You are on page 1of 2

DHANA YA FASIHI

Wapo wataalamu mbalimbali ambao wamekuwa na dhana tofauti tofauti kuhusu maana ya
istilahi fasihi na wamejaribu kutoa maana mbalimbali, hivyo basi katika sehemu hii tutaangalia
baadhi ya maelezo yaliyotolewa na baadhi ya wataalamu wa fasihi kufasili maana ya fasihi:

Fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe kwa hadhira au jamii
iliyokusudiwa.
Tigiti Sengo na Kiango wanasema, Fasihi ni mwamvuli wa mtu na jamii na utu na maisha wa
hadhi na taadhima.

Fasihi yaweza kuelezwa kwamba, hutegemea msanii ambaye huiumba kwa maneno katika tukio
maalum (Finnegan, 1970)

Ni fasihi inayotegemea mdomo ktk kutolewa na kuenezwa kwake… (M.L.Matteru, 1979)

Ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa
waasikilizaji na watumiaji waake (Balisidya, 1983)

Fasihi humaanisha fasihi itolewayo kwa neno la mdomo… (Okpewho, 1992) F.S ni kazi ya
sanaa inayotumia lugha kazi hii ya sanaa huhifadhiwa kwa kichwa na kusambazwa kwa njia ya
masimulizi ya mdomo… (M.Msokile, 1992)

Ni fasihi inayotungwa au kubuniwa kichwani na kuwasilishwa kwa hadhira kwa njia mdomo na
vitendo bila kutumia maandishi (Mulokozi, 1996)

Neno Fasihi linamaanisha hadithi za jadi, nyimbo, mashairi, vitendawili na methali ambavyo
hutolewa kwa neno la mdomo (Bukenya na Wenzake, 1997)

Sanaa hii iitwayo Fasihi, inaweza kuhifadhiwa kwa njia kuu mbili: kwa njia ya mdomo na
kimaandishi. Aina ya kwanza, ambayo tunajihusisha nayo katika sehemu ya kwanza inajulikana
kama F.S (Wamitila, 2003) Cheap Offers: http://bit.ly/gadgets_cheap

Fasihi ni kielelezo cha hisia za mwandishi juu ya mambo yanayomwathiri yeye, kikundi au jamii
nzima anamoishi na kwamba lengo lake kustarehesha au kufunza wasomaji wake. Fasili hii pia
haikidhi maana halisi ya fasihi, je! Kielelezo hicho cha hisia za mwandishi huwasilishwa kwa
kutumia nini?

Fasihi ni maandishi yanayohusu nchi au bara fulani, maandishi hayo sharti yawe ya kubuni.
Ukiangalia fasili hii ina upungufu kwani fasihi si lazima yawe maandishi inaweza kuwa ni
masimulizi, na si lazima yahusu nchi ama bara fulani, hivyo fasili hii inapotosha ukweli kuhusu
fasihi.
Fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe au fikra za fanani.

Fasihi ni kitu chochote kilicho kwenye maandishi. Hii fasili ina mapungufu sana, kwani fasihi si
lazima yawe maandishi, masimulizi pia yanaweza kuwa ni fasihi, lakini piasi chochote
kilichokwenye maandishi ni fasihi kwani fasihi ni lazima kuwa matumizi ya lugha ya kisanaa.

Fasihi ni sanaa inayoakisi maisha ya jamii.

Fasihi ni chombo cha utetezi wa maslahi ya tabaka moja au jingine na kwamba mwandishi ni
mtumishi wake anayejua au asiyejua, atake asitake mwandishi huyo huwa na lengo au dahamira
fulani anayotaka kuionesha,wasomaji wanaweza kuikubali au kuikataa nap engine kutokana na
fani, itikadi ya siasa inayotawala au jinsi mwandishi anavyoainisha.

Kwa ujumla tunaweza sema fasihi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe kwa
hadhira lengwa. Ibrahim mchuchuri

You might also like