You are on page 1of 39

KATIBA

YA
CHAMA CHA JAMII
(CCj)
Utangulizi

• Kwa kuwa mapambano ya kuleta uhuru wa nchi yetu yalikuwa na lengo


kuu la kumwondoa mwananchi kutoka kwenye unyonge wa kunyonywa,
kunyanyaswa na kudharauliwa na wakoloni, ambao ni ukombozi wa
mwananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii; na

• KWA KUWA uhuru tulioupata ulitupa fursa ya kujenga Nchi na Taifa


lenye kubeba matumaini ya wananchi wote kwa ujumla kwa kuweka
misingi imara ya kuheshimu na kuzingatia usawa wa binadamu, utawala
bora, utawala wa sheria, haki za binadamu, hifadhi na ustawi kwa
wananchi wote na utaifa wetu; na

• KWA KUWA ukombozi kamili wa mwananchi kisiasa, kiuchumi na kijamii


unahitaji juhudi, maarifa, moyo wa kujituma na ujasiri wa kuthubutu
kwa upande wa viongozi, vipaji ambavyo bado kuviona vikitumika nchini;
na

• KWA KUWA nchi yetu imedhamiria Kikatiba kuthamini na kuzingatia


Uhuru wa Mahakama katika utoaji haki bila woga wala upendeleo, na
Uhuru wa Bunge lenye madaraka kwa niaba ya wananchi kuisimamia na
kuishauri Serikali na vyombo vyake katika utekelezaji wa shughuli za
umma; na

• Kwa kuwa Tanzania inao utajiri wa kutosha wa rasilimali unaoweza


kuleta maendeleo ya haraka ya nchi kiuchumi na kuleta mabadiliko
makubwa ya maisha kwa kila mwananchi ikiwa ombwe la uongozi
litashughulikiwa; na

• KWA KUWA matumizi bora na endelevu ya utajiri wa rasilimali


yanawezekana tu katika Taifa ambalo lina uongozi wenye uchungu na
nchi na unaozingatia maadili kama yalivyoainishwa na kusimamiwa kidete
na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere; Taifa ambalo linawaandaa
vijana wake vizuri kielimu na kimaadili; ambalo wanawake wana fursa
sawa na wanaume; na ambalo mchango wa kila raia awe kijana, mzee,
mlemavu n.k unatambuliwa na kuthaminiwa; na

• KWA KUWA elimu ni moja ya misingi ya maendeleo ya taifa lolote lile,


msingi ambao baba wa taifa mwalimu J. K. Nyerere aliutumia kujenga
taifa jipya lenye matumaini, nchi yetu haina budi kuendeleza utaratibu
wa serikali kugharamia elimu ya wananchi wake; na

• Kwa kuwa adui mkubwa wa haki na maendeleo ni UFISADI, yaani


rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na uporaji wa rasilmali za Taifa,
adui ambaye hana budi kupigwa vita kwa nguvu zote na

• KWA KUWA Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar nim


ushahidi hai unabeba matumaini mahususi ya kuziunganisha nchi za
kiafrika kuwa moja katika kukabiliana na changamoto za utandawazi; na

KWA KUWA Tanzania ni Nchi iliyodhamiria Kikatiba kufuata mfumo wa


demokrasia ya vyama vingi; na

• Kwa kuwa lengo kuu la mfumo wa demokrasia ya vyama vingi ni kujenga


na kuimarisha nguvu za umma na uwezo wa wananchi mmoja mmoja na
kwa pamoja katika kubadilisha mazingira ya Nchi yao na maisha
wanayoishi; na

• Kwa kuwa lengo hili kuu la kujenga na kuimarisha nguvu za umma na


uwezo wa wananchi linawezekana tu ikiwa wananchi wataungana na
kuongozwa na chama cha siasa imara kisichoyumba kwenye masuala ya
msingi, chama chenye itikadi na sera za kimaendeleo, chama
kinachoweka hai matarajio ya wananchi baada ya uhuru ya kiuchumi na
kijamii, chama kinachopiga vita aina zote za ufisadi kwa kauli na
vitendo na chenye msimamo thabiti wa kujali Nchi na watu wake
kwanza kabla ya maslahi mengine yoyote:

• HIVYO BASI, SISI WANANCHI WAZALENDO tuliokutana hii leo


tarehe ... ... ... jijini Dar es Salaam kutekeleza wajibu wetu Kikatiba wa
kuunganisha pamoja mawazo yetu na kuunda chama cha siasa
kinachozingatia changamoto zote zinazoikabili nchi yetu tangu baada
ya uhuru na kichachobeba matarajio ya wananchi ya leo na kesho, kwa
jina la CHAMA CHA JAMII, kwa kifupi CCJ, ambacho lengo lake kuu ni
kuleta mageuzi ya kitaifa ya kidemokrasia, kiuchumi, kijamii na kisiasa
kwa faida yetu sote sasa na ya vizazi vijavyo.

SURA YA KWANZA

JINA, NEMBO, BENDERA, MAKAO MAKUU, ITIKADI, NA


LUGHA RASMI

• 1. Jina la Chama litakuwa CHAMA CHA JAMII; kwa kifupi CCJ.

• 2. alama kuu katika nembo ya CCJ ni Mikono Iliyoshikana Pamoja


ambayo ni ishara ya nguvu ya umoja.

• 3. bendera ya chama itakuwa na rangi kuu tatu ambazo ni Kijani, Nyeusi


na Dhahabu. Kijani inaashiria kilimo, mazingira na uoto wa asili; Nyeusi
inaashiria watu wa Tanzania; na dhahabu inaashiria rasilmali Nchi.

1. MAKAO MAKUU YA CHAMA yatakuwa katika Jiji la Dar es Salaam na


ofisi nyingine ndogo za makao makuu zitakuwa Zanzibar na Dodoma.
2. ITIKADI YA Chama Cha Jamii ni Ustawi na Hifadhi ya Jamii (social
welfarism), itikadi inayoambatana na demokrasia ya kijamii (social
democracy) na utawala wa katiba na sheria.
3. Lugha rasmi ya chama ni KISWAHILI.

Sura ya pili

IMANI, MALENGO NA MADHUMUNI

1. Chama Cha Jamii kinaamini kwamba:


1.
1. Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa;
2. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na
kuthaminiwa utu wake;
3. Hifadhi na ustawi wa jamii yetu vitapatikana kwa matumizi
bora na endelevu ya utajiri wa rasilimali tulizonazo,
serikali kuwajibika kwa wananchi ambao ni msingi wa
mamlaka yote katika nchi, na kupiga vita ufisadi kwa nguvu
zetu zote;
4. Umoja ni nguvu ya pekee ya wananchi katika kujenga jamii
yenye usawa na uhuru na katika kuondoa umaskini, ujinga,
maradhi na kupambana na ufisadi.

