You are on page 1of 2

ANZA SIKU NA BWANA

#0006

SOMO: KUPANDA NA KUVUNA

Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

Wagalatia 6 :7

MAVUNO HUWA NI JAMBO LA WAKATI TU.

Kama ukimfanyia mwenzako vibaya, kwa hila, ukimsema vibaya, ukimuhukumu, ukimtoa mahali kwa
hila, ukimsengenya, ukimchafua isivyo haki,

HIZI ZOTE NI MBEGU, NA UNAPANDA

UTAVUNA KILEKILE ULICHOKIPANDA

Kama ukiwasaidia watu wenye uhitaji, kuwatia moyo waliovunjika moyo, kuzungumza mazuri kuhusu
wengine, kuwafundisha wengine, kuwathamini wengine, kutoa muda kwa ajili ya wengine, kuwatendea
mema wengine.

HIZI ZOTE NI MBEGU NA UNAPANDA.

UTAVUNA KILE KILE ULICHOKIPANDA.

Ni jambo la muda
MUNGU AZIDI KUKUBALI NA UZIDI KUANGALIA VYEMA UNAVYOPANDA MBEGU ZAKO.

"AMEN"

Ni mimi ndugu yako;Kuhani na Mwl. Harrison Humphrey Mushenyera.

Kiungo katika mwili wa kristo.

Kwa maoni, ushauri na msaada zaidi

whatsap +255 768522999.

harrisonhumphrey25@gmail.com

Ubarikiwe sana Na nakuomba unisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu

You might also like