You are on page 1of 8

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

TAARIFA YA UFUATILIAJI WA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE


1. UTANGULIZI
Mnamo tarehe 27 Januari 2014, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipata taarifa za kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa homa ya
dengue katika Kliniki ya International School of Tanganyika iliyopo Manispaa ya Kinondoni katika jiji la Dar es Salaam. Taarifa hiyo
ya awali ilionyesha kuwepo kwa jumla ya wagonjwa 6 katika kituo hicho bila vifo.
Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es
salaam ambapo idadi ya watu 40 walithibitika kuwa na ugonjwa. Pia, kati ya mwezi Mei hadi Julai 2013, wagonjwa 172
walithibitishwa kuugua ugonjwa huu.
2. UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes. Dalili za ugonjwa huu ni
homa ya ghafla,mwili kuchoka, kuumwa na viungo, kuvimba tezi na kupatwa na harara. Uwepo wa homa, kuumwa kichwa
maumivu ya viungo na uchovu ndio dalili kuu za ugonjwa huu. Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia kati siku ya 3 na 14 tangu
mtu alipoambukiwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za
malaria. Kuna aina 3 tofauti za namna ugonjwa huu unavyoweza kujitokeza iwapo mtu aking`atwa na mbu mwenye virusi hivi;
i. Homa ya dengue (Dengue Febrile Illness): Aina hii huambatana na dalili kuu tatu za homa kali ya ghafla, kuumwa kichwa
na maumivu ya viungo au uchovu. Asilimia kubwa ya watu hapa nchini waliothirika wamekuwa na aina hii ya dalili.
ii. Dengue ya damu (Dengue Haemorrhagic Fever): Aina hii ya homa ya dengue huambatana na dalili za mgonjwa kutokwa
na damu kwenye fizi au puani, vile vile kutokwa na damu chini ya ngozi. Iwapo mgonjwa huyu ataumia sehemu yoyote ni
rahisi kwake kupoteza damu nyingi kupitia kwenye michubuko.
iii. Dengue ya kupoteza fahamu (Dengue Shock syndrome): Aina hii ya homa ya dengue huambatana na mgonjwa kupoteza
damu nyingi ambayo hupelekea mgonjwa kupoteza fahamu.
Aina ya pili na ya tatu ni aina zenye dalili mbaya ambazo zinaweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa na hatimaye kusababisha kifo.
Kwa Tanzania, hadi sasa ni aina ya kwanza ya Homa ya Dengue imeripotiwa.
Virusi vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu baada ya kuumwa na mbu aina ya Aedes. Mbu hawa hupendelea
kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi
katika mazingara ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu.
Ugonjwa huu hauenezwi moja kwa moja kutoka binadamu mmoja kwenda kwa mwingine bali kwa kupitia mbu aliyeambukizwa na
virusi vya homa ya dengue anapomuuma binadamu. Homa ya dengue inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali
mapema na kupatiwa matibabu ya haraka. Hakuna tiba maalum ya kutibu virusi vya denge wala chanjo bali mgonjwa
anatibiwa kutokana na dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue:
o Kuangamiza mazalio ya mbu
Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile, vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa
hovyo, nk.
Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo yaharuhusu maji kutuma
Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara
Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
o Kujikinga na kuumwa na mbu
Tumia dawa za kufukuza mbu mosquito repellants
Vaa nguo ndefu
Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (hasa kwa wale wanalala majira ya mchana)
Weka wavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi
2. HALI HALISI YA SASA YA UGONJWA NCHINI
11.1 Idadi ya Wagonjwa:
Kuanzia tarehe 27 Januari hadi tarehe 6 April 2014, jumla ya wagonjwa 399 (Kinondoni 322, Ilala 61 na Temeke 16)
wamethibitishwa kuwa na ugonjwa homa ya dengue. kati yao, wagonjwa wawili (2) wamepoteza maisha;
(i) Mwanamke, umri miaka 22, aliyefariki katika Hospitali ya Mwananyamala tarehe 14.3.2014.
(ii) Mwanamke, umri miaka 37, muuguzi, aliyekuwa mfanyakazi wa Hospitali ya Temeke ambaye alifia hospitali ya
MNH

