You are on page 1of 10

Maelezo Kuhusu Kushuka kwa Thamani ya Shilingi ya

Tanzania kwa Kamati ya Fedha Uchumi na Biashara


a. Utangulizi
1.1

Thamani ya Shilingi kwa Kipindi cha Mwaka 2010 mpaka 2014

Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani katika soko la jumla la fedha za
kigeni (Interbank foreign exchange market-IFEM) ilishuka kutoka shilingi 1,318 kwa dola
moja mwezi Januari 2010 na kufikia kiwango cha shilingi 1,543 kwa dola moja ya Marekani
mwezi Juni 2011. Katika kipindi hicho thamani ya shilingi katika soko la rejareja ilishuka
kutoka shilingi 1,333 kwa dola moja ya Marekani na kufikia shilingi 1,547 kwa dola.
Kushuka kwa thamani ya shilingi kulichangiwa na mfumuko mkubwa wa bei pamoja na
mauzo hafifu nje ya nchi hasa kufuatia mdororo wa uchumi duniani.
Thamani ya shilingi ilishuka kwa kasi zaidi kati ya mwezi Juni 2011 hadi Oktoba 2011
kufuatia baadhi ya washiriki wa soko la fedha za kigeni kucheza kamari/kufanya biashara ya
dola kwa lengo ya kujinufaisha (speculation). Kufuatia hali hii, hatua mbalimbali
zilichukuliwa na Benki Kuu ikiwa ni pamoja na kuongeza viwango vya akiba ambavyo
mabenki yanatakiwa kuhifadhi Benki Kuu (SMR) kutoka asilimia 20 mpaka asilimia 40 kwa
amana za serikali; kupunguza kiwango cha fedha za kigeni ambazo mabenki yanaruhusiwa
kubaki nazoambazo zinaweza kutumika kutafuta faida kwa miamala ya fedha za kigeni
(net open position, NOP)kutoka asilimia 20 hadi asilimia 10 na hatimaye asilimia 7.5.
Benki kuu pia iliongeza kiwango cha mauzo ya fedha za kigeni kwenye soko la jumla.
Kufuatia juhudi hizo, thamani ya shilingi iliimarika tena na kubaki tulivu kwa takribani
miaka mitatu hadi kufikia robo ya mwisho ya mwaka 2014 (Jedwali Na. 1 na Chati Na. 1a
& 1b).

Chati Na 1a: Wastani wa Mwenendo wa Thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya


Marekani

Chati Na 1b: Wastani wa bei ya dola kwa shilingi - soko la jumla

Kama inavyoonekana katika Chati Na. 2 hapo chini, thamani ya shilingi ilipungua kwa
wastani wa asilimia 8.6 kwa mwaka kati ya Januari 2010 hadi Mei 2011. Baada ya hapo kasi
ya kushuka thamani ilipanda hadi wastani wa asilimia 11.7 kwa mwaka kati ya Juni 2011
hadi Novemba 2011. Kutokea Desemba 2011 hadi Septemba 2014 thamani ya shilingi ilitulia
ambapo ilipungua kwa wastani wa asilimia 1.8 kwa mwaka.

Chati Na. 2: Mwenendo wa Thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani

b. Thamani ya shilingi kwa kipindi cha Machi 2014 hadi


Machi 2015
Katika kipindi cha Machi 2014 hadi Machi 2015, thamani ya shilingi ilishuka kwa asilimia
9.6 katika soko la jumla na asilimia 13.0 katika soko la rejareja (Jedwali Na. 1). Kushuka
huku kulitokana zaidi na kuimarika kwa uchumi wa Marekani. Kuimarika kwa uchumi wa
Marekani kumefananya wawekezaji wengi duniani kuwekeza zaidi Marekani na hivyo
kuongeza mahitaji ya dola ya Marekani. Kwa sababu hiyo sarafu za nchi nyingi duniani pia
zimeshuka thamani dhidi ya dola ya Marekani kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 2.
Baadhi ya sarafu hizo kama vile Euro ya Ulaya, Pauni ya Uingereza, Yen ya Japan, Shilingi
ya Uganda, na Rand ya Afrika Kusini, zimeshuka kwa kasi zaidi ya shilingi ya Tanzania.

Jedwali Na. 1: Mwenendo wa Thamani ya Shilingi dhidi ya dola ya Marekani


Machi 2014

Machi 2015

Badiliko

Soko la jumla (IFEM)

1,629.6

1,786.3

9.6%

Soko la rejareja (bureau-mean rate)

1,631.9

1,844.5

13.0%

Jedwali Na 2: Mwenendo wa Thamani za Sarafu Mbalimbali dhidi ya Dola ya


Marekani
Tanzanian Shilling
Great Britain Pound
Euro
Japanese Yen
Indian Rupee
Kenyan shilling
Ugandan Shilling
South African Rand
2.1

