadi kumuua Rushdie


TEHRAN Iran imeongeza kiwango cha zawadi itakayotolewa kwa atakayemuua murtadi Salman Rushdie aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW) na Waislamu. Kwa mujibu wa Ayatullah Sheikh Hassan Saneei, anayesimamia Waqfu wa 15 Khordad, zawadi hiyo imeongezwa kwa dola laki tano hivyo sasa imeka dola milioni tatu na laki tatu. Sheikh Saneei, ametangaza kuongezwa zawadi hiyo wakati akitoa taarifa ya kulaani utengenezwaji filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW). Itakumbukwa kuwa mwaka 1989, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini MA, alitoa fatwa ya kuuawa murtadi Salman Rushdie baada ya kitabu chenye anuani ya Aya za shetani Satanic Verses kinachomvunjia hehsima Mtume (SAW) na Waislamu. Ay a t u l l a h S h e i k h Hassan Saneei, amesema fatwa ya Imam Khomeini inalenga kukata mizizi ya njama za mawakala wa Marekani na Utawala wa Kizayuni. Amesema iwapo fatwa hiyo itatekelezwa, maadui hawatathubutu tena kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu.

RAIS wa Marekani Barack Obama mbalimbali imeshuhudia maandamano na mikusanyiko ya kulaani filamu hiyo. Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya kidini walikusanyika katika vyuo vyao na kulaani filamu hiyo, huku wakitoa wito wa kuchukuliwa hatua kali dhidi ya wahusika. Maandamano kama hayo yameshuhudiwa pia katika nchi za Somalia, Algeria, Tunisia, Sudan, Libya, Ubelgiji, Palestina na Lebanon. Nchi nyingine ambazo nako kumefanyika maandamano ni Yemen, Pakistan, Iraq na Misri.

Bunge la Australia lakataa ndoa za mashoga


SYDNEY Bunge la Australia mapema juzi lilikataa kuidhinisha ndoa ya watu wa jinsia moja baada ya wiki kadhaa ya mijadala mikali iliyoandamana na malumbano miongoni mwa wajumbe. Wabunge 98 wamepiga kura ya kupinga hoja hiyo huku 42 wakipiga kura ya kuiunga mkono. Waziri Mkuu Julia Gillard na kiongozi wa kambi ya upinzani, Tony Abbott, wamepiga kura ya kupinga muswada huo. Mbunge machachari,

Cory Bernardi kutoka chama cha kiliberali amepongeza hatua ya bunge ya kukataa kuidhinisha ndoa ya watu wa jinsia moja na kusema kuwa mustakabala wa muundo wa familia ulikuwa katika hatari ya kuangamia. Wa z i r i M k u u J u l i a Gillard, alikuwa amewataka wajumbe wa chama chake kuchukua uamuzi wa kibinafsi katika kuupigia kura muswada huo lakini pia akawataka kutumia mantiki wakati wanapofanya maamuzi kuhusu suala hilo.

6
KIBURI hiki wanakipata kutoka wapi?:-Tunaambiwa kuwa Ta n z a n i a ilishakabidhiwa kwa Papa Leo wa XIII, na hapa ingefaa tuiulize Serikali yetu kuwa tulipokabidhiwa Uhuru wetu mwaka 1961 kutoka kwa Serikali ya Uingereza, walituambia na kutuhakikishia kuwa walipomwondoa Mjerumani waliwanyanganya Wa k a t o l i k i m k a t a b a wa kuimiliki nchi yetu waliyokabidhiwa na Serikali ya Uerumani. Au ndiyo imekuwa hati miliki ya Kanisa la Roma mpaka sasa, na ndicho kiburi walicho nacho, kuwa asiyekuwa Mroma ni mtu wa kuja! We n y e w e k i n a P e n g o wamewaarifu waumini wao na wa Tanzania kwa jumla, katika kusherehekea kutimiza miaka 100, tangu kuanzishwa rasmi utekelezaji wa mkataba huo kwa kuanzia Pugu; Kanisa lilitoa kitabu chenye jina la Pugu hadi Peramiho 1888-1988. Wakielezea jinsi walivyokabidhiana nchi hii, wameandika hivi: Huko Roma iliamuliwa kulikabidhi Shirika la Wabenedikitini eneo lote la Kusini ya Tanzania kisheria eneo hilo likapata jina la: Prefecture Apostolic of South Zanzibar [Prefecture maana yake msimamizi, Apostolic ni kwa mamlaka ya Papa]. Uk.23. Mipaka yake ikapangwa kama ifuatavyo: Kuanzia Kunduchi ilielekea Kusini Magharibi, ikafuata latitude ya saba mpaka karibu na Dodoma ikakata ikaka karibu na Langenburg [Kyela]. Kutoka huko ikafuata Ziwa Nyasa na baadaye mto Ruvuma mpaka karibu Mtwara. Siku hizi sehemu hiyo ina majimbo 10, nayo ni, Dar es Salaam, Mahenge, Dodoma, Njombe, Songea, Mbinga, Tunduru-Masasi, Lindi, na Mtwara. Mkataba wenyewe ulitiwa saini na Baba Mtakatifu Leo XIII, Tarehe 16/11/1887. Hiyo ndiyo siku ya Wamisionari Wabenedikitini kukabidhiwa eneo lao la kimisionari. [Pugu hadi Peramiho 1888 hadi 1988 uk 24]. Serikali ya Ujerumani ilifanya makubaliano hayo hivi:-Mwanzoni mwa mwaka 1887 mwezi machi mashauri yakaanza kati ya mkubwa wa Shirika, Padre Andreas Amrhein, na kati ya Idara ya Mambo ya nje ya Berlin, na Waziri Mkuu wa ujerumani na Shirika la Kijerumani la Afrika Mashariki.Kwa hivi nchi ya Tanzania ilikuwa imetengwa ki-Misionari katika sehemu mbili: Ya Mashariki, chini ya Mapadre wa Shirika la Roho Mtakatifu

Makala/Matangazo

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012


Kusini; kwa maana hiyo ni kuwa kila Mwafrika aliyesilimu aliwekwa kwenye kundi la Waarabu, na ndiyo Maana vita vya Majimaji vilianzia ukanda huo wa Kusini vikiwalenga Waislamu. Na ukungu huo wa kuwaondoa Waislamu bado umeganda kwa Maaskofu na wafuasi wao; ndiyo maana Wazanzibari wakidai haki zao katika muungano maaskofu na waumini wao wanangaka kwa kusema kuwa Wazanzibari wanataka kumrudisha Sultani, waki maanisha kuurudisha Uislamu; ndiyo maana Mchungaji Msigwa anashangaa kuona kuwa Wazanzibari bado ni Waislamu na wanaheshimu maadili ya Uislamu na kukataza wanawake kwenda uchi. Anashangaa maana analinganisha kazi wanayoifanya na iliyofanywa toka mabigwa hao wa kuufuta Uislamu walipoingia Zanzibar wakati wa Mreno mpaka leo lakini bado watu ni Waislamu, wanaheshimu mwezi wa Ramadhani na kuvaa kwa adabu. Nimalizie kwa kuwataka Waislamu wa Tanzania kwa ujumla , Visiwani na Bara, kuwa waunganishe Umoja wao. Hii sio vita ya Uamsho pekee. Sote tunapigwa vita kwa lengo la kuutokomeza Uislamu.

AN-NUUR

Rejea historia hii utawajua vizuri


na Magharibi chini ya Shirika la Mapadre Wamisionari Waafrika [Mapadre Weupe]. Dr, Sivalon uk 23. Na nchi iliyokuwa na maguvu wakati ule ilikuwa ni Ujerumani; hivyo ilipewa jukumu la kuhakikisha Kuwa hiyo nchi waliyoiita Tanzania inakuwa chini ya mikono ya Kanisa likilelewa na Seriksli ya Ujerumani kwa hali na mali, kwa kuwa hiyo Serikali yenyewe ya Ujerumani ilikuwa ni ya Kanisa la Kilutheri. Na kweli walihakikisha kuwa Kanisa linahodhi kila kitu kwa ghilba na kwa damu za wa Tanzania kama tunavyosimuliwa vita vya Majimaji. Wenyewe wakiendelea kutufahamisha hivi:Mwaka 1868 Mapadre wa Shirika la Roho Mtakatifu walianza kueneza Injili katika nchi iliyoitwa Sasa Tanzania. Mwaka 1878 kikosi cha kwanza cha Wamisionari Waafrika [Mapadre Weupe] kiliwasili Tabora walielekea kwenye maziwa makubwa ya TanzaniaKatika wakati huo watu wa Siasa kutoka Ulaya walianza kuvuruga dola ya Waarabu wa Zanzibar na kuonyesha nia ya kueneza Utawala wao wenyewe katika nchi za Afrika ya Mashariki. Jambo hilo liliendeshwa kwetu na Shirika la Biashara la kundi Fulani la Wajerumani, kifupisho DOAG. [Dr. Sivalon uk 23]. Msomaji huo ndio ukweli walioandika viongozi wa Ukristo wenyewe kuwa ukoloni na Ukristo ni watoto pacha na waliingia Tanzani, Afrika kuuondoa Uislamu; ukiona wamesema walianza kuvuruga Dola ya Waarabu wanamaanisha Dola ya Waislamu. Hivyo Serikali ya Ujerumani iliingia hapa Tanzania ili kuiondoa Serikali ya Kiislamu chini ya uongozi wa Waarabu na Machifu, Maakida, ma-Liwali, Watemi, wa Mangi n.k. Ili kuweka Serikali ya Kikristo chini ya mwavuli wa Serikali ya Ujerumani na Uingereza. Na Mapadre wa Roho Mtakatifu, ni wale walioingia katika nchi za Kiarabu ikiwemo Hijazi [Saudia], wakajifunza lugha ya Kiarabu, wakausoma Uislamu vuzuri, kama nilivyoelezea hapo juu, na wakaufuatilia Uislamu kwa kila njia uliopitia na Waarabu; hao ndio waliokabidhiwa Ukanda wa Mashariki na makao yao makuu yakawa Zanzibar, ili waushughulikie Uislamu wakiwa katika kitovu

PAPA Benedict cha Uislamu katika ukanda wote wa Pwani ya Afrika ya Mashariki kuanzia Somalia hadi Kigoma. Na Mapadre Wamisionari Waafrika [Mapadre Weupe], maana yake, ni Mapadre Wazungu watakaowashughulikia Wa a f r i k a w a Ta n z a n i a ukanda wa Kaskazini ambao hawajasilimu, hao hawakuwa na elimu ya Kiislamu sana kama wale wa Roho Mtakatifu waliokabidhiwa ukanda wa

AHLUDAAWA HAJJ AND TRAVEL AGENCY


Inawatangazia Mahujaji wake wote kuwa Safari ya kuondoka ni tarehe 09/ 10/2012 na 11/10/2012 Kurudi ni tarehe 03/ 11/2012 na 05/11/2012 Mahujaji wote wamalize kuchanja haraka iwezekanavyo Paspoti zipelekwe osini kwa ajili ya Viza na Safari Semina Dar es salaam siku ya Jumapili tarehe 30/ 09/ 2012 Madrasatul Jabalhira Magomeni karibu na osini Zanzibar ni Suni Madrasa Mkunazini tarehe 08/09/2012. Wamalize malipo na taratibu zote za safari. Nafasi bado zipo bei zetu ni USD 3,375 tu kwa huduma zote pamoja na mahema maalumu ( VIP). Kwa mawasiliano zaidi piga simu. FOMU ZINAPA TIKANA A. Osi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel- 0713 730444 au 0773 804 101 AU 0785 930 444 AU 0773 930444. B. Osi ya Ahlul Daawa Zanzibar Raha leo Tel- 0777 484 982 0777 413987 C. Abubakari Maulana wa Markaz wa Kiwalani Dar es salaam Tel- 0784 453 838 D. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam Tel-0715724444 E. Salim Is-Haq Dar es Salaam Tel-0754 286010 au 0774 786101 F. Dukani kwa Abdalla Hadh Mazrui Wete-Pemba Tel-0777482665 G. Dukani kwa Mohammed Hadh Mazrui Mkoani Pemba Tel-0777456911 H. Sheikh Daud Hamis Sheha Tel-0777 679692 I. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel-0777 417736 Wahi kulipia Usisahau kikundi cha Ahlul Daawa ni cha bei nafuu kuliko vingine na huduma bora kuliko wengi Wabillah Tawq

