Professional Documents
Culture Documents
ISSN 0856 - 3861 Na. 1046 MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23-29, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Unguja itakomboka
Ataka Tanganyika iungane na Kenya Apaza sauti Mahakamani mnautaka?
Ni baada ya kukosa kibali kwa muda mrefu Wasema kama tatizo ni fedha waambiwe TCRA wasema malalamiko yapelekwe kwa DG
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Islamic Foundation na TV Imaan, Sheikh Aref M. Nahdi, amesema kuwa wametimiza mashariti yote yanayohitaka kupata
kibali cha kujenga Studio ya TV ila hawajui ni kwa nini mamlaka husika inachelewa kuwapa kibali hicho-yaani Construction Permit (CP). Nahd amesema kama ni
Inaendelea Uk. 11
2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Osi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
AN-NUUR
AN-NUUR
MAONI YETU
Wa n a s h e r i a w e n g i n e wa upande wa waendesha mashitaka waliosikiliza kesi hiyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Mashitaka ni Rashid Fadhil na Raya Issa Mselem ambaye aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali hoja ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwa hapo sio mahali pale na kama wanataka wafungue madai katika mahakama husika. Raya aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa kutokana na upelelezi kutokamilika. Katika uamuzi wake, George Kazi ambaye pia ni hakimu wa mahakama ya mkoa Vuga, alisema mahakama yake haiwezi kutoa tamko la ukiukwaji katiba, na kufahamisha kuwa Mahakama Kuu ndiyo pekee yenye Mamlaka ya kusikiliza na kutoa maamuzi yanayohusiana na ukiukwaji wa Katiba. Mrajis huyo wa Mahakama Kuu ameutaka upande huo wa utetezi kufungua madai yao hayo Mahakama Kuu, kwani ndicho chombo pekee chenye Mamlaka ya kusikiliza masuala ya Katiba na sio katika mahakama hiyo ambayo inasikiliza kesi inayowakabili watuhumiwa hao wanane. Mrajis wa Mahakama Kuu alikubaliana na ombi lililowasilishwa kutoka upande wa waendesha mashitaka kuiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 29 mwaka huu kwa kutajwa. Washitakiwa katika kesi hiyo ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52) wa Kwamtipura, Mussa Juma Issa (37) mkaazi Makadara na Azzan Khalid Hamdan (48) mkaazi wa Mfenesini. Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Suleiman Juma Suleiman (66) mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakari Suleiman (39) wa Tomondo pamoja na Ghalib Ahmada Omar (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe wote ni wakaazi wa Zanzibar. Wote hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka ya uvunjifu wa amani, ushawishi wa kuchochea na kurubuni watu, kula njama pamoja na Inaendelea Uk. 5
Habari
AN-NUUR
Israel imeangamzia raia 162 wasio na hatia Gaza kabla ya kutangazwa kusitishwa mashambulizi hiyo juzi. Kwa upande wa Israel imedaiwa kuwa wameuliwa watu watano kutokana na maroketi yanayorushwa na wapiganaji wa Hamas. Habari za mashambulizi kwa Wapalestina yamekuwa yakipotoshwa pale ilipodaiwa kuwa kuna vita kati ya Israel na Gaza. Hakuwezi kuwa na vita baina ya Wapalestina wa Gaza na Israel. Gaza ni sehemu iliyozingirwa na Israel hakiingii kitu wala mtu mpaka ruhusa ya Israel. Nyumba zilizoangamizwa na Israel mwaka 2009 mpaka leo hazijajengwa au kufanyiwa ukarabati kwa sababu toka mwaka huo mpaka leo, Israel haijaruhusu kupita hata mfuko mmoja wa saruji! Sasa watu kama hao wanapigana vipi? Katika shambulio moja wiki iliyopita, Israel iliangamiza nyumba ya familia moja ambapo watu 11 waliuliwa wakiwemo wanawake watano akiwemo bi kizee wa miaka 80 na watoto wanne. Shambulio hilo la kombora, liliangamiza kabisa nyumba ya familia ya Dalou katika wilya ya Sheikh Radwan. Ilikuwa kazi kubwa kufukua maiti za vichanga katika kifusi cha nyumba hiyo na kisha kupelekwa moshwari katika hospitali ya Shifa. Katika shambulio moja, nyumba ya familia moja iliangamizwa wakiuliwa watoto wawili, watu wazima wawili na wengine 42 kujeruhiwa. Hali ya kutisha ilielezwa kuwepo katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Shifaa ambapo zinaonekana maiti za watoto wachanga wakiwa wamewekwa pamoja wakiwa wamejaa damu na vumbi kutokana na kufukiwa na kifusi. Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la Associated Press (AP), watu wengi wameuliwa kutokana na nyumba zao kuangamizwa kwa makombora na hivyo kufukiwa katika vifusi. Katika waliokumbwa na balaa hilo wiki hii ni pamoja na familia ya Abdel Aal ambayo nyumba yao iliangamziwa kabisa. Kama inavyofahamika kuwa Gaza ni mji ambao una
Mashambulizi yasitishwa
Mateso mikononi mwa wakoloni na makaburu wa Kiyahudi, yamekuwa ndio maisha ya Wapalestina kwa miaka mingi sasa. Yamekuwa ndio hali yao ya kila siku. Hebu kiria kuishi katika mazingira ambayo hujui kama itaka jioni ukiwa hai au maiti! Mkirie mtoto anayezaliwa na kukulia katika mazingira haya ya kukaliwa kimabavu na Israel!
protection iliyotolewa ili kuwalinda raia. Umoja wa Mataifa na Katika Operation Cast Lead, ilikuwa msiba mkubwa Baraza lake la Usalama, lilikaa kwa Wapalestina. Kwanza kimya likitizama zaidi ya Israel, ukiacha silaha nzito Wapalestina 1,400 wakiuliwa kama Missiles, bombs, shells na makazi yao kuharibiwa ambazo Wapalestina hawana, kabisa. Katika operesheni hiyo, Israel ilitumia mpaka silaha haramu (illegal weapons) hakuna kilichosalimika. kama White phosphorus) Shule, Vyuo Vikuu, Misikiti, ambayo ni silaha ya kemikali hopitali, viwanda, mpaka osi za taasisi za Umoja wa inayounguza vibaya. Lakini pamoja na uhalifu Mataifa, ziliangamizwa kwa wote huo, hakuna Security mabomu na makombora. UN C o u n c i l n o - f l y z o n e kimyaa!