Machi 2014
1,629.60
0.60
0.73
103.27
59.97
86.55
2,588.73
10.57

Machi 2015
1,786.30
0.68
0.93
119.86
62.50
92.40
3,030.32
12.18

Badiliko
9.62%
12.65%
28.27%
16.07%
4.23%
6.76%
17.06%
15.26%

Sababu nyingine za kushuka kwa thamani ya shilingi kwa kipindi


cha Machi 2014 hadi Machi 2015

2.1.1 Kupungua kwa kasi ya upatikanaji wa dola nchini ukilinganisha na


mahitaji

Upatikanaji wa dola nchini umepungua kutokana na sababu mbalimbali kama


zinavyoainishwa hapa chini:
Kupungua kwa mapato ya mauzo nje ya nchi
Mapato yanayotokana na mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi yamekuwa yakiongezeka
kwa kiasi kidogo ukilingalisha na mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya kununua bidhaa na
huduma kutoka nje ya nchi. Kwa kipindi cha mwaka unaoishia Machi 2015, mauzo ya bidhaa
na huduma nje yalifikia dola za Marekani milioni 9,355.5 ukilinganisha na uagizaji wa
bidhaa na huduma kutoka nje ambao ulikuwa na thamani ya dola za Marekani milioni
13,456.9.
Eneo mojawapo ambalo mapato yake yamepungua ni mauzo ya dhahabu kutokana na
kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia na kupungua kwa uzalishaji wa dhahabu
nchini. Uzalishaji wa dhahabu ulipungua katika kipindi hicho kutokana na kufungwa kwa
baadhi ya migodi kama Tulawaka na Resolute. Kwa mwaka unaoishia Machi 2015, mapato
kutokana na dhahabu yalishuka hadi dola za Marekani milioni 1,377.2 kutoka milioni 1,588.9
zilizopatikana katika mwaka ulioishia Machi 2014. Hali hii imepunguza ahueni ambayo

ingeweza kupatikana kutokana na ongezeko la mauzo ya bidhaa za viwandani pamoja na


utalii.

Chati Na. 3: Mwenendo wa Mauzo ya Dhahabu Nje ya Nchi kwa Mwaka Unaoishia
Machi (Dola Million)

Ucheleweshwaji wa fedha kutoka kwa wahisani na mikopo ya kibiashara toka nje ya


nchi
Kuanzia robo ya pili ya mwaka 2014/15, wahisani hawakutoa fedha za kigeni kama
ilivyokuwa imetarajiwa. Katika kipindi cha robo tatu za kwanza za mwaka 2014/15 fedha za
wahisani zilizopokelewa zilikuwa dola za Marekani milioni 122 ikilinganishwa na makisio ya
dola za Marekani milioni 473.7. Hali hii imechangia katika upungufu wa fedha za kigeni
nchini na pia kuleta hisia ya kuwepo kwa uhaba katika soko la fedha za kigeni.
Katika mwaka 2014/15, serikali ilitarajia kupokea mikopo ya kibiashara kutoka nje yenye
thamani ya dola za Marekani milioni 800, lakini hadi mwezi Machi 2015 mikopo yenye
thamani ya dola milioni 310 tu ndiyo iliyokuwa imepatikana. Hali hii pia imechangia
upungufu wa fedha za kigeni nchini.

Chati Na. 4: Mwenendo wa Upatikanaji wa Fedha za Kigeni kwa Bajeti

Msimu wa mapato madogo (low-season) yatokanayo na utalii na bidhaa za kilimo


Kipindi cha mwezi Januari hadi Aprili ni msimu wa mapato madogo yatokanayo na bidhaa za
kilimo na utalii hali ambayo inachangia upungufu wa dola kwenye soko. Ni matarajio
kwamba hali hii itabadilika katika kipindi cha mwezi Mei hadi Septemba wakati wa msimu
wa utalii na mavuno ya kilimo.
Kuongezeka kwa malipo ya serikali nje ya nchi (foreign government obligations)
Malipo ya serikali nje ya nchi yameongezeka katika mwaka wa fedha 2014/15 yakijumuisha
yale ya mashirika ya umma kama TANESCO na TRL.

Chati Na. 5 Malipo ya serikali kwa dola

c. Thamani ya shilingi kwa kipindi cha mwezi April 2015


Katika mwaka ulioshia Machi 2015, shilingi ilishuka thamani kwa asilimia 13.0. Hata hivyo
kwa mwezi April 2015, kasi ya kushuka thamani iliongezeka ambapo shilingi ilishuka
thamani kwa asilimia 8.0 ndani ya mwezi mmoja tu (Jedwali Na.3).

Jedwali Na. 3: Mwenendo wa thamani ya Shilingi dhidi ya sarafu mbalimbali


(badiliko kwa asilimia)
Mar-14 to Mar 15

31st Mar-15 to 29th Apr-15

13.0
1.5
-11.7
-4.2
10.1
6.2
-3.2
0.3

8.0
12.6
12.0
9.1
6.7
5.5
7.8
11.2

US dollar
Great Britain Pound
Euro
Japanese Yen
Indian Rupee
Kenyan shilling
Ugandan Shilling
South African Rand

Sababu za kushuka thamani kwa kasi:


7

Shortage psychologyna speculation (hisia za upungufu)