7
Na Khatibu Juma Mziray

Makala

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21- 27, 2012 ya sameti [yaani mifuko inayo kuja na sukari]. Nisiendelee zaidi na kisa hicho; ila wakati hali hiyo inaendelea kina Pengo wanatumbua nchi na kuingiza giza la maombi kuwa hali hiyo iendelee. Dr. Sivalon anatufahamisha hivi: Msimamo wa viongozi wengine wa Kanisa: Wakati wa hali ngumu ya uchumi naweza kusema wazi karibu viongozi wote wa Kanisa walinungunika kama watu wengine, lakini Kanisa kama Kanisa halikutoa kauli yoyote wao walipewa fursa na Nyerere ya kuingiza vitu kutoka nchi za nje tena bila ya kodi wala ushuru. Ufupi wa maneno hawakuwa n a s h i d a . Wa l i p e w a upendeleo. Anasema Sivalon kuwa Kanisa liliruhusiwa na Serikali kuingiza vitu vingi nchini bila ushuru wala kodi. Vitu vya miradi ya maendeleo pamoja na vile vya ujenzi vilianza kuingizwa na mwisho hata mahitaji ya kawa- ida ya viongozi wa Kanisa. Mambo yote haya yalipunguza makali ya hali ngumu kwa viongozi hao wa Kanisa wasite kukosoa watawala wa Seriksli. [Dr. Sivalon uk.65]. Ukisikia Kardidali Pengo anazungumzia Uhuru wa Watanzania, na Watanzania ambao waneemeke hata kwa madhara ya wengine bila huruma, hadi leo na baadae Sio wengine bali ni kina Pengo kama Dr. Sivaloni alivyo tuelezea katika nukuu hizo hapo juu.Kwa maana hiyo ni kuwa kwa Kardinali Pengo na viongozi wenzake na Kanisa lake na waumini wake, hao ndio Watanzania, watu wengine ni vitendea kazi tu. Ndiyo maana ushauri wao na sera zao kwa marehemu Rais Nyerere ndio uliotufikisha hapa tulipo. Kiburi na utajiri na miradi ya Makanisa yanayojivunia imepatikana kwa njia hiyo ya kuhodhi mamlaka na madaraka na kuweka sera za kutotoa kodi za vifaa na kila walichoingiza kibia-shara. Na aliyeidhinisha dhulma hiyo ni Rais Nyerere kama alivyoandika Dr. Sivalon hapo katika uk. 65 wa kitabu chake mashuhuri Kanisa Katoliki na Siasa
Inaendelea Uk. 15

AN-NUUR

KAULI ya Kardinali Pengo aliyoitoa na kunukuliwa katika gazeti la Mwananchi la tarehe 25.6.2012 ikiwa na kichwa cha habari, kilichosema: Pengo: Wa h u n i w a s i a c h w e kuchoma Makanisa Zanzibar, haiwezi kupita bila kutolewa maoni. Ukiangalia kwa haraka utadhani kuwa Pengo kataja wahuni kama wahuni. La. Jina hilo amelitumia kuonyesha kuwa ni jinsi gani Maaskofu na viongozi wa kanisa wanavyowadharau viongozi wa Waislamu na Uislamu. Mwandishi wa gazeti hilo aliandika hivi: Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam Muadhamu Policarp Kardinali Pengo ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (CCM) kudhibiti wahuni wanaotaka kuvuruga amani visiwani humo. M w a n d i s h i anatufahamisha katika utangulizi wake huo, kuwa wahuni ni kina nani: Kauli hiyo ya Pengo ni ya kwanza tangu kuibuka kwa vurugu visiwani Zanzibar mapema mwezi huuhuku Makanisa yakilengwa zaidi na kikundi kinachojiita Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI). (Mwananchi ya tarehe 25.6.2012, Na. 043882 uk.4) Kwa maana hiyo ni kuwa viongozi wa Jumuiya ya Uamsho kina Farid na masheikh wenzake na Masheikh wote kwa jumla, ndio Pengo anawaita wahuni! Ingetosha kumwambia Kardinali Pengo kuwa, kuheshimiwa kwake kutakuwa na thamani kwa kuwaheshimu viongozi wa dini nyingine, vinginevyo tumwambie kuwa akome kuwadharau viongozi wa Waislamu. Akitoa kauli za kuichochea Serikali, ili iwachukulie hatua viongozi wa Kiislamu, alinukuliwa na gazeti hilo akisema: Kama sasa wahuni wameishinda nguvu Serikali ya watu kwa

Masheikh wetu Uamsho jueni huyu ndiye Pengo


Huu ndio mfumokristo unaowatafuna

SHEIKH Farid Had ( watatu kushoto) akiongoza maandanano ya amani yaliyoifanyika Zanzibar.

hiyo tutawaliwe na wahuni na wafanye wanalolitaka, tunajiuliza tunakwenda wapi? Kauli hii ya Kardinali Pengo, au kauli hizi za Maaskofu, huwezi kuzielewa undani wake, mpaka uwe umejishughulisha akili yako ili kujua maana yake na lengo la mfumokristo ulivyo ukusudia na unavyoukusudia kuufuta Uislamu tangu kuundwa kwa Kanisa Katoliki na kuzaliwa Makanisa mengine kwa jumla. Na ujue sera zao za kuutawala ulimwengu. Alichosema Kardinali Pengo ni kuwa: Kama Serikali ya Zanzibar imeshindwa nguvu na Wa i s l a m u [ w a h u n i ] , kwa hiyo tutawaliwe na Waislamu. Tunajiuliza [sisi Wakrito] tutaendelezea Ukristo wapi? Anamaanisha kuwa, watawala wa nchi hii ni Wakristo, hawawezi kutawaliwa na Waislamu.

Hata hivyo, Pengo akiwakebehi viongozi wa Serikali ya Zanzibar, mwandishi akimnukuu ameandika hivi: Tanzania ni huru sawa, lakini mimi sitaki kusadiki kuwa ni huru kwa kila Mtanzania. Wapo watu ambao wangependa wao waneemeke hata kwa madhara ya wengine bila huruma hadi siku ya leo. Niwakumbushe wasomaji kuwa, baada ya kuvunjwa lile Baraza l a Wa z e e w a TA N U lililokuwa linamshauri Nyerere, aliunda mbadala, wakiwa ni Maaskofu watatu wa kumshauri. Na hivyo, huenda baada ya Al-marhum Rais Idi Amin Dada alipompindua Rais Obote, ndio washauri hao walisaidia kumshauri Rais Nyerere kuwa na msimamo wa kukataa kuketi meza moja na Rais Idi Amini kujadili maendeleo na matatizo ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki jambo

lililopelekea kuvunjika kwa Jumuiya hiyo. Na huenda washauri hao ndio waliosaidia uamuzi wa kuingia vitani na Idi Amini katika vita vilivyobatizwa kwa kuitwa vita vya Kagera na baada ya vita tukaambiwa tufunge mikanda kwa miezi 18, kiasi kwamba mpaka sasa tumeshindwa kulegeza hiyo mikanda. Kwa wale walioshuhudia, ni kuwa tulikuwa na shida ya kila kitu, hata uzi wa kushonea nguo ujulikanao kwa jina la kibao na sindano ya kushonea nguo kwa mkono ilikuwa ni bidhaa adimu na muhimu, haikuweko na ukishikwa nayo unahesabiwa kuwa ni mlanguzi na mhujumu uchumi; sikwambii habari ya nguo, mpaka Waziri Mkuu wa wakati ule, Salim Ahmedi Salim, alilia machozi alipotembelea Mtwara na akawakuta watu wamekuja kumpokea na huku wamevaa mifuko

8
Na Abuu Jaafar Ali KWA mtu yeyote ambaye anatamani kuona siku moja Tanzania imeendelea, hawezi kupuuza madai ya wadau kuhusu ubovu wa NECTA. Kuna kila ushahidi kwamba kama hapakufanyika uchunguzi ambao utawaondolea wasiwasi baadhi ya wadau wake, itafikia mahali watu hao kudhani na hata kuamni kwamba Baraza hili limeundwa kwa njama (Conspiracy) dhidi ya jamii fulani. Kuhusu uundwaji wake kumbukumbu za Baraza lenyewe zinasema: It was felt that this was necessary part for consolidation of the countrys independence and disengagement from colonial restrictions in the education system. Kwamba ilionekana kwamba ili kuimarisha uhuru wetu na kujikomboa kutokana na mfumo wa elimu wa kikoloni ambao uliokuwa kikwazo kwa Watanzania, basi kuanzishwe NECTA. Hivyo Tanzania ilijiondoa kutoka Cambridge University Local Examinations Syndicate na hatimaye kujiondoa kutoka East African Examinations Council. Ilipofika Novemba 21, 1973 Sheria namba 21 kuhusu kuanzishwa kwa NECTA ilipitishwa na Bunge na kuanza kutumika rasmi Desemba 6, 1973. Katika vision ya NECTA imeandikwa kuwa, to contribute to national development through fair, efficient, and effective national examinations.. kwamba NECTA itachangia kuleta maendeelo ya taifa kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na uadilifu, ufanisi na tija katika mitihani ya taifa. Aidha kwenye orodha ya core values za NECTA imeandikwa kuwa ni ukweli/ uadilifu (integrity), tathmini ya kuaminika (valid assessment) na huduma za kukidhi matarajio ya wateja (customer satisfaction) miongoni mwa nyinginezo. Ukirejea hayo yanayodaiwa kusimamiwa na NECTA na hali halisi iliyopo ndani ya chombo hichi, utaona kwamba mambo yanasadifu barabara msemo wa Kizaramo wa vilongwa mbali na vitendwa mbali. Mwanzoni Baraza (Council) inayosimamia uendeshaji wa NECTA ilikuwa na wajumbe 27 ambao walipunguzwa hadi kukia 15 mwaka 1996 kufuatia marekebisho ya sheria ya NECTA. Kwa mujibu wa mfumo uliowekwa wa kulipa

Makala

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012


za Marian Girls za alama 7 hadi 9 mbona hazionekani miongoni mwa wataalamu wetu? Hoja ya msingi hapa ni kuwa wasomi hawa wanaofanya vizuri sana katika shule za sekondari, wanapotelea wapi? Mbona umahiri wao hauonekani huku juu? Yako maneno yanasemwa mitaani kuwa baada ya kazi ya kusahihisha kumalizika wapo watu wanajifungia NECTA kucheza na alama hadi kuweka sawa orodha ya shule zinazotesa. Lakini yapo pia madai kuwa Kamati hii inayoitwa ya kutunuku ambayo hufanya kazi zake kwa siri sana na ya Wakristo watupu, inaweza kuamua Kama mithili ya waganga wa kienyeji wanaweza kuamua kuwa katika somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu daraja C lianze na alama 60. Yeyote aliyepata alama 30 hadi 59 apewe daraja D. Au kwenye mtihani wa kidato cha sita ili mwanafunzi apate daraja la A katika somo la Advanced Mathematics basi apate alama labda 87 au 88. Mfano mzuri ni pale watati wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi walipoambiwa eti , alama za gredi zinazotolewa na kwa watahiniwa huamuliwa na jopo la wasahihishaji wa somo husika kwa kuzingatia kiwango cha ufaulu kwa mwaka husika . ( Tazama rasimu 2 uk 87 wa ripoti ya utati kuhusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu kidato cha nne 2010). Hakuna mwalimu yeyote aliyeko katika shule ya sekondari ya serikali au hata ya Binafsi ya kawaida anayeweza kufanya mapendekezo eti A ya Advanced Mathematics ianze na maksi 88. Au mwalimu anayefundisha shule ya Kiislamu apendekekeze eti alama C ianze na maksi 60. Hakuna kwa sababu huu ni wendawazimu na hakuna mwalimu mwenye wazimu anayechukuliwa kusahihisha mitihani ya NECTA. Kwa kila anayejua mambo, anapata hofu kubwa anapoanza kukiri ni kwa nini NECTA inaogopwa na wakuu wa nchi. Mtu anajiuliza hivi inasimamiwa na nani? Huyo mtu au kikundi cha watu kina nguvu za kisiasa kubwa kiasi gani? Hivi watoto wa masikini ambao hawaelewi kinachoendelea huko NECTA watakombolewa na nani? Maswali mengi hayana majibu. Hebu jiulize ni kwa nini serikali itumie pesa zake kufanya utafiti tangu mwaka 2010 lakini iogope kuiagiza NECTA kutekeleza Inaendelea Uk. 11

