You are on page 1of 18

TAARIFA KUHUSU ANDIKO LA MRADI

1. Jina la Mradi: Mti Wangu Kipato Changu


2. Jina na Anwani ya Mwombaji: Tanzania Sustainable Development Implementation
Organization (TSDIO)
3. Jina na anwani ya anayefanya mawasiliano MARIAM MARCO LOWASSAKAI, SIMIYU.
4. Mahali Mradi utakapotekelezwa MKOA WA SIMIYU WILAYA YA MEATU KATA YA
KISESA.
5. Eneo la kipaumbele la Mfuko wa Misitu Tanzania. Uanzishwaji wa Mashamba Madogo ya
Miti ya Kupandwa.
6. Aina ya Ruzuku inayoombwa RUZUKU KUBWA
7. Aina ya uwezeshwaji unaoombwa UWEZESHWAJI WA FEDHA, VIFAA NA
UTAALAMU.
8. Mantiki na uthibitisho wa kuwa na mradi
Uthibitisho wa mradi unadhihirika kwa kushirikisha serikali za mitaa na wakazi wa eneo
husika kusaidia uanzishaji wa sheria ndogo ndogo kwenye serikali za vijiji. Kuwepo kwa
wafanyakazi muda wote ili kulinda shamba darasa. Kipindi cha uvunaji kitaambatana na
utoaji elimu juu ya uvunaji wa miti na uuzaji wa mazao ya miti yaliyo pembuliwa ili
kuhamasisha jamii kupanda miti na kufata taratibu za uvunaji miti. Kipato kitakacho
zalishwa kitasaidia uboreshaji wa huduma za kijamii na kupanua shamba darasa katika
maeneo jirani.
Mradi huu utaendelea kufanyika katika eneo la kisesa kulingana na mkakati uliopo wa
kushirikisha wadau kutoa changizo la kuendeleza mradi, pia shirika linachukua hatua za
kubadili miche kuwa fedha (miche hii itapandwa na kusimamiwa katika ofisi zetu ndogo
zilizopo Meatu kata ya Kisesa na miche baadhi iliyopo katika makao makuu yetu hapa
Ubungo, Dar es salaam). Katika mradi huu ikiwa ruzuku itakoma shirika litaanzisha mradi
wa maji ya kisima ambapo kila mwananchi atanunua maji kwa bei ya shilingi mia tatu
(300/=) kwa ndoo kubwa (lita 20) na ndoo ndogo (lita 10) kwa bei ya shilingi mia na
hamsini (150/=) kwa sababu ya changamoto ya maji tunatarajia mradi huu utatoa gharama
ya kuendeleza mradi.
9. Malengo ya mradi
a) Kuwa na darasa kwa vitendo
b) Kutoa Elimu ya Utunzaji wa Mazingira na Jinsi inavyo saidia katika
kukabiliana na Mabadiliko ya tabia Nchi
c) Kutambua nafasi ya Mtoto, Mzee, Kijana na Mwanamke katika Utunzaji wa
Mazingira.
Viashria vya utendaji
a) Kushirikisha jamii katika eneo husika la Shamba darasa,
b) Kujitoa kwa watendaji wa shirika na Wasimamizi wa mradi
c) Na kushirikisha vyombo vya habari katika uhamasishaji wa Mti Wangu
Kipato Changu.
10. Matokeo yanayotarajiwa kutoka kwenye mradi BADILIKO LA TABIA YA UHIFADHI
MISITU KATIKA JAMII
11. Watakaonufaika na mradi WATOTO, WANAWAKE, WAZEE NA VIJANA
12. Jumla ya kiasi kinachoombwa kutoka Mfuko (Shilingi): MILIONI THELATHINI NA
TATU, LAKI TANO ELFU AROBAINI NA TANO TU (33,545,000/=)
13. Michango mingine ikiwemo ya hali na mali (Shilingi): MILIONI KUMI NA SITA, LAKI
TISA ELFU (16,900,00/=)
14. Muda wa utekelezaji wa mradi na mwezi ambao utekelezaji utaanza Miaka Mitano, Mwezi
wa Saba, Mwaka 2020.
MUHTASARI WA MRADI

Kisesa ni kata inayokua kwa kasi katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu kulingana na
uwekezaji wa kilimo cha pamba. Licha ya eneo hili kuwa pendwa kwa wageni, eneo hili
linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mvua wa mara kwa mara, ukataji miti pasipo kufata
sheria, uharibifu wa mazingira unaotokana na ongezeko la watu kwa mwaka, Watoto, Wazee,
Vijana na Wanawake wamekuwa hawapewi vipaumbele katika utunzaji wa misitu, pia
kumekuwa na baadhi ya wananchi ambao wamehamasika sana kupanda miti yao binafsi ingawa
hawafati kauli mbiu ya kata mti panda miti.

