You are on page 1of 124

PAROKIA YA BIKIRA MARIA MAMA WA HURUMA

Mt. Yohana Mtume - i


YALIYOMO
SALA YA KILA SIKU 9
SALA YA ASUBUHI 9

NIA NJEMA 9

SALA YA MATOLEO 9

BABA YETU 9

SALAMU MARIA 10

KANUNI YA IMANI 10

AMRI ZA MUNGU 10

AMRI ZA KANISA 11

SALA YA IMANI 11

SALA YA MATUMAINI 11

SALA YA MAPENDO 11

SALA YA KUTUBU 12

SALA KWA MALAIKA MLINZI 12

MALAIKA WA BWANA 12

MALKIA WA MBINGU 13
SALA YA JIONI 13

KUTUBU 14

KUOMBA KIFO CHEMA 14


SALA KWA NAFASI MBALIMBALI 15

KABLA YA KULA 15
Mt. Yohana Mtume - ii
KISHA KULA 15

KUOMBA NA KUSIFU 15

KABLA YA KAZI NA MAFUNDISHO 15

BAADA YA KAZI NA MAFUNDISHO 15

SALA YA KUMWOMBA MT. TERESIA 16

SALA YA MT. INYASI 16

TUNAUKIMBILIA 16

SALA BAADA YA KOMUNI0 16

SALA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU 17


ROZARI TAKATIFU 18
LITANIA YA BIKIRA MARIA 21
ROZARI YA HURUMA YA MUNGU 26
ROSARI YA BIKIRA MARIA MAMA WA MSAADA WA DAIMA 28
NJIA YA MSALABA 30
NOVENA YA PENTEKOSTE 45
NOVENA KWA HURUMA YA MUNGU 64
LITANIA YA HURUMA YA MUNGU 72
IBADA YA MAOMBOLEZO 75
NYIMBO KWA NAFASI MBALIMBALI 78
NYIMBO ZA MISA 78

1. NITAJONGEA ALTARE YAKO 78

2. NAYATAMANI MAKAO YA BWANA 78

3. NIMEINGIA HAPA MAHALI PATAKATIFU 79

4. KWA NYIMBO ZA SHANGWE 79


Mt. Yohana Mtume - iii
5. TWENDENI KWA BWANA TUPELEKENI: 79

6. KIKONDOO CHA MUNGU 80

7. KWELI MWISHO UWE UWINGU 80

8. EE BWANA TWAKUOMBA 81

9. ROHO YANGU YESU INAKUTAMANI 81

10. BWANA YESU ANATUITA 82

11. HIVI NDIVYO WOTE WENYE KUMCHA BWANA 82

12. NIKUPE NINI MUNGU WANGU 83

13. EE BWANA TWAKUOMBA UPOKEE 84

14. ROHO YANGU YESU INAKUTAMANI 84

15. MUNGU BABA POKEA SADAKA YETU LEO 84

16. EE BABA POKEA VIPAJI HIVI 85

17. HIKI NI CHAKULA CHA MBINGU 86

18. ENYI WATU WOTE PIGENI MAKOFI 87

19. TOA NDUGU, TOA NDUGU 87

20. EE BWANA POKEA VIPAJI VYETU 88

21. EKARISTI NI CHAKULA BORA 88

22. AULAYE MWILI WANGU 89

23. YESU ASANTE SANA 90


NYIMBO ZA BIKIRA MARIA 91

24. TUNAKUSHUKULU MAMA MARIA 91

Mt. Yohana Mtume - iv


25. JINA MARIA JINA TUKUFU 91

26. EE MAMA YETU MARIA 92

27. MIMI NI MTUMISHI WAKE BWANA 92

28. EE MARYAMU 93

29. TUMSIFU MARIA 93

30. TUMAINI LETU MAMA MARIA . 94

31. MAMA YETU MARIA 94

32. NAKUPENDA MARIA 95

33. SISI WANA WA DUNIA 95

34. EE MAMA YETU MARIA 96

35. MARIAMU EE ZIPOKEE 97

36. TUNAKUSHUKURU MAMA MARIA 98

37. MARlA ALlTEULlWA NA MUNGU 98


NYIMBO ZA KWARESIMA 100

38. KWA ISHARA YA MSALABA. 100

39. PASIPO MAKOSA 100

40. KRISTU ALIJINYENYEKEZA 101

41. TUMWANGALIE MKOMBOZI 101

42. WIMBO WAKUOMBA TOBA-TUMEKOSA 102

43. UTUREHEMU: 102

44. ASILEGEE MOYOWE 103

Mt. Yohana Mtume - v


45. ATANIITA 104

46. BABA MIKONONI MWAKO 105

47. MAMA PALE MSALABANI 105

48. MTAZAME MKOMBOZI MSALABANI 106

49. MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA 106

50. MUNGU WANGU MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA 108

51. NIMEKUKIMBILIA WEWE BWANA 108

52. UNIHURUMIE MIMI BWANA 109

53. WAKUPELEKA HUKUMUNI - P. F. Mwarabu 110

54. WATUMISHI WAKE BABA 111

55. YESU AKALIA - G. A Chavalla 112

56. YESU ALIA MSALABANI 113

57. YESU MSALABANI ALIPOTUNDIKWA - F. A. Nyundo 114

58. YESU WANGU NIOKOE - A. K. C. Singombe 114


NYIMBO NYINGINE 116

59. UJE ROHO MTAKATIFU SEKWENSIA 116

60. JIWE WA ULOKATAA WAASHI 116

61. NINAKULILIA KATIA UNYONGE WANGU 117

62. KESHENI KILA WAKATI 118

63. TUMAINI LETU NI KWA BWANA 118

64. BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU – J. Mgandu 119

Mt. Yohana Mtume - vi


65. HUO NDIO MWANZO 120

66. SIMAMA IMARA 120

67. TAWALA BWANA, TAWALA BWANA 121

68. TAWALA TAWALA 121

Mt. Yohana Mtume - vii


SALA KWA MT. YOHANE MTUME

Ewe Mt. Yohana uliyepend‐


wa na Yesu kiasi cha kusta‐
hili kuweka kichwa chako
kifuani kwake na
kukuachia mamae uwe
mtoto wake.
Tunakuomba utujalie
mapenzi ya kweli ya Yesu
na Maria, tuungane nao
hapa duniani na milele hu‐
ko mbinguni. Amina

Mt. Yohana Mtume - 8


SALA YA KILA SIKU
SALA YA ASUBUHI
Ee Baba yetu Mungu mkuu, Umenilinda usiku huu, Na-
kushukuru kwa Moyo, Ee Baba, Mwana, na Roho. Ni- linde
tena siku hii, Niache dhambi, nikutii. Naomba sa- na, Baba
wee, Baraka yako nipokee. Bikira safi, Ee Ma- ria, nisipotee
nisimamie, Mlinzi mkuu Malaika wee. Kwa Mungu wetu
niombee. Nitake, nitende mema tu, na mwisho nije kwako
juu. Amina.

NIA NJEMA
Kumheshimu Mungu wangu namtolea roho yangu, ni-
fanye kazi nipumzike, Amri zake tu nishike. Wazo, neno,
tendo lote namtolea Mungu pote, Roho, mwili, chote
changu, Pendo na uzima wangu, Mungu wangu nitamp-
enda, wala dhambi sitatenda. Jina lako nasifia, utakalo
hutimia, kwa utii navumilia, teso na matata pia. Nipe
Bwana, neema zako niongeze sifa yako. Amina.

SALA YA MATOLEO
Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa muungano
na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, ma-
sumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme
wako utufikie.

BABA YETU
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe, Ufalme
wako ufike, utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa
yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usi-
tutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.
Mt. Yohana Mtume - 9
SALAMU MARIA
Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yuu nawe,
umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa
tumbo lako, amebarikiwa. Maria Mtakatifu, Mama wa
Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa
kwetu. Amina

KANUNI YA IMANI
Nasadiki kwa Mungu, Baba mwenyezi, mwumba wa
mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristu, Mwana wa pekee,
Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,
akazaliwa na Bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya
Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa; akashukia
kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa
mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi;
toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, kanisa takatifu katoliki,
ushirika wa Watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko
wa miili, na uzima wa milele. Amina.

AMRI ZA MUNGU
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu Miungu wen-
gine.
2. Usitaje bure jina la Mungu wako.
3. Shika Kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu baba na mama, upate miaka mingi na
heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uwongo.

Mt. Yohana Mtume - 10


9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.

AMRI ZA KANISA
1. Hudhuria Misa takatifu Dominika na sikukuu
zilizoamriwa.
2. Funga siku ya Jumatano ya majivu; usile nyama siku
ya ljumaa Kuu.
3. Ungama dhambi zako zote walau mara moja kila
mwaka.
4. Pokea Ekaristi Takatifu hasa wakati wa Paska.
5. Saidia kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.

SALA YA IMANI
Mungu wangu, nasadiki maneno yote linayosadiki, lina-
yofundisha kanisa Katoliki la Roma: Kwani ndiwe uli-
yetufumbulia hayo, wala hudanganyiki, wala udanganyi.
Amina.

SALA YA MATUMAINI
Mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya
Yesu Kristu, neema zako duniani na utukufu mbinguni,
kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi, nawe mwamini. Ami-
na.

SALA YA MAPENDO
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote; kwani ndi-
we mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na

Mt. Yohana Mtume - 11


jirani yangu kama nafsi yangu kwa ajili yako. Amina.

SALA YA KUTUBU
Mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu, kwani
ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa
na dhambi. Basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio,
naomba neema yako nipate kurudi. Amina.

SALA KWA MALAIKA MLINZI


Malaika Mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho
na mwili.

MALAIKA WA BWANA
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
Naye akapata mimba kwa Roho Mtakatifu.
Salamu, Maria, ........... .

Ndimi mtumishi wa Bwana.


Nitendewe ulivyonena.
Salamu, Maria, ........... .

Neno la Mungu akatwaa mwili.


Akakaa kwetu.
Salamu, Maria, ........... .

Utuombee, mzazi mtakatifu wa Mungu.


Tujalie ahadi za Kristu.

Tuombe . Tunakuomba Ee Bw ana utie neema yako


mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya malaika
Mt. Yohana Mtume - 12
kwamba mwanao amejifanya mtu kwa mateso ya msal-
aba wake tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko. Tuna-
omba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.

MALKIA WA MBINGU
Malkia wa mbingu furahi, Aleluya.
Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya.
Amefufuka alivyosema, Aleluya.
Utuombee kwa Mungu, Aleluya.
Furahi, shangilia, ee Bikira
Maria.Aleluya. Kwani, hakika Bwana
amefufuka. Aleluya.

Tuombe Ee Mungu uliyependa kuifurahisha dunia, kwa


kufufuka kwake Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao;
Fanyiza twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi
furaha za uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya
Kristu Bwana wetu. Amina.

Roho ya Kristu, nitakase.


Mwili wa Kristu, niokoe.
Damu ya Kristu, nifurahishe.

Malaika Mlinzi wangu …..

SALA YA JIONI

Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji yote uliyotujalia


leo. Amina.
Baba yetu ... Salamu Maria ...
Sala ya lmani ... ya Matumaini. .. ya Mapendo.
Mt. Yohana Mtume - 13
KUTUBU
Tuwaze katika moyo wetu makosa ya leo tuliyomkosea
Mungu kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo, na kwa
kutotimiza wajibu.

(Jichunguze kidogo)

Nakuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu,


kwani nimekosa mno kwa mawazo, kwa maneno, kwa
vitendo na kwa kutotimiza wajibu, nimekosa mimi,
nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana nakuom-
ba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na Wa-
takatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwa-
na Mungu wetu.

Mungu mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu,


atufikishe kwenye uzima wa milele.
W. Amina.

KUOMBA KIFO CHEMA


Enyi, Yesu, Maria na Yosefu, nawatolea moyo na roho,
na uzima wangu !
Enyi, Yesu, Maria, na Yosefu, mnijie saa ya kufa
kwangu !
Enyi, Yesu, Maria, na Yosefu, mnijalie nife mikononi
mwenu !
(rehema ya siku 300)

Malaika Mlinzi wangu …..

Malaika wa Bwana/ Malkia wa mbingu ...

Atukuzwe Baba …. Amina.

Mt. Yohana Mtume - 14


SALA KWA NAFASI MBALIMBALI
KABLA YA KULA
Unibariki, Mungu wangu, mimi na chakula changu,
nipate nguvu za kukutumikia vema. Amina.

KISHA KULA
-Nakushukuru Mungu wangu, kwa chakula ulichonipa,
nipate nguvu za kukutumikia vema. Am ina.

KUOMBA NA KUSIFU
Mungu wangu, nawaombea watu wa nchi hii, wapate
kusikia maneno yako na kukupenda wewe Bwana Mun-
gu wetu.

Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.


Kama mwanzo, na sasa, na siku zote, na milele. Am ina.

KABLA YA KAZI NA MAFUNDISHO


Roho mkuu, mfariji mwema
Mwenye kila kitu chema,
Uje kutuangazia
Na imani kututia,
Tusikie mafundisho
Tuyashike mpaka mwisho. Amina.

BAADA YA KAZI NA MAFUNDISHO


Twakushukuru, ee Mungu Mwenyezi, sababu ya
mema yako yote. Unayeishi na kutawala, ee Mungu,
milele. Amina.

Mt. Yohana Mtume - 15


SALA YA KUMWOMBA MT. TERESIA
Ee Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, ulistahili kuitwa
Msimamizi wa misioni katoliki za dunia yote.
Kumbuka ile tamaa yako kuu uliyoonyesha huku
duniani ya "kusimika Msalaba wa Yesu Kristu, kat ika
nchi zote, na kuhubiri lnjili mpaka mwisho wa dunia".
Twakuomba kwa ajili ya maagano yako, wasaidie
mapadre, wamisionari, na Kanisa zima.
Ee Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu msimamizi wa misioni
utuombee

SALA YA MT. INYASI


Roho ya Kristu intakase,
Mwili wa Kristu uniokoe,
Damu ya Kristu inifurahishe,
Maji ya ubavu wa Kristu, yanioshe.
Mateso ya Kristu, nguvu yanizidishie. Ee
Yesu mwema, unisikilize.
Katika madonda yako, unifiche. Usikubali
nitengwe nawe.
Na adui mwovu unikinge. Saa ya kufa
kwangu uniite. Uniamuru kwako nije.
Pamoja na Watakatifu wako nikutukuze,
Milele na milele. Amina.

TUNAUKIMBILIA
Tunaukimbilia, ulinzi wako, mzazi Mtakatifu wa Mungu,
Usitunyime tukiomba katika shida zetu, utuokoe kila
tuingiapo hatarini, ee Bikira mtukufu mwenye baraka.
Amina

SALA BAADA YA KOMUNI0


Mt. Yohana Mtume - 16
Ee Yesu Mwema mno, nakuangukia nikiomba kwa
kutaka sana, upende kutia Moyoni mwangu imani na
matumaini na mapendo yako. Unifanye nitubu kweli
dhambi zangu, nitake sana kugeuza mwendo wangu.
Ndiyo hayo ninakuomba sasa niwazapo ninapoangalia
kwa akili yangu, madonda yako matano, kwa kukusik-
itikia sana Moyoni, na kukuonea huruma, nikikumbuka
maneno aliyonena nabii Daudi juu yako, akisema;
"wakanitoboa mikono na miguu, wakahesabu mifupa
yangu yote".
(Baba yetu .... Salamu Maria .... Atukuzwe Baba ......
kwa nia za Baba Mtakatifu)

SALA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU

Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, utulinde katika vita, uwe


kinga yetu katika maovu na maoteo ya shetani, Mungu
amtiishe, tunaomba sana, nawe Mkuu wa Majeshi ya
Mbinguni kwa nguvu ya Mungu uwaangushe motoni
shetani na pepo wabaya wengine wote, wanaozunguka
duniani, ili kuzipoteza roho za watu. Amina.

Mt. Yohana Mtume - 17


ROZARI TAKATIFU
Rozari takatifu – MAFUMBO/MATENDO YA ROZARI

Baada ya Salamu Maria kabla ya fumbo:

Atukuzwe baba na Mwana na Roho Mtakatifu, kama mwanzo


na sasa na siku zote na milele Amina.

Tuwasifu milele - Yesu Maria na Yosefu x1

Ee Yesu - Utusamehe dhambi zetu utuepushe na moto wa


milele. Ongoza roho za watu wote wafike mbinguni,hasa wale
wanaohitaji zaidi huruma yako

Damu ya Kristu - Iziokoe roho zinazoteswa toharani izijalie


mwanga wa milele. Amina.

Matendo ya furaha (Jumatatu na Jumamosi)


1. Malaika anampasha habari Maria kama atakuwa Mama
wa Mungu.
Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.

2. Maria anakwenda kumtembelea Elizabeti.


Tumwombe Mungu atujalie mapendo ya
jirani.

3. Yesu anazaliwa Betlehemu.


Tumwombe Mungu atujalie moyo wa ufukara,

4. Yesu anatolewa hekaluni.


Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.

Mt. Yohana Mtume - 18


5. Maria anamkuta Yesu hekaluni.
Tumwombe Mungu atujalie kuwatii wakubwa wetu.

Matendo ya uchungu (Jumanne na Ijumaa)


1. Yesu anatoka jasho la damu.
Tumwombe Mungu atujalie sikitiko la dhambi.

2. Yesu anapigwa mijeledi.


Tumwombe Mungu atujaJie kuacha dhambi za uchafu.

3. Yesu anatiwa miiba kichwani.


Tumwombe Mungu atujalie kushinda kiburi.

4. Yesu anachukua msalaba.


Tumwombe Mungu atujalie kuvumilia taabu.

5. Yesu anakufa msalabani.


Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu na Maria.

Matendo ya utukufu (Jumatano na Jumapili)


1. Yesu anafufuka.
Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.

2. Yesu anapaa mbinguni.


Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.

3. Roho Mtakatifu anawashukia Mitume.


Tumwombe Mungu atujalie bidii katika dini yetu.

4. Bikira Maria anapalizwa mbinguni.


Tumwombe Mungu atujalie kufa vizuri.

5. Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni.


Mt. Yohana Mtume - 19
Tumwombe Mungu atujalie kudumu katika njia njema.

