You are on page 1of 3

Wananchi wa Tanzania wapaza sauti zao na kusikika

na viongozi wa Dunia New York-Marekani.


Sautiza watanzania leo zinasikika duniani kote kwa viongozi wanchi na
dunia ambapo wananchi wanadai viongozi watimize ahadi zao juu ya afya
ya uzazi kwa kina mama, watoto na vijana.
Watanzania wana mchango mkubwa sana katika uzinduziwa ripoti hii ya
dunia ambayo inazinduliwa wiki hii katika nchi mbalimbali duniani ikitoa
wito wa uwajibikaj i na ushiriki wa wananchi katika ngazi zote katika
hudumaza afya.
Ripoti hii ni harakati za kipekee kwani zaidi ya mikutano 100 ya sauti za
wananchi imefanyika katika nchi 20 mwaka 2015. Watu wa rika zote,
kutoka katika aina tofauti za maisha wamesafiri kutoka katika vijiji na
miji yao ili kushiriki katika mikutano hii maalum ya kidiplomasia na
iliyowazi ili kukutana na wanasiasa, watoa huduma za afya na waandishi
wa habari. Wananchi waliongea na kuuliza maswali, viongozi walisikiliza
na kujibu ili kuitikia matakwa ya uhitaji wa ushirikishaji na uwajibikaji
wa nchi zao katika huduma za kina mama, watoto na vijana.

Tukio: Uzinduzi wa Ripoti ya Sauti za Wananchi


Tarehe:25/09/2015
Muda: Saa nne na nusu hadi saa tano na nusu asubuhi (4:30-5:30)
Mahali:
Ofisi za Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama
164C Msasani Beach, Kinondoni
S.L P 65543, Dar es Salaam
Parua Pepe: rose.mlay@gmail.com
Simu : +255 754 316 369
Mitandao ya kijamii: #CitizenPost

Mikutano ya Sauti za Wananchi pia ilifanyika katika wilaya na miji mikuu


ikiwemo Muheza, Kilindi, Handeni, Korogwe, Jiji la Tanga na Dar es
Salaam.
Pia mikutano hiyo ilitangazwa na ITV na Radio One ambapo wananchi
kutoka sehemu mbalimbali za nchi walipata nafasi ya kuchangia na
kuuliza maswali kwa viongozi wao. Pia wananchi waliweza kuchagua
wawakilishi wao-kwa mara ya kwanza kabisa-ili wazungumze kwenye
mkutano wa afya wa dunia uliofanyika mwezi Mei mwaka huu huko
Geneva.
"Suala kubwa kabisa la kusisimua katika (Mkutano wa afya wa dunia)
ilikua ni kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya Shirika la Afya

