You are on page 1of 40

Paukwa

Hadithi za Zanzibar
Regionale Arbeitsstellen
für Ausländerfragen,
Jugendarbeit und Schule
Paukwa
... husikika sauti ya mtoaji hadithi, pale anapotaka kuwasalimu Fukuchani
watizamaji wake.

Pakawa Z ANZIBAR

... hiki ni kiitikio cha wasikilizaji, ambacho lazima kiwe kwa Uzini
sauti kubwa, ili kumfanya mtoaji hadithi avutiwe, na hivyo
Bambi
aanze kutoa ahadithi.
Mikunguni Uroa

Chukwani

A F R I C A

TANZANIA
ZANZIBAR
Paukwa
Hadithi za Zanzibar

Kwa wanawake na wanaume wa vijiji


vya Bambi, Chukwani, Fukuchani, Uzini na Mikunguni
ambao walisimulia hadithi zao.
Yaliyomo
Utangulizi
Soma na uwasomeshe wengine 3

Hadithi za Chukwani
Asili ya Chukwani 7
Subiri ni sali 7
Wizi mbaya 11

Hadithi za Fukuchani
Asili ya Fukuchani 13
Mtu aliyekuwa tajiri na hakubahatika kupata mtoto wa kumfaa 13

Hadithi za Uroa
Asili ya Uroa 16
Nyoka mlafi 17
Mtoto wa Makame wa Makame 20

Hadithi za Mikunguni
Asili ya jina la mtaa wa Mikunguni 21
Samaki mkubwa 21
Mume wa ajabu 23

Hadithi za Uzini
Asili ya Kijiji cha Uzini 24
Hadithi ya mfalme na waziri wake 25
Hadithi ya Makame wa Makame 26

Hadithi za Bambi
Asili ya Bambi 29
Uchoyo 30
Tusiwadharau wadogo 30

Chanzo cha hadithi 34


Shukrani 35
Utangulizi
Soma na uwasomeshe wengine
Ni mradi wa Jumuiya ya Kijerumani (RAA) iliyopo wilayani Brandenburg, Ujerumani

Mradi huu umetekelezwa kwa pamoja kati ya walimu, wanafunzi na wasimulizi wa hadithi kutoka vijijini
vya Bambi, Uzini, Fukuchani, Chukwani, Uroa na Skuli ya Mikunguni.
Mradi huu uligundua mamia ya hadithi zilizokuwa zikisubiri kusimuliwa. Ugunduzi huo ulithibitishwa na
zoezi lililofanywa na vijana kutoka wilaya ya Brandenburg na Zanzibar walipotembelea vijiji vitano, pa-
moja na Skuli ya Mikunguni iliyopo mjini Zanzibar. Kwa muda wa wiki moja walipita nyumba hadi nyum-
ba kuwauliza wazee wa kike na wa kiume juu ya hadithi zao za utotoni. Wazee walifurahia kutoa simulizi
za hadithi kuliko hata walivyofanya kwa kuangalia televisheni, video, kutumia kompyuta au kuangalia
mchezo wa mpira wa miguu. Simulizi walizotoa zimewezesha kuandikwa kwa kitabu kizima, kutokana
na hadithi ambazo wazee wa Bambi, Uzini, Fukuchani, Chukwani, Mikunguni na Uroa walizozikumbuka
na kuzisimulia.
Kwa mara ya kwanza hadithi hizo zimekusanywa na kuandikwa ili kuzihifadhi kwa ajili ya watoto na vi-
zazi vijavyo.
Ingawa vitabu vinaonekana kama kwamba siyo sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya kila Mzanzi-
bari. Hata hivyo watoto walionekana wakisoma vitabu pale walipovipata. Ukweli huo ulithibitishwa pia
na mwandishi wa vitabu, Bwana Ali Rashid aliyesema kwamba, watu wanasoma na kuvithamini vitabu
na hata kuweza kuvinunua. Kwa upande mwingine Bwana Ali Rashid alijiuliza, kwa nini watu wawe-
ze kugharimia harusi mamilioni ya fedha na washindwe kununua kitabu kinachogharimu shilingi elfu
kumi tu? Kwa nini kuwepo na fedha za kununulia mivao ya kanga tisini na mbili na kukosekana fedha za
kununulia kitabu kimoja? Bwana Rashid anaamini kwamba kutonunua vitabu hakutokani na umasikini 1
Shirika la RAA la Brandenburg.
bali kunatokana pia na kutotoa kipaumbele katika matumizi ya vitabu hivyo. Brandenburg ni sehemu iliyopo
Pamoja na ufahamu mdogo kuhusu umuhimu wa vitabu, ukosefu wa fedha katika jamii pamoja na uha- Ujerumani Mashariki.
ba wa maktaba katika maeneo ya miji na vijiji huchangia ari ya usomaji wa vitabu visiwani Zanzibar. Shirika la RAA limeundwa mwaka 1992
Mwaka 2005 misaada ilitolewa kwa skuli za Fukuchani, Chukwani, Bambi, Uzini, Uroa na Mikunguni kwa kwa madhumuni ya kupambana na chu-
kujenga maktaba za skuli au kuboresha utunzaji wake kwa kutengeneza madawati, meza na viti pamoja ki dhidi ya wageni pamoja na ubaguzi
na kununua vitabu. wa rangi, pia kutoa fursa ya kubadilisha-
na mawazo. Shirika la RAA linashirikiana
Jumla ya shilingi milioni ishirini na moja zilitumika katika skuli sita kwa ajili ya mradi huo. Mradi huu uli-
na washirika wenzake Visiwani Zanzibar
dumisha mashirikiano ya miaka kumi na tano ambayo yaliwasaidia wanavijiji kujenga madarasa sitini na
tangu mwaka 1994. Wananchi wa Bran-
saba na kupata madawati kama mchango wa kuinua viwango vya elimu.
denburg pamoja na wa Zanzibar wame-
Ni wazi kwamba makabati na vitabu peke yake kamwe hayawezi kukuza tabia au utamaduni wa kupen- kuwa wakishirikiana katika kutekeleza
da kusoma. Ndiyo maana miradi imezingatia utoaji wa elimu ya maktaba. miradi mbali mbali tangu 1994
3
Utangulizi
Kila skuli humchagua mwalimu mmoja ambaye huwa na madaraka ya maktaba. Walimu wanaohusika
hupelekwa maktaba kuu ya Zanzibar kujifunza jinsi ya kuendesha na kutunza maktaba.

Kilichovutia zaidi kilitokana na mazungumzo ya pamoja na waandishi


na wachapishaji wa vitabu ambao wanaishi Zanzibar. Bahati mbaya
waandishi wa vitabu wa Zanzibar wanakabiliwa na matatizo katika
kuchapisha vitabu wanavyoviandika. Hata wanapofanikiwa kucha-
pisha vitabu hukabiliwa na matatizo ya soko. Hii inatokana na sa-
babu mbili kubwa zikiwemo, ukosefu wa utamaduni wa kununua
vitabu na kutotoa kipaumbele katika matumizi ya vitabu hivyo.

Inawezekana pia sababu hizo zikatokana na tabia ya jamii ya kupas-


hana taarifa kwa mazungumzo yasiyoandikwa. Kwa maana hiyo mtu
hupendelea kusikiliza hadithi baada ya kuzisoma. Pamoja na yote, vi-
tabu kamwe havisababishi kupuuzwa kwa hadithi za zamani. Vitabu
havigongani na simulizi zinazotolewa na wazee. Kutokana na umuhimu
huo ndio maana mradi huu umewashirikisha wazee na hadithi zao.

Wajerumani na Watanzania walishirikiana kutafuta hadithi za zamani na wa-


lisimuliwa hadithi nyingi.

Kwa mfano huko Fukuchani tulipata kujua jinsi jina la „Unguja“


lilivyopatikana.

Muda mrefu uliopita walikuja wakazi wa bara hapa visiwa-


ni kwa boti. Walikuja mikono mitupu, bila kuleta chochote.
Wakazi wa visiwani walikuwa wazuri sana, waliwakaribisha
wageni na kuwapa vitu vizuri vya kula na zawadi za kuchu-
kua wanaporudi nyumbani. Wale wasafiri walipofika bara
waliulizwa na wenzao: Huko kisiwani kuna nini? Jawabu
ikawa: Vitu vingi! Hivyo visiwa vikapa jina lake la ‘Ungu-
ja’ kutokana na utajiri uliopo, yaani Unguja ni: Ungo na
jaa, yaani ungo uliojaa, inayoonesha utajiri wa kisiwa.

Tumepata ungo uliojaa hadithi, huu ni utajiri wenye


maarifa ya muda mrefu, ambayo tulitaka tuyapate.

Ni muhimu kuzihifadhi hadithi zenye utajiri mkubwa na


elimu iliyotokana na miaka mingi iliyopita. Hadithi nyingi
zilizokusanywa na kuandikwa zitasomwa na watu wa Tanzania,
Ujerumani na kwengineko kote duniani. Hapo mwanzo kitabu hiki cha
hadithi kiliandikwa nchini Ujerumani.
4
Utangulizi
Wakati wa Krismasi ya mwaka 2006 kampuni moja ya kompyuta iliopo mji mdogo wa Hasselfelde ili-
nunua vitabu vya hadithi kutoka Zanzibar ili kuwazawadia wateja wake kusoma hadithi hizo. Kiasi cha
wateja 130 wa Kijerumani wa kampuni hiyo waliweza kujifunza hadithi za Zanzibar. Hatimaye fedha za
kutosha zilipatikana zitakazowezesha kuchapisha vitabu 1000 kwa lugha ya kiswahili.
Teknolojia ya kisasa ya barua pepe imewezesha kurahisisha mawasiliano kati ya washiriki 200 wa miradi
ya Zanzibar iliyofanyika kuanzia mwaka 1992 hadi 2005.
Watakaosoma kitabu hiki wanapaswa kuwashukuru watu wa Zanzibar walioshiriki kutoa hadithi pamoja
na waliozikusanya. Kitabu hiki cha hadithi katika lugha ya Kiswahili kitarudisha ujumbe nyumbani visi-
wani ambako ndio chimbuko la simulizi husika.
Ni tegemeo letu kwamba vijana watakitumia kitabu kuwasomea mababu zao.
Tungependa kuwakaribisha kusoma kitabu hiki cha hadithi na kuwatakia furaha.

