You are on page 1of 7

Mambo 30 usiyoyajua kuhusu utapeli wa Q-Net (Network

Marketing)

Habari wadau, niliwahi kuja na uzi hapa kuhusu D09 CLUB Miezi michache kabla
haijapotelea kusikojulikana na nilishambuliwa sana na waliliwa pesa zao na bila kujua
hatma yao wanarudishiwa vipi na nani. Leo naomba nije na mambo 30 usiyoyajua kuhusu
Qnet.

Qnet ni network marketing ambayo imevuta member wengi waliokua d09 Club kuingia huko
haina tofauti kubwa na network marketing zingine unazozijua wewe mfano lugha
wanayotumia kukushawishi zinafanana na wale wengine.

Kiuhalisia wanakuekea mazingira mazuri ya kuona unapata pesa kirahisi sana lakini
kiukweli hakuna pesa rahisi unawafanyia kazi na wanakulipa kama kazi zingine lakini
mfumo wao wa ulipaji na uendeshaji wa biashara yao ndio uko tofauti na wengine.

1. QNET ILIANZISHWA LINI?

Mwaka 1998 kampuni hii ilianzishwa huko Hong Kong mwaka ambao:

-Kampuni ya kutengeneza magari ya Benz iliinunua kampuni ya Chrysler kwa gharama za


$36 billion ambayo ilivunja rekodi ya Dunia na kua biashara kubwa zaidi kihistoria kufanyika
mpaka mwaka huo.

-Elton John anakua shoga wa kwanza kutunukiwa heshima ya "Sir" na malkia wa Uingereza
-Mwaka huo huo mwanzilishi mwenza wa google Larry Page na mwenzie Sergey Brin,
waliokutana Stanford University, wanaisajili rasmi kampuni ya google California
kwa ajili ya kutoa huduma mtandao
-Mwaka huo pia mmiliki na mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft anatupiwa ice cream usoni
akiwa Belgium

Ni mwaka uliokua na mapinduzi makubwa kiuchumi pamoja na vituko vingi vya kushangaza
Dunia.

2. NANI MWANZILISHI WA QNET?


-Vijay Aswaran akiwa kama mwenyekiti wa QI Group na mwenzie Joseph Bismark akiwa
kama Director wa QI Limited

3. Majina mengine ya QNET usiyoyajua:

• Questnet
• Goldquest
• and QI Limited
4. Makao makuu yake na Office zao:
Makao makuu ya QNET yapo Hong Kong lakini wana Ofisi katika miji ifuatayo:

• Malaysia
• United Arab Emirates
• Indonesia
• Ireland
• Singapore
• Rwanda
• Philippines
• Turkey
• India
• Algeria
• Azerbaijan
• Cote D’Ivoire
• Burkina Faso
• Georgia
• Guinea
• Moldova
• Kazakhstan
• Myanmar
• Niger
• Mandalay
• Ukraine
• and Russia

5. WALIANZA NA BIASHARA GANI?


QNET walianza kwa kuuza "Custom Coins" mfano zile zinazotumika kutunuku washindi wa
michezo mbalimbali katika mashindano ya michezo n.k na ilikua inaitwa Goldquest

6. QNET At The Olympics


Kampuni ya QNET ndio ilipata deal ya kutengeneza na kusambaza Olympic coins mwaka
2000 zilizofanyika Sydney,pia 2004 Athens Games na 2008 Beijing Games.

7. QNET At The World Cup


QNET tena wakalamba bingo la kombe la Dunia mwaka 2002 kama official coin distributor
for the 2002 FIFA World Cup soccer championships.

8. QNET na QVI Club


Ili kujitanua zaidi na kuongeza kipato QNET iliingia ubia na kua mwekezaji mwenza na QVI
Club kampuni inayohusika sana na Vacations and Travell.

9.QI Comm
Mwaka 2005 QNET ikaingia kwenye uwekezaji wa kampuni ya mawasiliano wakainunua
British communications company na kuibadilisha kua QI Comm.

10. Prana
Mwaka 2005,QNET ikaingia kuwekeza Thailand na kuinunua Prana Resorts and Spa

11. Cimier
Mwaka huo huo 2005 wakakinunua kiwanda kikubwa cha kutengeneza saa huko Uswisi
Swiss watch manufacturer Cimier.

12.Down To Earth
Mwaka 2007, kampuni ikapiga hatua zaidi na kununua kiwanda cha vyakula na afya huko
Hawaii kinachoitwa Down To Earth.

13. Meritus
Kampuni ya QNET inaanza kusponsor the Meritus Malaysian Motor timu ya mashindano ya
magari.Timu hiyo ilibadilishwa jina na kua MY QI Meritus.

