You are on page 1of 13

1 More Next Blog Create Blog Sign In

ChuoKenya
Your Gateway to World of Education

Home

VITENDAWILI

Mfano kitendawili, utegapo mtegaji

Jibule huwa twawili, wawatatiza majaji

Likawateka akili, waume walo magwiji

Mwisho hutolewa mji, mfumbi kutoshindika

(Boukheit Amana)

Kitendawili ni swali la kiistiari ambapo sehemu moja ya ulingannishi uliopo

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
inadokezwa tu ilhali ya pili inabakia ya kukisiwa. Kama sanaa, vitendawili
hutegemea uwezo alionao mtu kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu
vya aina tofauti katika mazingira yake. Hii ni sanaa inayotendwa
(performative) na inayosimama kivyake tofauti na sanaa tegemezi au elekezi
(illustrarive) kama methali.
Kitendawili ni kauli inayotenda mawili au inayotendwa na wawili. Ni mchezo
wa kuficha maana. Ni utandu wa maneno ambamo dhana husimuliwa
kijazanda ili mtu mwingine angamue. Vitendawili hulenga maisha ya jamii
na shughuli wafanyazo. Vitendawili vingi hushughulikia mambo tofauti
yanayomhusu binadamu kama kifo, uhai, chakula, maisha na mazingira.

Asili ya Vitendawili
Vitendawili vina asili mbalimbali
(a) Mahitaji ya Kisanaa Followers

Kila mtu ana hisia za kisaa ambazo zimefungamana na mazingira. Hisia hizi
Join this site
humfanya mtu kutumia sifa za uumbaji kuyaeleza mazingira hayo. Kwa njia w ith Google Friend Connect
hii mtu huweza kujitosheleza kihisia atoapo kitendawili.
Members (5)
(b) Mahitaji ya Matumizi
Mtu aliona hoja ya kumwelimisha mwenziwe. Lakini njia ya kumwelimisha
haikupatikana. Kwa hivyo aliamua kutumia mazingira yake ya sanaa kuitoa
elimu hiyo. Hii ndiyo maana vitendawili vingi hueleza mazingira ambayo ni
ya kabla ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Already a member? Sign in
(c) Mahitaji ya Kueleza Mazingira na Maendeleo
Mahitaji ya kueleza mazingira na maendeleo ya kisayansi nyakati hizo za
zamani kabla ya uvumbuzi na maelezo ya kutosheleza kuwepo. Kwa kuwa Blog Archive
mtu alijikuta katika mazingira, ilimbidi atoe maelezo kuhusu mazingira yake.
2010 (1)
Kwa sababu hii, binadamu alieleza mazingira kwa kutunga visasili vya
kuhalalisha kuwepo kwa vitu fulani katika mazingira yake. Kwa mfano 2012 (1)
kitendawili Uzi mwembamba umefunga dume kubwa usingizi 2013 (1)
(d) Misemo ya Kimtaa November (1)
Misemo ya kimtaa itumiwayo na watu wengi katika sehemu fulani. Matumizi Nov 05 (1)
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
ya misemo hii yanapoendelea kupannuka na kupata hadhira kubwa, misemo VITENDAWILI
hiyo hushika kani na kugeuka kuwa vitendawili.
2015 (4)
Sifa
Vitendawili hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine kwa sababu
About Me
vitendawili ni zao la utamaduni wa jamii. Licha ya tofauti hizi, vitendawili
huwa na sifa zifuatazo ambazo huonekana katika jamii zote: Kibe Paul
(a) Kuwepo kwa kitangulizi kwa mfano Kitendawili Tega katika jamii ya Software
Waswahili developer and
(b) Matumizi ya lugha ya kiistiari ambapo kitu hulinganishwa na kingine web designer.
(c) Matumizi ya lugha ya mkato, bila maelezo marefu isipokuwa tu katika View my complete profile
vitendawili visimulizi
(d) Aghalabu huwa na jibu moja. Hata hivyo vipo vitendawili vichache vya
majibu mengi
(e) Kufungamana na mazingira ya jamii husika kwa kutaja, kuirejelea na
kujifunga kwenye mazingira hayo
(f) Kuwepo kwa utaratibu wa kutegua kitendawili chenyewe hasa hadhira
inaposhindwa kupata jibu
(g) Kuwepo kwa pande mbili za wahusika mtegaji na mteguaji
(h) Maana kueleweka tu katika jamii husika
(i) Kuchura taswira kamili ya kinachorejelewa
(j) Hadhira kupewa muda kufikiri
(k) Kutumia tamathali mbalimbali za lugha