Matendo ya Mwanga (Alhamisi)


1. Ubatizo wa Yesu mtoni Yordani.
Tumwombe Mungu atujalie uaminifu kwa ahadi zetu za ubati-
zo.

2. Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana


Tumwombe Mungu atujalie kuukoleza ulimwenqu kwa chachu
ya Injili.
3. Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu.
Tumwombe Mungu atujalie kupokea ufalme wake kwa toba ya
kweli.

4. Yesu anageuka sura.


Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung'arisha ulimwengu
kwa uso wa Yesu.

5. Kuwekwa kwa Ekaristi.


Tumwombe Mungu atujalie neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya
wengine.

Mt. Yohana Mtume - 20


LITANIA YA BIKIRA MARIA

Bwana Utuhurumie Bwana Utuhurumie


Kristu Utuhurumie Kristu Utuhurumie
Bwana Utuhurumie Bwana Utuhurumie
Kristu Utusikie Kristu Utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie
Mwana mkombozi wa dunia Mungu Utuhurumie
Roho mtakatifu wa Mungu Utuhurumie
Utatu mtakatifu, Mungu mmoja Utuhurumie
Maria mtakatifu Utuombee
Mzazi mtakatifu wa Mungu Utuombee
Bikira mtakatifu, mkuu wa mabikira Utuombee
Mama wa Kristo Utuombee
Mama wa kanisa Utuombee
Mama wa neema ya Mungu Utuombee
Mama mtakatifu sana Utuombee
Mama mwenye moyo safi Utuombee
Mama mwenye ubikira Utuombee
Mama usiye na dhambi Utuombee
Mama mpendelevu Utuombee
Mama mstaajabivu Utuombee
Mama wa shauri jema Utuombee
Mama wa Mwumba Utuombee
Mama wa Mkombozi Utuombee
Bikira mwenye utaratibu Utuombee
Bikira mwenye heshima Utuombee
Bikira mwenye sifa Utuombee

Mt. Yohana Mtume - 21


Bikira mwenye enzi Utuombee
Bikira mwenye huruma Utuombee
Bikira mwaminifu Utuombee
Kioo cha haki Utuombee
Kikao cha hekima Utuombee
Sababu ya furaha yetu Utuombee
Chombo cha neema Utuombee
Chombo cha heshima Utuombee
Chombo bora cha ibada Utuombee
Waridi lenye fumbo Utuombee
Mnara wa Daudi Utuombee
Mnara wa Pembe Utuombee
Nyumba ya dhahabu Utuombee
Sanduku la agano Utuombee
Mlango wa mbingu Utuombee
Nyota ya asubuhi Utuombee
Afya ya wagonjwa Utuombee
Kimbilio la wakosefu Utuombee
Mfariji wa wenye uchungu Utuombee
Msaada wa wakristu Utuombee
Malkia wa malaika Utuombee
Malkia wa mababu Utuombee
Malkia wa manabii Utuombee
Malkia wa mitume Utuombee
Malkia wa mashahidi Utuombee
Malkia wa waungama Utuombee
Malkia wa mabikira Utuombee
Malkia wa watakatifu wote Utuombee
Malkia uliyeumbwa pasipo dhambi ya Utuombee
asili
Malkia Uliyepalizwa mbinguni Utuombee
Mt. Yohana Mtume - 22
Malkia wa Rozari takatifu Utuombee
Malkia wa familia Utuombee
Malkia wa amani Utuombee
Mwanakondoo wa Mungu uondoae Utusamehe Ee
dhambi za dunia . Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoae Utusikilize Ee
dhambi za dunia Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoae Utuhurumie
dhambi za dunia

K. Utuombee mzazi mtakatifu wa Mungu


W. Tujaliwe Ahadi za Kristo

Ee Bwana Mungu, twakuomba, utujalie sisi watumishi


wako afya ya roho na ya mwili siku zote, na kwa
maombezi matukufu ya Maria Mtakatifu, Bikira daima,
tuopolewe na mashaka ya sasa tupate na furaha za
milele, kwa Kristo Bwana wetu, Amina

Kumbuka
Kumbuka, ee Bikira Maria mpole sana, haijasikika bado
hata mara moja kwamba ulimwacha mtu aliyeukimbilia
ulinzi wako, Akiomba msaada na maombezi yako. Kwa
matumaini hayo nlnakukimbilia wewe, Ee mama, Bikira
wa Mabikira, ninakuja kwako ninasimarna mbele yako
nikilalamika mimi mkosefu. Ee mama. wa Neno la Mun-
gu usikatae maneno yangu, bali upende kuyasikia na
kuyasikiliza, Amina.

Salamu Malkia
Mt. Yohana Mtume - 23
Salamu Malkia mama mwenye huruma; uzima, tulizo na
matumaini yetu salamu. Tunakusihi ugenini hapa sisi
wana wa Eva. Tunakulilia, tunakulalamikia na kuhuzu-
nika bondeni huku kwenye machozi. Haya basi,
mwombezi wetu -Utuangalie kwa macho yako yenye hu-
ruma, na mwisho wa ugeni huu, -Utuonyeshe Yesu na
mzao mbarikiwa wa tumbo lako.
Ee mpole, Ee mwema Ee mpendelevu Bikira Maria.

Sala ya Mt. Yosefu


Ee Mt. Yosefu mwenye heri, tunakimbilia kwako katika
masumbuko yetu, na kisha omba shime ya Mchumba
wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi
wako. Kwa ajili ya mapendo uliyompenda Bikira Mtakatifu
Mzazi wa Mungu, na kwa ajili ya kumtunza Mtoto Yesu,
twakuomba sana, utuangalie kwa wema sie tuliokuwa
fungu lake Yesu Kristu, tukakombolewa kwa damu yake.
Tusimamie katika masumbuko yetu kwa enzi na shime
yako.
Ee Mlinzi amini wa jamaa takatifu, uwakinge watoto
wateule wa Yesu Kristu. Ee Baba uliyetupenda mno
tuepushe na kilema chochote cha madanganyo na
upotevu. Ee kinga yetu mwezaji, utusimamie huko juu
mbinguni ulipo, tunaposhindana na wenye nguvu wakaao
gizani. Kama vile siku za kale ukamwopoa Mtoto Yesu
katika hatari ya kuuawa, na leo hivi likinge Kanisa
Takatifu la Mungu katika mitego ya adui, na katika shida
yote; mtunze daima kila mmoja wetu, tufwate mfano
wako, ili tupate na msaada wako, kukaa na utakatifu
maisha, kufa kifo chema, na kupata mbinguni makao ya
raha milele. Amina.

Mt. Yohana Mtume - 24


.

Mt. Yohana Mtume - 25


ROZARI YA HURUMA YA MUNGU

1. Baba Yetu
2. Salamu Maria
3. Nasadiki
4. Baba wa Milele, ninakutolea MWILI na DAMU, ROHO
na UMUNGU wa Mwanao Mpenzi, Bwana wetu Yesu
Kristu kwa kulipia dhambi zetu na dhambi za dunia
nzima
5. Kwa ajili ya Mateso makali ya Yesu, Utuhurumie sisi
na dunia nzima.

Kumaliza
Mt. Yohana Mtume - 26
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu Mwenye Enzi Mtakatifu
Uishiye milele, utuhurumie sisi na dunia nzima. x 3

Mt. Yohana Mtume - 27


ROSARI YA BIKIRA MARIA MAMA
WA MSAADA WA DAIMA
Namna ya kusali Rozari kwa Bikira Maria Mama wa
Msaada wa Daima (Tumia rosari ya kawaida)

KILA FUNGU SALI SALA ZIFUATAZO:


1. Mwanzo, kwenye Msalaba:
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Amina.
2. Kwenye chembe ndogo za awali:
K: Ee Mungu utuelekezee msaada W: Ee Bwana
utusaidie hima
W: Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
Kama mwanzo na sasa na siku zote na milele.
Amina.

Maria ametusaidia,
Maria anataka kutusaidia,
Maria anaweza kutusaidia,
Maria atatusaidia.
3. Kwenye chembe kubwa:
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,
Kama mwanzo na sasa, na siku zote, na milele.
Amina.

Maria ametusaidia,
Maria anataka kutusaidia,
Maria anaweza kutusaidia,
Maria atatusaidia.

Ee Maria Mama wa Msaada wa daima


Mt. Yohana Mtume - 28
Sikiliza maombi ya roho zetu
Unaweza kutusaidia katika mahitaji yetu
Ee Maria kwa matumaini twakuita wewe.

4. Kwenye chembe ndogo:


Kama unasali mwenyewe: “Ee Maria, utusaidie!
(mara kumi)
Kama mnasali zaidi ya mmoja kwa pamoja: K; Ee
Maria, W: Utusaidie. (mara kumi)

5. MWISHO SALI SALA ZIFUATAZO:

Salamu Maria ….., Tunaukimbilia …….

Mt. Yohana Mtume - 29


NJIA YA MSALABA
Wimbo:
Tufate njia ya Msalaba,
Tuifate mpaka Kalivario
Tusimamepo bila haya
Msalaba, Msalaba huponya roho

SALA MBELE YA ALTARE

Ee Mkombozi wangu, ninakuja leo kufuata njia ile


uliyoshika siku ya kufa sadaka yetu. Nimetubu
dhambi zangu zote; ninataka kugeuza mwendo
wangu, ninaomba kwako niwapatie roho za wau-
mini marehemu waliomo toharani, rehema zote
zilizotolewa na Kanisa kwa Njia ya Msalaba.

Nawe Maria Bikira Mtakatifu, uliyefuata njia ile


nyuma ya Mwanao Yesu, uniangalie kwa wema,
unitie moyo mkuu, nisipende dhambi tena, ni-
kivumilia kazi na usumbufu na mateso na matukio
yatakayonipata

Wimbo:
Umekosa nini we Yesu
Kushitakiwa bure kwa Pilato
Wenye kustahili hukumu
Si wewe, si wewe Bwana, ni sisi.

KITUO CHA KWANZA

Yesu anahukumiwa afe


Mt. Yohana Mtume - 30
- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.
- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Pilato anamhukumu Yesu ingawa haoni kosa lake,


anawaogopa Wayahudi. Anabembeleza urafiki wa
Kaysari.

Ee Yesu usiye na kosa, hata mimi ningeweza kutenda


mema mengi, lakini naogopa macho ya wenzangu, na
maneno yao. Ee Bwana, uniimarishie utashi wangu ni-
jitegemee katika kushika madaraka yangu. '
Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba
K. Ee Bwana, utuhurumie W. Utuhurumie.
Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, wapumzike kwa amani. Amina

Wimbo:
Ole msalaba huo mzito
Apagazwa mwana mpenzi wa Mungu.
Mwili waenea mateso
Alipa, alipa madhambi yetu.

KITUO CHA PILI

Yesu anapokea msalaba

- Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako
mtakatifu.

Yesu anakubali kuelemewa na msalaba kwa ajili

Mt. Yohana Mtume - 31


ya wokovu wa watu. Ndivyo anavyonifundisha
moyo wa sadaka, moyo wa kujitolea na kujisahau
kwa ajili ya wengine.
Ee Yesu wangu mkarimu, mimi pia ninao msalaba wangu:
jirani zangu, mwenzangu wa ndoa, watoto wazazi wangu,
kazi zangu, joto, baridi, njaa, kiu, vi- shawishi magonjwa
na matatizo mengine ya maisha, wa11bu wangu kwa
Mungu, kwa Umma na kwa Kanisa. Hayo yote ni msalaba.
Unipe ukarimu wako ee Yesu ni- yapokee bila
kunung'unika, na kuyabeba vema.
Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba:

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, Wapumzike kwa amani. Amina

Wimbo:

Ona Muumba mbingu na nchi


. Yupo chini mzigo wamwelemea
Na mtu kiumbe chake kwa ukali
Ampiga, ampiga bila huruma.
KITUO CHA TATU

Yesu anaanguka mara ya kwanza

- Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Yesu amedhoofika sana, anaanguka chini, kasha


ana-simama, anaendelea na safari ya ukombozi.
Mt. Yohana Mtume - 32
Ee Yesu uliyeanguka chini ya msalaba kwa ajili ya
udhaifu, ukasimama tena; usiniache katika tamaa
nikianguka dhambini, bali nisimame mara moja, nikufu-
ate.
Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba:

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, Wapumzike kwa amani. Amina

Wimbo:

Huko njiani we Maria


Waonaje hali ya mwanao
Ni damu tupu na vidonda
Machozi, machozi yamfumba macho.

KITUO CHA NNE

Yesu anakutana na Mama yake

- Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Wote wawili mama na mwanawe wanaumia sana


moyoni kwa ajili ya dhambi zangu.

Ee Yesu, mwana wa Maria, unitilie moyoni mwangu up-


endo na ibada kwa Bikira Maria; unijalie na ulinzi wake,
nisitende dhambi tena.

Baba yetu ...Salam Maria ... Atukuzwe …


Mt. Yohana Mtume - 33
K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.
Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu , Wapumzike kwa amani. Amina

Wimbo:

Kwa Simoni heri ya weli, Mimi


pia YESU nisaidie, Kuchukua
mzigo wa ukombozi, Kuteswa,
kuteswa pamoja nawe.

KITUO CHA TANO


Simon wa Kirene anamsaidia Yesu

- Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Nausifu ukarimu wa Simoni wa Kirene. Ee Bwana,


unijalie ukarimu kama huo, nitie ushujaa kama
huo, niitikie nami wito wa kukusaidia kuchukua
msalaba.

Nitoe zaka na michango yote ya uenezaji wa dini; nijit-


olee mimi mwenyewe katika kazi ya maendeleo ya dini.
Uwajalie vijana wengi wito wa upadre, waweze
kuchukua msalaba pamoja nawe kwa ajili ya wokovu wa
dunia. Uwaimarishe viongozi wa dini. Usitawishe Moyoni
mwa waumini wote mwamko wa utume

Mt. Yohana Mtume - 34


Baba yetu ...Salam Maria ... Atukuzwe …

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa Mungu ,
Wap- umzike kwa amani. Amina

Wimbo:
Uso wa Yesu malaika
Betlehemu walikuabudu
Bahati yake Veronika
Kupangusa, kupangusa mfalme wa mbingu.

KITUO CHA SITA

Veronika anapangusa uso wa Yesu

- Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru:


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako
mtakatifu.
Mama huyu ni kinyume kabisa cha. Pilato. Veroni-
ka anajua analopaswa kutenda, na analitenda bila
kujali macho na maneno ya makundi ya watu
waovu.

Ee Yesu, uliyemtuza Veronika zawadi ya picha ya uso


wako juu ya kitambaa, unijalie ushupavu na ujasiri
wake wa kutenda mema, ili roho yangu ipambwe kwa
chapa ya uungwana na utakatifu wako.

Baba yetu • Salamu Maria • Atukuzwe Baba.

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Mt. Yohana Mtume - 35
Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Wimbo:

Wakimvuta huku na huku


Wauaji wanamchokesha bure
Chini wamtupa bado kwa nguvu
Aibu, aibu yao milele.

KITUO CHA SABA


Yesu anaanguka mara ya pili

- Ee Yesu tunakuabudu tunakushukuru


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa Msalaba wako
mtakatifu.

Ee Yesu uliyelegea mno kwa mateso makali, una-


poanguka mara ya pili kwa ajili ya udhaifu wa
mwili, wanionya kwamba hata mimi naweza ku-
rudi dhambini kwa udhaifu wa moyo.

Nipe basi neema ya kuepuka nafasi za dhambi na visa


vyenye kunikwaza na kunirudisha dhambini.

Baba yetu - Salamu Maria . Atukuzwe Baba

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, wapumzike kwa amani. Amina

Mt. Yohana Mtume - 36


Wanawake wa Israeli
Musilie kwa sababu hiyo
Muwalilie hao kwa dhambi
Upanga, upanga ni juu yao
KITUO CHA NANE

Akina mama wanamlilia Yesu

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Asanteni sana akina mama kwa moyo wenu wa


huruma.

Ee Yesu uliyetulizwa na wanawake, unipe moyo wa ku-


waheshimu akina mama wote. Uwaite na wasichana
wengi waingie utawa, ili watulize Moyo wako Mtakatifu
kwa sala na sadaka zao.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba.K. Ee Bwana,


utuhurumie. W. Utuhurumie.
Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Mwokozl sasa ni ya tatu


Waanguka chlni ya msalaba
Katika dhambi za ulegevu
Nijue, nijue kutubu hlma

Mt. Yohana Mtume - 37


KITUO CHA TISA

Yesu anaanguka mara ya tatu

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru. ·


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Ee Yesu unayezidi kudhoofika kwa mateso unaan-


guka kwa mara ya tatu, upate kunistahilia neema
ya kuutumikisha mwili wangu na kuusulibisha,
licha ya kuepuka nafasi za dhambi.

Mara nyingi mno ninajibovusha kwa kupenda mno


starehe, anasa na tafrija. Ee Yesu mwema, nisaidie
kuufuata mfano wa Mtakatifu Paulo. niutese mwili
wangu na kuutumikisha, ili nipate siku moia tuzo
mbinguni.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Muje malaika wa mbingu


Funikeni mwiliwe kwa huruma
Vidonda vyake na utupu

Askari, askari wamemvua.


KITUO CHA KUMI
Mt. Yohana Mtume - 38
Yesu anavuliwa nguo

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Askari wanamvua kwa nguvu nguo yake, iliyogan-


damana na madonda yake; wanayaamsha mara
moja mateso yote aliyoteswa tangu mwanzo.

Ee Yesu, unayavumilia mateso makali haya, upate kuni-


fundisha kuuvua kwa nguvu moyoni mwangu urafiki
mbaya, au kitu kingine cho chote kile kinachoharibu
urafiki wa Mungu, hata ikinipasa kutoa sadaka kubwa.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba.

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za waumini marehemu wapate rehema
kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Hapo mkristu ushike moyo


Bwana wako alazwa msalabanl
Mara miguu na mikono
Yafungwa, yatungwa kwa. misumari
KITUO CHA KUMI NA MOJA

Yesu anasulibishwa msalabani

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
Mt. Yohana Mtume - 39
mtakatifu.
-
Ee Yesu uliyepigiliwa misumari msalabani, naku-
tolea akili na utashi wangu, vifungwe pamoja na
miguu yako, nipate kuwaza, kusema na kutenda siku
zote yale tu yanayolingana na utukufu wa msalaba
wako mtakatifu.

Ee Yesu, mimi ni mfungwa wako. Nisaidie kuimarisha


kifungo hicho kwa sala, sakramenti na fadhila za
kikristu.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba.