11.2 Maeneo yaliyoathirika
Ugonjwa huu umeripotiwa katika kila eneo la Dar es salaam lakini Kata zilizoathirika zaidi kwa kuwa na wagonjwa wengi zaidi ni
kama zifuatatazo;
KATA IDADI
Msasani 93
Masaki 68
Magomeni 54
Kinondoni A/B/Manyanya 29
Mikocheni 21
Buguruni 20
Tandale 15
Sinza/Kijitonyama 13

11.3 Dalili za kuu zilizojitokeza
Wagonjwa wote 399 waliothibitishwa kuwa na ugonjwa walikuwa na na homa kali.. Aidha 82% ya wagonjwa walionyesha pia dalli
ya kuumwa kichwa. Dalili nyingine ni zilizojitokeza ni pamoja na kutapika, maumivu wakati wa kutoa haja ndogo, na kuumwa
tumbo.
11.4 Jinsia na Umri
Kati ya Wagonjwa 376, 214 (54%) walikuwa wanaume na 185(46%) walikuwa ni wanawake. Idadi kubwa ya wagonjwa
waliothibitika kuwa na ugonjwa huu wako katika Umri zaidi ya miaka 16 yaani asilimia 92. Aidha watoto chini ya umri wa miaka 5
walikuwa ni asilimia 2 tu.
1.1 Mwenendo wa Ugonjwa
Mlipuko huu wa tatu wa dengue hapa nchini ulianza tarehe 2 Januari 2014. Ongezeko kubwa la wagonjwa limejitokeza katika
mwezi wa tatu (3) mwishoni na kushika kasi mwezi wa Aprili, 2014 ambapo wagonjwa wengi wameongezeka.

