You are on page 1of 6

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA


ISO 9001:2008 CERTIFIED

Ndugu Waandishi wa Habari;


Tumewaita hapa leo ili tuwapatieni taarifa ya utekelezaji wa mpango wa
kuzuia simu bandia za kiganjani zisitumike kwenye mitandao ya simu hapa
nchini.
Kama ambavyo mnakumbuka, usiku wa tarehe 16 Juni 2016 simu bandia
zilizuiwa kutumika katika mitandao ya simu. Maagizo ya Serikali kuzuia
matumizi ya simu bandia kwenye mitandao ni sehemu ya mpango wa
kuanzishwa kwa rajisi kuu ya Namba Tambulishi za simu za mkononi, kwa
kifupi CEIR ambayo ni Central Equipment Identification Register.

Uthibiti wa matumuzi ya simu katika mitandao ya mawasiliano kunatokana


na kuongezeka kwa umuhimu wa simu na vifaa vya mkononi vya
mawasiliano

kama

nyenzo

muhimu

kimaisha,

kijamii,

kiuchumi,

na

kiusalama.
Vifaa vya mkononi vya mawasiliano ambavyo vinatumia laini ya simu, yaani
SIM card kuwasiliana vina namba maalum inayoitambulisha, ambayo inaitwa
IMEI kifupisho cha International Mobile Equipment Identity.
Mfumo wa Rajisi kuu ya Namba Tambulishi ni wa kielektroniki na unahifadhi
kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi
(IMEI). Lengo la Rajisi ni kufuatilia namba tambulishi za vifaa vinavyoibiwa,
kuharibika, kupotea au ambavyo havikidhi viwango (bandia) vya matumizi
katika soko la mawasiliano.
1

Kuanzishwa kwa Mfumo wa Rajisi kuu ya Namba Tambulishi kunatokana na


matakwa ya kisheria, ikiwemo masharti ya vifungu vifungu vya 84 hadi 90
vya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni za
Namba Tambulishi (Central Equipment Identity Register) za

mwaka 2011.

Sheria na Kanuni vinaipa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania nguvu ya


kusimamia kwa karibu vifaa vya kielektroniki vya mawasiliano vyenye namba
tambulishi.

Sheria na Kanuni hizi zinawataka watoa huduma za simu za kiganjani kuwa


na Mfumo wa ndani wa Rajisi ya Namba za Utambulisho wa simu za kiganjani
yaani Equipment Identity Register kwa kifupi EIR katika mitandao yao.
Mifumo hii imeunganishwa na Rajisi Kuu iliyoko hapa TCRA.
Aidha Sheria inawataka watumiaji kusajili IMEI za vifaa wanavyotumia.
Mfumo huu una faida zifuatazo:

Kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu, kwani simu


zote za kiganjani zitakuwa zinajulikana;

Kuzuia matumizi ya simu zisizokuwa na viwango hivyo kuepuka


madhara yatokanayo na simu zisizokuwa na ubora stahiki;

Kuthibiti wizi wa simu. Iwapo mtu atapoteza au ataibiwa simu ya


kiganjani na akatoa taarifa kwa mtoa huduma, simu hiyo tafungiwa
isiweze kutumika kwenye mtandao mwingine wowote wa simu za
kiganjani;

Kuhimiza utii wa sheria: Kifungu cha 128 cha EPOCA kinamtaka


mtumiaji wa simu kutoa taarifa ya kupotea au kuibiwa kwa simu au
laini ya simu. Kifungu cha 134 kinayataka makampuni ya simu
kutokutoa huduma kwa simu ambayo imefungiwa kama ilivyoelezwa
hapo juu.

Kujenga misingi ya matumizi ya simu halisi, zisizo bandia. Mtumiaji


ataweza kutambua iwapo simu aliyo nayo inakidhi viwango, ni halisi
na sio bandia.Hii pia itatoa fursa kwa wateja wa simu za kiganjani
kupata bidhaa inayolingana na pesa walizotoa kununulia simu hizo.

