You are on page 1of 37

2023

SIRI YA KCPE
Mwinyi P. Kuria (Masharubu) 0727 064403
Lengo la KCPE 99%

Alfabeti ya Kiswahili

Ina herufi thelathini (30).

a,b,ch,d,dh,e,f,g,gh,h,i,j,k,l,m,n,ng`,ny,o,p,r,s,sh,t,th,u,v,w,y,z

Irabu/vokali (5) Konsonanti(25)

a,e,i,o,u b,ch,d,dh,f,g,gh,h,j,k,l,m,n,ng`,ny,p,r,s,sh,t,th,v,w,y,z

Jambo muhimu la kukumbuka katika mtihani

 Kiswahili hakina herufi: c, q na x.

Kuhesabu silabi(syllables) katika maneno

a) Anayejipendekeza c) Iliyowambwa
a-na-ye-ji-pe-nde-ke- za I - li-yo-wa-mbwa= silabi 5
1 2 3 4 5 6 7 8 1 2 3 4 5
b) kitakacholetwa d) Mwanasheria
ki-ta-ka-cho-le- twa= silabi 6 Mwa- na –she-ri-a
1 2 3 4 5 6 1 2 3 4 5

Jambo muhimu la kukumbuka katika mtihani

 Kwanza,tenganisha silabi kwa vistari (-)

Kuhesabu sauti/ herufi katika maneno

Sauti ni herufi (letters)


Mfano
M /a/k/u/t/a/n/o= sauti/ herufi 8
Ch /a/k/u/l/a= sauti/ herufi 6

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Jambo muhimu la kukumbuka katika mtihani

 Herufi/ sauti ch, dh, gh, ng`, ny, sh, th huhesabiwa zikiwa sauti/ herufi mojamoja

Aina/ kategoria za maneno

Kategoria Aina zake Mifano

NOMINO  Kawaida(common) Nguo,nyumba,saa,

(Nouns)  Maalum, za pekee Kenya, Kuria, Selina, ziwa Viktoria, shule ya Alliance,

Majina ya: watu, (proper) bahari ya Hindi


vitu, mahali na hali
mbalimbali.  wingi/fungamano Maji, mafuta, maradhi, mazingira, chumvi

(uncountables)

 Za jamii/makundi Timu, thurea, finyo, shada, mkungu, umati

(collective)

 Dhahania(abstract Kimya, wema, bidii, heshima

 Ambata(compound) Mwekahazina, askarikanzu, kiinuamgongo

 Vitenzi-jina Kusoma, kurauka, kujitahidi

Kitenzi Kukimbia, kuelewana


kilichowekwa ‘Ku”
kuchambua

VIVUMISHI  Sifa Sifa Ambishi Sifa Kapa au tasa (havibadiliki)

(Adjectives) -chafu, -ema, -zuri, -erevu, - Bora, safi, hodari, rahisi,


oga, -pya,- baya, -bovu, -
Maneno Ghali, maridadi,
tulivu, -eupe
ambayo hutoa
habari zaidi  Viashiria Huyu Huyo Yule Radidi Visisitizi
kuhusu
/vionyeshi Hili hilo lile Hii hii Ii hii
nomino
 Vimilikishi -angu, -etu -ako, -enu -ake, -ao

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
.Kivumishi  -A- unganifu Wa Cha La wa wa Ya Ya Kwa Pa Mwa
hueleza
a- Vya Ya za ya Za Ya- Ku- Pa- Mu-
nomino:
wa ya ku pa mu
Ki- li- u- u- i-
 ikoje?
u-u vi ya zi ya zi i-i
 ni ngapi?
 iko umbali  Viulizi -pi? , ngapi? gani?

gani? Huyu atavikwa pete gani?


 kama ni
halisi/ya  Halisi/ pekee -enye,-enyewe -ote,-o-ote -ingine,-ingineo

pekee?
 Vivumishi nomino Nomino moja inapoeleza nomino ya kwanza
Mkulima msomi analima vizuri.

Mwalimu kijana anafunza darasani.

 Idadi Kamili Isiyodhihirika Ya nafasi

Moja, sita, milioni Haba, kadhaa, Wa kati, cha pili,


kochokocho

VITENZI/VIARIFA( verbs) Rudi, stahi/ heshimu, kama, toa, iba, waza, chuma, katana,
salimiana, kata, (vitenzi vya silabi moja) -fa, -ja, -la, -wa, -
Maneno ambayo huarifu kuhusu kitendo
nywa.
kinachofanywa

VIELEZI(adverb  Wakati Alfajiri, mapema, hapo mwakani(mwaka ujao), hivi punde


)
 Mahali Juu, kando, barabarani, hadharani, maktabani
Maneno ambayo
hueleza kitenzi  Namna Haraka, kwa makini, kishujaa, kiutuuzima, bila woga,
taratibu,
kilifanyika: vipi?,
lini? wapi? mara  Idadi Mara tatu, mara kwa mara, aghalabu, kila wakati
ngapi?

VIHISISHI/VIINGIZI  Furaha Alhamdulilahi! Hoyee! Shabash! Keba!

(interjections)  Mshangao Salale! Lo! Kefule! Ebo! Do! Lahaula!

 Makubaliano/kuridhika Hewaa! Hewala! Safi! Taib! Pepa! Marhabaa!

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Maneno ambayo  Dharau/chuki na hasira Ebo! Kefule! Kha! Pukachaka!
huonyesha hisia.
 Kuapa Wallahi ! Billahi! Tallahi! Haki ya Mungu!

 Woga Toba! Mama wee! Msalie mtume !

 Kukataa Ng`o! Hata! Katu! Kamwe! Abadan kataan !

 Majuto Laiti! Lau! Ole wangu!

 Huruma Maskini!

 Kutakia kitu Hamadi!


kipone/kinusurike

VIHUSISHI Vya mahali Juu ya,chini ya,mkabala wa, mvunguni mwa

(preposition) Vya wakati Tangu,hadi,kuanzia

Maneno ambayo Vya kulinganisha kuliko,kushinda


huonyesha uhusiano baina
ya nomino

VIUNGANISHI Maana Mifano katika sentensi

 Na Huunganisha  Binti Dola na Kuria ni marafiki wakubwa.


(and) maneno au sentensi.  Spencilisa alijitahidi na akapita Kiswahili.
Hukanushwa kwa Spencilisa hakusoma wala hakupita Kiswahili.
(ukanusho wa ‘na’ ikiwa katikati ya vitenzi)
wala
 Mathalan, Kama vile,  Tulikula matunda mengi mathalani: maembe, machungwa,
Mathalani maparachichi na ndizi.
Kwa mfano
(for example, for Shule ya Ruaraka huongoza katika Nyanja mbalimbali
instance) mathalani katika masomo, michezo, ushairi na uigizaji.

 Mradi, ilmradi, Bora tu,  Sijali ukinichukia mradi unipe haki yangu.
Almuradi  Unaweza kukinunua kitu chochote ukitamanicho
Haidhuru
(as long as, almradi uwe na pesa.
provided, so long as: )  Si kitu ukinyamaza mradi ufike mkutanoni.
 Angalau, angaa, Hueleza jambo lililo  Mgombea yeyote wa urais lazima awe na angaa miaka
angalao, walau, bora zaidi thelathini na mitano.
falau  Ili upate fursa ya kujiunga na shule ya kitaifa lazima
(at least) upate falau alama mia nne.

