You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA JIJI MBEYA

SHULE YA MSINGI NZOVWE

TAREHE 26/07/2023

TANGAZO LA KUMPATA FUNDI JAMII


1. . Shule ya msingi Nzovwe inawatangazia wananchi wa Jiji la Mbeya wenye sifa na uwezo wa
kujenga majengo ya Serikali kuomba kazi ya ukarabati wa madarasa kama Fundi jamii kwa
ajili ya Shule ya Msingi Nzovwe iliyopo kata ya Nzovwe.
2. .Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo;-
a) Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu (3) wa ujenzi wa majengo ya Serikali.
b) Awe na vifaa vya msingi katika masuala ya ujenzi kama kono bao,pima
maji,misumeno,nyundo nk.
c) Awe na fedha/ mtaji wa kuanzia kwa ajili ya kuwalipa vibarua atakao waajiri.Vilevile
awe na Akaunti ya Benki.
d) Awe na ujuzi wa kutosha na uwezo wa kusoma ramani za majengo ya Serikali.
3. Mwombaji mwenye nia na sifa anakaribishwa kuchukua FOMU YA MAOMBI na kupata
maelezo kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nzovwe,Halmashauri ya Jiji S,LP 1979
Mbeya.Ofisi iko wazi kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 9:30 Alasiri jumatatu mpaka ijumaa
isipokuwa siku za maombi zitatolewa bure.
4. Mwombaji mwenye nia na uwezo anaweza kufanya ziara ya kutembelea eneo la mradi.Ziara ya
kutembelea eneo la mradi itafanyika tarehe 27/07/2023. kuanzia saa 2:00 asubuhi /mchana kwa
gharama zake ili kutambua kujiridhisha na eneo la mradi pamoja na masuala yatakayohitaji
ufafanuzi
5. Maombi yote yawasilishwe kwa Mwalimu mkuu yakiwa ndani ya bahasha iliyofungwa
ipasavyo.Bahasha zenye maombi zionyeshe kazi unayoomba kwa upande mmoja na kuelekezwa
kwa anuani ifuatayo;
Mwalimu Mkuu
Shule ya Msingi Nzovwe Mbeya,
S.L.P 1979,
MBEYA
6.Mwisho wa kupokea maombi hayo ni siku ya Alhamisi .......................... saa 9:00
Alasiri.Waombji au wawakilishi wote wanaalikwa kuhudhuria ufunguzi wa maombi hayo
utakayofanyika tarehe ........................ katika shule ya Msingi Nzovwe.

7. Mombi yatakayochelewa na kutofunguliwa katika tukio la ufunguzi kwa hali yoyote ile
hayatakubaliwa.

……………………………….
Mwaji Ndele Mwashubila
MWALIMU MKUU
SHULE YA MSINGI NZOVWE
HALMASHAURI YA JIJI-MBEYA

You might also like