Uzimaji wa Simu
Usiku wa manane tarehe 16 Juni, 2016 simu ambazo zilikuwa hazina viwango
(bandia) zilizimwa kwa kuzingatia uchambuzi wa kina uliofanyika ili kubaini
namba tambulishi ambazo hazikuwa na viwango. Namba tambulishi ambazo
zilikuwa hazina viwango ilikuwa ni asilimia 2.96 ya simu zilizokuwa
zinatumika kwenye mitandao ya makampuni ya simu hapa nchini. Simu
zilizokuwa na namba tambulishi ambazo zimenakiliwa, yaani duplicates
zilikuwa asilimia 0.09 na asilimia 96.95 ilikuwa ni idadi ya namba tambulishi
za simu halisi (genuine).
Hadi kufikia sasa idadi ya namba tambulishi ambazo hazikidhi viwango
zimefikia 1,713,337.
Baada ya kukamilika kwa zoezi la kuzimwa kwa simu zenye namba
tambulishi ambazo hazikuwa za viwango (invalid IMEIS) na namba tambulishi
zilizonakiliwa (Duplicate IMEIs) hadi sasa idadi ya namba tambulishi
zilizonakiliwa ambazo zimezimwa imefikia 117,389.
Uelewa wa wananchi umechangia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha
mpango huu.
Kama mnavyokumbuka, Mamlaka ya Mawasiliano iliratibu na kuendesha
mpango wa elimu kwa umma kuhusu rajisi kuu ya namba tambulishi nchini
kote na kupitia vyombo vya habari kati ya 17 Desemba 2015 na 16 Juni
2016.

Katika kutelekeza mpango huu, tumekumbana na changamoto zifuatazo:

Uaminifu mdogo kwa baadhi ya wauzaji wa simu kwa kutoa punguzo


kwa wananchi ili kuwashawishi kuzinunua simu bandia kwa bei nafuu.
Hata hivyo ni jambo la kutia moyo kwamba wananchi wengi
hawakubali kudanganywa.

Gharama zinazohitajika katika kuwafikia wananchi na kuelimisha ili


waweze kuelewa zaidi juu ya mpango mzima wa kuhakiki simu zao.
Tanzania ni kubwa na hatukuweza kufika kila mahali kutokana na
ufinyu wa bajeti.

Baadhi

ya watumiaji kutokufuata maelekezo ya namna ya kuhakiki

simu zao katika kipindi cha mpito. Kwa mfano, wengi walikuwa
wanakosea kutuma ujumbe wenye Namba tambulishi kwenda 15090.

Baadhi ya watumiaji kuamini kwamba simu bandia ni zile za bei rahisi


au

ambazo

zimenunuliwa

hapa

nchini

na

hivyo

kulalamika

walipofungiwa simu walizonunua kwa bei kubwa na ambazo ni bandia.

Baadhi ya watoa huduma kushindwa kushughulikia malalamiko ya


wateja waliofungiwa simu zao kwa wakati.
Mamlaka

ya

Mawasiliano

Tanzania

inaendelea

kuwakumbusha

watanzania wote kuwa ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa simu


yake ni halisi na sio bandia. Pia wananchi wanakumbushwa kutoshikilia
simu zilizozimwa majumbani na kuzipeleka mahali husika kwa ajili ya
ukusanyaji (disposal).
Vilevile Mamlaka inawakumbusha wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya
mkononi na mafundi simu kuwa ni kosa kubadilisha namba tambulishi za
vifaa vya simu za mkononi (mobile devices). Kwa mujibu wa kifungu cha 127
cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA), mtu yeyote
ambaye anachakachua simu au lani ya simu kwa lengo la kubadilisha
uhalisia wake anatenda kosa ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua

shilingi millioni 30 au kifungo kisichozidi miaka kumi (10) au vyote kwa


pamoja.
Aidha, kifungu cha 135 cha EPOCA kimeweka adhabu ya faini ya shilingi
1,500,000 au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja kwa matu
ambaye anachakachua simu iliyofungiwa.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inatoa wito kwa wale wote wote
wanaofanya

biashara

za

kuingingiza

simu

hapa

nchini

kutoka

nje

wahakikishe kuwa simu wanazoleta zinakidhi viwango, zimehakikiwa kwa


mujibu wa wa Shirika la Viwango Tanzania.
Aidha Mamlaka inawakumbusha kwa mara nyingine kuwa wanapaswa kuwa
na leseni ya Mamlaka ya Mawasiliano kwa mujibu wa Sheria. Hii pia ni kwa
mafundi wote wa simu nchini, wanatakiwa kuanza mchakato wa kupata
leseni ya kutengeneza simu, ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu wa
kuwaorodhesha wanaoleta simu zao kutengenezwa ili kuepuka kuwa sehemu
ya mtandao wa wizi wa simu.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inawashukuru wadau wote walioshiriki
katika kufanikisha Mpango huu. Hao ni pamoja na makampuni ya simu za
mkononi, jeshi la Polisi, Viongozi wa mikoa ambako elimu kwa umma
ilitolewa, vyombo vya habari Tume ya Ushindani (FCC) pamoja na Shirika la
Viwango Tanzania (TBS).
Asanteni.

IMETOLEWA

NA

KAIMU

MKURUGENZI

MKUU,

TANZANIA
4 JULAI, 2016

MAMLAKA

YA

MAWASILIANO

You might also like