You are on page 1of 3

TAARIFA YA DARUBINI YA WIKI

MSOMAJI
MUDA DAKIKA 15
MWANZO
Hujambo mpenzi msikilizaji , hii ni Darubini Ya Wiki awamu ya saa saba mchana tarehe
11/2/2021, mimi ni Protus Nyansera .
1. Serikali za kaunti kupokea pesa Zaidi
2. Bunge la Kisumu lapitisha BBI
3. Yamkini Wawaniaji 13 waonyesha nia ya kumridhi Davidi Maraga kama jaji mkuu
4. Mwanafunzi apatikana na risasi shuleni Embu
5. Kimataifa ,'Vijana wa chini ya miaka 18 marufuku kufuga rasta' Zanzibar
6. Napia tunazo mkusanyiko wa taarifa ya spoti .
Karibu , takribani watu 13 wameonesha nia ya kutaka kumridhi aliyekuwa jaji mkuu Davidi
Maraga . Miongoni mwao nikama vile rais wa mahakamaya rufaa, jaji Wiliam Ouko, Jaji
Martha Koome, Jaji Shitembwe , aliyekuwa mkurugenzi wa mahakama ya umma Philip
Murgor , Jaji Said Juma chitembwe, , wakili Otondo , wakili Fred Ngatia na wakili Ombongi
Brian Matagaro . Watakaochaguliwa watahitajika kuhojiwa ambapo jina moja litawasilishwa
kwa rais na kisha kuidhinishwa na bunge.
Sasa ni rasmi kuwa , serikali za kaunti zitatengewa shilingi Bilioni 53.5 zaidi katika kipindi
cha mwaka wa pesa 2021/2022. Haya ni kutokana na makubaliano baina ya baraza la
kusimamia maswala ya bajeti la serikali pamoja na serikali za kaunti ulioongozwa na Naibu
Rais Wiliam Ruto hapo jana .Hii ina maana kuwa , serikali za kaunti zitapokea jumla ya
shilingi bilioni 409.88 kutoka shilingi bilioni 316.1 za mwaka wa fedha 2020/2021.
Kwingineko bunge la Kisumu limekuwa la hivi punde baada ya lili la Siaya kupitisha mswada
wa marekebisho ya katiba wa mwaka wa 2020 kupitia BBI.Kulingana na spika wa bunge hilo
Elisha Oraro , sheria zote zilifuatwa kikamilifu huku akiwapongeza wawakilishi wadi kwa
kupitisha mswada huo. Hata hivyo atahitajika kutuma nakala ya uamuzi wa bunge kwa
maspika wa bunge la kitaifa na seneti ili kufanikisha mchakato huo . BBI atahitaji kuungwa
mkono na mabunge 24 ya kaunti ili kufanikisha mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho .
Huku hayo yakijiri, polisi katika kaunti ya Embu wanamzuilia mwanafunzi mmoja
aliyepatikana na risasi katika shule ya upili ya wavulana ya Kamama.Mwanafunzi huyo
alikamatwa na mwenzake walipojaribu kuteketeza bweni moja la shule hiyo .Kulingana na
kamanda wa polisi wa Embu Daniel Rukunga , risasi hiyo ni ya bunduki ya AK-47 .Wanafunzi
hao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Munyatta huku uchunguzi ukiendelea .
Katika taarifa za kimataifa ,Mkuu wa Wilaya ya Mjini huko visiwani Zanzibar, Rashid
Msaraka ametangaza kuanza operesheni ya kuwanyoa nywele vijana wenye umri
chini ya miaka 18, waliofuga rasta au kunyoa mtindo wa 'panki.'Amesema kama
wanazitaka wakafugie sehemu nyingine na endapo wazazi wao wameshindwa
kuwakata hizo nywele, atawakata yeye mwenyewe . Kitendo hicho kimeibua mjadala
kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, watu wakihoji ni sheria ipi iliyomuongoza
kiongozi huyo kutoa agizo hilo kwa umma .

Hayo yakijiri , Shirika la afya dunaini limeshauri matumizi ya chanjo ya virusi vya
corona iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na AstraZeneca hata kama nchi
zinakabiliana na aina mpya za virusi vya corona. Baadhi ya aina za virusi hivyo
zinaonekana kuifanya aina hiyo ya chanjo kutokuwa na ufanisi wa kutosha wa
kuzuia maambukizi.WHO pia inasema chanjo hiyo inaweza kutumiwa kwa watu
wenye umri wa zaidi ya miaka 65, jambo linalozuiwa na baadhi ya nchi.

CHANZO CHA IMAGES


Michezoni ,Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino amesisitiza klabu yake
na wachezaji hawajaonesha ''utovu wa nidhamu'' kwa kuzungumzia nia yao ya
kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi .

CHANZO CHA IMAGES


Kiungo wa kati wa Ubelgiji Axel Witsel mwenye umri wa miaka 32, mshambuliaji
Mmarekani Giovanni Reyna18, kiungo wa Uiengereza Jude Bellingham 17 na
Halaand ni miongoni mwa wachezaji watakaouzwa na timu ya Dortmund ikiwa
imelenga kupata fedha.

Jose Mourinho amekiri kuwa kiungo wa Uiengereza Dele Alli aliye na miaka 24,
yawezekana amevurugwa na uvumi unaomuhusisha yeye kuondoka Tottenham.

CHANZO CHA IMAGES


Udinese haijaamua kumuuza kiungo wa kati Rodrigo de Paul, 26, baada ya taarifa
zinazomuhusisha mchezaji huyo kuhamia Livepool wakati wa dirisha la usajili la
Januari.

West Brom wameamua kutotoa mkataba wa Ahmed Musa baada ya majaribio na


mshambuliaji huyo wa Nigeria wa miaka 28.

CHANZO CHA IMAGES


Kocha msaidizi wa Aston Villa John Terry yuko kwenye orodha ya watakaochukua
nafasi ya kocha mkuu wa Bournemouth. Pia Kocha wa zamani wa Nice na kiungo
wa kati wa zamani wa Arsenal Patrick Viera ni miongoni mwa wanaowania nafasi ya
Kocha wa Bournemouth.

Kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo amesema mshambuliaji wa Mexico Raul


Jimenez, 29, amepiga hatua nyingine "ya kushangaza" katika kupona kwake kutoka
kwa upasuaji wa fuvu la kichwa lililovunjika mnamo Novemba.

Na mwisho ni kuwa ,Mlinzi wa Arsenal mwenye umri wa miaka 19 Mfaransa William


Saliba, ambaye anacheza kwa mkopo Nice, amemkosoa kocha wa Gunners Mikel
Arteta kwa kumhukumu kwa "mechi mbili na nusu".

Kwa kumalizia taarifa ya Darubini ya wiki huu hapa mukhutasari wake


1. Serikali za kaunti kupokea pesa Zaidi
2. Bunge la Kisumu lapitisha BBI
3. Yamkini Wawaniaji 13 waonyesha nia ya kumridhi Davidi Maraga kama jaji mkuu
4. Mwanafunzi apatikana na risasi shuleni Embu
5. Kimataifa ,'Vijana wa chini ya miaka 18 marufuku kufuga rasta' Zanzibar
6. Napia tumekujuza mkusanyiko wa taarifa ya spoti .

Tembelea tovuti ya www.pfm.co.ke kwa mengi Zaidi mimi ni protus Nyansera .

You might also like