1. Malengo na Madhumuni ya Chama:

• Malengo na Madhumuni ya CCJ yatakuwa kama ifuatavyo:-

1.
1.
1. Kuhakikisha kwamba utajiri wa rasilimali tulizonazo
unatumika kwa maendeleo ya wananchi kwa kuondoa
umaskini, ujinga, na maradhi;
2. Kuhakikisha kwamba uwekezaji unatekelezwa kwa
kumnufaisha mwananchi kutokana na rasilimali alizonazo
na zinazomzunguka na kamwe usitoe fursa kwa wageni
kuhodhi rasilimali hizo bila ushiriki wa wananchi.
3. Kuhakikisha kwamba shughuli za uchumi haziruhusu
ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka
ya watu wachache binafsi;

1.
1.
1. Kujenga umoja wa kitaifa kwa kutoa fursa sawa na za
kutosha kwa wananchi wote wake kwa waume bila kujali
rangi, kabila, dini au hali ya mtu;
2. Kuhakikisha kwamba aina zote za dhuluma, vitisho,
ubaguzi, uonevu, rushwa au ufisadi zinatokomezwa nchini;
3. Kuhifadhi na kuendeleza mazingira kwa ajili ya uhai na
afya ya binadamu na viumbe vingine na kwa faida ya vizazi
vijavyo ;
4. Kulinda haki ya kila raia ya kujielimisha au kutafuta elimu
katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote.
5. Kuhakikisha kuwa mfumo wetu wa uchaguzi ni huru na
unaotoa fursa stahili kwa wananchi kuchagua viongozi
wanaowataka bila kurubuniwa kwa rushwa na takrima za
aina yote yote ile;
6. Kudumisha maadili ya uongozi (uadilifu, uwajibikaji kwa
wananchi na kutenda haki) katika chama na serikali kama
yalivyoainishwa na kusimamiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere katika uongozi wake kitaifa
uliotukuka.


o
 (10) Kushinda katika chaguzi zote zinazofanyika nchini
kwa kutumia ushawishi wa nguvu ya hoja na kuunda
Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika pande zote mbili
za Muungano ili kuiwezesha CCJ kutafsiri malengo na
madhumuni yake kama yalivyoainishwa kwenye ibara hii
kwa vitendo


o

1. kuhakikisha k

Sura ya tatu
UANACHAMA

• 8. Sifa za Mwanachama:


o
1. awe ni raia wa Tanzania;
2. awe na umri usiopungua miaka kumi na nane;
3. awe na akili timamu;
4. awe anaikubali, anaiamini na kuitii Katiba ya CCJ na Kanuni
zilizotungwa chini yake;
5. awe na kadi iliyolipiwa ada stahili za Chama;
6. asiwe mwanachama wa chama kingine cha siasa;

1. Haki za mwanachama;
1.
1. Kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi wa chama wa
ngazi yoyote.
2. Kupata habari zote zilizojadiliwa na kutolewa uamuzi na
wanachama katika kumbukumbu za vikao vinavyomhusu.
3. Kushiriki katika mijadala, shughuli na kazi za chama bila
hofu wala upendeleo.
4. Kutoa mapendekezo au taarifa kwa njia ya mdomo au
maandishi kwenye ofisi yoyote ya Chama ngazi ya Shina,
Tawi, Kata Jimbo na Taifa kwa kuzingatia taratibu
zilizowekwa.
5. Kujitetea mbele ya kikao cha Chama kinachohusika katika
mashitaka au madai yoyote dhidi yake, haki ambayo ni
pamoja na fursa ya kukata rufani kwenye vikao vya juu
iwapo hakuridhika na uamuzi wa kikao cha chini.
6. Kumwona kiongozi yoyote wa Chama kwa kufuata taratibu
zilizowekwa.

1. Wajibu wa mwanachama:
1.
1. Kuwa mkweli, mwaminifu na mwadilifu kwa kauli na vitendo.

1.
1.
1. Kushiriki kikamilifu katika shughuli na uongozi wa Chama
na kueneza sera na programu ya Chama.

1.
1.
1. Kuwa tayari kijikosoa na kukosolewa ili kujiimarisha
kiitikadi na kiuongozi.

1.
1.
1. Kulipa ada za kila mwezi ili kufanikisha shughuli za Chama.
2. Kuhudhuria vikao vya Chama vinavyomhusu.
3. Kujitolea mhanga kufanya shughuli za Chama bila
kutegemea malipo na kuwa tayari kuchanga fedha na mali
kukijenga na kukiimarisha Chama.
4. Kukuza moyo wa ushirikiano na kuheshimu uamuzi wa
pamoja.
5. Kuwa mstari wa mbele katika kupambana na uvunjwaji wa
haki za binadamu, ufisadi na vitendo yanayoharibu maadili
ya jamii.
6. Kujielimisha, kujiendeleza na kujitegemea.
7. Kukilinda chama kutokana na mitafaruku, majungu na
vitendo vya kukigawa na kukidhoofisha Chama.
8. Kuhakikisha kuwa ameandikishwa kama mpiga kura katika
eneo analoishi.

1. Ukomo wa Uanachama:

• Uanachama wa mtu unakoma mambo yafuatayo yakitokea:-

1.
1.
1. Kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe.
2. Kufukuzwa baada ya kukiuka nidhamu, maadili, wajibu na
Katiba ya Chama.
3. Kwa kujiunga na chama kingine cha siasa.
4. Kwa kufariki dunia.


o
 ANGALIZO;

o
 Aliyejiuzulu au aliyefukuzwa uanachama atawajibika
kurejesha mali au amana za Chama alizonazo na
hatarejeshewa ada au mchango wowote aliotoa kwa
Chama. Aidha anaweza kuomba upya uanachama kwa
utaratibu ulioainishwa kwenye kanuni za Chama.

SURA YA NNE

UONGOZI

1. Sifa za kiongozi:
1.
1. Awe na sifa zote za mwanachama kama zilivyoainishwa
kwenye Katiba hii.
2. Awe ana rekodi ya kutetea na kueneza Katiba na sera za
Chama.
3. Awe mchapakazi na mwenye uwezo wa kuongoza.
4. Awe mkweli, mwaminifu, mwadilifu na mnyenyekevu kwa
wananchi wenzake kwa kauli na vitendo, mtetezi na
mpenda haki asiye na historia ya ufisadi au uhalifu wa aina
yoyote ile.
5. Awe na upeo mpana kiakili na kuwa tayari kujiendeleza
yeye binafsi kielimu na kutumia elimu aliyoipata kuleta
mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.
6. Awe na moyo na uwezo wa kufanya kazi na makundi mbali
mbali ya jamii katika mazingira mbali mbali.
7. Awe mtu aliye mstari wa mbele katika kujua matatizo ya
jamii na kuyatafutia ufumbuzi.
8. Awe ni mzalendo na mwenye uchungu na nchi yake na awe
na ushujaa na ushupavu wa kutetea masuala ya msingi
yanayogusa maslahi ya Taifa.
1.
1.
1. Asiwe mtu mwenye tamaa na rekodi ya ukigeugeu katika
siasa.
2. Awe na rekodi ya nidhamu ya kuheshimu vikao, viongozi na
wanachama wenzake.

