You are on page 1of 21

I: This is an IDI with a teenage mother at korogocho we are starting at eleven fifty

eight, sawa tuanze, ningependa kujua am ningependa unielezee kuhusu wewe


mwenyewe
P: Mimi
I:Mmh
P: Mimi nilpata mimba hii mwaka
I:Mmh, maybe we anza by niambie jina yako na miaka zako
P: Mimi naitwa Rahab, niko na seventeen years nilipata mimba hi mwaka
I:Mmh, mwezi wa ?
P: Mwezi January nikazaa mwezi wa kumi, mwenye alinipea mimbia sijui hadi penye
alienda hadi sahii naishii na mama yangu, lakini mama yangu ananilinda tu
I: Ulikuwa shuleni
P: Eeeeh
I: Ulikuwa which class ?
P: Nilikuwa Form two,ikabidi nimeacha
I:Mmh
P: Juu ya mimba, siezi endelea shule na mimba
I: Okay , huu ni mtoto wako wa kwanza
P:Mmhh
I:Mmh, ilikuaje experience yako na baba mtoto, mlipatana aje
P: Alikuwa tuu mtuu wangu, tulikuwa tunaishi area moja, saa sijui aliendaenda ajee
akapotea
I:Ulimjua for how long
P: For two years
I:Two years saa tuseme ulimjua kama bado ukoo primary
P: Eee
I: Alikuwa mtu mgani kwako?
P: Alikuwa, sii ni ile kutrust mtu,kumtrust, nilikuwa namtrust najua ananipenda haezii
niachaa, lakini mimi sijui vile alinitoka hivyo tuu
I: Mlifikaaa, mlianza kudate mkiwaa, ukiwa na darasa la ngapi
P: Nilikuwa eight
I:Ulikuwa class eight?
P: Eeee
I: Maisha ilikuwaje mkianza na yeye
P: Ilikuwa tuu poa
I: Alikuwa anakutreat aje?
P: Sii kama mtu wake tuu
I: ( laughing) kaa mtu wake inamaanisha?
P: Venye mtu anaezaa kutreat, ni kaa , ushaai pendwa na first love
I:Mmh
P: Nii hivyo
I: Alikuwa first lover wako?
P: Eeeh?
I: Mmmh, huajai kuwa na mpenzi mwingine
P: Nisha, aah sijai
I: Before yeye?
P: Before yeye nilikuwa seven na sikukuwa najua hizoo mambo… ( audio not clear)
I:Mmh, alafu ikakuajee ? sasa
P: Ndio tukakutana
I: Mmekuwa for how long
P: Sii nimekuambia two years
I:Mmh
P: From twenty, from twenty nineteen eeh
I: Mmmh,Saa hizi unafanya
P: Saa hii, kufanya azin kazi, bado bado sijafungua biashara napanga kufungua
I: Okay, so umeniambiaa mmejuana for two years alafuu akikukatiaa ukiwaa class
eight alikukatia ukiwa class eight eeeh
P: Mmh
I: So ukii, hiyo class eight mmekuwaa mmeanza, relationship yenyu ilikuwa inakaa
ajee, ulikuwa unatoka unaenda kumtembelea … (audio not clear)
P: Sindio, nilikuwa namtembela kwake
I: Anaishi karibu na kwenyu?
P: Eeeeh
I:Mmh, hebu nieleze ilikuajee ukajipata sasa na mtoto ?
P: Saa sijui venye alii … (giggling ), unajua akiingianga haujuangii
I:Mmmh
P: Saa sijui ni kaa yeee alijua niko na, mimi nilimwambia nikoo na mimba, kutoka
ajue niko na mimba hajai rudi sijui alienda wapi
I: So ulii, ulimwambia ukoo na mimba na hivyo ndio akapotea
P: Mmmh
I: Ok, kabla tufike hukoo mahali umekuwa na mimba, mlikuwa mnaprotect
P: Protection ?
I:Mmh
P: Eeeh
I: Mara ngapi, ulianza kuhave sex ukiwa unatoshana aje?
P: Form two,
I: Form?
P:Tuseme ni this year nikiingia form two
I: Ndio ulianza kuhave sex
P: Eeeh
I: Ukiwa na yeye form one
P: Aaa
I: Hamhu have sex
P: Mmm
I: So ulihave sex mara ngapi ndio ukapata boll
P: Mara mbili
I:Okay, ya kwanza ulifanyaje
P: Tulitumia protection
I: Ya pili
P: Ya pili alinibembelezaa tukafanya hivyo hivyo
I: Alikubembeleza, mmh mmh ,
P: Ni hivyo tuu
I: Alikubembelezajee hebu take ma through
P: Sii ni ile kuhurumia mtuu akii
I: Mmmh
P: Alisemaa hataki kutumia protection mimi nikamhurumia
I:Unahurumia mtuu ajee
P: ( laughing)
I: Haukuogopa mimba
P: Aaah
I:Mmh
P: Sii nilimwambiaa asimwagee
I:Mmh
P:Lakini wanaumee sijui wanfikirianga na nini
I:Mmh
P: Sijui alitumia vibaya ikaingia
I: So alimwaga ( laughing)… Sasa after kumwaga wewe hukujua unaeza shika
mimba
P: Sikujua, nilijua mwezi wa tatu ikiwa na mwezi mbili
I: Umewai skia kuna hizii apart from umewai skia kuna contraceptives
P: Mmm
I: Haujaiskia, hizi family planning
P: Oooh, Family planning ninishai skia
I:Mmh
P: Saa siii unajua mtu, niliambiwa mtu kaa hadi han mtoto hafai kuweka family
planing
I:Mmh
P: Saa sii unaona sahii nimepata huyu mmoja sahii sii naezaa ekaa
I:Mmh, unatumia
P: Juu inaezaa kuwa… ( auidio not clear)… sana
I: Unatumia yoyote
P:Mmm, alafu hiyo siku nilitumia pills,saa sijui kaa ni kubounce
I: Oooh, so ulikuwa after kutumia nini, after the sex ulienda ukatumia pills ulitumia
gani
P: Before
I: Ulitumia before uu nini
P:Eee
I: uu have sex,
P: Eee
I: Yaani ulikuwa unamezajee unameza sahizoo ukienda ama ulikuwa unameza saa
ngapi
P: Sii imekuwa after thirty minutes saa ni kaa ili zilibounce
I: So ulimeza pills after thirty minutes ukaenda kuhave sex, ok, I think ulikuwa unafaa
kumeza after
P:Lakini iko tuu sawa
I: Atii
P: Iko sawa basi (laughing)
I: Umesema ikoo sawa, aje
P: Mtoto tuu ni wangu
I:Iko saswa mtoto ni wako