BAADHI ya watuhumiwa wa kesi ya kiwanja cha Markazi Changombe, Jijini Dar es Salaam, waliotoka kwa dhamana mapema wiki iliyopita, wamesema wamejifunza na kubaini mambo mengi wakiwa gerezani. Akiongea na Waislamu katika Msikiti wa Mtambani, katika maadhimisho ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu 1434, Ijumaa ya wiki iliyopita, mmoja wa watuhumiwa hao, Ustadh Abubakar Juma, amesema kikubwa kilichotawala huko ni udhalilishaji. Akifafanua Ustadh Juma, alisema kuna namna nyingi za kudhalilisha Uislamu na mbaya zaidi ni pale Muislamu anapowekwa uchi, kwani alidai baada ya kukishwa gerezani waliamuliwa Waislamu wote kuvuliwa nguo. Alisema, walimueleza kiongozi wa gereza kuwa haiwezekani wakavuliwa nguo katika mazingira hayo, hata hivyo kiongozi huyo, alidai atakachoweza kuwasaidi ni kuwatenganisha wale wenye umri mdogo na wenye umri mkubwa. Yu l e b w a n a a l i s e m a wenye umri chini ya miaka 35, watavuliwa kivyao na wale wazee kwa wazee watavuliwa kivyao. Hii ni hali iliyokuwepo huko. Alisema. Lakini kwa upande mwingine alisema, wamefurahiya maisha ya gerezani kwani kwa mwenye kujitambua hupata muda mwingi wa kufanya ibada, na kwa muda huo waliowekwa mahabusu wameweza kusilimisha Wakristo zaidi ya 11.
lakini Waislamu waliakiana aongozane na Waislamu wengine watatu kituoni hapo, akiwemo Ustadhi Mukadam (anayeshikiliwa na Polisi hadi sasa). Alisema, lengo kuu la kuitwa Polisi, walielezwa ni kukutanishwa na yule aliyeuziwa eneo lile, alidai kinyume na matarajio hayo walikuta ramani ya eneo hilo ambayo haionyeshi mwanzo wa kiwanja wala mwisho wa kiwanja. Wakiwa huko wajumbe hao, walitakiwa waandike maelezo, jambo ambalo hawakulifanya kwa maelezo kuwa wao si viongozi bali wapo viongozi wanaopaswa kutoa maelezo hayo kwa maandishi wanayoyataka. Alisema, wakiwa Markazi Changombe majira ya saa tano usiku, walipata taarifa kuwa Sheikh Ponda, kakamatwa akiwa Masjidi Tungi, Temeke, na usiku huo huo wa saa tisa zilivamia gari za Polisi zisizopungua kumi na mbili, kikiwemo kikosi cha mbwa, walivunja geti na kuanza kamata kamata. Alisema, baada ya kuingia hapakuwa na mtu katika jengo la Markaz zaidi ya kinamama wasiopungua 12, ndani ya Msikiti wa Markaz, na Waislamu wengine walikuwa katika Msikiti walioujenga wakiwa pale. Ilisikika sauti ya afande ikisema, piga risasi wale kwa kweli tulijua kuwa ndiyo yametimia, tuliwaambia msipige risasi sisi hatuna silaha yoyote, sauti ile iliamrisha tena toka mbele hatua tano tukatekeleza amri hiyo, ikatoka amri nyingine, inua mikono juu, tukainua piga magoti tukapiga.
Inaendelea Uk. 5
Habari
AN-NUUR
Press Release Sultan Qaboos Academic Fellowship (SQAF) Program for the State University of Zanzibar (SUZA)
16th Novemba, 2012 Kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mkuu wa SUZA, Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, nina furaha kubwa kupata heshima ya kuitangaza Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA kwa ajili ya Wazanzibari kwa mintarafu ya kujenga uwezo katika rasilimali watu utakaokuwa na wataalamu watakaomudu kuleta maendeleo, utangamano na ustawi bora wa uchumi wa Zanzibar. Bila shaka yoyote Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA itachangia kwa ujumla katika maendeleo ya Zanzibar na kwa ajili hiyo kuyatimiza matarajio mema ya Sultan Qaboos bin Said, Sultan wa Oman na ya Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kujenga amani na mustakbal mwema wa Zanzibar. SUZA ndiyo taasisi pekee ya kizalendo ya umma iliyokuwa na mtaala wa kuandaa rasilimali watu na maendeleo endelevu katika muktadha wa kuangalia kwa mapana maendeleo ya muda mrefu ya Zanzibar kama kisiwa katika Bahari ya Hindi kilicho na mazingira ya kipekee ilhali kipo karibu sana na Bara la Afrika. Kuna aina tatu za wanafunzi wenye sifa ambao wataweza kuomba nafasi katika Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA: 1. Waombaji ambao ni waajiriwa wa SUZA. 2. Waombaji ambao si waajiriwa wa SUZA lakini watapatiwa Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA lakini watafanya kazi SUZA baada ya kumaliza masomo yao. 3 . Wa o m b a j i m a k i n i kutoka taasisi nyingine wenye kuonyesha uwezo na utayari wa hali ya juu. Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA itakuwa na utaratibu wa kuwafunza wasomeshaji katika fani ya elimu, afya, mazingira, miundo mbinu, ujasiriamali katika ngazi ya Cheti, Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu kutegemea mahitajio ya kistratijia ya muda mfupi, wa kati na mrefu wa Zanzibar. Aina tatu ya waombaji watanufaika katika nyanja za usomi, ufundi na utawala katika vyuo vya Ulaya, Marekani na Asia na msisitizo maalum utakuwa katika elimu na uhifadhi wa rasilimali watu ndani ya Zanzibar kupitia Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA. Wizara ya Elimu ya Juu ya Oman itashirikiana na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA katika kuutekeleza mpango huu na SUZA itashirikiana moja kwa moja na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na taasisi stahili zilizopo kwa lengo la kuwapata wanafunzi bora kutoka sehemu zote za kijamii na za kielimu za Zanzibar watakaoomba nafasi kutoka Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA. Maombi yatakuwa bure kupitia mtandao ambao utaonyesha taarifa zote kuhusu sifa za kuchaguliwa, usajili na ukomo wake na taarifa hizi zitatolewa kwa njia ya matangazo kupitia vyombo vya habari ikionyeshwa pia kuanza rasmi kwa mwaka wa masomo wa 2013-2014. Natoa shukurani zangu za dhati na kumuomba Mola amlipe kheri nyingi Sultan Qaboos bin Said kwa juhudi zake katika kutia nguvu maendeleo ya kujenga raslimali watu kwa ajili ya amani na utengamano wa Zanzibar Amin. Imetayarishwa na Kamati ya Muda ya SQAF ya baina ya Zanzibar na Oman. Kupata taarifa zaidi kuhusu Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA tafadhali wasiliana na: Prof. Idris A. Rai Makamu Mkuu wa Chuo Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) Tel: 0772 195 965 Email: vc@suza.ac.tz
