You are on page 1of 3

Discipline at the Workplace

Discipline refers to the practice of making people obey rules. Furthermore, it also means following
certain acceptable standards of behavior. Discipline is certainly an essential thing in everyone’s life. A
life without discipline is a life full of chaos and confusion. Most noteworthy, discipline makes a person
into a better human being. Discipline is a trait of paramount importance or discipline the practice of
training people to obey rules or a code of behaviour, using punishment to correct disobedience

Nidhamu (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: "discipline") ni adabu njema kwenye familia, jeshi,
hata kwenye shule. Mtu mwenye nidhamu ni mtu ambaye anafanya kinachotakiwa kufanywa ili kufikia
malengo yake na ya jamii.

Kufanya mtoto kuwa na nidhamu pengine ni kwa kumuadhibu pindi anapoonesha tabia mbaya. Kuchapa
kulichukuliwa kama aina ya nidhamu.

Hata hivyo muhimu zaidi ni nidhamu binafsi, ambayo ni kujitawala kwa kusimamia matendo na hata
mawazo yako mwenyewe yawe ya kufa tu.

Nidhamu ya kijeshi inafundisha watu kuheshimu sheria na amri. Mwanajeshi mwenye nidhamu ni mtu
ambaye anaweza kutenda hata akiogopa kwa maisha yake.

Utovu wa Nidhamu

Utovu wa nidhamu maana yake ni kufanya mambo kinyume na mwongozo au tararibu za ajira sehemu
ya kazi. Katika mahusiano ya kiajira baina ya mfanyakazi na mwajiri kuna mfumo wa mwenendo ambao
unatarajiwa mfanyakazi auishi katika kutekeleza majukumu yake. Kutoka nje ya mfumo huo wa
kimatendo kunasababisha makosa ambayo yanaonekana ni utovu wa nidhamu ‘misconduct’. Utovu wa
nidhamu ni sababu mojawapo ambayo inakubalika kwa mujibu wa Sheria ya Kazi na Ajira kupelekea
usitishwaji wa ajira endapo itathibitishwa na kufuata utaratibu wa haki.

Leo tunaanza kuangalia baadhi ya makosa ya utovu wa nidhamu yanayoweza kusababisha usitishwaji wa
ajira ya mfanyakazi.

1. Utoro kazini

Kumekuwa na tabia ya utoro kazini kwa wafanyakazi wengi sana. Wafanyakazi hawaji kazini pasipo na
sababu au kutoa sababu za uongo za kuwafanya wasije kazini. Sheria ya Kazi na Ajira kupitia Kanuni za
Utendaji Bora ‘Employment and Labour Relations (Code of Good Prictice)’ inaeleza kuwa

‘kutokuwepo kazini pasipo ruhusa au sababu ya msingi kwa zaidi ya siku 5 za kazi ni kosa linaloweza
kusababisha kusitishwa ajira kwa utovu wa nidhamu’

Endapo mfanyakazi atashindwa kufika kazini kwa siku 5 basi mwajiri anayo haki ya kuanzisha mashtaka
ya kinidhamu na ikithibitika kuwa mfanyakazi ametenda kosa hilo, mwajiri anaweza kusitisha ajira ya
mfanyakazi husika.
Wapo wafanyakazi kwa visingizio vingi mara kwa mara wanashindwa kufika kazini au wanashindwa
kutoa sababu za msingi za kuwafanya wasifike kazini.

Ni muhimu kufahamu kuwa suala la utoro kwa siku 5 za kazi si lazima ziwe mfululizo kama jumatatu –
ijumaa inawezekana utoro huo ukawa wa vipindi vifupi vifupi kwa siku 2 au 3 kwa wiki kisha utoro wa
siku nyingine 2 au 3. Tafsiri hii ilitolewa na Mahakama ya Kazi kwenye shauri la marejeo Na.48/2015 kati
ya Bulyanhulu Gold Mine Ltd dhidi ya George Allen Gwabo, ambapo Mheshimiwa Jaji Mipawa aliona
kuwa Mjibu Maombi (George Allen) japo hakuwa mtoro wa siku 5 mfululizo lakini alikuwa na mtoro
aliyejenga tabia ya utoro uliokithiri na hivyo ni sahihi kwa mwajiri kumwachisha kazi kwa sababu ya
utoro.

Ili kuepuka changamoto hizi za utoro kazini inapaswa kuwepo na utaratibu mahali pa kazi wa namna
mfanyakazi anaweza kuufuata ili kupata ruhusa ya kutokufika kazini endapo kuna tatizo limejitokeza.

 Uwepo wa daftari maalum la kuthibitisha uwepo wa mfanyakazi kazini. Siku hizi teknolojia
imesaidia vipo vyombo vya kielekroniki vinavyoweza kutumiwa kuonesha ‘attendance’ ya
mfanyakazi.

 Uwepo wa kanuni zinazoweza kuongoza juu ya sababu za msingi ambazo mfanyakazi anaweza
kuomba ruhusa ya kutokufika kazini.

 Uwepo wa fomu maalum ambayo mfanyakazi anapaswa kuijaza ili kuomba ruhusa ya kutokufika
kazini.

 Kuthibitishwa kwa fomu husika na mwajiri au kiongozi wa eneo la kazi kwamba sababu
inayotolewa ni ya msingi.

 Mfanyakazi kuleta uthibitisho kulingana na sababu aliyoomba ruhusa. Mfano anaomba ruhusa
ya kwenda hospital basi alete cheti cha daktari kikionesha mahali alipoenda kutibiwa, au
anaenda safari basi alete tiketi zinazoonesha safari aliyoenda.

Hitimisho

Wafanyakazi wengi wanapenda kutumia mifumo dhaifu ya mwajiri na kusababisha tabia ya utoro wa
kazi kukithiri sana. Ni dhahiri kwamba wafanyakazi wengi hawapendi kufanya kazi kwa uaminifu, kila
wakati zipo sababu nyingi za kuwafanya wasifanye kazi au wasije kazini huku wakitaka kupata malipo
pasipo kuzalisha. Ni muhimu sana kwa waajiri kuweka mfumo mzuri wa kudhibiti mwenendo wa
wafanyakazi hasa tabia ya utoro kazini.

Kumbuka ‘kutokujua sheria si utetezi iwapo utatenda kosa lolote’ tafuta maarifa sahihi ya kisheria
yakusaidie kufanya maamuzi sahihi kila siku.

Muhimu

You might also like