TSDIO imekusudia kutoa elimu ya upandaji miti kwa njia ya vitendo na elimu ya sheria ya
ukataji miti, kutoa hamasa kwa jamii kuhusu nafasi ya mtoto, mzee, kijana na mwanamke katika
utunzaji miti, na kuhamasisha jamii jirani.

Utoaji elimu kwa njia ya vitendo utachochea badiliko la kifikra katika jamii juu ya umuhimu wa
kuhifadhi misitu asilia na misitu ya kupandwa. Kubadili mtazamo wa jamii juu ya ushiriki wa
Watoto, Wanawake, Wazee na Vijana katika upandaji wa miti na kuhifadhi mazingira, kupitia
upandaji miti jamii itanufaika kujiongezea kipato. Kwa kufanya hivyo kutapunguza kama sio
kuondoa kabisa ukataji wa miti kiholela.

Uthibitisho wa mradi unadhihirika kwa kushirikisha serikali za mitaa na wakazi wa eneo husika
kusaidia uanzishaji wa sheria ndogo ndogo kwenye serikali za vijiji. Kuwepo kwa wafanyakazi
muda wote ili kulinda shamba darasa. Uwepo wa vitalu vya miti vya shirika kutasaidia upandaji
wa miti katika maeneo jirani pindi Uwezeshaji wa TFS utakapo koma.

Kipindi cha uvunaji kitaambatana na utoaji elimu juu ya uvunaji wa miti na uuzaji wa mazao ya
miti yaliyo pembuliwa ili kuhamasisha jamii kupanda miti na kufata taratibu za uvunaji miti.
Kipato kitakacho zalishwa kitasaidia uboreshaji wa huduma za kijamii na kupanua shamba
darasa katika maeneo jirani.

UTANGULIZI

Mradi huu wa Mti wangu, Kipato changu ni aina ya mradi uliojikita katika ubunifu wa aina ya
upandaji miti na usimamizi wake, miti inayotarajiwa kupandwa ni miti ya mbao, miti ya matunda
na vitalu vya miti ya mapambo na ya vivuli. Ni mradi ambao umekusudia kushirikisha jamii
moja kwa moja katika kila hatua mpaka hatua ya uvunaji wa miti ambapo kila mwajamii
atafanikiwa kupata ujuzi wa kina juu ya kuanzisha shamba la miti (Msitu binafsi). Katika kila
1
hatua itakayokuwa ikifanyika itakuwa na kipindi cha likizo ya wiki mbili hadi mwezi hii
itasaidia kuweza kuanzisha darasa jingine katika kata jirani.

Changamoto kubwa ambayo mradi huu imekusudia kuitatua ni uhaba wa elimu ya kutosha juu ya
uhifadhi wa miti inayopandwa na njia bora za uvunaji wa miti iliyopandwa. Nusu ya Misitu
iliyopandwa yageuzwa Mkaa1 katika Wilaya za Meatu na Bariadi kupitia mradi wa Kiserikali
uliopewa jina la Hifadhi ya Ardhi Shinyanga (HASHI). Kutokana na uhaba wa elimu hii
kumepelekea uharibifu mkubwa sana na kuongeza uhasama kati ya wafugaji na wakulima
kutokana na ongezeko la ukame pia wafugaji wamekuwa wakivamia hifadhi za misitu kwa ajili
ya malisho. Vijiji jirani kama Igobe, Mhanuzi, Mwandoya, Mwamishali, Bukundi na Nkoma
imeharibika sana kutokana na madhara ya ukame. Kwa kutambua hilo kama Shirika licha ya
jitihadi za kujitolea kutoa elimu katika kata hizo ivyo tunatumaini kwa kufanya mradi huu katika
kijiji cha Kisesa ambacho hakijaathiriwa sana kama kata tajwa hapo kutasaidia kuendeleza uoto
wa asili katika eneo bila ya kuharibiwa. Jitihada zilizokwisha fanyika ni pamoja na waharibifu
wa misitu kupelekwa Mahakamani ingawa kesi zao hazijatolewa hukumu stahiki. Kwa
unyambuzi zaidi Wanakijiji, Watendaji na Askari walitoa maoni hayo 2,