5
Inatoka Uk. 1 Aidha, ametakiwa kufahamu kuwa anachofanya ni kwa ajili ya nchi yake na watu wake, kwa hiyo asitizame madhara anayopata kama mtu binafsi, bali atizame vile ambavyo wapigania nchi kama ilivyokuwa katika mapinduzi, watu walikuwa tayari kupoteza maisha kwa ajili ya nchi yao. Katika kupigania masilahi ya nchi, mara nyingi gharama huwa kubwa ambapo watu huwa tayari hata kufa, ninachomuomba Rais Mstaafu Karume ajue kuwa katika struggle (mapambano) yoyote hapakosekani watu wagumu kuelewa na hata wasaliti, sasa hawa ni wa kuwahurumia maana hawajitambui, ile kukaliwa muda mrefu kumewadumaza hata ule uwezo wao wa kukiri na kuyaona mambo na kuyapima, mimi namwomba asamehe na asikasirike maana akikasirika atakata tamaa kukimbia struggle, amesema Mzee mmoja kada wa CCM ambaye hata hivyo hakutaka kutaja jina lake akisema hali ya hewa hairuhusu. Maoni hayo yanakuja kufuatia hali inayoendelea
Habari za Kimataifa
AN-NUUR
hivi sasa Zanzibar ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakimfanyia dhihaka Rais Mstaafu Mheshimiwa Amani Abeid Karume kwa msimamo wake kuwa kila mtu ni lazima asikilizwe hata anayetaka muungano wa mkataba maana hiyo ndiyo demokrasia. Ukitaka kujua kuwa watu hawa hawajitambui au wamelemaa, wewe angalia misaada kupitia serikalini kutoka kwa Sultan wa Oman wanapokea, hutawasikia wakisema serikali imetekwa na Sultan, lakini Wazanzibari wanaposema wanataka Kiti chao Umoja wa Mataifa, mara propaganda za kurudi Sultani zinaibuka, mbona Bara wakipigania mambo yao hatusikii wakitishiana kurudi Malikia wa Uingereza au Kansela wa Ujerumani? Mbona ujinga huu tunakuwa nao sisi tu wa Visiwani tunaolalamikia kero za muungano? Aliongeza na kuhoji Mzee huyo wa makamo ambaye amesema kuwa yeye msimamo wake ni kuwa na
RAIS Mstaafu Amani Abeid Karume serikali ya Zanzibar yenye mamlaka kamili kuliko ilivyo hivi sasa na kwamba maoni hayo atayasema wazi mbele ya Tume ya Jaji Warioba. Alitaja mfano wa misaada kutoka kwa Sultan kuwa ni pamoja na msaada wa kielimu unaojulikana kama Sultan Qaboos Academic Fellowship (SQAF), maalum kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Serikali Zanzibar (State University of Zanzibar-SUZA). Mbona watu hawa
wanaowatishia watu kurudi Sultan, hatuwasikii wakimshambuliwa Waziri wa Elimu Mheshimiwa Shamhuna kwa kupokea Skolashipu hizo? Mbona watoto wao wanaomba kupata msaada huo wa kielimu, tena wanataka wapewe upendeleo; huku ni kupumbazwa na kupumbaa mpaka inafikia mtu hajui hata lipi la kukusaidia, alisema Mzee huyo akionyesha kukerwa na watu wanaopiga propaganda ya kurudi Sultan. Toka Rais Mstaafu Amani Abeid Karume atoe hotuba Dodoma inayopinga hali ya kutishana Zanzibar na kutaka watu wapewe fursa ya kutoa maoni yao hata wale wanaotaka muungano wa mkataba, kumekuwa na makundi ya watu ambao wamekuwa wakipita kungoa picha zake na wakati huo huo wakitoa kauli za kejeli dhidi yake. Watu hao wanadhaniwa kuwa ni wale wahafidhina ambao hawakutaka hata
Inatoka Uk. 3 waambieni wenzenu wasogee, walikuwa msikitini wakatoka pia, kisha tukaambiwa tulale chini. Alisema, akihadithia tukio hilo. Alisema, utii wa amri zile za maafande kwa Waislamu, ambao alidai walitii kwa ajili ya kuepusha shari, uliwatia mashaka na kuhisi kuwa ulikuwa mtego wakidhani kuwa walikuwepo wengine wenye silaha katika eneo lile. Alisema, baada ya hapo kilichofuata, walianza kuwasachi mifukoni na kuchukua simu zao na pesa na walipojiridhisha kuwa Waislamu wale hawakuwa na silaha, pamoja na kutii amri, askari hao walianza kuwashushia vipigo mfululizo. Alisema, baada ya kutoka pale, walisogea katika jengo la Markazi, waliingia na kufanya upekuzi huku wakitoka na vifaa walivyoweza kuvibeba na kuingiza katika magari yao. Alisema, katika hali ya kushangaza askari wale walikuwa wamegawanyika kwani alidai kuna waliokuwa wakiwapiga na wengine
wakiwatetea na zaidi miongoni mwao walikuwa wakitokwa na machozi baada ya kuona wenzao walivyo washushia vipigo akina mama wa Kiislamu waliokuwa wakiwatoa ndani ya Msikiti wa Markazi. Kina mama wale wa Kiislamu pamoja na vipigo vikali kutoka kwa maafande wale, walikuwa wakitoka wakitamka Shahada, kwa kumtaja Mwenyezi Mungu na Mtume wake, huku wakiitwa Malaya, na matusi mengine mazito mazito, inasikitisha kuona jeshi la Polisi wanakuwa makatili kiasi kile bila kujali wale ni wanawake. Alisema Ust. Abubakar. Alisema, majira ya saa kumi na moja na nusu, walimaliza uvamizi wao na kujiridhisha na kuondoka nao, na katika tukio jingine ni pale ambapo wanawake wa Kiislamu walipogoma na kuonyesha msimamo wa kutokukubali kuvuliwa Hijab zao na kupigwa picha na maafande wa kiume, mpaka pale walipopewa afande wa kike kwa ajili ya shughuli hiyo.
