You are on page 1of 4

Mada ya Kwanza: Mbinu za Ufundishaji na Ujifunzaji wa Lugha ya Pili

Muhtasari wa Mada
Mada hii inatalii kwa muhtasari uga wa mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa lugha ya pili.
Inaelezwa bayana kuwa katika karne ya 20, tafiti katika eneo hili zilijikita katika kutafuta mbinu
moja iliyo muafaka kuliko nyngine zote na hivyo kuweza kutumiwa katika mazingira yote.
Aidha, mwelekeo huu unaonekana kubadilika katika zama hizi za karne ya 21. Leo tafiti katika
eneo hili hazijikiti katika kutafuta mbinu moja muafaka. Imebainika kuwa mazingira ya
ufundishaji yanatofautiana na hivyo mwalimu sana anapewa nafasi ya kutumia mbinu anayoiona
uafaka kulingana na mahitaji yaliyopo darasani kwake na katika mazingira yake. Kwa muhtasari,
tunaelezwa juu ya mbinu mbalimbali zilizojitokeza huku baadhi zikiwa maarufu na kukubaliwa
zaidi huku nyingine zikishindwa kuwa na ukubalifu katika eneo pana. Mwisho, mada hii
inajikita katika kufafanua sababu za watafiti kuachana na jitihada za kutafuta mbinu moja
muafaka ya ufundishaji na ujifunzaji wa lugha.

Malengo ya Ujifunzaji
Kufikia mwishoni mwa mada hii, wanafunzi wataweza:
 Kueleza mambo ya msingi yanayoshughulikiwa katika uga wa mbinu za ufundishaji wa
lugha;
 Kulinganisha tafiti kuhusu mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa lugha za kipindi cha
kabla ya karne ya 21 na zile za kipindi cha karne 21;
 Kujadili sababu za kujikita kutafuta mbinu moja muafaka ya ufundishaji na ujifunzaji;
 Kujadili sababu za kuachana na mwelekeo wa kutafuta kuwa na mbinu moja muafaka.

NOTISI ZA MADA YA KWANZA


Kwa muda mrefu hususani karne yote ya 20, tafiti kuhusu mbinu za ufundishaji na ujifunzaji wa

lugha ziliegemea katika kutafuta mbinu moja muafaka ya ufundishaji na ujifunzaji wa lugha. Hii

ilisababisha mbinu iliyotangulia kutenguliwa na mbinu iliyofuatia. Hivyo kwa kila mbinu

iliyokuwepo ilikuwa na chukulizi kuwa yenyewe ni mbinu bora zaidi na iliyoegemezwa katika

nadharia kuhusu lugha na zile kuhusu ujifunzaji zinazotazamwa kuwa bora zaidi. Hivyo basi,

1
katika karne hii ya 20, kulikuwa na mabadiliko na uvumbuzi wa mara kwa mara. Hii ilichangia

mikabala ya ufundishaji na ujifunzaji wa lugha kuibuka kwa kuchochewa na mabadiliko

yaliyojitokeza katika mbinu za ufundishaji. Hii ni sawa na kusema kuwa badala ya mkabala

kuongoza ujitokezaji wa mbinu za ufundishaji wa lugha, mbinu ndizo zilizoongoza kuibuka kwa

mikabala (Richard & Rodgers, 2001; Richard, C. J. & Renandya, 2002).

Historia yote ya ufundishaji wa lugha imetawaliwa na utafutaji wa njia muafaka zaidi ya

ufundishaji wa lugha ya pili au kigeni. Kwa zaidi ya miaka mia moja, midahalo na mijadala

katika taaluma ya ufundishaji imejikita katika masuala kama vile nafasi ya sarufi katika mtaala

wa lugha, ukuzaji wa usahihi na ufasaha katika ufundishaji, uchaguzi wa mwego wa silabasi

katika uundaji wa kozi, nafasi ya msamiati katika ujifunzaji wa lugha, ufundishaji wa stadi za

kiuzalishaji na kiupokezi, nadharia za ujifunzaji na matumizi yake katika ufundishaji, kukariri na

ujifunzaji, umotishaji wa mwanafunzi, mikakati muafaka ya ujifunzaji, tekiniki za ufundishaji wa

stadi nne za lugha, nafasi ya zana za ufundishaji na teknolojia. Licha jitihada kubwa kufanyika

kuhusiana na haya yote, bado jitihada zinazendelea ili kuboresha zaidi (Richard & Rodgers,

2001; Richard, C. J. & Renandya, 2002).

Hivyo basi, mabadiliko katika mbinu za ufundishaji wa lugha katika kipindi chote cha historia

yameakisi utambuzi wa mabadiliko katika aina ya ustadi unaohitajiwa na wanafunzi, kama vile

hatua kuelekea katika ustadi wa mazungumzo badala ya usomaji wa ufahamu kama malengo ya

ujifunzaji wa lugha. Aidha, yameakisi pia mabadiliko ya nadharia kuhusu namna lugha ilivyo na

zile za ujifunzaji wa lugha.

