You are on page 1of 1

NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013 AWAMU YA PILI.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, anapenda kuwaarifu Wataalamu wa Kada za Afya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi kutokana na maombi ya kazi waliyowasilisha kwake kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na kwa kuzingatia nafasi za kazi zilizoidhinishwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Watalamu wote waliopangiwa vituo vya kazi wanatakiwa kuripoti katika vituo hivyo kabla ya tarehe 15 Agosti, 2013. Baada ya muda huo kumalizika waajiri wanatakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili wale ambao hawajaripoti nafasi zao ziweze kujazwa. Aidha, Waajiri wote wanakumbushwa kukagua vyeti halisi (Original) vya kidato cha nne na kidato cha Sita pamoja na vyeti vya taaluma vya wahusika kabla ya kuwaajiri. Orodha ya majina ya Wataalamu waliopangiwa kazi na vituo walivyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz. Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyokuwa hapo awali. Nawapongeza kwa kupata nafasi hii ya kutumia utaalamu wenu katika kuwahudumia wananchi. Nawatakieni kazi njema na utumishi uliotukuka. KAIMU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII JULAI, 2013

TANGAZO

You might also like