Inatoka Uk. 2 shitaka la kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani, ambalo linamkabili Azzan Khalid Hamdan pekee yake. Katika shitaka la uvunjifu wa amani chini ya kifungu cha 3 (d) cha sheria za Usalama wa Taifa sura ya 47 sheria ya mwaka 2002, washitakiwa wote hao walishitakiwa kwa kuhusishwa na matukio yaliyotokea Oktoba 17 na 18 mwaka huu kuanzia saa 12:00 za asubuhi hadi usiku wa manane. Katika shitaka hilo, kupitia barabara tofauti zilizomo ndani ya mkoa wa Mjini Magharibi Unguja walidaiwa kuharibu barabara, majengo, vyombo vya moto na pikipiki, na walifanya hivyo bila ya kuwepo sababu za msingi za kuharibu na kuteketeza kinyume cha maslahi ya umma na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi 5,000,000. Shitaka la pili linalowakabili ni la ushawishi na uchochezi, ambapo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa baina ya Mei 26 hadi Oktoba 19, 2010 watuhumiwa hao walifanya mikutano katika maeneo tofauti yakiwemo Lumumba,
Khalid Hamdan, ambalo katika shitaka hilo alidaiwa kumtolea maneno ya kashfa na matusi Kamishna wa Polisi wa Zanzibar Mussa Ali Mussa. Mbali na kudaiwa kumshambulia kwa matusi Kamishna huyo lakini pia kiongozi huyo alidaiwa kumwambia Kamishna huyo kuwa mjinga, jambo ambalo mahakama ilidaiwa kuwa lingeliweza kusababisha uvunjifu wa amani katika jamii. Washitakiwa hao pia walitarajiwa kupandishwa tena katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe, mbele ya hakimu Ame Msaraka Pinja, kwa ajili ya kuendelea na kesi ya uchochezi wa kufanya fujo inayowakabili ambapo wiki iliyopita walipewa sharti gumu la dhamana ya kila mmoja kutakiwa kuwasilisha shilingi million moja taslimi na wadhamini watatu na kila mmoja aje na kiwango hicho cha fedha na awe na barua ya sheha na awe na kitambulisho vya Mzanzibari mkaazi na lazima wadhamini hao wawe ni wafanyakazi wa Serikali ya Mapnduzi Zanzibar.
6
Na Omar Msangi, Ramallah IJUMAA iliyopita Novemba 16, ilikuwa ngumu kwa Wa p a l e s t i n a . Wa k a t i mabomu na makombora yakivurumishwa Gaza, Yerusalem askari wa Israel walitanda kila mahali na hakuna mwanamume aliyeruhusiwa kuswali Ijumaa ila wazee tu. Kila aliye na umri chini ya miaka 50 hakuruhusiwa kupita vikwazo vya askari kwenda msikitini. Hayo yakijiri Yerusalem, Ramallah ilikuwa ni mapambano ya askari wa Israil wenye silaha kali na vijana wa Kipalestina waliokuwa wakivurumisha mawe. Ilikuwa mara tu baada ya mshuko wa Ijumaa watu walimwagika barabarani kuandamana, kwanza ikiwa ni kawaida yao kila wiki kuonyesha kupinga kwao uvamizi na ukaliaji wa kinguvu wa Israil katika ardhi yao. Na pili, kuwaunga mkono ndugu zao Gaza ambao kwa muda huo walikuwa wakishambuliwa na Israil. Tunaka katika makutano ya barabara mahali penye kizuizi cha polisi, tunakuta askari wengi wakifyatua risasi na mabomu ya machozi. Kwa mbele tunaona wanaolengwa ni vijana wa Kipalestina waliokuwa wakirusha mawe. Tunapita harakaharaka eneo hilo, mbele tunakuta askari wengine wakifyatua mabomu kuwatimua vijana waliokuwa wakiandamana huku wakiwarushia mawe askari wa Israil wakiwaambia watoke katika nchi yao. Tu n a p o f i k a h o t e l i n i tulipofikia tunakutana na wenzetu kutoka Canada ambao waliondoka asubuhi kuelekea Yerusalem kisha Tel Aviv kwa ajili ya kupanda ndege kurudi makwao. Wanasema wamekwama njiani kwa sababu ya mapambano ya vijana na askari wa Israil. Barabara zimefungwa. Wakati wa Isha unapoingia, kishindo cha risasi na mabomu kinasikika jirani na hoteli na tunaambiwa kuwa mitaani hakupitiki kwa sababu askari wa Israil wametanda mitaani ikitarajiwa kuwa kutakuwa na maandamano usiku kupiga mashambulizi Gaza. Kwa hiyo tunalazimika kubaki ndani japo tulitamani tungetembea kidogo kutizama mji ikiwa ni kuuaga kwa vile asubuhi yake ilikuwa tunaondoka kuelekea Amman, Jordan ambapo napo kupitia televisheni tunaona ghasia za kupinga serikali zinapamba moto.
Makala
AN-NUUR
Hakuna kuswali Ijumaa ila wazee tu Bethlehem mji uliomkataa mwokozi Qalqilyah, mji gereza, kutoka kwa kibali
JUU bango likionesha muda wa kutoka na kuingia getini. Chini mtoto wa Shule kachelewa, Yahudi keshafunga lango hajui la kufanya.