duniani na Baraza lake, mkutano ulioongozwa na asasi ya kiraia


ulifanyika ili kuimarisha uwajibikaji wa kisiasa kwa afya ya dunia hasa
kwa afya ya kina mama na watoto. Muungano wa Utepe Mweupe pamoja
na serikali za Bangladesh na Sweden ziliitisha majadiliano ya kwanza ya
dunia kati ya wanachi na serikali. Lilikua ni suala la kihistoria. Majadilia
no haya ya sauti za wananchi msingi wake ni mikutano ya sauti za
wananchi liyofanyika katika nchi 20 ambapo asasi za kiraia ziliweza
kukubalika katika kuimarisha hali ya afya duniani -kwa wakati ujao"
Richard Horton,Mhariri Mwandamizi, Lancet.
Katika moja ya vipengele vya ripoti ya sauti za wananchi mbacho kina
akisi mapendekezo yaliyotolewa na wananchi waTanzania,mwananchi
kutoka Tanga, Peter Katuka anasema;
'Tuna sera nzuri lakini hazitekelezwi. Kwa mfano, sera ya serikali inasema
kwamba kuwe na zahanati katika kila kijiji na kituo cha afya katika kila
kata'
Mapendekezo ya wananchi kwa viongozi;
1. Kuakisi sauti za wananchi katika vipaumbele vya sera na kuchukua
hatua ilikuboresha afya ya ya uzazi kwa kina mama, watoto na vijana.
2. Kuanzishwa kwa mfumo thabiti wa uwajibikaji kutoka ngazi ya serikali
ya mtaa hadi taifa.
3.Kuunga mkono wito wa kuwa na mfumo wa uwajibikaji ulio huru na
unaoruhusu ushirikishaji katika ngazi ya dunia.
Sauti za Jamii zimeimarika zaidi wa kati huu ambao dunia inazindua
malengo mapya ya maendeleo, Malengo Endelevu ya Dunia (SDGs) katika
baraza la Umoja wa Mataifa huko New York. Wakati huo huo, katibu
Mkuu waUmoja wa Mataifa Ban Ki -moon anatangaza mkakati wake wa
pili kwa ajili ya afya ya kina mama na watoto. Na haya yote yamekuja
sasa kwa sababu tumeona kwamba malengo ya kidunia, kitaifa na ya
kijamii yanaweza kufikiwa pale tu sauti za wananchi zitasikilizwa.
Na hii ndio sababu wakati viongozi wadunia wanakuta na katika Baraza
la Dunia la mwaka 2015 ili kuweka ahadi zao kwa miaka kumi na mitano
ijayo, sisi tunasema kwamba "hakuna linalotuhusu sisi wenyewe
hatutashiriki" -hii ndio kauli mbiu ya maelfu ya wananchi ambao
walishiriki zaidi ya mikutano 100 ya sauti za wananchi duniani
(http://www.citizens-post.org/).
Wakati huo huo, tarehe 26 Septemba 2015, Ripoti ya Sauti zaWananchi
itazinduliwa huko New York na shughuli hii itafanywa na (PMNC)mbele
ya viongozi wa dunia na wanachi kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Pia, huko New York, waandaji wa SAUTI ZA WANANCHI wanaandaa
'Hakuna kinachotusu kama sisi wenyewe hatutashiriki' ili kuonyesha
ushiriki wa wananchi katika uwajibikaji katika sekta ya afya na kutoa
dondoo juu ya ahadi mpya ya asasi ya kirai katika mkakati wa dunia kwa
afya ya kina mama, watoto na vijana. Hii itafanyika siku ya Ijumaa
tarehe 25 Septemba.

Kumekua na maendeleo makubwa na ustawi wa afya wakati wa malengo


ya milenia. Hata hivyo mamilioni ya kina mama na watoto wamekua
hawafaidiki na na lengo la 4 na la 5 la milenia na muenendo wa sasa
unaonyesha kuwa ifikapo mwaka 2030 watoto milioni 4 n awanawake
200,000 watakua wamefariki kutokana na sababu ambazo zingeweza
kuzuilika ambazo zinaendana naujauzito na kujifungua. Ili kumalizia
agenda ambayo haikumalizwa -ya- kuzuia vifo vya watoto wachanga,
kinana mama na watoto ndani ya miaka kumi na tano ijayo inaweza
tukutokea kama kutakua na mfumo madhubuti wa uwajibikaji. Ili
maendeleo endelevu ya dunia yaweze kufanikiwa, wananchi lazima wawe
mbele katika kufanya maamuzi.Asasi za kiraia zina kazi kubwa ya
kufanya katika kutengeneza mazingira haya ya maendeleo.
Katika wiki hii, mazungumzo ya wanahabari na taarifa kwa umma
zitakuwa zikitolewa katika nchi ambazo zilifanya mikutano ya sauti za
umma ili kuzindua ripoti hii na mapendekezo yaliyomoili na kutoa
mchango katika kuondoa hali ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya
karibu na mrejesho juu ya vipaumbele vya afya katika ngazi za kitaifa na
kimataifa.
Imetolewa na Rose Mlay-Mratibu wa Taifa, Muungano wa Utepe Mweupe
wa Uzazi Salama Tanzania.

You might also like