Birgit Mitawi,
Mkuu wa Mradi, RAA Brandenburg,
Berlin, Zanzibar 2007

5
Hadithi za Chukwani
Asili ya Chukwani
Imesimuliwa na Mzee Suleiman Khamis Faraji

Hapo zamani katika kijiji hiki waliishi watu, sio wengi sana kwani nyumba zilihesabika. Miongoni mwa
watu hao alikuwepo bibi na wajukuu zake ambao aliwapenda sana na aliwapa kila walichotaka amba-
cho aliweza kukimiliki. Kwa bahati mbaya kijiji hiki kilikuwa hakina jina.
Siku moja wale watoto walikiona kitu ndani ya nyumba yao. Kile kitu yule bibi alikihitaji na wale wali-
kipenda sana kile kitu kiwe chao. Kwa hivyo walimshika sana bibi yao awape kile kitu kwa kusema, bibi
Suleiman Khamis Faraji
tupe we, bibi tupe. Yule bibi aliwanasihi wale watoto wawe na subira kwani subira huvuta heri.
Kutoka Chukwani ana umri wa miaka
Lakini wale watoto kwa pupa za kukitaka kile kitu waliendelea kumshikilia bibi yao awape kile kitu mpa- 80 Ameacha kuwa sheha wa kijiji
ka akakasirika na kuhamaki sana. Kwa ukali yule bibi aliwambia wale wajukuu zake maneno yafuatayo: miaka miwili iliyopita na kupata
- Chukwani kwa maana ya kuwa wachukue – kile walichokuwa wanakihitaji. wakati wa kutosha kusimulia hadithi.
Kwa bahati nzuri walipita watu karibu na ile nyumba nakusikia yale maneno anayozungumza yule bibi
na wajukuu zake kwa hasira pamoja na yale maneno aliyoyasema „Chukwani.“ Kwa hivyo walipokuwa
wakipita karibu na ile nyumba ya yule bibi husema; „Bibi Chukuwani leo yupo?“ Nao humsalimia na
kwenda na safari zao. Ile hali ikaendelea kwa muda mrefu mpaka yule bibi alipofariki. Ile sehemu watu
wakaipa jina kutoka lile neno chukuwani na kuliita eneo hilo „Chukwani.“ Ndio maana hadi sasa eneo
hilo linaitwa kijiji cha Chukwani.

Subiri ni sali
Imehadithiwa na Khalfan Mwita

Hapo zamani za kale alikuwepo mfanyabiashara ambaye aliheshimika kama mfalme wa mji. Alikuwa na
wafanyakazi wa kila aina.
Siku moja alipokuwa akijiandaa kwenda nchi za ng’ambo kwa ajili ya shughuli za biashara aliwaita wa-
toto wake saba na kuwaambia;„wanangu mimi ninasafiri nakwenda katika shughuli za kibiashara, lakini
ninachotaka kwenu ninyi ni kuwa na tabia nzuri ambayo haitawaudhi watu wengine, muwe na heshima
na kupendana.” Hivyo kila mmoja alimpa kioo cha kujionea ambapo atakayekwenda kinyume na mam- Khalfan Mwita
bo aliyoyasema baba yao kioo chake kitafifia na hakitaonesha kitu. Kutoka Chukwani ana umri wa
miaka 34. Anafanya kazi ya ualimu
Hapo mfanyabiashara yule alifunga safari na kuwaacha watoto wake pamoja na mama yao. Kawaida
na anazipenda hadithi alizosimuliwa
mfanyabiashara huyo anaposafiri huondoka na wafanyakazi wengine pamoja na makuhani yaani wa-
na babu yake ambazo huendelea
ganga wa kienyeji.
kuwasimulia wengine skuli.
Lakini wale watoto walisahau, na wakaanza kwenda kinyume na mambo waliyoambiwa na baba yao. Ku- Ana mtoto mmoja.
7
Hadithi za Chukwani
likuwepo na watoto sita watundu na hawasikii wanayokatazwa na wakubwa zao, isipokuwa mdogo wao
wa mwisho tu ndiye ambaye alikuwa mtiifu na alisikiliza na kufuata yale waliyoambiwa na baba yao. Kadiri
siku zilivyoenda wale watoto wengine walizidi kuwa wakorofi na hatimae vioo vyao vilianza kufifia na vika-
wa havitoi taswira yoyote isipokuwa kile kioo cha mtoto wa mwisho ambaye yeye alikuwa mtiifu.
Baada ya muda kupita ililetwa taarifa kuwa baba yao anategemea kurudi. Walipopata taarifa zile wato-
to sita waliokuwa wakorofi waliingia hofu kwani waliambiwa atakaporudi baba yao atakaeonekana na
kioo kilichofififa atakatwa kichwa. Hivyo walivyosikia habari za kurudi kwa baba yao waliogopa sana na
wakawa wanamuonea kijicho mdogo wao, walimtenga, wakawa hawampendi na walimchukia sana.
Oh, siku ya kurudi kwa mfanyabiashara huyo iliwadia, na kama kawaida anaporudi hupigiwa mizinga
kwa kumpa heshima na baada ya kupokea heshima hiyo alielekea kwenye vyumba vya watoto wake
kuangalia vioo.
Hapo watoto wake sita walikuwa wanaogopa sana na mwisho walipanga mpango wa kukichukua kioo
cha mdogo wao. Mipango yao ilifanikiwa kwa kukibadilisha na kumuekea kioo kilichoharibika.
Mara baba yao alianza kuvikagua vioo kwa kupitia katika kila chumba. Alianza chumba cha mtoto wake
wa kwanza na alipokiona kioo alifurahi sana na kumpongeza kwa tabia nzuri aliyo nayo. Alipokua aki-
toka walikirudisha kioo na kukiingiza katika chumba chengine alipoingia mfanyabiashara kwa mtoto
mwengine naye alipongezwa kama alivyopongezwa yule wa mwanzo. Walifanya tendo la kubadilisha
kioo hadi chumba cha mtoto wa sita na mzee alifurahishwa sana kwa jinsi alivyoviona vioo vya watoto
wake.
Mambo yalibadilika alipoingia chumba cha saba ambacho ndio cha mwisho, kioo kilikuwa kimebanduka
sana na mfanyabiashara alikasirika sana. Ndipo alipowaita wafanyakazi na akawaamrisha wamchukue
mtoto yule wampeleke msituni wakamchinje na baadae watie damu kwenye kifuu wamleletee kama ni
ushahidi.
Wafanyakazi walitii amri ya mkuu wao na wakamchukua mtoto na kwenda naye msituni, lakini walipofi-
ka msituni walimuonea huruma kwa kuwa walimuona yule mtoto alikuwa mtiifu sana. Hivyo walitafuta
paa na kumchinja na kuchukua damu yake kwenye kifuu ili kumuonesha mfanyabiashara huyo na baa-
dae walimtafutia chakula yule mtoto na kumjengea kibanda cha kujihifadhi. Hapo ndipo wakarudi na
kumuonesha mfanyabiashara damu ndani ya kifuu na mfanya biashara aliridhika.
Mara alifunga safari nyengine na aliwaita watoto wake na kuwataka kila mmoja aagize zawadi anayoi-
penda.
Kama kawaida alisafiri kwa kutumia meli na meli ile ilipofika katikati ya bahari ilikwama na ikawa haiwe-
zi kwenda mbele wala kurudi nyuma. Na mfanyabiashara aliwaita makuhani ili wapige ramli. Makuhani
walipiga ramli na wakasema:„Wewe una watoto saba, lakini watoto sita umewaambia waagizie zawadi,
mtoto mmoja hukumwambia, hivyo unatakiwa urudi ukamuulize ili safari yako iweze kuendelea.”
Mfanyabiashara alikasirika sana, lakini ilibidi arudi na akawauliza wafanyakazi kwa nini hawakumuua
8
Hadithi za Chukwani
yule mtoto? Na ndipo akawaambia wafuatane na mkewe wakamuulize nini anataka haraka sana maana
anachelewa safari yake.
Mama yule alifunga safari pamoja na wafanya kazi mpaka alipofika sehemu ambayo mtoto alikuwa ana-
kaa, kwa bahati yule mtoto alikuwa anataka kusali akamwambia „Subiri ni Sali.” Mama alifahamu mwa-
nawe anataka zawadi ya „subiri ni sali” na mama akarudi nyumbani na kumuelezea zawadi anayoitaka.
Mzee alisafiri na baadae alinunua zawadi za watoto wake na kurejea nyumbani lakini alipokuwa katikati
ya bahari meli ilikwama tena na wakaitwa makuhani ili kutabiri. Makuhani walisema:„wewe una wato-
to saba lakini umenunua zawadi za watoto sita na mmoja umemsahau, hivyo hutaweza kuendelea na
safari yako mpaka uipate zawadi ya huyo mtoto.”
Mzee alianza kuhangaika kutafuta zawadi kila duka aliulizia „subiri ni sali” lakini hakuipata na alikuwa
amechoka sana hadi siku moja alikuwa anapita chini ya nyumba moja akipiga kelele „subiri ni sali“. ali-
tokea msichana mmoja na akampa ubawa na akamwambia auchome baada ya kusali na atapata „subiri
ni sali”.
Mzee alichukua ubawa ule na akarudi nchini kwake na alipofika akamuagizia mkewe ampelekee zawadi
yake na akamwambia achome kidogo tu atapata „subiri ni sali”. Mama akapeleka ubawa ule kwa mtoto
na akamwambia afanye alichoagizwa, mtoto alishangaa. Kwani yeye alimtaka mama asubiri amalize ku-
sali. Lakini mtoto aliupokea ubawa ule na mama yake akarudi nyumbani.
Hivyo ilipofika jioni baada ya kumaliza kusali alichoma sehemu ndogo ya ubawa ule. Alitokea msichana
mzuri ambae alikuwa wa ajabu. Oh! Alikuwa mzuri mno wa umbo na sura utatamani umuangalie jinsi
alivyoumbika, matiti kama ncha ya msumari.
Msichana alimuuliza yule kijana;„kwa nini unakaa msituni peke yako?” Na yule mtoto alimuelezea mkasa
uliompata mpaka akawa anaishi msituni. Baadae wakawa marafiki, na kila jioni alichoma ubawa na yule
msichana mzuri alitokea. Waliendelea hivyo hivyo mpaka wale ndugu zake sita walipajua alipokuwa
anakaa ndugu yao.
Siku moja walimuona yule msichana na walimuonea wivu na wakapanga njama za kutaka kumuua yule
msichana. Hivyo walipokutana na mdogo wao walimwambia amuulize yule msichana;„akitaka kuuliwa
kwa haraka afanye nini?” Yule mtoto alimuuliza na yule msichana alikasirika sana lakini kwa kuwa ali-
kuwa anampenda sana alimwambia;„ukitaka kuniua kwa haraka nikikanyage kigae; mimi nitakufa kwa
haraka.” Siku ya pili yule mtoto aliwasimulia kaka zake.
Siku moja alipokuwa akirudi katika shughuli zake alikuta vigae chini ya mlango, na yule mtoto
alivikusanya na kuvitupa. Kumbe kilibakia kipande kidogo cha kigae chini ya mlango na alipokuja yule
msichana akakikanyaga kigae kile na kikamkata. Kwa huzuni yule msichana akamtaka achome ubawa
ili apate kurudi nyumbani kwao. Masikini msichana mzuri alitoweka kwa huzuni na maumivu makali
aliyokuwa nayo.
Sasa yule mtoto kila akichoma ubawa, yule msichana akawa hatokei. Alichukuwa kipindi kirefu sana. Na
mara alipata habari kuwa baba yake amefariki. Baada ya siku nyingi kupita, siku moja alifunga safari ya
9
Hadithi za Chukwani
kwenda kumtafuta „subiri nisali”. Alichukua chakula na maji kwani alisafiri kwa miguu na kuwa muda
mrefu. Baada ya machofu ya muda mrefu, alipofika mahali pamoja akaona mti na aliamua kwenda
kupumzika kwa ajili ya kupata chakula na mara usingizi mzito ulimchukua. Alipozindukana alisikia
sauti za ndege wa ajabu wanaongea.„Mtoto wa mfalme anaumwa lakini ukichukua majani ya mti huu,
ukimpulizia atapona haraka sana.”
Hivyo kijana aliposikia vile aliinuka haraka sana na akatoa chakula chake chote na akatia majani.
Alipofika mtaani aliona mabango yanasema binti mfalme anaumwa lakini atakaemtibu atamuoa na
kama atashindwa atakatwa kichwa.
Yule mtoto alikwenda hadi kwenye kasri la mfalme na akajitangaza yeye anaweza kumtibu binti wa
mfalme. Wafanyakazi walimuonesha vichwa vya watu waliokatwa, lakini yule mtoto alisema ataweza
kumtibu.
Hivyo alichukuliwa hadi ndani ya nyumba ya mfalme na akafikishwa kwa mfalme. Mfalme alimuita
yaya ili ampeleke katika chumba cha „subiri nisali”. Alipofika akatoa dawa yake akampulizia, mara „Subiri
nisali” aliinuka kitandani alipolala na alipona na kila mmoja alishangaa kumuona „Subiri nisali” amepona.
Hapo „Subiri nisali” alifuatana na yule kijana hadi kwa baba yake. Mfalme alishangaa na alifurahi sana
na akasema huyu ndie atakaekuoa. „Subiri nisali” alimwambia baba yake kuwa maradhi aliyoyapata
yalisababishwa na huyo mtoto.
Mfalme alikasirika na akaamrisha auliwe lakini yule kijana alisema sio mimi niliyefanya kitendo hicho,
ndugu zangu ndio waliofanya hivyo. Mfalme alitaka apelekwe waliko watoto hao na alipofika aliwakata
vichwa wote sita na baadae ilifanywa arusi na mwisho akatawazwa kuwa mfalme. Wakaishi kwa raha
mustarehe.