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Yesu mpenzi nakuabudu


Msalabani unapohangaika
Nchi yatetemeka kwa hofu
Na jua, na jua linafifia.

KITUO CHA KUMI NA MBILI

Yesu anakufa msalabani

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Mt. Yohana Mtume - 40


Ee Yesu uliyekufa msalabani kwa ajili ya dhambi
zangu, unijalie niichukie dhambi, nisiishi kamwe
katika dhambi.

Nifahamu kwamba nilipobatizwa kwa jina lako, niliba-


tizwa katika mauti yako, ili utu wangu wa kale
usulibishwe nawe, mwili wa dhambi uangamizwe, nisitu-
mikie tena dhambi.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba.

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

Mama Maria mtakatifu


Upokee maiti ya mwanao
Tumemwua kwa dhambi zetu
Twatubu, twatubu kwake na kwako

KITUO CHA KUMI NA TATU

Yesu anashushwa msalabani

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Ee yesu uliyeshushwa msalabani baada ya kufa,


unijalie nidumu katika maisha ya kujitoa sadaka
mpaka siku ya kufa kwangu.

Mt. Yohana Mtume - 41


Nielewe na nikubali kwamba baada tu ya kufa ndiyo
mwisho wa vita na mashindano ya kikristu.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba.

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Roho za wa umini marehemu wapate rehema
kwa Mungu, wapumzike kwa amani. Amina

Pamoja nawe kaburini


Zika dhambi na ubaya wa moyo
Yesu tuwe wakristu kweli
Twakupa, twakupa sasa mapendo

KITUO CHA KUMI NA NNE


Yesu anazikwa kaburini

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Ee Yesu ulizikwa kaburini, ukafufuka siku ya tatu.


Mimi pia nilizikwa pamoja nawe kwa njia ya ubati-
zo katika mauti yako.

Kwa vile wewe ulifufuka katika wafu kwa njia ya utukufu


wa Baba, unijalie nami nifufuke, yaani nishike mwenen-
do mpya, mwenendo wa uzima wa neema.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba. ·

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Mt. Yohana Mtume - 42
Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu. wapumzike kwa amani. Amina.

Katika roho yangu Bwana


Chora mateso niliyokutesa
Nisiyasahau madeni
Na kazi, na kazi ya kuokoka.

(Hiari yako - mbele ya Altare:)

KITUO CHA KUMI NA TANO

Yesu amefufuka

- Ee Yesu tunakuabudu, tunakushukuru.


- Kwa kuwa umewakomboa watu kwa msalaba wako
mtakatifu.

Habari Njema aliyotuletea Yesu ni kwamba baada


ya kila ljumaa Kuu huja sikukuu ya Pasaka; kwam-
ba punje ya ngano isipoanguka ikafa, hukaa hali
hiyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao
mengi.

Twakushukuru, ee Yesu. kwa mateso yako, lakini twa-


kushukuru hasa kwa ufufuko wako, kwa kuwa huo ndio
unaotupa hakika ya kuwa hatukuzaliwa kwa ajili ya
mateso na maumivu, bali kwa ajili ya heri ya milele.

Baba yetu - Salamu Maria - Atukuzwe Baba.

K. Ee Bwana, utuhurumie. W. Utuhurumie.


Mt. Yohana Mtume - 43
Roho za waumini marehemu wapate rehema kwa
Mungu, wapumzike kwa amani. Amina.

SALA YA MWISHO
(Mbele ya Altare)

Yesu wangu, kwa uchungu wote ulioona juu ya


msala- ba, na kwa kuzimia kwako kwa ukali wa
mateso, unijalie nguvu ya kuvumilia kwa moyo
taabu zote sasa na saa ya kuzimia kwangu. Nawe
Maria Mamangu, kwa uchungu wote ambao moyo
wako umejaa ulipomwona Mwanao mpenzi
kuinama kichwa na kuzimia, unifadhili nife kifo
chema

Mt. Yohana Mtume - 44


NOVENA YA PENTEKOSTE
SIKU YA KWANZA IJUMAA
ROHO MTAKATlFU ANATUFARIJI

Yesu alipokuwa akiagana na Mitume wake, kabla ya Kupaa


mbinguni, aliwaambia wasiondoke Yerusalemu mpaka hapo
watakapokuwa wamempokea Roho Mtakatifu. Aliwaambia:
"Wakati Roho Mtakatifu atakapowashukieni, mtajazwa nguvu,
nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika nchi
yote ya Yuda na Samaria, hata kwenye mipaka yote ya
dunia."(Mdo. 1:8)
Waliendelea kusali pamoja toka hapo Yesu alipopaa mbinguni
mpa- ka siku ya Pentekoste. Waliomba Roho Mtakatifu awashukie,
awajaze na mapaji yake. Na baada ya siku tisa Roho Mtakatifu
aliwashukia hao kundi dogo, nao wakawa chanzo cha Kanisa
lililopata kuenea duniani kote.
Siku hizo tisa za kusali zinaitwa NOVENA; na kila mwaka wakati
huu, wakristu wakifuata mfano wa Mitume, wanasali muda wa
siku tisa kabla ya sikukuu ya Pentekoste. Wanamwomba Roho
Mtakatifu awashukie, awajaze nguvu na wingi wa mapaji yake.
Wakati huu wa NOVENA, tunayo mengi ya kuliombea Kanisa na
kujiombea sisi wenyewe. Kwa hiyo tumwombe Roho Mtakatifu
atu- saidie kusali vema na kuomba yale yote tunayoyahitaji kwa
masilahi yetu ya roho na mwili.
Na kama Mtume Paulo alivyowaambia wale wakristu wa kwanza,
Roho Mtakatifu huja kutufariji katika udhaifu wetu. Basi
tumwombe atufariji kwa sala hizi za NOVENA, atuwezeshe kusali
na kuomba ina- vyotupasa kusali.

1. Ee Baba wa milele, tunakuomba umtume Roho Mtakatifu


atu- shukie sisi taifa lako, awashe ndani yetu moto wa upendo
Mt. Yohana Mtume - 45
wako.
W. Twakuomba utusikie
2. Ee Baba mwema, tunakuomba utujalie faraja ya Roho
Mtakatifu sisi wanao tulio katika dhiki na taabu nyingi mno hapa
duniani.
W. Twakuomba utusikie.

3. Ulijalie Kanisa lako mapaji ya Roho wako Mtakatifu, liweze


ku- tekeleza vema utume wake wa kuwahudumia watu wote hapa
duni- ani.
W. Twakuomba utusikie.

4. Utujalie sisi tudumu katika NOVENA hii mpaka mwisho kama


Maria na Mitume walivyodumu pamoja wakisali kabla ya
Pentekoste ile ya kwanza.
W. Twakuomba utusikie.

5. Utujalie neema zote tunazohitaji tuweze kumshuhudia Kristu po-


pote kwa mwenendo na matendo yetu ya kila siku, tukiongozwa na
Roho Mtakatifu.
W. Twakuomba utusikie.

6. Uzijalie familia zote za wakristu neema na nguvu za Roho


Mtakati- fu tupate kuendelea pasipo kuchoka katika sala na katika
matendo mema siku zote.
W. Twakuomba utusikie.

7. Ewe Roho Mtakatifu, uwajalie vijana wetu moyo wa ujasiri,


wapate kulijenga Kanisa lako na kueneza Utawala wako katika
jumuiya zetu za kikristu.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Mt. Yohana Mtume - 46
Ee Mungu, uliye Mwumba wa vitu vyote, tunakuomba usikilize
kwa wema sala zetu sisi taifa lako, utuongoze sote tufuate siku zote
utarati- bu wa mapenzi yako; naye Roho Mtakatifu atutegemeze
mpaka mwisho wa NOVENA hii. Tunaomba hayo kwa njia ya
Kristo Bwana wetu.
W. Amina

SIKU YA PILI JUMAMOSI


ROHO MTAKATIFU ANATUSAIDIA KUENEZA INJILI

"Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho hawezi


kamwe kuingia katika Utawala wa Mungu (Yn 3.5)
Kanisa limepewa na Yesu ujumbe wa kuwaletea watu wote uzima
mpya, uzima wa Mungu. Yesu aliwaambia mitume wake:
"Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni, basi,
mkawafanye wa- tu wa makabila yote kuwa wafuasi wangu.
Wabatizeni kwa jina la Ba- ba na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.
Wafundishes kuyashika maa- gizo yote niliyowapeni. Nami nipo
pamoja nanyi siku zote; mpaka mwisho wa nyakati" (Mt 28: 18-20)
Sisi tuliobatizwa tumepata kuwa viungo vilivyo hai vya mwili wa
fum- bo wa Kristu; kwa Kipaimara tumeimarishwa na kuthibitishwa
na Roho Mtakatifu. Tumekuwa taifa teule; tumeshirikishwa ule
ukuhani wa Kristu; tumepokea ujumbe wa kueneza Utawala wa
Mungu.
Tunapopokea Sakramenti, na hasa ile Sakramenti ya Ekaristi,
tunali- sha Imani na kuongeza mapendo ambayo ni msingi wa
utume wowote ule. Mapendo yanatuhimiza kueneza Utawala wa
Mungu na kumpenda Yesu Kristu aliyekuja kuwakomboa
wanadamu wote.
Kila aliyebatizwa anao wajibu wa kueneza Imani ya Mungu na
Uta- wala wake. Kwa hiyo tumwombe Roho Mtakatifu atuwezeshe
kutimi- za wito huo.

Mt. Yohana Mtume - 47


1. Ee Baba wa mbinguni, tunakuomba umpeleke Roho Mtakatifu
aliangaze Kanisa na kuliongoza, liweze kuwafikishia mataifa yote
Ha- bari Njema ya wokovu.
W. Twakuomba utusikie.

2. Ee Yesu Mkombozi wetu, umtume Roho Mtakatifu awahimize


wakristu wapate kutimiza wajibu wao wa kueneza neno lako
popote du- niani.
W. Twakuomba utusikie.

3. Ewe Roho Mtakatifu Mfariji, uamshe katika mioyo ya vijana


wengi hamu ya kupenda kulitumikia Kanisa lako na kulihudumia
taifa lako kwa uaminifu.
W. Twakuomba utusikie.

4. Ewe Mwanga wa mataifa, uwajalie wanafunzi wasikie sauti


yako moyoni mwao, nawe unapowaita wasikose kuisikia sauti
yako, wawe tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya ndugu zao.
W. Twakuomba utusikie

5. Uwasaidie wazazi wawalelee vema watoto wao uwatie moyo


katika wito wao, wapate pia kuishiriki vema ile kazi ya kueneza
neno lako kwa jirani zao.
W. Twakuomba utusikie.

6. Ewe Roho Mtakatifu, uwasaidie wakristu wote kueneza Habari


Nje- ma ya wokovu, kwa sala, kwa sadaka na kwa mifano ya
maisha yao ya uchaji.
W. Twakuomba utusikie.

7. Ewe Mpaji wa mema, uwajalie waumini mapaji yako saba,


wasi- choke kulieneza neno lako kwa hekima pasipo hofu.
Mt. Yohana Mtume - 48
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Ee Mungu, unapenda watu wote waokoke, wafikie kweli yako. Tu-
nakuomba upeleke wafanya kazi walio wengi na wema katika
shamba lako. Uwajalie kulihubiri neno lako kwa imani kuu, ili neno
lako lienee na kupokelewa na mataifa yote, wapate nao kukujua
wewe peke yako Mungu wao, Mungu wa kweli. Tunaomba hayo
kwa nguvu ya Roho Mtakatifu anayeliongoza Kanisa lako sasa na
milele
W. Amina.

SIKU YA TATU JUMAPILI


ROHO MTAKATIFU ANATUFANYA KUWA MITUME

Bwana alisema kwa kinywa cha Nabii Yoeli: “Katika siku zile za
mwi- sho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho
wangu. Wa- toto wenu, waume kwa wake, watautangaza ujumbe
wangu; vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota
ndoto.... Hata wa- tumishi wenu watamiminiwa Roho wangu katika
siku zile, nao watau- tangaza ujumbe wangu" (Mdo. 2: 17-21)
Siku ile ya Pentekoste, baada ya Roho Mtakatifu kulishukia
Kanisa, Mtume Petro aliwakumbusha watu maneno hayo ya Nabii
Yoeli. Na miaka mingi baadaye. Petro aliwaandikia barua wakristu
wa kwanza, akiwaamba "Kila mmoja anapaswa kutumia kipaji
alichojaliwa na Mungu kwa faida ya wengine, kama vile wakili
mwema wa zawadi mbalimbali za Mungu. Anayesema kitu,
maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia
anapaswa kutumikia kwa nguvu aliyojaliwa na Mungu, ili katika
mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristu, ambaye
utukufu na nguvu ni vyake milele na milele"(1 Pet. 4: 10-11)
Mtaguso wa II wa Vatikano ulitukumbusha jambo hilohilo
ulipose- ma: "Roho Mtakatifu anayelitakasa taifa la Mungu kwa
Mt. Yohana Mtume - 49
njia ya Sakramenti amewapa waumini mapaji ya pekee na
kumjalia kila mmoja kadiri apendavyo. Kwa hiyo kila mmoja
amgawie mwenzake kadiri ya vipawa alivyopewa, awe mgawaji
mwaminifu wa neema ya Mungu, alijenge Kanisa zima katika
upendo."
Tunao wajibu wa kutumia vipawa tulivyojaliwa na Roho Mtakatifu
kwa manufaa ya Kanisa zima, na kwa faida ya watu wote.
Tuunganike sote pamoja na wachungaji wetu katika kazi hiyo ya
utume. Tum- wombe nasi Roho Mtakatifu atusaidie kutumia vema
vipawa vyake alivyotujalia katika kazi hiyo ya utume. Tumwombe
basi Roho Mta- katifu atusaidie kutumia vema vipawa vyake
alivyotujalia.

1. Ewe Roho Mtakatifu uwape wakristu neema na nguvu za kutumia


vema vipawa ulivyowajalia kwa ajili ya kulijenga Kanisa lako po
pote duniani, na kwa ajili ya wokovu wa watu wote.
W. Twakuomba utusikie.

2. Utujalie sisi sote mapaji yako saba, tupate kukutumikia kwa uchaji.
W. Twakuomba utusikie.

3. Utujalie tuwe mitume wa kweli wa wenzetu tushirikiane na wa-


chungaji wetu katika huduma za kuwaongoza watu wote na
kuwafiki- sha mbinguni.
W. Twakuomba utusikie.

4. Utujalie hekima na nguvu za kuwahudumia watu wote kwa


mapen- do ya kweli yasiyo na kinyume.
W. Twakuomba utusikie.

5. Utujalie neema ya kumpenda Mungu kwa moyo wote, na


ku- wapenda jirani zetu kama tunavyojipenda wenyewe.
W. Twakuomba utusikie.
Mt. Yohana Mtume - 50
6. Utupe neema za kulisikia neno lako na kulifuata, nayo
mawazo yetu na matendo yetu yafuate daima mwongozo wako
mtakatifu.
W. Twakuomba utusikie.

7. Uwazidishie mapaji yako wale wote wanaotumia vema vipawa


vyao, uwarudishe na wale wanaotumia vibaya rehema zako.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Ewe Roho wa Mungu, ndiwe unayewapa waumini vipawa vyako
kwa kadri unavyotaka. Utujalie tuyapokee na kuyatumia vema
mapaji yako mengi kwa ajili ya utukufu wa Jina lako, na kwa ajili
ya wokovu wa watu wote. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu
Bwana wetu.
W. Amina.

SIKU YA NNE JUMATATU


ROHO MTAKATAIFU ANALlUNGANISHA KANISA

"Atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza kwenye


ukweli wote."(Yn. 16:13)
Baada ya kusema hayo, Yesu aliinua macho yake kuelekea
mbinguni, akasema: "Mimi nimekutukuza hapa duniani;
nimeikamilisha ile kazi uliyonipa niifanye. Naomba ili wote wawe
kitu kimoja kusudi ulim- wengu upate kuamini kwamba wewe
ulinituma." (Yn.17:4,21)
Nasi tunamwomba Mungu Mwenyezi alijalie Kanisa lake umoja
wa kweli, awaunganishe wakristu wa madhehebu yote katika zizi
moja chini ya Mchungaji mmoja.
Popote duniani watu wengi, makundi kwa makundi wanavutwa na
neema hiyo ya kuungana na kuufikia umoja wa Kanisa. Hata ndugu
Mt. Yohana Mtume - 51
zetu waliotengana nasi wanazidi kukubali mwongozo wa Roho Mta-
katifu na kutaka kurudi katika nyumba ya Baba na kuwa kundi moja
chini ya Mchungaji mmoja. Isitoshe, hata sasa tena twaweza kuona
kwamba kwa namna fulani wamejiunga nasi katika Roho Mtakatifu;
naye Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kumshuhudia hata
kwa kumwaga damu yao.
Tena katika hao ndugu zetu waliojitenga, Roho Mtakatifu analisha
katika mioyo yao ile imani inayowaunganisha wafuasi wote wa
Kristu. Tumwombe basi mwenyezi Mungu atujalie hima huo umoja
wa Kani- sa lake tunaouania mno.

1. Ee Yesu, Bwana wetu, wewe umetuombea kwa Mungu Baba


tuwe kitu kimoja kama wewe ulivyo kitu kimoja na Baba. Utujalie
huo umoja, ili ulimwengu uone na kukiri kwamba ndiwe Bwana
na Mkombozi wa watu wote.
W. Twakuomba utusikie.

2. Ee Yesu, utujalie moyo wa kulishika neno lako kwa uaminifu,


wala usituache kufuata njia zetu sisi wenyewe na kufarakana.
W. Twakuomba utusikie.

3. Ee Yesu uliye mchungaji wetu mwema, ondoa ndani yetu ile


tabia ya utengano, tupate kuwa sote kundi moja chini yako wewe
uliye Mchungaji wetu mmoja.
W. Twakuomba utusikie.

4. Ee Yesu, uliye Mchungaji mkuu, uwajalie wachungaji wetu


wawe siku zote na upendo wa jina lako, wasichoke kulichunga
vema kundi lako hapa duniani na kuliweka pamoja lisitengane.
W. Twakuomba utusikie.