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
 Sembuse, Seuze Hutumika  Mwalimu ameshindwa kujibu swali hilo seuze wewe?
kefu, kaifa, fakaifa kulinganisha  Umeshindwa kuandika insha moja kaifa kitabu?
(why not; what mambo.  Wanyama wanaathirika na ukame kefu binadamu.
about, let alone, not  Umeshindwa kununua mandazi fakaifa pizza?
to mention)

 Bali, lakini, Huonyesha kasoro  Timu ilijitahidi bali haikushinda.


ingawa, japo, ya jambo  Nimekula japo sijashiba.
ijapokuwa,  Ingawa nilimwita kwa sauti ya juu hakusikia.
licha ya  Licha ya mwalimu kutufunza kwa bidi kuna wanafunzi
(but, although , walikosa kusikiliza.
however)

 Maadamu, Kwa kuwa,  Maadamu mvua imenyesha hatutaenda sokoni.


Madhali  Alifungwa jela maadamu aliiba .
Kwa vile,
(now that,  Madhali Mark Nations ni kiranja mzuri Mungu atambariki.
because, provided, Kwa sababu  Mbuguz ataongoza katika Kiswahili kote nchini madhali
since) yeye ana bidii.
 Pindi/ punde Wakati uo huo  Pindi tu mgeni wa heshima alipowasili , tulianza sherehe.
(immediately, the  Pindi tu mwalimu alipoingia, tulisimama.
moment)

 Yakini Bila shaka,  Yakini Collins Munene ni gwiji wa Kiswahili; wanafunzi


(for sure, with no wote humsifu.
Kwa hakika
doubt)  Ama kwa yakini bidii hulipa.

 Yamkini, Huonyesha  Yamkini mvua itanyesha leo; sina uhakika.


yumkini, uwezekano  Yumkini mgeni atakuja leo; hajathibitisha.
Pengine,Huenda,  Asaa mwalimu Juma ana umri wa miaka hamsini, sina uhakika
Yawezekana  Yamkini likizo inaanza Alhamisi, tungali tunangoja ripoti
(Possibly, kamili kutoka kwa mwalimu mkuu.
probably,likely)

 Mintaarafu ya Kulingana na,  Mintaarafu ya katiba ya Kenya, ni hatia kumwajiri mtoto


 (according to; in mdogo.
kwa mujibu wa
accordance with,  Kwa mujibu wa ujumbe niliyopokea sherehe zitaanza
concerning, with adhuhuri.
regard to) .
 Ilhali, hali, na Huonyesha kinyume  Umemwachia funguo za sefu ilhali unajua yeye ni mwizi?
(whereas) na matarajio  Umemwachia mtoto kisu hali unajua kitamkata?
(kulalamika).  Umekataa kumaliza kazi ya Kiswahili ilhali unajua adhabu?
 Iwapo,Ikiwa, Huonyesha masharti  Iwapo hutasoma kwa bidii, hutafaulu.
endapo,iwapo, au kutokuwa na  Tutamwacha endapo hatafika mapema.
kama hakika.  Kama Mellanie ataitwa ataenda haraka.
(if)

 Lau, kama Huonyesha majuto  Lau si kwa mjomba wake tungeshindwa na kazi hiyo.
 Lau ningalikuwa tajiri ningalinunua gari kubwa.
Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
(if only)

 La sivyo, Lau  Soma kwa makini la sivyo hutapita mtihani.


sivyo  Tii sheria za nchi lau sivyo utaadhibiwa.
(Or else; Failure  Rudisha vitu vya Andy Kihara la sivyo hatakupa tena.
to which)

 Minghairi ya, Bila ya  Usianze kula minghairi ya kunawa mikono.


bighairi,pasipo,pas  Msithubutu kwenda nyumbani bighairi ya kumaliza kazi.
i na  Huwezi kufaulu maishani pasipo kufanya bidii.
(without; unless,
except)

 Kwa ajili ya, Kuonyesha sababu ya  Tulienda hospitalini kwa minajili ya kutafuta matibabu.
Kwa minajili ya jambo Fulani  Wakili alienda kortini kwa ajili ya kumtetea mteja wake.
(for the purpose
of)

 Kana kwamba Mfano wa  Anazungumza kana kwamba yeye ni mgonjwa.


(as if)  Yeye huringa kama kwamba dunia yote ni yake.
 Ila, isipokuwa  Niliongoza masomo yote ila Sayansi.
(except, apart  Wanafunzi wote walikuwa huku ila Gakombe.
from)

 Ama…au  Nataka niwe ama daktari au mhadhiri wa chuo kikuu.


(either…or)  Ama ufanye kazi au urudi nyumbani.
 Licha ya Huonyesha kinyume  Licha ya nyumba kuwa kubwa haikuwatoshea wageni.
( inspite of, cha matarajio  Alishinda katika riadha licha ya kuwa mgonjwa.
although)

 Licha ya Viunganishi vya Elaine Nyambu ni msichana mrembo. Ana sauti ya ninga. Isitoshe,
Isitoshe, vilevile, kuongezea
ana macho ya gololi. Aidha, meno yake ni meupe pepe na
kando na,
yamepangika vizuri. Isitoshe, ana shingo ya upanga na nywele za
halikadhalika, pia,
singa. Fauka ya hayo, ana ngozi laini na midomo yenye wekundu
mbali na, zaidi ya,
juu ya, fauka ya, wa ini. Hakika yeye ni malaika.
Aidha, waaidha,
(in addition to;
furthermore;
besides)

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Viambishi

Neno Viambishi awali Mzizi Viambishi tamati


Unapendelea u-na- -Pend- -el-e-a

Waliongozana Wa-li- -ongoz- -an-a

Anayeimbisha a-na-ye- -Imbish- -ish-a

Chunguziana -------------------------- -chunguz- -i-an-a

Waliogeukia Wa-li-o- -geuk- -i-a

Wanaobusiana Wa-na-o- -bus- -i-an-a

yaliyomwagwa Ya-li-yo- -mwag- -w-a

mnamokataliwa m-na-mo- -kata- -liw-a

zilizochanganywa Zi-li-zo- -changany- -w-a

atakayerudishiwa a-ta-ka-ye- -rudish- -iw-a

aliyenitwangisha a-li-ye-ni- -twang- -ish-a

zilizovuliwa Zi-li-zo- -vu- -liw-a

waliowazalishia Wa-li-o wa- -za- -lish-i-a

sogeleana ---------------------- Soge- -le-an-a

V.I.P.(Very Important Point)

 Viambishi awali hutenganishwa sawa na tunavyotenganisha silabi.


 Mzizi/ shina/ kiini ni sehemu ya neno isiyobadilika.
 Viambishi tamati HAVITENGANISHWI KAMA SILABI KAMWE ; huwa tunatenganisha kwa
kuzingatia viambishi vya minyambuliko mbalimbali ya vitenzi.

kauli kiambishi mfano


kutendea e, i omb-e-a, pig-i-a,
kutendeana ean, ian omb-ean-a, pig-i-an-a,
kutendwa w som-w-a
kutendewa ew, iw omb-ew-a, pig-iw-a
kutendeka ek pend-ek-a
kutendesha esh, ez, ish, iz kom-esh-a, ing-iz-a
kutendana an finy-an-a

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Siri nyingine muhimu
Tahadhari sana na vitenzi ambavyo huishia kwa irabu/vokali mbili zikifuatana mwishoni na

ambavyo, aghalabu, vikinyambuliwa huambishiwa ‘ li’ au ‘le’. Hiyo `li`au ‘le’ hushikanishwa
na viambishi vya mnyambuliko( isipokuwa katika kauli ya kutendeana ambapo ‘li’au ‘le’
hujisimamia).
mifano

Kitenzi kiishiacho Kitenzi Mzizi Viambishi tamati


kwa irabu mbili kilichonyambuliwa

Oa Olewa -o- -lew-a

Ua Uliwa -u- -liw-a

Kaa Kalishwa -ka- -lish-w-a

Vaa Valika -va- -lik-a

Vua Vulisha -vu- -lish-a

Zaa Zaliwa -za- -liw-a

fungua funguliana -fungu- -li-an-a

toa toleana -to- -le-an-a

Aina za sentensi

(i) Sentensi za taarifa

Hutoa taarifa kuhusu jinsi mtu alivyo, kitu kilivyo au hali ilivyo.

