You are on page 1of 2

NAHAU ZA KISWAHILI NA MAANA ZAKE PAMOJA NA MASWALI YA KITAIFA YA KCPE

1. Mafungulia ng’ombe -Saa mbili hadi saa tatu asubuhi.


2. Kutia kiraka- Fichia siri.
3. Kumlainisha mtu – kumzungumzia mtu maneno.
4. Kutia utambi -kuchochea
5. Kumeza maneno moyoni – kuficha siri
6. Kula njama – kufanya mkutano wa siri
7. Kazi ya majungu – kazi ya kumpa mtu posho.
8. Kumwonyesha mgongo – kujificha.
9. Kuona cha mtema kuni – kupata mateso/ tabu/shida/ kujuta.
10. Maneno ya uani – maneno ya porojo/upwaji;yasiyo na maana
11. Mkubwa jalala – kila lawams hupitia kwa mkubwa.
12. Mkaa jikono – mvivi wa kutembea.
13. Paka mafuta kwa mgongo wa chupa – danganya
14. Mtu mwenye ndimi mbili – kigeugeu
15. Kupiga supu – tegea.
16. Kupiga mali shoka – gawana;fuja mali
17. Kula chumvi nyingi – ishi miaka mingi.
18. Kuwa popo – kuwa kigeugeu
19. Vaa miwani/chapa maji – lewa pombe[chakari]
20. Kuchungulia kaburi – mahututi /gharighari ya kifo
21. Fimbo zimemwota mgongoni – ana alama ya fimbo mgongoni.
22. Hamadi kibindoni – akiba iliyopo kibindoni.
23. Hawapikiki chungu kimoja / hawakai zizi moja – hawapatani
24. Kupika majungu – kufanya mkutano wa siri
25. Vika kilemba cha ukoka – kumpa mtu sifa asizostahili.
26. Kujipalia makaa – kujitia matatani/shidani
27. Mwaga unga – fukuzwa kazini.
28. Ongezewa unga – pandishwa cheo.
29. Uma mtu sio – kumnong’ononezea mtu jambo la siri.
30. Chimba mtu – kumpeleleza mtu siri zake.
31. Kutia chumvi – kuongeza Habari za uongo.
32. Kula vumbi/mumbi/mwata – pata tabu
33. Kodoa macho – tazama sana kutokana na mshangao.
34. Kutoka shoti – kimbia kwa kasi sana.
35. Kushtaki njaa – kula.
36. Kutiwa mbaroni/kutiwa nguvuni – kushikwa au kukamatwa has ana polisi.
37. Kuweka nadhiri- kutoa ahadi
38. Fua dafu – faulu.
39. Lilia ngoa – onea wivu kutokana na hali Fulani nzuri.
40. Kupiga chafya – kuchemua.
41. Pigwa kalamu – achishwa kazi.
42. Zunguka mbuyu/kula rushwa/ piga mtu konde la nyuma – honga
43. Kanyaga chechele – potea njia.
44. Chukuliwa na chechele – sahau.
45. Chimba mikwara – fanyia mtu vitisho.
46. Ponda mali – fuja mali/tumia mali vibaya.
47. Pangu pakavu tia mchuzi – maskini.
48. Kula kalenda – fungwa gerezani.
49. Kula Ndonga – tumia afyuni/tumia mihadarati.
50. Vimba kichwa -kuwa kaidi.
51. Kula Yamini – apa
52. Kula mwande – kosa ulilolitarajia.
53. Pata jiko- oa
54. Pata nyumba -olewa.
55. Ona kizunguzungu-ona kisunzi.
56. Ona riahi/ ona kichefuchefu/ kitefutefu/kekefu – hisi kutapika.
57. Ramba kisogo – sengenya.
58. Kupiga vijembe -sema mtu kwa mafumbo.
59. Kula vya mwiku – kula uporo/kula chakula kilichobaki.
60. Kushika sikio-kukanya.
61. Enda nguu – kata taa,angema
62. Tia mrija – tegea mtu kwa kila jambo.
63. Joka la mdimu – wivu/inda
64. Jicho la nje – kutokuwa mwaminifu katika ndoa.
65. Bwaga zani- zua fujo/rabsha
66. Vuliwa mbeleko/mbeko – shushwa cheo / madaraka
67. Valisha mbeleko / mbeko – pewa madaraka.
MASWALI YA NAHAU KATIKA MTIHANI WA KITAIFA WA KCPE NA MWAKA WA UTAHINI.
1. KCPE 2017 Swali la 26
2. KCPE 2011 Swali la 22
3. KCPE 2008 Swali la 25
4. KCPE 2003 Swali 17
5. KCPE 2002 Swali 17
Makala haya yametayarishwa na George Mitigoa almaarufu Aso DOA Wala TOA

You might also like