5. Ewe Roho Mtakatifu, uziangaze akili za watu wote, wapende


siku zote kuishi kwa amani, umoja na mapendano.
Mt. Yohana Mtume - 52
W. Twakuomba utusikie.

6. Ee Mungu, utufungulie mlango wa mwungano wako wa kweli


sisi tulio ndugu katika Bwana wetu Yesu Kristu.
W. Twakuomba utusikie.

7. Utujalie mapatano na amani, tudumu tumeungana katika familia


zetu, katika jimbo letu na katika nchi yetu yote.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Ee Mungu, utuunganishe sisi kondoo wako tuliotawanyika, tuwe
chi- ni ya Mwanao mpenzi, tupate sote kuushiriki ule utawala wako
wa kweli na haki, utawala wa neema na amani, utawala wa upendo
wako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.
W. Amina.

SIKU YA TANO JUMANNE


ROHO MTAKATIFU ANAWATAKASA WAUMINI

Walio wa Mungu hutafuta yaliyo ya Mungu, na wale walio wa


dunia hutafuta yaliyo ya dunia. Ni mauti kutosheka na mambo
yaliyo ya dunia. Uzima na faraja ya kweli hupatikana tu katika
mambo ya Mungu.
Kwa nguvu zetu sisi wenyewe hatuwezi kutenda lolote jema.
Kuweza kwetu kwatoka kwa Mungu, kwatoka kwa Yeye
anayetupa kujua, kupenda na kutenda.
Mtu anapotenda dhambi, hawezi kuongoka ila kwa msaada wa
Roho Mtakatifu, ndiye Yeye anayempa mkosefu neema ya
kutambua ubaya wa kosa lake na kuamua kuliacha. Ndiye
anayempa pia mkosefu kutambua uzuri wa neema aliyoipoteza na
kumrudishia neema hiyo. Ndiye anayempa nguvu za kudumisha
neema hiyo na kuiongeza.
Mt. Yohana Mtume - 53
Isitoshe, Roho Mtakatifu ndiye anayemwezesha mtu kuwa na
maendeleo katika fadhila na utakatifu. Ndiye anayemjalia imani
iliyo msingi wa maisha ya kikristu. Ndiye anayetujalia akili ya
kushika ma- fumbo ya Dini yetu na kuishi imani yetu mpaka kufa.
Lakini imani peke yake haimtoshi mtu aokoke. Imani pasipo maten-
do haifai kitu; "Imani bila matendo imekufa." (Yak. 2:26) Roho
Mta- katifu anamwezesha mtu kumwamini Mungu na kumpenda
kuliko vitu vyote na kumpenda jirani kama kujipenda mwenyewe.
Ndiyo maana Roho Mtakatifu huitwa chanzo cha matendo yetu yote
yaliyo mema. Basi tumwombe Roho Mtakatifu aitakase mioyo yetu
sisi wau- mini wake, atuzidishie imani, atuwezeshe kutenda
matendo yaliyojaa imani.

1. Ewe Roho Mtakatifu, utudumishie imani, uyatakase mawazo


ya mioyo yetu yafuate daima maongozi yako na amri zako.
W. Twakuomba utusikie.

2. Uzigeuze nia zetu zipate kumwelekea daima Mungu.

W. Twakuomba utusikie.
3. Utuwezeshe kuendelea katika utakatifu na kutenda mema
kwa imani siku zote za maisha yetu.
W. Twakuomba utusikie.

4. Utuzidishie imani, matumaini na mapendo, tuweze kushika


kwa moyo thabiti yale yote tunayofundishwa na Kanisa lako
takatifu.
W. Twakuomba utusikie.

5. Uiwashe mioyo yetu na moto wa mapendo yako, tupate


kumpenda Mungu kweli na kumpenda jirani yetu pasipo unafiki.
W. Twakuomba utusikie.

Mt. Yohana Mtume - 54


6. Utusaidie tuishi vema kwa imani na matumaini siku zote za
mai- sha yetu.
W. Twakuomba utusikie.

7. Utujalie kudumisha mioyoni mwetu ile neema ya utakaso


tuli- yoipata mwanzo katika Ubatizo wetu.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Ee Mungu, mbele yako mioyo yote iwazi; wewe wajua yote, wala
haku- na siri iliyofichika mbele yako. Uyatakase mawazo ya mioyo
yetu kwa kutupelekea Roho Mtakatifu, ili tuweze kukupenda na
kukutukuza kama unavyostahili. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu
Bwana wetu.
W. Amina.

SIKU YA SITA JUMATANO


ROHO MTAKATIFU ANATUPA NGUVU

Nitamwomba Baba, naye atawapelekea Mfariji mwingine


atakayekaa nanyi siku zote. Katika maisha yetu hapa duniani
tunahitaji mno kitulizo cha Mungu. Ni jambo la hekima kutafuta
kitulizo hicho kwa Mungu wala si kwa viumbe; maana kitulizo
kinachopatikana kwa vi- umbe hapa duniani hakidumu; bali kitulizo
kitokacho kwa Mungu ni cha kudumu.
Roho Mtakatifu ndiye kitulizo chetu cha kweli. Baba ndiye
aliyetuum- ba, Mwana ndiye aliyetukomboa, naye Roho Mtakatifu
ndiye anayeit- akasa mioyo yetu na kutufariji.
Kazi ya Roho Mtakatifu Mfariji siyo tu kuwatuliza wale walio na
huzuni, bali pia kuwapa moyo wa kuvumilia taabu zozote kwa
saburi. Tunahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili tuweze kuishi
maisha mema ya Kikristu. Katika juhudi zetu za kumtumikia
Mungu mara nyingi tunakutana na shida; naye Roho Mtakatifu
Mt. Yohana Mtume - 55
ndiye anayetufariji na kutupa nguvu za kupambana na matatizo
yote. Maisha yetu hapa du- niani yamejaa misalaba. Na misalaba
hiyo hatuwezi kuichukua kwa nguvu zetu wenyewe. Roho
Mtakatifu ndiye anayetupa moyo wa kuvumilia. Basi, tumwombe
aje kutufariji na kutupa nguvu za kuchukua msalaba wetu kwa
saburi kila siku.

1. Ee Yesu Bwana wetu, tunakusihi wewe na Baba mumtume Roho


Mtakatifu atufariji, awajalie kitulizo wale wote walio katika taabu
na majonzi.
W. Twakuomba utusikie

2. Ewe Roho Mtakatifu, uwafariji wale walio katika taabu za


namna zote, ili waweze kuvumilia kwa saburi mateso yao kwa
faida ya roho zao na roho za ndugu zao.
W. Twakuomba utusikie.

3. Uwafariji wale walio wagonjwa, uwajalie afya ya roho na mwili.


W. Twakuomba utusikie.

4. Uwasaidie yatima, wajane na wote walioachwa, wasikose


kupata siku kwa siku mahitaji yao ya lazima.
W. Twakuomba utusikie.

5. Uwajalie wale wote walio walegevu na wakosefu


neema ya kuongoka na kurejea hima katika amani ya
upendo wako.
W. Twakuomba utusikie.

6. Uwaimarishe wale walio wema, uwajalie neema ya kudumu wa-


silegee katika kutenda mema leo na kesho na siku zote za maisha
yao.
W. Twakuomba utusikie.
Mt. Yohana Mtume - 56
7. Utujalie nguvu za kutafuta na kudumisha amani ya kweli
katika mioyo yetu na kati ya ndugu zetu katika jumuiya zetu za
kikristu.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Ee Bwana Mungu wetu, tunakuomba neema ya Roho Mtakatifu itu-
angaze akili na mioyo yetu na kutujaza nguvu ya upendo wako.
Tuna- omba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.

W. Amina.

SIKU YA SABA ALHAMISI


ROHO MTAKATIFU ANATUPA HEKIMA

Hekima tunayopewa na Roho Mtakatifu si sawa kama hekima


inayo- patikana katika ulimwengu huu.
Hekima ya Roho Mtakatifu ni ile Mt. Paulo aliyowaambia Wako-
rintho, ya kuwa: "Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii
hawakui- elewa; maana kama wangaliielewa, hawangalimsulubisha
Bwana wa utukufu. Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko
matakatifu: 'Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona wala sikio
kuyasikia, mambo am- bayo binadamu hajapata kuyafikiria
moyoni, hayo ndiyo Mungu ali- yowatayarishia wale
wampendao"'(l Kor. 2:8-9).
Mtakatifu Paulo alisema: Kama vile Roho ya mtu ndiyo yenye
kufahamu na kutambua yaliyo ndani yake; hivyo pia Roho
Mtakatifu ndiye anayefahamu mambo ya Mungu na kutufumbulia
sisi mioyoni mwetu.
Katika sikukuu hii ya Pentekoste, tunatazamia kumpokea Roho
Mta- katifu. Yeye aliye hekima ya Mungu atatufumbulia siri za
Mungu na ukweli wake. Ndiye atakayeamsha ndani yetu mapendo
Mt. Yohana Mtume - 57
ya Yesu Msulubiwa, Mkombozi wetu. Ni yeye atakayetuongoza
kutenda mema na kuacha mabaya. Tunamhitaji sana Roho
Mtakatifu katika maisha yetu ya kila siku, atupe hekima ya
kuchagua na kutenda daima yaliyo mema. Katika Novena hii tuzidi
kumwomba Mungu atushushie Roho Mtakatifu, atujaze na hekima
yake.

1. Ee Mungu, uwabariki viongozi wa Dini na wasaidizi wao


wapate kutuongoza kwa hekima na mapendo.
W. Twakuomba utusikie.

2. Ewe Roho Mtakatifu, utujalie hekima ya kutambua mambo


ya Mungu na kuyatekeleza kwa uchaji.
W. Twakuomba utusikie.

3. Utujalie kuyajua mapenzi ya Mungu na kuyapokea kwa furaha.


W. Twakuomba utusikie.

4. Uamshe ndani yetu mapendo ya Yesu Msulubiwa, utuwezeshe


kutimiza vema wajibu wetu kama wafuasi wa kweli wa Kristu,
Bwana wetu.
W. Twakuomba utusikie.

5. Utuwezeshe kuchagua daima yaliyo mema na kuyatekeleza,


tupate kulijenga na kulidumisha Kanisa lako hapa duniani.
W. Twakuomba utusikie.

6. Utuepushe na mafundisho yo yote yaliyo na upotovu,


utujalie hekima ya kuzidi kutambua ukweli wako na
mafundisho yako yaletayo wokovu.
W. Twakuomba utusikie.

7. Hekima ya Roho Mtakatifu ituongoze katika safari ya maisha


Mt. Yohana Mtume - 58
yetu hapa duniani, tupate mwishowe kukurudia wewe Mwumba
wetu, uli- ye mwanzo wetu na mwisho wetu
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Ee Mungu, Baba wa utukufu, tunaomba utupe Roho wako wa
heki- ma, atuwezeshe kukufahamu vema, atuongoze tuishi maisha
yenye kukupendeza. Utusaidie kupambana na matatizo ya maisha,
tupate kuishi maisha mema hapa duniani na mwishowe tupate
tuzo la heri na furaha yako huko mbinguni. Tunaomba hayo kwa
njia ya Kristu Bwana wetu.

W. Amina.

SIKU YA NANE IJUMAA


ROHO MTAKATIFU ANATUPA MWANGA

Roho Mtakatifu anaangaza akili zetu tuweze kuona ukweli wa


Mungu na kuufuata. Bila Roho Mtakatifu akili zetu zimo katika
giza nene, wala hatuwezi kuona njia ya kutuelekeza kwa Mungu.
Mungu alipoumba ulimwengu, dunia ilikuwa giza tupu, haina kitu.
"Mungu alisema: Iwe nuru; ikawa nuru, Mungu akaiona nuru, ya
ku- wa ni njema". (Mwa. 1:3-4). Vivyo hivyo akili ya binadamu
bila nuru ya mwanga wa Roho Mtakatifu ni tupu, ina giza, haiwezi
kuona mam- bo yanayotuelekeza kwa Mungu. Tukiwa na nuru ya
Roho Mtakatifu tunauona ukweli wa Mungu jinsi ulivyo.
Roho Mtakatifu anapoijia roho ya mtu, anaiangaza akili yake iweze
kuona mambo yanayofaa kwa wokovu. Naye akiisha kuiangazia
akili ya mtu, huimarisha utashi wake na kumwezesha kuchagua
daima yali- yo mema.
Roho Mtakatifu huiangazia akili iweze kuona ukweli. Kabla ya
Ku- waaga Mitume, Yesu aliwaambia kuwa atawapelekea Mfariji
mwingine atakayekaa nao siku zote, Roho wa ukweli ambaye
Mt. Yohana Mtume - 59
dunia haiwezi kumpokea kwa sababu hawakumfahamu, lakini wao
Mitume watamfahamu kwa maana atakaa nao siku zote. Yesu
ametuahidi pia sisi Roho huyo akae nasi.
Leo hivi duniani kuna uongo na udanganyifu mwingi: kuna dhu-
luma, vita, na maovu ya kila namna. Hii ni kwa sababu dunia
haijam- tambua bado Roho Mtakatifu na kumpokea, yeye aliye
mwanga wa dunia na asili ya kweli yote.
Mtaguso wa II wa Vatikano watuambia ya kuwa Roho Mtakatifu
anakaa katika Kanisa na katika mioyo ya waumini kama katika
heka- lu. Roho analiongoza Kanisa na kulifanya liwe na umoja;
analipamba na mapaji yake mbalimbali.Tumwombe Mungu Baba
ampeleke huyo Roho Mtakatifu katika Kanisa lake aliongoe na
kulilinda lisipate kutengana, bali alisaidie kueneza Utawala wa
Mungu po pote duni- ani.

1. Ewe Roho Mtakatifu, utujalie kuona mwanga wa kweli yako


na kuifuata.
W. Twakuomba utusikie.

2. Uwape waregevu neema ya kuirudia tena njia ya kweli yako.


W. Twakuomba utusikie.

3. Utuwezeshe sisi sote waumini wako tutembee siku zote katika


nuru ya kweli yako na sheria zako.
W. Twakuomba utusikie.

4. Utuangazie akili ya mioyo yetu tuchague daima yale


yanayokupen- deza.
W. Twakuomba utusikie.

5. Uwape mwanga wako viongozi wetu wa Dini na Serikali,


wapate kutuongoza kwa hekima na uchaji, wasisahau kamwe
kwamba uwezo walio nao unatoka kwa Mungu.
Mt. Yohana Mtume - 60
W. Twakuomba utusikie.

6. Utupe mwanga wako tuwaone watu wote kama ndugu zetu,


tuishi kidugu na kusaidiana kidugu.
W. Twakuomba utusikie.

7. Ewe Roho Mtakatifu, ndiwe mpatanishi wa mioyo: tunakuomba


uondoe udhalimu, uonevu, udanganyifu na maovu yote katika
mioyo ya watu wote.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Ee Yesu Bwana wetu, uliyesema: Pasipo mimi hamwezi kitu;
umpeleke Roho Mtakatifu atuangaze akili zetu, tupate kufahamu
mapenzi yako na kuyatimiza kwa imani na uchaji. Roho
Mtakatifu atuongoze katika mambo yote, yeye anayeishi na
kutawala nawe pamoja na Baba, daima na milele.
W. Amina.

SIKU YA TISA JUMAMOSI


ROHO MTAKATIFU ANATUPA MAPENDO

Maandiko Matakatifu yanatuambia ya kuwa, Roho Mtakatifu,


Nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, ndiye upendo katika Baba na
Mwana.
Upendo hujieneza. Naye Roho Mtakatifu aliye pendo lenyewe la
Mungu, hupenda kujieneza na kujishirikisha nasi, na kuwasha
ndani yetu moto wa mapendo yake.
Roho Mtakatifu ndiye mwenye kutakatifuza roho zetu kwa neema
ya utakaso. Neema hiyo ni uzima wa Mungu, ndio huo upendo wa
Mun- gu tunaoshirikishwa. Roho isiyo na neema ya utakaso
imetengana na Mungu, haina uzima wake, haina upendo wake; kwa
hiyo haiwezi pia kuwa na mapendo ya kweli ya jirani.
Mt. Yohana Mtume - 61
Ingawa tunaona ishara nyingi za watu kupendana kidugu hapa
duni- ani, mapendo hayo si mapendo ya kweli wala si kamili kama
haya- tokani na neema ya utakaso rohoni mwa mtu. Kama hakuna
neema ya utakaso ndani yetu, Mungu pia hayupo kati yetu.
Roho Mtakatifu anatuunganisha na Mungu katika upendo. Pasipo na
mapendo hapana mapatano, hapana masikilizano wala mwungano.
Watu wanaopendana wanaungana na kulingana katika fikra zao na
nia zao. Roho Mtakatifu anayetutia mapendo rohoni na kutuwashia
moto wa mapendo, ndiye anayetuwezesha kuwa na mawazo ya
namna moja na nia moja.
Watu wanaopendana hupenda kukaa pamoja, kuishi pamoja na ku-
saidiana. Roho Mtakatifu aliye chanzo cha mapendo ya kweli
hutuwe- ka pamoja katika Kanisa lake.
Hukaa ndani yetu, hukaa katika Kanisa na kuwasha moto wa mapen-
do yake ndani yetu. Roho Mtakatifu anatuwezesha kukaa kwa amani
nyumbani, kazini na katika jumuiya zetu. Basi, tumwombe sasa
Roho Mtakatifu atuongezee hayo mapendo yake ndani yetu
1. Ewe Roho Mtakatifu, uwashe mioyoni mwetu moto wa mapendo
yako, tupate kuwapenda jirani zetu kama tunavyotaka kupendwa
nao
W. Twakuomba utusikie.

2. Udumishe ndani yetu neema hiyo ya mapendo yako, tuweze


kuishi kwa amani leo na siku zote za maisha yetu.
W. Twakuomba utusikie.

3. Utujalie neema na nguvu za kutekeleza mema yote


tunayokusudia kuyatenda siku hii ya leo.
W. Twakuomba utusikie.

4. Uongoze nia zetu na maazimio yetu, yalingane na juhudi zetu


za kutaka ku1eta mafanikio ya roho na mwili kati yetu.
W. Twakuomba utusikie.
Mt. Yohana Mtume - 62
5. Utubariki, ili baada ya maombi haya, tuwe na juhudi ya
kutimiza vema zaidi wajibu wetu wa kikristu kwa moyo mkuu.
W. Twakuomba utusikie.