10
Hadithi za Chukwani
Wizi mbaya
Imesimuliwa na Zubeda Abdalla Omar

Alitokea Chanjagaa akajenga nyumba akakaa, mwanangu Mwanasiti kijino kama chikichi, cha kujengea
vikuta na vilango vya kupita.
Hapo zamani za kale alikuwepo bwana mmoja, aliekuwa na wake watatu mmoja alikuwa mwizi. Yule
bwana alikuwa anafuga mbuzi, siku moja kati ya wale wake zake mmoja aliiba mbuzi na kumchinja na
kumpika bila ya yeye kujua. Aliporudi safari yake aliuliza nani alimchinja mbuzi? Wote walikataa. Yule Zubeda Abdallah Omar
bwana akasema basi mimi nitafanya dawa. Wakajibu sawa, yule bwana akafanya mambo yake kisha Kutoka Chukwani ana umri wa miaka
akawapeleka mtoni. Walipofika aliwambia mmoja mmoja aanze kuingia mtoni na huku akiimba. 47. Yeye ni mama wa nyumbani.
Amesimuliwa hadithi na mzee wa
Aliingia wa kwanza huku akiimba nyimbo:
Kingoni, Ambaye alikuwa jirani yake
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Alipomaliza kuimba akaibuka, kwani yeye hakuwa mwizi. Akafuata wa pili huku akiimba:
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Yeye pia akaibuka na kukaa pembeni. Akafuata yule wa tatu akaingia huku akiimba:
Kachiriri, kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Mani nenga Kachiri
Depala dipolo kachiri
Dipolo dabambo kachiriri
Kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri kachiriri.
Lakini yeye alizama.
Kuona vile yule bwana akajua kwamba yule mke wa tatu ndie mwizi. Hapo akafanya dawa zake na yule
bibi akaibuka, alimuomba radhi mumewe na kuahidi kuwa hatorudia tena kosa lake. Na yule bwana
alikubali na wakaendelea kuishi kwa raha mustarehe.

11
Hadithi za Fukuchani

12
Hadithi za Fukuchani
Asili ya Fukuchani
Imesimuliwa na Pandu Mkoba Faki

Jina hili la Fukuchani lilikuwa lipo tangu zamani lakini tu lilikuwa halijuikani kama linavyoeleweka leo:
Sehemu ya kijiji hiki ilikuwa pahali penye mchanga mwingi kwa kiasi ambacho watu wengi wanapopita
kwenye mchanga huo ilikuwa hawapati hatua nzuri katika mwendo wao.
Kwa hali hii watu wengi walikuwa hawapiti hapo na walikuwa hupitia sehemu au njia nyengine amba-
ko huko walikuwa wanakuita Bonde Uyongo. Huko ilikuwa ni sehemu nzuri na walikuwa wakipita vizuri Pandu Mkoba Faki
sana. Kutoka Fukuchani ana umri wa mia-
ka 73. Yeye ni mvuvi.
Kutokana na wengine kupitia kwenye mchanga na wengine kupita Bonde Uyongo hapo walikuwa wa-
kiulizana mbona nyinyi mmekawia yaani kwa maana ya kuchelewa? Na hapo walipokuwa wakiulizana
na majibu yao yalikuwa,„Sisi tumechelewa kidogo kwa sababu hatuendelei vyema, kuna fukacha, yaani
mchanga mwingi. Kwa hiyo lazima twende kwa kufukuchuyo (kidogo kidogo).”
Kwa hiyo jina hilo likaselelea kuwa ni Fukuchani hadi hii leo.

