You are on page 1of 6

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012 1.0 UTANGULIZI Mtihani wa Kidato cha Nne, 2012 ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8/10-25/10/2012. Baraza la Mitihani la Tanzania katika kikao chake cha 94 kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2013 liliidhinisha matokeo haya 2.0 USAJILI NA MAHUDHURIO Jumla ya vituo 5,058 vilitumika katika kufanya mtihani huo ikilinganishwa na vituo 4,795 vilivyotumika mwaka 2011. 2.1 Taarifa za Watahiniwa

Jumla ya watahiniwa 480,029 walisajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,587 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,442 sawa na asilimia 54.67. Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ni 458,139 sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa 21,890 sawa na asilimia 4.56 ya watahiniwa wote waliosajiliwa, hawakufanya mtihani. 2.2 Watahiniwa wa Shule

Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 411,225 wakiwemo wasichana 182,982 sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,243 sawa na asilimia 55.50. Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani walikuwa 397,138 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,087 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ugonjwa na vifo. 2.3 Watahiniwa wa Kujitegemea

Watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,804 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia 50.30 na wavulana 34,199 sawa na asilimia 49.70. Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,918 na wavulana 30,083 wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,803 sawa na asilimia 11.34 hawakufanya mtihani.

3.0

MATOKEO YA MTIHANI

3.1

Maandalizi ya matokeo

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yalitangazwa tarehe 18 Februari 2013 na kufutwa Machi 2013 kutokana na sababu za kitaalamu katika matumizi ya taratibu za kuchakata matokeo. Matokeo yaliyofutwa yalikuwa yamechakatwa kwa kutumia utaratibu wa Fixed Grade Ranges. Matokeo yanayotangazwa sasa yamechakatwa kwa utaratibu huo huo lakini yamefanyiwa Standalization. Kimataifa kuna aina kuu mbili za kuchakata matokeo ya mtihani : Flexible Grade Ranges na Fixed Grade Ranges. Flexible Grade Ranges hutumia viwango tofauti kuchakata matokeo ya watahiniwa kwa kuzingatia kiwango cha ufaulu cha somo husika kwa kila mwaka. Hivyo viwango vya kuchakata matokeo hubadilika kila mwaka kulingana na ufaulu wa watahiniwa kwa kila somo husika. Katika mfumo wa Fixed Grade Ranges viwango vya aina moja hutumika kuchakata matokeo kwa masomo yote bila kujali kiwango cha kufaulu kwa somo husika. Viwango vya kuchakata matokeo hutumika hivyo hivyo kila mwaka bila mabadiliko. Kwa miaka mingi Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likitumia mfumo wa Flexible Grade Ranges. Mwaka 2012, mfumo wa Fixed Grade Ranges ulitumika kuchakata matokeo kwa mara ya kwanza Mabadiliko hayo yalitokana na maoni ya wadau yaliyotokana na utafiti uliofanywa na Wizara mwaka 2010 kufuatia kushuka kwa ufaulu wa mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huo. Pia kwa kuzingatia maelekezo ya Tume maalum iliyochunguza dosari zilizojitokeza kwenye matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2012 katika somo la Islamic Knowledge.

3.2 Matokeo ya Watahiniwa wa Shule Jumla ya watahiniwa wa shule 159,609 kati ya watahiniwa 397,138 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wamefaulu. Wasichana walikuwa ni 60,751 na wavulana walikuwa ni 98,858. 3.3 Matokeo ya Watahiniwa wa Kujitegemea Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 26,191 kati ya watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani. Wasichana waliofaulu ni 11,581 na wavulana ni 14,910. 4.0 UBORA WA UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI

Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 35,349 wamefaulu katika madaraja I III ambapo kati yao wasichana ni 10,924 na wavulana ni 24,425.