6. Utuwezeshe kueneza mapendo na amani kati yetu na katika


ju- muia zetu za kikristu.
W. Twakuomba utusikie.

7. Utuwezeshe kuwa kweli chachu ya wema na mapendano kati


ya watu, ili nao wapate rehema zako kwa maombezi yetu.
W. Twakuomba utusikie.

TUOMBE
Ee Mungu, tunakushukuru kwa neema ulizotujalia, hata tukaweza
kuifanya ibada hii ya Novena takatifu mpaka mwisho. Utujalie
mema yote tuliyoomba; utusaidie kutekeleza yote yale
tuliyokusudia kuten- da. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana
wetu.
W. Amina.

Mt. Yohana Mtume - 63


NOVENA KWA HURUMA YA MUNGU

SIKU YA KWANZA

Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina:


"Uniletee leo wanadamu wote, hasa wakosefu wote na
uwazamishe katika bahari ya Huruma yangu; hivyo
utanifariji katika huzuni yangu kali inayosababishwa na
upotofu wa roho za wanadamu".

SALA:
Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, unayetuonea huruma
na kutusamehe, usizitazame dhambi zetu ila tu matu-
maini tuliyo nayo katika wema wako usio na mipaka;
utupokee sisi sote katika makao ya Moyo wako wenye
huruma na usituache kamwe. Tunakusihi kwa njia ya
upendo wako unaokuunganisha na Baba na Roho Mta-
katifu.

Baba wa milele, uwatazame kwa jicho la Huruma yako


wanadamu wote, hasa wakosefu waliofungwa katika
Moyo wa Yesu wenye huruma na kwa ajili ya mateso
yake makali utuonee huruma, tuweze kuusifu daima
ukuu wa Huruma yako milele yote. Amina.

SIKU YA PILI

Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina:


"Uniletee leo roho za mapadre na watawa na uzizamishe
katika Huruma yangu isiyo na kipimo. Roho zao zilini-
patia nguvu ya kustahimili mateso makali; kwa njia yao
kama kwa mifereji Huruma yangu humwagwa juu ya
Mt. Yohana Mtume - 64
wanadamu wote".

SALA:
Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, uliye asili ya mema
yote, tuongezee neema ya kutenda matendo ya huruma
ili wote wanaotutazama, wamtukuze Baba wa Huruma
aliye juu mbinguni.

Baba wa milele, ulitazame kwa jicho la Huruma yako


kundi la wateule wako katika shamba lako la mizabibu
roho za mapadre na watawa na uzijalie nguvu za baraka
zako, na kwa ajili ya hisia za Moyo wa Mwanao zilimo-
fungwa, uzijalie nguvu na mwanga wako ziweze ku-
waongoza wengine katika njia za wokovu na hatimaye
kuitukuza Huruma yako milele yote. Amina.

SIKU YA TATU

Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina:


"Uniletee leo roho zote chaji na aminifu na kuzizamisha
katika bahari ya Huruma yangu; roho hizo zilinifariji
katika Njia ya Msalaba, zilikuwa kwangu kama tone la
asali katika bahari ya Uchungu".

SALA:
Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, unayewajalia wote
neema zako tele kutoka katika hazina ya Huruma yako,
utupokee sisi katika makao ya Moyo wako wenye Hu-
ruma na usituache kamwe. Tunakusihi kwa njia ya up-
endo wako wa ajabu ulio nao kwa Baba wa milele.

Baba wa milele, uzitazame kwa jicho la Huruma roho


Mt. Yohana Mtume - 65
aminifu kama urithi wa Mwanao na kwa ajili ya mateso
yake makali, uzibariki na kuzilinda daima zisipoteze up-
endo na thawabu ya imani takatifu, bali pamoja na
umati wa Malaika na Watakatifu wote ziitukuze Huruma
yako isiyo na mwisho milele yote. Amina.

SIKU YA NNE
Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina:
"Uniletee leo wapagani na wote wasionijua bado. Hata
wao niliwafikiria katika mateso yangu makali na bidii
yao ijayo iliufariji Moyo wangu. Uwazamishe katika ba-
hari ya Huruma yangu".

SALA:
Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, uliye nuru ya ulimwen-
gu mzima, uzipokee kwenye makao ya Moyo wako
wenye Huruma roho za wapagani zisizokujua bado; mi-
ali ya neema zako iziangaze ili nazo pamoja nasi
ziitukuze Huruma yako ya ajabu na Wewe mwenyewe
usiziache kamwe.

Baba wa milele, uzitazame kwa jicho la huruma roho za


wapagani na za wote wasiokujua bado, zilizofungwa
katika Moyo wa Yesu wenye Huruma. Uwavute kwenye
nuru ya Injili . Roho hizi hazijui ni heri gani ilivyo ku-
kupenda Wewe. Uzijalie ziitukuze Huruma yako milele
yote. Amina.

SIKU YA TANO

Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina:

Mt. Yohana Mtume - 66


"Uniletee leo roho za waumini wa madhehebu mengine
ma uzizamishe kwenye bahari ya Huruma yangu. Katika
mateso yangu makali walirarua Mwili na Moyo wangu,
yaani Kanisa langu. Wanaporudi kwenye umoja kamili
na Kanisa, majeraha yangu hupona na hivyo wananifari-
ji katika mateso".

SALA:
Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, uliye wema kamili,
Wewe hukatai kuwajalia wakuombao mwanga wako; uz-
ipokee kwenye Makao ya Moyo wako wenye Huruma
roho za ndugu zetu wa madhehebu mengine na uzivute
katika mwanga wako ili ziwe na umoja na Kanisa;
usiziache kamwe, bali uzijalie neema ya kuuabudu
ukarimu wa Huruma yako.

Baba wa milele, uzitazame kwa jicho la Huruma roho za


ndugu zetu wa madhehebu mengine, hasa zile
zilizopoteza talanta zako na kuzitumia vibaya neema za-
ko zikidumu katika makosa yao kwa ukaidi. Usiya-
kumbuke makosa hayo, bali tu upendo wa Mwanao na
mateso yake makali aliyoteswa kwa ajili yao, kwa saba-
bu roho hizo nazo zimefungwa katika Moyo wa Yesu
wenye Huruma. Uzijalie nazo pia ziitukuze Huruma yako
kuu milele yote. Amina

SIKU YA SITA

Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina.


" Uniletee leo roho za waumini wapole na
wanyenyekevu na roho za watoto wadogo na uzi-

Mt. Yohana Mtume - 67


zamishe katika Huruma yangu. Roho hizi zinafanana sa-
na na Moyo wangu; zilinifariji katika mateso yangu ma-
kali. Niliziona kama Malaika wa hapa duniani ambao wa-
takaa daima madhabahuni. Ninazijalia mito ya neema.
Roho nyenyekevu tu ndiyo iwezayo kupokea neema
yangu; tumaini langu li kwa roho nyenyekevu".

SALA:
Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, uliyesema: "Jifunzeni
kwangu, kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa
Moyo", uzipokee roho pole na nyenyekevu pamoja na za
watoto wadogo katika makao ya Moyo wako wa Hu-
ruma. Roho hizi zinastaajabisha mbingu zote na
kumpendeza Baba wa mbinguni kwa namna ya pekee;
ndizo shada yenye harufu tamu iliyopo mbele ya kiti cha
enzi cha Mungu; harufu ambayo yampendeza Baba.
Roho hizi zina makao ya milele Moyoni mwako na daima
zinaimba wimbo wa upendo na Huruma. Baba wa
milele, uzitazame kwa jicho la Huruma roho pole na
nyenyekevy na za watoto wadogo, zilizofungwa katika
makao ya Moyo wa Yesu wenye Huruma. Roho hizi
zafanana sana na Mwanao; harufu tamu ya roho hizo
inapaa kutoka dunia hii na kukifikia kiti chako cha enzi.
Ee Baba wa Huruma na wa Wema wote, ninakusihi kwa
njia ya upendo na upendeleo wako kwa roho hizo,
uibarikie dunia yote ili roho zote ziimbe kwa pamoja sifa
za Huruma yako milele yote. Amina.

SIKU YA SABA

Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina:

Mt. Yohana Mtume - 68


"Leo uniletee roho zinazoabudu na kutukuza kwa namna
ya pekee Huruma yangu na uzizamishe katika Huruma
yangu. Roho hizi ndizo zilizoombolezea mateso yangu
na kuyaelewa vizuri zaidi. Roho hizo ni picha halisi ya
Moyo wangu wenye Huruma. Zitang'aa katika Utukufu
ujao kwa mwangaza wa pekee. Hata moja haitaingia
motoni. Nitakuwa nikiitetea roho hiyo saa ya kufa
kwake".

SALA:
Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, ambaye Moyo wako ni
upendo kamili, uzipokee kwenye makao ya Moyo wako
wenye Huruma roho ziabuduzo na kutukuza kwa namna
ya pekee ukuu wa Huruma yako. Nguvu yao ni nguvu
ya Mungu mwenyewe, katika masumbuko na magumu
zinasonga mbele zikiitumainia Huruma yako. Roho hizo
zimeungana na Yesu na kuubeba ulimwengu mzima ma-
begani mwao. Roho hizo hazitahukumiwa vikali, bali Hu-
ruma yako itazilinda saa ya kufa kwako.

Baba wa milele, uzitazame kwa jicho la Huruma roho


ambazo zinatukuza na kuabudu sifa yako kubwa kuzidi
zote, yaani Huruma yako isiyo na mipaka; roho ambazo
zimefungwa katika Moyo wenye Huruma wa Mwanao
Yesu. Roho hizo ni Injili hai, mikono yao imejaa maten-
do ya huruma na mioyo yao iliyofurika furaha
inamwim- bia Yule aliye juu, wimbo wa hururna.
Ninakusihi, ee Mungu, uzionee Hururna yako kwa ajili
ya rnatumaini ziliyokuwa nayo. Ahadi ya Yesu itimie juu
yao, aliyese- ma kuwa roho zitakazoabudu Hururna
yake isiyo na mwisho atazitetea katika uzima huu na
Mt. Yohana Mtume - 69
hasa katika saa ya kufa kwao kama Utukufu wake.
Amina.

SIKU YA NANE
Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina:
"Leo uniletee roho zilizomo Toharani na kuzizamisha
katika Shimo la Huruma yangu; mito ya Damu yangu
ipoze joto lao. Nazipenda sana roho hizo zote. Zinalipia
fidia kwa Haki yangu. Wewe una uwezo wa kuziletea
unafuu. Tumia rehema zote za Kanisa langu na kuzitoa
kwa ajili yao. Laiti ungejua mateso yao, ungekuwa un-
atoa fidia ya dhambi zao na kulipa madeni yao kwa Haki
ya Mungu".

SALA:
Ee Yesu mwenye Hururna nyingi, uliyesema mwenyewe
kuwa wataka huruma; basi, naingiza kwenye makao ya
Moyo wako wa Huruma roho zilizomo Toharani, zi-
nazokupendeza, ambazo lazima kwanza zitoe fidia kwa
Haki yako. Mito ya Damu na Maji vilivyomwagika kutoka
moyoni mwako viuzimishe moto wa Toharani ili napo pia
Huruma yako itukuzwe.

Baba wa milele, uzitazame kwa jicho la Huruma roho


zinazoteseka Toharani na zilizofungwa katika Moyo wa
Yesu wenye Huruma. Nakusihi kwa njia ya mateso ma-
kali ya Yesu Mwanao na kwa njia ya uchungu ambao
Roho yake Takatifu iliuonja, uzionee huruma roho
zilizochini ya jicho lako la haki. Uzitazame roho hizo
kupitia kwa Majeraha Matakatifu ya Yesu Mwanao
mpendwa, kwani twasadiki kuwa wema wako na
Mt. Yohana Mtume - 70
rehema zako hav- ina idadi. Amina.

SIKU YA TISA

Maneno ya Yesu kwa Sista Faustina:


"Leo uniletee roho baridi na uzizamishe katika Shimo la
Huruma yangu. Roho hizi zaumiza sana Moyo wangu.
Nimechukizwa nazo zaidi kuliko mateso yangu yote hu-
ko Gethsemani. Roho hizi zilikuwa sababu ya kusema:
'Baba, kama wapenda, ukiondoe kwangu kikombe hiki
cha mateso; hata hivyo mapenzi yako yatimizwe na si
yangu'. Kwazo msaada wa mwisho ndio kuikimbilia Hu-
ruma yangu".

SALA:
Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, uliye wema kamili,
naingiza katika makao ya Moyo wako wenye Huruma
roho baridi zipate kuota moto wa mapendo yako safi;
roho hizi zinazofanana na maiti na kukuchukiza Wewe.
Ee Yesu mwenye Huruma, tumia ukuu wa Huruma yako
uzivute roho hizo na kuziweka katikati ya moto wa
mapendo yako, uzijalie upendo mtakatifu kwani Wewe
waweza yote.

Baba wa milele, uzitazame kwa jicho la Huruma roho


baridi zilizofungwa Moyoni mwa Yesu. Ee Baba wa Hu-
ruma, nakusihi kwa ajili ya mateso makali ya Mwanao,
hasa kwa ajili ya masaa matatu ya kufa kwake msal-
abani, uziruhusu roho hizo pia ziutukuze Ukuu wa Hu-
ruma yako. Amina.

Mt. Yohana Mtume - 71


LITANIA YA HURUMA YA MUNGU
Huruma ya Mungu, iliyomwagika kutoka kifuani mwa
Baba, nakutumainia.
Huruma ya Mungu, fadhila kuu kuliko zote alizonazo
Mungu, nakutumainia
Huruma ya Mungu, fumbo lisiloweza kueleweka, .. .
Huruma ya Mungu, chemchemi inayomwagika kutoka
fumbo la Utatu Mtakatifu, ...
Huruma ya Mungu, isiyopimika kwa waelevu
wote,binadamu na malaika, .. .
Huruma ya Mungu, utokamo uzima na furaha, .. .
Huruma ya Mungu, iliyo bora kuliko mbingu, ..
Huruma ya Mungu, chimbuko la Miujiza na Maajabu, ...
Huruma ya Mungu, iuzungukao ulimwengu wote, ...
Huruma ya Mungu, ishukayo duniani katika nafsi ya Ne-
no aliyejifanya mtu, ...
Huruma ya Mungu, iliyotiririka kutoka katika kidonda
wazi Moyoni mwa Yesu, ...
Huruma ya Mungu, iliyofungiwa Moyoni mwa Yesu kwa
ajili yetu, hasa wadhambi, ...
Huruma ya Mungu, isiyopimika katika Hostia Takatifu, ..
Huruma ya Mungu, katika kuanzisha Kanisa Takatifu, ..
Huruma ya Mungu, katika Sakramenti ya Ubatizo, ...
Huruma ya Mungu, katika kutufanya wenye haki kwa
njia ya Yesu Kristu, ...
Huruma ya Mungu, iambatanayo nasi katika maisha
yetu yote, ...
Huruma ya Mungu, itukumbatiayo hasa katika saa ya
kufa, ...
Mt. Yohana Mtume - 72
Huruma ya Mungu, itujaliayo maisha ya milele yasiyo na
kifo, ...
Huruma ya Mungu, ifuatanayo nasi kila nukta ya maisha
yetu, ...
Huruma ya Mungu, itukingayo na moto wa milele, ...
Huruma ya Mungu, iongoayo wakosefu wenye shingo
ngumu, ...
Huruma ya Mungu. Mshangao wa Malaika, isiyofahamika
kwa Watakatifu, ...
Huruma ya Mungu, isiyopimika katika mafumbo yote ya
Mungu, …
Huruma ya Mungu, ituondoayo kwenye dhiki na
umaskini wote, ...
Huruma ya Mungu, chimbuko la furaha, .. .
Huruma ya Mungu, iliyotusuluhisha sisi, .. .
Huruma ya Mungu, ikumbatiayo matendo na kazi zote
za mikono yake, ...
Huruma ya Mungu, iliyo taji ya kazi zote za Mungu, ...
Huruma ya Mungu, ambamo sote tunazamishwa, ...
Huruma ya Mungu, nafuu bora kwa mioyo yenye
huzuni, ...
Huruma ya Mungu, tumaini la pekee kwa roho zinazoka-
ta tamaa, ...
Huruma ya Mungu, pumziko la mioyo, amani kati ya
woga, ...
Huruma ya Mungu, furaha kuu ya roho zote, ...
Huruma ya Mungu, itiayo matumaini ya kweli, ...

Mungu wa milele, ambaye ndani mwako Huruma


Mt. Yohana Mtume - 73
haina mwisho, hazina za Huruma hazikauki, utu-
angalie kwa wema na utuongezee Huruma yako,
ili tusikate tama wakati tunapopata magumu
maishani, bali tujinyenyekeze kwa imani na, ma-
tumaini na kujiweka chini ya mapenzi yako am-
bayo ni MAPENDO na HURUMA yenyewe. Amina!