1. Kuacha Uongozi:

Kiongozi ataacha uongozi ikiwa mambo yafuatayo yatatokea:-

1.
1.
1. Muda wa uongozi umemalizika.
2. Amefukuzwa au kuachishwa kutokana na kukiuka Katiba ya
Chama, maadili, wajibu, nidhamu au sera za Chama.
3. Amejiuzulu mwenyewe kwa sababu zake binafsi.
4. Amejiuzulu kutokana na uamuzi wa wanachama walio wengi
anaowaongoza kufuatia kupigiwa kura ya kutokuwa na
imani naye na uongozi wake kwa mujibu wa Kanuni za
Chama.
5. Kupatikana na hatia mahakamani kwa kosa ambalo chama
kitaona halistahili kutendwa na kiongozi wa chama.
6. Kwa kufariki.

1. Haki za Kiongozi;

Kiongozi atakuwa na haki zifuatazo:-

1.
1.
1. Kujitetea katika kikao kinachoamua tuhuma dhidi yake.
2. Kupinga hatua ya kufukuzwa uongozi kwa kukata rufani
kwenye kikao cha juu iwapo hakuridhika na uamuzi wa
kikao cha chini.
SURA YA NNE VIKAO VYA CHAMA

1. Muundo wa vikao vya Chama:

• Vikao vya chama vitakuwa kwa ngazi zifuatazo:-


1.
1.
1. Shina
2. Tawi
3. Kata/ Shehia
4. Jimbo, na;
5. Taifa

1. Shina:
1.
1. Litakuwa ngazi ya mwanzo kabisa katika muundo wa CCJ,
ngazi ambayo itakuwa na wanachama wasiopungua watano
na wasiozidi thelathini.
2. Litakuwa na vikao viwili tu, yaani Mkutano wa Shina
unaofanyika mara moja katika miezi mitatu na Mkutano wa
Mwaka wa Shina.
3. Shina linaweza kuitisha mikutano maalum wakati wowote
kufuatana na hali inayojitokeza.
4. Wajumbe wa Mikutano ya Shina:


o
1. Mwenyekiti wa Shina (Balozi),
2. Katibu wa Shina,
3. Wanachama wote wa Shina husika.

1.
1.
1. Kazi za Mikutano ya Shina


o

1. Kumchagua Mwenyekiti wa Shina (Balozi) na Katibu
wa Shina unapofika wakati wa Uchaguzi.
2. Kusimamia shughuli za Chama katika Shina hilo.
3. Kutekeleza maamuzi na maelekezo ya kikao cha juu
yake.


1.
1.
1. Kazi za Mwenyekiti wa Shina (Balozi)


o

1. Kuongoza mikutano ya Shina.
2. Kusimamia shughuli za kila siku za Chama katika
Shina.

(7) Kazi za Katibu wa Shina


o

 (a) Kuchukua na kutunza kumbukumbu za mikutano.


o
1.
1. Kutunza daftari la orodha na kumbukumbu za
wanachama waliopo katika shina.
2. Kukusanya ada za chama na kuziwasilisha kwa
Mtunza Hazina wa Tawi baada ya kumpatia
mwanachama risiti ya ada aliyotoa.


1.
1. Kuwajibika na kutoa taarifa kila mwezi kuhusu utendaji wa
shughuli za Chamakatika shina kwa ngazi ya Tawi.

1. Tawi

1.
1.
1. Litakuwa na wanachama wasiopungua 30 na wasiozidi 150.
2. Kutakuwa na tawi katika kila eneo la serikali ya mtaa kwa
mijini na tawi katika kila eneo la serikali ya kijiji.
3. Vikao vya tawi:


o

 (a) Mkutano wa Tawi


o
1.
1. Kamati ya tawi
2. Wajumbe wa Mkutano wa Tawi


o

1. Mwenyekiti.
2. Katibu.
3. Mweka Hazina.
4. Mwenyekiti wa mtaa/kijiji aliyechaguliwa kwa tiketi
ya CCJ.
5. Wenyeviti wa vitongoji vilivyopo katika tawi
waliochaguliwa kwa tiketi ya CCJ.
6. Mwenyekiti na wajumbe wa serikali ya mtaa au kijiji
na wa kila serikali ya kitongoji aliyechaguliwa kwa
tiketi ya CCJ.
7. Wenyeviti na Makatibu wa vitengo vya chama.
8. Wanachama wote kutoka mashina yaliyopo katika
tawi hilo.


o
1. Kazi za Mkutano wa Tawi.


1.
1. Kupokea taarifa ya Kamati ya tawi.
2. Kuchagua Mwenyekiti wa tawi na Mtunza Hazina wa tawi
unapofika wakati wa uchaguzi.
3. Mkutano wa Tawi utafanyika angalau mara moja katika kila
miezi sita.


o
1. Wajumbe wa Kamati ya Tawi:
1. Mwenyekiti.
2. Katibu.
3. Mweka Hazina.
4. Mwenyekiti wa mtaa/ kijiji aliyechaguliwa kwa
tiketi ya CCJ.
5. Wenyeviti wa vitongoji vilivyopo katika tawi
waliochaguliwa kwa tiketi ya CCJ.
6. Wenyeviti na makatibu wa vitengo vya chama
vilivyopo katika tawi hilo.
7. Wenyeviti wa mashina (Mabalozi) waliopo katika
tawi hilo, isipokuwa wale ambao idadi ya wanachama
wao ni chini ya watano.


o
1. Kazi za Kamati ya Tawi:


o
1.
1. Kuendesha shughuli za kila siku za Chama.
2. Kusimamia utekelezaji wa sera za chama.
3. Kubuni na kusimamia vyanzo vya mapato ya tawi na
miradi ya chama.
4. Kusimamia matumizi ya fedha katika shughuli za
chama.
5. Kuwasilisha mawazo ya wanachama kwa wananchi.
6. Kuwahimiza wananchi kujiandikisha, kufanya
kampeni na kuhakikisha kuwa chama kinapata
ushindi.
7. Kuwaandaa wanachama kushirikiana na wananchi
wengine katika kuleta demokrasia ya kweli na
maendeleo kwa kushirikiana na vyama vya kijamii.
8. Kutafuta wanachama wapya.
9. Kusimamia ustawi wa mashina yaliyopo katika tawi
hilo.
10. Kujadili maombi na kuteua wagombea uongozi wa
chama ngazi ya shina.
11. Kuchagua Mweka Hazina wa tawi.
12. Kuandaa Mkutano wa tawi.
13. Kuongoza katika eneo lake, harakati za kupinga
uonevu unaoweza kufanywa na serikali au kikundi
chochote na kuwaelekeza wananchi jinsi ya kupata,
kutetea na kulinda hazi zao.
14. Kumjadili aliyejiuzulu uanachama na ambaye
ameomba kurudi katika chama na kutoa
mapendekezo kwa kamati ya Wilaya.
15. Kujadili maombi ya wanaoomba kugombea uongozi
wa serikali za mitaa na kuyawasilisha kwa Katibu wa
Kata/Shehia wa chama.
16. Kuteua wajumbe watano wa kamati ya nidhamu.
17. Kamati ya Tawi itakutana angalau mara moja katika
kila miezi mitatu


o
1. Kazi za Katibu wa Tawi.