Muundo wa Vitendawili
Muundo ni jumla ya uhusiano unaokuwako kati ya vijisehemu mbalimbali
vinavyotengeneza kitu kamili. Katika muktadha wa vitendawili, muundo ni
utaratibu unaofuatwa wakati wa kutega na kutegua kitendawili.
(i) Kiingizi
Pia huitwa kitangulizi. Hapa mtambaji hutanguliza kwa swali Kitendawili.
Kifungu hiki hutumiwa kila mara kiasi cha kuwa kama ruwaza fulani.
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Kitangulizi hiki huwa na umuhimu ufuatao:
(a) Kuhanikiza hali ipasayo
(b) Kutangaza majilio ya kitendawili
(c) Kukatiza yaliyokuwa yakiendelea ili kuwatazamisha hadhira kwenye
kitendawili
(d) Kuifanya hadhira kuzingatia kitendawili husika
(e) Kubainisha mtegaji kwa kumtenga na hadhira
Ifuatayo ni mifani ya viingizi kutoka jamii mbalimbali

Kitangulizi Kikaribisho Jamii


Kitendawili Tega Waswahili
Kinawia Njo Kipare
Namunayi/ Kuupa/ Kwitse Lumasaaba
Munayi (Uganda)
Kwata ndai Nakwata Kamba
Hamne/ Mnaye Kwithe Luo
Gwata nda Ndagwata Kikuyu
Tangoch Choo Nandi
Rhipo Himbiriki Pokomo
Oyiote Euo Maasai
Wata Nawada Taita
Getandagwiri Tega Abagusii
Chirondoni Tseka Duruma
Tangalie Ega Digo
Gwata ntai Ndagwata Meru
Tukio Ember Abasuba
(ii) Kikaribisho
Hili ni jibu kutoka kwa hadhira lionyeshalo kukubali kwao kutegewa
kitendawili
(iii) Mwili

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Hapa kitendawili chenyewe hutegwa
(iv) Muda wa kufikiri
Hadhira hupewa muda kufikiri na kujaribu kutafuta jibu la kitendawili
(v) Kichocheo
Hadhira ikishindwa, tuzo au mji hutolewa kwa mtegaji ili awapatia jibu.
Waswahili hutoa mji, Waluo hutoa msichana
(vi) Jibu
Jibu hutolewa na mtegaji baada ya kukubali tuzo aliyopewa

Kutegua Vitendawili
Maana na majibu ya vitendawili hutegemea mazingira ya jamii husika.
Tupatapo kitendawili kuna uwezekano wa majibu matatu Kitendawili ni
tatizo la kutatuliwa, jibu la sehemu ya kitendawili na na kichocheo baada ya
hadhira kushindwa ni sehemu ya kitendawili. Hatua na mambo ya kuzingatia
tunapotegua vitendawili ni:
(a) Kuelewa kipindi cha wakati kinacholengwa na kitendawili. Kwa mfano
kitendawili Baba ana mguu mmoja tu chaweza kuwa na majibu kama Uyoga
(jadi) au mwavuli (sasa)
(b) Kufahamu mazingira ambamo kitendawili kilitungiwa ili kupata picha
kamili ya kitendawili. Kwa mfano kitendawili Mwarabu wangui nimemtuoa
biwini kitaeleweka ikiwa mtu ataelewa mazingira ya pwani ambapo jibu ni
machicha ya nazi
(c) Kuchunguza maana ya maneno. Kitendawili nyumba ya bibi imejaa
wapangaji chatubidi kuelewa kuwa wapangaji si watu wa kudumu. Basi
maana tupatayo ni kuwa bibi ana chombo anamoweka vitu vya matumizi
yake ambavyo havidumu. Jibu ni vijiti vya kiberiti
(d) Kuchunguza jinsi linalozungumziwa linafungamana na tabia, picha au
umbo la kitu. Kitendawili kipo lakini hukioni lina mpangilio wa maneno
unaoonyesha kuwa pengine jibu litaanza na kiambishi ki-. Jibu ni kisogo