Mt. Yohana Mtume - 74


IBADA YA MAOMBOLEZO
Kufungua
Wimbo – Ninakulilia katika unyonge wangu – Na 61
Rozali & litania ya huruma ya Mungu
Wimbo – Kesheni kila wakati – Na. 62
Somo – Lk 12: 16-21 Au 1Thes 4:13-17
Sala: Ee Mungu, unayeshika maisha ya kila mtu katika
mikono yako mitakatifu, na kumwekea kila mmoja
hesabu ya siku zake kwa kadri ulivyonuia, uitazame sa-
la ya kanisa lako. Kwa ajili ya mapendo ya Kristo uis-
amehe ruoho ya mtumishi wako uliyemwamuru ahame
dunia hii. Usitazame makosa na dhambi zake, bali kwa
huruma yako umpeleke kwenye furaha ya uzima wa
milele. Kwa ajili ya Kristu Bwana wetu. Amina
Wimbo – Tumaini letu ni kwa Bwana - Na. 63
Rozali matendo ya uchungu &Litania ya Moyo mt.
Yesu
Wimbo: Huo ndio ni mwanzo - Na.65
Somo: Ayubu 14:1-6 Au Yn. 11:21-27 Au Mat 24:42-51
Wimbo: Simama imara - Na. 66
Sala: Ee Mungu mwenyezi wa milele, umemuita mtumishi
wako Jina ….., atoke hapa duniani na kuja kwako. Basi
twakuomba, uitimize kazi ya neema yako uliyomtakasa
na mumkamilisha mapema. Uiokoe roho yake katika
Mt. Yohana Mtume - 75
kila kosa na adhabu. Kwa ajili ya mapendo ya Kristu
umjalie sadaka ya maisha ya maisha yake duniani impa-
tie furaha ya uzima wa milele. Kwa Kristu Bwana wetu
Wimbo: Watumishi wake baba/Bikira Maria
Somo: Ufunuo 20: 11-21:2 Au Yn. 6:37-40 Au Mat. 25:1-
13
Sala: Ee Bwana usikie sala zetu sisi tunakuomba huruma
yako, ili roho ya mtumishi wako Jina……… uli-
oihamisha hapa duniani. ikae katika amani na mwanga
pamoja na watakatifu wako.
Ee Baba wa rehema na Mungu wa faraja, wewe unatupen-
da kwa mapendo ya milele unageuza kivuli cha mauti
kuwa mwanzo wa nuru ya uzima.
Tunakuomba uwatazame hawa watumishi wako wanaoom-
boleza Ee Bwana uwe kimbilio na nguvu yetu tuinue
kutoka giza na majonzi ya msiba huu mpaka kwenye
nuru ya amani ya kukuona wewe.
Na kwa kuwa Mwanao Bwana wetu ameharibu kifo chetu
kwa kufa kwake na kuturudishia uzima kwa kufufuka
kwake, tunaomba utujalie tumkimbilie hivi kusudi
baada ya safari ya uzima huu wa duniani tuwekwe siku
moja pamoja na ndugu yetu; mahali ambapo machozi
yote yatafutwa.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
Wimbo – Bwana ndiye mchungaji wangu – Na. 64
Kumaliza

Mt. Yohana Mtume - 76


Mt. Yohana Mtume - 77
NYIMBO KWA NAFASI MBALIMBALI
NYIMBO ZA MISA
1. NITAJONGEA ALTARE YAKO

Kiit:
Nitajongea Altare yako,
Furaha yangu na heri yangu siku zote.

1. Ee Mungu, nirudishie haki yangu,


Niponye na waovu wangu waniangaisha,
Wewe Mungu, mbona wanitupa
2. Peleka mwanga wako na uaminifu wako,
Viniongoze, vinipeleke kwako,
Katika hekalu zako takatifu.
3. Nami nitajongea Altare ya Mungu,
Mungu wa furaha yangu, nami nitakusifu,
Moyo wangu kwani wasikitika.

2. NAYATAMANI MAKAO YA BWANA

Kiit:
Nayatamani, nayatamani makao ya Bwana x2
maskani yake Bwana yapendeza kama nini. x2

1. Nafsi yangu, inazionea shauku nyua za Bwana.


2. Nitaingia nyumbani mwa Bwana, kwa shangwe
nikamwabudu.
3. Heri yetu, kumwabudu Bwana, tukazipate neema
Mt. Yohana Mtume - 78
3. NIMEINGIA HAPA MAHALI PATAKATIFU

Kiit:
Nimeingia (hapa) hapa mahali patakatifu. Unipokee
(kwako) unitakase nipate neema. x2

1. Nimeingia kwako nimeingia, hapa mahali patakatifu.


2. Ee Bwana mwema wewe mfadhili sana, nakuja kwako
kukutukuza.
3. Nakuabudu pia nakusujudu, nisaidie mimi ni wako.
4. Mimi Mkristo pokea sala zangu, ninakuomba unisikie

4. KWA NYIMBO ZA SHANGWE

Kiit:
Kwa nyimbo za shangwe: Twendeni wote, twendeni wote,
tumwabudu Bwana. Kwa furaha. Twendeni wote, twendeni
wote, tumwabudu Bwana.

1. Ndiye muumba wetu na vitu vyote ni vyake.


2. Ulimwengu wote mali yake twatambua.
3. Ni wajibu wetu kumwabudu ni hakika.
4. Mbele ya miungu tumsujudu muumba wetu.
5. Sifa na uwezo vyatoka kwake jamani.
6. Atukuzwe Bwana muumba wa yote milele

5. TWENDENI KWA BWANA TUPELEKENI:

Kiit: Twendeni kwa Bwana tupelekeni x2


Twendeni twendeni (twendeni kwa bwana
Mt. Yohana Mtume - 79
Tupelekeni vipaji vyetu tukampe bwana) x2

1. Sadaka yetu twaileta mikononi mwa Bwana


(Uibariki aa ikupendeze ee Bwana Mungu) x2

2. Mazao yetu twayaleta mikononi mwa Bwana


(Uyabariki na yakupendeze ee Bwana Mungu) x2

3. Na fedha zetu twazileta mikononi mwa Bwana


(Uzibariki ah zikupendeze ee Bwana Mungu) x2

4. Vipaji vyetu twavileta mikononi mwa Bwana


(Uvibariki na uvipokee ee Bwana Mungu) x2

6. KIKONDOO CHA MUNGU

Kiit:
Kikondoo cha Mungu, Mkate wa mbinguni,
Mlishi wa roho yangu, Nakuabudu

1. U Baba yangu mwema, na


msimamizi, Mpaji wa uzima, wangu
moyoni,
2. Ee Rabi mtu Mungu, uniridhishe,
Njoo shuka kwangu,
kanishibishe
3. Anakaribia, mpenzi naamini,
Hata kaingia, mwangu
moyoni.

7. KWELI MWISHO UWE UWINGU

Kiit:
Mt. Yohana Mtume - 80
Kweli, kweli, wisho uwe uwingu x 2

1. Mwisho uwe uwingu, neno la


kushangaza, Nataka kuliwaza, lina sharti
kwangu.
2. Mwisho uwe uwingu, mazito
yakijaa, Usikate tamaa, fahamu kwa
Mungu.
3. Mwisho uwe uwingu, ujitoe sadaka,
Mapenzi hukushika, wajitoa
sadaka.
4. Mwisho uwe uwingu, ukatukanwa bure,
Wavumilia pote, mzuia uchungu.
5. Mwisho uwe uwingu, ukakosa hakiyo,
Wana nguvu we siyo, mkumbuke Mungu.
6. Mwisho uwe uwingu, una magonjwa muno,
Dawa haifai neno, baya lako fungu.

8. EE BWANA TWAKUOMBA

Kiit:
Ee Bwana twakuomba upokee vipaji vyetu (x2),
Hivyo vyote ni mali yako,
Tumepata kwa wema wako pokea. (x2)

1. Mkate divai twakutolea, Twakuomba Baba upokee.


2. Mazao ya shamba twakutolea, Twakuomba Baba upokee
3. Nayo sadaka twakutolea, Twakuomba Baba upokee.

9. ROHO YANGU YESU INAKUTAMANI

Kiit:
Mt. Yohana Mtume - 81
Roho yangu Yesu inakutamani,
Njoo kwangu Yesu unipe heri (x2).

1. Njoo kwangu Yesu nakungojea, kwani wewe u rafiki


mkuu.
2. Na uzidi Yesu kuwa nami, unipe mkate wa uzima.
3. Maumbo ya mkate na divai, umo ndani
kweli nasadiki.

10. BWANA YESU ANATUITA

Kiit: Bw ana yesu anatuita kw enye karamu yake Karamu


ya upendo na uzima milele
Bwana yesu anatuita kwenye yake karamu ya
Uzima na tumaini
Jema (karamu} yenye heri isiyo na gharama
Na isiyo na ubaguzi kwa uzima wetu sisi kwa
Nini tusiende wote kwa bwana tushiriki naye.
1. Ni mapendo gani tutayo wanadamu
Mapendo ya Bwana Mungu kwetu hayana kikomo.

2. Ni chakula gani tena na kinywaji wanachotaka '


Karamu ya Bwana Yesu mtu na imekamilika.

3. Ni fadhili gani tena tunaomba kwake Mungu


Alimtwaa mwanae akomboe ulimwengu.

11. HIVI NDIVYO WOTE WENYE KUMCHA BWANA

Kiit:
Hivi ndivyo wote wenye kumcha Bwana
watakavyobarikiwa naye x2.
Mt. Yohana Mtume - 82
1. Amchaye Bwana atastawi; kama mwerezi wa
Lebanoni.
2. Heri yule amchaye Bwana, na kupendezwa na amri
zake.
3. Wazao wake watakuwa hodari, kizazi cha waadilifu
kitabarikiwa.

12. NIKUPE NINI MUNGU WANGU

Kiit:
Nikupe nini Mungu wangu,
Nikupe nini we Mwokozi,
Nikupe nini Bwana wangu cha kukupendeza (x2)

1. Nakutolea mkate toka mmea wa ngano,


Nakutolea divai ni tunda na mzabibu,
Ninakuomba mwokozi nifanyie msamaha na
unipokee,
Mema unayoyatenda nitafanya nini mimi nikurudish-
ie.
2. Nikiwa katika shida, wewe unaniongoza
Nikiwa katika raha, wewe wanisimamia,
Na nikiwa safarini, waniepusha ajali,
Ninakuomba mwokozi, nifanyie msamaha na
unipokee,
Mema unayoyatenda nitafanya nini mimi nikurudish-
ie.

3. Kila nitakachotoa naona kidogo,Mema


unayotenda kwangu, mimi naogopa,
Mt. Yohana Mtume - 83
Ninakuomba Mwokozi nifanyie
msamaha na unipokee,Mema
unayoyatenda nitafanya nini mimi
nikurudish- ie.

13. EE BWANA TWAKUOMBA UPOKEE

Kiit: Ee Bwana twakuomba upokee vipaji vyetu


(x2), Hivyo vyote ni mali yako,
Tumepata kwa wema wako pokea. (x2)

1. Mkate divai twakutolea,


Twakuomba Saba upokee.
3. Nayo sadaka twakutolea,
Twakuomba Saba upokee.
2. Mazao ya shamba twakutolea,
Twakuomba Saba upokee

14. ROHO YANGU YESU INAKUTAMANI

Kiit:
Roho yangu Yesu inakutamani,
Njoo kwangu Yesu unipe heri (x2).

1. Njoo kwangu Yesu nakungojea, kwani wewe u rafiki


mkuu.
2. Na uzidi Yesu kuwa nami, unipe mkate wa uzima.
3. Maumbo ya mkate na divai, umo ndani kweli
nasadiki.

15. MUNGU BABA POKEA SADAKA YETU LEO

Mt. Yohana Mtume - 84


Kiit:
lpokee sadaka yetu ,ndilo fumbo la kupendeza Ya
Baba na ya Mwana na ya Roho Mtakatifu .. X2

1. Mungu Baba pokea sadaka yetu leo,


Tukutoleayo kwa jina la mwanao,
Ya Abel na Ibrahim ilikupendeza
Yetu Saba ipendeze ipokee tu.
2. Njoni wote tutoe sadaka yetu leo,
Kwa sifa na utukufu wake Mwenyezi,
Mkate huu na divai ndiyo mwili wake,
Kwa heshima kuu sadaka tumtolee.
3. Kama mwanzo Mungu Baba naye
asifiwe,
Na mwanawe ndiye aliyetukomboa,
Roho Mtakatifu ndiye wetu mfariji, Utatu
Mtakatifu Mungu mmoja twakiri.

16. EE BABA POKEA VIPAJI HIVI

Kiit:
Ee Baba pokea vipaji hivi,
Sadaka ya Mwanao Mpenzi.

1. Ee Baba twakutolea mkate,


Ugeuze mwili wa Yesu.
2. Ee Baba twakutolea divai,
lgeuze damu ya Yesu.
3. Nafsi zetu pia tunazitoa,
Pamoja na sadaka hii.
4. Sadaka ya mwanao ni kamili,
Mt. Yohana Mtume - 85
ltuwezeshe kuja kwako.
5. Zawadi hizi ndogo tutoazo,
Baba twaomba zipendeze
6. Mazao na mali yetu twakupa
Kwa njia ya mwanao mpenzi.
7. Juhudi na kazi tuzifanyazo,
Zijenge utukufu wako.
8. Kwa njia ya sadaka ya mwanao
Tujalie furaha leo.
9. Yeye amejifanya mwanadamu,
Ajitoe sadaka safi.

17. HIKI NI CHAKULA CHA MBINGU

Kiit:
Hiki ni chakula cha mbingu,
Mkate safi kwa wampendao,
Kweli ni uzima wa roho.

1. Yesu shibisha roho yangu,


Kaa katika roho yangu,
Bwana tuliza hofu yangu.
2. Nipe nguvu ya kukujia,
Nipe neema ya kukufuata,
Nipe moyo wa kukupenda.
3. Mbali nawe ninasumbuka,
Bila wewe ninataabika,
Ukiniacha naaibika.
4. Uzima wako nipatie,
Pendo lako unijalie,
Na imani nizidishie.
Mt. Yohana Mtume - 86
5. Wewe ni neno Ia uzima,
Wewe chakula cha uzima,
Wewe kinywaji cha uzima.
6. Uniongoze mashakani ,
Uniepushe mashakani,
Unifikishe uwinguni.

18. ENYI WATU WOTE PIGENI MAKOFI

Kiit:
Enyi watu wote pigeni makofi,pigeni makoti,
Mshangilie, Mshangilieni mungu kwa sauti ya
shangwe.

1. Bwana ndiye nguvu kwa watu wake, ndiye kinga ya


wokovu kwa Kristo wake.
2. Ee Bwana uwaokoe watu wako , uubariki urithi wako,
uwachunge hata milele.
3. Ee Bwana nitakuita wewe mwamba wangu , usiwe
kwangu kama kiziwi.
4. Ee Mungu twakumbuka huruma yako , katika hekalu
lako.
5. Hivyo hata sifa yako yaenea mpaka kingo za dunia,
mkono wako wa kuume haki.

19. TOA NDUGU, TOA NDUGU

Kiit:Toa ndugu, toa ndugu, x 2 Ulichonacho wewe,


Bwna anakuona, Mpaka moyoni mwako.

1. Sasa ndiyo wakati wakutoa sadaka kila mtu aanze


kujifikiria.

Mt. Yohana Mtume - 87


2. Ewe ndugu usimame nenda mbele ya bwana
kamtolee sadaka na mapendo yote.
3. Kumbuka Bwana Yesu alivyojitolea pale msalabani ni
kwa ajili yako.
4. Wiki hii nzima Bwana amekuandalia vyema sasa na-
we ndugu yangu ujifikirie.
5. Tolea moyo wako pawe mapendo yako naye Bwana
Mungu wako.

20. EE BWANA POKEA VIPAJI VYETU

Kiit:
Ee Bwana twakuomba upokee vipaji vyetu x2
Hivyo vyote ni mali yako,
Tumepata kwa wema wako pokea.

1. Mkate divai twakutolea , twakuomba baba vipokee,


2. Mawazo pia matendo yetu , twakuomba baba
upokee,
3. Twakutolea na nyoyo zetu kwa upendo baba upokee,
4. Sadaka zetu uzibariki , pia nasi baba tubariki.

21. EKARISTI NI CHAKULA BORA

Kiit:
Ekaristi ni chakula bora,
Yesu Kristo akaa ndani yake,
Atulisha atushibisha daima.

1. Leo Kristu atuombea kwa Mungu,


Mt. Yohana Mtume - 88
Sala zetu apeleka kwa Baba,
Nasi tumtolee shukurani zetu
2. Mwili wa Yesu ni chakula chetu,
Damu yake ni kinyaji chetu,
Roho yake ni uzima wetu.
3. Tumtolee shukrani zetu leo,
Nyimbo nzuri pia
tumwimbie, Tupige magoti
tumwabudie.
4. Jongeeni kwa kalamu yake,
Kwa ibada kuu mkampokee,
Kwa heshima kuu mumwabudie

22. AULAYE MWILI WANGU

Kiit:
Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu,
Asema Bwana, hukaa ndani yangu nami hukaanda-
ni yake.

1. Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu, ana


uzima wa milele .
2. Njoni enyi wenye njaa, njoni enyi wenye kiu, njoni
kwangu niwashibishe.
3. Aniaminie mimi, na kuyashika nisemayo, nitamfufua
siku ya mwisho.
4. Mlapo chakula hiki, mnywapo kikombe hiki, mwatan-
gaza kifo cha Bwana.

Mt. Yohana Mtume - 89


23. YESU ASANTE SANA

Kiit:
Yesu asante sana,Yesu asante sana,
Kujifanya chakula, Kujifanya chakula
Kujifanya chakula, Kutuletea shibe alama ya pendo
x2
1. Uloonyesha kwetu ni mapenzi mazito yasiyo na mwi-
sho,
Na wenye sikitiko unawapa tulizo kuwaponyesharoho.
2. Mapenzi yoko Yesu hatuwezi kupima sisi wana wako,
Ulionyesha pendo ukajifanya wewe mlo wetu sote.
3. Kushukuru twashindwa mapenzi ya kulipa roho tun-
ashindwa
Ukae mwangu Yesu nami nikae mwako daima milele.

Mt. Yohana Mtume - 90


NYIMBO ZA BIKIRA MARIA
24. TUNAKUSHUKULU MAMA MARIA

Kiit:
Tunakushukulu Mama Maria,
Kwa neema unazotujalia,
Asante Mama wa Yesu uliye na huruma,
Uzidi kutuombea mpaka saa ya kufa.

1. Mama wa Yesu, mama mfariji wetu,


Ahsante sana kwa kutusimamia,
2. Neema zako zinatutia nguvu ahsante,
Mama Maria Mtakatifu.
3. Mama Maria mama safi wa

25. JINA MARIA JINA TUKUFU

1. Jina Maria jina tukufu, lafurahisha latutuliza

Kiit:

Hata malaika wanaliimba siku zote, wakisema (siku


zote) bila mwisho (Ave Maria) Ave, Ave, Ave Maria.

2. Jina Maria jina tukufu, lafurahisha lat-Utuliza.


3. Jina Maria jina tukufu, latuletea neema ya Mungu.
4. Jina Maria jina tukufu, lawafukuza pepo wabaya.
5. Jina Maria jina tukufu, lawapendeza watakatifu.

Mt. Yohana Mtume - 91


26. EE MAMA YETU MARIA
Kiit:
Ee Mama yetu Maria twaomba sana ee Mama
usituache gizani kwa mwanao tuombee x 2

1. Mama yetu Maria, -Utusikilize, sisi wana wako


tuna- osumbuka.
2. Maisha yetu mama hayana furaha, tujaze neema,
tu- pate faraja.
3. Utuombee kwake mwanao mpendwa, atutie
nguvu tushinde maovu.
4. Dunia ina giza, dunia ni ngumu, bila nguvu
yako hatuwezi kitu.
5. Tuombee Maria, tuombee mama, ili wanawako
tufike mbinguni.