Jedwali No 1: Mwenendo wa Ugonjwa wa Dengue kuanzia utokee,2 Januari 2014- 6 May 2014 (N=399)
2. HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA WIZARA
2.1 Hatua za Muda mfupi
WAUJ imetoa tamko la Serikali kwa wananchi kwa nyakati tofauti kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Dengue. Tamko la kwanza
lilitolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 04 Februari 2014 na Machi 2014. Aidha, uelimishaji kwa wananchi unaendelea
kupitia Radio, TV na magazeti. Aidha matumizi ya Vipaza sauti katika ngazi za chini utaanza na kusimamiwa na
Halmashauri za Wilaya mkoani Dar es salaam.
Kuendelea kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa
Tanzania Bara. Aidha taarifa hii pia inajumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa),
Ukweli Kuhusu Ugonjwa(Fact sheet) na mwongozo wa uchukuaji wa sampuli na matibabu. .
Kuendelea kutoa elimu kwa Watumishi wa afya madaktari pamoja na wanaofanya maabara kuhusu namna ya
kutambua ugonjwa huu. Aidha watumishi wa hospitali za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Temeke wamekwisha
kupewa mafunzo haya na bado yanaendelea kutolewa kupitia mikutano ya kila asubuhi ya kiltaaluma (Clinical
meetings). Halmashauri zinaendelea pia kuyatoa mafunzo haya katika ngazi za chini.
Kufuatilia kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyo kuwa ya malaria kwa Mikoa na Wilaya zote nchini ili
kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo kuna ugonjwa huu.
Kuanzishwa kwa vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika Hospitali za Manispaa za jiji la Dar es Salaam
(Mwananyamala, Amana na Temeke Hospitali), aidha, Kituo cha International School of Tanganyika IST kilichopo
Manispaa ya Kinondoni pia kinaendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huu pamoja na Kituo cha Hospital ya Muhimbili.
Kuimarisha uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya Taifa (NHLQATC) ambapo mpaka sasa
kumethibitishwa kuwepo kwa aina 2 za virusi hivi yaani DENV2 na DENV3. Vile vile Wizara imepeleka kiasi kidogo
cha vipimo vya awali yaani Dengue Rapid Test Kits kwa baadhi ya vituo vya Dar es salaam kuimarisha utambuzi na
vituo hivo ni pamoja na Muhimbili, Amana hospital, Mwananyamala hospitali, Temeke Hospital, na IST kliniki.
Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na mipakani kupitia mfumo wa
ufuatiliaji wa magonjwa (saveilensi) ya IDSR . Aidha, Wizara imetoa maelekezo kwa Waganga wakuu wa mikoa na
wilaya kutoa taarifa za wagonjwa wa Dengue Fever kupitia taarifa za kila wiki (Infectious disease week ending)
Kutoa miongozo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani kuhusu kutokuwepo kwa aina yoyote ya
vikwazo vitakavyowekwa kwa ajili kwa wasafiri. Aidha maelekezo hayo yameainisha kuwa iwapo msafiri anayeondoka
au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze
kuchukuliwa.
Kudhibiti mbu kwa kupulizia dawa ( Fogging) katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika katika mkoa wa Dar es salaam.
Aidha mpango wa WAUJ ni kufikia maeneo mengi zaidi pamoja na kufanya kuweka dawa ya kuua viliwi luwi
(Larviciding) kwa viluwiluwi
Kupeleka taarifa ya mlipuko huu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kama mwongozo wa Kimataifa uvyaoelekeza
Kupitia Timu ya Taifa ya Maafa, Wizara imeandaa mpango kazi na mkakati wa muda mfupi wa namna ambavyo
ugonjwa huu utadhibitiwa ukishirikisha wadau mbalimbali. Kimabatanisho namba 1 kinafafanua kazi zilizoaninishwa.
3.2 Hatua za muda mrefu
WAUJ imeandaa Mpango Mkakati (2014 2018) wa kukabiliana na magonjwa ya Viral Haemerrhagic Fevers
ikihusisha na ugonjwa wa homa ya dengue.
Halmashauri za mkoa kutengeneza strategic plan ya kwao kwa kuangalia prototype plan ya WAUJ
4. Changamoto
4.1 Kutokuwepo na vitendanishi vya kutosha kuanisha ugonjwa huu kwa ngazi za chini (Rapid Diagnostic kits). Hii
inapelekea ufuatiliaji wa ugonjwa huu kuwa mgumu kwa watumishi wa vituo vya afya na kulazimu sampuli zipelekwe
Maabara kuu ya Taifa -- NHLQATC
4.2 Kutokuwepo na mpango mkakati shirikishi wa pamoja na wadau mbalimbali wa namna ya kukabiliana na ugonjwa huu.
Aidha Wizara imeitisha mkutano wa pamoja na wadau ili kuweza kushirikiana nao. Mkutano huu umefanyika 7.5.2014
ambao umeainisha hatua za kuchukuliwa.
4.3 Upungufu wa wataalum waliobobea katika kukabiliana na wadudu wadhurifu Entomologists katika ngazi ya mbalimbali.
Na hii inapelekea uratibu wa kazi za vector kutoratibiwa katika kiwango stahiki
4.4 Kutokuwepo na fedha za kutekeleza mikakati mbalimbali ya Integrated Vector control activities pamoja na kukabiliana
na milipuko kwa ujumla kutoka ngazi ya Taifa mpaka chini
4.5 Jamii kutokukuelewa kuhusu ugonjwa huu na hii ni kwa sababu ugonjwa huu bado ni mpya nchini Tanzania. Kupitia
mpango mkakati unaoandaliwa na Wizara, ushirikishwaji wa wadau wengine zaidi ya wa afya utaanishwa ili kuweza
kuandaa vielemishi na kutafuta njia nyingine za kufikisha ujumbe.