Sentensi za taarifa elezi/arifu Sentensi za taarifa ulizi


 Uliletewa hilo. Uliletewa hilo?
 Kazi imeisha. Je, kazi imeisha?
 Uvutaji bangi ni haramu. Ni kweli kuwa uvutaji bangi ni haramu?

(ii) Sentensi za amri/maagizo


 Meza tembe mbili kila siku.
 Andika vizuri.
(iii) Sentensi za masharti
Huonyesha uwezekano, utegemeano wa mambo au kutokuwa na uhakika.
Sentensi hizi hutumia:
Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
(a) ‘ki’ ya masharti.
(b) Hali tegemezi ‘nge’/ngali
(c) Maneno: huenda, pengine, labda, yawezekana, yamkini.

Mifano

 Angekuwa rafiki wa kweli angenifaa.


 Ukijitahidi utafanikiwa maishani.
 Pengine mvua itanyesha jioni.

Mnyambuliko wa vitenzi

Kutendea/kutendewa

(a) Kuonyesha mahali kitendo kilipofanyiwa.


Mfano
Ashley Wangui anachezea mpira uwanjani (kutendea)
Mpira unachezewa uwanjani na Ashley Wangui (kutendewa).
(b) Kuonyesha kufanya kitendo kwa niaba ya mwingine
Mfano
Martin Gichuhi anampangia Victor Kiragu vitabu. (kutendea)
Victor Kiragu anapangiwa vitabu na Martin Gichuhi. (kutendewa)

Kutendwa

Hutumiwa kuonyesha kuwa kitu au mtu anayepokea kitendo lakini si moja kwa moja.Aidha
huonyesha kuwa jambo lilifanywa kwa niaba ya mtu.

Mfano

(a) Mwinyi anakunywa maji. (Kauli ya kutenda)

Mtenda kitendo kitendwa


(b) Maji yananywewa na Mwinyi. (Kauli ya kutendwa)

Kitendwa kitendo mtenda


(c) Mafundi watajenga nyumba.
Nyumba zitajengwa na mafundi.(kauli ya kutendwa)

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Kutendesha/kufanyiza

Huonyesha kufanya, kulazimisha, kuongoza, kusaidia kitu au mtu kufanya jambo.

Mfano

i. Tatuli alimfanya Jeni kufahamu jambo hilo.

Tatuli alimfahamisha Jeni jambo hilo. (kutendesha)

ii. Yuna alimfanya Ruga aandike barua.

Yuna alimwandikisha Ruga barua.(kutendesha)

Kutenda Kutendesha/kufanyiza
Kutenda Kutendesha/kufanyiza

Oa Oza (ku)la Lisha


Fuata Fuatiliza Poa Poza
Lewa Lewesha/levya Ona Onesha/onyesha
Lia Liza

Kutendana

Mhusika mmoja anamtenda mwenzake kitendo na yeye anamtenda vivyo hivyo alivyotendwa.

Fuata - fuatana Pisha - pishana

Tenga - tengana Ona - onana

Kosa - kosana Himiza - himizana

Bisha - bishana Taja - tajana

Uundaji wa maneno

Kuunda nomino kutokana na vitenzi

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Vitenzi Nomino/majina

Kawaida Hali(dhahania) Mtendaji

Dhulumu dhuluma udhalimu Dhalimu

iba - wizi mwizi

imba wimbo uimbaji mwimbaji

andika mwandiko uandishi mwandishi

ua kifo uuaji mwuaji

lipa malipo ulipiaji mlifi

rithi mirathi urithi mrithi

lia kilio/mlio ulizi mlizi

tibu maibabu utabibu tabibu

sali sala usalihina salihina

safari safari usafiri msafiri

lima kilimo ukulima mkulima

winda windo uwindaji mwindaji

anza mwanzo uanzilishi mwanzilishi

soma somo usomi/usomaji msomaji

iba - wizi mwizi

hama mahame uhamaji mhamaji

umba maumbile uumbaji mwumba

ua mauaji uuaji mwuuaji

kumbuka kumbusho/ kumbukizi/ ukumbusho mkumbushaji


kumbukumbu
oa uoaji mwoaji
ndoa
lima ukulima mkulima
kilimo

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Vivumishi vya sifa kutokana na vitenzi
Kitenzi Sifa kitenzi Sifa

tii tiifu Angalia Angalifu

iva bivu danganya danganyifu

nyamaza nyamavu potea potevu

ona onevu amini aminifu

vumilia vumilivu danganya danganyifu

sikia sihivu kamilika kamilifu

cheka cheshi stahimili stahimilivu

staafisha staafu dhulumu dhalimu

samehe samehevu changamka changamfu

legea legevu angalia angalifu

chafua chafu kosa kosefu

safisha safi timia timilifu

haribu haribifu okoa okovu

nyoosha nyoofu tulia tulivu

potoka potovu sumbua sumbufu

Kinyume

Vinyume vya vitenzi


(i) Kutendua/ Kufanyua (ii) Kubadili uhalisia

Kitenzi Kinyume Kitenzi Kinyume

Fumba Fumbua Meza Tapika

Funga Fungua Andika Futa

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Ezeka Ezua Cheka Lia

Bandika Bandua Tabasamu Nuna

Umba Umbua Kufa Fufuka

Panga Pangua Tenga Unga

Lewa Leuka Enda Rudi

Angika Angua Bariki Laani

Ficha Fichua Lala Amka

Bana Banua Panda Shuka/vuna

Ziba Zibua Pata Kosa

Tia Toa Wahi Chelewa

Funika Funua Kashfu Sifu

Panda Pindua Ganda Yeyuka

Ficha Fichua Chafua Safisha

Kaza Kazua Uza/nadi Nunua

Fuma Fumua Kauka Loa

Kunja Kunjua Zaa Avya

Ania Anua Penda Chukia

Pamba Pambua Dunisha Dumisha

Choma Chomoa Zubaa Zinduka

Kwea Shuka

Kataa Kubali

Haramisha Halalisha

Heshimu Dharau

Twika Tweka

Tekeleza Telekeza

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Vinyume vya sifa
Sifa Kinyume Sifa Kinyume

-nene/-nono -embamba -kubwa -dogo

Thabiti/madhubuti/ -legevu -tamu -kali/chungu


jadidi/imara
-bivu Rahisi Ngumu/epesi
-bichi
Shujaa/jasiri -kali -pole
-oga
-zee Karimu -choyo/ bahili/ -
-pya nyimivu
-zuri/-ema Safi
-ovu -chafu
Laini/-epesi -pana
-gumu -embamba
Bandia Tajiri
Rasmi Maskini
Maridhawa -refu
Haba -fupi
Bahasa -eupe
Ghali -eusi
Halali -kali
Haramu -butu
Shari
Shwari

