You are on page 1of 2

ECT 720

1.0 Maelezo ya Somo


Uelewa wa mbinu za lugha na fasihi ni jambo muhimu sana kwa
mwalimu ye yote. Somo hili linalenga kuangazia maswali nyeti katika
ufundishaji wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Utaangazia vilevile maswali
ya sera za elimu, stadi za lugha, dhima ya fasihi, na maandalizi ya
mwalimu kwa madhumuni ya kufundisha somo fulani.
2.0 Madhumuni ya somo
Somo hili lina madhumuni ya kuwezesha mwalimu mtarajiwa kuwa na
uwezo wa:
2.1 Ufahamu bora wa mbinu tofauti za kufundisha stadi za lugha na fasihi.
2.2 Kutathimini mbinu za kufundisha lugha ya Kiswahili na fasihi yake.
2.3 Kuteua na kutumia mbinu zinazostahili katika mazingira tofauti.
2.4 Kuandaa na kuteua nyenzo/vifaa mbalimbali vya kufundishia lugha na
fasihi ya Kiswahili.
2.5 Kufanya maandalizi ya ufundishaji.
2.6 Kutathimini maendeleo ya wanafunzi.
3.0 Yaliyomo/Mada
3.1 Hadhi ya Kiswahili na Sera za Elimu nchini.
3.2 Lugha na sifa zake
3.3 Nadharia za lugha
 Lugha ya kwanza
 Lugha ya pili n.k
3.4 Stadi za lugha: Kusikiliza, Kuongea, Kusoma, Kuandika.
3.5 Ufundishaji wa sarufi na msamiati.
3.6 Sifa na Dhima ya Fasihi ya Kiswahili.
 Fasihi kama kioo cha jamii
 Fasihi kama chombo cha mawasiliano ya kijamii
 Fasihi kama matini
 Fasihi kama mbinu ya kujieleza kisanii
 Fasihi kama chombo cha urithi na tamaduni za jamii
 Fasihi kama burudani
3.7 Ufundishaji wa Tanzu mbalimbali za Fasihi.
 Fasihi Simulizi
 Fasihi andishi
3.8 Maandalizi ya mwalimu
a) Mwongozo wa somo (Syllabus)
b) Maazimio ya kazi (Scheme of work)
c) Mpangilio wa kipindi (Lesson plan)
d) Kumbukumbu ya kazi (Record of Work)
3.9 Isimu jamii
3.10 Kutahini/Utathimini

You might also like