Mtu aliyekuwa tajiri na hakubahatika


kupata mtoto wa kumfaa
Imesimuliwa na Ngwali Mashaka

Hapo zamani za kale alikuwepo bwana mmoja aliyekuwa akiitwa Hassan Saira. Bwana huyo alikuwa ni
tajiri sana kwa wakati wake.
Vile vile alikuwapo mtu mmoja katika kijiji hicho ambae ni masikini sana bwana huyo alikuwa akiitwa
Bwana Vuai Pandu.
Bwana Hassan ni mtu mmoja wapo aliyepewa uwezo mzuri na Mwenyezi Mungu. Bwana huyo alioa na
akapata mtoto mmoja wa kiume aliyeitwa Maulid. Ngwali Mashaka
Kutoka Fukuchani ana umri wa
Mtoto wake huyo alikuwa ni mgonjwa, lakini moyo wake ulipenda amuozeshe na huenda ikawa bahati
miaka 77. Yeye ni mganga wa
nzuri akapoa na kupata mtoto ambaye aliweza kumfaa babu yake. Bwana Hassan alikwenda kwa jirani
kienyeji na anapendwa kutokana
yake Bwana Vuai Pandu ambaye alikuwa na watoto wengi wake na waume. Bwana Hassan alikwenda
na kusimulia hadithi.
kuposa katika nchi moja wapo ya kifalme na kumwambia mzee Vuai kuwa mtoto wangu nimemposea
lakini ni mgonjwa haifai kuonekana. Lakini nimekuja kwako unipe mtoto wako mmoja aitwae Yunus.
Bwana Vuai alisema na kumwambia Bwana Hassan mimi mtoto wangu ni masikini jee atawezaji kufika
13
Hadithi za Fukuchani
kutoka nchi hizo za kifalme na akaonekane kuwa ni mtu? Bwana Hassan alijibu kuwa ataonekana kuwa
ni mtu, usijali.
Bwana Vuai alimuelezea mkewe Bibi Khadija kadhia hiyo. Bi. Khadija alimwambia mumewe jee haitakuwa
taabu baada ya kwishakuoana, kwa sababu kila mmoja atakuwa anampenda mwenziwe? Mzee Vuai
alisema si tatizo nitamnasihi sana baada ya kurudi hapa tu kuwa amwache. Hapo alimwambia asili
ya kukwambia hayo sisi hapa ni masikini tusipokubali anaweza hata kutufukuza, tutafanya nini? Kwa
hiyo ni bora tukubali. Baada ya maneno hayo Bi Khadija aliridhika na Bwana Vuai alipeleka jawabu kwa
Bwana Hassan Saira kuwa ameridhika kumpa mtoto wake. Na hapo ilifanywa safari, akasafiri kwa meli,
huku mtoto wa Bwana Vuai akapambwa na kuonekana ni mtoto wa mfalme. Pia askari walichukuliwa
wakenda kwenye harusi.
Mizinga ilisikika siku ile ya kupokewa bwana harusi na kukaribishwa wapite ndani ya kasri ya Mfalme.
Gari nyingi za watu zilikuja katika sherehe hiyo na mtoto wa mfalme akachukuliwa na kufanyiwa kama
ilivyo ada ya harusi na wafalme wote waliohudhuria walifurahi sana kwa kupata mchumba mzuri wa
kifalme.
Baada ya hapo ilifanyika safari ya kurudi nyumbani ambapo alikabidhiwa watumishi mbali mbali,
wa kike na wanaume. Mizinga ya harusi ya kurudi ilisikika na watu wote walikuja kumpokea harusi.
Shangwe na vigelegele vilizagaa mtaani kwa Bwana Hassan Saira. Na walipofika maharusi nyumbani
kwao watu walikaa na kushereheka usiku wa kucha.
Ilipofika siku ya pili Bwana Vuai alikwenda kuomba kuonana na mwanawe Yunus. Yunus hakupinga amri
ya mzee wake na hapo Yunus akamuaga mkewe kuwa anakwenda kuangalia bustani zake na alitoka nje
kwa muda mchache na hatimayae mtoto wa mfalme akaletewa mume mwengine na kuambiwa huyu
ndie mumeo. Bi harusi alisema huyu siye mume wangu niletewe mume wangu na hapo alilia kwa muda
mrefu na kilio kilizagaa katika nyumba mpaka watu wote wakatetemeka.
Aliitwa Bwana Hassan na kuelezwa kuwa Bi harusi hataki lolote na anataka kurudi kwao au aletewe
mume wake kwani aliyeletewa siye mumewe halisi.
Bwana Hassan alipofika mabibi wa nyumbani walimwambia utuletee mume wetu kwa haraka. Si hivyo
tunakwenda zetu. Ikabidi Bwana Hassan kusema kuwa huyu ndiye mume wako lakini bibi harusi
akasema aitwe baba yake mzazi. Bwana Hassan alipeleka barua ya ugonjwa ili kumrudisha kwao kwa
sababu tu hataki kukaa na mume aliyekuwa siye aliyeozeshwa.
Mfalme alipopata barua na kufika kule nyumbani aliletewa mwanawe. Baada ya kuzungumza na watu
wa nyumbani alihisi kuwa hana sifa ya ugonjwa. Hivyo bwana mfalme aliandika barua ya kumshitaki
Bwana Hassan kwa kitendo alichokifanya ambacho si cha ukweli. Bwana Hassan alishitakiwa na
kutakiwa kulipa fidia kwa kitendo alichokifanya cha kuozeshwa mtu mgonjwa .
Bwana Hassan alikubali na kulipa fedha pamoja na masharti yote aliyopewa.
Baada ya hapo mtoto wa mfalme alimwambia mzee wake kuwa alifanya hadaa tu kumletea mtu mzima
14
Hadithi za Fukuchani
na baadae kupewa mbovu, kwa hivyo mimi ninamtaka yule niliyeozeshwa mwanzo. Nina hakika bado
kijana yule hajafa katika nchi ile, hivyo nikaozeshwe yule yule na niletewe mwenyewe.
Kwa kweli mfalme alisononeka sana kwa kitendo hicho kwa sababu mtoto wake alikuwa hali wala
halali.
Mfalme alitoa askari na kwenda kwa Bwana Hassan Saira na kumtaka apewe yule kijana aliyekuja
kumuozesha mwanawe na wampeleke kule aliko mwana wa mfalme. Hapo Bwana Hassan alikwenda
kwa Bwana Vuai na kumwambia kuwa mfalme amekuja na anamtaka yule kijana wako tumpelekee.
Lakini Bwana Vuai alimwambia Bwana Hassan kuwa mwambie mfalme aje mwenyewe na asitume
askari. Baada ya hayo askari walipeleka ujumbe na mfalme akaja kutokana na shida ya mwanawe.
Mfalme baada ya kufika kwa Bwana Hassan, akapelekwa kwa Bwana Vuai Pandu. Bwana Vuai alitakiwa
kumwita mtoto wake ili waende pamoja. Walipofika alisema; „nasikia umetuma ujumbe kuwa nije
mwenyewe nisitumize mtu yeyote, kwa hivyo tayari nimekwishafika.” Hapo Bwana Vuai alisema huyu
ndie mtoto wangu alichukuliwa kwa hadaa ili kuozeshwa mtoto wako.„Jee wewe ukiangalia anastahiki
kuchukuliwa kuja huko?”
„Unakuja kuchukua mtoto wangu, kutokana na umasikini tulio nao hebu twende ukaangalie nyumba
yetu ilivyo tunavyoishi,” alisema. Mfalme alikubali hayo yote na baada ya kufika aliona nyumba yao
na alimwambia warudi tena kwa Bwana Hassan. Na baada ya kufika aliamrisha aletewe yule mtoto
aliyekuwa mgonjwa, kwa kweli mfalme alisikitika sana baada ya kuona hali yake.
Baadae mfalme alizungumza na Bwana Vuai juu ya shida iliyompata kutokana na mtoto wake, hivyo
ninakiri umasikini wako na kwamba nitakujengea nyumba yako na nitakusaidia kama ipasavyo
lakini mtoto wako amuoe mtoto wangu, kwa sababu ninaridhika vya kutosha. Na hapo Bwana Vuai
alikubaliana na mfalme na wakaandikiana mkataba kuhusu hayo waliyoyazungumza.
Ilipofika siku ya sita mfalme alifika na zana zote, na kuanza shughuli za ujenzi. Na baada ya siku kidogo
nyumba ilimalizika na kwenda kufunga ndoa. Hapo tena baada ya ndoa mtoto wa mfalme alipoa
matatizo yake na hatimae mtoto wa Bwana Vuai alipewa mali nyingi sana na mfalme na unyonge
pamoja na umasikini waliokuwa nao awali ukaondoka na akawa wakati wowote anaruhusiwa kwenda
kuwaona wakwe zake.

15
Hadithi za Uroa
Asili ya Uroa
Imehadithiwa na Haji Abdallah

Hapo zamani za kale alikuwepo Makame wa Makame, alikaa na akaamua kutafuta mke na wakabaha-
tika kupata watoto wawili, mwanamke mmoja na mwanamme mmoja. Wakalelewa mpaka wakakuwa,
na yule mtoto wa kiume akaenda baharini, akawaona wageni wengi wamehudhuria katika eneo lile na
Haji Abdallah walianza kumuuliza hapa ni wapi? Na wakati huo bado hapajajuulikana jina lake, na yule mtoto aliogopa
Kutoka Uroa ana umri wa miaka na kurudi nyumbani na kwenda kumhadithia mama yake, na yule mama mtu alimjibu, hapa hapajuulika-
sabini. Hadithi alizosimulia ni jina lake, na siku ya pili walitokezea tena na kumuuliza kama mwanzo, na akajibu mimi silijui jina lake,
zimetolewa na babu yake. na siku ya tatu hivyo hivyo.
Siku ya nne alienda tena baharini, na wale watu wakamwambia kesho tutakuja utwambie jina la hii se-
hemu, aliendelea kumwambia nyinyi mnakaa sehemu hamuijuwi jina lake? Wakati huo watu walikuwa
wanasafiri kwa majahazi, wakaja watu waliokuwa wanaitwa Madeburi, na wakawa wanamfuata mfalme
na kumletea biashara. Siku moja walikaa wale Madeburi na kuulizana huu si ujinga tunaoufanya? Sisi
tunakaa sehemu hatuijui jina lake na yule tunaempelekea tunamjua ni mfalme tu, jee akatunyanganya
tutafanya nini?
Wakaendelea na biashara yao mpaka siku moja wakaja kwa yule mfalme, na kumwambia tunataka hii
nchi yako kuipa jina. Mfalme alikataa akawambia nyinyi leteni mali tu kwanza, wakaendelea kuleta mali

16
Hadithi za Uroa
na kurudi kwao. Mara nyengine walipokuja tena walikaa na kusema huyu mbona anasema hivi hata-
ki kutunyanganya, lakini ukitizama hii nchi yake mwenyewe mbona hataki kutupa jina lake? akauliza
mmoja wao jee tutaenda kumshtiki wapi atapotunyang‘anya? Hapo Madeburi waliamua kugoma kuleta
mali, na wakaondoa chombo chao na kuondoka. Mfalme kuona vile alimtuma mwanawe kwenda kuwai-
ta waje kutoa jina lakini walikataa. Ikatokezea siku moja wakaja na mali nyingi katika chombo chao, wa-
kakiweka kwenye ukingo wa bahari na wao wakashuka bila ya mali kuiteremsha. Wakaenda kwa mfalme
kwa bahati hakuwepo, kahama. Wote kwa pamoja walisema “Hii hasara, mfalme ashatunyang‘anya na
hapo likatolewa jina na kuitwa ,Urowa‘”.