Vinyume vya jinsia


Kiume Kike Kiume Kike

Babu Nyanya/bibi njeku Mori

bin Binti mori/dachia Njeku

pora Tembe mjane Mfaruku

jogoo/jimbi Koo ghulamu/mvuli/rijali Banati/kigori

shaibu/buda Ajuza/bikizee fahali Mtamba

ami/amu Halati kapera/mseja Mwanamwali

adamu Hawa mwamu Wifi

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
mtanashati Mrembo mfalme Malkia

gumba Tasa

Vinyume vya nomino/majina


(Hali ya pindu)
Jina Kinyume Jina Kinyume

Razini Chakaramu Juu Chini

Sakafu Dari Mauti Uhai

Mji Kijiji Pwani Bara

Dhiki Faraja Baridi Joto

Ukubwa Udogo Uongo Ukweli

Shibe Njaa Giza Mwangaza

Kiongozi Masika Mchana Usiku

Raha Karadha Amani Ghasia/fujo

Mzee Kijana Shina Kilele

Ujinga Werevu

Jambo muhimu katika kujibu swali kwenye mtihani

Tofautisha kati ya kinyume na ukanushaji

Ukanushaji

Kukanusha ni kukataa au kupinga


Kanuni za kukanusha Kanusha vitenzi VYOTE katika sentensi
isipokuwa:
Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
(i) Kitenzi chenye ‘o’ rejeshi  Kanusha vitenzi VYOTE.
(awali/tamati).  Kikanushi wala huwekwa kabla ya
(ii) Kitenzi kinachofuata kirejeshi ‘amba’. kitenzi cha mwisho.

Mifano  Kiambishi ‘ka’ hukanushwa kwa


kiambishi wakati cha kitenzi cha
 Shida ikiwa kubwa achana nayo.
kwanza.
Shida isipokuwa kubwa usiachane nayo.
Mifano
 Mchwa akijenga kichuguu huishi humo.
Mchwa asipojenga kichuguu haishi (i) Selina amepika chakula kikaiva.
humo.
Selina hajapika chakula wala hakijaiva.
 Mahali kuliko na ukame kwahitaji
msaada. (ii) Maji yalichotwa kisimani

Mahali kusiko na ukame hakuhitaji yakaisha.

msaada. Maji hayakuchotwa kisimani wala


hayakuisha.
 Meza iliyoundwa na seremala iliuzwa.
(iii) Mwinyi ameenda maktabani
Meza iliyoundwa na seremala
akaazima kitabu.
haikuuzwa.
 Gari lililonunuliwa liliuzwa tena. Mwinyi hajaenda maktabani wala

Gari lililonunuliwa halikuuzwa tena. hajaazima kitabu.

Kukanusha ‘ki’ ya masharti.


 Abiria ambao wamejeruhiwa
‘ki’ ya masharti hukanushwa kwa ‘sipo’
wametibiwa.
Abiria ambao wamejeruhiwa Mfano
hawajatibiwa.
Ukija nitakukaribisha.
 Nguo ambazo zilinunuliwa
Usipokuja sitakukaribisha.
zimerudishwa.
 Nguo ambazo zilinunuliwa Kukanusha kiunganishi ‘na’
hazijarudishwa.
‘Na’ hukanushwa kwa ‘wala’

Mfano
Kukanusha sentensi yenye ‘ka’ ya
Mtoto amekula na ameshiba.
mfuatano wa vitendo
Mtoto hajala wala hajashiba.

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Jambo muhimu katika kujibu swali kwenye mtihani
Bainisha sehemu zote zitakazobadilika kwanza

Njeo/nyakati

Wakati/Njeo Uliopita Timilifu ( Uliopo ( na) Ujao ( ta) Mazoea ( hu ) Tegemezi


(li) me) (nge/ngali)

kikanushi Ku Ja na ta hubaki Hukanushwa Singe/singali


huondolewa kama wakati
na herufi ya uliopo
mwisho
huwa ‘-i’

Ukanusho

Ki na ndi Amri Vitenzijina: Ku ni

ukanusho sipo Wala si si mfano:njoo hapa-usije to si mfano:


hapa
kusoma- mimi ni wakili.
kutosoma
Mimi si wakili.

Wingi

U-U U-ZI A-WA


Uyoga- Uyoga Ubao/bao –mabao Seremala - maseremala
Udongo-udongo Uzi - nyuzi Mwashi - waashi
Ufisadi-ufisadi Ufagio – fagio Baharia - mabaharia
Wema-wema Uwanja - nyanja Karani - makarani
Usafi-usafi Uteo – teo Fundi mafundi
LI-YA Waraka - nyaraka Tarishi - matarishi
Jivu - majivu Utamaduni - tamaduni Mtume - mitume
Pazia - mapazia Ufunguo - funguo Kobe – makobe

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Karai - makarai Waya - nyaya Jogoo – magoo
Kabati - makabati Uga - nyuga Sogora – masogora
Kufuli - makufuli Uwanja - Nyanja Chura – vyura
Blanketi - mablanketi Ubawa - mbawa Chura – machura (matopasi)
Bao - mabao Ukanda - kanda Wakili -mawakili
Soko - masoko Wadhifa - nyadhifa Hakimu-mahakimu
Bawa - mabawa Uta-uta Jaji-majaji
Ua-nyua Rubani -marubani
Wakati-wakati Dereva-madereva
Moyo-nyoyo
I-ZI U-YA YA-YA
Familia - familia Unyoya - manyoya maradhi-maradhi
Taa - taa Ulezi - malezi mazingira-mazingira
Dawa - dawa mandhari-mandhari
Saa - saa matibabu-matibabu
Pua - pua makao-makao
Timu - timu mafuriko
Shule - shule I-I
Barabara - barabara Sukari-sukari
Chupa - chupa Chai-chai
Bahari-bahari Damu-damu
Nchi-nchi Hewa-hewa
Asali-asali
Mvua-mvua

Kanuni za kuandika usemi taarifa

 Wakati uliopita ndio hutumiwa.


 Alama za kunukuu (“ ” ), hisi (!), kiulizi (?) na nukta pacha (:) (ya kutenganisha msemaji na
yale aliyosema) HAZITUMIWI.

kubadilisha usemi halisi kuwa usemi taarifa.

Usemi halisi Usemi halisi Usemi halisi

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
(a) Viashiria vya karibu huwa Hii Hiyo/ile
vya mbali/mbali sana Huyu Huyo/Yule
(b) Nafsi ya kwanza na ya pili Mimi (ni) na wewe (u) Yaya (a)
huwa nafsi ya tatu Sisi (tu) na nyinyi (m) wao (wa)
(c) Vimilikishi vya nafsi ya -angu na -ako -ake
kwanza na nafsi ya pili -etu na –enu -ao
huwa vya nafsi ya tatu
(d) Wakati hali timilifu huwa Me ….likuwa…me
wakati timilifu hali ya “Nimeandika insha,” akasema. Alisema kuwa alikuwa ameandika
kuendelea insha.
(e) Wakati uliopo hubadilika Na ….likiwa... ki
kuwa wakati uliopita hali “Tunajivunia shule yetu,” Mwanafunzi alisema kuwa
ya kuendelea mwanafunzi akasema. alikuwa akijivunia shule yao.
(f) Wakati ujao huwa hali Ta Nge
tegemezi Akasema,”Nitaenda kesho.” Alisema kuwa angeenda siku
ambayo ingefuata.