7
Inatoka Uk. 6 alipokuja Mtume Muhammad (s.a.w) ilikuwa rahisi kwa Wapalestina kumkubali. Pili walisema kuwa hata wale Wakristo wachache waliokuwepo, mji huo ulipovamiwa na Israil, Wakristo wengi walikimbia wakiwaacha Waislamu ambao uzalendo wao ni mkubwa na wanaamini katika Jihad na kumtegemea Mwenyezi Mungu kutetea nchi yao, ardhi yao na haki zao na ndio mpaka leo wanapambana na Israil japo Israil ina maguvu ya kijeshi na ikiungwa mkono na mataifa makubwa. Pengine jambo jingine muhimu kusema hapa ni kuwa ardhi hii takatifu kwa Waislamu na Wakristo, hivi sasa ipo mikononi mwa Israil (Mayahudi) ambao hawamuamini Yesu wala kumfuata Mtume (s.a.w). Lakini kwa sasa wanaingiza pesa nyingi sana kupitia utalii kwa sababu watu wengi sana huja kuona alipozaliwa Yesu na anapodaiwa kuteswa na kuzikwa. Japo Bethlehem na Tomb Garden zipo Palestina, lakini hivi sasa zinakaliwa kimabavu na Israil na kuingia hapo unaingia kwa kibali cha Mayahudi. Mpalestina ni marufuku kukanyaga hapo ila yule aliyezaliwa Yerusalem na amepewa kitambulisho rasmi. Nimeipa makala haya kichwa cha habari Unahitaji kuona kuamini kwa sababu yapo mambo huwezi kukiria kuwa yanafanyika katika dunia hii ambapo Umoja wa Kimataifa (UN) na inayoitwa jumuiya ya kimataifa inapiga kelele kila siku juu ya haki za binadamu, uhuru, demokrasia na kuna na Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ambapo watu kadhaa washapelekewa huko. Sasa sikiliza: Qalqilyah ni mji mdogo katika PalestinaWest Bank, wenye idadi ya watu wasio pungua 50,000. Katika sensa ya 2007 walikuwa 47,730. Wavamizi Israil wameuzungushia mji huu mdogo ukuta mkubwa wenye urefu wa kilometa 700 kuzunguka mji mzima na urefu wa kwenda juu mita 8 hali inayoufanya mji huo kuwa kama gereza na kuacha lango moja tu la kutokea. Lango hilo hulindwa na askari na Wapalestina hawaruhusiwi kutoka hapo ila kwa muda maalum. Kwa upande mwingine Mpalestina asiye mkazi wa hapo, kwa maana ya kuwa hajapewa kipande maalum kutoka serikali ya Israil kuwa ni mkazi wa Qalqilyah, haruhusiwi kuingia hata kama ana ndugu zake humo. Kwa hiyo kama unakwenda shamba, kazini,
Makala
AN-NUUR
WATOTO wa shule wakijaribu kupanda ukuta baada ya kufungiwa lango na askari wa Israel wakati wakirudi nyumbani kutoka shule. muda wa kufunguliwa lango. Ukichelewa, lango likifungwa hata kama ni mama mjamzito kashikwa na uchungu, atajifungulia au kua hapo langoni maana Yahudi hatafungua lango mpaka muda uke. Unafika asubuhi unakuta watoto wa skuli wamewahi wamepiga foleni wanasubiri askari wa Israil aje awafungulie. Wakitoka jioni ni hivyo hivyo. Kama kwa bahati mbaya mtoto atachelewa lango likafungwa, itabidi akatafute mahali pa kulala. Yahudi hatamfungulia mlango hata akilia vipi na akimghasi anaweza kumpiga risasi. Hebu jaaliya eneo lote la Sinza, Kijitonyama mpaka Mwenge au Kariakoo na Ilala yote linazungushwa ukuta mkubwa ambao mtu huwezi kuruka halafu kunawekwa lango moja tu la kutokea na kuingia. Halafu inawekwa ratiba ya kutoka na kuingia. Asubuhi saa 1 mpaka saa 3. Lango linafungwa, linafunguliwa tena saa 6 mpaka saa 9. Kisha linafungwa na kufunguliwa saa 11 mpaka saa 1 jioni. Kama unakwenda kazini, hospitali, shule na jambo askari wenye silaha kali. Utatoka kwa ratiba. We hata mkeo akishikwa na uchungu au mtu kapata kiharusi au ugonjwa wowote akawa mahututi, huwezi kuomba kupita kumpeleka mgonjwa hospitali ya Muhimbili au Mwananyamala/Amana nje ya ratiba ya kufunguliwa mji mdogo wa Qalqilyah kwa muda wa miaka 9 sasa. Ukuta huo ulijengwa mwaka 2003. Labda jiulize, kuna uvunjaji wa haki za binadamu uliozidi huu? Unageuza mji mzima kuwa gereza!! Jiulize tena, ulishawahi kumsikia Ban Ki-moon, Bila shaka hujasikia wala hujui kama kuna watu duniani wanafanyiwa unyama huo kwa sababu hiyo sio habari kwa BBC, CNN, Aljazeera, Sky News, Sauti ya Ujerumani (tunazoziona za maana sana)! Ndio maana nikasema, unahitaka kuona kuamini.
VIJANA wa Kipalestina wakimsaidia mwenzao aliyejeruhiwa katika maandamano mjini Ramallah Ijumaa iliyopita.