14. Virgin Racing


Mwaka 2010, wakaingia ubia na Virgin racing ambao walikua wanashiriki pia the Grand Prix
series mashindano makubwa ya mbio za magari Duniani.Haikufanya vizuri na waliacha
nayo 2011.

15. Bidhaa ambazo QNET imewekeza tangu 1998 mpaka 2010


Mpaka mwaka 2010 QNET ilikua na bidhaa tofauti tofauti sokoni na zingine zikiwa ni zile
mahitaji mhimu kwa binadamu kama afya na chakula.Kampuni ikaanz kujikita zaidi katika
kutafuta wasambazaji katika category tofauti tofauti;

• Health and wellness


• Vehicle motor care
• Personal Care
• Beauty
• Technology
• Jewelry and watches
• Holiday and recreational travel
• and Education

Post ijayo ntakuja kuelezea namna QNET inavyolipa na nchi kadhaa ilikofungiwa na mmiliki
wake kukamatwa mara kadhaa kwa mashtaka ya kutakatisha fedha (baadhi ya nchi).........

======

Naomba tuendelee sehemu ya pili kisha ntatoa hitimisho kwa mtazamo wangu.......karibuni

16. Namna wawakilishi/waliojiunga na QNET wanavyopata mgao


Haina tofauti sana na networking market zingine ama ile d09,lakini huku yule TOP (ambae
ni QNET) ndio ananyonya member na member aliejuu yako hali jasho lako bali kwa juhudi
zake ndivyo anapata commission zaidi na namna anavyoingiza member wapya ama kuuza
bidhaa za QNET. kuna njia 10 za kupata pesa ya mgao wako baada ya kufanya kazi ya
maana;
1. Retail Profits
2. Early Payout
3. Step Commissions
4. Repeat Sales Points
5. Year-Round Incentives
6. New Program Bonus
7. Main Plan Rank Advance
8. RSP Plan Rank Advance
9. RSP Rank Advance Bonus
10. and RSP Rank Maintenance Bonus

Sitazielezea hizi kwa undani kwa sababu si nia ya huu uzi labda tukijaliwa nafasi siku
nyingine,nia ya huu uzi ni kukujulisha usalama wa uwekezaji wako juu ya QNET kisha
uamue kujitundika mwenyewe....tuendeleee

17.Quest University
Hiki ni chuoa cha QNET kipo Malysia (Perak) na wanatoa kozi za Afya na Uuguzi na
zingine nyingi so far hakuna review mbaya kuhusu hiki chuo.

18. Australia
The Australian Office of Consumer and Business Affairs waliitaja QNET kama pyramid
scheme 2002.

19. Nepal
Mwaka 2003, the Nepalese Home Ministry walifunga kazi na biashara zote zinazoihusu
QNET nchini humo.

20.Sri Lanka
Mwaka 2005, waliishutumu QNET imeisababishia nchi hasara ya $15,000,000 kwa
kuikosesha kodi na kufanya biashara zinazofanana na utakatishaji wa pesa, serikali ya Sri
Lanka ikaipiga banned QNET nchini humo.

21.Iran
Mwaka huo huo 2005,Serikali ya Iran waliishtumu shutma zile zile QNET ilizokutana nazo
Sri Lanka kua imesababisha hasara kwa nchi ya takribani $500,000,000 wakaipiga banned
QNET pia nchini Iran.

22.kukamatwa kwa Vijay nchini


Mwaka 2007, Direct Selling Association huko Indonesia waliishtaki QNET kwa serikali ya
nchini humo, kua ni pyramid scheme. Interpol walimkamata Vijay Eswaran na wahusika
wengine na kuwafungulia mashataka ya fraud. Wiki chache baadae washtakiwa wote
waliachiwa huru na mashtaka yalifutwa na QNET ikaendelea kuoperate nchini Indonesia.

23.Maandamano ya kuipinga QNET nchini Afghanistan


QNET ilianza shughuli zake Afghanistan mwaka 2006.Na ilishika kasi kwa speed na kupata
washirika wengi ndani ya mda mfupi na mwaka 2008 ikasajiliwa rasmi nchini humo.Ghafla
siku moja kukazuka maandamano makubwa takribani watu 3,000 wakipinga namna QNET
inavyofanya biashara zake nchini humo na mamlaka zikaibana QNET na kuipa masharti ya
namna ya kujiendesha ikiwa nchini humo.

24.Sudan
Serikali ya Sudan government ika bann shughuli zote za QNET nchini humo kwa sababu ya
malalamiko kutoka kwa watu walifanya nao biashara kutokupokea vitu walivyonunua na
hata kama wakiletewa hivyo vitu quality yao ni mbovu Duniani hakuna hapo ilikua mwaka
2009.