Usemi halisi Usemi taarifa


(g) Aliuliza Aliuliza/alitaka kujua
(h) Kiambishi tamati Huonyesha amri/maagizo.
‘-ni’ mwishoni mwa kitenzi : Mfano Aliwaamuru waweke vyumba safi.
“Viwekeni vyumba safi,” alisema.
(i) Juzi Siku mbili zilizopita/zilizotangulia
(j) Jana Siku iliyopita/iliyotangulia
(k) Leo Siku hiyo/ile
(l) Kesho Siku iliyofuata/ambayo ingefuata
(m) Kesho kutwa Siku mbili zilizofuata
(n) Wiki ijayo Wiki ambayo ingefuata
(o) Mwaka ujao Mwaka ambao ungefuata

Kuandika ukubwa na udogo.

Kundi Sheria Mifano Ukubwa Udogo

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
1. Yaanzayo kwa Ondoa M Mguu- guu Pachika
silabi ‘M-‘ pekee Mlima- lima Ki (umoja)
na hufuatwa na Mzigo -zigo Vi (wingi)
silabi mbili au Mkoba -koba mwanzoni
zaidi Mkoba-koba Mwa
neno
2. Yaanzayo kwa Ondoa M Mto - jito lililo
silabi ‘M-‘ pekee Weka Ji Mke - jike katika
na kufuatwa na Mji - jiji ukubwa
silabi moja tu. Mbwa – jibwa
3. Yaanzayo kwa Ondoa K Kiatu - jiatu
silabi ‘Ki-‘ Weka J Kisu - jisu
Kikombe - jikombe
4. Yaanzayo kwa Ondoa Mw Mwana - jana
Mw- Weka J Mwizi - jizi
Mwanamke - janajike
Mwanaume - janadume
5. Yaanzayo kwa U- Ondoa U Uteo - jiteo
na kufuatwa na Weka Ji Ufagio - jifagio
silabi mbili au Ubao - jibao
zaidi
6. Yaanzayo kwa U- Ongeza Ji mwanzoni Ua - jiua
na kufuatwa na Uta - jiuta
silabi moja tu Ufa - jiufa
7. Yaanzayo kwa JI- Ongeza Ji mwanzoni Jina - jijina
Jino - jijino
Jiko - jijiko
8. Yaanzayo kwa Ongeza JI- Nyundo - jinyundo
Ny- mwanzoni. Nyati - jinyati
ISIPOKUWA Nyani-jinyani
 Nyoka Nyoka - joka
 Nyumba Nyumba - jumba

 Nyungu Nyungu – jungu

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
9. Yaanzayo kwa Ondoa N/M Ndege - dege
sauti Ndoo - doo
mwambatano Ndizi - dizi
Nd- Mbuga - buga
Mb- Mbuzi - buzi
Ng- Nguo - guo
Nj- Ngazi - gazi
Ng’- Ng’ombe – gombe
10. Majina mengine Ongeza Ji- mwanzoni Samaki - jisamaki
Kofia - jikofia
Kanzu - jikanzu
Pete – jipete

Uakifishaji

(a) : Nukta pacha, (a) Hutanguliza maneno katika orodha.


Nukta mbili, Mfano : Mama aliniagiza ninunue matunda kama vile :
Koloni parachichi,fenesi,tomoko na chungwa.
(b) Hutenganisha msemaji na maneno aliyosema.
Mfano
Mwinyi: Napenda Kiswahili.

(b) ; Nukta mkato, (a) Hutenganisha sentensi kuonyesha kuwa maneno baada ya
Semi koloni nukta mkato (;) ni ufafanuzi wa sehemu iliyotangulia.
Mfano
Hasira hasara; Mtu akikasirika huharibu mambo.
(c) ( )Mabano/parandesi Hufungia maelezo ya ziada kwenye sentensi.
Mfano:mwalimu wetu(Masharubu Mwinyi)hufunza vyema.
(d) / Mkwaju Huonyesha visawe.
Mfano:mtu/mja/binadamu/adinasi/mahuluku/insi
(e) “ ”Vinukuu/Alama za Kufungia maneno halisi yasiyosemwa.
usemi Kumbuka:
Kama nukuu imekatizwa, sehemu ya pili huanza kwa herufi ndogo.
Mfano
KCPE 2018-23

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
“Naam,” akasema, “nitakusaidia.”
(f) ‘ ’ (a) Huonyesha nukuu ndani ya nukuu.
Mfano
Mwalimu alisema, “Hayati Nyerere alipenda kusema, ‘Ukabila ni
hatari,’ hivyo basi tusiwe wakabila.”
(b) Kutaja majina ya: Magazeti, sinema, vitabu n.k
Mfano
Tutasoma gazeti la ‘Taifa Leo.’
...nukta za dukuduku Huonyesha kuwa maelezo Fulani yameachwa na kwamba kauli
inaendelea
Mfano
Hakika,asiyesikia la mkuu...
-kistari Kuyafungia maneno ya ziada kwenye sentensi ambayo si lazima
yawepo kwenye sentensi.Mfano Mwalimu Mwinyi – aliyestaafu
mwaka jana- alikuwa gwiji wa lugha wa Kiswahili.
` Ritifaa/king’ong’o Hutumiwa : a) kuonyesha kwamba herufi imeachwa katika neno
Mfano : ‘sikate tamaa - usikate tamaa.
b) kuonyesha maneno yaliyo na sauti ya king’ong’o
(zinazotamkiwa puani) .
Mfano : nga’aa,ng’oa.

Matumizi ya viambishi mbalimbali na maneno maalum

Matumizi ya Mifano katika Matumizi ya KARIBU


KI sentensi
1. Kifananishi/  Tembea kijeshi. 1.Nusra 1. Salale! Mtoto
 Valia kitamaduni. karibu aanguke.
Kielezi 2. Karibu Esta awe
 Cheka kijinga.
Kifani Ki. mshindi.
3. Kazi karibu
imlemee.
2.Ngeli  Usikiangushe chuma. 2.Idadi ya 1. Makini ina karibu
 Chakula kilipikwa. makadirio/ walimu 300.
(kiambishi 2. Mawakili hulipwa
ngeli)  Kiazi kinanuka. Makisio kima cha karibu
 chungu hakijavunjika. shilingi milioni.
takriban
3.Udogo  kijito kitafurika. 3.Makaribisho 1. Karibu tule.
 usiache kijikaratasi. 2. Karibu Kenya;
hakuna matata.
Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
4.Masharti Ki...ta 4.Maagano 1. Safiri salama
karibu tena.
hukanushwa kwa sipo. 2. Kwaherini karibu
mara nyingine.
 ukisoma utafaulu.
 mkitafuta mtapata.
5.wakati …kuwa…ki…. 5.kihusishi cha 1. Simama karibu
endelezi / .kuta…ki…. mahali meza.
2. Precious hupenda
Hali ya ….pata…ki… kuketi karibu na
kuendelea dirisha.
 Tumekuwa tukisoma 3. Kwangu si karibu
vitabu. na kwao.
 ulimkuta akifanya nini? 4. Pendo yu karibu na
 Mvua itatupata Gathoni.
tukilima.
6.vitendo  Usile ukiongea 6.Kielezi cha 1. Mtihani itaanza
vinavyofanyika utasakamwa. wakati hivi karibuni.
wakati mmoja  Ng’ombe anakamwa 2. Tutaoana hivi
akila. karibuni.
Vitendo 3. Hivi karibuni
 Tuliimba tukicheza
sambamba Paulo
densi.
atastaafu.
 Mwinyi hufunza
akichekesha.