Nyoka mlafi
Imehadithiwa na Hassan Mambo Kombo

Hapo zamani za kale palikuwepo na visima, baadhi ya siku vilikuwa vinakauka maji kama kule Chukwani,
watu wanakosa maji, na kule kwenye kisima cha Uwamba hakukauki maji lakini hakwendeki kuna nyoka
mkubwa, na nyoka huyo ana vichwa saba. Hakwendeki, kila mtu anaogopa. Wanakijiji wakasema sasa
maji hatuna tutafanya nini?
Hassan Mambo Kombo
Kwa bahati walihamia watu, wakazaa mpaka na wao wakafa, wakabakia watoto wao wawili Makame Kutoka Uroa ana umri wa miaka
na Miza. Lile joka likaja kumposa Miza hapo wakaulizana si ataenda kumla huyu, wakamruhusu kwanza sabini. Hadithi imesimuliwa na babu
aende, wakabakia kushauriana. Joka lile likarudi, wakaamua bora wakubali ili wayapate yale maji, yake.
wengine walipinga kwa kuhofia kuliwa mtoto wao, hadi siku ya saba wakakubali na harusi ikapangwa.
Siku ya harusi kuwadia kucha hawakulala, wakachimba shimo kubwa likajazwa kuni na juu likazibwa
vizuri bila kujua kwamba pana shimo na harusi ilipangwa saa nne. Ilipotimia saa tatu ulikolezwa moto.
Karibu ya lile shimo aliwekwa bibi harusi na pale kwenye shimo pakatandikwa mikeka mizuri kwa ajili ya
bwana harusi. Alipokuja tu bwana arusi akakaa na bibi harusi na bibi harusi akaanza kusema:
Huja masikini bwana wangu hujaaa weee huja
Nipe pete yangu, moja hujaaa weee huja
Nikuoneshe mguu wako, hujaaa weee huja
Na joka likaitikia.
Huja weee masikini bibi yangu hujaaa weee huja
Shika pete yako moja, hujaaa weee huja
Unioneshe mguu wangu, hujaaa weee huja
Joka likatoa pete na yule bibi harusi akaimba tena.
Huja weee masikini huja bwana yangu hujaaa weee huja
Nipe pete yangu, moja hujaaa weee huja
Nikuoneshe mkono wako, hujaaa weee huja
17
Hadithi za Uroa

18
Hadithi za Uroa
Na joka likaitikia.
Huja weee huja masikini bibi wangu hujaaa weee huja
Shika pete yako moja, hujaaa weee huja
Unioneshe mkono wangu, hujaaa weee huja
Hapo akafunuliwa mkono wake na akapewa pete.
Huja weee huja Masikini bibi yangu hujaaa weee huja
Nipe pete yangu, moja hujaaa weee huja
Nikuoneshe sikio lako hujaaa weee huja
Huja wee huja Masikini bibi yangu hujaaa weee huja
Shika pete yako moja, hujaaa weee huja
Unionesh, Masikini bwana wangu hujaaa weee huja
Nipe pete yangu moja, hujaaa weee hujaaa
Nikuoneshe uso e sikio langu hujaaa weee huja
Akapeleka pete ile akaoneshwa shikio. Akaendelea kuimba na bibi akaitikia:
Hujaaa weee hujaaa wako, hujaaa weee hujaaa
Tayari moto ukaanza kumpata akaanza kuomba maji ya kunywa.
Nikuoneshe uso wako hujaaa weee hujaaa
Na yeye akaitikia.
Huja weee hujaaa masikini bibi wangu hujaaa weee hujaaa
Shika pete yako moja, hujaaa weee hujaaa
Unioneshe uso wangu, hujaaa weee hujaaa
Kuomba tena maji ya kunywa. Akaendelea kuimba tena.
Hujaaa weee hujaaa, Masikini bwana wangu hujaaa weee hujaaa
Nipe pete yangu moja, hujaaa weee huja
Nikuoneshe nywele zako, hujaaa weee hujaaa
Na yeye akaitikia kwa sauti ya chini, joto lilikuwa lishampata.
Masikini bibi yangu, hujaaa weee huja
Shika pete ylako moja, hujaaa weee hujaaa
Nikuoneshe nywele zak,o hujaaa weee hujaaa
Akapeleka pete na hapo ikawa tayari amekwishachoka anatapatapa akajitumbwikiza kwenye moto.
Hapo watu wote wakakusanyika wakaanza kumfukia kwa dongo na mawe mpaka likawa halionekani.
Na wakafurahi kwa mpango wao kufanikiwa na wakaanza kutumia maji bila ya hofu.

19
Hadithi za Uroa
Mtoto wa Makame wa Makame
Imehadithiwa na Subira Abassi

Hapo zamani za kale alikuwepo bwana mmoja akiitwa Makame wa Makame, akajenga nyumba na aka-
tafuta mke akaowa. Walikaa na walibahatika kupata mtoto wa kiume. Waliendelea kuishi na wakatafuta
paka wakafuga, na hatimae paka huyo akawa mkubwa na nunda na akawala watu wote pale kiamboni,
na zile nyumba za mtaani zikawa tupu, hazina watu, mpaka Makame wa Makame pia akaliwa, na alibakia
yule mke mtu na mtoto wake tu.
Subira Abassi Waliishi yule mtoto na mama yake siku moja mtoto alimuuliza mama yake „Mama mbona nyumba zote
Kutoka Uroa ana umri wa sitini hizo haziishi watu?”. Mama mtu alimjibu mwanawe;„Mwanangu we hapo zamani baba yako alikua ana-
Amesimuliwa hadithi akiwa mtoto fuga paka sasa yule paka kageuka nunda na amewala watu wote mpaka baba yako ameliwa isipokuwa
na babu yake. sisi tu ndio hatukuliwa na paka huyo.”
Yule mtoto alimwambia mama yake atafutiwe vibuyu saba na manda saba, akatafutiwa vibuyu saba
vya maji na manda saba na akapewa mshale wa baba yake. Mtoto huyo aliondoka na kuelekea mwituni,
akaranda, siku ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne, ya tano, ya sita hadi siku ya saba akamkuta kima akam-
piga alimchukua na alirudi nyumbani kwao huku akiimba.
Mama wee ndie huyu nunda mla watu eee mama
Aliimba mpaka alipofika kwao alikua akiimba nyimbo hiyo. Na Mama mtu alimjibu mwanawe.
Mwanangu wee sie huyo nunda mla watu watu eee mwana eee
Baada ya siku mbili mtoto alimuagiza mama yake amtafutie vibuyu vyengine saba vya maji na manda saba,alipewa,
akatoka akenda kule msituni akamkuta paa akampiga, akamchukua na kurudi kwao huku akiimba nyimbo.
Mama wee ndie huyu nunda mla watu eee mama
Mama mtu akamjibu mwanawe.
Mwanangu wee sie huyo nunda mla watu
Alipofika akaambiwa siye. Akakaa siku mbili akapumzika. Hapo akasema, siji mpaka nije nae, akahan-
gaika mpaka ikafika siku ya saba vilipomalizika vitu vyake, maji na manda, alimkuta mnyama mkubwa
sana akampiga, akaenda nae na alipofika nyumbani akaanza kuimba.
Mama wee ndie huyu nunda mla watu eee mama
Na mama mtu akamjibu mwanawe.
Mwanangu wee ndie huyo nunda mla watu
Hapo akamuweka mpaka asubuhi. Ilipofika asubuhi akatafutiwa chai na alipomaliza akauliza kisu cha
baba kipo wapi? Akapewa kile kisu akampasua kwa bahati mbaya ndani ya lile tumbo alikuwemo baba
yake akamtoga kisu cha jicho, hapo wakatoka watu wote aliowameza, ikisha wale watu waliuliza iliku-
waje? Mama mtu akajibu;„alisema apewe mshale wa baba yake akamtafute huyo mnyama aliemeza
watu, na huyu mtoto ndie aliekutafuteni hadi kufika hapa, kila mtu akaenda nyumbani kwake wakam-
pa vitu walivyojaaliwa navyo.”
Na baba mtu akauliza kwa nini watu wote wametoka salama isipokuwa mimi nimetoka jicho moja?
Hapo watu akamuombea yule mtoto na akasamehewa.
20
Hadithi za Mikunguni
Asili ya jina la mtaa wa Mikunguni
Imesimuliwa na Murshid Rashid

Historia ya jina la mtaa wa Mikunguni imeanzia mbali sana. Hapo kabla ya jina hilo kulikuwa na mti
mkubwa uitwao mkungu. Mti huo ulitumika kwa ajili ya kivuli kwa watu ambao walikuwa wanakwenda
mazikoni kwa wakati huo.
Mti huo ulikuwepo nje kidogo ya ukuta wa Skuli ya Mikunguni. Kutokana na umaarufu wa mti huo mtaa
huo ulijulikana kwa jina la Mkunguni. Murshid Rashid
Kutoka Mikunguni ana umri wa
Kwa bahati miti ya aina hiyo ya mikungu iliendelea kupandwa na kuwa mingi kuelekea bondeni mwa
miaka 65. Ana watoto wawili na
barabara hiyo ya Mikunguni iliyokuwepo sasa.
mara zote huishi pamoja na wajukuu
Kutokana na wingi huo wa miti hiyo ya mikungu jina nalo likabadilika kutoka Mkunguni hadi Mikungu- nyumbani.
ni.

Samaki mkubwa
Imesimuliwa na Akama Pandu Saleh

Hapo zamani za kale walikuwepo watu ambao walikuwa wanaishi karibu na pwani. Kazi yao ilikuwa ku-
vua, na siku zote walikuwa wanavua samaki wadogo wadogo. Siku moja alitokezea bwana mmoja aka-
enda baharini akabahatika kuvua samaki mkubwa sana.
Yeye mwenyewe akaanza kushangaa kumuona yule samaki mkubwa, na akaanza kusema ningempata
samaki kama huyu ningetajirika. Kila siku tunakuja pwani tunapata samaki wadogo wadogo, hapo aka-
jiuliza samaki huyu nimfanye nini?
Akama Pandu Saleh
Akaenda kumwita baba yake na baba mtu alipofika akaanza kushangaa na kusema samaki huyu mkub- Kutoka Mikunguni ana umri wa
wa sijawahi kumuona, sasa wakaanza kushauriana. Baba mtu akasema bora tukawaite jamaa waje miaka 63. Alikuwa na watoto 17,
kumtizama, wakaenda kuitwa wale jamaa walipofika na wao wakaanza kushangaa na kusema;„Samaki ambao 11 kati yao wako hai.
mkubwa, samaki kama huyu hatujawahi kumvua maisha yetu.” Na wao wakasema;„twendeni tukamwi-
te sheha.” Na sheha alipokuja alishangaa na akasema;„Bora tukawamwite Mfalme aje kumuona.”
Alipokuja Mfalme na yeye alishangaa na kusema; „Bora tukamwite mzungu aje kumpiga picha.” Hapo
waliondoka wakaenda kumchukua mzungu, na mzungu alipofika akasema; „Mngelimuweka kwa kule
nikampiga picha lakini hapa anazunguuka nitampiga vipi?” Wale watu wakajibu mpige hivyo hivyo, na
huku maji yanajaa na yule samaki akachukuliwa na maji, na kuenda zake baharini wakakosa utajiri pa-
moja na samaki.
21
Hadithi za Mikunguni