AN-NUUR

NECTA: Mbuyu uliomsinda Kawambwa una siri gani?


kanisa fursa bora, kila mara Council hii huwa ni miliki ya Wakristo watupu. Ukiona mjumbe ambaye ni Muislamu, basi ametokea Bakwata au Zanzibar. Aidha hakuna katika historia ya NECTA wakati ambao kumewahi kuwepo na Mwenyekiti au Katibu Mtendaji Muislamu. Na zaidi Idara zote za NECTA zinaongozwa na Wakristo tangu kuanza kwake. Kasoro zote hizi zimekuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu sasa lakini hakuna mtu aliyeko tayari kutizama ukweli au uwongo wa madai haya ya Waislamu na athari zake. Wenye nchi wamechagua kufumba macho, kuziba masikio au kupuuza madai ya wadau ambao NECTA inadai kuwa itawapa huduma hadi waridhike! Matatizo ya kudumu katika NECTA ni pamoja na kuvuja kwa mitihani na wizi wa vyeti. Aidha yamekuwepo madai ya muda mrefu kuwa NECTA inatekeleza majukumu yake kwa upendeleo mkubwa. Wanaochukuliwa kutunga mtihani, wanao-moderate na wale wanaosahihisha huchaguliwa kutoka kundi la watu fulani. Kila paneli wamo. Haya ni madai. Na inadaiwa kuwa Kazi yao ni kuhakikisha kwamba shule za kimisheni au kama zinavyojulikana siku hizi shule za Seminari zinatesa. Ufumbuzi sio kuyapuuza. Uchunguzi wa hakika unahitajika. Wenyeviti wa paneli wanachaguliwa kwa makini ili wasije kuingia watu wasiofaa. Kama madai haya ni kweli, je, usahihishaji wa shule za Kikristo utakuwa sawa na wa shule nyingine? Kitu gani kitawaondolea Waislamu ule wasiwasi aliosema Mzee Edwin Mtei kuwa wakikaa mahali watu wa serikali na wakiwa wengi wa dini moja, basi akili na namna yao ya kufanya kazi hutawaliwa na kuongozwa na mwelekeo wao wa kidini. Mind set hii anayozungumzia Mzee Mtei, ndiyo iliyowagharimu vijana wa Kiislamu katika somo la Islamic Knowledge 2012. Huko Kamati ya Kutunuku hakuna mtu aliyekuwa hata na nafasi ya kuangalia wasahihishaji wanasemaje. Wala hakuna aliyepata fursa ya kulinganisha matokeo ya 2012 na yale ya 2011 kama wanavyodai kuwa huzingatia hilo. Pia hakuna aliyepitia normal curve iliyotolewa na watu wa mfumo wa kompyuta. Haraka ilifanyika kupandisha alama ya ufaulu. Hakuna mwenye nafasi ya kuhangaika na Waswahili, tangu hapo kufeli ni kawaida yao! Ushahidi wa haya hupatikana pale wanapojikuta wakiwa takribani peke yao katika shule na vyuo vya umma. Aidha kila kunapotolewa orodha ya wakubwa waliaojiriwa au kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali serikalini pia wanaopata fursa hizo kwa kiasi kikubwa ni Wakristo. Uholela huu wa NECTA umeachwa hadi sasa taifa linalalamika kuwepo wahitimu feki wa Vyuo Vikuu kama ilivyoripotiwa hivi karibuni na mtafiti mmoja wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, IFM. Wahitimu hao inadaiwa hawajiamini na kwa sababu hiyo wale wanaosomea shahada za uzamili wanaandikiwa tansifu zao na watu wengine. Aidha imedaiwa pia katika utafiti wa mtaalamu huyo kwamba wengine wamekuwa wakiwasilisha kazi ambazo zimeshafanywa katika vyuo vingine. Huu ni udanganyifu. Udanganyifu huu unaweza kutusaidia kujibu baadhi ya hoja za baadhi ya watu wanaohoji hizo divisheni wani

Makala

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21- 27, 2012

AN-NUUR

Uhalifu wa Marekani dhidi ya Binadamu


Historia ndiyo adui wataalamu wa ubadilishaji kra wanaposhika hatamu
uliokithiri, au kujiua (kwani Wa m a r e k a n i w a l i o j i u a wenyewe wanalingana na wale waliokufa vitani), wala kushindwa na jeshi la kujihami la jamii masikini. Ilikuwa, kwa mujibu wa Bw. Hopey Changey (tumaini la mabadiliko, Change we can believe in) moja ya matukio ya kushangaza ya ujasiri na uadilifu katika historia ya kijeshi (ya Marekani). Siku iliyofuata, gazeti la New York Times lilichapisha makala ndefu iliyoonyesha jinsi Obama mwenyewe anavyochagua nani watakaouawa kwa mabomu ya drone, ndege za kivita zisizo na rubani, maeneo tofauti duniani. Anafanya hivyo katika Jumanne za kigaidi, ambako anaangalia picha ndogo ziliowekwa katika orodha ya wanaotakiwa kuuawa, baadhi yao wakiwa na umri chini ya miaka 20, mmojawapo akiwa msichana ambaye alionekana mdogo kuliko hata miaka yake 17. Wengi wao hawajulikani au wamefikia tu umri wa kuingia jeshini. Zikiwa zinaongozwa na marubani walioketi mbele ya vioo vya kompyuta mjini Las Vegas (Marekani), drone hizo zinalenga makombora ya Hellre (Moto wa Jahannamu) ambayo yananyonya hewa kutoka kwenye mapafu na kulipua watu wabaki vipande vipande. Mwezi Septemba (mwaka jana) Obama alimwua raia wa Marekani, Anwar al-Awlaki kwa habari za kuvumishwa tu kuwa alikuwa akichochea ugaidi. Huyu ni rahisi, ananukuliwa na wasaidizi wake akisema wakati akitia saini kifo cha mtu huyo. Hapo Juni 6, drone iliua watu 18 katika kijiji Afghanistan, wakiwemo watoto, wanawake na wazee waliokuwa wakifurahia harusi. Makala hiyo ya New York Times haikuwa imetokana na kuvuja kwa habari au kuchuliwa. Ilikuwa ni taarifa ya majigambo iliyoasisiwa na utawala wa Obama kuonyesha jinsi amiri jeshi mkuu alivyo thabiti katika mwaka wa uchaguzi mkuu. Ikiwa atachaguliwa tena, Brand Obama (bidhaa) itaendelea kutumikia wenye fedha, kufuatilia wanaosema ukweli, kutishia nchi, kueneza virusi vya komputa na kuua watu kila Jumanne. Vitisho dhidi ya Syria, vinavyoratibiwa Washington na London, vinakia ngazi mpya ya unafiki. Tofauti na propaganda za wazi zinazotolewa kama habari, uandishi wa kichunguzi wa gazeti la Ujerumani,

Na John Pilger

BAADHI ya maasa wa polisi wa Marekani wakimdhibiti mmoja wa waandamanaji nchini Marekani wanaopinga dhulma inayofanywa na serikali yao kwa nchi nyingine. NIKIWA naingia katika kijiji cha Vietnam Kusini, niliwaona watoto wawili wadogo waliokuwa mashuhuda wa vita virefu zaidi katika karne ya 20. Ulemavu wao wa kutisha ulikuwa unaonekana sehemu nyingi. Eneo lote la Mto Mekong, ambako misitu ilikuwa imeteketezwa na kubaki kimya, watu waliobadilika vinasaba waliishi vyema kiasi walichoweza. Leo, katika hospitali ya watoto ya Tu Du mjini Saigon, chumba cha upasuaji cha zamani kinaitwa chumba cha makusanyo, lakini lugha rasmi ni chumba cha kihoro. Ina milolongo ya chupa kubwa zenye vitoto vya kutisha vilivyoharibikia tumboni. Wakati wa uvamizi wake wa Vietnam, Marekani ilitumia kemikali ya kupukutisha majani katika mapori na vijiji kumchua adui, Hii ilikuwa Agent Orange, iliyokuwa na dioxin. sumu kali ambazo zinaeweza kusababisha kifo cha kitoto tumboni, kutoka kwa mimba, kudhurika vinasaba na saratani. Mwaka 1970, Ripoti ya Senate ya Marekani ilichua kuwa Marekani imemwaga (juu ya Vietnam Kusini) kemikali za sumu kiasi cha ratili sita (karibu kilo tatu) kwa kila mkazi, wakiwemo wanawake na watoto. Jina la siri la kumwaga silaha hiyo ya maangamizi iliitwa Operation Hades (yenye maana ya kuzimu au Jehanamu). Baadae ilibadilishwa ikaitwa Operesheni Ranch Hand, (kama vile ni shamba la mifugo). Leo hii inakisiwa kuwa waathirika milioni 4.8 wa Agent Orange ni watoto. Len Aldis, katibu wa chama cha uraki wa Uingereza na Vietnam, hivi karibuni alirudi kutoka Vietnam akiwa na barua kwenda kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kutoka Umoja wa Wanawake wa Vietnam. Rais wa umoja huo Thi Thanh Hoa, alielezea athari kubwa za kimaumbile (zilizosababishwa na Agent Organge) kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Aliitaka OIC kukiria upya kukubali ufadhili wa Michezo ya Olimpiki ya London uliokuwa ufanywe na Kampuni ya Dow Chemical Corporation, moja ya makampuni ambayo yalitengeneza sumu hiyo na imekataa kuwadia waathirika wake. Aldis aliwasilisha barua hiyo katika ofisi ya Lord Coe (Sebastian Coe, mwanariadha mashuhuri wa Uingereza zamani), ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki, London. Hajapata jibu lolote. Wa k a t i A m n e s t y International ilipokumbusha kuwa mwaka 2001 Dow Chemical ilinunua kampuni iliyohusika na uvujaji wa gesi huko Bhopal nchini India (mwaka 1984) ambayo iliua watu kati ya elfu saba na elfu kumi papo kwa papo na wengine 15,000 katika miaka 20 iliyofuata, David Cameron (Waziri Mkuu wa Uingereza) aliita Dow kuwa ni kampuni yenye sifa. Hivyo ni furaha na vijo wakati camera za televisheni zinapoonyesha pambo lenye thamani ya pauni (za Kiingereza) milioni saba linalofunika uwanja wa Olimpiki (London), linalotokana na mkataba wa miaka kumi kati ya OIC na mharibifu huyo aliyekubuhu. Historia imezikwa na waliokufa na kuharibiwa wa Vietnam na Bhopal. Na historia ndiyo adui mpya. Mnamo Mei 28, Rais Obama alizindua kampeni ya kubatilisha historia ya vita vya Vietnam. Kwa Obama, hapakuwa na Agent Orange, wala maeneo ya kushindilia risasi bila kizuizi, hapakuwa na kucha mauaji ya watu wengi, wala ubaguzi

Frankfurter Allgemeine Zeitung zinawataja wahusika wa mauaji ya watu wengi mjini Houla kuwa ni waasi wanaosaidiwa na Obama na Cameron. Waliolihafamisha gazeti hilo ni pamoja na waasi wenyewe. Uthibitisho huo haujapuuzwa moja kwa moja nchini Uingereza. Akiandika katika blogu yake binafsi, kimya kabisa, Jon Williams, mhariri wa habari za kimataifa wa BBC, anaongeza ufuatiliaji wake binafsi wa suala hilo, akiwanukuu maosa wa nchi za Magharibi wakisema kuwa operesheni ya kiakili dhidi ya Syria ilikuwa imefana sana. Ilifana kama kuvunjiliwa mbali kwa Libya, na Irak na Afghanistan. Na pia ni ya kufana kama ubunifu wa gazeti la Guardian likimkuza Alastair Campbell, mshirika mkuu wa Tony Blair katika uvamizi hadisi wa Irak. Katika kumbukumbu zake za tarehe hizo, Campbell anajaribu kupaka damu ya Irak kwa pepo liitwalo Murdoch (mmiliki wa magazeti yaliyofikiwa na kashfa ya kusikiliza simu za watu binafsi). Ipo ya kutosha kuwalowesha wote. Lakini kukubali kuwa vyombo vya habari vyenye hadhi, vya kiliberali na vinavyompenda Blair vilikuwa na nafasi ya ziada muhimu katika uhalifu huo mkuu kumechwa na kumebakia ni jaribio muhimu la kitaaluma na kimaadili nchini Uingereza. Ni kwa kitambo gani tutaendelea kuwa chini ya serikali kivuli ya aina hiyo? Kielelezo hicho cha propaganda ya kupotosha kilitumiwa kwanza na Edward Bernays, mpwa wa Sigmund Freud (mwanzilishi wa psychoanalysis) aliyetunga fani ya mahusiano (public relations), haijawahi kuonekana bayana kiasi hicho. Kutunga uhalisi ambao haupo kunahitaji kusahau historia, kusema uwongo kwa kukwepa, na kuhamisha kilicho muhimu katika visivyo muhimu, Kwa njia hii, mifumo ya siasa inayodhamiria usalama na haki kijamii imedilishwa na uharamia, kufunga mkanda na vita visivyoisha - ukereketwa wenye nia ya kuangamiza demokrasia. Ingekuwa ni mtu binafsi angeweza kuitwa mwendawazimu, Kwanini tunaikubali? (Imefasiriwa na Anil Kija kutoka makala ya John Pilger yenye kichwa cha habari: U.S. Crimes Against Humanity? History is the Enemy as Brilliant Psy-ops Become the News. www.johnpilger. com)