7.Kiwakilishi  Chuma ki motoni.


(huru cha  Kikulacho ki nguoni
mwako.
nomino)
 Kisu ki mfukoni.
tanbihi  Choo ki wazi.
Kikiwa peke
yake
8.Mnyambuliko  Huku hakukaliki.
(Kutendeka)  Hati yake haisomeki.
 Haambiliki hasemezeki.

MATUMIZI YA NA MATUMIZI YA KA
1.Ufupisho wa nafsi 1. Na mimi - 1.Mfululizo/mfuatano/ 1. Nilimfunza
nami Evans akajua.
2. Na sisi - Mwandamano wa 2. Alishinda
nasi vitendo akashangiliwa.
3. Na wewe - 3. Alituzwa
nawe akafurahi.

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
4. Na wao -
nao

2.Mtendaji 1. Ametuzwa na 2.Amri 1. Kamwite aje


mfadhili. upesi.
2. Nchi huongozwa kuagiza 2. Nendeni
na rais. mkajisomee
3. Mtavamiwa na vitabu.
magaidi. 3. Nenda
ukamsaidie.
3.Kiunganishi 1. Munyiva na 3.Kuonyesha kuwa 1. Nyumba
Melissa ni kitendo kimetendeka imekamilika.
masahibu. 2. Maji
2. Pika wali, nyama yamemwagika.
na chapati.
3. Kiswahili na
Kiingereza ni
lugha rasmi.
4.Pamoja na 1. Fuga kuku 4.Kusudi/lengo/nia 1. Alienda shuleni
na nguruwe. akasome.
2. Endeni na 2. Nimeenda
yeye kwao. nikamsalimie.
5.Umilikiji 1. Tunavyo vitabu MATUMIZI YA KIAMBISHI NI
bora.
2. Mwinyi ana gari
zuri.
3. Wewe huna 1.Mahali Darasani
pesa. (PA-KU-MU) Njiani
6.Hali ilivyo 1. Kenya kuna
amani. Msalani
2. Yaonekena siku
hizi ana
maringo.
3. Tumekubaliwa
na shinda tele.
7.Wakati uliopo 1. Tunasoma wao 2.Nafsi ya kwanza- 1. Ninaenda
wanacheza. umoja maabarani.
2. Taa zinawaka. 2. Usinikumbushe
(inasimamia mimi) yaliyopita.
3. Nyinyi
mnanihadaa.
8.Wakati uliopo 1. Naja kwako. 3.Wingi na amri Umoja
2. Napika chakula Wingi
[Hali kitamu.
isiyodhihirika/huria] 3. Naenda kujionea Toka tokeni
mwenyewe.
Tanbihi Fika fikeni
Yaonyesha nafsi Ondoka
pia. ondokeni

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
9.Makubaliano 1. Mgeni naaje 4.Kitenzi 1. Messi ni gwiji
akitaka. wa soka
2. Haya nawafanye (kishirikishi 2. Kiswahili ni
watakavyo. kipungufu) somo rahisi
10.Mnyambuliko Tendeana 5.kulinganisha 1. Beyonce ni
tendana ninga.
 Tendeana (sitiari) 2. Kinjabi ni
 tendana Pimiana mpingo;mweusi
pimana pi!
3. Elimu ni uti wa
Someana
mgongo bora ya
somana siku za usoni.
Tumiana
tumana

MATUMIZI YA JI MATUMIZI YA KWA


1. Mtendaji Msomaji,mkimbiaji 1.Kifaa/ala 1. Lima kwa jembe.
(matumizi) 2. Kata nyama kwa kisu.
Mwogeleaji, mshonaji 3. Safari kwa garimoshi.

2. Nafsi 1.Ninajiheshima 2.Sababu/nia 1. Alituzwa kwa bidii zake.


/ 2. Tunampenda Kuria kwa
Tunajiheshimu ucheshi.
lengo/azma/ 3. Alifungwa jela kwa wizi.
2.Mnajiponza
kusudi
Unajiponza

3.Hali Ushonaji,ukimbiaji,usomaji 3.Mahali 1. Huku ni kwa daktari Amanda.


2. Tutaenda kwa Omolo
Ufundishaji uhusiano wa tumwone.
mtu na 3. Usikae kwa walevi ;si wazuri.
mahali
4.Ukubwa Jike jijiwe 4.Kielezi 1. Karibishwa kwa heshima.
2. Soma kwa makini.
Jito jijicho (namna/jinsi) 3. Ita kwa sauti.
Jibwa jichwa
5.Pamoja 1. Walimu kwa wanafunzi
walienda karamu.
2. Sisi hula sima kwa mboga.
6.Sehemu ya 1. 1/3 moja kwa tatu
kitu 2. Nusu kwa nusu.
kizima/Akisa 3. Bao moja kwa manne (1:4).
mi

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
7.Nahau/sem 1. Ana kwa ana.
i 2. Sako kwa bako.
Matumizi ya PO 3. Bega kwa bega.
4. Moja kwa moja.
5. Shilingi kwa ya pili.
8.A – 1. Kufunza kwa Masharubu ni
Unganifu kuzuri sana.
2. Kuimba kwa Rihanna
Hutumiwa na kunapendeza.
kitenzi jina 3. Kuzunguza kwa Stephen
hupendeza.
9.Umilikaji 1. Nyumbani kwangu kuna
wakati maua.
mahali 2. Kwao kuna vinywaji vyovyote.
3. Kucheza kwako na masomo
kutakuletea shinda.
1. Yeye hugugumiza 1. Hapo 10.Swali 1. Kwa nini umechelewa?
anapozungumza. pamechafuka. najibu Nimechelewa kwa sababu ya
2. Nilipomkataza 2. Waliposimama msongamano wa magari.
alikataa pana mavumbi.
kusikiliza. 3. Nlipoketi ndipo 2. Umekosa kumaliza kazi kwa
3. Nyumba pana siafu. sababu ipi?
ilipoanguka 4. Panapolimwa Samahani ,nilishindwa kumaliza
tuliponea chupu lazima pawe na kazi kwa kuwa nyumbani hakuna
chupu. rutuba. umeme.
11.Kuonyesha 1.Alifungwa kwa miaka mingi.
kipindi cha
2.Tulikaa gwarideni kwa saa tatu
wakati
mfululizo.
3.Nimekuwa rubani kwa karibu
miaka kumi.

Maamkuzi

Salamu jibu Wakati Salamu jibu Wakati

Chewa chewa asubuhi Ndoto njema Ya mafanikio usiku

Sabalkheri alkheri asubuhi Lala unono Nawe pia usiku

Masalkheri alkheri jioni Kwaheri Ya kuonana Maagano ya muda


mfupi

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Wambaje/wasemaje Sina la Wowote Buriani Buriani dawa Maagano ya muda
kuamba mrefu

Salaam aleikum Aleikum Wowote Karibu tule starehe Kukaribisha mtu


salaam chakula

chewa chewa Wowote Ugua pole Asante nishapoa Kumpa pole mtu
mgonjwa
(Kwa watoto pekee)

Maneno ya adabu

Neno Jibu Wakati

1. Hodi Karibu/kongoni Neno la kubishia mlango ,uombaji ruhusa ya kuingia kama vile nd
nyumba.Piga hodi au bisha hodi.

2.Tafadhali Unayo mara Kumwomba mtu afanye jambo kwa hisani yako.