22
Hadithi za Mikunguni
Mume wa ajabu
Imesimuliwa na Farasha Saidi Kombo

Hapo zamani za kale alikuwepo Makame wa Makame ambaye aliishi na mkewe, Mize wa Mize pamoja na
watoto wao wengi. Mmoja miongoni mwa watoto wake wa kike aliolewa katika kijiji kingine cha mbali,
na mtu mmoja ambaye hakujulikana mapema kama alikuwa shetani.
Bila ya kujua mkewe alimzalia mumewe, aliyekuwa na umbo la binaadamu watoto wawili. Siku moja
mume alimuomba mkewe kwenda kumchukua mdogo wake wa kike ili aje kumsaidia kazi za nyumba-
ni. Mke alikubali kutokana na kuwa na kazi nyingi sana za ndani na shambani ambazo hakuweza kuzi-
kamilisha akiwa peke yake. Kwa hivyo mwanamke alifanya kama alivyotakiwa na kwenda kumchukua
mdogo wake wa kike. Kuanzia hapo mdogo wake wa kike alibaki nyumbani na watoto na yeye kufanya Farasha Saidi Kombo
kazi shambani. Kutoka Mikunguni ana umri wa
Siku moja mumewe alirudi nyumbani ghafla na kumwambia shemeji yake kwamba alitaka kwenda ku- miaka themanini. Ana watoto
sali. Wakati huo shemeji yake alikuwa akitwanga mtama. Lakini yule bwana hakutoka nyumbani bali wanne. Wajukuu zake wanawapenda
alijificha sehemu ambapo aliweza kusikia mtama ukitwangwa. Yule bwana, ambaye alikuwa shetani ha- babu na bibi yao.
kupenda chengine zaidi ya ule mlio wa kutwanga.
Yule bwana alipogundulika kuwemo ndani ya nyumba, alimwambia shemeji yake kwamba alikuwa aki-
sikiliza mlio wa kutwanga, ambao ulikuwa mlio takatifu na hairuhusiwi mtu yeyote mwingine kujua.
Alimlazimisha kuimba nyimbo ifuatayo akiwa anatwanga:
„Rudia na endelea kutwanga mtama, sina kazi, lakini ninafanya kazi na rafiki zangu.”
Yule bwana alifurahia sana kitendo hicho na kumfanya kuwepo kila siku, wakati mtama ukitwangwa na
nyimbo ikiimbwa. Alijificha katika chumba kingine ambacho alidiriki hata kucheza.
Siku moja shemeji yake alimgundua akiwa anacheza ngoma ya mashetani. Alishtushwa na kushindwa
kuamini macho yake na kuamua kurudi nyumbani kwao na kuanza kuwasimulia watu. Siku moja alimta-
ka dada yake kurudi mapema nyumbani ili aweze kujionea mwenyewe mambo yanayofanywa na mume
wake. Ilipofika jioni, yule mwanamke alimuelezea mumewe madai aliyotoa mdogo wake. Kama kawaida
yule mwanamke alipigwa na butwaa na kuendelea kudadisi.
Siku iliyofuata yule bwana alimtaka shemeji yake kutwanga mtama huku akiwa anaimba ili aweze ku-
cheza ngoma yake ya mashetani. Kitendo ambacho kilisababisha mkewe aendelee kuwaeleza majirani
kisa chote. Hatimaye aliwataka majirani kufika nyumbani wakati wa sala na kujificha na kujionea weny-
ewe kilichokuwa kikifanywa na mumewe. Kwa huzuni wale wanawake walikubali kufuata maelekezo
waliyopewa.
Yule bwana alipofika nyumbani wakati wa sala na kutaka kuanza kucheza ngoma yake ya kichawi, wale
wanawake waliokuwa wamejificha waliibuka na kumpa maneno yake. Yule bwana ghafla alijigeuza
shetani akiwa katika umbo la ndege na chura na kutoweka huku akiiacha familia yake ikiwa pweke
nyumbani.
23
Hadithi za Uzini
Asili ya Kijiji cha Uzini
Imehadithia na Mwalim Ramadhani Ali

Kijiji cha Uzini asili yake hasa ni sehemu ambayo ipo kando kidogo na kijiji hicho kilipo hivi sasa. Kijiji
hicho cha mwanzo kilipatikana upande wa magharibi mwa kijiji hicho cha hivi sasa, karibu na Kwa kas-
hata.
Kijiji hicho cha awali wazee wa wakati huo walikizindika, ili kuzuia maadui kukidhuru. Sasa wazee wa wa-
kati huo walichimba mtaro ukazunguka kijiji chao. Halafu walichukua uzi na kuuzika kwenye mtaro huo
Mwalimu Ramadhani Ali waliochimba na kukizungushia kijiji chote. Uzi huo ulikuwa umefanyiwa dawa za kimazingara.
Kutoka Uzini ana umri wa miaka 58,
Kuanzia hapo ikawa ndio mwanzo wa jina la Uzini kupatikana, ambapo watu walianza kuita hivi „Ah! Un-
ni baba wa watoto wanne.
akwenda sehemu yenye uzi hapo.” Na hatimae watu wa wakati huo wakakata tu na kusema;„nakwenda
uzini.” Baada ya hapo hadi leo jina limesehelea na kijiji hicho mpaka sasa kinaitwa ‘Uzini’.
Kabla ya kupatikana jina hilo, majina ya asili yalitumika katika kijiji hicho, kwa mfano Beshomari, nakad-
halika. Lakini baada ya kupatikana jina la Uzini, majina mengine yote yalizoeleka kabla yaliacha kutumi-
wa tena.

24
Hadithi za Uzini
Hadithi ya mfalme na waziri wake
Imehadithiwa na Ali Rehani Ali

Hapo zamani za kale alikuwepo mfalme na waziri wake ambao walikuwa na tabia ya kwenda kusaka po-
rini, siku tatu kwa kila mwezi. Siku moja waziri huyo wa mfalme alisafiri na kwenda nchi za nje. Alipofika
huko aliona upanga ambao unamfaa mfalme wake, kwani mpini wake ulikuwa wa dhahabu hivyo alim-
nunulia na aliporudi nchini kwake alimpa upanga ule mfalme wake kuwa ni zawadi.
Mfalme aliupokea na akawa anacheza na ule upanga, lakini upanga ule ulimkata kidole kimoja cha mko-
no wa kushoto hivyo mfalme alikasirika sana na alitwaa ule upanga na kumfunga gerezani waziri wake Ali Rihani Ali
kwa mwaka moja. Kutoka Uzini ana umri wa miaka
Baada ya kupita kipindi fulani, mfalme ilimjia hamu ya kwenda kusaka na siku ile alikwenda peke yake 51 na ni baba wa watoto sita. Yeye ni
kwani waziri wake alikuwa bado anatumikia kifungo gerezani. Alipofika porini alianza kusaka, lakini kule sheha kijijini kwake.
porini kulikuwa na watu wa mizimu, na watu hao waliambiwa na shetani wa mzimu ule kuwa, anataka
mtu wa muhanga.
Kwa bahati mbaya miongoni mwa watu walikuwepo pale mzimuni wote walikuwa na ulemavu, yaani
wana upungufu wa viungo katika miili yao.
Hivyo punde wale watu waliokuwepo mzimuni walimkuta mtu mmoja walimvamia. Kumbe yule mtu
alikuwa ni mfalme, walimfunga mikono na miguu ili awe ni muhanga kama walivyoagizwa mzimuni
kwao. Kabla hawajamuathiri mmoja wa watu wale waliomvamia mfalme yule, aliwakataza wenzake na
kuwaambia; „Huyu hatufai kwani hana kidole chake kimoja cha kushoto.” Hivyo walimfungua, na kum-
piga makofi kidogo kwa vile ameyafeli mambo ya watu na baadae walimwachia aende zake kwa vile ni
mlemavu wa kidole.
Mfalme alirudi nyumbani kwake na kuwaamuru askari wake, wamchukue yule waziri waliyemfunga ge-
rezani na wamlete nyumbani kwake. Baada ya waziri kukutana na mfalme. Mfalme alimwambia waziri
wake „Ah! Umeniokoa kweli kweli kwa kuniletea ule upanga mkali ulionikata kidole, la si hivyo, ningeli-
kuwa nishakufa“.
Na waziri alimjibu mfalme wake kuwa „na mimi umenihifadhi kwani safari hiyo ilikuwa twende sote
kusaka, na mimi mwili wangu hauna ulemavu wowote hivyo ningeuliwa“.