25. Syria
Mwaka huo huo 2009, the Syrian Ministry of Economics wakaishtaki QNET kwa kufanya
biashara kubwa nchini humo na bila kulipa kodi lakini pia kampuni inaendesha shughuli
zake kwa mtindo wa pyramid scheme ambao ni kinyume na sheria za nchi hiyo QNET was
not allowed to operate in Syria anymore.

26. Turkey
Mwaka 2010 huku ikijulikana kama Questnet, watu wanaojihusisha na Questnet wapatao
80 walikamatwa na 40+ walifunguliwa mashtaka ya "gaining an unfair
advantage".Wakabadili jina la kampuni na kuanza kuitwa QNET, serkali ikaanzisha
uchunguzi wa kina kuhusu QNET wizara ya biashara ya Uturuki. Mwaka 2011, QI Group
wakanunua Dögan Hotel iliyopo Antalya, Turkey.

27.Egypt
Kampuni ilipelekwa katika chombo kinaitwa Dar al-Ifta al-Misriyyah ambacho kinasimamia
maswala ya elimu na maadili ya kiislam. Dar al-Ifta al-Misriyyah wakasema QNET ni
kinyume na hairuhusiwi pia italeta madhara kwa uchumi wa Egyptian hapo ilikua 2012.

28.Saudi Arabia
Mwaka 2010, the Saudi Arabia Ministry of Commerce and Industry walitoa onyo kali kwa
wananchi wake kujihusisha na kampuni kama QNET. Na ilifungiwa mara moja kufanya
shughuli zake nchini humo.

29.Kamata kamata nchini India


Mwaka 2008, the Central Bureau of Investigation huko India walianza uchunguzi na
kupeleleza shughuli zote zinazofanywa na viongozi wa QNET.Walipitia historia ya
mashtaka yote aliyoshtakiwa Vijay Eswaran and QNET ikiwa ni pamoja na yale ya
kujihusisha na utakatishaji wa pesa. Walifreeze account za QNET na mwaka 2013 walianza
kukamata wahusika wote

Serikali ya India haikua na sheria inayozungumzia kuhusu direct selling and multilevel
marketing,hivyo hakuna mahakama ya India iliyoweza kuwatia hatiani wahusika wa QNET
wakawa huru.

30. Sura nyingine ya QNET


Tutizame positive side ya QNET na Vijay kwa kiasi;

• Forbes listed Vijay Eswaran as one of the biggest philanthropy heroes. You can read
about that here: 48 Heroes Of Philanthropy
• It is listed on the World Economic Forum
• QI Comm is one of the fastest growing tech companies in the United Kingdom.

QNET inaendesha biashara zake kwa mfumo wa Multi-level


marketing ambao unatumika sana na pyramid scheme nyingi
kama d09 iliyokufa hivi karibuni na zingine.

Kinachofanya usione kama ni pyramid scheme wanatumia kivuli cha bidhaa na vitu
wanavyomiliki ili kuficha uhalisia wa pyramid scheme (ntaielezea siku nyingine hii).

Utajiuliza kwa nini haifungiwi sehemu nyingi duniani mpaka kutokee majanga ???
Ni kwa sababu sehemu nyingi duniani nchi nyingi hazina sheria inayosimamia multi level
marketing na operations zake pamoja na direct selling kama ilivyotokea nchini India kweli
mnaona kuna uovu unatokea watu wanarun business kinyume kabisa na mipango ya nchi
lakini mnawatia nguvuni na kuwashtaki kwa sheria ipi ? Hii imefanya hawa jamaa
kuendelea kupeta nchi nyingi ikiwemo na hapa kwetu na ndio maana hujasikia mtu
kakamatwa kwa kupotea na pesa za d09 hata hii QNET itakuja kuishia hewani tu kama
mvuke........(haya ni maoni yangu)

Mfumo wa Forever Living au Oriflame ni tofauti sana na mfumo wanaotumia hawa QNET as
network market na hicho ndio kinachofanya kue na doubt nchi nyingi inakoingia na kuanza
ku operate.

Niwakumbushe wanaotamani kuingia huku usiwekeze kiasi kikubwa cha pesa ambacho
hutamudu kukipoteza namaanisha don't invest amount of money that you couldnt afford to
loose it,that is risk management.....hata siku unaambiwa ime collapse au imefungiwa nchini
kwetu hutaumia kwa ile pesa ulikua umeweka kule utaumia kwa mda ulio poteza ungeweza
kufanya uwekezaji mwingine wenye tija.
Kwa wafanya biashara nafikiri ukiweza ku adopt hii system ya mult level marketing
(kumfanya mtu awe part ya uwekezaji wako au part ya biashara yako na si kumuajiri) ni
mfumo mzuri sana.

Kwa TRA kuna mirija ya upotevu wa pesa hasa kwa shughuli kama hizi niliwahi hata kuuliza
hivi google,facebook si wanarusha matangazo yao online wanalipa kodi ? sheria
zinasemaje ?

You might also like