You are on page 1of 4

MKATABA WA PANGO

KAT I YA

Dr. GWAMBAYE O.K

NA

UMETAYARISHWA NA:

Dr.GWAMBAYE O.K,
P.O. BOX 335,
NZEGA.
MKATABA WA PANGO

MKATABA HUU WA UPANGISHAJI umesainiwa leo tarehe.mwezi2011, KATI YA DR.


GWAMBAYE O.K wa Sanduku la Posta 335 Nzega (ambaye atatambuliwa MWENYE NYUMBA
katika mkataba huu, tafsiri ambayo itatambuliwa pia kwa mtu yoyote mwenye uhusiano na
MWENYE NYUMBA aidha awe ni mwakilishi au mrithi wake ) kwa upande mmoja
NAwa sanduku la Posta.Nzega (ambaye atatambuliwa kama MPANGAJI
katika mkataba huu ,tafsiri ambayo itatambuliwa pia kwa mtu yoyote mwenye uhusiano na
mpangaji aidha awe ni mwakilishi binafsi au mrithi wake ) kwa upande mwingine.

INATHIBITISHWA kwamba:-

1. Mwenye nyumba anapangisha kwa mpangaji vyumba/chumba


viwili/vitatu/kimoja katika nyumba iliyopo Nyasa Nzega kwa shughuli za Makazi kuanzia
tarehe.....mwezi .. 20 kwa kipindi cha...(.) na kwamba mkataba unaweza
kuendelezwa kwa kipindi kingine chini ya makubaliano kati ya pande mbili husika kwa
sharti la Mpangaji aeleze nia yake ya kundelea kupanga na kulipia vyumba/chumba.
Mpangaji atawajibika kutunza maeneo yanayozunguka nyumba.

2. Mpangaji anaingia makubaliano na Mwenye nyumba kama ifuatavyo:

a) Amelipa kiasi cha Sh.(Sh) tu kabla ya kusainiwa kwa


mkataba baina ya pande mbili husika ikiwa ni kodi ya miezi(...); kwa
kuondoa shaka, fedha hizo zimekwisha kulipwa.
b) Kutokufanya au kuruhusu au kuwezesha kufanyika kwa shughuli ambazo ni kinyume
cha sheria;
c) Kusirikiana na wapangaji wengine katika usafi wa nyumba na hasa matumizi ya
chooo na bafu;
d) Kulipa kwa kushirikiana na wapangaji wengine bili za umeme na maji (on prorata
basis)
e) Kutokurithisha au kupangisha au kutoa chumba/vyumba katika nyumba au sehemu
ya nyumba bila idhini ya mwenye nyumba;
f) Kutumia chumba/vyumba alichopangisha kwa shughuli za makazi tu;
g) Mwisho wa mkataba au panapo majadiliano ya kuendelea au kutokuendelea na
mkataba nyumba iwe katika hali na mazingira mazuri

3. Mwenye nyumba anaingia makubaliano na mpangaji kwamba

a) Mwenye nyumba au mtu yeyote mwenye haki juu ya nyumba hiyo anaahidi kutoingilia
upangaji endappo atazingatia mashariti na makubaliano yaliyomo katika
mkataba.
b) Mwenye nyumba atalipa kodi aina zote zilizopo na nyingine zitakazoikabili nyumba

4. IZINGATIWE NA INAKUBALIWA KWAMBA

a) Ikiwa makubaliano yoyote ya upangaji kwa upande wa Mpangaji hayakufuatwa au


kuzingatiwa, Mwenye nyumba atakuwa na haki kisheria kuingia katika nyumba au
sehemu ya nyumba hiyo na mkataba huu wa upangaji utatumika kuamua hatima ya
ukiukwaji huo wa makubaliano.
b) Mwenye Nyumba hatahusishwa na lolote lile endapo ajali au madhara yoyote yatatokea
kwa mpangaji au mtu mwenye ruhusa ya mpangaji/wapangaji kuingia katika nyumba
iliyopangwa, au kitu chochote, watumishi, mwakilishi au mtu yeyote au mali yoyote
katika nyumba.
c) Yeyote kati ya mwenye Nyumba au mpangaji atakuwa na uhuru wa kukatisha mkataba
huu kabla ya kumalizika kwa muda a upangaji kwa kutoa notisi ya taarifa ya maandishi ya
miezi mitatu ya kalenda na baada ya kuisha kwa muda wa taarifa hiyo mpangaji
atakabidhi chumba/nyumba kwa Mwenye Nyumba. Notisi ya mpangaji iwe ya maandishi
na katika kipindi chote cha notisi hiyo cha miezi mitatu,Mpangaji atapaswa kulipa kodi ya
pango kama kawaida.
d) Endapo utatokea mgogoro. kesi kati ya Mwenye Nyumba na Mpangaji, kodi ya nyumba
lazima ilipwe kwa wakati unaotakiwa wakati kesi ikiendelea kusikilizwa. Kesi
itakapokwisha Mpangaji anaweza kuondoka na kurejeshewa fedha zake baada ya
Mpangaji mwingine kuingia, endapo atadai aondoke kabla ya muda wa kodi yake
kumalizika. Iwapo Mpangaji atakuwa anadai kodi kabla ya kesi kuanza kusikilizwa, kodi
ilipwe kabla ya kesi husika kuanza kusikilizwa.
e) Mpangaji hatakua na ruhusa ya kutengeneza au kufanya marekebisho ya aina yeyote
katika chumba/nyumba bila kumuarifu/makubaliano na Mwenye Nyumba.
f) Kabla ya kusaini mkataba mpya,mpangaji atatakiwa kuonesha stakabadhi (risiti) ya
malipo ya awali.

5. Taarifa yeyote kwa mujibu wa mkataba huu itakua kwa mandishi na taarifa yeyote kwa
Mpangaji itachukuliwa kuwa imefika endapo imeandaliwa kwa anuani ya Mpangaji na
kupelekwa katika makazi ya Mpangaji au kwenye anuani yake ya mara ya mwisho mahali popote
pale alipokuwa katika Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania na taarifa yoyote kwa Mwenye
Nyumba itachukuliwa kuwa imemfikia yeye au mtu yeyote menye idhini yake kuipokea siku kumi
na nne ( 14) tangu itumwe kwa njia ya Posta.
INATHIBITISHWA na pande zote mbili kuwa mkataba huu umesainiwa katika tarehe na mwaka
kama inavyoonekana.

IMESAINIWA na KUTOLEWA hapa . na


Dr. GWAMBAYE O.K MWENYE NYUMBA
Mbele yangu leo tarehe.mwezi20.

Saini

Anuani

Sifa

IMESAINIWA na KUTOLEWA hapa na

.... MPANGAJI
Mbele yangu leo tarehe.mwezi20..

Saini

Anuani

Sifa

IMESAINIWA na KUTOLEWA hapa . na

.... SHAHIDI
Mbele yangu leo tarehe.mwezi20 ..

Saini

Anuani

Sifa
UMETAYARISHWA NA:-
Dr. GWAMBAYE O.K
P.O.BOX 335,
NZEGA.

You might also like