P: Mmmh
I:Mtoto mwenyewe hana makosa, so lakini sasa ndio nakuambia just in case ujipate
kwa situation kaa hiyoo,you unaeza… ( audio not clear)
P: After
I: Eeeh, ndio maana utapata zingine zinaitwa morning after,
P: Oooh
I: Morning after pills, So ukisha acess unameza within seventy two hours, lakini saa
hio, saa hapo tulishapita, tulisha sasa wewe ulimeza pills thirty minutes before
ukahave sex ukaenda home ukijua
P: Sina, sina kitu
I: (laughing) usiseme hauna kitu mmmh;, sasa nani alikupatia boll
P: Mm
I: Nani alikupatia boll
P: Boll sii ni huyo mtu wangu tuu
I: Unaeza sema ni the first
P: Love
I:Ok, how does it feel kukuwa na, kukuwa in love
P: Inakuanga tamu lakini masaa ingine
I: Mmh, ni nini ulipenda about huyo boy
P: Venye alikuwa ananipenda
I; Alikuwa anakufanyia nini
P: Kitu yoyote nikiitisha alikuwa ananipea, lakini after nimekuwa na mimba hawezi
nipea hizo vitu, vijana wanakuanga wajinga tu
I: Unasema wanakuanga wajinga, sasa niambie vile ulifind out uko na mimba
P:Kufind out
I:Mmh
P: Nilikuwa nalala, nimekuambia nimejua after hii mwaka mwezi wa tatu ilikuwa
mwezi mbili,
I:Mmh
P: nilikuwa nalala natapikaa
I:Mmh
P: Nikaenda kununua ilee nini ya kupima, inajiitanga ajee, nikaenda kununua ilee kitu
ya kupima nikajipima
I:Mmh
P:... (audio not clear) Ndio nikajua nikoo na boll
I: Unaishi na nani sahii
P: Mamangu
P: Na babako
I: Mamangu ni single mother
P:Ok babako ako wapi?
I: Sijui
P: Hujai kutana na yeye ama
I: Sijaimpata, venye nilizaliwa sikumpata
P: Hukumpata na unaskia ana exist
I: Eee
P: Unaskia ako arround, lakini hujui ako wapi, mko nwatoto wangapi
I: Tano
P: Watano we ni wa ngapi
I: Tatu
P: Tatu, kuna wawili nyuma yako
I: Eee
P: Vijana ama wasichana
I: Msichana na kijana tena mbele yangu kuna kuijana na msichana
P: Wako wapi?
I: Kwetu tuu, sii tuanaishi nao, lakini wenye wako nyuma wenye nikoo mbele yao
ama nyuma, hao wakubwa
P:Mmh
I: Wanaishi makwao
P: Wanaishi makwao,ni wasichana
I: Msichana na kijana
P: Wameolewaa
I:Msichana ameolewa kijana anjikalisha
P: Anaji?
I: Anajikalisha peke yake
P: Oooh, msichana aliolewa akiwa class
I: Akiwa form three
P: Form three, naa ni watoto wenyu kutoka kwa mamako wote
I: Mmmh, eeee sii ni wa mamangu wote
P: Na hao wenye wanakufuata pia haukluwai ona budako akiwa wakizaliwa
I: Miii niliwapata saa sii nilikuwa mdogo
P: sii umesema wee ni wa tatu
I: Eeee
P: saa sii kuna waa nne wa tano
I: hao wadogo
P: Uliwapata pia
I: sasa mimi sijuiii babangu, sii nilikuwa na kaa na shosho yangu before
P:Okay
I:ndio nikaa Ndio mamangu akanichukua tukaanza kukaa na yeye
P: ulikaaa na shosho yakoo ukiwaa wapii
I: Nilikuwaa mdogo, ama place
P: Eeee
I: kiamichael
P: kiamichael Shosho yako pia anakaaa huku
I:Eeee
P: soo ulishii na yeye kwa mda wa miaka ngapi
I: Nilikuwaa mdogo,nikachukuliwa nikiwa na miaka saba
P:Miaka saba ndio ukaanza kuishii na mamako
I:Mmmm
P: Saa venye ulianzaa kushi na mamako hawa ndugu zako wadogo walikuwaa wapii
I:Sii niliwapata poa
P: Uliwapata kwenyu tuu
I: Eeee wamefuatanishwaaa
P:ooohhh
I: Ni kufuatanishwa wamefuatanishwa
P: Sasa wewe vile ulizaliwa ukiwa last born kabla hawa wazaliwe walizaliwa kama
haukoo
I: Sii nimekuambia nilikuwaa kwa shosh
P: Oooh, so ukarudii tuu ukawapata na bado hukuwa unajua babako hiyoo time
I:lakini naskianga hukuwa
P: Oooh, ako wapi?
I: Sijui akoo tuu hii Nairobii
P: Hakuna communication anaongea na mamako,babako...(audio not clear)... So hebu
niambiee mmh, ulikuwa unaniambiaa vike umepata,vile ulidiscover ulikuwa na boll
ulianza kuniambia ulikuwa unalala alafu ikakuwa aje
I: After kujua
P: Ulijuaje ?
I: Sii hiyo nini, kupima na kulala na kutapika so ukiwa na boll unajuanga hizo
reactions
P: Ulikuwa umetapika for how long
I: For one week
P: Mmmh
I: Kulala, kulala unalala mwezi moja
P:Ulikuwa bado unaenda shuleni
I: Eeee
P:Mmmh
I: nikaacha shule nini... ( Audio not clear)
P: Achaa tuendelee, haya hebu tuendelee na story yaa vile uligundua uko na boll
I: Venye niligundua nilikuwa na boll, nilikuwa najaribu hadi kuitoa
P:Mmmh
I: Nilijaribu hadi kunywa majani, nilikunywa majani nikatapika
P:Hebu niambie ilikuwa which year
I: This year
P: Enheee, so ulikuwaa wapi, ulikuwaa shuleni ama ulikuwa home
I: Shule
P: Soo, ikakuwajeee, hebu niambie venye ulianza kugonjeka
I: Kugonjeka azin?
P: Sii ulikuwaa umeniambia ulikuwa unatapika
I:Mmm
P: Mmmh
I: Sii unagonjekaa unalala, mamangu akaanza kunishukuu nikoo na boll
P: Ulikuwaa unalala shuleni ama nyumbani
I: Hadi shulee,nikisoma nakaa huko back bencher nalala ndio nikaambianga
mamangu niko na boll
P:Ulijuaje uko na boll
I: Kupima inajiitajee hiyoo thermometer
P: ...( Audio not clear)..