Kiambatanisho namba 1,
MAAZIMIO YA KIKAO CHA TIMU YA TAIFA YA MAAFA KUHUSUIANA NA DENGUE FEVER
TAREHE 7.5.2014
Kazi Shughuli Mhusika Muda wa Utekelezaji
Uratibu wa shughuli za
Dengue Kitaifa
Kuwasilisha mpango kazi ulioandaliwa
kwa ngazi za juu ili pia uweze
kuwasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu
WAUJ: Epidemiolojia
Mara moja
Uratibu wa shughuli za
Dengue mkoani Dar es
salaam
Kuandaa mpango mkakati wa namna ya
kukabiliana na Dengue kwa kutumia
prototype plan ya mpango mkakati wa
Kitaifa
Halmashauri 3 za Ilala,
Kinondoni na Temeke
Tarehe 12.5.2014
Udhibiti wa Mbu na viluwiluwi
Kuua mazalio ya mbu yaani viluwili
(Larvidicing) kwa kutumia bio-larvicide
ambao iko kwa kiasi iliyokuwa inatumika
katika mradi wa Bio larvicide kati ya
Cuba na WAUJ kupitia NMCP. Aidha
kutakuwa na ushirikishwaji wa serikali za
mitaa na CORPS
Kuendelea na kufanya fogging (kuua
mbu wapevu) wenye tayari vimelea
kutumia viautilifu vya kuua mbu katika
maeneo yaliyotoka idadi ya wagonjwa
wengi. Aidha kutakuwa na ushirikishwaji
wa serikali za mitaa na CORPS
Halmashauri 3 za Ilala,
Kinondoni na Temeke
Mara moja (Angalizo:
utategemea pia hali ya
hewa na mvua)
Usafi wa mazingira: Maafisa Afya wote
wa Halmashauri watahusika katika
kusimamia na kuhamasisha usafi wa
mazingira kwa kutumia sheria ndogo
ndogo ilizojiwekea ikiwemo na kutoa faini
WAUJ: Kitengo cha Usafi wa
Mazingira
Halmashauri 3 za Ilala,
Kinondoni na Temeke
Mara moja

Maafisa Afya ikiwemo wa kata
wataelemisha wananchi namna ya
kudhibiti ugonjwa kwa vipaza sauti,
WAUJ: Kitengo cha Usafi cha
mazingira na Elimu ya Afya

uongozi wa mitaa, kugawa vielemishi. Na
vilevile kuendelea kutumia vyombo vya
habari na TV
Halmashauri 3 za Ilala,
Kinondoni na Temeke
Elimu kwa watumishi wa Afya
Kutoa elimu kupitia clinical meetings
katika hospitali zote za wilaya na pia
kupitia APHTA
WAUJ: Epidemiolojia
Halmashauri 3 za Ilala,
Kinondoni na Temeke
Mara moja
Kuimarisha utambuzi wa
ugonjwa
WAUJ kuwasiliana na MSD kuhusu
upatikanaji wa Dengue Rapid Kits ili
Halmashauri ziweze kufuata utaratibu wa
manunuzi
Halmashauri na pia MNH kupanga katika
mipango yao fedha za kununua kits hizi
Kwa kipindi hiki ambapo kits
zinaonekana kupungua katika maeneo
tajwa yaani MNH, na Hospital za Wilaya
mkoani Dar es salaam, NHLQATC
itatumika kupima vipimo hivi ili kuwepo
na mwenendelezo wa Sentinel
Surveillance
WAUJ: Epidemiolojia na
Diagnostic
Halmashauri 3 za Ilala,
Kinondoni na Temeke
Mara moja
Kuimarisha ufuatiliaji wa
ugonjwa
Kutengeneza protocol ya Surveillance
pamoja na alogarithm ya matibabu
WAUJ: Epidemiolojia na
Diagnostic
10.5.2014

Kuweka messages katika Point of Entry WAUJ: Kitengo cha Afya ya
Mazingira
Mara moja
Ushirikishwaji wa wadau
mbalimbali katika kukabiliana
na ugonjwa huu
WAUJ kuandika barua kwa RAS Dar es
saalam kuanisha maeneo ya utekelezaji
ambao yako chini ya mamlaka yake
WAUJ kuandika barua ya kuomba zaidi
msaada wa Dengue Rapid Kits WHO,
CDC na USAID
WAUJ: Epidemiolojia na
Diagnostic
WAUJ: Epidemiolojia na
Diagnostic
Mara moja

UNICEF kusaidia na IEC materials yaani
Posters na leaflets ambazo tayari
zimeshatengenezwa
WAUJ: Kitengo cha ELimu ya
Afya kwa Umma
Mara moja maana tayari
kuna mawasiliano

WHO kusaidia katika uelimishaji kwa
kupitia kifungu cha fedha za World
Health Day iliyolenga masuala ya
vector
WAUJ: Kitengo cha ELimu ya
Afya kwa Umma
Utekelezaji unategemea
barua kuandikwa kutoka
WAUJ kwenda WHO
Imeandaliwa na:

Kitengo cha Epidemiolojia na Ufuatiliaji wa Magonjwa

May, 2014

You might also like