8
Na Ibn Rajab
KITABU cha Jan P. van Bergen, Development and Religion in Tanzania, kimemnukuu Mwalimu Nyerere akisema kwamba maslahi ya dini yake (Ukatoliki) yanakuja mwanzo na kwamba kamwe hatokwenda kinyume na kanisa lake. Huu ni ushahidi wa wazi kwamba Nyerere alitawala nchi hii kwa maslahi ya kanisa lake. Ikumbukwe kwamba Waislamu wa Tanzania ndiyo waliokuwa wa kwanza duniani kuchangia fedha kwa ajili ya Wakatoliki waliotaka kujitenga nchini Nigeria katika jimbo la Biafra. Nyerere aliwachangisha fedha Waislamu wa Tanzania, ili zisaidie kupigana na Waislamu wenzao wa Nigeria. Harakati za Ukatoliki Nigeria, nchi yenye Waislamu wengi barani Afrika, zilitaka kulitenga jimbo la Biafra linalokaliwa na Wakristo wengi, ili kuepukana na kile walichoita a calamitous slavery in an ocean of Muslims (balaa la utumwa katika bahari ya Waislamu). Isitoshe, Nyerere alipoivamia Uganda mwaka 1979 na kumpindua Idd Amin Dada, inasemekana kuna askari walipewa maelekezo maalumu ya kuangamiza miji ya Waislamu nchini humo. Dk. Sengendo, msomi mashuhuri kutoka
Makala/Tangazo
AN-NUUR
Uganda, alimwaga machozi pale Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, wakati alipogusia nukta hiyo katika mazungumzo yake na Waislamu mwanzoni mwa miaka ya tisini. Nyerere alimrejesha madarakani ndugu yake katika Msalaba, Milton Apollo Obote, Mkristo aliyemsaidia sana kuunda taifa la Tanzania kwa msaada wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), ambalo Mkurugenzi wake wakati ule alikuwa George Bush, ambaye baadaye akaja kuwa Rais wa Marekani. Ujenzi wa makanisa makubwa nchini Tanzania, wingi wa Seminari za Kikristo, utitiri wa mashirika ya Kikristo, idadi kubwa ya mapadri wa kigeni na masista wao makanisani, ni ushahidi mzito kwamba Taasisi za Kikristo hapa nchini, zina mafungamano na zinatumiwa na mataifa ya kigeni. Kwa sababu si rahisi, kwa michango ya waumini wao peke yake kuendesha shughuli hizo, ikiwa ni pamoja na kugharimia staili ya maisha ya juu ya viongozi wa makanisa. Makanisa yote ya
ZAWADI ZA MASHINDANO
Kamati ya Da-awah ya Afrika inawatangazia Waislamu wote kwamba zile zawadi za washindi wa mashindano kuhusu Familia ya Mtume (s.a.w.) na maswahaba (r.a.) yaliyofanyika mwaka huu 1433/ 2012, zitatolewa siku ya Ijumaa tarehe 23/ 11 / 2012 katika Msikiti wa Morogoro, Ilala Dar es Salaam maratu baada ya swala ya Ijumaa. Nyote mnakaribishwa. Wabillahi tawq
Makala/Tangazo
AN-NUUR
yaliendelea. Katika hospitali ya Al Shifa, Kandili aliwatembelea waathirika. Alilaani mashambulizi ya Israel, akisema: Mkasa huu hauwezi kupita kimya kimya, na dunia lazima iwajibike kuzuia ushambuliaji huu. Cairo itajitahidi kutafuta njia ya kurudisha amani, aliongeza. Kuanzia Jumamosi, zaidi ya Wapalestina 40 waliuawa. Mamia wengine walijeruhiwa. Wengi wako mahututi. Dazeni za mashambulizi ya ndege zinaendelea. Vifo na majeruhi vinaweza kuongezeka kwa kasi kubwa. Matarakimu ya hivi sasa yanadumaza athari halisi kwa sababu baadhi ya waathirika wamelala chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa. Kituo cha Kimataifa cha Habari za Mashariki ya Kati (IMEMC) kilisema Israel ilifanya mashambulizi 30 katika muda usiozidi dakika 30 siku ya Ijumaa. Kunako saa nne usiku Alhamisi, jeshi la Israel lilisema lilipiga maeneo lengwa 70 katika saa nzima iliyopita. Maeneo ya raia na majengo ya serikali yalipigwa mabomu na mizinga. Shule mbili za Umoja wa Mataifa zilipigwa. Uharibifu
Inaendelea Uk. 11
NAFASI ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO UALIMU WA MAARIFA YA UISLAMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI - 2013
Tunachukua fursa hii kuwatangazia Waislamu wanaume na wanawake nafasi za mafunzo ya Ualimu wa Maarifa ya Uislamu kwa shule za Msingi na Sekondari yatakayoanza Februari 2013. SIFA NA MASHARTI YA KUJIUNGA Muombaji atimize sifa na masharti yafuatazo:(i) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya Uislamu Darasa la Watu wazima kabla ya kujiunga. (ii) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne na awe anafundisha Madrasa au Maarifa ya Uislamu katika kipindi cha dini shule za Msingi au Sekondari kwa muda usiopungua mwaka mmoja. (iii) Awe anajua kusoma Quran kwa ufasaha. FOMU ZINAPATIKANA CHUONI UBUNGO KWA GHARAMA YA SHILINGI ELFU TANO TU. MUHIMU Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11/2012. Usaili utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 01/12/2012 saa 2 asubuhi. Wabillah Tawiq MKUU WA CHUO
10
Habari
AN-NUUR
SIKU ya Jumatano, Novemba 14 mwaka 2012, majeshi ya Israeli yamemuua Ahmed Al-Jabari, kamanda wa kijeshi wa Hamas, mtoto wake wa kiume na Wapalestina wengine kadhaa. Mashambulizi dhidi ya Gaza bado yanaendelea na idadi ya Wapalestina waliouawa na kujeruhiwa kupitia mashambulizi hayo inazidi kuongezeka kila uchao. Watu wengi duniani, kwa usahihi kabisa, wamelaani kitendo hiki cha kihalifu. Kufuatia matukio hayo, ni vizuri kuweka bayana nukta chache zifuatazo, ili kuwafanya wasomaji watafsiri matukio hayo kwa kutumia akili zao wenyewe, badala ya kulazimishwa na vyombo vya habari. Ajabu ya Rahman, vyombo vya habari vya Magharibi vinajenga picha ulimwenguni kana kwamba Wayahudi ndiyo wanaokandamizwa na Wapalestina, kwa hiyo wana haki ya kujihami kwa kuwaangamiza kwa makombora! 1-Mashambulizi ya kinyama ya Israeli dhidi ya Wapalestina wa Gaza, yanathibitisha wazi kwamba taifa hili la kiyazuni halina heshima hata kidogo na uhai wa binadamu. Hawajali kitu kwa sababu walishalaaniwa pia katika mauaji waliyofanya mjini Jenin, Lebanon na Gaza siku za nyuma. Miito ya mchakato wa amani (peace process) katika eneo la Mashariki ya Kati, inazidi tu kuiimarisha Israeli dhidi ya Wapalestina. Ufumbuzi wa kuunda dola mbili zilizo sambamba (A two-state solution), yaani dola ya Israeli na Palestina, kama unavyopendekezwa na mataifa ya Magharibi, utazidi tu kuwatia utumwani Waislamu wa Palestina. Kwa sababu dola ya Wapalestina itakuwa dhaifu mno na uzoefu unaonyesha kwamba haitaundwa na Wapalestina wenyewe. Matukio ya mara kwa mara ya utumiaji nguvu, vitendo vya mauaji, vitisho na kibri, ndiyo majibu ya madhalimu wote katika historia, katika kuhalalisha mauaji na ukandamizaji wao ili waweze kuwepo. Bila ya hivyo hawawezi kuwepo ngo! 2-Ni majeshi tu ndiyo yanayoweza kuwalinda watu wanaokaliwa kimabavu na