Umuhimu wa Vitendawili
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
(a) Kutumbuza, kupumbaza na kuburudisha watoto hasa wakati wa jioni
(b) Kuhifadhi historian a utamaduni wa jamii
(c) Kama njia ya kuanzia, kukatizia au kumalizia usimulizi
(d) Huwa msingi wa kuyachambua maisha ya jamii
(e) Kuonyesha hisia za wanajamii kuhusu mtu au kitu fulani
(f) Kuelimisha kuhusu mazingira, imani, amali, mawazi na historia
(g) Kuchochea kufikiria kwa wanajamii kwa njia ya kupevusha kukabiliana
na maisha yao
(h) Kukuza lugha kwa kuchangia katika kuiongezea msamiati
(i) Kudhihaki na kukejeli sifa na tabia zisizofaa
(j) Kukuza uwezo wa kukumbuka mambo muhimu na kujamii na kielimu
(k) Kuchochea udadisi na hamu ya kutaka kujua zaidi pamoja na utafiti
(l) Kukuza uhidari wa kusikiliza na wepesi wa kujibu maswali hivyo
kuwatayarisha kukabili changamoto nyingi
(m) Kutajirisha na kupamba mazungumzo
(n) Kujenga ari ya kushindana hivyo kujenga uhusiano mwema kati ya
wahusika (mtegaji na mteguaji)
(o) Huwa hatua ya mwanzo ya ushairi

Aina za Vitendawili
(a) Vitendawili sahili
Huwa na muundo rahisi wa maneno machache, aghalabu sentensi fupi hata
neno moja. Huwasilishwa kama kauli wazi kuliko swali. Huwa na wazo
moja. Mara nyingi hutegewa watoto.
Mifano ya vitendawili sahili ni pamoja na:
(i) Afuma hana mshale nungunungu
(ii) Akikosekana maana imekosekana kamusi
(iii) Akiona mwangaza wa jua hufa samaki
(iv) Babu kasimama kwa mguu mmoja uyoga / mwavuli
(v) Chauma bila meno, chaumiza bila ya silaha moto
(vi) Dege kuu linainamia wanawe nyumba
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
(vii) Fimbo yangu ndefu haina shina wala ncha ulimwengu
(viii) Hata kama wataka kukitafuna hukiwezi, ni hafifu maji
(ix) Hufa ukafufuka bahari
(x) Nyumba yangu haina mlango yai
(b) Vitendawili Tata/ Changamano
Huwa kama fumbo refu. Huwa na wazo zaidi ya moja. Huhitaji kufikiri
kwingi ili kupata jibu. Huwasilishwa kwa msamiati teule na maswali
yaliyopangwa vilivyo.
Mifano ya vitendawili changamano ni pamoja na:
(i) Ana vichwa vitatu, miguu minane, masikio sita na mkia watu wawili
mgongoni mwa farasi
(ii) Mwenye miguu minne juu ya mguu minne akimsubiri mwenye miguu
minne paka juu ya meza akimngoja panya
(c) Vitendawili Mkufu
Ni vitendawili ambavyo sehemu ya kwanza inahusiana moja kwa moja na
sehemu ya pili kimuundo. Sehemu hizi mbili hujalizana na kuchangiziana.
Mifano ya vitendawili mkufu ni pamoja na:
(i) Nikitembea yuki, nikikimbia yuko, lakini nikiingia nyumbani hupotea
kivuli
(ii) Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna kioo
(iii) Nikienda pole huenda pole, nikikimbia hukimbia, nikiketi huketi
kivuli
(iv) Aliyekiona hakukikimbilia, aliyekikimbilia hakukiokata, aliyekiokota
hakukila, aliyekila hakushiba lakini aliyeshiba hakufanya kazi yoyote
tumbo la binadamu na viungo vya mwili
(v) Aliyenunua hakutumia, aliyetumia hakuiona sanda
(vi) Aliyechuma hakula, aliyekula hakumeza, aliyemeza hakushiba
mkono, kinywa na koo
(vii) Ukimwona Halima utasema ni Fatuma; ukimwona Fatuma utasema
ni Halima tui na maziwa
(viii) Ukiona njigi utadhani ni njege, ukiona njege utadhani ni njigi
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
maziwa na tui la nazi
(ix) Teketeke huzaa gumugumu na gumugumu huzaa teketeke mahindi
ama yai
(d) Vitendawili visimulizi
Ni vitendawili vinavyosimulia hadithi kama msingi wa kitendawili chenyewe
Mifano ya vitendawili visimulizi ni pamoja na:
(i) Kulikuwa na wasichana wawili waliokuwa wamesimama upande
mmoja wa mto. Ngambo ya pili alikuwako baba yao na maembe mawili.
Daraja lililokuwako mtoni lingemtoshea mwanamume mmoja na embe
moja. Lakini lazima avuke mto huo na maembe yote mawili mara moja kwa
ajili yao. Angefanya nini? apande darajani na kuvuka akirusha maembe
yake kwa zamu hadi avuke
(ii) Mtu alikuwa anakimbizwa na simba, akapanda juu ya mti. Juu
kulikuwa na mzinga wa nyuki. Chini samba alimngoja. Mti huo ulikuwa
karibu na mto. Ndani ya mto kuna mamba. Mtu huyu alikuwa na panga
mkononi. Je, atajiokoa vipi? atakata tawi la mti alitupe mtoni. Mamba
atalikimbilia akidhani ni mtu Y ule. Kisha mtu yule ataogelea majini avuke na
kuenda zake salama
(iii) Nimeona mti wa ajabu; una mashina mawili na kila shina moja lina
mizizi mitani; una matawi mawili na kila tawi lina majani matano mtu
(e) Vitendawili vya Tanakali
Huundwa kwa sauti za miigo fulani. Mifano ya vitendawili hivi ni pamoja na:
(i) Chubluu! Jiwe liangukapo mchangani
(ii) Diii! Halina mshindo Difu au ndifu
(iii) Drrrr! Hadi ngambo Utandabui
(iv) Huku unasikia pa! Huku unasikia pa! Mkia wa kondoo atembeapo
(v) Mti pakapaka! Mti haa! - zumari
(vi) Prrrrr! Hadi Makka Utelezi
(vii) Tse! Sindano mchangani (Kikamba)