o
1.
1. Kutunza daftari la orodha na kumbukumbu za
mashina na wanachama waliopo katika mashina ya
tawi hilo.
2. Kutunza kumbukumbu za mali za chama
zisizoondosheka na zinazoondosheka na
kumbukumbu nyinginezo muhimu.
3. Kusimamia vyanzo vya mapato na miradi ya chama
iliyopo katika tawi hilo.
4. Kuwajibika na kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu
utendaji wa kazi za chama katika tawi kwa ngazi
ya kata.

1. Kata/Shehia:

1.
1.
1. Kata/shehia itakuwa na kikao cha Kamati ya kata/shehia.


1.
1.
1. Wajumbe wa Kamati ya kata/shehia.


o

 (a) Mwenyekiti.


o
1.
1. Katibu.
2. Mweka Hazina.
3. Diwani wa kata/shehia hiyo aliyechaguliwa kwa
tiketi ya CCJ.
4. Wenyeviti wa matawi yaliyopo katika kata/shehia
hiyo.
5. Wenyeviti wa matawi yaliyopo katika kata/shehia.
6. Katibu wa kitengo cha wanawake wa kata/shehia
hiyo.
7. Wanawake wenyeviti wa mitaa au vijiji au vitongoji
vya kata/shehia hiyo walichaguliwa kwa tiketi ya
CCJ.


o
1. Kazi za kamati ya Kata/Shehia:


o

1. Kuwachagua Mwenyekiti na Mtweka Hazina wa
kata/shehia unapofika wakati wa uchaguzi.
2. Kuteua makatibu wa matawi ya chama yaliyopo
katika kata/shehia hiyo kutokana na mapendekezo
ya katibu wa chama wa kata/shehia.
3. Kujadili maombi na kuteua wagombea nafasi za
uongozi katika matawi ya chama yaliyopo katika
kata/shehia hiyo.
4. Kujadili maombi na kuteua wagombea uongozi katika
serikali za mitaa, vijiji na vitongoji zilizo katika
kata/shehia hiyo.
5. Kujadili maombi na kutoa mapendekezo kuhusu
wanaoomba kugombea udiwani na kuyawasilisha kwa
katibu wa chama wa wilaya.
6. Kusimamia utekelezaji wa shughuli za chama katika
kata/shehia hiyo.
7. Kubuni na kusimamia vyanzo vya mapato na miradi
ya chama.
8. Kusimamia matumizi ya fedha za chama katika
kata/shehia hiyo.
9. Kutoa mikakati na miongozo kuhusu maendeleo ya
chama katika kata/shehia hiyo.
10. Kupima utekelezaji wa shughuli za chama katika
matawi ya chama ya kata/shehia hiyo.
11. Kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufani za
wanachama na viongozi toka matawi ya chama ya
kata/shehia hiyo.
12. Kubuni mikakati na kuhamasisha kwa shabaha ya
chama kupata kuungwa mkono na watu.
13. Kuhamasisha wanachama kugombea uongozi na watu
kujiandikisha na kupiga kura, kufanya kampeni kwa
ustadi na kuhakikisha kwamba chama kinapata
ushindi wakati wa uchaguzi
14. Kutathmini maendeleo ya kata/shehia na kutoa
msimamo na mapendekezo ya chama kwa
wanaohusika.
15. Itafanya angalau kikao kimoja katika kila miezi
mitatu.


o
1. Kazi za Katibu wa kata/shehia:

o

1. Kutunza orodha ya matawi, idadi ya mashina na
wanachama wa kila tawi lililoko katika kata/shehia
hiyo.
2. Kutunza kumbukumbu za mali za chama
zisizoondosheka na zinazoondosheka zilizopo katika
au chini ya ofisi ya chama ya kata/shehia hiyo.
3. Kuwajibika na kutoa taarifa za kila mwezi kuhusu
utendaji wa shughuli za chama katika sheia kwa
ngazi ya Wilaya.

1. Jimbo


o
1.
1.
1. Jimbo litakuwa na Vikao vya vifuatavyo:


o
1. Mkutano wa Jimbo.
2. Kamati ya Jimbo.


1. Wajumbe wa Mkutano wa Jimbo:


o

 (a) Mwenyekiti.


o

 (b) Katibu.


o

1. Mweka Hazina .
2. Wenyeviti na Makatbu wa kata/shehia.
3. Mbunge au Wabunge waliochaguliwa kwa tiketi ya
CHAMA CHA UMOJA WA TANZANIA katika
Jimbo hilo.
4. Mwakilishi au Wawakilishi waliochaguliwa kwa tiketi
ya CCJ katika Jimbo hilo.
5. Madiwani waliochaguliwa kwa tiketi ya CCJ katika
Jimbo hilo.
6. Wenyeviti na Makatibu wa Jimbo wa vitengo vya
Chama.


1. Kazi za Mkutano wa Jimbo:.


o
1.
1. Kutoa mikakati na miongozo kwa ajili ya maendeleo
ya chama katika Jimbo hilo.
2. Kupima utekelezaji wa shughuli za chama katika
Jimbo hilo.
3. Kutathmini maendeleo ya Jimbo hilo.
4. Kumchagua Mwenyekiti wa Chama wa Jimbo.
5. Mkutano wa Jimbo utafanyika angalau mara moja
katika kila miaka miwili.
2. Wajumbe wa Kamati ya Jimbo:


o

1. Mwenyekiti.
2. Katibu.
3. Mweka Hazina.
4. Mbunge au Wabunge waliochaguliwa kwa tiketi ya
CCJ katika Jimbo hiloo.
5. Mwakilishi au Wawakilishi waliochaguliwa kwa tiketi
ya CCJ katika Jimbo hilo.
6. Meya au Naibu Meya au Mwenyekiti au Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya jiji au manispaa au
mji au wilaya au Mwenyekiti wa madiwani
waliochaguliwa kwa tiketi ya CCJ katika wilaya
husika.
7. Wenyeviti wa Jimbo hilo wa vitengo vya Chama.
8. Wenyeviti wa kata/shehia wa Chama wa Jimbo hilo.
9. Madiwani waliochaguliwa kwa tiketi ya CCJ katika
Jimbo hilo.