I: Ni thermometer ama nini , sii thermometer ilee kitu ya kujipima ya chwani
P: Pregnancy test
I: Eee hiyoo
P:Enhee sasa nini ulifanyaa ukapima na ulipimaa wapii
I: Kujishuku
I: Mmhh
P:Nilipima nikiwa home, nilikuwa najishuku niko na boll juu ya venye nareact
I: Mmmh
P: Kutapika hiyo Kugonjeka ni kaa ukona malaria
I: Saa ukatoka ukaenda kununua
P:Eeee
I: Enhee alafu, mtu wa pharmacy alikutreat aje
P: Skumambia mii nilinunua tuu nikaendaa
I: Okay, hakukulizaa
P: Azin kuuliza kaa nko na boll
I: Eeee, mbona unanunua hiyo kit
P: Mii nilimuulizaa tuu venye mtuu hupima, venye kaa ukoo na boll ukipima inafika
wapi hiyoo makojoo sindioo akanielezea nikacome nikajipima
I: Mmmh
P: Nikagundua nko na boll
I: Hivyoo tuu anhaa so
P: Saa kuelezea mom ndio ilikuwa ngumu juu
I: Hebu niambie umegundua uko na boll kabala uelezee mam uliskiajee
P: Vibaya
I: Ulijihisi ajee
P: Nilikuwa naskiaa ehee bana,ni kaa naezaa toa , ni kaaa nimwambiee hadi naogopa
kumwambiaa bado
I: Mmmh, so ulifikiria kutoa ukafikiria nini tena
P:Lakini ilibidi tuu nimwambie juu, juu ni yee bado tunakaa na yeye
I:Nini ilfanya hauku, haukuitoa
P: Ilikataa
I:Ulijaribu
P: Mii nilijaribu eheee
I: Ulijaribua ajee, hebu niambie
P: Na majani
I: Ulikunywa majani , kiasi gani
P: ubaya ya majani mtuu ana anchokanaga
I:Uuuuh, tuendelee, ulikuwaa unaniambia ulijaribu kutoa, ulijaribu kutoaaa na nini
P: Majani
I: Aje sasa
P: Nilipika string tea nikaekaa majani mingi,nikaikunywa once
I: Mmmh
P: Kuikunywa once,nikatapika yote
I: Mmmh
P: Ikakataa kutoka,mii nkaachana nayoo,nikambia mamangu nko na boll
I: Hiyo fikira ya kuii, kuchukua Majani mingii kukunywa ilitoka wapi
P: Ni story tuu za watu venye watu husema mara
I: Ulikuwa umeuulizia ama
P: Sikuulizia , venye naeza... ( Audio not clear)... Venye watu hueleze njee kutoa boll
I:Mmmh
P: Nikaskia haadi majani inaeza toa
I: Ulikuwa umeskia kwa watu
P: Eeee, sa hizoo si mii sina doo ya kutoa
I:Mmmh
P:Nikaenda nikajaribu majani
I:Mmmh
P: Majani ikashindwa,nikagive up,nikasema tuu acha niseme
I: Ulikuwa na how many months saa hizoo ukijaribuu kuitoa
P: Ni nne
I:Nne
P: Mmh
I:Sasa ile siku yenye umepima, na ile siku yenye unatoa ilikuwa imetake how long
P: Ni two months ata
I: Ulipima ikiwa how many months
P: sii nakuambia nilijua April
I:Ulijua April ukiwa ushafika three months.
P: Mmm
I:Sasa iii, haukufikiria ni mimba ama uliaususpect tuu lakini haukutaka kupima
P:Nilijua niko na mimba nika nika nini, nikataka kuwa sure
I: Okay
P: Sure
I: Mmmh
P: Ndio nikaipima
I: Ooh,so ulipima through test, wee mwenyewe ulipima, sasa vile haikutoka ukajaribu
tena ,ukajaribu the fourth month
P: Sikujaribu tena, niliachana nayo, sii after kujaribu na majani,nilijaribu na majani
nika give up
I:Ikakataa, so ulitake how long kuambia mamako
P: One month
I: So ulipima ukatake one month,ukajaribu kutoa after one month ikashindikana then
ukaambia mamako after, saa ngapi sasa hiyo siku yenye ulitoaa?
P: Hiyo siku yenye nilipima
I:Hiyo siku yenye ulipima, uliambia mamako siku yenye ama siku ulikuwa unajaribu
kutoa
P: Siku nilikuwa najaribu yaani kutoa sii siku nilitoa
I: Ooh, ningependa, nilikuwa nataka kuelewa hiyo point,so venye uliambia mama
yako,mm, uli, kabla uniambia venye uliambia mamako so tunaeza sema since
haukufanya protection ama hauku, hakujiprotec...(audio not clear)... tunaeza sema
ulikuwa umepanga kupata mtoto
P: Sikukuwa nimepanga
I: Mmmh
P: Sii nilikuambia ... ( Audio not clear)...haitamake, sitashika boll
I: Sasa venye umehspima ukapatikana yko na mimba, umeniambia ulishtuka, na hata
ukafikiria kutoa nini tena ilikuwa inago through your mind
P: Venye ntalea
I: Veneye utalea, ahaa
P: Venye nitaendelea na kulea
I: Part from kuahtuka were you
P: Kusoma, bado sijamalizaa kusoma
I: ulikuwa worried pia
P: Eeee
I: Mmmh,sawa sawa, sasa ukaambia mama yako ulimwambia ajee
P: Sii nilimface tuu
I:Mmmmh
P: Nilimface tuu nikaambiwaa,juu hakuna haja yaa kuogopa na tayari imeingia
I: So ni hiyo siku ulikuwa unajaribu ndionukamwambia
P: Mmmm
I:Sasa how was it, ukimwambia, alihisi aje
P: Nilkuanga hadi naskia aibu hadi alikuwa anasema namuaibisha lakini ilibidi tuu ...(
Audio not clear)
I:Hebu niambie siku ulikuwa unamwambia experience yake ilikuaje. Ulimwitaa
ukamkalisha chini ama ulimpata wapi
P: Sii nilimkalisha tuu chini kwanza.