25
Hadithi za Uzini
Hadithi ya Makame wa Makame
Imehadithiwa na Ali Rehani Ali

Hapo zamani za kale alikuwepo Makame wa Makame ambaye alikuwa ni mfanyabiashara baina ya Asia
na Afrika ya Mashariki. Siku moja alipokuwa katika biashara zake huko Asia alikutana na mtu mmoja am-
baye alitaka kujua kwanini Makame wa Makame alikuwa huko? Makame wa Makame alimjulisha yote.
Pia alimjulisha kuwa yeye ni mfanyabiashara hivyo anataka kununua bidhaa ili apeleke kwao Afrika Ma-
shariki kwa ajili ya kuuza biashara hiyo.
Lakini mtu huyo alimueleza Makame wa Makame kuwa anavyo vitu fulani ili amuuzie, ambapo mtu
huyo alihitaji rupia tatu kutoka kwa mfanyabiashara huyo. Mfanyabiashara huyo alifurahi sana baada
ya kuambiwa atapata bidhaa kutoka kwa mtu huyo. Lakini bidhaa alizompa mfanyabiashara huyo ilikua
ni misemo mitatu tu, Mfanyabiashara huyo alikasirika sana kwa sababu alikuwa hana pesa nyengine na
ikamlazimu kurejea katika hali ya umasikini zaidi.
Misemo aliyopewa au kuuziwa mfanyabiashara huyo ni „utakachokipata utosheke”,„ukiaminiwa ujiami-
nishe”,„ukikaribishwa ukaribie”.
Mfanyabiashara huyo aliuziwa misemo hiyo bila ya kuambulia bidhaa alizofikiria. Matokeo yake akawa
hana pesa yaani masikini.
Siku moja alipokuwa bado yumo nchini humo alikutana na bibi kizee, Makame wa Makame aliulizwa
kwa nini alikuwa hapo alimuhadithia yote yaliyomsibu. Hatimaye bibi kizee yule alimchukua Makame
wa Makame hadi kwenye kibanda chake na alimtaka kuandika barua ili bibi kizee huyo aipeleke kwa
Mfalme apatiwe msaada.
Makame wa Makame aliandika barua hiyo na hatimaye bibi kizee huyo alimlipa Makame wa Makame
senti tatu. Makame wa Makame aliziona pesa hizo ni kidogo sana kulingana na kazi aliyofanya. Laki-
ni alikumbuka msemo aliopewa;„utakachopata utosheke.”
Barua ilifika kwa Mfalme, aliisoma na hatimaae aliwatuma watumishi wake waende kwa yule bi kizee
ili awajulishe nani aliyeandika barua ile. Bi kizee alimtafuta Makame wa Makame na kumjulisha kuwa
anaitwa kwa mfalme. Makame wa Makame alishituka na kuogopa lakini alikumbuka msemo wa pili ali-
opewa;„ukiaminiwa ujiamini” na alikwenda kwa Mfalme.
Alipofika kwa Mfalme aliulizwa barua hii umeiandika wewe? Makame wa Makame alijibu ndio nimean-
dika mimi. Mfalme alimtaka Makame wa Makame aelezee alivyoiandika barua hiyo. Hatimae alielezea
kila kitu jinsi alivyoiandika barua hiyo na mfalme alikubali kuwa hiyo imeandikwa na Makame wa Ma-
kame.
Mfalme kuamini hivyo alimwambia Makame wa Makame kuanzia leo utakuwa ni waziri wangu. Mfalme
alimuamini sana Makame wa Makame na alikwenda nchi za nje bila ya matatizo. Yule waziri wa mwanzo
26
Hadithi za Uzini

27
Hadithi za Uzini
aliyeshushwa cheo na kupewa madaraka Makame wa Makame alikuwa na choyo na wivu mkubwa kwa
waziri mpya, Makame wa Makame.
Siku moja Mfalme aliporudi safari yake kutoka nchi za nje yule waziri wa zamani alimwambia Mfalme
kuwa Makame wa Makame anamchukua mkewe na kufanya nae mapenzi wakati akiwa hayupo nchini.
Mfalme alikasirika na kuamuru askari wake waende vijijini huko „shamba” wakachimbe shimo kubwa, na
halafu mfalme atamtuma mtu na atakuja huko na atauliza;„je kazi ya bwana imekwisha?” Akiuliza hivyo
msukumeni shimoni halafu mrudi nyumbani.
Siku ya pili mapema askari walikwenda kuchimba shimo huko walikoagizwa na mfalme. Baada ya muda
fulani kupita mfalme alikisia ile kazi ya kuchimbwa shimo imekwishamalizika. Mfalme alimuagiza Maka-
me wa Makame aende liliko shimo na akifika awaulize;„Je kazi ya bwana imekwisha?”
Madhumuni ya Mfalme ni kwamba Makame wa Makame asukumwe shimoni. Makame wa Makame
alipewa farasi, alimpandia na kuelekea alikoagizwa aende na Mfalme. Alipofika kati kati ya safari yake
aliikuta sehemu kuna watu wengi wakiwa harusini, walimkaribisha lakini aliendelea na safari yake. Kwa
bahati Makame wa Makame alikumbuka msemo usemao „ukikaribishwa ukaribie.” Hivyo alirudi na ku-
kaa pale harusini.
Baada muda mrefu kupita Mfalme alimtuma mwanawe anaempenda sana ili akatizame kama kazi imek-
wisha au vipi . Alipofika aliwauliza wale askari;„Je kazi ya bwana imekwisha?”askari walimjibu; „imekwisha
twende ukaone.” Walipofika walimsukuma shimoni yule mtoto wa Mfalme na kumfukia.
Baada ya Makame wa Makame kumaliza kula pale harusini aliendelea na safari yake kule alikoagizwa na
Mfalme, aliwakuta wale askari wako katika hatua ya mwisho ya kumfukia yule mtoto wa Mfalme.
Baada ya kazi kumalizika Makame wa Makame na wale askari walirejea nyumbani kwa Mfalme. Walipo-
fika Mfalme alikuwa yupo juu ya ghorofa ya nyumba yake na alimuona Makame wa Makame akirudi na
wale askari. Mfalme alipata mshituko mkubwa wa moyo na hatimae kupoteza maisha yake. Baada ya kifo
cha Mfalme huyo, Makame wa Makame akashika wadhifa huo na kuwa mfalme wa nchi hiyo.

28
Hadithi za Bambi
Asili ya Bambi
Imesimuliwa na Omar Abdalla

Miaka mingi iliyopita wakaazi wa kisiwa cha Zanzibar walikuwa wakiishi kando kando ya bahari kwenye
ufukwe. Maisha yao yalitegemea uvuvi kwavile ardhi yao ni ya mawe na kichanga, kwa hivyo hawaku-
weza kulima chochote.
Kwa muda mrefu hawakuchukua juhudi zozote kuingia ndani ya kisiwa, kwenda kwenye misitu kutafiti
au kulima mazao ya mboga na ngano. Walikuwa wakikumbuka maelezo ya mwarabu mmoja, ambaye
katika safari yake moja kuelekea ndani ya kisiwa haikuwa na taarifa njema. Wakazungumzia mikasa mi-
wili kuhusu sehemu hii ya Bambi. Inaponyesha mvua, wakasema, huko ukenda kunabonyea na mtu hul- Omar Abdallah
azimika kujichomoa haraka kwenye tope. Halafu linapotoka jua vumbi jekundu huchafua nguo. Kutoka Bambi ana umri wa miaka
Tahadhari hizo mbili hata hivyo baadae ziliwafanya Waswahili wenyewe wakatafiti zaidi na hivyo waka- 54. Anafanya kazi za ufundi katika
fika katika kijiji cha Bambi. Wale wakazi wa ufukweni walikuta miti mikubwa iitwayo Bambi. Majani ya kituo cha Televisheni Zanzibar (TVZ).
miti hiyo huanguka chini na huifanya ardhi kuwa na rutuba. Baadae miti hiyo ikakatwa kabisa. Kilicho- Amesaidia kuandika hadithi kutoka
baki sasa ni ardhi tu yenye rutuba, jina la Bambi na wale wakazi waliotoka ufukweni, ambao kwa vizazi kijijini kwake pia kutoa maelezo juu
kadhaa sasa wamekuwa wakiishi kama wakulima. ya maana ya jina la kijiji.

29
Hadithi za Bambi
Uchoyo
Imesimuliiwa na Hussein Ali Vuai

Hapo zamani za kale alikuwepo mzee Subira na mzee Pandu, wote walikuwa marafiki na walikuwa maji-
rani. Mzee Pandu alikuwa anakawaida ya kusikitika. Siku moja mzee Pandu alioteshwa aende porini yeye
na rafiki yake Mzee Subira wakachukuwe mapesa.
Kwa bahati Mzee Subira alikuwa na punda, mzee Pandu alienda kumchukua yule punda na kumvalisha
soji bila ya yeye mwenyewe kumwambia. Alimchukua punda yule wakaenda porini kule alikofahamish-
wa. Alipofika huko aliyakuta mapesa mengi na mali za kila aina.
Hussein Ali Vuai
Kutoka Bambi ana umri wa miaka Alizipakia mali zote zile alizozikuta na kumbebesha yule punda. Kwa bahati mbaya ukavuma upepo na
50 na ana jumla ya watoto 15. Yeye ukamchukua mzee Pandu. Punda alipoona vile alifuata njia na kuelekea kwao, alifuata njia mpaka kafika
ni kulima, mwalimu wa Kuruani na kwao, alifika kwao pamoja na ule mzigo aliobebeshwa, alipofika akaanza kulia kwa kelele kubwa; Gha!
ni mfanyakazi wa serikali kuanzia Gha! Gha! Gha! Gha! Gha! mpaka mzee Subira akaamka, na alipotoka nje alimuona punda kaja na mzigo
mwaka 1975. wa mapesa.
Mzee huyo alishangaa kuona punda kavalishwa soji na kubebeshwa mzigo. Aliuchukua ule mzigo na ku-
utia ndani na punda akamuweka pahala pake pa kawaida. Ilipofika asubuhi akaenda kumuamsha jirani
yake ambaye hakuwemo ndani ya nyumba.
Hayumo!!! alishangaa sana kuona asubuhi ile mzee Pandu hayumo ndani mwake. Akaanza kujiuliza
huyu bwana kaenda wapi? Kuona hivyo, aliwaelezea wenzake kwamba mzee Pandu haonekani, alianza
kufanya ramli na dawa za miti shamba pamoja na majini ili ajuwe aliko. Mwisho wake alijua kwamba ali-
chukuliwa na upepo mkubwa baada ya kufanya dawa .

