You are on page 1of 2

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail:
ikulucommpress@googlemail.co
m
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENTS OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA
ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Mheshimiwa Ali Nasoro Rufunga kuomboleza vifo vya watu 38 huku
wengine 82 wakijeruhiwa usiku wa kuamkia tarehe 4 Machi, 2015.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika Kata ya Mwakata iliyoko katika
Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kufuatia mvua kubwa ya mawe
iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali, hivyo kuathiri watu 3,500. katika Kata
Mwakata iliyoathiriwa zaidi, kaya 350 zimeathiriwa katika Kijiji cha Makata
wakati katika Kijiji cha Ngumbi, kaya 100 zimeathirika. Katika Kijiji cha
Magunghwa, kaya 50 zimeathiriwa..
Nimepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya
watu 38 waliopoteza maisha na wengine 82 waliojeruhiwa na kukimbizwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa matibabu baada ya nyumba zao
kusombwa kabisa na maji kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana
na upepo mkali kunyesha, amesema Rais Kikwete akiomboleza msiba huo.
Rais Kikwete amesema msiba huo siyo wa Wana-Shinyanga pekee bali ni
wa Taifa zima ambalo limepoteza nguvukazi muhimu kwa maendeleo yake na
ustawi wa jamii ya Watanzania kwa ujumla.
Naomba upokee Salamu zangu za Rambirambi kutoka dhati ya moyo
wangu kwa kupotelewa ghafla na wananchi 38 kwa mara moja katika Mkoa
wako. Kupitia kwako naomba Rambirambi zangu na Pole nyingi ziwafikie
wafiwa wote kwa kuondokewa na wapendwa, ndugu na jamaa zao.
Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema azipokee na kuzilaza Roho

za Marehemu wote Mahala Pema Peponi, Amina, amezidi kuomboleza Rais


Kikwete katika Salamu zake.
Rais Kikwete amewaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu,
utulivu na subira wakati huu wa majonzi makubwa kwao wanapoomboleza vifo
vya ndugu na jamaa zao, lakini amewataka wasisahau ukweli kwamba kazi ya
Mungu haina makosa. Aidha amewahakikishia wafiwa wote kuwa binafsi yuko
pamoja nao katika kipindi chote cha kuomboleza msiba huu mkubwa kwao na
kwa Taifa.
Namwomba Mola awawezeshe majeruhi wote wa tukio hilo wapone
haraka ili waweze kuungana tena na familia, ndugu na jamaa zao na kuendelea
na maisha yao kama kawaida, amemalizia kusema Rais Kikwete katika Salamu
zake za Rambirambi.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
04 Machi, 2015

You might also like