You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

Simu: +255-26-232-2484/232-4560 Mlimwa Kusini,


11 Barabara ya Edward Sokoine,
Nukushi: +255-26-232-1955, S. L. P. 980,
Barua-pepe: pm@pmo.go.tz 41193 – Dodoma,
Tovuti: www.pmo.go.tz Tanzania.

31 Machi, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


WAZIRI MKUU AWAOMBA VIONGOZI WA DINI WAPIGANIE NA
KUILINDA AMANI
*Asisitiza mapambano dhidi ya viashiria vya uvunjifu wa amani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini popote walipo


wahakikishe wanaipigania na kuilinda amani kwa kila hali ikiwa ni pamoja na
kupambana na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Machi 31, 2018) kwenye Mkutano
Mkuu wa BAKWATA uliofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma,
ambapo amesisitiza kuwa ni muhimu wasaidizi wa Mufti wakasimamia suala hilo.

“Dini ni taasisi muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku ndio maana Serikali
inaheshimu na kuzitambua dini zote kutokana na mchango wake mkubwa katika
amani ya nchi yetu. Niwaombe viongozi wangu popote mlipo muilinde amani yetu”

Waziri Mkuu amesema amani ni miongoni mwa neema kubwa sana kwa binadamu
na ndio maana wote wanamtambua Mwenyezi Mungu, hivyo wasiruhusu mtu au
kikundi chochote kujaribu kuchafua na kuharibu amani iliyopo nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi Baraza Kuu la


Waislamu Tanzania (BAKWATA) wahakikishe kuwa chombo hicho kinaendelea
kuwaunganisha waislamu bila ya kujali makabila yao, rangi zao au madhehebu
yao.

Waziri Mkuu amesema Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar bin Zubeiry ambaye
ndiye kiongozi wa Waislamu nchini mara zote amekuwa akisisitiza jambo hilo na
kuwataka waislamu popote walipo watambue kuwa hicho ni chombo chao.

1
“Ni muhimu sana kwa ninyi wasaidizi wa Mufti mlio kusanyika hapa muhakikishe
mnalisimamia hili katika maeneo yenu. Katika hili napenda kuwahakikishia kuwa
Serikali yenu iko pamoja Mheshimiwa Mufti kutekeleza nia hiyo njema.”

Amesema ahadi ya Rais Dkt. Magufuli ni kuwa Serikali anayoiongoza ipo tayari
kusikiliza maoni, ushauri na mapendekezo yeyote kutoka kwa viongozi wa dini .
‘Milango iko wazi saa zote ‘

Ameongeza kuwa yeye si mtaalamu sana kama walivyo Masheikh hao lakini
anakumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu ndani ya Qur’ani sura Al Imran aya ya
103 yanayosema “ Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala
msifarakane”

Mkutano huo umehudhuriwa na Sheikh Mkuu wa Mufti wa Tanzania Sheikh


Zubeir, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, wajumbe wa Baraza la Ulamaa,
Masheikh na viongozi wa BAKWATA wa mikoa na wilaya zote Tanzania.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, MACHI 31, 2018.

You might also like