You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua


Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la
Zimamoto nchini.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo tarehe 25
Aprili, 2016.
Kamishna wa Polisi Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius
Makuru Nyambacha ambaye amestaafu.
Kabla ya uteuzi huo Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa
Utawala na Utumishi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Donan
Mmbando kuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.
Uteuzi wa Dkt. Donan Mmbando umeanza tarehe 24 Aprili, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Aprili, 2016

You might also like