You are on page 1of 2

Ecolebooks.

com

KISW P1
MWONGOZO

1. TAWASIFU

Umealikwa katika jopo lililoteuliwa kuchagua kiongozi wa masuala ya watoto


wanaorandaranda mitaani katika kaunti yenu. Andika tawasifu utakayowasilisha katika jopo
hilo kuonyesha ufaafu wako.

SURA

- Atumie nafsi ya kwanza


- Atumie aya kuwasilisha hoja zake
- Maisha ya kuzaliwa, kukua na elimu ichukue nafasi ndogo katika tawasifu
- Mtahiniwa ashughulikie ufaafu wake.

BAADHI YA MAUDHUI

- Yeye mwenyewe kwa mtoto wa kurandaranda


- Aokolewa na ajiunga na elimu
- Kuwa kiongozi wa shirika la kusaidia watoto shleni – aelezee shughuli walizohusika
nazo
- Shahada yake ni kuhusu nini?
- Baada ya kuhitimu ameshughulikia mradi ipi?
- Je kuna masuala aliyochangia kimaadhishi
- Je amehusika na makao mangapi ya watoto wanaorandaranda

Tashbihi

- Akitumia mtindo wa hotuba kama vile salamu hana sura – 4mm ( sura)
- Lazima atumie nafsi ya kwanza
- Akikosa – 4 mm (sura)

2. Mitandao ya kijamii ina faida nyingi katika jamii. Thibitisha

SURA

- Hili ni swali elekezi kila hoja itajwe, ifafanuliwe na ikamilike


- Ikiwa hoja haijakamilika isituzwe
- Lazima mtahiniwa awe na hoja zaidi ya saba kuhitimisha maudhui
- Lazima atumie hoja mufti

DOWNLOAD MORE RESOURCES LIKE THIS ON ECOLEBOOKS.COM


Ecolebooks.com

BAADHI YA HOJA

1. Hufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu


2. Hufanikisha biashara
3. Hufanikisha elimu
4. Hukuza utangamano
5. Kuboresha mahusiano
6. Kuboresha usalama
7. Huburudisha – husaidia watu kukabiliana na matatizo k.v msongo wa mawazo n.k

3. Andika kisa kinachothibitisha ukweli wa methali “kutangulia si kufika”

- kisa kinafaa kioana na methali


- Mwanafunzi azingatie methali husika
- maana ya hiyo iwe anayekutangulia si lazima akamilishe mkondo anaweza kukosa
kufika
- mtahiniwa atunge kisa kimoja
- aonyeshe sehemu zote mbili za methali
- dhana ya kutangulia ionekane vizuri
- dhana ya kutofika ijitokeze hata kama ni aya chache au sentensi moja

4. Andika kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo

Nilishusha pumzi kutokana na ufanisi niliopata baada ya masaibu tele.

Jibu

- Mtahiniwa ajikite katika kisa ambacho kinaelezea mambo magumu ambayo


yamezunguka maishani hadi kufikia upeo wa ufanisi
- Mtahiniwa pia aeleze namna ambavyo amefanikiwa maishani baada ya masaibu
mengi
- Kisah kisimuliwe katika nafsi ya kwanza

DOWNLOAD MORE RESOURCES LIKE THIS ON ECOLEBOOKS.COM

You might also like