I: Ukamwambia
P: Niko na mimba na asiskiee vibaya
I: Mmmh
P: Juu bado nimejaribu kutoa Ikakataa
I: Response yake ilikuwa
P: Aaaah
I: Response yake ilikuwa
P:Kushtuka
I: Alishtuka
P: Aibu, eeeh
I: Aibu
P: Yenye watu wataongea huko
I: Mmmh
P: Yaani venye namuaibisha
I: Alikuwa ...( Audio not clear)
P:Lakini after all, eeeh, after all sii aliniitikia
I: Hivyo tuu,hiyo reaction yake kusemaa unamuaibisha amefeel aibu ilikufanya
ukafeel ajee wewe
P: Lazima tuu mtuu afeel vibaya
I: Mmmh
P: Lakini sii ninmimi ndo nilikosea
I:Mmmh
P:Sasa wewe alikuwa akikuambia hivyo unasema nini?
I: Singerudisha
P: Namuachaa tuu aongeee
I:So, after kusema hivyoo ikakuwajee, alikuwachaa ama ikakuajee
P: Matusi sasa
I: Eeeee
P:Alikuwa ameshinda amenitusi
I: For how long
P: Hakunitusi sana
I: Na anything yenye alifanya yeenye ilikuwa mzuri after venye ulimuambia uko na
mimba
P: Alfurahia tu juu, ni juu sikutoa
I: Alifurahia juu hukutoa mmmh , alikuambia ajee
P: Alikuwa anakuja kuniambia saa... (Audio not clear)... mwezi wa saba
I: Mmmh
P: Heri hivyo sikutoa mimba
I: Mmmh
P: Juu hadi ni first born, ingekuwa sii bado ningekuwa tasa
I: Mmmh,
P:Mmm
I:So alikuwa anfeel pia poa hukutoa
P: Juu bado ni aibu
I:Sasa hiyo ni this year sasa,
P:Mmm
I: Okay, huyo mtoi ako how many months saa hizi
P: One
I: just one month, umemzaa last month
P:Mmm, date ...(audio not clear)
I:So, ukiambia mamako about your pregnancy,lakini baba mtoto alikuwa wapi hiyo
time
P:Sii nimekuambia alikuwa ashaenda
I: After mmehave na yeye sex the last time ali, ali, alienda wapi
P: Sijui penye aliendaa, hivyo ndio alipotea
I: Ulimwambia about mimba
P:Eeenhe
I: Ulimwambia ajee
P: Niko na mimba
I: Mmh, Ulimwambia through simu ama ulimtafuta
P: Simu
I: Enhee
P: Nilimwabia niko na mimba hiyo siku niligundua
I: Mmmh, ulimwambia tuu hiyo siku
P:Mmmm
I:Alafu
P: Hakuongea
I: Hebu niambie sasa nimemwambia,nimekupigia simu ama umempigia simu
ukamwambia mimi niko na mimba, response yake ilikuwa aje
P: Kushtuka, sasa sijui hiyo kushtuka ilimfamya asirudi ama ni nini
I: Mmmh
P: Ni kama aliogopa responsibility akahepa
I: Akahepa,ulikuwa unajua mahali anaishi
P: Najua tuu penye mamake anaishi
I: Na nyinyi mkiwa na yeye mlikiwa mankitana wapi
P: Kwake
I:Kwake
P: Na kwake si alibeba vitu
I: Ooh, inshort unasema alihama ata hapo, akaenda na kila kitu
P: Mmmm
I: Okay, wewe kugundua amehama na ameshtuka na amehama, ilikufanya ufee aje
P:Sii vibaya
I:Mmh,hebu niambie what went through you mind,ulikuwa unafikiria nini
P:Nilikuwa nafikiria nimerukwa (laughing)
I:Mmmh
P: Juu hadi mapigia simu nimuambie,hataki kuskia
I:Mmmh, alikuwa anashika simu zako bado
P:Mmm, lakini sahii ashikangi
I:After kuzaa
P:Mmm
I:Okay, so yeye venye alidisappear hivyo uliskia vibaya alafu ukaskiaje tena
P: Yeye, nimeksiaa, mtu tuu huskia tuu vibaya hizo siku za kwanza
I:Mmmh
P: Lakini sahii si ni mii najilelea mtoto
I:Mmmh
P: Hajanisaidia kuu ...(audio not clear)
I: Responsibility yeyote ukiwa na mimba alichukua
P: Aaa
I: Umesema wewe venye ulimwambia
P: Ni hivyo ndio alii
I: Umesema ulimwambia at three months
P:Eeee
I: Sasa wewe kuconfirm kukuwa pregnant uliconfirm peke yako,
P:Mmmm
I: haukuenda hosi, mmh na ni wakati mgani uliambia mama yako
P: Niliambia mama yangu nikiwa na mimba ya miezi, miezi tano
I: Miezi tano,sasa saa hizo ndio...(baby crying)...sii umeniambia, after kujaribu
kutoa...(crying continues)...Sasa tuendele kidogo saa hizo venye ana nyonya, so
umesema yeye akadisappear, mamako umemwambia mwezi wa tano na wazazi wake
wako wapi
P: Mii najua tuu mamake
I:Mamke ako wapi
P: Ako huku Dandora
I: Ushai ongea na yeye
P: Mmm
I: Ushai hata mwambia, wanajua uko na mtoto wao
P:Mmm, mimi sijai handa mamke juu sii yeye alinipea mimba
I:Nakuambia tu familia yake ama ushai kama familia yake inajua,Okay na ye pia
hajai amabia familia yake
P: Charles sijui kama aliwaambia juu angekuwa amewaambia wangukuwa
wamecome kuniona
I: Okay, so ningependa kujua, vile ulishikaa hii boll attitude ya marafiki yako ilikuwa
aje, niambie kabla ushike boll alafu saa hizi venye umeshika,saa hizi venye umeshika
boll imekuwaa ajee
P:Marafiki sii wanakuchekeleanga tuu kidogo alafuu
I: Kwa nini unadhani wanakuchekelea
P: Sii juu...(laughing)... Lazima wakuchekelee juu pia
I: Wanasema nini
P:Mimba, nikona mimba nimejazwa...(giggling)
I:Mmmh
P: Nikona mimba sahii hakuna kuenda mahali
I:Ulikuwa na marafiki wangapi
P: Marafiki siezi hesabu niko na marafiki wengi mimi
I: Wengi, na saa hizii bado ni marafiki zako vile umezaa saa hii
P: Sii wote
I: Mmmh
P:Wenye wamezaa tuu, wenye wako na watoto ndio tunashinda nao, wenye hawana
watoto tunajua hao bado
I:Mmmh
P: Bado wanakula raha,acha wakule
I:Aaaahm na hivyo wakikuambia, na hivyo wakkikuongea wee huskia ajee
P: Sii vibaya sana,lakini bado naskia vibaya kidogo
I:Kidogo, what about community ya hapo mahali unaishii ,wamechukuliajee hii,
wamekuchukuliajee wewe kama msichana mdogo umeshika boll umeachaa shule
P: kuongea lazima waongee
I: Wanasema nini
P: Sii unajua tuu mamoshene za watu
I:Mmh
P: Kameshika mimba kakiwa mapema hivii
I:Mmh
P: Lazima wapige moshene mahali
I:Ushwai kuwa na experience mahali mtu amekusema
P: Sana, eenhee tena nikiwa na boll walikuwa wanongea sana
I: Sana,wakionfea inakufanya unafeel aje
P: Vibaya
I:Mmh, unadhani ni kwa nini wanaongea
P: Sii juu siku, sikumaliza shule na nimeshika boll
I: Okay,Specifically ni akina nani, jirani wamama
P: Wamama wote hadi majirani wote
I:Mmmh,watu wa wapi pia
P: Hadi watu wa nini, wa vibanada ,hawa watu wa vibanda wa kukata mboga
wanaongeanga hadi waduka wengi
I:Zinakufikia hivyo vitu
P:Mmh, lazima zinifikie
I: Sasa waki
P: Lakini si unawanyamazia tu
I: Sasa wakisema, nani anakurudishia? Ama wanasema ukipita
P: Kuna wale wanasema wakipita,kuna wale wanaambia marafiki zangu wananiletea
I:Mmh, soo wanakuambia kitu kama gani ?