Mchanganuo wa ufaulu kwa kila daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo: Wavulan a Idadi 2,179 7,267 14,979 24,425 74,433 98,968 104,259 Wasicha na Asilimia 1.07 3.58 7.37 12.02 36.65 48.66 51.33 Jumla Idadi 1,063 3,088 6,773 10,924 49,827 60,779 106,587 0.64 1.85 4.05 6.54 29.78 36.30 53.7 Asilimia 3,242 10,355 21,752 35,349 124,260 159,747 210,846

Daraja I II III I-III IV I-IV 0

5.0

SHULE KUMI BORA NA SHULE KUMI ZA MWISHO Ubora wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha Grade Point Average (GPA) kuanzia A = 1 na F = 5. Shule zimegawanywa katika makundi mawili kulingana na idadi ya watahiniwa kama ifuatavyo:

(i) (ii)

Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi (Jumla ni 3,396) Shule zenye watahiniwa pungufu ya 40 (Jumla ni 753). 5.1 Shule Kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi

Shule zifuatazo zimepangwa kwa kuanza na ya kwanza hadi ya kumi katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi.

NAFAS I RANK 1

JINA LA SHULE CENTRE NAME ST. FRANCIS GIRLS S S

IDADI REGIS TERED 90

MKOA REGION MBEYA

2 3 4 5 6 7 8 9 10

MARIAN BOYS' S S FEZA BOYS' S S MARIAN GIRLS S S CANOSSA S S FEZA GIRLS' S S ROSMINI S S ANWARITE GIRLS S S ST. MARY'S MAZINDE JUU S S JUDE MOSHONO SS

75 69 88 66 50 78 49 83 51

PWANI DAR ES SALAAM PWANI DAR ES SALAAM DAR ES SALAAM TANGA KILIMANJARO TANGA ARUSHA

5.2 Shule Kumi za mwisho zenye watahiniwa 40 na zaidi Shule zifuatazo zimepangwa kwa kuanza na ya kwanza hadi ya kumi kutoka mwisho. NAFA SI 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 JINA LA SHULE MIBUYUNI S S MAMNDIMKONGO S S CHITEKETE S S KIKALE S S ZIRAI S S MATANDA SECONDARY SCHOOL KWAMNDOLWA S S CHUNO S. S MBEMBALEO S S MAENDELEO S S IDADI 40 63 57 60 41 53 89 143 56 103 MKOA LINDI PWANI MTWARA PWANI TANGA LINDI TANGA MTWARA MTWARA DAR ES SALAAM

5.3

Shule Kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 40

Shule zifuatazo zimepangwa kwa kuanza na ya kwanza hadi ya kumi katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi.

NAFAS I 1 2 3

JINA LA SHULE THOMAS MORE MACHRINA SS S QUEEN OF APOSTLESUSHIROMBO SEMINARY BETHELSABS GIRLS S S

IDADI 20 24 33

MKOA DAR ES SALAAM SHINYANGA IRINGA

4 5 6 7 8 9 10

PRECIOUS BLOOD S S MAUA SEMINARY ST. MARY'S JUNIOR SEMINARY CARMEL S S SANU SEMINARY BROOKEBOND S S ST.CAROLUS SECONDARY S S

34 31 28 36 37 27 37

ARUSHA KILIMANJARO PWANI MOROGORO MANYARA IRINGA SINGIDA

5.4 Shule kumi (10) za mwisho zenye watahiniwa chini ya 40 Shule zifuatazo zimepangwa kwa kuanza na ya kwanza hadi ya kumi kutoka mwisho. NAFAS I 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 JINA LA SHULE DODEANI TECH. S S KALAMBA S S HURUI S S USUNGA S S MANDWANGA S S BETTY MITCHEL S S CHONGOLEANI S S MMULUNGA S S NYUAT S S MWAKIJEMBE S S IDADI 10 11 12 13 13 17 17 17 20 13 MKOA PEMBA DODOMA DODOMA TABORA LINDI MOROGORO TANGA MTWARA ARUSHA TANGA

6.0.

HITIMISHO

Kuanzia sasa matokeo ya mithani ya kidato cha Nne na Sita yatachakatwa kwa kutumia Fixed Grade Range na Standardisation. Natoa wito kwa wadau wote wa elimu kutoa ushirikiano tuweze kuboresha elimu nchini.

7.0.

KUANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012 Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE), 2012 yanapatikana katika tuvuti zifuatazo : www.matokeo.necta.go.tz www.necta.go.tz www.udsm.edu.ac.tz, au www.moe.go.tz

Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (Mb) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi 30/5/2013

You might also like