27. MIMI NI MTUMISHI WAKE BWANA

Kiit:
Mimi ni mtumishi wake Bwana, nitendewe ulivy-
onena x 2
Nitendewe ulivyonena, mimi ni mtumishi wa Bwa-
na (wa Bwana) mimi ni mtumishi wa Bwana ni-
tendewe ulivyonena x 2

1. Salamu uliyejaa neema/ Bwana yu pamoja nawe.


2. Usiogope Maria / Mungu kakupendelea.
3. Tazama utapata mimba utamzaa mwana /
utamwita jina Yesu.
4. Huyu atakuwa mkuu / ataitwa mwana wa aliye juu.
Mt. Yohana Mtume - 92
5. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi / cha baba
yake Daudi.
6. Ataitawala nyumba ya Yakobo hata milele /
ufalme wake hautakuwa na mwisho.
7. Roho Mtakatifu atakushukia / na nguvu ya yule
aliye juu itakutia kivuli.
. Ndiyo maana huyo mtoto atakuwa mtakatifu / Naye
ataitwa mwana wa Mungu.
.

28. EE MARYAMU

1. Ee Maryamu, wafahamu, Wanao wa uge nini.


Tupe, Mama , usalama, utulinde hapa chini x 2
2. Nyota nzuri ya bahari, Tuliza dhoruba mbaya
Na za mwovu vunja nguvu, Simwache kutuogofya.x2
3. Na memayo Jaza nyoyo, Za mayatima waombi;
Utukaze, tuongoze, Tusichafuke na dhambi.x 2
4. Ukaako, wana wako, Maria Mama Bikira,
Uwinguni kwa amani, Waonje furaha bora. x 2

29. TUMSIFU MARIA

1. Tumsifu Maria, enyi wanawe. Tutoe salaamu, tum-


shagilie.

Kiit:
Salaam, salaam, salaam Maria x 2

2. Nyota ya bahari, mlango wa mbingu, Mwondoa hata-


Mt. Yohana Mtume - 93
ri, Mama wa Mungu.
3. Maria Bikira ndiwe mteule. Umechaguliwa tangu
milele.
4. Hatuna mwombezi aombeaye Kwa Mungu mwenyezi
kuliko wewe.
5. Mamangu, mbinguni tumshangilie Mwanao mpenzi
pamoja nawe.

30. TUMAINI LETU MAMA MARIA .

Kiit:
Tumaini letu mama (yetu), Mama Maria
tumaini letu mama (yetu), ee mama mwema ndiwe
tumaini letu ewe mama yetu Maria x 2

1. Mama Maria malkia wa mbingu, umetukuka kweli Ma-


ria sifa zako maana tutaziimba.
2. Maana Yesu ulimtunza vema, nasi pia tutunze Maria,
sifa zako maana tutaziimba.
3. Katika shida za mwili na roho usituache kamwe Maria
-Utusaidie mama yetu mpenzi.
5. Mama Maria, tumaini letu tusaidie tushinde Maria
tumwone mwanao huko mbinguni.

31. MAMA YETU MARIA

Kiit:
Mama yetu Maria tunakukimbilia (mama)
sisi wanawako tunaosumbuka ugenini x 2
Mt. Yohana Mtume - 94
1. Utulinde katika shida na taabu zote -Utujalie neema
zako tunapo anguka.
2. Mama yetu mpendelevu -Utusimamie, -Utukinge na
mabaya yote ya mwovu shetani.
3. Twakuomba bila kuchoka ewe mama yetu -Utuinulie
macho yako -Utusikilize.
4. Sala zetu uzifikishe kwa mwanao mpenzi atuondolee
dhambi zetu tulizozitenda.

32. NAKUPENDA MARIA

Kiit: Nakupenda Maria (mama) mama uliye bora.


Furaha yangu Maria nikae nawe daima
nipate neema zako, nifike juu mbinguni x 2

1. Mama mwema Maria, unikinge, unilinde nifanye yote


mema, nayo mabaya niyashinde.
2. Uliyebarikiwa, Maria mpendelevu, unijaze baraka ili
niwe mnyenyekevu.
3. Uyatulize mama, mashaka ya moyo wangu, neema
za mwana wako zifariji roho yangu.
4. Njoo kwangu Maria, ukae pamoja nami, nijalie faraja
ili niishi kwa amani.

33. SISI WANA WA DUNIA


Kiit:
Sisi wana wa dunia tukumbuke maneno
aliyosema Bikira Maria.
Alipowatokea watoto wa Fatima, Lucia Francisi na
Mt. Yohana Mtume - 95
Yasinta.
Alisema tusali, tusali Rozari, tupate amani.
Na tuwaombee, wale wakosefu, wasio na
mwombezi.
Na wasio mwamini Yesu mwokozi, wamuamini ili
waokoke.

1. Mama yetu anahuzunishwa sana na matendo yetu


maovu, anajua adhabu yetu ijayo hivyo anaona hu-
ruma sana.
2. Atusihi tuache dhambi kwa dhati, tuache kumkosea
Yesu, tuyatubu makosa yetu yote ili Bwana atupatie
huruma.
3. Tunatumaini kwako mama yetu, tumekuja: mbele
yako, tunaleta maombi yetu kwako, ee mama -
Utusikilize -Utusaidie sisi wanao.
4. Hapa duniani kuna vishawishi vingi, vinavyotusonga
sana, tunashindwa tukiwa peke yetu, ee mama -
Utusaidie tuvishinde vishawishi vyote.
5. Hapa duniani kuna mambo mengi, yanayotutia giza,
tunaomba -Utuangazie, ee mama'
Utuonyeshe njia iendayo kwa mwanao mbinguni.

34. EE MAMA YETU MARIA

Kiit:
Ee mama yetu Maria twaomba sana
Ee mama usituache gizani, kwa mwanao tuombee x
2

1. Mama yetu Maria utusikilize


Mt. Yohana Mtume - 96
Sisi wana wako tunaosumbuka.
2. Maisha yetu mama hayana furaha
Tujaze neema tupate faraja.
3. Utuombee kwake mwanao mpendwa
Atutie nguvu tushinde maovu.
4. Dunia ina giza, dunia ni ngumu
Bila nguvu yake hatuwezi kitu.
5. Tuombee Maria tuombee mama
Ili wana wako tufike mbinguni.

35. MARIAMU EE ZIPOKEE

Kiit:
Mariamu ee zipokee hizo zako heshima
Twakuimba, twakuomba, utuelekee mama

1. Pamoja na malaika, Mariamu mama


wetu Kuimba sifazo twataka,
zipende nyimbo zetu.
2. Mazuri ya ulimwengu, si kitu mbele
yako Hata nyota za uwingu zawia
mbele yako.
3. Bikira usio mfano, sifazo kuzitaja
Sitoshi haba maneno, kubwa yako
daraja.
4. Ewe Maria mpole, sikia ombi letu
Tujalie kifo chema, mwisho tufike
kwako huruma.

Mt. Yohana Mtume - 97


36. TUNAKUSHUKURU MAMA MARIA

Kiit:
Tunakushukuru Mama Maria,
Kwa neema unazotuombea,
Asante Mama wa Yesu uliye na huruma,
Uzidi kutuombea mpaka saa ya kufa.

1. Mama wa Yesu, mama mfariji wetu,


Ahsante sana kwa kutusimamia,
2. Neema zako zinatutia nguvu ahsante,
Mama Maria Mtakatifu.
3. Mama Maria mama safi wa moyo,
Tusaidie tushinde vishawishi.

37. MARlA ALlTEULlWA NA MUNGU

Kiit:
Maryam Bikira aliteuliwa na Mungu mwenyezi ku-
shiriki ukombozi wa taifa lake na dunia yote.
Naye akazaa mtoto mwanaume atakayewachunga
mataifa yote kwa fimbo ya chuma na mtoto wake
akanyakuliwa kwangu, na kwa kiti chake cha enzi.

1. Maajabu yamenenwa juu yako Maria, mama wa Mun-


gu na kwako limetokea jua la haki Kristu Mungu
wetu.
2. Wokovu wangu na ufalme wa Mungu sasa umekuwa,
mamlaka ya Yesu Kristu mwana wake yanatawala.

Mt. Yohana Mtume - 98


Mt. Yohana Mtume - 99
NYIMBO ZA KWARESIMA
38. KWA ISHARA YA MSALABA.

Kiit:
Kwa ishara ya msalaba tuokoe x2

1. Na adui zetu ee Bwana / utuokoe sisi Bwana Mungu


wetu.
2. Mbona mataifa ee Bwana / wanafanya ghasia mbele
ya Mungu wetu.
3. Pia makabila ee Bwana / nao wanatafakari ubatili.
4. Wafalme nao wa dunia / naowajipanga panga.
5. Wakuu wafanya shauri / juu ya Bwana na wasihi
wake.
6. Tupasue vifungo vyao / tuzitupe mbali nazo kamba
zao.
7. Yeye aketiye mbinguni / anacheka na kuwadhihaki
wote.

39. PASIPO MAKOSA


1. Pasipo makosa mkombozi wetu,
Katika baraza la wakosefu
Na wote walia asurubiwe,
Aachwe Baraba, naYesu afe.x 2

2. Ee Yesu, washika msalaba wako,


Na unakubali kufa juu yake,
Ee Yesu useme, sababu gani?
Ya nini mateso makali hayo? x 2

Mt. Yohana Mtume - 100


3. Ni pendo la Baba wa uwinguni, Ni
huruma yangu kwa wakosefu ;
Wee mkristu, kumbuka mateso yangu :
Uache makosa, uache dhambi. x 2

40. KRISTU ALIJINYENYEKEZA - E. I. Kalluh

Kiit:
Kristu alijinyenyekeza x2.
Akawa mtii hata mauti na-am mauti ya msalaba x2

1. Kwa hiyo Mungu alimwadhimisha mno I akamkirimia


jina lile lipitalo kila jina.
2. Ninyi mnaomba Bwana I msifuni enyi wote mlio
wazao wa Yakobo mtukuzeni.
3. Wote wanionao hunicheka sana
Hunifyonza wakitikisa vichwa vyao

41. TUMWANGALIE MKOMBOZI

1. Tumwangalie Mkombozi akitundikwa msalabani


tutatambua upesi, aliotupenda moyoni.

Kiit:
Twimbe, twimbe jamani, salamu Yesu msalabani.

2. Msalabani sio mtini, tunaotaka kuheshimu, ila ni Yesu


mwenyewe kwa binadamu mwaga damu.
3. Tuusifu sana mti huu, Yesu akauchagulia kwa mapen-
do yake makuu, deni zetu kuzilipia.

Mt. Yohana Mtume - 101


42. WIMBO WAKUOMBA TOBA-TUMEKOSA

Kiit:
Tumekosa, kweli tumekosa, tunaomba Bwana
tusamehe makosa yetu twayatubu.

1. Tumekukosea Bwana, tukafuata nia zetu, tukakuacha


ee Bwana.
2. Tumekukosea Bwana tukafuata makosa yetu,
utusamehe Bwana.
3. Tumekukosea Bwana, twajifanya wa hekima,
twakuzidi ee Bwana.
4. Tumekukosea Bwana, twajifanya ni miungu yetu sisi
wenyewe.
5. Tumekukosea Bwana, twachukua nafasi yako, ukawa
chini yetu.
6. Tumekukosea Bwana, twajifanya kulingana na wewe
Mungu wetu.
7. Tumekukosea Bwana, twakufanya ni kiumbe chetu
sisi wenyewe.
8. Tumekukosea Bwana, twajifanya tuna nguvu, twaku-
shinda Ee Bwana.
9. Tumekukosea Bwana, tumekosa imani kwako, Ee
Mungu Baba wetu.
10. Tumekukosea Bwana, tumekosa tumaini kwako,
Ee Bwana Mungu wetu.
11. Tumekukosea Bwana, tUm.ekosa kuk.upenda,
Ee Mungu Baba yetu.

43. UTUREHEMU:
Mt. Yohana Mtume - 102
Kiit:
Uturehemu ee Bwana kwa kuwa tumetenda
dhambi x2

1. Ee Mungu uturehemu / sawa sawa na fadhili zako.


2. Kiasi cha wingi wa rehema zako / uyafute
makosa yangu.
3. Unioshe kabisa uovu wangu / unitakase dhambi
zangu.
4. Maana nimejua mimi makosa yangu / na dhambi i
mbele yangu daima.
5. Nimekutenda dhambi wewe peke yako / na kufanya
maovu mbele za macho yako.

44. ASILEGEE MOYOWE

1. Asilegee moyowe, asitokwe machozi


Akimkumbuka Munguwe, kwa yake makombozi
Mtoa roho msalabani, mtaka kufa mwenyewe
Kwa sababu kumpendani, nani mfunga moyowe.
2. Bustani mle Getsemani, amwomba Mungu Baba
Je mtu Mungu ana nini, nguvu zake ni haba
Rabbi wangu waziona, dhambi za binadamu
Mwili wako umetona, kama jasho la damu.
3. Salamu Rabi salamu, anena Yuda mbaya
Mwenye moyo wake mgumu, ambusu pasi haya
Aliwaambia “basi, ntakayembusu ndiye
Mtwaeni na kwa upesi”, Yuda nani nisiye.
4. Yuda nani ila yeye, aliyetenda dhambi
Akikosa kwa Munguwe, mtenda kwa hia na
Mt. Yohana Mtume - 103
dhambi
Mwenye kumtendea mema, mtaka dhambi haoni
Kwamba ni kutupa neema, kumwendea shetani
5. Wote ni kupiga mbio, mitumewe pamoja
Wamtia mikono yao, askari walokuja
Wampeleka hukumuni, aamuliwe na mtu
Ye kutoka uwinguni, Mwanzi mkuu wa watu
6. Mtume Petri amkanusha, amenena “simjui”
Uhodari umekwisha, machoye hainui
Pilato amwona Rabbi, hakukosa ‘ta neno
Asema “sioni dhambi”, lakini ni mwoga mno.
7. Athubutu kumwachia, “si hukumu” aomba
“Mmoja nitamfungulia, Yesu au Baraba
Wayahudi mwamtakani”, “Baraba aachwe tu
Yesu afe msalabani, damuye juu yetu”
8. Pilato “hukumu gani? simo nanawa mkono
Mkimtaka Yesu mwueni”, la mwamzi hilo neno
Mara askari wamwanza, ni kupiga kelele
Kumcheka na kumchokoza, mwenye mema
milele.

45. ATANIITA - Fr. G. F. Kayeta

Kiit:
Ataniita nami nitamwitikia,nitamwokoa, na
kumtukuza X2

1. Nitakuwa naye taabuni,


nitamwokoa na kumtukuza
2. Kwa siku nyingi nitamshibisha,
Mt. Yohana Mtume - 104
Nami nitamwonyesha wokovu wangu.
3. Kwa kuwa amekaza kunipenda,
Nitamwokoa; na kumweka mahali palipo juu.
4. Kwa kuwa amenijua jina langu,
Ataniita nami nitamwitikia.

46. BABA MIKONONI MWAKO

Kiit:
Baba mikononi mwako, naiweka roho yangu

1. Baba uwasamehe, kwani hawajui wanalofanya


2. Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja
nami paradisoni,
3. Mama tazama huyu ndiye mwanao, tazama huyu
ndiye mama wako
4. Ili andiko litimizwe, Yesu alisema naona kiu
5. Baada ya kupokea siki alisema yametimia
6. Mungu wangu Mungu wangu, mbona umeniacha
7. Baba mikononi mwako naiweka roho yangu

47. MAMA PALE MSALABANI

Kiit:

Mama pale msalabani, macho yatoka machozi


Akimwona mwanaye, kweli ni huzuni kubwa

1. Kweli vile akilia, uchungu kama upanga,


Mt. Yohana Mtume - 105
Ukampenya moyowe
2. Mwenye moyo mgumu nani, asimhurumie basi
Mama amlilia mwana
3. Ewe Mama mtakatifu, usulubiwe na Yesu
Moyo wangu mwenye dhambi
4. Naye Mwokozi niteswe, na madonda nigawie
Pamoja na ukombozi
5. Nisimame msalabani, niwe nami wako mwenzi
Wa uchungu na msiba
6. Nisianguke motoni, uniwie msimamizi,
Ewe bikira mwema
7. Msikilize mama yako, niponye siku ya mwisho
Ewe Mwokozi wangu
8. Nitakapokufa mimi, upokee roho basi
Niende kwako Mungu

48. MTAZAME MKOMBOZI MSALABANI

Kiit:
Mtazame Mkombozi Msalabani
Alivyotundikwa pasipo na kosa
Ili sisi sote tukombolewe X 2

1. Shaka we Mkristu, ukawaze,mateso yake Bwana


2. Jasho la damu, limemtoka Mateso yakazidi tu
3. Msalaba walimtwika Kalvari alikwenda nao

49. MUNGU WANGU MBONA UMENIACHA – G.A.


Chavalla

Mt. Yohana Mtume - 106


Kiit:
Mungu wangu mbona umeniacha mimi
Katika taabu zote hizi
Maisha yangu ni ya mashaka
Kwani sina raha nimekosa amani
Matatizo mengi yananisonga (sana)
Nakuomba Bwana nisaidie
Maadui zangu wananiwinda (kutwa)
Wanitega ili wanikamate

Ninalala macho wazi mimi (kama ndege)


Kama ndege mkiwa juu ya paa
Nimekuwa kama mhuni mimi (fanya hima)
Fanya hima Bwana kuniokoa

1. Nimekuwa kama kichekesho kwa watu jamani


mimi Bwana
Kila nipitapo hunisema na kunicheka
Wananizushia maneno ya uongo jamani mimi
Bwana
Mimi nimekuwa ni jalala la kila baya
2. Maadui zangu kutwa wanisimanga jamani mimi
Bwana
Wananidhihaki wanisonya na kunitusi
Jina langu limekuwa gumzo lao jamani mimi
Bwana
Sasa ndilo walitumialo kwa kulaania
3. Na majivu yamekuwa chakula changu jamani
mimi Bwana
Na machozi yangu yamekuwa kinywaji changu
Na siku zangu zinapita kama moshi jamani mimi

Mt. Yohana Mtume - 107


Bwana
Nakuomba usinichukue bado kijana

50. MUNGU WANGU MUNGU WANGU MBONA


UMENIACHA - G. A Chavalla

Kiit:
Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha

1. Wote wanionao huncheka sana


Hunifyonya watikisa vichwa vyao husema
hutegemea Bwana na amponye
Na amwokoe sasa maana apendezwa na yeye
2. Kwa maana mbwa wamenizunguka
Kusanyiko la waovu wamenisonga
Yamenizua mikono na miguu
Naweza kuihesabu mifupa
3. Wanagawanya nguo zangu
Na vazi wanalipigia kura
Nawe usiwe mbali
Ee Mungu wangu fanya haraka kunisaidia
4. Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu
Katikati ya kusanyiko nitakusifu
Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni
Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo mtukuzeni.