P: Venye naiibisha mamangu
I:Mmmh
P: Unajua bado ukishika boll bado ni aibu lakini
I:Mmmmh, sasa hivyo venye ulikuwa na boll ulikuwa unasema wanaongea na saa hizi
venye umezaa?
P: Saa hizi
I: Hao majirani kwa ploti yako, hao mama wa mboga wenye uliniambia sahii
wanafeel ajee?
I: Sahi hawaongei sana
P: Unaksia wakisema nini now that ushazaa?, Ukitembea na mtoto wako mahali
ulikuwa unaongelewa ukiwa na mimba ukipita na mtoto wanasemaje
I: Sii nii kusalimia tuu mtoto, alafu huwezi wakataza kuona mtoto bado
P: Wanataka kuona mtoto sasa
I: Wanataka kuona mtoto sasa, walikuwa wanakutukana lakini sahizi
P: Wanataka waone mtoto
I: So wanakuambia ajee
P: Nishazaa
I: Mmmh
P: Hadi wananiuliza mtoto mwenye nimezaa sahii,
I:Oooh
P:Eeenhee, ati wanataka kumuona
I: Na wale marafiki zako, how is their attitude by saa hizi
P: Marafiki zangu sii wote nakaanga nao siku hizi
I: Mmmh, before
P: Kiasi tuu
I: Wale walikuwa wankusema saa hizi wanasema nini
P: Hawaongei
I:Mmmh, na hao wenye
P: Unajua unasemangea sana ukiwa na boll kuliko ukiwa na mtoto
I:Oohh, unafeel hivyo
P:Enheee
I: Okay ,unadhani kwa nini sasa saa hizi walikuwa wankuongelea vibaya hao
macommunity, community members na sa hizi ushazaa wnataka tuu kuona mtoto
hawaonge sana,unadhani nini ilikuwa inawafanya
P:Sii labda ni hiyo aibu yenye nilikiwa nayo,ya kubebana na ...(audio not clear)
I:Okay, na walimu
P: Mii sijai rudi shule (laughing)
I: Haujairudi shule,haujai kutana na walimu wako
P: Eenhee, juu nilikuwaa naenda shule nikiwa na boll ndogo saa nikiwa na kubwa
nikaachaa kuendaa
I:Ukaacha?
P:Mmmh
I: So, uliacha hadi kuenda shule ulisema tuu leo siendi ama mimba ilianzaa kuwa
kubwa ukaamua tu sasa huendii
P:Niliguve up keunda,nilisema tu siendi
I:Hawakukuuliza,haukuulizwa,hawakufuatilia
P:Aaah
I:Okay, shule yenyu watu hawafuatiliangi,
P:Mmm,
I: Shule yenyu watu hawafuatiliangi
P: mmm hawafuatiliangi sana
I: Sawa,ningependa kujua ulienda clinic ukiwa na mtoto
P: Clinic? Eenhee
I:Mmmmh
P:Mimi hukuwa naenda
I: Ulienda clinic ngapi
P:Nilienda clinic mara tatu
I: Mara tatu, ulianza ukiwa na miezi ngapi
P: Saba, nane na tisa
I: Ulienda ,saba, nane na tisa,mbona saba, nane na tisa, mbona hukuanza mapema
P: Kuanza mapema bado inachokesha
I:Mmmh
P:Izoo shindano,niliachaa kuenda shindano,niliacha kuenda clinic juu yaaa,nilienda
kudingwa shindano ya korona
I:Mmmh
P:Ikanochokesha
I:Ulidundea shindano ya korona,kabla huende clinic
P: Nikianza kuenda ndio nikadungwa
I:Ulianza mwezi wa
P: Wa saba
I: Hiyo mwezi wa saba ndio ilikuwa clinic yako ya kwanza
P:Nikaenda ya pili, ya tatu niakaambiwa tena nidungwe shindano ya korona nikakataa
I:Alafu,
P:Hivyo ndio niakaacha clinic
I: Ulikuwa unaogopa shindano
P: Sii nilisikia shindano ya korona inaharibikia mama ako na mimba na hao
wanajidunga
I: Ooh,okay, soo unaeza sema ulianza kuenda late ulikuwa unafeel, ulikuwa unaogopa
kudingwa shindano ya korona
P:Kuanzanga late,mi ni kuchanuliwa na rafiki yangu,huendangi clinic na uko na
mimba ndio akaanza kunipeleka
I:Rafiki yako kutoka wapi
P:Mwenye tunaishi na yeye
I: Mnaishi na rafiki yako?
P: ploti moja
I: Yee ndiye alikuambia,mama yako hakukuambia story ya clinic,mmh, saa yeye
alikuchanua ukiwa seven months sas hapo ndio
P:Nikaanza kuenda
I:Ukaona uanze kuenda clinic,so unataka kusema haukujua story ya clinic before
P:Nilikuwa najua lakini sikukuwaaa nafikiriaa kuenda
I:Cinic iko mbali na home
P:Unajua kwa chief?