10
Na Abuu Rayhaan. NENO amani limekuwa likitumiwa na watu wa kada mbali mbali katika dunia hii. Mara nyingi watumiaji humaanisha ni hali ya utulivu isiyokuwa na uhasama wala matumizii ya nguvu. Ni kwa mujibu wa tafsiri hii, Tanzania kwa miaka mingi sasa, imekuwa ikitolewa mfano na mataifa ya kilimwengu kuwa ni kisiwa cha amani. Dunia ilishawishika kutoa nembo hiyo ya upendeleo ya lulu ya amani kutokana na ukimya uliotanda katika nchi hii yenye Waislamu wengi kutokana na kutokuwa na heka heka ambazo zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani hiyo. Wa t a w a l a n c h i n i hawakubaki nyuma pia katika kujisifu juu ya amani hiyo. Katika kudodosa juu ya ni kwa nini Tanzania imeweza kudumu na amani hiyo utapata majibu anuwai kama vile ni nchi inayozingatia utawala bora, utawala wa sheria ambapo kila mmoja anapata haki yake kwa mujibu wa sheria za nchi. Huu ndio upatu maarufu ulioenea kwenye masikio na akili za walio wengi hasa wa mataifa ya nje. Hata hivyo ukweli unabaki kuwa, kwa tafsiri hiyo ya neno amani, Tanzania imeweza kudumu katika hali hiyo kwa sababu kubwa tatu; kwanza watu walio wengi kutojua haki zao, pili kwa waliobahatika kuzijua haki zao kutokuwa tayari kuzidai ama kwa sababu ya woga au kutojua njia muafaka ya kupitia kuliendea hilo na tatu wale waliozijua na wakawa kwa muda mrefu wanatumia njia ya kidiplomasia katika kuzidai haki hizo na wakaendelea hivyo hivyo hata pale walipopuuzwa na madhalimu hao. Nathubutu kusema bila kicho kuwa Waislamu ndilo kundi linaloangukia kwenye makundi haya kwani limekuwa ndilo tabaka dhulumiwa katika uchumi, elimu, siasa, mamlaka (uongozi), kijamii na katika nyanja nyingine nyingi zinazotengeneza mustakabali wa maisha katika nchi yao huru. Waislamu walinyamaza kwa lengo zuri la kuendelea kulinda amani ya nchi yao. Kwa bahati mbaya kila walipojitahidi kuendelea kuvuta subira na kunyamaza, ukimya ule ulilipelekea kundi dhalimu kuendelea kugandamiza palepale penye jeraha na hivyo kuzidisha maumivu kwa Waislamu. Hii imedhihirisha wazi

Makala

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012


amani ya nchi! kama ilivyo kawaida kuwa muovu hukaa gizani. Vipo vikao kadhaa vinafanyika baina ya baadhi ya Waislamu na Wakristo ili amani ya nchi isivurugwe. Mfano mzuri ni mkutano uliofanyika ukumbi wa Movenpick Royal Palm jijini Dar es Salaam tarehe 9/2/2011 (siku chache baada ya kongamano la Diamond Jubilee juu ya mfumo kristo) uliokuwa na anuani Nafasi na Wajibu wa Viongozi wa dini katika ujenzi wa amani ambapo mgeni rasmi katika mjumuiko huo alikuwa ni Mzee Reginald Mengi. Huyu alikuja kuwahutubia viongozi wa baadhi ya Waislamu na viongozi wa wakristo. Yaani maana yake Quran ilikosa mafunzo kwa Waislamu hao waliohudhuria mkutano huo na hivyo kuona wangeyapata kwa muheshimiwa mgeni rasmi. Muendesha ratiba kwa u p a n d e w a Wa i s l a m u alifungua kwa salamu iliyosomeka hivi Assalaam alaykum warahmatullah wabarakatuh, Bwana Yesu a s i f i w e , Tu m s i f u Ye s u Kristu. Baadae mwendesha ratiba kwa upande wa wakristu alimkaribisha askofu Philemon ambaye ni mwenyekiti wa maaskofu mkoa wa Dar es Salaam ili asome sala ya ufunguzi. Aliongea mengi katika sala yake hiyo lakini ilikia hatua akiwa anasikilizwa kwa utulivu kutoka kwa Waislamu na Wakristo waliohudhuria kwenye mkutano huo wa aina yake alisema miongini mwa maneno yake kuwa Katika jina la Yesu, mwana wako wa pekee, Mungu mkuu na mfalme Ni kutokana na sura hii ya mkutano huu baadhi ya raia wema Tanzania waliuita mkutano wa umoja wa baadhi ya Waislamu na baadhi ya wakristo (UBWABWA). Sina hakika kama wale viongozi wa baadhi ya Waislamu waliohudhuria hawazijui aya hizi za Allah (sw) katika Quran; (3:118 - 120) Allah (sw) anapoeleza kuwa Enyi mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu wasiokuwa katika nyinyi: hao hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yale yanayokudhuruni. Bughudha (yao juu yenu) inadhihirika katika midomo yao. Na yanayofichw a na vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekubainishieni dalili (zote) ikiwa nyinyi ni watu wa kufahamu. Oh! Nyinyi mnawapenda (maadui zenu hao), hali wao hawakupendeni! . . . wanapokuwa peke yao wanakuumieni vyanda kwa Inaendelea U. 11

AN-NUUR

Tanzania kisiwa cha amani kisicho amani

kuwa kumbe kunguru hafugiki!! Ni kwa sababu hii imekia hatua Waislamu wakaona kuwa dhulma hizi hazitokei kwa bahati mbaya na hazina mpango wa kukia kikomo kama hakuna jitihada za kujihami kwa lugha ambayo itafahamika wazi kwa dhalimu. Uislamu hauruhusu dhulma, lakini pia haukubali mtu kudhulumiwa haki yake. Na mtu kupigana ili kulinda haki au heshima yake hadi mauti yakamkuta ni katika jihadi na mtu huyu hufa shahidi. Uislamu ni dini ya amani na Waislamu ni watu wa amani pale watakapoheshimiwa na kulindwa hadhi yao na ya dini yao. Kinyume chake ni sawa sawa. Waislamu wa Tanzania kama kwamba sio raia wa nchi hii, wamekuwa wakionewa, wakidhalilishwa, wakibezwa, wakikejeliwa, wakitukanwa na kufanyiwa kila aina ya uovu na serikali inayoendeshwa na mfumo wa kanisa. Mfano mzuri tukiacha makubwa mengine, tuchukue muda huu mfupi wa sensa ambapo baadhi ya nyumba za Waislamu zimekuwa zikivamiwa usiku wa manane na kuwakamata watu kwa sababu eti ya kukataa kuhesabiwa. Kweli hiki kilichofanya hivyo ni

chombo cha usalama au majambazi? Hizi ni sheria gani zinazoruhusu kuingilia uhuru wa faragha ya mtu? Huku ni kupindukia mipaka. Ni kwa sababu hizi za kujipa mamlaka kinyume na sheria za kiutendaji zilivyo, mkuu wa kituo cha polisi Mkuyuni Morogoro aliripotiwa kuingia nyumbani kwa Muislamu bila ya mwenye nyumba wala mke wake kuwepo na kupekua nyumba nzima eti kwa sababu mwenye nyumba amegomea sensa!!! Askari kama hawa wanaovunja katiba wamepata wapi mamlaka haya? Faragha ya mtu ni haki ya kikatiba kwenye ibara ya kumi na sita (16) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara). Ni kwa sababu hizi hizi za kiuonevu, iliripotiwa huko Kyaka katika mkoa wa Karega kuwa askari waliendesha operesheni ya kamata kamata kwa Waislamu waliowaita wenye ndevu na suruali fupi eti na wao hawajashiriki sensa. Hivyo akili ya chombo hicho cha usalama iliagiza kuwa akionekana Muislamu yeyote mwenye ndevu na/au suruali fupi (la kisunnah) basi huyo hajahesabiwa, kwa hiyo akamatwe. Katika kushughulikia matatizo ya kijamii ni kanuni kuwa usishughulikie matokeo

ya tatizo bali angalia kiini cha tatizo ni nini. Hivi ni kweli kuwa pamoja na udhalili wote unaofanywa na serikali/kanisa dhidi ya waislamu, madai yao hadi sasa hayajulikani? Au yameshajulikana na hiyo ndiyo njia muafaka, nzuri na nyepesi ya kuyatatua? Yo t e n i d a l i l i k u w a si serikali wala chombo kingine chochote cha dola kilichokuwa tayari kutatua m a t a t i z o y a Wa i s l a m u . Sasa Waislamu wameamua kujitatulia matatizo yao wao wenyewe moja baada ya jingine. Imefikia hatua Waislamu wamesema basi! Itadumu kanuni ile ile ya usishughulike na mbwa aliye juu ya mti bali shughulika na yule aliyempandisha maana ukimwacha mpandisha mbwa ukashughulika na kumshusha mbwa, ukiondoka atampandisha tena. Hata hivyo ukiona mbwa yule anaweza kupata ujasiri wa kuruka na kukujeruhi pindi ukianza kumshughulikia mpandishaji basi anza na mbwa kisha shughulika na mpandishaji. Waisalamu wamechoka kuwa ngazi ya kupandia. Ni kutokana na kuona ishara za kuwa Waislamu wameamua kushughulikia mambo yao, baadhi ya wanyonyaji wameanza kuweweseka na kutafuta mbinu za kuendelea kulinda

11

Makala

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21- 27, 2012

AN-NUUR

NECTA: Mbuyu uliomsinda Kawambwa una siri gani?