o
1. Kazi za Kamati ya Jimbo:


o

1. Kukisimika Chama katika jamii kwenye Jimbo.
2. Kutekeleza sera na kazi za chama katika Jimbo hilo.
3. Kubuni na kusimamia vyanzo vya mapato ya Chama
katika Jimbo hilo.
4. Kuweka leja ya wanachama na ya viongozi wa chama
katika Jimbo.
5. Kutathmini maendeleo katika Jimbo hilo na kutoa
msimamo na mapendekezo kwa wanaohusika.
6. Kumchagua Mweka Hazina wa Jimbo.
7. Kubuni mikakati ya kuhamasisha watu kwa shabaha
ya kuungwa mkono.
8. Kujadili au kupendekeza wanaoomba kugombea
Ubunge au Uwakilishi na kupeleka mapendekezo kwa
Kamati Kuu.
9. Kujadili na kupendekeza wanaoomba kugombea
uongozi wa Chama ngazi za wilaya na taifa na
kupeleka mapendekezo kwa Kamati Kuu.
10. Kujadili maombi na kuteua wagombea uongozi wa
Chama ngazi ya kata/shehia.
11. Kujadili maombi na kuteua wagombea udiwani katika
Jimbo hilo.
12. Kuhakikisha kwamba wakati wa uchaguzi kampeni
inafanywa kwa ustadi na Chama kupata ushindi.
13. Kuteua makatibu wa Chama wa kata kutokana na
mapendekezo ya katibu wa Jimbo.
14. Kujadili na kupitisha uamuzi juu ya maombi ya
waliojiuzulu au kufukuzwa kujiunga tena na Chama.
15. Kuwaondoa madarakani viongozi wa ngazi ya
kata/shehia kwa sababu za kukiuka katiba, kanuni,
maadili, nidhamu na sera za Chama..
16. Kujadili na kuamua rufani za wanachama na viongozi
kutoka ngazi za chini.
17. Kuchunguza mwenendo wa viongozi na wanachama
katika Jimbo hilo na kutoa adhabu pale ambapo
hapana budi.
18. Kuelekeza na kusimamia maandalizi ya umma kwa
ajili ya uchaguzi ili kukipatia Chama ushindi.
19. Kufanya maandalizi ya Mkutano wa Jimbo.
20. Kuwajibika na kutuma kwa ngazi ya taifa taarifa
za kila mwezi kuhusu utekelezaji wa shughuli za
Chama katika Jimbo.
21. Kamati ya Jimboa itafanya angalau kikao kimoja
katika kila miezi mitatu.

1. Taifa

1.
1.
1. Kutakuwa na vikao vifuatavyo katika ngazi ya Taifa:


1.
1. Mkutano wa Taifa.
2. Kamati Kuu.
2. Wajumbe wa Mkutano wa Taifa:

o

1. Mwenyekiti.
2. Makamu Mwenyekiti (Bara).
3. Makamu Mwenyekiti (Zanzibar).
4. Katibu Mkuu.
5. Naibu Katibu Mkuu (Bara).
6. Naibu katibu Mkuu (Zanzibar).
7. Mweka Hazina.
8. Wajumbe wa Kamati Kuu.
9. Makamisaa wa chama.
10. Wakuu wa Vyuo vya Chama.
11. Wenyeviti wa Chama wa Majimbo.
12. Wenyeviti na Makatibu wa Taifa wa vitengo vya
Chama.


1. Kazi za Mkutano wa Taifa:


o

1. Kuchagua Mwenyekiti wa Chama wa Taifa.
2. Kuchagua Makamu Mwenyekiti wa Chama wa Taifa
kwa ajili ya Tanzania bara na Makamu Mwenyekiti
wa Chama wa taifa kwa ajili ya Tanzania Zanzibar.
3. Kuchagua wajumbe wanane wa Kamati Kuu ambao
kati yao watano watakuwa wanatoka Tanzania Bara
na watatu watakuwa wanatoka Tanzania Zanzibar.
4. Kuchagua wajumbe watatu wa Kamati Kuu
wanawake, wawili kutoka Tanzania Bara na mmoja
kutoka Tanzania Zanzibar.
5. Kutunga na kurekebisha katiba ya chama.
6. Katiba na marekebisho yoyote ya katiba ya chama
yatafanywa kwa kuungwa mkono na kura
zisizopungua theluthi mbili ya wajumbe
watakaokuwa wamehudhuria mkutano uliokusudiwa
kufanya marekebisho hayo.
7. Kujadili na kuteua wagombea urais wa Jamuhuri
ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa tiketi ya CHAMA CHA JAMII.
8. Kupokea, kutafakari, kubadili au kukataa taarifa ya
kazi za chama itakayotolewa na Kamati Kuu.
9. Kutoa maelekezo kuhusu utekelezaji itikadi, sera na
malengo ya Chama.
10. Kumwondoa madarakani kwa mapendekezo ya
Kamati Kuu kiongozi yeyote kwa kura zaidi ya nusu
ya wajumbe waliohudhuria zitakazokuwa zinaunga
mkono.
11. Mkutano Mkuu wa Taifa utafanyika kila baada ya
miaka mitano isipokuwa kama kuna suala la dharura
Mkutano maalum wa taifa unaweza kuitishwa kwa
agizo la Kamati Kuu.


1. Wajumbe wa Kamati Kuu:


o
1. Mwenyekiti.
2. Makamu Mwenyekiti (Bara).
3. Makamu Mwenyekiti (Zanzibar).
4. Katibu Mkuu.
5. Naibu Katibu Mkuu (Bara).
6. Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar).
7. Mtweka Hazina.


o

1. Wajumbe watano kutoka Bara.
2. Wajumbe watatu kutoka Zanzibar.
3. Wajumbe watatu wanawakewawili kutoka bara na
mmoja kutoka Zanzibar.
4. Wenyeviti wa vitengo vya chama.
5. Wajumbe watatu walioteuliwa na Mwenyekiti.