Fani Katika Vitendawili


open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Lugha ya vitendawili huwa ya kitamathali. Baadhi ya tamathali katika
vitendawili ni pamoja na:
(a) Tashhisi
Vitu hupewa sifa za uhai kama wa binadamu. mifano ya vitendawili vya
kitashhisi ni pamoja na:
(i) Askari wamekaa na mfalme yuko katikati moto (mafiga
yanalinganishwa na askari ambaye ni kiumbe hai)
(ii) Hana wema wowote sumu
(iii) Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti mvua
(iv) Hamwogopi mtu yeyote njaa
(v) Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi giza
(vi) Dadangu ana jicho moja sindano
(vii) Ngombe wangu nisipomshika mkia hali myasi uma, jembe au
kijiko
(b) Kwelikinzani
Kauli inayosemwainaonyesha ukinzani fulani kijuujuu lakini undani wake
huwa hauna ukinzani huo. Pia huitwa ukinzani. Mifano ya vitendawili vya
ukinzani ni:
(i) Aenda mbio lakini hana miguu nyoka (tunatarajia anayeenda awe
na miguu)
(ii) Ana meno mengi lakini hayaumi shanuo au kitana (tunatarajia
meno yaweze kuuma)
(iii) Ajenga ingawa hana mikono ndege (awezaye kujenga tunatarajia
awe na mikono)
(iv) Mwanamke hana mume lakini huzaa watoto wengi mgomba wa
ndizi (asiye na mume kawaida hazai)
(v) Nala lakini sishibi mate
(c) Takriri
Ni urudiaji wa maneno, sauti au vifungu fulani. Ifuatayo ni mifano ya
vitendawili vinavyojumuisha takriri.
(i) Huona hapa, huko, huku na kule kinyonga
open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
(ii) Bak bandika bak banduka nyayo (za mtu atembeapo)
(iii) Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna kioo
(iv) Amezaliwa Ali, amekufa Ali amerudi Ali nywele
(v) Aliwa, yuala, ala aliwa papa
(vi) Ganda mgando ulimbo
(vii) Mti mnyama, mti kerekeche, mti ali, mti ali! ngoma na upatu
(viii) Mahepe mahepe magendo
(d) Sitiari
Kitu kimoja hulinganishwa na kingine bila ya kutumia viungio. Ifuatayo vi
mifano ya vitendawili vya kistiari.
(i) Popoo mbili zavuka mto macho (macho kulinganishwa na popoo)
(ii) Gari la kila mtu miguu (miguu kufananishwa na gari)
(iii) Embe langu la duara haliliki mpaka lipikwe boga (embe
linalinganishwa na boga)
(iv) Mhuni wa ulimwengu nzi (kumfananisha nzi na mhuni

Posted by Kibe Paul at 1 0:25 PM


+1 Recommend this on Google

1 comment:

Seiff Kibwana May 28, 2015 at 5:57 AM


mnashukuriwa kwa jitihada hii nzuri ya kukuza fasihi ya kiswahili.
Reply

Enter your comment...

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Comment as: Select profile...

Publish Preview

Newer Post Home Older Post

Subscribe to: Post Comments (Atom)

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Loa din g ...

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com
Simple template. Template images by luoman. Powered by Blogger.

open in browser PRO version Are you a developer? Try out the HTML to PDF API pdfcrowd.com

You might also like