Ufundishaji wa maada (neno hili ni tofauti na mada) yeyote ya somo mara nyingi huegemezwa

katika uchambuzi wa namna somo lenyewe lilivyo na matumizi ya kanuni za ufundishaji na

ujifunzaji zinazopatikana kutoka katika tafiti na nadharia zilipo katika saikolojia ya elimu.

2
Matokeo yanayopatikana hapa ndiyo ambayo kwa ujumla hurejelewa kama mbinu ya

ufundishaji au mkabala. Kwa pamoja hurejelewa kama seti kuu za kanuni za ufundishaji na

ujifunzaji zikiwa kwa pamoja na utendaji mbalimbali wa darasani unaotokana na kanuni hizo.

Hali ipo hivihivi hata katika ufundishaji wa lugha. Uga wa ufundishaji umekuwa hai sana katika

ufundishaji wa lugha toka miaka ya 1900. Mbinu na mikabala mipya imeshamiri sana katika

kipindi chote cha karne ya 20. Baadhi yake ilifanikiwa kupata kiwango cha juu cha umaarufu na

kukubalika katika vipindi fulani vya wakati na baadaye kutenguliwa na mbinu nyingine

zilizojiegemeza katika mawazo au nadharia mpya. Mifano ya mbinu hizi ni pamoja na Mbinu ya

Moja kwa Moja, Mbinu ya Sauti-Lugha, na Mkabala wa Kihali (Richard & Rodgers, 2001).

Baadhi ya mbinu kama vile Mbinu ya Ufundishaji Lugha Kimawasiliano ilikubalika duniani

pote. Ilifikia hata hadhi ya kuwa ndiyo mbinu inayoaminika kukubalika. Wakati huohuo, kuna

mbinu zilizjitokeza kama mdadala mbinu zilizokuwa zikikubalika zaidi, mbinu hizi zilipta kiasi

fulani cha uungwaji mkono katika uga wa ufundisha wa lugha. Pamoja na hayo, mbinu hizi

hazikufanikiwa kuwa na matumizi kwa kiwango kikubwa. Miongoni mwa mbinu hizi ni pamoja

na mbinu zilizojitokeza katika miaka ya 1970 kama vile Mbinu ya Ukimya, Ujifunzaji - Nasaha,

Sajestopedia, Mwitikio Kamili wa Kimwili, ikiwa ni pamoja na mbinu na mikabala mdala ya

hivi karibuni (Richard & Rodgers, 2001).

Tumeona kuwa karne yote ya 20, wataalamu waliweka jitihada kubwa kutafuta mbinu moja ya

ufundishaji itakayokuwa muafaka kuliko mbinu nyingine zote. Kufikia katikati ya miaka ya

1980, wataalamu walianza kubaini kuwa utafutaji wa mbinu moja tu hauna mashiko na ni

upotezaji tu wa muda (Stern 1985 kama anavyorejelewa na Brown (2002).

Brown anatabahisha kwa nini leo hii upataji wa mbinu moja muafaka ya ufundishaji sio malengo

tena muhimu katika safari ya ufundishaji wa lugha:

3
 Mbinu zinanekana kuwa ni zenye maelekezo sana huku zikiwa na chukulizi zilizozidi

kiasi kuhusu muktadha kabla hata muktadha wenywe haujabainishwa;

 Kwa ujumla, mbinu zinaonekana kuwa na upekee hususani mapema mwanzoni mwa

hatua za kozi ya lugha na tena huonekana kutokutofautiana na nyingine katika hatua za

mbele za kozi ya lugha;

 Mara ya kwanza ilifikiriwa kuwa mbinu za ufundishaji wa lugha zinaweza kupimwa kwa

kutumia mbinu zile za kisayansi za kijarabati;

 Imedhihirika na kudhihirishwa kuwa mbinu za ufundishaji wa lugha za kigeni huasisiwa

na wale wenye nguvu. Hivyo zimekuja kutazamwa kama nyenzo za ubeberu wa kiisimu.

David Nanun (1991) kama anavyorejelewa na Brown (2002) anaeleza kwa nini hakuna tena haja

ya kujiegemeza katika utafutaji wa mbinu moja tu ya ufundishaji itakayokuwa muafaka kuliko

zote, anasema: “Sasa imedhihirika kwamba hakujawahi kuwa na huenda hakutakuja kutokea

kuwa na mbinu moja ya ufundishaji kwa wote.” Nunan (khj) anaendelea kutanabahisha kuwa

katika miaka ya hivi karibuni mkazo umekuwa katika utengenezaji wa kazi za darasani ambazo

zinaendana na kile tunachokijua kuhusiana na upataji wa lugha ya pili na zinazochukuana na

mabadiliko ya darasa lenyewe.

Hivyo basi, inapaswa kufahamika vema kuwa sisi kama walimu tuliopata mwanga, tunaweza

kufikiria uwezekano wa mbinu mbalimbali ambazo tunaweza kuzitumia kutokana na mikatadha

mbalimbali tutakayokutana nayo darasani kwetu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba katika

kipindi hiki mkazo umeondolewa kutoka katika mbinu za ufundishaji kuwekwa katika ujifunzaji.

Hivyo mkzao umewekwa zaidi katika mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji na mchango wa

mwalimu binafsi katika pedagojia ya ufundishaji lugha.

You might also like