1. Kazi za Kamati Kuu:


o

1. Kuchagua Katibu Mkuu.
2. Kuchagua Mweka Hazina.
3. Kuteua, kubadilisha, kusimamisha na kuondoa
wadhamini wa chama.
4. Kuteua Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini.
5. Kuteua Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu.
6. Kuteua na kuondoa Makamisaa na makatibu wa
Majimbo kutokana na mapendekezo ya Katibu
Mkuu.
7. Kujadili na kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa
Taifa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na urais wa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa tiketi ya CCJ.
8. Kujadili na kuteua wagombea Ubunge, Uwakilishi
na Uspika kwa tiketi ya CCJ.
9. Kutoa uamuzi wa mwisho juu ya maombi ya
wanachama wanaojiunga upya na Chama baada ya
kufukuzwa uanachama.
10. Kupanga shughuli za Chama.
11. Kutunga sera za chama kuhusu uchumi na maendeleo
ya jamii zitakazogusa kila sekta na kuziwasilisha
mbele ya Mkutano wa Taifa.
12. Kutekeleza sera za chama kama zilivyopitishwa na
Mkutano wa Taifa.
13. Kufuatilia mkoa hadi mkoa kuhakikisha kwamba sera
za chama zinatekelezwa kikamilifu na kuwa na
matokeo yaliyokusudiwa.
14. Kutathmini utekelezaji wa shughuli zote za chama
nchini.
15. Kupokea na kuchambua taarifa ya mapato na
matumizi ya Chama ya mwaka uliopita na taarifa ya
wakaguzi wa hesabu za Chama.
16. Kuandaa kupitia sekretariati nakala maalum za
kitaalam kuhusu maendeleo ya Taifa, na masuala
mbalimbali yanayoigusa jamii kwa ajili ya kujadiliwa
na kupitishwa na Mkutano wa Taifa.
17. Kuweka kanuni na taratibu kuhusu vifaa, fedha,
uchaguzi, uajiri, nidhamu, uenezi, vitengo na mambo
mengine ambayo itaona inafaa kuyawekea kanuni na
taratibu.
18. Kutunga ilani ya uchaguzi ya chama.
19. Kubuni, kujenga na kudumisha uhusiano mwema kati
ya chama na wananchi na kuwaelimisha kuhusu sera,
malengo na mwelekeo wa chama.
20.Kupanga ada za chama na michango ya kitaifa kwa
shughuli mbalimbali za chama.
21. Kupendekeza kwa Mkutano wa Taifa marekebisho
ya katiba ya chama.
22.Kuonya, kusimamisha au kuondoa madarakani
kiongozi yeyote wa Chama wa ngazi ya Jimbo.
23.Kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa Taifa,
Makamu Mwenyekiti wa Taifa na kiongozi yo yote
wa Taifa anayewajibika kwa Mkutano Mkuu.
24.Kamati Kuu itakutana angalau mara moja katika kila
miezi minne.


1. Kamati Maalum ya Kamati Kuu:


o

1. Itakuwa ni sehemu ya Kamatu Kuu.
2. Itafanya kazi yake kwa maelekezo ya Kamati Kuu
3. Itawajibika kwa Kamati Kuu.
4. Itafanya kazi yake katika eneo la Tanzania
Zanzibar.
5. Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) atakuwa
mwenyekiti wa kikao na Naibu Katibu Mkuu
(Zanzibar) atakuwa katibu wa kikao.


1. Wajumbe wa Kamati Maalum ya Kamati Kuu:


o

1. Makamu Mwenyekiti (Zanzibar).
2. Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar).
3. Wajumbe wa Kamati Kuu toka Tanzania Zanzibar
4. Wenyeviti / Makamu wenyeviti/ Makatibu wakuu,
Naibu Makatibu wakuu wa Taifa wa vitengo vya
chama Zanzibar.
5. Wenyeviti wa Wabunge na Wawakilishi
waliochaguliwa kwa tiketi ya CCJ katika Zanzibar.
6. Makatibu wa CCJ wa mikoa ya Tanzania Zanzibar.


1. Kazi za Kamati Maalum ya Kamati Kuu:


o

1. Kuunda sekretariati chini ya Naibu Katibu Mkuu
(Zanzibar) na kuipa majukumu kwa namna
itakavyoona inafaa kwa Zanzibar
2. Kuchagua katibu wa sekretariati ya Kamati Maalum
ya Kamati Kuu
3. Kumchagua Mweka Hazina
4. Kupanga shughuli za Chama katika Zanzibar
5. Kutekeleza sera za chama kama zilivyopitishwa na
Mkutano wa Taifa
6. Kuweka ufuatiliaji wa kutosha mkoa hadi mkoa
kuhakikisha kwamba kazi za chama zinatekelezwa
kikamilifu na kuwa na matokeo yaliyokusudiwa.
7. Kutathmini utekelezaji wa shughuli zote za Chama
katika Zanzibar.
8. Kubuni, kujenga na kudumisha uhusiano mwema kati
ya Chama na wananchi na kuwaelimisha juu ya sera,
malengo na mwelekeo wa Chama.
9. Kujadili na kutoa maoni kwa Kamati Kuu juu ya
wanachama wanaoomba kugombea urais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
10. Kamati Maalumu ya Kamati Kuu itafanya kikao
angalau mara moja katika kila miezi minne.


o SURA YA TANO


o SEKRETARIATI YA KAMATI KUU

1. Sekretariati ya Kamati Kuu:


1.
1. Sekretariati ya Chama itaundwa na kupewa majukumu na
Kamati Kuu kwa namna itakavyoona inafaa.
2. Katibu Mkuu atakuwa kiongozi wa Sekretariati, atakuwa
na uwezo wa kupanga, kubadilisha na kuwaondoa wajumbe
wa sekretariati bila kuathiri misingi ya kuundwa kwa
sekretariati iliyowekwa na Kamati Kuu.
3. Naibu Katibu Mkuu (Bara/Zanzibar) atakuwa katibu wa
vikao vya sekretariati iliyowekwa na Kamati Kuu.
2. Sekretariati ya Kamati Maalum ya Kamati Kuu:
1.
1. Itaundwa na kupewa majukumu na Kamati Maalum ya
Kamati Kuu kwa namna itakavyoona inafaa.
2. Itashughulikia masuala ya Chama katika Zanzibar.
3. Naibu Katibu Mkuu atakuwa kiongozi wa Sekretariati,
atakuwa na uwezo wa kupanga, kubadilisha, na kwaondoa
wajumbe wa sekretariati bila kuathiri misingi ya kuundwa
kwa sekretariati iliyowekwa na Kamati Maalum ya Kamati
Kuu.
4. Katibu wa vikao vya Sekretariati atachaguliwa na Kamati
Maalum ya Kamati Kuu.

SURA YA SITA
VITENGO VYA CHAMA

1. Chama kitakuwa na vitengo vifuatavyo:


o
1. Vijana.
2. Wanawake.
3. Wazee.
4. Wabunge na Wawakilishi.

1. Vitengo vyote vya Chama vitakuwa chini ya uongozi wa Chama wa ngazi


husika na vitawajibika pale.
1. Kila kitengo kitatunga kanuni Za kusimamiwa uendeshaji wa kitengo na
kanuni hizo zitaanza kutumika baada ya kupitishwa na Kamati Kuu.

SURA YA SABA BARAZA LA WADHAMINI

26. Kutakuwa na Baraza la Wadhamini wa Chama.


1.
1.
1. Wajumbe wa Baraza la Wadhamini:


o
1.
1. Mwenyekiti.
2. Katibu (Mweka Hazina wa Chama).
3. Wajumbe watano.


