You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA


SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU
MWAKA 2015/16

JIHADHARI NA MATAPELI

Kumekuwepo na Tangazo la upotoshaji kuhusu Ajira ya walimu


wapya kwa mwaka 2015/16 (TANGAZO No. T.022/15TMS 2015)
linalodaiwa kuwa limetolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi na kusambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii. Taarifa
zilizotolewa katika tangazo hilo siyo za kweli na Wizara haihusiki
nazo.
Aidha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inapenda
kuufahamisha umma kuwa ajira ya Walimu wa ngazi ya Cheti,
Stashahada, na Shahada hufanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Ajira kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi haihusiki moja kwa moja na zoezi hilo.
Kutokana na mgawanyo wa majukumu ya Wizara mbalimbali, taarifa
sahihi kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka huu wa fedha
zitatangazwa na Mamlaka inayohusika yaani Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI mara watakapokamilisha taratibu zinazotakiwa.

Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
23 Machi, 2015

You might also like