You are on page 1of 2

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angela

Kairuki, amesema kimbunga kikubwa zaidi kinakuja cha kukagua vyeti, ambapo
ukaguzi utaelekezwa kwa wauguzi ili kubaini wenye vyeti visivyo halali na feki.

Kairuki ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maaluum aliyasema hayo jijini Dar es
Salaam wakati akizungumza na wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Segerea. Ukaguzi wa vyeti
unaendelea, katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
baada ya kukamilisha ukaguzi wa vyeti vya madaktari tutaenda kukagua vya
wauguzi, alisema.

Alisema katika ukaguzi wao wamebaini kuna madaktari wenye vyeti feki jambo
ambalo ni hatari unajua unaweza kwenda hospitali halafu unashangaa huponi
kumbe unahudumiwa na watu wasio na sifa jambo ambalo ni hatari. Kwenye hili la
vyeti, sitaangalia sura ya mtu hata katika awamu iliyopita familia nyingi
zimeguswa na sasa kimbunga kikubwa zaidi kinakuja.

Alisema wapo wanaomuuliza kwanini hana ulinzi wakati anafanya kazi kubwa na
ya hatari ya kugusa maisha ya watu, lakini yeye anamtegemea Mungu na amejitoa
mhanga, hivyo atapambana na wenye vyeti feki, labda ahamishwe wizara.
Nawaomba tutoe ushirikiano mfano katika uhakiki uliopita watu wengi
walikuwa wakilalamika na tumetoa fursa ya kukata rufaa lakini waliokata rufaa
hata asilimia 10 haifiki.

Kweli watu wengi wana vyeti visivyo halali na wengine vimebadilisha matokeo,
unakuta mtu alipata D anaenda kukitengeneza anabadilisha anajiwekea B au C
ni bora ukabaki na D yako, alisema. Aliwataka wenye vyeti feki kuanza
kujiondoa wenyewe, badala ya kusubiri Serikali kufanya utaratibu wa kuwatafuta
kwa kufanya kazi bila sifa na hivyo kuhatarisha maisha.

Kairuki alisema wenye vyeti feki na watumishi hewa, wamekuwa wakiliingizia


Taifa hasara kubwa ya mabilioni ya shilingi huku baadhi ya watu ambao hawana
sifa wakiwa ofisini, lakini sasa mambo yatabadilika. Alisema Serikali ina nia
njema na kuwataka kumtetea Rais na kumuunga mkono katika harakati zake za
kuhakikisha haki inatendeka na waliopo ofisini ni wale wenye sifa.

Katika ziara hiyo aliyoifanya Kitunda katika Jimbo la Ukonga na Jimbo la Segerea,
Kairuki aliambatana na wabunge wa Viti Maalumu Dar es Salaam wakiwamo
Mariamu Kisanji na Stella Ikupa. Pia alikuwepo Mbunge wa Segerea, Bonnah
Kaluwa na viongozi wa UWT.
CHANZO:HABARI LEO

You might also like