You are on page 1of 12

Wimbo niupendao

© 2021 ya RTI International kwa nchi zote isipokuwa Jamhuri ya Kenya.


RTI International ni alama na jina la kibiashara la Research Triangle institute.
Haki ya kunakili ya Jamhuri ya Kenya inashikiliwa na wizara ya elimu Kenya.
Chapisho hili limefanikishwa kupitia kwa ufadhili kutoka kwa shirika la kimataifa na maendeleo la America (USAID) kupitia mradi wa USAID - Tusome.

Kazi hii inapatikana chini ya leseni ya Attribution Non-Commercial No Derivatives 4.0 International (CC BY-NC-ND 4.0). Ili kuona nakala ya leseni hii, tembelea
https://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0/legalcode ama tuma barua kwa Creative Commons, Sanduku la Posta 1866, Mountain View, CA 94042, USA.
Kunukuu na kutambua kazi asili — Ukinakili na kusambaza kazi hii yote nzima, bila kubadilisha maandishi au vielezo, tafadhali dondoa kazi hii ifuatavyo:
Imenakiliwa kutokana na kazi asili ya RTI International na kupewa leseni chini ya Attribution-NonCommercial 4.0 (CC BY-NC 4.0).
Kuigaiga na kusambaza — Ukiichanganya, kuibadilisha au kuitumia kama msingi wa kazi nyingine, tafadhali toa sifa kwa kazi asili kama ifuatavyo:
Imetengenezwa kutoka kwa kazi asili ya RTI International chini ya Leseni ya Attribution-Noncommercial 4.0 International (CC BY-NC 4.0).
Si ya Biashara — Usitumie kazi hii kwa nia ya kibiashara.
Kazi ya mtu wa tatu — Sio lazima RTI International kumiliki kila kipengele cha maudhui yaliyomo katika kazi hii. Hivyo basi, RTI international haikuhakikishii
ya matumizi ya kipengele chochote cha kazi ya mtu mwingine au baadhi ya kazi yake haitakiuka haki za watu hao. Utawajibika kutokana na hatari ya kudaiwa
kutokana na kuingilia haki za wengine. Ukitaka kutumia tena kipengele cha kazi hii, ni jukumu lako kuamua kama imeruhusiwa kutumia tena na kupata ruhusa
kutoka kwa mwenye haki ya kunakili. Baadhi ya mifano ya vipengele hivi ni majedwali, maumbo na picha.

Kimechapishwa nchini Kenya kwa ufadhili kutoka kwa USAID (U.S. Agency for International Development)
kupitia mradi wa Tusome Early Grade Reading Activity.
Toleo la Kwanza
Kimechapishwa 2015
Wimbo niupendao

Kila asubuhi nikiamka, mama


huniwekea maji ya kuoga bafuni.
Mama huniambia, ni vizuri kuoga.
Mtoto safi hapati magonjwa.
1
Kwanza, mimi husafisha kinywa kwa kupiga mswaki.
Ninatumia mikono kuoga.
Ninasugua mwili wote kuanzia kichwa, tumbo hata
magoti.

2
Nikimaliza kuoga, mimi huchana nywele kisha
hunywa chai.
Baada ya kunywa chai, mimi huweka mkoba wa
vitabu mgongoni.
Kisha humuaga mama na kwenda shuleni.
3
Mimi na rafiki zangu hutembea hadi shuleni.
Sisi hutembea kando ya barabara kwa uangalifu.
Hatuchezi barabarani.

4
Kabla ya kuingia darasani, mwalimu huangalia kama
tumechana nywele.
Mwalimu pia huangalia kama kucha zetu na nyuso
ni safi.
Akimaliza, sisi huingia darasani.
5
Darasani, sisi huimba wimbo wa sehemu za mwili.
“Kichwa, mabega, magoti, miguu, magoti miguu,
magoti miguu.”
“Kichwa, mabega, magoti, miguu, macho, pua,
masikio na mdomo.”

6
Baada ya wimbo, sisi hujibu maswali machache
kama vile:
Sehemu ya nyuma ya kichwa huitwaje?
Tunatumia sehemu gani kupumua?
7
Saa nne ikifika, sisi
huenda uwanjani
kucheza mpira.
Sisi hupiga mpira kwa
miguu, kichwa, magoti
na hata mgongo.
Sisi sote hufurahia.

Maswali
1. Mama hufanya nini kila asubuhi?
2. Mimi hufanya nini nikimaliza kuoga?
3. Mwalimu hufanya nini kabla hatujaingia darasani?
4. Tunatumia sehemu gani kupumua?
5. Tunatumia sehemu gani kupiga mpira?

You might also like