I:Eenhee,nimeiskia
P: Hapo tuu kwa chief
I:Mmh,ulikuwa unaenda tuu hapo,ilikuwa inakucost pesa ngapi ukienda huko,
P:Kwa chief haulipangi ni bure tuu
I:Haulipii,sasa kwa chif hapo ukienda clinic unaezaa sema experience yakoo ilikuwaa
ajee?
P:Kuenda clinic?
I:Mmmh,Ulikuwa unapata ugumu kuenda, ulikuwa na any difficulties,ulikuwa
unajificha ukienda ama ulikuwa unaendajee?
P:Sii nilikuwa tuu naenda tuu,sikukuwa naskia ugumu,juu bado niliambiwa watu
wengi...(audio not clear)...lakini ni venye nilianza late
I:Mmmh, soo unaeza sema clinic ni mbaya ama ni mbaya
P:Ni mzurii, kwanza shindano ilinisaidia
I: Na hapo kwa chief ni kizuri ama kubaya?
P: Kuzurii
I:Kuzuri
P:Watu wako na mimba wanahudumiwa vizurii
I:Wakona
P: Watu wako na mimba
I: Okay, hao manurses wanafanya hapo wanawatreat watu wako na mimba aje sana
sana wasichana wadogo
P: Wanawatreat vizuri lazima wawahudumie
I:Kuwaongelesha wanawaongeleshajee ?
P: Kuongeleshwa clinic azin
I:Wakiwaongelesha wanawaongelesha vizuri
P:Eenhee
I:Uliwai experience yoyote,uliwai kuexperince mtu kukutukana ama?
P:Sijaitukanwa
I:Haukujai, mtu Kuongelesha vibaya, na wamama wenye pia walikuwa wamekuja
hospitali waliwakukuongelsha
P: Hapana
I:Mmh, sasa sahio ukienda ulikuwa unaongea kina nani hapo
P: Sii ni kaa ukienda tuu hosi unaeza ongelesha mtu yoyote
I:Ulipata marika zako hapo pia walikuwa wame nini,walikuwa na mimba
P:Mmh
I: Hao pia walikuwa wamekamia
P:Mmh
I:Hao pia walikuwa wamekujia mimba, wamekujaa clinic
P:Mmh
I:Na walikuwa wanakuambia imekuwajee
P:Kukuwa na mimba sii rahisi
I:Sii rahisii, ulizaa mtoto wako wapi?
P:Pumwani
I:Pumwani, alipata clinic, alipata chanjo zote?
P:Mmmh
I: Ama sa hizi ako one month amepata tuu chanjo moja
P:Enheee, anafaa kupelekwa apate ingine?
I:Naulizaa siii, amedungwa gani hiyo
P:Alidungwa tuu mkono ya left
I:Enheee
P:Hiyo tuu ndio alidungwa hiyo siku
I:Lakini si anafaa kurudii nyingine imeandikwa kwa kitabu ya clinic utaangalia,
sindio
P:Mmm
I: Aaah, mbona ulichagua pumwani
P:Sikuchagua,ni mwenye alinipeleka tuu alinipeleka huko
I:Okay, na ukienda clinic mara ya kwanza uliniambia nani alikupeleka , rafiki yako
anaishi?
P:Tunaishi na yeye plot moja
I: Ako na mtoto pia yeye?
P:Eenhee
I:Anatoshana ajee?
P: wa miezii nne
I:Wa miezii nne, yee pia ni teenage mother
P:Mmmh
I: So tunaeza sema rafiki yako alikusupport kwa kukupeleka.
P:Enhee
I:So reaction yake ukiwa na boll ilikuwa ajee, yee alichukulia ajee?
P: Yee haku nini, halukataa kukaa na mimi,tilukuwa tuu tunashinda na yeye, tukienda
mbali na yeye, kila kitu ni na yeye,tulikuwa tuu tunshinda na yeye
I:Mmh
P:...(audio not clear)... Nimelemewa namsaidia ananisaidia,kaa tuseme venye
nilikuwa nimechoka kuchoka ile kichoka za..(audio not clear)... ananisaidia kuoshaa
vyombo,kufua na mii namsaidia tuu kumbebea mtoto
I:So mtoto wako akiwa mgonjwa unampelekanga wapi
P: Mtoto wangu, nampelkanga hapo kwa chief anaandikiwa madaws nambuyia.
I: Ashai kuwa mgonjwa?
P:Mara moja tu.
I:Mbona kwa chief?
P:Juu nimezoea, nimezoea hosi ya karibu
I:Atiii
P:Ni hosi ya karibu
I:Ooh ni hosi ya karibu,malipo yake?
P:Hawalipishi,kaa ni dawa either wanakupea kaa hakuna wanakuandikia huende
ununue.
I:Okay,unaeza sema mimba ya hiyu mtoto imekuletea athari yoyote kwa mwili yako?,
Ilikuwa na effect gani apart from kugonjeka ni nini uliexperience
P:Sikugonjeka tena
I:Kiakili
P: Isipokuwa kuchoka tuu
I:Mmmh, kiakili
P: Akili yangu ama yako
I:Yako
P: Ni siku tuu za mwisho kaa nimechoka
I:Mmh
P:Unajua venye mtu akichoka na mimba weehh
I:Kuna mahali umeniambia ulikuwa unafikiria pia kutoa alafu haikutoka
P:Hizo siku za kwanza kwanza
I:Hizo siku za kwanza kwanza, hiyo fikiraa imeisha ama uliendelea nayo mapakaa
ukaa
P: Iliisha.
I: Kazi zako ni za masaa kawaida
P:Aaaah
I:Mmh,so venye ulikuwa na mimba ni challenges gani ulikuwa unapitia?
P: Maswara ...(laughing)
I:Enheee?
P: Mtu akikuwa na mimba anakuanga na swara sana
I:Mmh,kama nini
P:Azin vile tulikuwa tunafungiwa nyumba
I:Kwenyu? Mmmmh, nini tena
P: Bado manguo za mtoto sikukuwa nimenunua
I:Mmh
P: Ni hivyoo
I: Challenges zingine,kulish, kujilishaaa
P:Kulishwaa,kujilishaa sikuwa nweza kuijilishaa nilikuwa nalishwa na mamangu.
I:Mamako anafanya kazi gani?
P:Anafulia watu
I:Anafulia watu kwa etsate alafu
P:Ni hivyo
I:Anapata pesa ngapi hivi?
P:Inalingaa.
I:Mmmh
P:Si kazi zote inatoshana doo.
I:Mmmh, so nani alikuwa anakuprovidia hiyo time yeye bado.
P: Siku gani
I:Mamako ndio alikuwa anakuprovidia,tunaeza sema hiyo ilikuwa challenge kwako?