Inatoka Uk. 8 mapendekezo yaliyotolewa baada ya utati huo? Ta z a m a b a a d h i y a mapendekezo mapendekezo ya utati wa serikali: Uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo, uadilifu na uwajibikaji. Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalamu, tathmini na tati za kisayansi ili kuleta ufanisi. Mfumo rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika kwa wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki kwa watahiniwa. alama za CA zitumike katika mtihani wa taifa wa kidato cha nne kama ilivyoelekezwa katika mwongozo wa mazoezi endelezi na Uteuzi wa wasahihishaji unafanyika kwa upendeleo na hivyo hupoteza umakini katika usahihishaji. Kama mapendekezo haya yangefanyiwa kazi tatizo lililotokea katika somo la Islamic Knowledge lingeweza kuepukwa. Serikali inaambiwa na w atafiti w ake kw amba NECTA iweke wazi gredi za masomo kwa wadau wake, lakini inaogopa kuiagiza NECTA kufanya hivyo. Sisi Tuelewe kwamba NECTA ni kubwa kuliko serikali au waliounda NECTA wana

DKT. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Tanzania kisiwa cha amani kisicho amani


Inatoka Uk. 10 uchungu (wa kukuchukieni). Ikikupateni kheri huwasikitisha. Na ikikupateni shari wanaifurahia. Na kama nyinyi mkisubiri na mkamcha Mungu hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua vizuri yote wanayoyatenda Katika nasaha za kufunga mkutano huo mgeni rasmi alinukuu maneno ya Mmarekani mmoja Martin Luther King Junior aliposema Ukiuona uovu unatokea mahali, ukimwona mwenzako anamfanyia mwenzake uovu na ukashindwa kuukemea, wewe ni sehemu ya ule uovu kisha akaendelea kuwa Jambo baya kuliko yote ni pale watu wema wanapoona mabaya yanatendeka wakanyamaza Wajumbe mliohudhuria katika mkutano huo, hivi ni kweli tokea hapo hamjaona mabaya yanatendeka nchina ili myakemee? Au kwenu nyie uovu una maana gani? Mtume (s.a.w) ameeleza kuwa atakayejifananisha na kundi fulani basi yeye pia ni katika kundi hilo. Na sasa Waislamu wameamua kuondoa uovu/ uvundo unaotishia hali ya hewa Tanzania kwa kutumia mikono yao. Mkutano huo ulipitisha maazimio kumi lakini kwa leo nitataja na kuongelea azimio moja tu ambalo kwa kutajwa lilikuwa ni la pili. Linasomeka hivi; Viongozi wa dini na serikali katika ngazi zote wasimamie utendaji wa haki ambalo ndilo tunda la amani la nchi yetu Baada ya kusoma maazimio yote kumi, msomaji wa maazimio hayo ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi alisikika akisema kuwa kwa yaliyoongelewa, kila mwenye akili salama lazima akubaliane nayo. Vizuri lakini sasa mbona mmeyakana kiutendaji nyie wenyewe? Au akili salama haipo tena hata kwa waliohudhuria? Ilitarajiwa kuwa viongozi wote kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja na kuendelea wawe ni waangalizi wa kuhakikisha haki inatendeka na kuwa tayari kukemea pale linapotokea jambo la kuhatarisha amani hiyo kwani haki ndilo tunda la amani la nchi yetu Kinyume chake baada ya hapo yameshuhudiwa mengi w a k i f a n y i w a Wa i s l a m u katika nchi hii na hakuna aliyediriki kunyanyua ulimi wake angalau kulaumu kwa nini Waislamu wanatendewa hivyo. Mathalan kamata kamata ambayo imekuwa ikiendelea kipindi chote cha sensa, maoni ya Waislamu kupuuzwa bila hoja za kuyadhoofisha, baadhi ya Waislamu kuvamiwa usiku wa manane na kukamatwa kilichopelekea kuwavunjia utu na haiba yao, baadhi ya waislamu kutukanwa na vyombo vya usalama kwa sababu za kadari ya Allah (sw) kama ilivyotokea huko Arusha kwa Bi Rukia Dereva, kuwalaza watoto wachanga mahabusu bila kujali sheria za nchi na za kimataifa zinasemaje, kuwaondoa watu katika uislamu kwa sababu ya kukataa kufuata rai za watu fulani zilizotolewa kinyume na maamuzi ya shurah, kuwavamia na kuwashambulia Waislamu wakiwa katika dua ya pamoja kwenye majonzi baada ya meli kupata ajali karibu na bandari ya Zanzibar na mengine mengi. Wahudhuriaji wa mkutano wa amani Movenpick haya hamyaoni? Mbona kimya? Mko wapi? Au haya hayahatarishi amani? Au kwenu nyie haki ambayo ni tunda la amani la nchi yetu maana yake nini? Au ndo mnazidi kudhihirisha kuwa

haki ni kwa baadhi ya watu fulani na wengine hawana haki? Hamuoni kuwa kufanya hivyo ni uvunjifu wa wazi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kama ilivyo katika idara ya kumi na mbili na kumi na tatu? Wa i s l a m u Ta n z a n i a wamechoka kuwa wapangaji katika nyumba waliojenga wenyewe. Ni kwa sababu hii Waislamu wanatakiwa waunganishe nguvu zao pamoja ili kumwondoa dhalimu wao kwa lugha itakayokuwa rahisi kufahamika kwake. Waislamu wasidhulumu na wasikubali kudhulumiwa, na wasimamie uadilifu popote pale walipo hata kama itakuwa ni kutoa uhai wao. Wasikubali dini yao kuchezewa kwani dini ndiyo haiba ya utu wao vinginevyo hakuna sababu ya kuendelea kuishi katika ardhi ya Allah (sw).Na tumtangulize Allah (sw) katika tuyafanyayo kwani ndiyo ufanisi kama alivyosema kwenye Quran kuwa Na msilegee wala msihuzunike, maana nyinyi ndio mtakaokuwa juu ikiwa mnaamini kweli (3:139). Waislamu bado nafasi ya ushindi iko wazi tusikate tamaa.

Bible Knowledge akipata 50 hupewa C. Yote haya ni madai ambayo yanahitaji uchunguzi wa kina na makini kwani yanaashiria kuwepo kwa matumizi mabaya ya osi!. Kwa muda mrefu sasa hakuna Mratibu wa somo la Kiarabu wala Islamic Knowledge/Elimu ya Dini ya Kiislamu aliyeajiriwa NECTA kama kanuni zinavyotaka. Badala yake analazimishwa kuratibu mtu ambaye hana ujuzi n a y o . Wa k a t i h a y o y a k i t e n d e k a N E C TA imemwajiri mchungaji M E Mtelezi kuwa Mratibu wa Bible Knowledge na Divinity. Katibu Mtendaji wa NECTA pamoja na BARAZA wote wanadai kwamba wamenyimwa vibali vya kufanya ajira mpya pamoja na ajira mbadala. Je, kibali cha ajira ya mchungaji kilipatikanaje? Maendeleo ya nchi hayataletwa na wasomi wanaotumiwa kupiga vita maendeleo ya jamii nyingine katika nchi moja. Leo kwa sababu ya utaratibu mbaya na wa siri usiofahamika kwa wadau,
NECTA huchukua zaidi ya miezi miwili kutangaza matokeo baada ya kazi ya kusahihisha kumalizika. NECTA haikosi kuwa na mfumo wa compyuta ambao kwa muda ya chini ya siku moja unaweza kufanya kazi yote na kutangaza matokeo. Hata kama ni suala la kushughulikia kasoro zilizorekodiwa, hili halihitaji muda wa zaidi ya siku saba kuingiza maksi katika mfumo na kurekebisha kasoro hizo. Swali ni je, muda wote huu NECTA inaotumia kukaa na majibu ya mitihani, inafanya nini?

uwezo wa kuwashughulikia akina Mheshimiwa sana Shukuru Kawambwa kwa hiyo inabidi wabaki kumsifu Dr. Joyce Ndalichako? Yapo madai kuwa katika somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu, baadhi ya wakati mwanafunzi akipata 59 hupewa D wakati yule wa

12
Jihadi ya Wasakatonge!!!
Mnada ulonadiwa, na BAKWATA wa JIHADI, Si vyema kunyamaziwa, ni lazima kuurudi, Kwa pumbaze pembuliwa, na wa batini muradi, WITO huu wa JIHADI, SI wa DINI bali TONGE. Wito wao ni wa TONGE, si wa ya dini JIHADI, Falau hili wapinge, kulinena sina budi, Ni ya TONGE hili GENGE, linoinadi JIHADI, WITO huu wa JIHADI, SI wa DINI bali TONGE. GENGE hili kwa hakika, hufanya kila juhudi, Na wenziye washirika, WAGALA na WAYAHUDI, Dhidi ya dini hakika, ya Mola wetu MAJIDI, WITO huu wa JIHADI, SI wa DINI bali TONGE. Adaye siyo kujenga, bali mambo kusidi, Kumbuka lilivyolonga, kwa SENSA na kuahidi, Keshoye likabananga, kwa TONGE si kwa weledi, WITO huu wa JIHADI, SI wa DINI bali TONGE. Fedheha imelikumba, kwa ya SENSA kukaidi, Kwa kote kwake kulumba, kwa uvumba na kwa udi, Lengole ni kujikomba, na TONGELE kusanidi, WITO huu wa JIHADI, SI wa DINI bali TONGE. Kaditama nimeka, beti sita sitazidi, GENGE hili kulizika, kamwe nyuma tusirudi, Hadi litapofutika, na wa kwake usadi, WITO huu wa JIHADI, SI wa DINI bali TONGE. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Barua/Shairi

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012

AN-NUUR

Maono YANAIFEDHEHESHA SERIKALI


Ndugu Mhariri NAOMBA Unipe japo Nafasi Kidogo name nitoe duku duku langu la moyoni, Ni jambo linalofahamika vyema kwamba elimu ndiyo ufungo wa maisha na na maendeleo. Nchi zote zilizoendelea na zinazoendelea zimefikia hapo zilipo kutokana na kuwekeza vya kutosha katika elimu na kuithamini kiukweli elimu yenyewe. Elimu ni mwanga, utati na majibu ya changamoto mbalimbali katika jamii nan chi kwa ujumla. Lakini kwa bahati mbaya hapa nchini kwetu imekuwa kinyume! Baada ya elimu kutoa majibu sahihi ya mambo mbali mbali, serikali imekuwa inategemea MAONO ya mwalimu Nyerere au ya mababa Askofu katika kutoa uwamuzi au majibu ya mambo ya kitaifa. Kwa namna ambayo elimu ya siasa ilivyo ratibiwa na kusimamaiwa na hayati Mwalimu Nyerere, sasa inaonekana kila jambo ni lazima liwe kwa mujibu wa Nyerere na maaskofu, Sasa Wasomi wa Bongo wamelemaa. Usoni wao hausaidii nchi kupata majibu sahihi na kusonga mbele kwa wakati. Wao wanatumia na kuamini maono badala ya utati! Matokeo ya hali hii, tunaona nchi inavyoyumba na kupepesuka yanapokuja mambo yanayohitaji majibu sahihi, uwamuzi wakweli, wa kisomi haki na kisheria, hasa suala lenyewe likawa linahusu uislamu na waislamu. Tukiangalia kwa ufupi matukio ya hivi karibuni; Sensa, Baraza la mitihani na tume ya maoni ya katiba mpya tunaon, dhahiri sahiri, Jinsi serikali inavyofedheheka mbele ya wananchi na dunia kwa ujumla. Imekuwa kama wananchi wanathibitisha kuwa, kweli hawa si viongozi wao, bali ni mamluki Fulani! Hoja za waislamu zinasimama , tena wima ( Sensa), hazipingiki na kweli, lakini wanatukanwa, kupuuzwa na kusimangwa kwa sababu naono ya Nyerere na wenzie yashakataa. Au Kwa Sababu washirika wa serikali na kanisa wa Miaka mingi, Bakwata nao eti wakiwapinga waislamu wenzao waliogomea Sensa, Ingawa ndiwo walioshika njia nzuri ya kisomi, kiadilifu na kiimani, hata kama hawa mabakwata wangelikuwa wengi, bado isingelikuwa hoja, wingi wao. Mwaka 1992 Serikali ilikubali mfumo wa vyama vingi kwa kukubali mwaka 1992 serikali ilikubali mfumo wa vyama vingi kwa kukubali maoni ya mwananchi 20% badala ya 80% waliokataa. Hapa Serikali ilizingatia usoni na utambuzi wa mambo. Hata hivyo Mahmoud Nejad na Iran yake Jeuri yake ipo katika elimu na utati, siyo maono, serikali isiwe kinyume na usomi na uadilifu. Na kuhusu NECTA, hali ni ile ile hujuma zinaoekana wazi na kuthubitika. Hakuna siri tena, waislamu wanatembea na ushahidi wao mikononi, unaonyesha wanavyobaguliwa na kufelishwa pale

NduguYangu Mhariri, Ninawapongeza sana kwa kazi ngumu lakini mkijitahidi kuifanya kwa ufanisi kulingana shida ya sisi wasomaji wenu. AN-NUUR niko na nyinyi mda mrefu sana nikiwa msomaji wenu upo wakati mwingine mnayumba kidogo haraka

Nawapongeza
sana mnarejea kwenye mstari. Sishangai sana kwakuwa nchi zetu haziko kidemokrasia na tuna tatizo jingine mfumo kristo. Hongereni sana na ALLAH awajalie afya njema ulinzi na msimamo usiyoyumbishwa Ameen. Tukiwa kwenye jitihada za kujitoa kwenye minyororo ya mfumo kristo nafikiri umefika wakati kuwa na Gazeti la KILA SIKU mfano wa An nuur. Ahsanteni sana. N d u g u Ye n u k a t i k a Iman Aboubakar Shekirindi Dar es Salaam

