You are on page 1of 1

Ungana na Simon Kivamwo kupambana na Kansa ya Utumbo

mara kutokana na maumivu makali ya


tumbo!

Ndugu Marafiki,
Baadhi yenu mnafahamu kwamba ndugu
na rafiki yetu, Adolf Simon Kivamwo,
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa
Habari za UKIMWI Tanzania (AJAAT), ni
mgonjwa na anasumbuliwa saratani ya
utumbo mpana toka mwaka 2012.
Tangu wakati huo, amekuwa akitibiwa na
kuhudhuria matibabu na kliniki katika
Taasisi ya Saratani Ocean Road (OCRI).
Wataalamu wa tiba ya saratani wanamtibia kwa dawa mchanganyiko dawa tofauti
kwa mtindo wa chemotherapy. Tiba hizo
zinalenga kudhibiti kasi ya kuenea kwa
ugonjwa kwa kushauriana na mgonjwa.
OCRI ni taasisi inayoendeshwa na serikali
inatoa tiba ya saratani bila malipo kwa
wagonjwa. Hata hivyo, kutokana na
uhaba wa rasilimali, taasisi hiyo inapokea
kiasi kidogo au kutopokea dawa muhimu
kutoka Bohari ya Dawa ya Serikali
(Medical Stores Department - MSD). Hali
hiyo ni jambo la kawaida kwenye hospitali
za serikali. Kutokana na hali hiyo,
wagonjwa wanalazimika kununua dawa
kwenye maduka binafsi na kuzipeleka
OCRI kwa ajili ya tiba.
Hiyo ndiyo sababu Simon amekuwa
akitumia wastani wa Tshs 500,000/ -

(laki tano) kwa wiki kwa ajili ya kununua


dawa za tiba za chemotherapy. Amefanya
hivyo kwa kuuza mali zake na kutokana
na michango ya marafiki kwani hana bima
ya afya kugharamia matibabu yake.
Ni miaka mitatu sasa hali yake ya afya si
ya kuridhisha. Afya yake imezidi kudhoofu
siku baada ya siku. Na sasa hawezi
kufanya shughuli zake mwenyewe kwani
muda mwingi hulala nyumbani kwake
Mbezi na kuhudhuria matibabu Ocean
Road kila baada ya wiki mbili.
Kwa bahati mbaya, Simon amekuwa
akikatisha dozi za tiba kwa kukosa fedha!
Ugonjwa huo umekuwa ukimshambulia
kwa kumsababishia maumivu makali, hali
inayomfanya kulazwa hospitali mara kwa

Baada ya kugundua mwenzetu Simon


anateseka akiugulia kitandani, sisi
marafiki zake wengi ambao ni wana
habari kupitia mtandao wa Facebook
tumekuwa tukipeana taarifa za maendeleo ya afya yake na kuendesha mchango
wa kumsaidia. Michango hiyo ndiyo
ilimwezesha kurejea kwenye matibabu
Ocean Road, ambapo madaktari walimtaka pia afanye vipimo vya CT-Scan katika
hospitali binafsi ili kuangalia ukubwa wa
tatizo lilivyo. Michango hiyo iligharamia
CT-Scan.
Sambamba na michango, pia tulianza
jitihada za kuwasiliana na viongozi
serikalini ili kutafuta uwezekano wa
kumpeleka nchini India kwa ajili ya
matibabu. Wizara ya afya iliahidi kutoa
ushirikiano endapo maoni na ushauri wa
wataalamu wa OCRI ungeridhia hilo.
Sasa majibu ya vipimo vya CT Scan
yamepatikana na imeshauriwa kwamba
kwa sasa si busara kumpeleka India,
kwani anapaswa kuendelea kwanza na
dozi ya chemotherapy ambayo aliikatiza.
Na hivyo atalazimika kupata dozi 10 za
Chemotherapy, kuanza tarehe 20,
ambapo atakuwa akipata dawa hizo kila

baada ya wiki mbili.Mpakakumalizika


kwamzunguko tutahitaji jumla ya shilingi
shilingi milioni 5.
Hii ndiyo sababu tunaandika kwenu
wadau na marafiki kuomba msaada wa
fedha. Huu ni msaada mkubwa kwa
Simon Kivamwo aliyewahi kufanya kazi
akiwa mwandishi wa habari katika Kampuni ya The Guardian Limited kabla ya
kuanzisha AJAAT. Na kama inavyojulikana,
AJAAT ni moja ya mdau muhimu katika
mwitikio wa UKIMWI kupitia kwa mafunzo
kwa waandishi kuhusu uandishi sahihi wa
habari na makala za UKIMWI. Kivamwo
amejitolea kwenye hili maisha yake yote,
japo yeye mwenyewe haishi na virusi vya
UKIMWI.
Tunaomba mchango wako ndugu na
rafiki yetu. Tuma mchango kwa namba hii:
Simon Kivamwo0767300219.
Kwa Mawasiliano zaidi kuhusu mgonjwa
karibu:
Benjamin Thompson
Email:benjathom@gmail.com
Simu,Whatsapp, sms au piga simu:
0787303067/0767383067

You might also like