3.Kunradhi/niwie Ni radhi Kuomba msamaha.


radhi

4.Simile/heria/sumil Hewaa/ewaa Unapoomba kupishwa njia upite.


e,habedari

Neno Jibu Wakati

5.Asante Hewala Kutoa shukrani kwa wema au fadhila uliyotendewa.

6. Ugua pole Asante/nishapoa Huambiwa mgonjwa ili kumtakia afueni.

7. Pole Nishapoa a)kumliwaza aliyefikwa na jambo baya k.v.kupoteza kitu.

b) kumpoza mtu aliyetoka safarini au aliyekamilisha kazi ngumu.

8.makiwa Tunayo au yamepita Kumfariji au kumhani mtu aliyefikwa na msiba wa kufiwa.

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
9.samahani Umesamehewa a)Upochachawiza ,kumdakiza au kumkata kalima mtu katika
mazungumzo.

b)kuomba radhi au kumtafadhalisha mtu.

10. hongera Asante au nimehongera Kumpongeza mtu aliyefanya jambo zuri sana k.v. kupita
mtihani,kujifungua mtoto n.k.

TAMATHALI ZA USEMI

Tashbihi/tashbiha

Ulinganishaji wa vitu kwa kutumia Mifano


majina:kama,mithili ya,mfano wa,tamthili
ya,mshabaha wa,ja...

i. Lingana kama sahani na kawa vii. stawi kama mgomba

ii. Fahamikiana kama kinu na mchi viii. chipuka kama uyoga

iii. Baidika kama ardhi na mbingu ix. pofu kama jongoo/popo

iv. Ambatana kama kupe na mkia x. lingana mithili ya sahani na kawa

v. Chafu kama fungo/kilihafu xi. shirikiana mithili ya viungo vya


mwili
vi. Shirikiana kama viungo vya mwili

Misemo na nahau

Msemo au nahau maana Ramba kisogo Sema mabaya ya mtu hasa


anapokuwa hayupo
Kichwa chepesi Kuelewa mambo haraka
Ona kisunzi Kuwa na kizunguzungu
Tia mrija Tegemea mtu kwa kila
jambo Bwagia zani Sababishia mtu matatizo

Piga vijembe Sema mtu kwa mafumbo

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Vimba kilemba cha Kumpa mtu sifa za urongo Kula mwata/mumbi Pata taabu
ukoka
Kula mwande Kosa kupata ulichotarajia
Jitia purukushani kupuuza
Kisebusebu na kijoyo Kujifanya hutaki kiyu ilhali
Msemo au nahau maana ki papo unakitamani

Tia shemere Pumbaza mtu Enda nguu Poteza matumaini

Kaa kitwea Kaa bila kusema wala Kuwa na inda kama Wivu wa kuzuia wengine
kutenda jambo kutokana na joka la mdimu kutopata kitu usichokitumia
woga

Istiara/sitiari

ulinganisho wa moja kwa moja

mfano

i. Mwakio ni sungura(ana ujanja mwingi)

ii. Zainabu ni kinyonga(hana msimamo)

Tashhisi/uhuishi/uhaishaji- personification

Hii ni hali ya kukipa kitu kisicho uhai sifa za binadamu


Mfano
i. Upepo ulivuma kwa kasi ungedhani ulikuwa umechokozwa.
ii. Mlango ulimkodolea macho mgeni.
iii. Nilifuata amri ya moyo wangu.
iv. Mawimbi ya bahari yalinizungumzia.
Majazi

Upaji wa majina kulingana na tabia,hulka au sifa za mtu au mahali

i. Bw.Majivuno-mtu anayejidai

ii. Mtaa wa Huruma-kuliko na shida nyingi

Tasfida

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
Kutumia maneno ya adabu au fiche kuficha ukali wa maneno yanayokera watu.

Mfano

Tasfida/tauria Si adabu

Amejifungua/amejikopoa amezaa

Waliaga dunia Walikufa

Kutabawali/kubeua/haja kukojoa
ndogo

Kinaya/stihizai

Huonyesha hali iliyo kinyume na matarajio ya kawaida

Mfano

Tajiri alikufa kwa njaa

Chuku- exergeration

Kuongeza maneno yasiyo ya kweli; kutia chumvi.

Sifa ya kitu inakuzwa au kufifizwa kwa namna isiyokuwa ya kawaida.

Mfano

i. Ni mrefu sana ;maji ya bahari humfika magotini na anaweza kugusa kilele cha mlima Kilimanjaro kwa
mkono

ii. Hapumui anapozungumza ;anaweza kusema maneno mia moja kwa dakikka moja.

Ishara

Dalili,kitu kinachoelekeza kwenye jambo,hali au tukio

Kitu au jambo huashiria kitu kingine

Mfano

i. Giza ni ishara ya matatizo


Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
ii. Sauti ya bundi huwa ishara ya msiba;kisirani

iii. Jua kuchomoza vizuri na sauti za ndege wakiimba ni ishara kuwa siku itakuwa nzuri yenye mafanikio.

Ushairi

 Aina/bahari za mashairi

Hutegemea idadi ya mishororo katika kila ubeti.

Idadi ya mishororo katika kila Jina la shairi


ubeti

1. Mmoja Tathmina

2. Miwili Tathnia

3. Mitatu Tathlitha

4. Mine Tarbia

5. Mitano Takhimisa

6. Sita Tasdisa

 Ngonjera/malumbano – Shairi la majibizano


 Mizani – Silabi katika mshororo
 Vina – Mizani za mwisho zinazofanana
 Malenga – anayetunga mashairi
 Mghani – anayeimba mashairi
 Lakabu – Jina analojipatia mshairi lisilo jina lake kamili.
 Diwani-kitabu cha mashairi
 Vipande vya shairi

Ukwapi, utao, mwandamizi, ukingo

 Majina ya mishororo
1. Mshororo wa kwanza mwanzo
2. Mshororo wa pili mloto
3. Mshororo wa tatu mleo
Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
4. Mshororo wa nne kimalizio
 Mshororo wa mwisho unaorudiwarudiwa:
Kibwagizo/kiitikio/kipokeo/mkarara/pambio.

Nomino makundi/jamii

 Peto la/kipeto cha barua  Hadhira ya watazamaji/wasikilizaji


 Shumbi (heap) la/mshumbi wa wali  Msoa wa watalii au wasafiri
au udongo  Chane ya/mkungu wa ndizi
 Bumba la nyuki  Wingu la moshi au nzige
 Kitita cha pesa  Funda la maji
 Kicha cha sukumawiki,mboga au  Tonge la ugali
funguo  Safu ya milima au ghorofa
 Numbi ya/mtungo wa/kishazi cha  Korija ya vitu ishirini (20)
samaki  Jozi (pair) ya vitu viwili (2)
 Shada la/koja la maua  Baraza la wazee au mawaziri
 Genge la wezi/vibarua
Mahakamani/Kortini

 Kizimbani-asimamapo mshtakiwa  Kata rufaa-tuma maombi ya kutaka


mahakamani. kesi isikilizwe upya.

 Rumande-anapozuiliwa mshtakiwa  Kuungama-kukiri/kukubali


kesi inapokuwa ikiendelea. mashtaka.