KONGAMANO LA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE JUU YA SEMINA ELEKEZI YA KUJIANDAA NA MTIHANI WA TAIFA
Jumuia ya wanafunzi na vijana wa kiislam Tanzania (TAMSYA) mkoa wa Dar es salaam inawaalika wanafunzi wote wa kiislam kidato cha nne kuhudhuria kongamano la semina elekezi ya kujiandaa ya mtihani wa Taifa (NECTA) litalofanyika inshallah. TAREHE: 23/09/2012. JUMAPILI MAHALI: UKUMBI WA SHULE AL-HARAMAIN MUDA: SAA 1:30 ASUBUHI HADI SAA 6:30 MCHANA

Mada mbalimbali zitawasilishwa. Katibu Habari 0654 290 875

Necta. Waapiga kelele lakini Serikali haihitaji ushahidi wa o na kwa kweli haionekani kutaka kurekebisha upungufu ulioko pale kwa maslahi chanya ya taifa. Kufanya hivyo itakuwa kupingana na maono ya Mwalimu Nyerere na Maaskofu. Kina COBA waliojazana serikalini wajue, enzi za usiri siri zimepita, kila jambo na kila hatua vinapimwa, kuonekana na kuhakikiwa na jicho lenye nuru angavu na akili iliyotimilika, ili kuweka maslahi ya nchi mbele kwa faida yetu sote na vizazi vyetu. Huyu ndugu yetu kawambwa anashangaza! Mbona wenzie kina magufuli, Mwakyembe, kigoda na Kagasheki hawarembi? Hajiamini nini huyu?. Au ana maslahi funani pale Necta? Tunataka katiba sa na nzuri. Tume nzuri, huru hasa ya uchaguzi 2015, ni hatari serikali kuchelewa ay kutotoa majibu stahiki kwa mambo yaliyowazi kabisa kama vile sensa, Necta na katiba, kwa sababu ya kuendekeza maono. Imani ya Umma ikitoweka kabisa, hapo tena hakuna ajuaye ya mbele. Wa k a t i h u u n c h i inaposokomezwa kwenye migogoro ya mipaka, hasa na Malawi na akina Chadema, Madaktari na waalimu, nao wakisuka yao, ni muhimu sana Serikali iwe karibu na sikivu kwa wananchi wake, wanaolalamikia mambo ya kweli na haki. Itowe haki kwa wakati ikiwa haina wasomi wa ukweli iwatafute na wapo. Iache kasumba, tunapoteza. Mungu Ibariki inchi yetu Nzuri Tanzania. Mohamed Mohamed Dar es salaam

13
Na Rajab Nkawa NILIWAHI kusimuliwa na rafiki yangu mmoja jinsi bosi wake alivyo mwajiri mtu kwakuwa tu jina lake lilikuwa la kabila lake. Mkasa wenyewe ulikuwa kama hivi: Kampuni ilikuwa kubwa na yenye vitengo vingi. Lakini mwenye sauti ya mwisho katika kupendekeza nani aajiriwe ni mkuu wa kitengo husika. Sasa katika vitengo vingine watu waliajiriana kiukabila. Bosi huyu jambo hilo likamkera naye akaamua kufanya kama wafanyavyo wengine. Katika kitengo chake pakawa na nafasi ya kuajiri mtu mmoja, katika maombi yaliyokuwa mbele yake palikuwa na jina la mtu wa kabila lake. Kwakuwa yule rafiki yangu naye alikuwa kabila moja na bosi, akaitwa osini kuthibitisha lile jina kama kweli ni la kabila lao. Baada ya rafiki yangu kuthibitisha, ndipo bosi akamwambia ukweli kuwa huyu atamwajiri kwa kuwa vitengo vingine watu wanaajiriana kikabila. Kuka hapo ndipo raki yangu naye akajua kumbe naye yuko pale kwasababu ya hasira za bosi wake dhidi ya ukabila wa wakuu wa vitengo vingine. Bosi yule, kwa maoni yangu, alikuwa anapenda nafasi za ajira katika kampuni yao zitolewe kwa uadilifu. Lau kama angelikuwa ndiye mtoa maamuzi katika kampuni ile, basi angelisimamia hilo. Lakini kwakuwa si mtoa maamuzi na kwakuwa mfumo ndivyo ulivyojengeka, akaamua naye kufanya mambo nyuma ya pazia. Kwa kufanya hivyo naye akawa sehemu ya mfumo anaouchukia. Mfumo wa kupendeleana. Mara baada ya makala yangu ya wiki mbili zilizopita kutoka gazetini nilitumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kutoka kwa wasomaji wawili tofauti. Nikaona ni busara kuwajibu kupitia makala kuliko kujibu zile meseji zao kwa kutumia simu. Kwa faida ya wasomaji wapya, labda nieleze japo kwa muktasari tu juu ya nini nilikiandika katika makala iliyopita. Nukta muhimu ni kwamba nchi hii haina dini, ila raia wake wana dini zao. Na kwakuwa raia wana dini zao, basi serikali haitapendelea dini mojawapo. Hoja yangu ikawa kwanini wakati wenzetu Wakristo wakisimama kidete kutetea dini yao mbele ya Serikali isiyo na dini sisi Waislamu tunashindwa kufanya hivyo?

Makala

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012


mgomo wa sensa na madai y a Wa i s l a m u a l i k u w a sahihi, kwamba Waislamu wazidharau takwimu zitolewazo na makanisa na serikali yake mwenyewe? Hiki si kiroja? Je, Rais kikwete anajua kuwa Waislamu wako huru kama walivyo Wakristo kunzisha jumuiya mbalambali na si lazima wawe chini ya BAKWATA? Kama anajua kwa nini kiutendaji serikali yake inaipa kipaumbele BAKWATA kama chombo cha kuwasemea Waislamu nchini? Haoni kuwa Waislamu kuepukana na mikono ya BAKWATA ni moja kuwaondolea dhulma? Mauaji yanapotokea tume inabidi iundwe kuchugunguza mazingira ya kifo na hatimaye kuwakisha katika mikono ya sheria wahusika. Hivi kwa nini mpaka leo tume ya kuchunguza mauaji yaliyofanywa na Polisi pale msikiti wa Mwembechai haijaundwa, lakini tume iliundwa ya kuchunguza kuuawa kwa mbwa Immigration. Je, Rais Kikwete haoni kuwa kutoundwa kwa tume ile ya uchugunguzi ni dhulma dhidi ya Waislamu wenzake? Je, Rais Kikwete anajua kuwa baadhi ya makabila yamefanya baadhi ya idara za serikali au mashirika yake kuwa ni vitengo vya makabila fulani au dini fulani? Kipo kisa cha kijana mmoja aliyeajiriwa kwa bahati mbaya katika benki fulani ambayo serikali inahisa. Alipotoka na wenzake aliowakuta kazini kwenda kazi za nje katika tawi mojawapo, aliyekutwa kule kwa kujiamini akauliza, je huyu naye ni mwenzetu?, akajibiwa hapana, akashangaa imekuwaje. Yule kijana wa Kiislamu akaelewa somo. Sasa haya na mengine mengi ndio mambo ya msingi ambayo tunategemea wenzetu huko juu serikalini watusaidie. Kwamba sisi na wao ni kitu kimoja katika kudai na kutetea maslahi ya Uislamu na Waislamu nchini. Hawa sio watu kufanya mambo nyuma ya pazia. Hawa lazima wawe wawakilishi wetu serikalini kama wenzetu Wakristo wanavyofanya. Lazima wajenge na kutetea hoja panapozuka dalili ya dhulma dhidi ya Waslamu. Sasa kwa muktadha huu mtu akiniambia kuna mengi wanayafanya nyuma ya pazia kwa ajili ya Uislamu na Waislamu mimi wananichanganya. Hawa si watu wa nyuma ya pazia. Wapo wa nyuma ya pazia mfano wa yule bosi lakini si wao. Namalizia makala hii kwa kuwauliza ndugu zetu walioko serikalini ni jambo gani linalowaogofya na kuwatisha kiasi cha kushindwa kusimama kidete kutetea dini yao?

AN-NUUR

Huyu naye ni mwenzetu?

Ndipo mfumokristo ulipotukisha


Kuna Waislamu walioko serikalini wa aina mbili. Wapo wale wenye uwezo wa kimaamuzi, yani wale wanaoingia katika vyombo vya maamuzi, pamoja na wale ambao wao ni watendaji tu. Hawa ambao ni watendaji tu wakifanya mfano ule wa yule bosi aliyeajiri kwa kigezo cha kabila atakuwa amepatia kwa kipindi cha mpito, lakini si lengo. Lengo lisiwe kusaidiana kwa mtindo wa nyuma ya pazia, hapana, hii nayo pia ni katika dhulma. Dini ya Kiislamu ni dini ya uadilifu. Tunataka watu waajiriwe kwa uwezo wao si kwa sababu ni Muislam au Mkristo, hapana. Naomba niwaulize swali. H i v i Wa z i r i w a E l i m u Dk Shukuru Kawambwa hajalielewa bado sakata la Baraza la Mitihani Ta n z a n i a ( N E C TA ) ? Mbona yuko kimya? Je, kashindwa kumshauri Mheshimiwa Rais juu ya mambo yanaolalamikiwa na Waislamu nchini? Sasa haya ndiyo mbambo ambayo wenzetu serikalini wanapaswa kuyashughulikia. Mambo ambayo yataondosha dhulma, sio vijimambo vidovidogo vya nyuma ya pazia, kisha tuwaone eti nao wanafanya jitihada katika dini ya Mungu. Waige mfano wa Manju Msambya, Mzee Kitwana Kondo na Kighoma Malima. Aidha wapo wakuu wa mikoa na wilaya ambao sikupenda namna walivyolishughulikia suala la mgomo wa s e n s a k w a Wa i s l a m u . Maana unamwangalia mtu anavyoongea katika televisheni, unaona wazi kuwa yule hakerwi bali anaona sawa tu tena anawashangaa nduguze katika imani wanaosusia sensa, kwa hoja zilezile dhaifu kwamba serikali haipangi mambo yake kwa mujibu wa dini za watu. Kumbukeni kuwa hapa ndugu zenu katika imani walikuwa wanapambana kuufumua mfumo wa dhulma uliopo, nanyi mlipaswa kuwaunga mkono. Haya ndio mambo ya msingi si vimemo vya kusaidana nyuma ya pazia. Tuiulize serikali, hivi kweli haikulielewa somo la kugomea sensa kama lilivyowakilishwa na Waislamu nchini? Je, ile barua iliyoandikwa na TAMPRO kwenda kwa Waziri Mkuu mbona haikujibiwa? Na je yale majibu aliyoyatoa Rais wakati wa hotuba yake ya kila mwezi alipozungumzia

DKT. Shukuru Kawambwa Aidha nikahoji kwanini wakati wenzetu Wakristo kuanzia Mwalimu Nyerere na hata waliomfuata baada yake wakihalifu ahadi ya kutopendelea dini moja na kulibeba kanisa kiasi cha kutotofautisha lipi la kanisa na lipi la serikali, sisi Waislamu tumeendelea kutekeleza ahadi? Nawashauri wale ambao hawakuisoma makala ile waipitie ili twende sawa. Sasa turejee katika ule ujumbe mfupi wa maandishi. Mmoja wa wasomaji alinishutumu tu kuwa sijawatendea haki Waislamu walioko serikalini. Msomaji mwingine alinipa ushauri kwamba ni vema kwangu ningefanya utafiti kwanza kuliko kuwalaumu Waislamu walioko serikalini kwa ujumla wao kwamba hawako kwa maslahi ya dini yao na Waislamu wenzi wao. Naithamini michango yao na nawashukuru sana. Inaonesha wanacho wanachokijua kuhusiana na jitihada za Waislamu wenzetu walioko serikalini. Nami ninajua kuwa zipo jitihada za mtu mmoja mmoja miongoni mwa hao Waislamu wenzetu walioko serikalini, na kwa ajili hiyo nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awalipe kwa nia zao njema za kuupeleka Uislamu mbele Inshaallah. Ila kuna nukta muhimu ya kuzungumzia katika hili. Mwanzo wa makala nimerekodi kisa cha yule bosi ambaye hakuwa na njia ya kuukabili mfumo na kuufumua, isipokuwa kwa kufanya mambo nyuma ya pazia, na kujikuta naye ni sehemu ya mfumo anaouchukia. Kisa hiki cha kweli kinafanana sana na viongozi wetu wa Kiislamu serikalini. Wanapenda sana wajulikane kuwa wanafanya jambo fulani kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu, kumbe wanachokifanya si uadilifu bali mwendelezo wa mfumo wa dhulma uliotamalaki hapa nchini.