51. NIMEKUKIMBILIA WEWE BWANA


Mt. Yohana Mtume - 108
Kiit:

Nimekukimbilia wewe Bwana, nisiaibike milele


Ee Baba mikononi mwako Baba naiweka Roho
yangu x 2

1. Umenikomboa ee Bwana Mungu wa kweli


Ee Baba mikononi mwako naiweka Roho yangu
2. Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu
Naam hasa kwa jirani zangu
1. Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu
Walioniona njiani walinikimbia
2. Nimesahauliwa kama mtu asiyekumbukwa
Nimekuwa kama chombo kilichovunjika
3. Maana nimesikia masingizio ya wengi
Hofu ziko pande zote

52. UNIHURUMIE MIMI BWANA

Kiit:

Unihurumie mimi Bwana


Nimetenda dhambi mimi Bwana
Ninakusihi ee Mungu wangu
Unisamehe makosa yangu
(Niliyokutendea ewe Mungu wangu
na jirani yangu x 2)
Mt. Yohana Mtume - 109
1. Nami nimetengwa nawe Bwana nihurumie,
Mimi ni mkosefu
2. Naogopa uso wako unihurumie baba,
Mimi ni mkosefu
3. Wewe Baba Mwenye huruma unihurumie
Mimi nimetenda dhambi

53. WAKUPELEKA HUKUMUNI - P. F. Mwarabu

Kiit:

Wakupeleka hukumuni Yesu,


ili uamuliwe na mtu
Tendo gani umefanya Yesu,
hata wakutaka usulibiwe
Ulikuja kwangu, mi mdhambi
Ili uniokoe katika taabu zangu zote
Unipatanishe na Mungu Baba
Ili nifike kwake kwenye uzima wa milele

Kwa nini unateseka hivyo,


Bwana usiye na kosa lolote
Mimi ndiye mwenye kosa Yesu,
Nawe ndiwe wa kunihukumu
Msalaba mzito waubeba
Mijeredi kupigwa, taji la miiba kuvalishwa
Yote umekubali, juu yangu
Ili unikomboe, mimi mdhambi wa huzuni
Mt. Yohana Mtume - 110
{ Nimekosa mimi nimekosa
Unihurumie Mungu wangu } *2

1. Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu


Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza
Toka mbinguni Mungu aliwachungulia wanadamu
Aone kama yupo mtu mwenye akili amtafutaye Mungu
2. Ee Mungu kwa jina lako uniokoe
Na kwa uweza wako unifanyie hukumu,
Ee Mungu uyasikie maombi yangu
Uyasikilize maneno ya kinywa changu.

54. WATUMISHI WAKE BABA

Kiit:

Watumishi wake Baba wangapi waliopo


Wanakula na kusaza chakula chake Baba
Nami - Nami nataabika hapa
Nashi - Nashiriki na nguruwe
Chaku - Chakula kisichofaa, yanipasa kurudi
Nita - Nitarudi na kusema
Baba - Baba yangu nisamehe
Nime - Nimekosa kwake Mungu, na mbele yako Baba

Mt. Yohana Mtume - 111


1. Baba kamwona yu mbali kashikwa na huruma
Akakimbia kumlaki kamkumbata na busu
2. Baba sistahili tena kuitwa mwana wako
Unifanye kama mmoja wa watumishi wako
3. Baba yangu nimekosa ninaomba huruma
Unisamehe nirudi nikakutumikie
4. Bwana karibisha mimi kwenye karamu yako
Meza imeandaliwa inaningoja mimi
5. Nasongea ninakuja ninakukimbilia
Mimi ni mtoto mpotevu Baba unipokee
6. Nimekula nimeshiba nakushukuru Baba
Chakula kama asali asante sana Baba

55. YESU AKALIA - G. A Chavalla

Kiit:

Yesu akalia kwa sauti kubwa,


{ Akasema,
Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu } x 2
1. Alipokwisha kusema hayo, akakata roho
Yule akida alipoona hayo, akasema
Huyo hakika alikuwa mwana wa Mungu

Mt. Yohana Mtume - 112


2. Na makutano yote ya watu, waloshuhudia
Wakafadhaika wakaenda zao, wakiomba
Wakapigapiga vifua kuomba toba
3. Na wote waliojuana naye, waloandamana
Wakimfuata toka Galilaya, kwa pamoja,
Wakasimama wakitazama mambo hayo.

56. YESU ALIA MSALABANI

Kiit:

Ee mwanadamu lipi ambalo linalonipasa kuwatendea


Ambalo sikuwatendeeni, hata ikanipasa msalaba

1. Yesu alia msalabani. Asikitika juu ya dhambi zetu


Asulubiowa asiyekosa kwamba yeye ni mosaji
2. Magonjwa yote aliyaponya, wafu nao aliwafufua
Kundi la watu aliwaponya, lipi alilokosa
3. Watu wa Mungu Bwana alia asikitika juu ya dhambi
zenu
Asulubiwa asiyekosa kwamba ni mkosaji
4. Wana wa Mungu, Bwana alia, asema nyinyi
mwamsulubisha,
Msipobeba misalaba yenu kwani nyinyi m wakosaji
5. Tazama Bwana akulilia, akuita ndipo akuokoe
Tazama haya mapenzi yake Bwana hayana mwisho

Mt. Yohana Mtume - 113


57. YESU MSALABANI ALIPOTUNDIKWA - F. A.
Nyundo

Kiit:

( Yesu msalabani, alipotundikwa


Hakuwa na dhambi, mkombozi wetu ) *2
Dhambi zetu nyingi sana, ndizo zilimtesa
Hakuwa na kosa, mkombozi wetu

1. Aliteswa msalabani kwa ajili ya ukombozi wetu sisi


2. Akasubulibiwa kwa ajili ya ukombozi wetu sisi

58. YESU WANGU NIOKOE - A. K. C. Singombe

Kiit:
Yesu wangu niokoe,
( Ulimwegu nilimo ni wa mateso
Nishike mkono wangu Bwana niokoe
Ulikuja duniani kwa wadhambi,
Nitakase kwa damuyo Bwana nitakate
Bwana nakukimbilia ) x 2

1. Nionyeshe uso wako uso mkunjufu, nisamehe dhambi,


Nakusihi Mwokozi, Bwana unisikie

Mt. Yohana Mtume - 114


2. Nimefanana na mwana mwana mpotevu, dhiki na
karaha
Vimenisonga sana Bwana unisikie
3. Wewe ndiwe ngome yangu ngao yangu tumaini langu
Ninakutegemea Bwana unisikie
4. Roho yangu mwili wangu vyote ni vyako ndivyo
ulivyoumba
Viimarishe Bwana, Bwana unisikie
5. Mungu Baba Mungu mwamba Mungu mkombozi
Mungu wa mapaji, Utatu Mtakatifu usifiwe milele

Mt. Yohana Mtume - 115


NYIMBO NYINGINE
59. UJE ROHO MTAKATIFU SEKWENSIA

1. Uje Roho Mtakatifu, Tuangaze toka mbingu,


Roho zetu kwa mwangao.
2. Uje Baba wa maskini, Uje mtoa wa vipaji,
Uje mwanga wa mioyo.
3. Ee Mfariji mwema sana, Ee Rafiki mwa(a)nana,
Ewe raha mustarehe.
4. Kwenye kazi U pumziko, Kwenye joto burudisho,
U mfutaji wa machozi.
5. Ewe mwanga wenye heri, Uwajaze waumini,
Neema yako mioyoni.
6. Bila nguvu yako wewe, Mwanadamu hana kitu,
Kwake yote yana kosa
7. Osha machafuko yetu, Panyeshee-e pakavu petu,
Na kuponya majeraha
8. Ulegeze ukaidi, Pasha moto ubaridi,
Nyosha upotevu wote.
9. Wape waamini wako, Wenye tumaini kwako,
Paji zako zote saba.
10. Wape tuzo ya fadhila, Wape mwisho bila ila,
Wape heri ya milele.
11. Amina Alleluia, Amina Alleluia
Amina Alleluya

60. JIWE WA ULOKATAA WAASHI

Kiit:
Mt. Yohana Mtume - 116
Jiwe walilokata waashi limekuwa jiwe kuu
lapembeni, limekuwajiwe kuu lapembeni.

1. Bwana Mungu ndiye aliyefanya jambo hili nalo ni kiajabu sana


kwetu
2. Hii ndiyo siku aliyoifanya Bwana Mungu basituish-
angilie kwa furaha
3. Utuokoe sisi sate eeBwana Mungu tunakusihi utupe
tanaka
4. Abarikiwe ajaye kwa jina lake Bwana alete baraka ta-
ka mbinguni
5. Wewe ndiwe Mungu wangu nami ninakuishukuru nina
kutekwa Ee Mungu wangu.
6. Mshukuruni mwenyezi Mungu kwa kuwa ni Mungu na
fadhili zake ni za milele.

61. NINAKULILIA KATIA UNYONGE WANGU

Kiit:
Ninakulilia. katika unyonge wangu, ewe kinga
yangu

I. Toka vilindini nakulilia ee Bwana


Usikie sauti yangu, sikiliza sauti ya dua zangu

2. Kama wewe ungehesabu maovu,


kama usingeturehemia kati yetu sole nani anges-
imama
.
3. Kwako msamaha ni mwingi na neema na fadhila
Mt. Yohana Mtume - 117
Kwako Bwana ukombozi wazidi.

4. Nimemngoja Bwana Roho yangu imemngoja,


Neno lake nimelitumainia.

62. KESHENI KILA WAKATI

Kiit:
Kesheni kila wakati, ndugu kila wakati, mpate kuo-
koka.

1. Hamjui siku wala saa, atakayokuja mwana wa Mungu


2. Jiwekeni tayari kwa ujio wake, msije mkaanguka
hukumuni
3. Maana yeye huja kama mwizi, anayeotea bila
kutegemewa
4. Heri yule mwanadamu ambaye Bwana atamkuta yu
tayari
5. Bwana atamweka nyumbani mwake, atamfanya
msimamizi wa mali yake.

63. TUMAINI LETU NI KWA BWANA

Kiit:
Tumaini letu ni kwa Bwana, kwa maana ana uwezo
wa milele.

1. Tutamsifu Bwana siku zote.


Wote: Kwa maana anauwezo wamilele
Mt. Yohana Mtume - 118
2. Yeye ndiye mwanzo wa uzima
3. Yeye ndiye aliyetuumba
4. Vitu vyote vimeumbwa naye
5. Yeye ndiye kwetu Kiongozi
6. Tumwabudu tumsifu daima
7. Ni yeye anayetuongoza.
8. Sifa na uwezo ni vyake
9. Nguvu na wokovu ni kwa Bwana
10. Uzima na wokovu ni kwake
11. Atukuzwe katika Utatu
12. Kama mwanzo na sasa na daima.

64. BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU – J. Mgandu

Kiit:
Bwana ndiye Mchungaji wangu sitapungukiwa na
kitu

1. Bwana ndiye Mchungaji wangu, sitapungukiwa na


kitu
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,
Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
2. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake,
naam nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti
sitaogopa mabaya;
kwa maana wewe upo pamoja nami, Gongo lako na
fimbo yako vyanifariji.
3. Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi
wangu,

Mt. Yohana Mtume - 119


umenipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe
change kinafurika.
4. Hakika wema na fadhili zitanifuata. Siku zote za mai-
sha yangu, nami nitakaa nyumbani mwa Bwana
milele.

65. HUO NDIO MWANZO

Kiit:
Huo ndio ni mwanzo wa ufalme wa Mungu.

1. Umpende Mungu kwa moyo wote maana ndiye Baba


yako
2. Heri ukiwa maskini moyoni, maana ufalme wa
mbingu ni wako
3. Heri ukiwa mpole maana utapata nchi
4. Heri ukiona huzuni, maana utatulizwa
5. Heri ukiona njaa na kiu ya kupata utakatifu maana
utashibishwa
6. Heri ukiwa na huruma maana utahurumiwa
7. Heri ukiwa na moyo safi maana utamwona Mungu.

66. SIMAMA IMARA

Kiit:
Simama imara jilinde Neno lake Bwana, imara
kesha kila siku uombe utasimama x 2

1. Milima yote na mabonde vitayeyuka, Neno lake Bwa-


Mt. Yohana Mtume - 120
na imara litasimama.
2. Si mchana wala usiku uombapo rehema, Bwana Yesu
ndiye Mkomoozi atuokoa.
3. Ee Bwana Mungu nijalie baraka za enzi, tegemeo langu
li kwako Mwokozi wangu.

67. TAWALA BWANA, TAWALA BWANA

Kiit:
Tawala Bwana, Tawala Bwana

1. Mungu baba katupa vyote, Tawala .. .. .


2. Tawala, mwana wa Maria, Tawala .... .
3. Tawala Malkia wetu, Tawala .....
4. Tawala Bwana Yesu Kristo Tawala .... .
5. Tawala Malkia wa mbingu, Tawala .... .
6. Tawala Jumuiya yetu, Tawala .... .
7. Tawala Parokia yetu, Tawala .... .

68. TAWALA TAWALA

Kiit:
Tawala tawala, tawala kwetu,
Bwana Yesu.

1. Tawala kwetu mfalme wetu,


2. Tawala na kigango chetu,
3. Tawala jumuiya yetu,

Mt. Yohana Mtume - 121


Mt. Yohana Mtume - 122
Mt. Yohani alizaliwa Betsaida mkoani Galilaya (Israel). Baba yake
alikuwa Zebedayo na mama yake Salome. Alikuwa ndugu ya Mt.
Yakobo Mkuu. Yohani, akiwa pamoja na Petro na Yakobo, ali-
yashuhudia mambo makuu yaliyotukia maishani mwa Bwana. Hivyo,
Bwana alipogeuka sura mlimani Tabor, na tena alipokuwa akisali
bustanini Getsemane, Yohani alikuwapo. Aidha, Bwana alipomponya
mama mkwe wa Petro, vile vile alipomfufua binti Yairo, mtume
Yohani alikuwapo pamoja na Petro na Yakobo.

Yohani hujulikana kama ni mwanafunzi aliyempenda Yesu. Huyo


ndiye yeye ambaye wakati wa Karamu ya Mwisho alikuwa ameketi
karibu na Yesu, na baadaye, saa alipokuwa akifa Yesu, ni yeye tu kati
ya Mitume wote aliyesimama karibu na msalaba pamoja na Bikira
Maria, Maria wa Kleopa na Maria Magdalena.

Baada ya Yesu kufa msalabani, Yohani alimchukua Bikira Maria


akae nyumbani kwake. Alipoletewa habari ya Bwana kufufuka, mara
alikimbia pamoja na Petro; japo Yohani alikimbia upesi zaidi kuliko
Petro na kutangulia kufika kaburini, alimsubiri Petro ili huyo apate
kuwa wa kwanza kuingia ndani. Lakini Yohani ndiye aliyeanza
kuamini kwamba amefufuka alipokiona kitambaa alichofungiwa Yesu
kichwani, kimekunjwa na kuwekwa mahali pa peke yake.

Yohani aliishi akawa mzee sana. Wakati wa utawala wa Kaisari


Dornisiani alihamishwa kwa nguvu hadi kisiwa cha Patmos, na hapo
ndipo alipokiandika kitabu cha UFUNUO. Katika maisha yake, Yohani
alipata kudhulumiwa na kuteswa sana, bali kati ya Mitume wote ni yeye tu
ambaye hakuuawa. Aliandika barua tatu ambazo ni sehemu ya kitabu cha
Agano Jipya. Katika barua hizo, kama vile ilivyo katika Injili yenye jina lake,
Yohani hasa ni mtangazaji wa uhai mpya wa neema ambao tumeletewa na
Kristu.
Alivyoandika katika barua yake ya kwanza (1 Yoh.l:3), kazi yake kuu
ilikuwa kukitangaza kile alichokiona na kukisikia yeye mwenyewe muda
Mt. Yohana Mtume - 123
wote alipokuwa akishirikiana na Bwana Yesu. Aliyaandika yale yote ili watu
wapate kushirikiana na Mitume katika umoja waliokuwa nao na Baba na
Bwana Yesu. Kazi hiyo, Yohani aliitekeleza kwa furaha kubwa, kiasi cha
kuikamilisha furaha yake.
Katika ujana wake, yeye, Yohane, pamoja na ndugu yake Yakobo,
walikuwa wakali kidogo kwa tabia, hata siku moja, walitaka kuamuru
moto ushuke kutoka mbinguni ili uwaunguze wenyeji wa kijiji kimoja
cha Wasamaria, eti, kwa sababu walikataa kumpokea Yesu. Waliwahi
kupewa na Yesu jina Boanerge, maana yake "wanangurumo". Mahali
pengine katika Injili imetajwa ile hamu ya ukuu waliyokuwa nayo hao
ndugu wawili. Imeandikwa kwamba walimsukuma mama yao
awaombee kwa Yesu ruhusa ya kuketi hapo baadaye upande wake wa
kulia na wa kushoto. Sasa, kuna hadithi moja kumhusu Yohani mtume
ambayo yafaa kuikumbuka kwa vile inavyoonyesha jinsi tabia yake
ilivyobadilika. Yasemwa kwamba alipokuwa mzee, hakuweza tena
kufundisha sana, lakini siku zote alikuwa akilikariri neno lile lile moja:
"Wanangu, mpendane". Hatimaye, wakristu walichoka kulisikia neno
hilo, wakamnung'unikia na kumwuIiza: "Je, hujui neno jingine ila hilo
tu?" Naye akawajibu: "Neno hilo ni arnri ya Bwana wetu; mkilifuata
vema, basi yatosha".

Mt. Yohana Mtume - 124

You might also like