Tusiwadharau wadogo
Imehadithiwa na Tatu Juma

Hapo zamani za kale alikuwepo Mfalme ambaye alioa na kupata mtoto, wa kike. Alikuwa mzuri na akasi-
fiwa na kila mtu katika kijiji chake. Siku moja walijitokeza marafiki wawili, Ng’ombe na Kinyonga na wa-
kaanza kumsifu yule mtoto kwa ajili ya kutaka kumuoa. Kati ya wale marafiki kila mmoja alitaka kumuoa
yule binti.
Tatu Juma
Kati ya wale marafiki kila mmoja alitoka kisiri siri na kwenda kwao kumposa bila ya mwenziwe kujua.
Kutoka Bambi ana umri wa miaka
Mfalme aliposikia vile aliamua kupigisha mbiu kwa ajili ya kuitisha mkutano.
60, ana watoto sita na ni mama wa
nyumbani Mfalme aliwajuilisha lengo la kuwekwa mkutano ni posa ya mwanawe na kuoneshwa waposaji hao,
Amesimuliwa hadithi na baba yake Ng‘ombe na Kinyonga. Waposaji hao walikuwa wote ni marafiki. Kila mmoja alistaajabu kuona wana-
30
Hadithi za Bambi

31
Hadithi za Bambi
gombania mtu mmoja. Mfalme alitoa siku na alisisitiza na kusema ataefika mwanzo ndie ataeowa. Kuo-
na vile ng’ombe alimcheka kinyonga na kumdharau, kwa kumuona kinyonga ni mdogo sana na kumuo-
na hana mwendo.
Siku ilipofika ng’ombe alijiandaa na kinyonga alijiuliza, nitafanya nini mimi nifike mapema nipate niwa-
hi na mimi mwendo wangu mdogo mdogo? Lilimjia wazo zuri na kuanza kupanga, kinyonga alipanga
kama hivi: Atatoka kwake mapema kabla siku ya shughuli na kukaa kwenye tawi la mti. Siku ilipowadia
ng’ombe alikamilisha ahadi yake, alianza kutoka mbio kwake alipofika tu kwenye mti kinyonga aliurukia
mkia wa ng’ombe bila ya yeye mwenyewe kujua kama Kinyonga kakaa kwenye mkia wake.
Ng’ombe alipofika kwenye shughuli aliwakuta watu wengi wamefika, lakini kumuangalia kinyonga ha-
kumuona na alianza kufurahi akajua kwamba hajafika kwa hiyo alihisi yeye ndie atakaekuwa mshindi.
Alipotaka kukaa tu alisikia sauti ya kinyonga na kumuuliza;„Mbona unataka kunikalia.“
Ng’ombe aliposikia ile sauti ya kinyonga alilia sana na kuhuzunika huku akisema; „Dunia imenianda-
ma! Dunia imeniandama! Dunia imeniandama! Dunia imeniandama! Dunia imeniandama! Dunia
imeniandama!“ Aliona kwamba mke kamkosa kwa kuchelewa kufika. Hapo alisimama mfalme na aka-
chaguliwa kinyonga kwa kufika mapema na kuozeshwa mtoto wa mfalme. Na kuona vile Kinyonga ali-
furahi sana kwa kuona amemshinda mshindani wake kwa kupata mke ambae walikuwa wanamgomba-
nia. Hapo Kinyonga akaanza kubadili nguo za kila aina hadi leo.

32
Hadithi za Bambi

33
Chanzo cha hadithi
Vikundi vya Ujerumani na Watanzania viliwatembelea wasimuliwaji na wasimuliaji hadithi katika vijiji
tofauti, na kuandika hadithi kwa lugha ya Kiswahili ambazo baadaye zilitafsiriwa kwa lugha ya kijeru-
mani.
Vikundi hivyo vinawajumuisha wafuatao:
Gabriel Gollnick, Daniela Hesse, Khamis Yussuf ambao walifanya mazungumzo na Bwana Ngwali Mas-
haka na Pandu Mkoba Faki huko Fukuchani.
Madeleine Kreutzman, Kersten Kühne, Riziki Vuai Mohammed, Swaghir Mwadin walizungumza na Tatu
Juma, Omar Abdallah na Hussein Ali Vuai kijijini Bambi.
Matthias Mnich, Christian Kopp, Kersten Kühne, Michael Nischik, Khalfan Mwita na Chande Omar walisi-
muliwa hadithi na Suleiman Khamis Faraje na Zubeda Abdalla Omar huko Chukwani.
Christian Kopp, Madeleine Kreutzmann, Michael Nischik, Jabirr Kheri Mohammed walipata hadithi ku-
toka kwa Akama Pandu Saleh, Murshid Rashid na Farasha Said Kombo wa Mikunguni.
Madeleine Kreutzman na Matthias Mnich aliongea na Hassan Mambo Kombo, Haji Abdullah na Subira
Abass kutoka Uroa.

Picha:
Birgit Mitawi, Gabriele Gollnick,
Michael Nischik, Daniela Hesse,
Matthias Mnich, Christian Kopp,
Madeleine Kreutzmann
waliosimama nyuma kutoka
kushota kwenda kulia.
Subira Abassi aliyesimama mbele
wapili kutoka kushoto. Haji Abdalla
aliyesimama mbele wapili kutoka
kushoto. Hassan Mambo Kombo
Aliyechutama watatu kutoka
kushoto pamoja na mwalimu
kutoka Uroa.

34
Shukrani
Mradi huu wa RAA Brandenburg umegharimiwa na
Shirika la mashirikiano kati ya Kaskazini na Kusini (North-South-Foundation).
Programu inayojulikana kama: Vijana kwa mashirikiano ya maendeleo ya Serikali ya Brandenburg kwa kupitia Wizara ya Kazi,
Jamii, Afya na Familia (MASGF)
Watu wote walichangia zaidi ya Euro, 11,000 kwa mradi huu wa Soma na Uwasomeshe wenzako.
V. Adenstaedt, Dr. Anders, H. Barsch, C. Berner, W. Beyer, Dr. Birkholz, I. Carstensen, E. Ehrhardt, K. Freier, E. Garske, G. Gollnick,
E. Goltz, V. Göritz, I. Heide, H. Hieckel, S. Itzerott, K. Just, C. Kopp, K. Korn, K. Kühne, M. Lehn, U. List, H. Lotzmann, A. Löwisch,
G. Meise, S. Meise, B. Mikat, E. Mnich, Dr. Piasecki, R. Rietzel, G. Saupe, K. Scherf, J. Schröder, Dr. Thonicke, R. Thürmer, K. Ullmann,
F. Vetter, H. Viehrig, K. Volkmann, S. Wiedemann, S. Wiegartz, Dr. Zuckermann – asanteni sana.
Shukurani nyingi ziwafikie pia wanafunzi wa kike na wa kiume wa Skuli ya Sekondari ya Postdam na pia Skuli ya Gymnasium
ya Rober-Blun ya Berlin, Umoja wa akina mama wa nyumbani wa Reinckendorf pia wanachama wa kanisa la Neukoln Martin
– Luther- King wa Berlin.
Shukurani za aina yake zinatolewa kwa Sabine Meise anayesomesha Kijerumani nchini Japan ambaye pia ameanzisha mashi-
rikiano kati ya Skuli ya Chukwani, Zanzibar na Kyoto nchini Japan. Kutokana na juhudi zake, kikundi cha muziki kijulikanacho
kama Sinfonierochester kilifanya onyesho na kukusanya fedha kwa ajili ya mradi huu.
Mradi ulifadhiliwa kupitia mchezo wa Bahati nasibu, misaada ya watu binafsi, msaada uliotolewa na Bwana Mueller, kiongozi
wa „Innomed Leipzing GmbH, na Bwana Krueger, Imker kutoka Beeskow.
Shirika la Twende pamoja lilisaidia mradi kwa Euro 1400 zilizokusanywa kutokana na shughuli mbali mbali.
Tunawashukuru pia wale wote waliosaidia mradi huu kwa hali na mali.

2006
Kujifunza na kufundisha vizuri zaidi
Kupata vitabu zaidi kutokana na misaada
Msaada wa jumla ya Euro 1,525,75 uliotolewa na kampuni ya RR Software GmBH iliopo Hasselfelde na shirika la „Kula“ uliweza
kununua vitabu kwa skuli sita mwezi August 2006.
Shukrani nyingi zinatolewa kwa msaada huo.
Ni tegemeo letu kwamba wataendelea kutoa misaada zaidi ambayo itasaidia kutoa elimu za sayansi katika vijiji vya Zanzibar.
Misaada yao itawezesha kununua vitabu vipya viliopo madukani. Kwa mashirikiano na wao tutaweza kukuza maktaba ziliopo
na hatimaye kupunguza tofauti ziliopo kati ya nchi tajiri za kaskazini na nchi masikini za kusini.

35
Upigaji chapa

Uchapishaji wa hadithi hizi za Kiswahili kutoka Zanzibar umefanaywa kwa ufadhli wa Bwana Karl Heinz Remmers pamoja na mchango
wa marafiki kadhaa wa mpango wa ‚ Kutana na Zanzibar‘

Kimetungwa na: Yumuiya ya Demokrasia na Ushirikishaji wa wageni


Ofisi ihusayo mambo ya wageni, kuwakuza vijana na elimo, Mkoa wa Brandenburg,
Idara ya kujifunza kimataifa

Mkuu wa mradi: Bibi Birgit Mitawi

Mpangelio: Gabrielle Lattke

Michoro: Mohamed Jafari, Gabriele Gollnick, Daniela Hesse

Muhariri wa Kiswahili: Hassan A. Mitawi, Yussuf Yussuf

Haki miliki © RAA Brandenburg 2007

Anwani: Demokratie und Integration Brandenburg e.V.


RAA Brandenburg,
Bereich, Globales Lernen
Benzstraße 11/12, 14482 Potsdam
Simu/Fax 0049 0331 74780-0 (20)

Barua pepe: globaleslernen@raa-brandenburg.de


Internet: http:/www.raa-brandenburg.de

Kimechapishwa na: Central Printing, Dar es Salaam, Tanzania

36
Paukwa
... husikika sauti ya mtoaji hadithi, pale anapotaka kuwasalimu Fukuchani
watizamaji wake.

Pakawa Z ANZIBAR

... hiki ni kiitikio cha wasikilizaji, ambacho lazima kiwe kwa Uzini
sauti kubwa, ili kumfanya mtoaji hadithi avutiwe, na hivyo
Bambi
aanze kutoa ahadithi.
Mikunguni Uroa

Chukwani

A F R I C A

TANZANIA
ZANZIBAR
Paukwa
Hadithi za Zanzibar
Regionale Arbeitsstellen
für Ausländerfragen,
Jugendarbeit und Schule

You might also like