14

Makala/Tangazo

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012

AN-NUUR

upole huingia katika sehemu nyingi za maisha na viashirio vyake na huruma za wazi kabisa ni kama hizi :1. U P O L E WA FAMILIA : Na tuna dalili toka kwa Mtume (S.A.W) kiigizo chema kwani walikusanyika nyumbani Dr. Samir Mahmoud kwake, wanawake wengi kiasi ambacho hakukusanyika SHUKRANI zote anastahiki kwa wingi nyumba nyingine M w e n y e z i M u n g u n a na akawa ni mfano bora Rehema na Amani zimkie kwa upole na huruma na mjumbe wa Mwenyezi kusamehe kwa watu wa Mungu. Ama baada ya nyumbani kwake Mtume utangulizi huu, upole (S.A.W) na akauhimiza uma ni miongoni mwa tabia wake kujipamba na tabia hizi inayohimizwa na Uislamu kwa familia yake. 2. U P O L E K W A kwa waumini wake juu ya MFANYAKAZI WAKO kujipamba na tabia hii ya (MTUMISHI) : Anasema upole na wema. Anasi (ra) Nimemtumikia A m e s e m a M w e n y e z i Mtume kwa muda wa miaka Viongozi wa Dini ya kiislam wakiwa katika semina ya kinamama iliyoandaliwa na chuo Cha kiislam Mungu mtukufu, Na kwa kumi hajapatapo kunigomba markazi changombe, ambapo kinamama hao wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanakuwa katika rehema za Mwenyezi Mungu juu ya jambo aliloniamrisha malezi yaliyo bora aliyoyafundisha mtume wetu. Na kuwa makini na utandawazi unao waathiri umelainika kwao na laiti nilifanye nami sikulifanya vijana wengi katika jamii inayotuzunguka. Semina hiliyo iliwashirikisha kinamama wapatao mia ungekuwa mgumu wa moyo na wala hajapata kunigomba na hamsini kutoka mkoa wa Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. wangekukimbia. NAMNA juu ya jambo nililoliacha kwa juu ya mtumishi kumfanyia upole wake pale aliposema nikanyamaza. Na alipotoa ZA HURUMA :-Kwa hakika nini umeliacha, na ameusia wema kwa mazingatio juu ya (watumishi wenu ni ndugu s a l a m M t u m e ( S . A . W ) zenu, amewaweka Mwenyezi ninaapa kuwa hakunigomba KITUO CHA MAFUNZO NA AJIRA CHA TAMPRO Mungu chini ya mikono wala hakunichukia na wala yenu. Na atakaye kuwa hakunitukana. Bali alisema, na mtumishi basi amlishe Kwa hakika hii ni swala, chakula anachokula yeye na hivyo hayatakiwi tena maneno amvishe nguo kama anazovaa ya viumbe bali kinachotakiwa yeye. ni Tasbihi, Dhikiri na kusoma 3. U P O L E K W A Qur an MAFUNZO YA JINSI YA KUANZISHA WATOTO : Toka kwa Aisha 6. UPOLE JUU YA (RA) amesema, Alikuwa KUSIMAMIA NA KUKUZA BIASHARA KWA KUMARISHA MEMA NA Mtume (S.A.W) wakimjia watoto na kuwoambea dua KUKATAZA MABAYA KUMLENGA MTEJA NA SOKO na kuwabariki na alikuwa : Pia hapa tuna kisa cha siku moja juu ya mimbari Mwarabu ambaye amekojolea Kutokana na maombi ya wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati, Jumuiya ya wataalam wa kiislam wakaja Hassan na Hussein Msikiti na kwa kusudia Tanzania (TAMPRO) kupitia kitengo chake cha Ajira na Mafunzo kinawatangazia wafanyabiashara na wanatambaa akateremka masahaba kumpiga lakini wajasiriamali wote kuwa kitaendesha mafunzo maalum ya Kuanzisha, kusimamia na kukuza biashara Mtume (S.A.W) toka katika Mtume ambaye ni mpole kwa kumlenga mteja na soko. Mafunzo yatakuwa kama ifuatavyo:mimbari na kuwakumbatia akamwita na akamwambia, kwa ajili ya kuwahurumia Kwa hakika huu ni Msikiti Lengo: kuwapa mbinu na kuwajengea uwezo wajasiriamali juu ya kuanzisha, kusimamia na kukuza watoto wakiwa wadogo kisha hautakiwi mkojo, hii ni kwa biashara kwa kumlenga mteja na soko. wanatambaa. ajili ya swala, dua na kusoma 4. U P O L E K W A Qur an. Mahali: Ukumbi wa mikutano TAMPRO makao makuu O M B A O M B A : To k a 7. U P O L E K W A kwa Anasi (RA) amesema, Muda: Jumamosi tarehe 29/09/2012 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni KUISHI VIZURI NA Nilikuwa pamoja na Mtume Mada zitakazo wasilishwa: Ujasiriamali na taratibu za kuanzisha biashara, kukuza biashara kwa (S.A.W) akaja Mwarabu M A K A F I R I : U p o l e mmoja na akamkuta Mtume haukulenga katika wema kwa kumlenga mteja, kuunda mikakati ya kufanikisha biashara, kukuza biashara kwa umahiri wa kuuza, (S.A.W) Akamkunja nguo Waislamu tu bali umefika Namna ya kuweka kumbukumbu za biashara. kwa nguvu akasema ewe hadi kwa wasio Waislamu. Gharama: Shilingi 20,000/= kwa mtu mmoja. (Kwa ajili ya cheti cha ushiriki, vitini vya mafunzo, na Muhamad nipe katika mali ya Amesema Mwenyezi Mungu Hawakatazini chakula) Mwenyezi Mungu uliyonayo, mtukufu, Mungu juu ya wale Mwenyezi A k a t a b a s a m u M t u m e wasiokupigeni vita katika dini Kujisajili: Ili kujisajili tuma SMS yenye jina lako kwenye namba 0714 151532, 0767151532, 0719988919 (S.A.W) akaamrisha apewe na wala hawakutoeni katika au fika TAMPRO Makao Makuu, Magomeni Usalama, jirani na Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni. mali. majumba yenu kuwafanyia 5. U P O L E K W A wema na uadilifu kwao TANBIHI: Ili kufikia lengo la mafunzo TAMPRO itatumia Wataalamu wenye uwezo na uzowefu katika MJINGA : Na hii miongoni 8. U P O L E K W A nyanja ya biashara mwa muono wa Uislamu WA N YA M A : U p o l e nao ni upole kwa mjinga haukuishia kwa binadamu Wahi kuijiandikisha kwani nafasi ni chache. ambaye hajui sheria. Toka tuu, bali umeka hadi kwa Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0714 151532, 0767151532, 0719988919, 0767989909, kwa Muwania mtoto wa wanyama ametoa habari 0688988919 au info@tampro.org Hakim amesema nilikuwa Mtume (S.A.W) kwamba ninaswali pamoja na Mtume mwanamke mmoja ameingia (S.A.W) akapiga chafya mtu motoni kwa sababu ya paka Imetolewa na ambaye amemfungia bila mmoja nikasema Mwenyezi ya chakula wala hakumpa Mungu akurehemu wakawa uhuru wa kujitafutia chochote masahaba wananitupia macho ardhini na Amaeingia mtu MRATIBU MAFUNZO na wanajipigapiga mapaja Peponi kwa kumpa maji TAMPRO MAKAO MAKUU yao nilipowaona hivyo mbwa.

Ufahamu wa upole ni wema katika Uislam

15

Habari

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21- 27, 2012

AN-NUUR

Masheikh wetu Uamsho jueni huyu ndiye Pengo


Inatoka Uk. 7

Inatoka Uk. 15

Elimu ya Dini yahimizwa

Tanzani. Lakini hata haya madudu tunayoyasikia bungeni na Serikalini, pamoja na ufisadi na mafisadi yanafanywa na wasomi walioandaliwa katika mashule na vyuo vya Kanisa, na waalimu wa Kanisa waliofundisha katika mashule na vyuo vya Serikali; Namwomba msomaji atulizane katika fahamu zake na tafakuri zake, nukuu hizi za Dr. Sivalon:A Letter to My Supreiors: Padri Bernard Joinet amekuwa akijihusisha kwa mapana na marefu kwenye shughuli za kijamii za Kanisa Katoliki. Kitaaluma

amesomea saikolojia na aliwahi kufanya kazi katika Chuo cha Nyegezi. Amefanya kazi parokiani pamoja na kuwa Mchungaji wa wanafunzi wa udaktari Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1983, baada ya kutoa mhadhara kwa Maaskofu na viongozi wa Mashirika ya dini aliombwa kuendelea kutoa ushauri kwao na kwa viongozi wengine wa Kanisa juu ya hali ya uchumi. Alifanya hivyo kwa kuandika na kuchapisha mwenyewe jarida liitwalo A Letter To My Superiors. [Dr. Sivalon uk 65-66]. Vuta kra. Kuwa, huyo ni mtaalamu wa Elimu ya saikolojia aliyepewa jukumu na Kanisa kupitia

kulifanyia mtihani somo la Maalifa ya Uislamu kwa shule za Msingi, Ust. Shaaban, alisema somo hilo ni somo lenye umuhimu mkubwa kwa watoto. Alisema, kumekuwa na kauli za upotoshaji kwamba

somo hilo ni la hiyari ukitaka unasoma au una weza kuachana nalo. Akasisitiza kuwa, hizo ni fikra potofu, kwani unapohiyari kusoma dini ina maana unahiyari ya kumuabudu Allah (sw), kwani hutoweza kuwa Muislamu sahihi bila kusoma Dini.

MHADHIRI mashuhuri nchini, SHEIKH SAID RICCO ni mgonjwa wa macho. Jicho lake la kushoto linavuja damu kwa ndani. Ametibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, KCMC Moshi, CCBRT Dar es Salaam bila mafanikio. Hatimaye alipelekwa Hospitali ya NM India. Baada ya uchunguzi ilionekana unahitajika upasuaji mkubwa na kwa gharama za dola 5500 sawa na 8,800,000 za Kitanzania. Alirejea nyumbani na mpaka sasa amefanikiwa kupata dola 4,000 bado Dola 1,750 ili aweze kurejea India kwa ajili ya matibabu. Tayari tiketi ya ndege anayo ya Emerate Airlines Flight No. EK 726 na anatakiwa kuondoka tarehe 30 Septemba mwaka huu. Hivyo anahitaji msaada wa haraka wa kiasi kilichosalia. Mchango wako upeleke AKAUNTI Na. 048201001220 NBC tawi lolote au TIGOPESA 0715 979779 AU MPESA 0753 979779. Anawashukuru sana Waislamu wa Arusha, Tanga, Mwanza na Morogoro kwa kumsaidia kupata Dola 4000 na tiketi ya ndege. WABILLAH TAWFIIQ

Sheikh SAID RICCO anahitaji msaada wa haraka

Serikalini, kuwa Mchungaji wa wanachuo wa udakitari katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Jalia kuwa hao ndio mabingwa tunaojivunia sasa, na matukio yanayotokea ya upasuaji wa kichwa badala ya goti, na migomo ya madakitari inavyoua watu, linganisha na Mchungaji aliyewachunga wanachuo wake Wakristo safi waliolishwa Neno wenye kuongozwa na Roho Mtakatifu! D r. S i v a l o n anatufahamisha kazi iliyofanywa na Mchungaji huyo: Imani yake kwa u j a m a a w a Ta n z a n i a inaonyeshwa katika kila nakala ya jarida lake kwa wakati huo. Kuhusu hali ngumu ya uchumi, anamalizia kwa kusema kwamba: Namna gani kuendeleza uzalishaji ambao ni wa Kiafrika, Kijamaa na wenye ushindani ndio swali. Sina jibu, lakini ningeshauri kuwa hilo ndilo swali ambalo Chama na Serikali lazima wajibu, na Sisi kama waumini tungejibu ikiwa tunahusika na miradi ya maendeleo. Ukiona miradi ya maendeleo ya Kanisa, na makubaliano ya Serikali na Makanisa mwaka wa 1992 Chini ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mh. Lowasa [MOU] yalipikwa na wataalamu kama hao, na Serikali ilitiwa kitanzi kwa msaada wa Rais Nyerere, wa kulipa Kanisa a good chanse. Dr. Sivalon, akitueleza jinsi Mchungaji huyo alivyofundisha maelezo yake yalielekea kutetea watawala wa sasa hapa Tanzania. Mwanzoni, alifananisha Tanzania na Ufaransa na muda ambao Ufaransa ilichukua kupata kundi la watumishi waaminifu wa Serikali. Aliandika hivi: Nakiri katika mwaka wa 1985 Ufaransa inalo kundi la watumishi ambao kwa wastani ni waaminifu, wenye juhudi, ambao hujivunia kazi yao na siyo wapenda rushwa. Ilichukua kutoka