P:Mmmh, juu siezii jitafutia unajua mtu akitoka haezi jitafutia?
I: Mmmh naelewa,challenge ingine yoyote ulikuwa nayo ...(audio not clear)...
Tuaneza sema,umeniambia baba ya mtoto alienda,tunaeza hiyo pia ilikuwa challenge
because sasa,
P: Enheee, si pia ni challenge
I:Nini tena ulikuwa unafeel ni kama uli, imekuwa challenge kwako
P:Kubebeshwa, na hakuna mtu mwenye amekubebsha yako
I:kubebeshwa aje?
P:Kubeba mimba na mtu amekubebesha hayuko
I:Okay
P: Hiyo si bado ni challenge
I:Enhee, hiyo ni challenge, hata kuongelewa pia ni challenge sindio, okay, sii
umeniambia ukoo umepata hizoo challenge acha tunge vile wewe hutake care of huyu
mtoi wako ama kumsupport,nani hukulindia mtoto?
P:Kumlinda, sii ni mimi nakaanaga nayo
I:Nani tena wanakusaidianga kumbeba
P:Mamangu na huyu rafiki yangu ...( Audio not clear)
I: ningependa kukuliza about baba mtoto lakini ushaniambia hayuko,sindio, umesema
kwa familia yako mamako anakusaidia kumbeba, kuna watoto wenyu wengine
wanakusaidia?
P: Enheee sii akilia lazima wambebe pia wao
I:Okay
P:Lakini si unajua hao bado wanaenda shule.
I:Ooh,Okay,mmmh, support yoyote yenye wanakupatia,rafiki yako umeniambia
ankupatia support ya kusaidia ku?
P:Kumbeba niliwa na kazi
I:Enhee, mama yako?
P:Mamangu ananisaidianga ...(audio not clear)
I:Okay,mmmhh, anakusaidia kwa njia gani?
P:Aaah akirudii ananinyoroshea mtoto
I:Anamnyorosha
P:Akimwosha anamnyoroshaa.
I:Mmmh,
P:Akilia usiku anaskia kumbeba
I:Mmmh
P:Ni hivyo tu
I:Okay, na rafiki yako, apart from kumbeba,kukusaidia kulea?
P:Anasnisaidianga tu kumbeba tu sana
I:Na nguo za mtoto, manguo za mtoto umetoa wapi?
P:Ni yee bado aliboost kunisaidia zingine nilibuy soko
I:Nani huyo
P:Rafiki alinisaidia nguo ndogo za ...(audio not clear)..zingine nimajiendea.
I:Zingine ukajiendea,naa mama yako, tunaeza sema venye anakupatia place unaishi
inaeza kuwa ni anakussiport?
P:Hadi chakula sii ananisupport bado
I:Mmmh, support ingine anakusupport,sister huyo mwenye ameolewa amekussuport
aje?
P:Alinisupport tuu siku za kwanza...(audio not clear)
I:Alikupatia nini
P:Nikiwa mgonjwa,nikitoka hosi tu. Alikuwa nanisaidia kutoka kutoka
I:Hivyo tuu
P:Kupika
I:Alikuwa anakuja home?
P:Enheee,kunisaidia kazi kidogo kidogo
I:Anatoka kwake akikuja hapo,alafu analala ama anarudi?
P:Anarudi
I: Hiyo support ulikuwa unapewa inatosha?mmmh
P:Alinipea hizo siku Lakini sii ilitosha hizo siku
I:Okay.
P:Ni venye hizo siku sikuwa najiweza, sahii sii najiwezaa, naeza jisupport.
I:Saa hizi uko sawa, na chakula unapewa from home inatosha,inakutosha wewe na
mtoto?
P: sii ni mi naikula yee anainyonya
I:Umesema wee unakula ye anainyonya,so uneza sema iko tuu sawa?
P:Enheee
I:So saa hizi venye ushazaaa, Uneongea challenges zako ukiwa na mimba, sahii venye
ushazaa ni challenges gani zenye unaface?
P:Sahii, challenges ni kulea tuu
I:Mmmh
P:Hiyo tuu
I:Kama, kule ajee? Umeniambia mtoto analia usiku, sii umesema hiyoo ni challenge
P:Eenhe
I:Na nini tena
P:Hiyo tuu
I:Naa, hiyo kulea usiku mtoto akilia unacope nayo aje,ulikuwa umeniambia mamako
anakusaidia sivyo, kuna challenge nyingine, mtoto kukuwa mgonjwa,umeniambia
amewai kuwa mgonjwa?
P:Enhee, Mara moja tuu
I:Ulicope nayo ajee,mmmh ulicope nayo aje ulimpeleka hosi, ulimpelekaa hosii
ulipata wapii pesa?
P:Nilimpeleka hosi nikambuyia dawa ,pesa kidogo
I:Ulitoa wapi?
P: Sii ni zile za maziwa nilikuwa naletewa ...(audio not clear)...nikiwa mgonjwa
I: Ulikuwaa unaletewanga vitu ukiwa.ulikuwa unaletewa pesaya maziwa na pampers
kaa haujazaa?
P: Aaah, kaa nimezaa,venye mtu hukuwa ...(audio not clear)... akicome kuona mtoto.
I:Saa kina nani walikuwa wana, akina nani walikuwa wanakuletea?
P: Majirani, masisters wangu, maauntie zangu
I:Oohh, waliku support pia.
P:Wakiniletea hizoo doo nasave,saa sii unaona zimenisaidia
I:Si tunaeza,so tunaeza sema ,kuna maauntie zako walikusaidia pia walikusupport pia
na pesa ya maziawa kaa umezaa, Okay,Hebu tuambie juu ya education yako soo what
happens,what happened to your education after ushashika boll?
P: Sii nilidrop tuu ,nilidrop out tuu
I:Mmmh
P:Nikaacha hivyo shule
I:Unapanga kurudi shule?
P:Sioni sababu naeza rudi shule,lakini naeza enda course.
I:Unaeza enda course?
P:Napanga kuenda course
I: Course gani?
P:Aaah beauty
I: Unataka kufanya beauty,ukitoka beauty
P: Hairdressing
I: Beauty and hairdressing,mmh, na unajua zile policy zenye ziko zenye zinitwa
school re-entry policy, unaeza wacha shule na urudi tena ujoin?
P:Sasa sahii naeza rudii shule na niko na mtoto?
I:Sii baadaye
P:Anasoma Nasoma
I:Hautaki msome pamoja (laughing) wee unaona huwezi rudi shule?
P:Naezaa lakini heee,ni ngumu.