1. Mamlaka ya uwezo wa Baraza la Wadhamini.


o

1. Baraza litakuwa na mamlaka na uwezo wa kuyatumia
hayo mamlaka kama ilivyopewa na sheria ya
wadhamini.
2. Baraza litafanyaka kazi zake chini ya usimamizi na
maelekezo ya Kamati Kuu na litatoa taarifa ya
shughuli zake kwake.
3. Mdhamini atakuwa kwenye nafasi ya udhamini kwa
muda wa miaka mitano na aweza kuteuliwa
kuendelea na nafasi hiyo baada ya kipindi chake
kumalizika.


o
1. Mdhamini anaweza kuondolewa katika Baraza na Kamati
Kuu ikiwa:
2.
1. Ana afya mbaya kiasi cha kushindwa kufanya kazi
zake.
2. Ameonyesha uwezo mdogo katika kutekeleza
majukumu yake.


o
1.
1. Kama ameishi nje ya nchi kwa miaka miwili
mfululizo.
2. Kama atakuwa amekiuka Katiba na maadili ya Chama.
3. Kama atapatikana na hatia ya kosa ambalo kamati
Kuu itaridhika kuwa halikustahili kufanywa na
mdhamini wa chama.
4. Kama atafilisiwa na kushindwa kujikomboa katika
kipindi cha miezi sita.
2. Madhamini atajiuzulu kutoka katika Baraza kwa kutoa
tamko la maandishi kwa Kamati Kuu kupitia kwa
Mwenyekiti wa Baraza.
3. Kama itatokea nafasi wazi kutokana na kifo,
4. Kujiuzulu au kufukuzwa kwa mdhamini, nafasi hiyo
itajazwa mara moja kufuatana na taratibu za Katiba hii na
sheria inayotumika.
5. Kama Mwenyekiti wa Baraza atashindwa kuhudhuria vikao,
wajumbe watamchagua mmojawapo kati yao kuwa
Mwenyekiti wa kikao cha siku hiyo.
6. Mwenyekiti wa Baraza atakuwa na haki ya kutumia kura
yake, mbali na ile yake ya kawaida, kuamua pindi kura za
wajumbe zikifungana.


1. Kazi za Baraza la Wadhamini:


o
1.
1. Kuweka chini ya uangalizi wake mali zote za Chama
zinazoondosheka na zisizoondosheka.
2. Kuingia katika shughuli zozote za Uchumi ambazo
zinaendana na madhumuni na malengo ya chama kwa
kibali cha Kamati Kuu.
3. Kuunda Kamati ndogo ndogo na kukasimu kwa kamati
hizo madaraka yake ya utendaji na utekelezaji wa
shughuli zake.
4. Kutoa taarifa ya utendaji ya mwaka katika kikao
cha Kamati Kuu.


o

1. Bila ya kuathiri masharti ya Sheria na Kanuni ya
Baraza la Wadhamini, Baraza linaweza kuitisha
mkutano maalumu pale itakapolazimu ni lazima
kufanya hivyo.

Sura ya nANE

Viongozi wakuu wa chama

1. Viongozi Wakuu wa Chama watakuwa:



1.
1. Mwenyekiti wa Chama wa Taifa.
2.
1. Makamu Mwenyekiti wa Chama - Tanzania Bara.
2. Makamu Mwenyekiti wa Chama - Tanzania Zanzibar.
3. Katibu Mkuu.
4. Naibu Katibu Mkuu - Tanzania Bara.


o
1.
1. Naibu Katibu Mkuu - Tanzania Zanzibar.
2. Mweka Hazina.

27. Mwenyekiti


1.
1. Atakuwa msemaji Mkuu wa Chama na kiungo cha vikao
vyote vya Taifa.
2. Atakuwa ndiye mhamasishaji Mkuu wa Chama.
3. Atachaguliwa na Mkutano wa Taifa.
4. Atakuwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Taifa na Kamati Kuu.
Utakapofika wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya wa
ngazi ya Taifa, atachaguliwa Mwenyekiti wa muda wa
kuongoza kikao badala ya Mwenyekiti ambaye muda wake
unamalizika.
5. Ataweza kuondolea kwenye madaraka baada ya
mapendekezo ya Kamati Kuu kwa azimio la Mkutano wa
Taifa kwa theluthi mbili za kura za wajumbe
waliohudhuria mkutano huo.

1. Makamu Wenyekiti.


1.
1. Makamu Mwenyekiti atakayetokea Zanzibar atafanya
zaidi shughuli za chama Zanzibar na anayetoka Bara
atafanya zaidi shughuli za Chama Bara.
2.
1. Watakuwa wasaidizi wakuu wa Mwenyekiti wa Taifa.
2. Watachaguliwa na Mkutano wa Taifa.
3. Watashika nafasi hiyo kwa miaka mitano bali waweza
kuchaguliwa tena baada ya kipindi hicho kumalizika.
4. Wataweza kuondolewa kwenye madaraka baada ya
mapendekezo ya Kamati Kuu kwa azimio la Mkutano wa
Taifa kwa zaidi ya nusu ya kura za wajumbe waliohudhuria
mkutano huo
5. Watakuwa wajumbe wa Mkutano wa Taifa na Kamati Kuu.
6. Watahusika zaidi na shughuli za uhamasishaji na kampeni
za Chama.

30. Katibu Mkuu.


1.
1. Atachaguliwa na Kamati Kuu ya Taifa.
2. Atakuwa Katibu wa vikao vya Mkutano wa Taifa na Kamati
Kuu.


1.
1. Ataratibu na kusimamia shughuli zote za sekretariati na
atakuwa mwenyekiti wa sekretariati.

Atakuwa mtendaji mkuu wa chama na hivyo:


o
1.
1. Atakuwa na uwezo wa kurekebisha , kupanga,
kupangua au kuondoa wajumbe wa sekretariati bila
kuathiri misingi ya kuundwa kwa sekretariati
iliyowekwa na Kamati Kuu.
2. Atakuwa na uwezo wa kuajiri, kufukuza na
kusimamia nidhamu ya watumishi wote wa Chama
kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu za Chama.
3. Atawajibika kuitisha vikao vyote baada ya
kushauriana na Mwenyekiti wa Chama.
4. Anaweza kuondolewa au kusimamishwa utendaji
kwenye nafasi hiyo na Kamati Kuu.
5. Atapewa nafasi ya kujitetea dhidi ya tuhuma au
madai ya aina yeyote kabla ya kuchukuliwa hatua.
6. Ataajiri watumishi katika Ofisi yake kwa idhini ya
Kamati Kuu.

1. Manaibu Katibu Wakuu.


1.
1. Watachaguliwa na Kamati Kuu na watakuwa wajumbe wa
Kamati Kuu.
2.
1. Mmojawapo atamsaidia Katibu Mkuu na kukaimu kiti chake
wakati Katibu Mkuu hayupo.
2. Watafanya kazi nyingine zote watakazopewa na Katibu
Mkuu.
3. Naibu Katibu Mkuu kutoka Zanzibar atafanya zaidi
shughuli zake huko Tanzania Zanzibar na anayetoka Bara
atafanya zaidi shughuli za Chama Tanzania Bara.