MH. Edward Lowassa.

miaka 600 kupata watumishi waaminifu: Kwa mafundisho ya Ukristo, hakuna kuhoji anachosema Askofu, Padre, Mchungaji au kiongozi wa Kanisa, kulingana na shemere zilizotiwa vichwani kwa waumini wao, ni kuwa, anachosema Askofu kinatoka kwa Mungu, sikwambii huyo aliyesema ni Padre Mzungu mtaalamu mwana saikolojia na Thiolojia ya Kanisa. Watanzania tunahangaika na kuhangaishwa rushwa, usadi na masadi na ukosefu wa watumishi waadilifu na waaminifu wakiwemo Madakitari, kumbe wasomi walifundishwa wakiwa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, kuwa, kutokana na kuwa watawala wa kikoloni walisomesha na kukemea rushwa na uaminifu na uadilifu kwa muda wa miaka 600 hivyo aliwafundisha kuwa kwa Tanzania itachukua miaka:Hakika Afrika siyo Ulaya, na Tanzania sio Ufaransa. Kulinganisha nchi hizi mbili itakuwa siyo ya mkini. Vilevile mwaka 1985 ni tofauti na mwaka 1300 na kwamba watumishi wa Serikali ya Tanzania wanaingia moja kwa moja katika ulimwengu wa kompyuta. Lakini pamoja

mwaka 1300 hadi 1900, ndio kusema kiasi cha

na hayo ikiwa Tanzania inaweza kupata watumishi waaminifu na wenye juhudi kwa kipindi cha miaka 300, hayo yatakuwa ni mafanikio makubwa. [Dr. Sivalon uk.66]. Hizo ndizo sera za Kanisa kupitia kwa kina Pengo na viongozi wake; ndiyo maana anawashangaa Jumuiya ya Uamsho, kuwa wanataka kuwaamsha wa Zanzibar kabla kusherehekea miaka 300 iliyowekwa na Padre Bernad Joinet, mtaalamu wa saikolojia na thiolojia ya Kanisa Katoliki. Waislamu na wa Tanzania, tunategemea nini kwa viongoai wa aina hiyo kama hatuwakemei? Na hao ndio walikuwa na ndio washauri wa viongozi wa Serikali yetu! Wanatuambia kuwa wanaowasomesha hawawezi kuwa waaminifu wala waadilifu mpaka iishe miaka 300, ndiyo maana kila anayeajiriwa anatumbua nchi maana amesoma na kusomeshwa Jarida la liitwalo A Letter My Superiors haoni dhambi kuwa fisadi kwa kuwa aliyeandika ni Padre kuwa watakao fisidi kwa rushwa n.k kabla ya kwisha miaka 300 wanahesabiwa kuwa ni majinuni. Inna lilaahi wa innailayhi rajiuun. HUO NDIO MFUMO KRISTO.

16

AN-NUUR
16
Na Waandishi wetu
akiwamo Muwakilishi wa Kwamtipura, Bw. Hamza Hassan Juma, Muwakilishi wa Kiembe Samaki, Bw. Mansour Yussuf Himid, na Mwakilishi kutoka Jimbo la Mji Mkongwe wa Zanzibar, Bw. Ismail Jussa Ladhu. Wo t e k w a p a m o j a Wawakilishi hao walionelea ikibidi ipo haja ya Wajumbe, kwa Maslahi ya Nchi, kuwadhibiti hata kwa kura ya kutokuwa na imani, Viongozi wote, akiwamo Balozi Seif Iddi, ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Serikali ndani ya Bunge hilo la Zanzibar .

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPTEMBA 21 - 27, 2012


www.tawheedtz.org Unakuhimiza ufanye Ibada ya Hijja 2012 Fanyeni Haraka Kuhiji. Maana Hajui Mmoja Wenu Kitakachomtokea Ibn Abbas Mkabala na Msikiti wa Makonde, Kariakoo, Dar es Salaam 022 2182068; 0776 070770; 0719 689528
Shaka ilikuja zaidi pale miongoni mwa Wakuu wa Serikali walipoonekana katika nyendo zisizokuwa za kawaida katika mazingira ya Majeshi, Vikosi vya Ulinzi, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, ZEC, Usalama wa Taifa, na pia katika kambi za wale vijana maarufu waliozoeleka kuleta vurugu nyakati za uchaguzi almaarufu janjaweed hata kabla ya kuanza kwa Kampeni za Uchaguzi huo. Licha ya CUF na Mgombea wake, Mhe Issa Khamis Issa, kupinga matokeo ya uchaguzi huo uliompa ushindi, mgombea wa Chama cha Mapinduzi, CCM, Bw. Hussein Ibrahim Makungu, la kuwasikitisha wananchi ni kuona kwamba tokea maandalizi na hadi utekelezaji, zoezi hilo kwa ujumla lilivamiwa kisiasa na Vyombo vya Ulinzi, Dola, Serikali Kuu, Usalama wa Taifa, Majeshi, Mamluki, Makada na hata vijana wahalifu wajulikanao kama janjaweed, ilisema sehemu ya Taarifa ya CUF kwa Vyombo vya Habari. Pamoja na shaka hiyo lawama nyingine, zilizopelekea ule uoni kwamba Mshindi aliyetangazwa na Tume kupitia Uchaguzi huo, ni Muwakilishi wa Majeshi, ni pale mabavu, nguvu na hujuma za ziada za Vikosi vya Ulinzi dhidi ya wananchi, hasa wale waliojaribu kubainisha na kueleza hisia zao kwamba waliokuwa wakipelekwa Vituoni kupiga kura chini ya Ulinzi mkali wa Majeshi, walikuwa mamluki na siyo wapiga kura halali wa Jimbo la Bububu. Tumewaona Maafisa wa ZEC, watu wa Usalama, na hata majeshi wako ndani ya Kambi ya KMKM waseme wale wakitafuta nini mule kama si kuharibu Uchaguzi,

Mtandao wa Tawheed

AN-NUUR

Dhuul-Qaad 1433, IJUMAA SEPT. 21-27, 2012

MIONGONI mwa mambo yaliyompa matumaini Raisi wa Zanzibar Dokta Ali Mohamed Shein, mwanzoni mwa utawala wake, mara baada ya kutangazwa kushika wadhifa huo mwishoni mwa mwaka 2010, ni pale alipojisikia faraja kuona ipo safu imara ya Wasaidizi wake wakuu akiwamo Makamu wa Pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi. Raisi Dokta Shein aliwahi kukaririwa akisema faraja yake inatokana na msaada mkubwa alioutarajia kutoka kwa panga mbili imara ambazo ni Wasaidizi wake akiwamo Balozi Seif Iddi, na pia Makamu wa Kwanza wa Raisi wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, hisia zilizoleta matumaini hata kwa Wananchi wengi wa Unguja na Pemba. Matumaini hayo yaliambatana na msingi kwamba kulihitajika Viongozi makini walioelewana tabia zao, wakatumia busara, wakaweka mbali ukereketwa na chuki za kisiasa, ili kuitumikia kwa uadilifu Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, sambamba na kupigania maslahi ya Nchi hii irejeshe mamlaka yake kamili kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyolalamikiwa kudhoosha Visiwa vya Unguja na Pemba katika nyanja zote za kimaisha. Waheshimiwa la kusikitisha ni kuona kiongozi wa juu aliyepewa mamlaka ya kutetea maslahi ya nchi hana silaha nyengine isipokuwa vitisho kwa anaowaongoza .nakwambieni mimi huyo simuogopi .. na nyie nakwambieni huyo ni mtu hatari sana mumuepuke, alisema mmoja wa wachangiaji katika Semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar juu ya Muungano, iliyofanyika hivi karibuni Mjini Unguja. Muwakilishi huyo, kupitia Chama Tawala, Chama Cha Mapinduzi CCM, ambaye hakupendelea jina lake litajwe hapa, ingawa sauti ya mchangio wake huo ilisikika hadharani katika masikio ya wengi waliofuatilia Semina hiyo, aliongeza kwa kusema masikini kiongozi huyu watu walimuwekea matarajio lakini hatimaye Maslahi ya Zanzibar ameyapa kisogo. Lawama kama hizi ziliendelea kutajwa hadharani kupitia wachangiaji wa Semina hiyo, ndani ya Ukumbi wa B a r a z a l a Wa w a k i l i s h i ,

Masikini Zanzibar
Ama kweli hakuna dereva bingwa kwa gari bovu sasa nimeamini haya yote yanakuja juu ya watu hawa tuliowaamini waitetee Zanzibar , alitamka nje ya Ukumbi mmoja wa Wajumbe wachangiaji. F u n g u j i n g i n e limeambatanishwa na lawama hizo, kwamba baadhi ya Watendaji Wakuu wa Serikali ya Zanzibar, wamejumuika katika kuvuruga zoezi zima la Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Bububu, Wilaya ya Magharibi Unguja, uliofanyika Jumapili iliyopita ya Tarehe 16 Septemba, 2012.

Hizo ni lawama kutoka kwa Wakaazi wa Jimbo la Bububu, Viongozi wa Kisiasa, na baadhi ya Waangalizi, wakiwamo Watendaji wa Chama cha Wananchi, CUF; ambapo pia taarifa ziliwanukuu hata wale wa CCM, walioonekana katika heka heka za Uchaguzi huo, baada ya kuona hali ilielekea kutishia amani. Sidhani kwamba Bububu watapata Muwakilishi atakayependelewa na wananchi kwa hali hivi ilivyo, alisema mmoja wa Waangalizi na Wafuatiliaji wa Uchaguzi huo kutoka Asasi za Kiraiya.

Elimu ya Dini yahimizwa


Na Bakari Mwakangwale WANAFUNZI wa Kiislamu waliohitimu elimu ya Msingi, Septemba 20, wameelezwa kuwa wana jukumu la kujifunza zaidi dini katika safari yao ya kimasomo. Wito huo umetolewa na Mratibu wa Islamic Education Pannel, Mkoa wa Dar es Salaam, Ustadhi Ibrahim Kunema, akiongea katika Mahafali ya wanafunzi mbalimbali wa Darasa la saba, katika viwanja vya Shule ya Msingi Karume, Jijini Dar es Salaam, Jumapili iliyopita. Ustadh Kunema, aliyekuwa Mgeni rasmi katika Mahafali hayo, aliwataka wanafunzi hao kufahamu kuwa, maisha ya dunia yana kikomo, bali Akhera ni ya milele. Alisema, si busara kwa mwanafunzi wa Kiislamu kuweka pembeni somo la Dini ya Kiislamu akidhani tu kwamba halina tija na manufaa katika maisha yake. Kwa wale wanafunzi mnaohitimu elimu ya Msingi, bado mna jukumu zaidi la kujifunza dini yenu. Mtambue kuwa maisha ya dunia yana kikomo hivyo ni lazima mtoe muda wenu katika program za dini katika ngazi ya Sekondari na vyuo. Alisema Ustadh Kunema. Alisema, hitajio la kuufahamu na kuusoma Uislamu lipo kwa kuwa wengi miongoni mwa Waislamu hawaufahamu Uislamu wao.

POLISI wakirandaranda katika mitaa ya jimbo la Bububu, Zanzibar katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni.

Inaendelea Uk. 3

Naye Ustadhi Abubakar Shaaban, akiongea katika Mahafali hayo, alielekeza kiliochake kwa wazazi wa Kiislamu kwa kushindwa kusimamia vijana wao katika somo la Dini. Alisema, katika malezi na safari ya kimasomo ya mtoto, mzazi ndio dira ya safari hiyo lakini alidai wazazi wamekuwa wakizembea kuwahamasisha vijana wao kulipenda somo la dini. Akihimiza usomaji na Inaendelea Uk. 15

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like