 Dhamana-malipo atoayo mshtakiwa  Daawa-Kesi


aachiliwe kwa muda kesi
 Kula kalenda-kutumikia kifungo
inapoendelea.
jela/gerezani.

Watu na kazi zao

 Mjume - Hutia nakshi (urembo) kwenye vitu.


 Mjumu - Hufua visu.
Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
 Sonara - Hutengeneza mapambo kwa madini.
 Sogora - Bingwa wa kucheza ngoma.
 Saisi - Hutunza wanyama wa uchukuzi
k.v.punda,ngamia,farasi n.k.
 Mchuuzi - Huuza bidhaa rejareja yaani kitu kimoja kimoja.
 Mzegazega - Huuza maji kwa mkokoteni au rukwama.
 Dalali/mnadi - Huuza bidhaa mnadani kwa kutangaza bei.
 Mkalimani - Hutafsiri lugha moja kwa moja.

Vifaa vya ufundi

 Mizani - hupimia Uzito.


 Utepe - hupiamia Urefu.
 Fuawe - Mhunzi huwekelea chuma anachofua.
 Patasi - Hutoboa mashimo kwenye mbao.
 Timazi - hukadiria Usawa wa ukuta.
 Pimamaji - hutumiwa kupimia unyookaji wa kitu
 Msasa - hutumiwa na maseremala kulainishia mbao
 Jiriwa - kushikilia imara chuma au mbao ifanyiwapo kazi
 Bisbisi - kufungia na kufungulia parafujo
 Keekee - hutumiwa kutobolea mashimo kwenye mbao.

Nyakati za siku

 Machweo/magharibi - wakati wa jua kutua


 Usiku wa manane – kati ya sita na saa tisa usiku
 Majogoo – majira baina ya saa tisa na saa kumi na moja alfajiri
 Alfajiri/liamba - majira ya kuanzia saa kumi na moja hadi jua
linapochomaza.
 Macheo/mawio/mapambazuko - wakati wa jua kuchomoza
 Jua la mtikati – saa sita kamili mchana
 Adhuhuri - wakati baina ya saa sita na saa tisa mchana.
 Alasiri - wakati kati ya tisa mchana na jua kuzama.

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
 Kasorobo - enye upungufu wa robo ; imebakisha dakika kumi na
tano.
 Mfano: saa nane kasorobo ni sawa na saa saba na
dakika arubaini na tano

Malipo

 Riba - Ya ziada kwa mkopo.  Dhamana - hutolewa na


 Ada -Ya daktari. mshtakiwa aachiliwe kwa

 Ridhaa -Kumharibia mtu jina. muda;asiwekwe rumande kesi

 Arbuni -Sehemu ya bei ya kitu inapoendelea.

inayotolewa mwanzoni.  Mtaji -fedha za kuanzisha

 Fidia - Kwa ajili ya hasara. biashara.

 Karadha - mkopo bila riba.

Michezo
 Mpira wa pete-netbali  Kwata-mazoezi ya kuvinyoosha
 Mpira wa magongo-hoki viungo vya mwili

 jugwe-kushindana kwa kuvuta  Kibafute-kubahatisha idadi ya


kamba vitu vilivyofumbatwa mkononi

 Miereka-kushikana na  Kibemasa-kujificha na kutafutana


kuangushana  Gungwi-watoto kurukaruka kwa
mguu mmoja.

ukoo

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria 0727064403
 Mkaza - Mke wa mtu;mkazamjomba-mke wa mjomba.
 Umbu - wanavyoitana kaka na dada.
 Mnuna -(younger sibling )– ndugu mdogo.
 Mkwe/mcheja - Mzazi wa mke wa mtu.
 Mkoi/binamu - Mtoto wa ami, shangazi, mjomba au hale.
 Mpwa - Mtoto wa umbu; wa kaka au dada yako.
 Mwanyumba - Wanavyoitana wanaume waliooa madada.
 Mwamu/mlamu - Kaka wa mke au mtu.
 Kivyere - Waitanavyo wazazi wa mke au wa mume.
 Wifi - Wanavyoitana mke na dada wa mume wake.

Vikembe 8.Simba...Shibli
9.Sungura..Kitungule
1.Bata-kiyoyo. 10.Nyuki..jana
2.Chui.Kisui. 11.Nyati..ndama
3.Chura..kiluwiluwi 12Ndege...kinda
4.Farasi...mwanafarasi 13Mbwa.kidue,kilebu
5.Kondoo...Katama, mwanakondoo 14.Papa..kinegwe
6.Mbuzi.kimeme,mwanambuzi 15.Kipepeo.kiwavi
7.Punda..kihongwe 16.Fisi .....bakaya

Sheria muhimu za Kiswahili

1. Kitenzi kilichokanushwa/si ........ tu….. bali pia


Mfano
 Raia wenye afya hawamudu tu kukabiliana na changamoto bali pia huwa na hamu
ya kutenda kazi.
 Gitonga si mwalimu tu bali pia ni msanii maarufu.

2. Namna…..
Vile……….
Jinsi……… hufuatwa na‘–vyo-‘
Kadri…….
Mfano

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria


0727064403
 Kadri alivyozidi kukimbia ndivyo adui alivyozidi kumfikia.
 Tueleze jinsi mlivyomudu kuwa namba moja.

3. Ni makosa kutumia kirejeshi ‘amba-‘ pamoja na ‘o’ rejeshi katika sentensi moja.
Mfano
Mbwa ambaye anayebweka ni hatari. (kosa)
Mbwa ambaye anabweka ni hatari. (sahihi)
Mbwa anayebweka ni hatari. (sahihi)

4. Ni makosa kwa kivumishi cha pekee ‘-enye’ kufuatwa na kitenzi.


Mfano
Mgeni mwenyeanakuja ni mzuri. (kosa)
Mgeni ambaye anakuja ni nzuri. (sahihi)

5. Hali tegemezi ‘-nge-‘ na ‘-ngali’-


 Ni makosa kuzitumia nge na ngali katika sentensi moja.
 Hazikanushwi kwa ‘ha-‘ au ‘hu’. Hukanushwa kwa ‘si’
 Unapokanusha, hakikisha kwamba umeweka kiambishi cha nafsi ya mtendaji.
Mfano
Ningefika mapema ungenipata
 Singefika mapema hungenipata. (kosa)
 Nisingefika mapema usingenipata. (sahihi)

6. ‘-ni’ ya mahali itumikapo, vihusishi vifuatavyo havitumiki: ndani ya, katika, kwenye,
penye na mwenye.
Mfano
 Tunaenda kwenye darasani. (kosa)
 Tunaenda darasani. (sahihi)
 Tunaenda kwenye darasa. (sahihi)
7. Ni makosa ‘-enye-‘ kufuatwa na kitenzi

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria


0727064403
 ‘-enye-‘ ni kivumishi cha pekee ambacho huonyesha umilikaji.
 ‘-enye-‘ hufuatwa na jina (nomino)
Kosa Sahihi
(a) Mtu mwenye anaenda. Mtu ambaye anaenda.
Mtu anayeenda.
(b) Sijui vyenye anataka. Sijui vile anavyotaka.
Sijui kile anachotaka.
(c) Aliniambia vyenye Aliniambia vile/jinsi/namna
walienda. walivyoenda.

Kiswahili si kigumu; ni kitamu. Kuwa na MTAZAMO CHANYA. Mwalimu Mwinyi P. Kuria


0727064403

You might also like