Taharuki iliyoletwa na hisia za upungufu katika soko zimesababisha ongezeko la mahitaji ya
dola hata kwa wale ambao hawana mahitaji ya kimsingi ya dola. Aidha wengine wanafanya
biashara/kamari ya dola kwa malengo ya kujinufaisha na mabadiliko ya thamani
(speculation).
Wasiwasi unaohusiana na uchaguzi (uncertainty)
Katika nchi nyingi ambazo zimekuwa na historia ya matukio hatarishi wakati wa uchaguzi;
wawekezaji na wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kuhamisha kwa muda mali/fedha zao
nje ya nchi wakisubiri matokeo ya uchaguzi. Katika nchi hizo kumekuwa na tabia ya baadhi
ya watu kuhamisha familia zao kwenda kusubiri matokeo nje ya nchi. Hii imesababisha
ongezeko la mahitaji ya fedha za kigeni ili kukamilisha uhamisho huo. Takwimu za illicit
flows mara nyingi zinaonyesha kuongezeka kwa kasi ya uhamishaji huo katika kipindi cha
uchaguzi. Ingawa kwa Tanzania, matukio mabaya yanayohusiana na uchaguzi ni nadra,
takwimu za illicit flows zinaonyesha kuwepo kwa uhusiano na election cycles. Kuna
uwezekano mkubwa kuwa sehemu ya taharuki inayohusisha uhamishaji wa fedha za kigeni
imechangia kuongezeka kwa mahitaji.

d. Madhara ya kushuka kwa thamani ya shilingi


i.

Kupanda kwa bei za kuagiza bidhaa nje (import bill) na hivyo kusababisha mfumuko

ii.

wa bei (imported inflation).


Kuongezeka kwa mzigo wa malipo ya mikopo ya nje kwa mikopo ya serikali na ya

iii.

sekta binafsi.
Wasiwasi wa uchumi kwenda mrama unaweza kupunguza uwekezaji.

Wapo Walionufaika:
i.

Wanaouza bidhaa nje wanapata shilingi nyingi zaidi kwa kila dola. Kwa mfano
kwenye biashara ya utalii, wauzaji mazao ya kilimo, bidhaa za viwanda, madini na

ii.

kadhalika nje ya nchi.


Wanaopokea fedha toka kwa jamaa zao nje (remittances).

iii.

Kuongezeka kwa mapato ya serikali yatokanayo na kodi za bidhaa na huduma kutoka


nje (ushuru wa forodha) pamoja na misaada na mikopo kutoka nje.

e. Matarajio na hatua zinazochukuliwa


Kwa kipindi kijacho mambo makubwa matatu yatasaidia kupunguza kasi ya kushuka kwa
thamani ya shilingi:
i.

Kuanza kwa msimu wa mapato ya utalii mwezi Mei 2015 ambapo inatarajiwa kuongeza
mapato yanayotokana na shughuli za utalii nchini. Mapato yatokanayo na mauzo ya
bidhaa za kilimo nje ya nchi nayo yanatarajiwa kuongezeka kuanzia mwezi Agosti
2015.

ii.

Kutolewa kwa fedha za wahisani (World Bank na AfDB) na kupatikana kwa mikopo
yenye masharti ya kibiashara (ENCB). Matarajio yetu ni kwamba fedha hizo kutoka nje
zitaingia kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha 2014/15. Hali hii itaongeza upatikanaji
wa fedha za kigeni.

iii.

Mategemeo ya kutengemaa kwa uchumi wa ukanda wa Euro na kuimarika kwa uchumi


wa nchi za Ulaya. Hii itaongeza mahitaji ya bidhaa kutoka Tanzania.

Hatua zinazochukuliwa na Benki Kuu


Benki Kuu ya Tanzania inaendelea kuchukua hatua mbalimbali, hasa za utekelezaji wa sera
za fedha ili kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania.
i.

Benki Kuu imeongeza mauzo yake ya dola kwenye soko la jumla. Katika kipindi cha
Januari hadi Aprili 2015, Benki Kuu imeuza dola milioni 339 katika IFEM, takriban
sawa na kiasi kilichouzwa kipindi kama hicho mwaka 2014, ingawa malipo nje ya nchi
yalizidi yale ya mwaka 2014 kwa zaidi ya dola za milioni 300.

ii.

Kupunguza ujazi wa fedha katika uchumi ili kudhibiti kasi ya ukuaji wa miamala katika
soko la fedha za kigeni. Hii ikiwa ni pamoja na kuongeza SMR ili kupunguza uwezo wa
mabenki kutumia zaidi fedha walizonazo kufanya miamala katika IFEM ili
kujinufaisha.

iii.

Kudhibiti biashara za fedha za kigeni


a. Swaps: Benki Kuu imeongeza maturity
b. Net Open Position (NOP)- Kupunguza kiwango cha fedha za kigeni ambazo
mabenki wanaruhusiwa kubaki nazo ambazo zinaweza kutumika kutafuta faida
kwa miamala ya fedha za kigeni.

Matarajio ya mwelekeo wa thamani ya Shilingi


Kasi ya kushuka kwa thamani ya Shilingi inatarajiwa kupungua katika siku zijazo kutokana
na hatua zinazoendelea kuchukuliwa kama ilivyotokea mwaka 2011.

10

You might also like