akina Salahuddin Ayubi au Muhammad al Fatih. Watawala hawa walihamasisha majeshi yao, walikomboa ardhi zilizokaliwa kimabavu na kutawala nchi za Waislamu kwa haki, amani na utulivu. Ukisoma historia ya Mashariki ya Kati, utaona kwamba hakuna kipindi ambacho eneo hili lilikuwa tulivu zaidi na lenye amani kuliko kipindi kile lilipotawaliwa Kiislamu. Huu ni ukweli ambao mabeberu wa Magharibi hawawezi kuusema ingawa wanaufahamu. 6-Kuungwa mkono kwa Israeli na Mataifa ya Magharibi, kama Marekani na Uingereza, kusiwashangaze sana watu. Wazo la kuundwa Israeli ni la Serikali ya Uingereza kupitia azimio la Balfour. Taifa hili la Kizayuni katikati ya mataifa
ya Waislamu, limekuwa likilelewa na kuimarishwa na mataifa ya Magharibi kwa miaka mingi, ili kulinda maslahi yao katika eneo la Mashariki ya Kati. Bila shaka watajaribu kufufua mazungumzo yaliyokwama ya mpango wao wa Road Map kuelekea two - state solution kwa maslahi ya mataifa yao. Lakini kwa Waislamu wa Palestina, mpango huo ni maangamizi kwa sababu unahalalisha kukaliwa kimabavu. Palestina inahitaji kukombolewa kabisa kutoka kwenye makucha ya Israeli. Huu si wakati wa mikutano, vikao vya wakuu wa nchi za Kiarabu, wala mazungumzo ya kuleta amani. Israeli kwa mara nyingine tena imemwaga d a m u y a Wa i s l a m u w a Gaza, na Mwenyezi Mungu
ameamrisha Jihad kama suluhisho kwa vitendo hivyo vya woga vinavyofanywa na Israeli. Majeshi ya Waislamu duniani kote yaitikie wito wa Mwenyezi Mungu pale aliposema: Hawawi sawa Waislamu wanaokaa wasende vitani, isipokuwa wenye dharura. (Hawawi sawa) na wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu amewafadhilisha katika cheo wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nafsi zao na mali zao kuliko wakaao (wasende kupigana). Ingawa Mwenyezi Mungu amewaahidi wote (kupata) wema, lakini Mwenyezi Mungu amewafadhilisha - wale wapiganao kuliko wakaao - kwa ujira mkuu Qur(4:95).
KONGOWE- MJI WA KIBAHA VINAUZWA (SURVEYED PLOTS AT KONGOWE- KIBAHA TOWNSHIP) Plan Na E`373/109 Reg. No. 70995 Plots No. Eneo / Sqm Bei 5 2,259 13,554,000 6 1,566 9,396,000 8 1,984 11,904,000 9 3,564 21,384,000 10 2,842 17,052,000 11 3,732 22,392,000 15 2,292 13,752,000 16 2,367 14,202,000 17 2,423 14,538,000 NB: Kila Sqm ni shilingi Elfu 6000/tu. Kilo Mita Moja kutoka Barabara ya Morogoro, Kuna Umeme, Maji na Barabara. Kwa mawasiliano zaidi piga simu zifuatazo. 0755 090754 au 0715 090 754
VIWANJA VILIVYOPIMWA
11
Habari
AN-NUUR
mashambulizi ya kiharamia.Uhalifu mwingi wa kivita na dhidi ya binadamu unafanyika. Mengi yako hatarini Palestina, eneo la Mashariki ya Kati na nje ya hapo. Mashambulizi ya kivita ya Washington yanaendelea. Vita nyingine zinapangwa. Israel ni mshirika muhimu. Nchi hizo mbili zina ajenda za kibabe juu ya nchi nyingine. Vita ni njia muhimu ya kuzikia. Michel Chossudovsky anaita kushambuliza na kuvamia Gazasehemu ya ajenda pana ya kijeshi ya Marekani-NATO na Israel. Kwa msingi wa kile kilichotokea baada ya 9/11, tarajia mabaya zaidi baadaye. (Makala hii Targeting Civilians: Israels Specialty iliyoandikwa na Steve Lendman, imefasiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija)
ada inayohitajika wamelipa ikiwa ni pamoja na kutoa maelezo ya sera na ratiba ya vipindi. Hata hivyo akasema, kwa muda mrefu wamekuwa wakizungushwa kupata CP na bado wanafuatilia kibali hicho. Mwenyekiti huyo wa TV Imaan ametoa maelezo hayo kufuatia malalamiko kutoka kwa Waislamu wengi waliotaka kujua ni kwa nini mpaka sasa TV hiyo haijakuwa na Studio na kuanza kurusha vipindi. Kwa muda mrefu sasa, TV Imaan imekuwa katika majaribio ambapo ilitarajiwa kwamba mpaka sasa wangekwisha kamilisha taratibu zote zilizowekwa na Mamlaka husika, yaani Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), na hivyo kuanza kurusha matangazo rasmi. Kwa muda sasa baadhi ya Waislamu wamekuwa wakihoji, ni kwa nini TV Imaan haianzi kurusha matangazo na imebaki tu katika kufanya majaribio katika satelaiti. Kufuatia malalamiko ya Waislamu waliofika katika ofisi za An nuur, Mwenyekiti wa TV Imaan ameongea na mwandishi akisema kuwa kwa upande
wao wametimiza mashariti yote na kwamba hata wao wanajiona wapo katika wakati mgumu kwa sababu wanajua hamu waliyo nayo Waislamu kuona TV yao ikiwa hewani. Akasema, bado wanafanya subra wakiamini kuwa TCRA itawapa kibali kinachohitajika, lakini kama muda utazidi kuwa mkubwa watalazimika kuwaita Waislamu waliokusanyika pale Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Arusha ili kuwaeleza vikwazo wanavyokumbana navyo katika kuanzisha TV hiyo. Akifafanua Aref amesema kuwa hawataweza kuepuka kuwaita Waislamu kama watakwama kwa sababu kama Waislamu walivyochangia fedha zao, wana haki pia ya kujua nini kinakwamisha TV hiyo kuanza. Akieleza hatua w aliy o f i k i a a m e s e m a kuwa walipewa mambo ya kutekeleza yakiwa ni kupata mkataba na MUX Operators ambapo wameshaingia mkataba na Star Media (T) Limited. Jambo la pili lilikuwa kuwasilisha sera ya TV (Editorial Policy) ambayo washapeleka na tatu kulipa ada ya dola 1,500 ambayo nayo washalipa. Aref amesema, ni imani yao kuwa TCRA watawapa kibali hicho, CP, kabla ya shinikizo kutoka kwa
Waislamu kuwazidia nguvu na kuamua kwenda tena Uwanja wa Taifa kujieleza kama walivyojieleza wakiomba michango ya Waislamu. Kwa upande wa TCRA, An nuur iliwasiliana na F. N. Ntobi na Chacha ambao ni katika maosa waandamizi wa taasisi hiyo ambao walisema kuwa kama TV Imaan wana malalamiko, hawana sababu ya kusemea pembeni, bali wafike waonane na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka. Hata hivyo, kwa upande wa TV Imaan, wanadai kuwa walishawasilisha malalamiko yao kwa Mkurugenzi huyo baada ya kuona wanazungushwa sana katika ngazi za chini. Katika barua yake kwa Mkurugenzi Mkuu (TCRA DG) Kumb. Namba TVI/ T C R A / V. 0 4 / 2 0 1 2 y a tarehe 6 Novemba, 2012, Mwenyekiti wa TV Imaan Aref Nahdi baada ya kutoa vielelezo vya kukamilisha mashariti waliyopewa, alimwomba DG huyo kuingilia kati suala hilo kwa vile kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipewa ahadi hewa. Akamalizia kwa kasema kuwa kuchelewa kwao kutoa kibali, kunasababisha sintofahamu baina ya viongozi wa TV Imaan na Waislamu waliotoa sadaka zao kwa ajili ya TV.