1. Mweka Hazina:


1.
1.
1. Atakuwa katibu wa Baraza la Wadhamini.
2.
1.
1. Atadhibiti mapato na matumizi ya fedha za Chama.
SURA YA TISA


o
 WAGOMBEA URAIS

1. Masharti kuhusu Mgombea Urais:


1.
1. Awe ametimiza masharti ya Katiba ya nchi kuhusu
mgombea wa kiti cha Urais.
2.
1. Awe tayari ni mwanachama wa CCJ aliyetimiza sifa za
kuwa Kiongozi na awe amejihusisha katika uongozi wa aina
yoyote katika jamii.
2. Aungwe Mkono na wanachama wasiopungua mia mbili.
3. Awa anaelewa Katiba na Sera za Chama.
4. Atateua kwa kushirikiana na Kamati Kuu, mwanachama
mwenye sifa zinzokubalika kichama kuwa mgombea
mwenza wakati wa Kampeni za Urais.
5. Atateuliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa kwa mapendekezo
ya Kamati Kuu ya Chama.
6. Iwapo mgombea Urais atashinda, basi ndiye atakuwa
mtunzaji na msimamizi wa Sera za Chama serikalini.
7. Isipokuwa kwa masharti ya ibara ndogo ya (5) ya ibara
hii masharti haya yanamhusu pia mgombea Urais
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

SURA YA KUMI MAMBO YA JUMLA

1. Taasisi na nafasi nyingine za chama


(1) Kutakuwa na taasisi za Chama kama ifuatavyo:
(i) Vyuo vya Chama
(ii) Kampuni za uchumi za Chama
(iii) Vyombo vya habari vya Chama


(2) Kamati Kuu itaunda taasisi zilizoorodheshwa katika Ibara ya 34 (1)
na itakuwa na mamlaka ya kuunda taasisi nyingine yoyote ambayo
haijaorodheshwa katika ibara ndogo hii, kama itakavyoona inafaa kwa
masilahi na maendeleo ya Chama.

• (3) Makamisaa wa Chama


(i) Makamisaa wa Chama ni makada maalumu watakaoteuliwa na Kamati
Kuu kila itakapoona inafaa kutekeleza majukumu maalumu ya kisiasa na
kiutendaji.
(ii) Kamati Kuu itakuwa na mamlaka ya kuunda nafasi na kuteua
mwanachama kuishika nafasi hiyo kwa maslahi na maendeleo ya Chama.

1. Uchaguzi:
1.
1. Uchaguzi wa viongozi wa chama utafanyika kila baada ya
miaka mitano

1.
1.
1. Katika uchaguzi kila ngazi ya uongozi kuanzia Shina hadi
Wilaya itasimamiwa na ngazi ya juu yake na ngazi ya Taifa
itajiwekea utaratibu wake.
2. Ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutokana na aliyekuwa
ameshikilia nafasi hiyo kujiuzulu au kufariki au kufukuzwa
kwa mujibu wa katiba hii, uchaguzi unaweza kufanyika
wakati wowote kabla ya miaka mitano kupita.
3. Uchaguzi wa Chama ngazi zote utakuwa kwa kura za siri.
4. Wakati wa mkutano wa uchaguzi, Mwenyekiti wa muda
ambaye siyo mgombea atachaguliwa kuongoza mikutano.

1. Akidi ya vikao:

• Akidi ya kila kikao cha Chama itakuwa nusu ya wajumbe wanaostahili


kuhudhuria kikao hicho.

1. Uitishaji wa vikao:

• Kila kikao cha Chama kitaitishwa na katibu baada ya kushauriana na


kukubaliana na Mwenyekiti wa kikao hicho.
1. Mjumbe wa kikao kupoteza sifa:

• Mjumbe ambaye hatahudhuria vikao vitatu mfululizo bila udhuru kwa


uongozi unaohusika au sababu inayokubalika atakuwa amejivua ujumbe
katika kikao hicho.

1. Ratiba ya Vikao:

Kila kikao cha Chama kitafanyika katika muda uliotajwa katika katiba hii
isipokuwa likitokea jambo la dharura linalohitaji kikao kifanyike.

1. Vikao kukasimu mamlaka na madaraka:

1.
1.
1.
1. Kikao chochote cha Chama kinaweza kukasimu
mamlaka na madaraka yake kwa kikao kilicho chini
yake.
2. Katika kufanikisha shughuli zake kikao chochote
cha chama kinaweza kuunda kamati au tume kwa
ajili hiyo na kamati au tume hiyo itapewa hadidu za
rejea na kikao hicho na kuwajibika kwa kikao hicho.

1. Kukaimu Madaraka:

Iwapo mwanachama kiongozi yeyote, kwa sababu yoyote ile hawezi kutekeleza
kazi zake kwa muda au amesimamishwa au amevuliwa madaraka kwa mujibu wa
katiba, kanuni na taratibu za Chama, mamlaka iliyo na uwezo wa uchaguzi au
uteuzi wa nafasi hiyo inaweza kumteua mwanachama mwenye sifa
zinazohitajika kukaimu nafasi hiyo ya uongozi iliyowazi.

1. Kura za uamuzi:
1.
1.
1.
1.
1.
1. Uamuzi wowote utafikiwa kwa
kuungwa mkono na zaidi ya nusu
ya kura zote za wajumbe
waliohudhuria kikao.
2. Mwenyekiti wa kikao atakuwa na
kura ya uamuzi iwapo pande
mbili zitakuwa na kura
zinazolingana.

1. Uteuzi wa Makatibu wa Chama:

• Makatibu wa Chama wa ngazi zote isipokuwa ngazi ya Taifa watateuliwa


kama ifuatavyo:-


1.
1. Makatibu wa Chama wa matawi watateuliwa na Katibu wa
Chama wa Kata/ Shehia na kuidhinishwa na Kamati ya
Chama ya Kata/ Shehia.
2. Makatibu wa Chama wa Kata/ Shehia watateuliwa na
Katibu wa Chama wa Wilaya na kuidhinishwa na kamati ya
chama ya Jimbo.


1.
1. Makatibu wa Chama wa Wilaya watateuliwa na Katibu
Mkuu wa Chama na kuidhinishwa na Kamati Kuu ya Chama.

1. Marekebisho ya katiba.

• Katiba inaweza kurekebishwa na Mkutano wa Taifa kutokana na


mapendekezo ya Kamati Kuu yatakayoungwa mkono na theluthi mbili ya
wajumbe wa Mkutano wa Taifa wenye haki ya kipiga kura.

KUVUNJA CHAMA


o
1. (1) Chama kinaweza kuvunjwa au kuungana na chama au
vyama vingine kwa azimio la Mkutano wa Taifa wa Chama
linaloungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe wa
mkutano huo.


o
 (2) Azimio la kuvunja chama au kuungana na chama au
vyama vingine litawasilishwa na Kamati Kuu kwa wajumbe
wa Mkutano wa Taifa siku tisini kabla ya kikao.

***************************************

You might also like