I:Okay, haujai ona watu wamerudi shule,haujai
P:Sijai ona mtu amerudi shule na ko na mtoto?
I:Oooh, hata kuwacha mtoto wake nyumbani akirudi shule haujai ona?, Na kama kuna
mtu ameshikaa boll na hajaa achaa
P:Ya boll nishai ona
I: Hao pia ushai ona,anaenda tuu nayo shule
P:Mmmh
I: Unadhani watu kama hao wanafaaa kuwa supported aje wakiendelea na shule na
ako na mimba
P: Atii?
I:Sasa,hivyo venye anaenda shule unadhani anafaa kuwa supported aje,asaidiwe aje
ndio asiskie ugumu akienda shuleni?
P:Mtu ako na boll anafaa kusaidiwa sana
I:Hebu tuanzee na wanafunzii wa shule?
P: Mmama
I: Wanafunzii wa shule
P:Ni venye mii naeza msaidiaa?
I: Wanafunzii wenye wako shule, sii anaenda shuleni kila siku? Eeee marafiki zake
shuleni
P:Eeeerrr, hiyo si ni kuchekelewa tuu.
I: Ni kuchekelewa
P:Ukienda shule na boll utaangaliwa, kuchekelewa, aibuu
I:Mmmh, sasa unadhani wanaeza saidiwa aje na walimu
P: Kusaidiwa?
I:Na walimu, wakiwa shuleni?
P: Sii wanasaidika tuu
I:Waambiwe nini, wafanyiwe nini?
P:Kufanyiwa nini azin?
I: Wakiwa shuleni wanafaa kusupportiwa aje? Wasaidiwe kivipi, Okay, sasa umesema
wewe haurudi shuleni mmmh? Readon yako kubwa ya kutorudi shuleni ni nini?
P: juu ya mtoto
I:Mmmh
P: Saa ni yeee nitatafutia ama ni mimi nitajisomeshaa? Bado sahii nikisema nii
kurudii shule mam anaezaa kunilipia shule,mii sii ni mmama
I: Na uko na hofu yoyote about kurudi shule ama?
P:Siezi somea daro yetu.
I:So na wale wamerudi shule, sii kuna wale wamerudi shule ama wewe umesema
haujawaona hao kabisa?
P:Wasichana wa mimba nimewaona lakini wa watoto
I:Wa watoto haujawaona,incase mtu anadecide anataka kurudi shule anafaa
kusupportiwa ajee?
P: Kulipiwa shule,kubebewa, kushikiwa mtoto, lakini si mtoto unaeza mpelekaa day
care
I:Unaeza mpleka?
P:Daycare
I:Oooh, unafanya kazi gani saa hizi?
P: Bado sija sijaanza kazi
I: Sasa mtoto wako anakula, anasupportika aje, survive ajee,ulikuwa umeniambia
mamako ana provide kuna njia ingine pia wewe unapata?
P:Ndio napanga.
I:Mmh
P: Ndio napanga vile ntamtafutia.
I: Okay, utahitaji nini ndio uwezi kujisupport na usupport mtoto wako?
P:Kazii tu
I: Kazi kaa gani?
P:Ndio nilikuwa napanga niende nini,course nisome hiyo Hairdressing hiyo
I:Mmmh
P: Nifungue nini yangu?
I:Ufungue?
P:Kazi yangu, hiyo ya beauty and hairdressing hiyo na beauty
I: So, utahitaji job?
P: ...(audio not clear)
I: Na uko na future gani for yourself and the baby?
P: Tuuu
I:What is your future unapanga hapo mbeleni hujee ufanyee nini
P: sii nimtafutie tuu ndio najisaidia na nisaidie mamangu
I:Ungependa kusaidia mamako, na huyu mtoto ungependa kumwona ajee, hebu
niambie future yake venye inakaa
P:Vizuri,mimi napenda kumuona kaa nini yangu future yangu na yeye
I: Unapendaaa, Ungependa kumwona ajee?
P:Nimampangia mambo mengi?
I: Kama gani?
P: Asiache shule kaa mimi, amalizee shule ,asiparare, hivyo tuu
I:Ni sa...
P:asikose kukula
I:Ingine,
P:Hizo tuu.
I:Kuna support zozote zenye ziko kwa hii area yenyu yenye wanapatia young
mothers, ushaiskia?
P:Sii nimeona hii ya kwanza
I: Umeona hii ya kwanza, haujai skia support group zozote zenzye zinasupport
wasichana kwa hii community?
P:Eeenhee
I:Hakuna? Wasichana wajawazito wadogo, Okay,hata NGO yoyote ,hata trainings
zozote
P: Training, training nimeona,
I:Umeona training ya kina nani?
P:Mayouth,
I:Wenye wako?
P: Yenye nimeona,ni ya nini, inajiitanga ajee hii mradi Dreams unajua dreams?
I:Enheee
P:Hiyo, hiyo ndio nimeonaaa pekee
I:Wanasupport youths pekee yake, na young mothers
P:Young mothers sijaona
I: Haujaona, okay, wale wamama wako na watoto haujaona wakiwa wanawasaidia.so
out of kile kenye tumediscuss sasa sahii uko na one month kukuwa mama nini
unafind so rewarding about kukuwa mama, ni nini ukiangalia unaona ni kama enyewe
ishafanyika lakini mimi nafurahia ...(audio not clear)
P:Sii mtoto tuu
I:Enhee
P: Naona tuu mtoto naona tuu mimi nishakuwa mumama
I: So mtoto wako ndio anafanya unaskia hivyo? Na nini unafanya, umegundua ni
challenging kukuwa na , kukuwa mumama?
P:Kubeba,kubeba mingi,
I:Mmmmh
P: Iko na challenges mingi
I:Alafu kulea?
P:Kulea bado sijalea ,nimelea tuu one month
I: Okay,na kubeba iko na challenges gani tena, unaeza ongezea?
P:Kuchoka,hiyo mabo ya kuongelelewa hiyo tuu.
I: Okay, umesema for hii one month haujapata challenge yoyote?
P:Jua ni kunyonya tuu, challenge yenye nimepata ni kulia,
I:Kuliaaa (laughing)
P: Alikuwa tuu analia.
I:Alikuwa analia usiku, okay, ama mchana pia
P:Mchana hakalii
I:Kuna kitu yoyote ungependa kuongezea.
P:Aaaah
I:Kama sii hivyoo,tumemaliza, we’ve finished at twelfe fifty four.Asante kwa
kuchukua mda wako kuafanya na sisi hii interview,nimeshkuru.

You might also like