AN-NUUR
12
Na Bakari Mwakangwale
TAASISI za Kiislamu nchini zimetakiwa kuwasaidia vijana wa Kiislamu wasiokuwa na uwezo wa kujilipia ada ya masomo ya Vyuo Vikuu ili kuendeleza Uislamu na wataalamu kwa ujumla. Wito huo umetolewa na Mweyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro, Dr. Mussa Assad, mbele ya Mkuu wa Chuo hicho katika mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo, mwishoni mwa wiki iliyopita. Akisoma nasaha hizo kwa niaba ya Dr. Assad, Bw. Ahmad Sagafu, aliye mjumbe wa Baraza la Chuo hicho alisema, kutokana na idadi kubwa iliyopatikana mwaka huu kwa vijana wengi wa Kiislamu kukosa mkopo toka Serikalini kupitia Bodi ya Mikopo, ni vyema Taasisi za Kiislamu zikajipanga ili kuwanusuru vijana hao siku za mbele. ili kusaidia wanachuo wasiokuwa na uwezo wa kujilipia kwa ajili ya masomo yao, na haswa wanapokosa mkopo wa serikali, Taasisi za Kiislamu nchini zingejipanga katika kusaidia kuwalipia wale wanachuo wasio na uwezo ili kuuendeleza Uislamu na wataalamu nchini. Alisema Bw. Sagafu. Wito huo kwa Taasisi za Kiislamu umekuja kufuatia wanafunzi wapatao 1600, ambao walitegemea kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo, kukosa mikopo hiyo, hivyo kushindwa kujiunga na Chuo. Alisema, hali hiyo imesababisha na kuchangia upungu wa wanafunzi waliotarajiwa kujiunga Chuoni hapo, baada ya kukosa Mikopo na kutokuwepo njia mbadala ya kuweza kuwanusuru na kuwasaidia vijana hao kujiunga na Chuo. Upungufu huo unatokana
MKUU wa Chuo cha Waislamu Morogoro (MUM) Hajat Mwantum Malale (katikati) akiwa na baadhi ya wahitimu mara baada ya kutunukiwa shahada zao wiki iliyopita chuoani hapo. Waliofanikiwa kumaliza na ukweli kwamba wanachuo kuanzishwa kwake mwaka masomo yao salama na ambao waliopata mikopo ni 251 tu, 2005, alisema jumla ya wahitimu leo (Jumamosi iliyopita) kutoka kwenye orodha ya 509, wamefanikiwa kumaliza wanatunukiwa shahada zao ni wanachuo 1800 waliopatiwa masomo yao salama na kustahiki 509. Nawaombea kwa Allah nafasi ya kujiunga na masomo kutunukiwa shahada zao. (s.w) ajaalie elimu yao iwe ni mwaka huu wa masomo. Prof. Njozi, alitumia fursa yenye manufaa katika jamii Alisema Bw. Sagafu, hiyo kuwaombea dua kwa yetu. Alisema Prof. Njozi. Naye Makamu Mkuu wa Mwenyezi Mungu wahitimu Awali Prof. Njozi, alisema Chuo hicho, Profesa Hamza hao awajaalie elimu waliyoipata wahitimu hao ambao awali Musafa Njozi, akiongea katika iwe ni yenye manufaa katika walikuwa 622, wamesomea mahafali hayo ya Tano toka jamii kwa ujumla.
MASHEIKH na Wanazuoni wa Kiislamu wa Jijini Dar es Salaam, wametakiwa kuwakia Waislamu waliopo vijijini ili kutoa elimu kwa Waislamu walioko huko badala ya kuishia Jijini. Wito huo umetolewa na Imam wa Msikiti wa Nur, Masaganya, Wilayani Kisarawe, Sheikh Salum Omari Kongoro, katika haa fupi iliyofanyika Msikitini hapo baada ya kutembelewa na Hajjat Rehema Amir Gama. Imamu Kongoro alisema
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.
Alisema, baada ya kukabidhiwa ardhi hiyo, Hajjat Gama, alisema atatafuta wadhamini pamoja washirikiane katika harakati za kujenga kituo hicho. Nitakuwa bega kwa bega na watoto pamoja na wajane hawa, nimekabidhiwa shamba la heka moja kwa ajili ya kujenga kituo cha yatima iwapo nitapata kuungwa mkono nitashukuru Mungu. Alisema Hajjat Gama, ambaye anaendesha Madrasatu Jannatil Islaamiyah, iliyopo Ilala, Mtaa wa Nzasa, namba 17..