You are on page 1of 6

Zana za kufundishia na kujifunzia ni vifaa anavyotumia mwalimu wakati wa mchakato wa

ufundishaji na ujifunzaji ili zimrahisishie ufundishaji wake na kuwafanya wanafunzi waelewe


somo kiurahisi zaidi.Kwa hiyo zana za kufundishia na kujifunzia ni vifaa vinavyotumika katika
mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji.

AINA ZA ZANA

Zana za kujifunzia na kufundishia zipo za aina mbalimbali kama ifuatavyo;-

I. Zana maono, hizi ni zana ambazo hutumika katika mchakato wa kufundishia na


kujifunzia ambapo vitu halisi huhusishwa,kwa kutumia vitu halisi mwanafunzi anajifunza
kwa udadisi,kuchunguza na kupindua,pia vitu halisi vinampa mwanafunzi nafasi kubwa
ya kujifunza kwa vitendo na kutumia milango mingi ya fahamu kwa wakati mmoja.Kwa
ukosefu wa vitu halisi mambo au vitu bandia huchukua nafasi ya pili,mwanafunzi
anapata kuona,kusikia,kuhisi kana kwamba anatumuia vitu halisi.Bandia ni igizo la vitu
halisi, hivyo huchangia kiasi fulani cha ukweli, mfano; chati,picha,mabango,grafu na
ramani.
II. Zana masikizi, zana hizi humsaidia mwanfunzi kujifunza kwa kusikia.Vipindi maalumu
hutayarishwa kwa ajili ya shule au wanafunzi wanaosoma kwa masafa, mfano;redio,tepu-
rekoda,santuri.
III. Zana masikizi maono, zana hizi zinachangia kuonesha vitu kama vilivyo,hali hii kuna
ukweli ndani ya zana hizi.Zana hizi zinamuwezesha mwanafunzi kusikia na kuona
matendo wakati ule ule yanapofanyika.Kwa mfano; luninga,sinema,ngamizi na vifaa
vingine vinavyohusisha kuona na kusikiliza.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UANDAAJI WA ZANA ZA KUJIFUNZIA NA


KUFUNDISHIA

Katika uandaaji na utumiaji wa zana ,kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kama ifuatavyo;

Somo na mada, mwalimu anapaswa kuandaa zana zinazosadifu somo na mada husika , kwa
mfano; kama somo ni historia ,mwalimu anapaswa kuandaa zana kama vile ramani kutegemeana

1
na mada husika.Pia kama somo ni la Kiswahili katika mada ya aina za mmaneno,mwalimu
anaweza kuandaa chati inayoonesha aina za maneno.

Umri au kiwango cha elimu cha wanafunzi, mwalimu anapaswa kuandaa zana zinazoendana
na umri pamoja na kiwango cha elimu ya wanafunzi wake,kwa kufanya hivyo itawarahisishia
wanafunzi kuelewa mada husika kwa urahisi zaidi,pia itamsaidia mwalimu kufundisha kwa
wepesi zaidi.

Zana inapaswa ibebeke, mwalimu anapaswa atumie zana ambayo ni rahisi kubebeka na
kuhamishika ili iwe rahisi kwa wanafunzi kuiona kwa makini na kwa urahisi zaidi,kwani zana
isiyobebeka wala kuhamishika kwa urahisi zinakua ni kikwazo kikubwa kwa wanafunzi katika
kujifunza.Hivyo zana itakayo tumika inatakiwa iwe nyepesi na yenye kuhamishika kutoka
sehemu moja hadi sehemu nyingine.

Zana haipaswi kua inayotisha, mwalimu anatakiwa kuandaa zana isiyotisha hasa kwa
wanaojifunza.Baadhi ya zana hazipaswi kutumika kwa wanafunzi wenye umri mdogo kwani
zinaweza kuwaogopesha hata kuwahamisha darasani kisaikolojia , kwa mfano ; matumizi ya
picha za wanyama wakali kama vile simba na nyoka.

Zana inatakiwa iwe yenye kuonekana, mwalimu anatakiwa atumie zana zinazoonekana ili
wanafunzi waweze kuelewa kitu husika kinachoelekezwa kwa kuangalia picha yake au kitu
halisi ambapo mwanafunzi anaweza kudadisi ,kuchunguza na kugundua nini
kinachomaanishwa,kwa mfano; matumizi ya chati,picha za vitu,mabango,grafu na ramani.

CHANGAMOTO WAKATI WA UANDAAJI W A ZANA ZA KUFUNDISHIA NA


KUJIFUNZIA

Katika mchakato wa kuandaa zana za kufundishia na kujifunzia ,changamoto zifuatazo zinaweza


kujitokeza;

Gharama ya zana husika, katika mchakato wa uandaaji wa zana za kufundishia na kujifunzia


,kuna baadhi ya zana ambazo hugharimu kiasi kikubwa cha fedha na hivyo kumfanya mwalimu
ashindwe kuzipata zana hizo,hivyo basi hulazimika kufundisha bila kutumia zana.

2
Kukosekana kwa ujuzi na ubunifu, mwalimu anatakiwa kuwa mbunifu na awe na ujuzi wa
kutengeneza na kuandaa zana zinazoendana na somo pamoja na mada husika ambazo zitamsaidia
mwalimu kufundisha vizuri na kwa urahisi na kuwawezesha wanafunzi kumuelewa mwalimu
kwa urahisi zaidi.

Ukosefu wa vifaa vya kutengenezea zana, katika uandaaji wa zana ,mwalimu anaweza kukosa
vifaa vya kutengenezea zana husika.Changamoto hii inaweza kusababishwa na utofauti wa
mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, kwa mfano; mwalimu anayetaka kutumia mimea au
wadudu kama zana zake katika ufundishaji wa somo husika ni vigumu kuwapata wadudu au
mimea hiyo hasa wakati wa kipindi cha kiangazi ,mwalimu anaweza kukosa vifaa vingine katika
mazingira ya karibu ,mfano wa vifaa hivyo ni kama gundi,karatasi ngumu na hata rangi.

Uandaaji wa zana unagharimu muda, katika uandaaji wa zana hizo ,mwalimu anatakiwa
kutenga muda wake wa ziada wa kuzitafuta na kuziandaa zana hizo,hivyo swala hili humpa
changamoto kubwa mwalimu katika utengaji wake wa muda ,swala ambalo linaweza
kusababisha mwalimu kufundisha pasipo kutumia zana pale tu atakapokosa muda wa kuzitafuta
na kuziandaa zana hizo.

CHANGAMOTO WAKATI WA UTUMIAJI WA ZANA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA

Kukosekana kwa maarifa katika kutumia zana hizo, hapa tunamaanisha kuwa,zana zinakuwepo
tayari ,pengine zimenunuliwa,zimefaraguliwa au zimetengenezwa na mwalimu mwingine wa
somo hio,lakini katika utumiaji inaweza kutokea baadhi ya walimu kukosa maarifa ya kutosha
katika uelezeaji ili kurahisisha ujifunzaji.Hii inaweza kupelekea hasa kutoeleweka kwa mada
lengwa au kumsumbua mwalimu katika kutafsiri.mfano; matumizi ya jedwali au chati ya aina za
maneno isipotafsiriwa vizuri inaweza kumfanya mwalimu asieleweke.

Kunahitajika umakini wa hali ya juu wakati wa utumizi wa zana ,mwalimu hana budi kutoa
maelezo ya kina kwa wanafunzi wake katika kutumia zana hizo,kwa mifano baadhi ya dhana
zimetengenezwa kwa vioo hasa katika masomo ya sayansi ,hivyo mwalimu na wanafunzi
wanatakiwa kuwa makini wanapotumia zana hizo ili zisiweze kuvunjika hata kuwadhuru
wanafunzi.

3
Kwa ujumla ,zana za ufundishaji na ujifunzaji ni muhimu sana katika suala zima la ufundishaji
na ujifunzaji kwani humsaidia mwalimu kuongeza ustadi na ujuzi zaidi juu ya mada husika,pia
humsaidia mwanafunzi kutumia milango yake ya fahamu zaidi ya mmoja, kitu ambacho
humfanya mwanafunzi huyo kuielewa mada kwa undani zaidi na kuihifadhi kichwani kupitia
utumizi huo wa zana moja kwa moja Kama vile utumizi wa zana masikizi,zana maono na zana
maono-masikizi

MAREJELEO

4
1. Wanjara S.F. na J.M.Kavoi (2012).Stadi za mawasiliano na mbinu za kufundishia
kswahili.Mwama :Serengeti Educatinal publishers(T) Ltd.
2. Syambo .B. na wengine (1987).Jinsi ya kufundisha Kiswahili katika shule za
msingi.Nairobi:Heineman Kenya.
3. Ndunguru S. (1986). Kanuni na mbinu za kufundishia ,Dar es salaam:Mbogo
International Graphic Arts.
4. Tuntufie,N.D (1972). Jinsi ya kufundisha Kiswahili. Dar es salaam: Tanzania publishing.

KITIVO : ELIMU.
IDARA : LUGHA NA ISIMU.

5
JINA LA KOZI : MBINU ZA KUFUNDISHIA KISWAHILI
MSIMBO : CT126.
JINA LA MHADHIRI : KILAVE Y.
MWAKA WA MASOMO: MWAKA WA KWANZA, 2016/2017.
AINA YA KAZI : KAZI YA KIKUNDI.
MKONDO : BAED 1 A.
KUNDI : NAMBA 04.
NAMBA MAJINA NAMBA ZA USAJILI SAHIHI

1. BENSON SHILLA AM/BAED/160291


2. EMILY ERICK AM/BAED/160354
3. JUMANNE SALUMU AM/BAED/160477
4. KALITASI LIMBU SAYI AM/BAED/160482
5. BERNADI ESTER PAULO AM/BAED/160292
6. LEONARD STUMAHI AM/BAED/160567
7. CYPRIAN PIETHA AM/BAED/160330
8. ELIAS JOSEPH AM/BAED/160347
9. DAUD ELISHA AM/BAED/160337
10. ZEPHANIA VERONICA AM/BAED/15352
11. AUGOSTINO NDAYILAGIJE AM/BAED/160272
12. MVUMBA MAGRETH LAITON AM/BAED/160772
13. MASHAKA MUSA AM/BAED/160635
14. MCHEMBA MUSTAPHA AM/BAED/160685
15. MWASIKILI KELVIN AM/BAED/160801
16 MWALONGO DIGNA E AM/BAED/160787
17 RULAKUZE CHRISTINA M AM/BAED/160912
18 GEORGE SAMWEL AM/BAED/160388
SWALI:
Fafanua zana za kufundishia na kujifunzia kwa kuangalia aina zake,mambo ya
kuzingatia,changamoto unazoweza kukumbana nazo wakati wa uandaaji na utumiaji wa
zana.

You might also like