AZMA NA MADHUMUNI YA MRADI NA MATOKEO YANAYOTARAJIWA

Utekelezaji wa mradi huu utachangia kwa kiasi kikubwa sana katika uendelezaji wa misitu kwa
muktadha wa kumshirikisha mwananchi moja kwa moja kwenye hatua zote zinazohitajika
kuhifadhi mti. Mwananchi atafundishwa sheria mbali mbali zinazohusu uhifadhi wa miti, faida
za miti na athari atakazo kabiliana nazo pindi atakapo kiuka sheria hizo. Mradi huu kwa
kutambua jinsi ambavyo viongozi wa vijiji walivyo shindwa kusimamia ipasavyo kulingana na
ukosefu wa sheria ndogo ndogo ikiwa ni pamoja na Ulinzi shirikishi, utatoa elimu kwa viongozi
namna ambavyo watatunga sera na sharia ndogo ndogo ambazo zitasaidia katika kuhifadhi
misitu na usalama wa jamii kwa ujumla.

1
Haya ni maneno madogo katika kichwa cha habari “MIAKA 30 YA KUNUSURIWA” ni taarifa ilinakiliwa kutoka kwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Bariadi, Mr. Robert Rweyo alipokuwa akizungumza na chanzo cha habari IPP
media tarehe 24/11/2016. Kwa maelezo zaidi soma kupitia https://www.ippmedia.com/sw/makala/miaka-30-ya-
kunusuriwa-nusu-ya-misitu-iliyopandwa-imegeuzwa-mkaa. Aligusia wilaya za Meatu na Bariadi.
2
“Kesi ilipelekwa Mahakama ya Wilaya Meatu, nasi viongozi akiwamo mwenyekiti wa kijiji na wajumbe wake,
tuliitwa mahakamani kutoa ushahidi, lakini mpaka leo hatujui kinachoendelea kwenye kesi hiyo,” anasema
Mwandu. Kwa maoni mengine soma kupitia https://mtanzania.co.tz/kasi-uharibifu-mradi-wa-hifadhi-ya-miti-
yatisha/
2
Kwa kutekeleza shughuli tatu ainishi zitachangia kwa kiasi kikubwa sana kwenye mambo
yafuatayo; -

a) Kubadili tabia ya kuharibu misitu kuwa tabia ya kujali na kuthamini thamani ya miti. Hii
itafanyika kwa kuwajengea uwezo wa kupanda miti binafsi ambayo itatumika kwa
matumizi ya mbao, kuni na mkaa. Hii itawafanya wananchi wengi kufanya hivi baada ya
kupokea elimu kwa njia ya vitendo kupitia shamba darasa.
b) Utii wa sheria bila shuruti. Mazoea ya kutii sheria ya uhifadhi mazingira bila shuruti
yataimarishwa kwa kila Mwanachi pindi elimu ya sheria itakapotolewa kuhusu kuhifadhi
misitu na rasilimali zao binafsi. Kwa kuanzisha ulinzi shirikishi itasaidia kwa kiwango
kikubwa sana maana kila mtu atakuwa mlinzi wa mwenzake.
c) Kuongeza ujuzi kwa wananchi kujiongezea kipato kwa kuuza mkaa unaotokana na mti wa
mwanzi na kutoa ajira kwa wakazi. Miti aina ya mianzi itapandwa kando kando ya mito
ili kuzuia pia mmomonyoko wa ardhi na kutumika kwa matumizi ya mkaa. Elimu ya
kutengeneza mkaa unaotokana na mianzi itatolewa kupitia wataalamu wetu tulionao
katika ushirika wa pamoja. Ajira zitatolewa katika utekelezaji wa mradi.

Punde matokeo ainishi yakiendelea kuonekana jitihada madhubuti zitachukuliwa kuendeleza


elimu katika kata jirani za Igobe, Mhanuzi, Mwandoya, Mwamishali, Bukundi na Nkoma
ambazo zimeathirika sana na ukame kama matokeo ya kutotambua thamani ya mti na njia sahihi
za kujipatia kipato. Mkakati wa kujumuisha vyombo vya usalama kutoa taarifa mbali mbali juu
ya hatua za kisheria zilizochukuliwa katika uharibifu wa miti zaidi ya miti milioni nne
(4,000,000) kati ya miti zaidi ya milioni sita (6,000,000)3 iliyopandwa kwa makadirio ya miti
500 kwa hekari moja.

Kwa taarifa zaidi tazama Jedwali la bao la Mantiki (Jedwali namba 1).

MBINU ZA UTEKELEZAJI

Mradi huu umekusudia hasa kutoa huduma hii kwa jamii kwa kushirikisha wadau mbali mbali
wa maendeleo kupitia redio na luninga. Changizo hili litafanyika Mwezi mmoja baada ya kuanza

3
Idara ya misitu katika halmashauri ya wilaya hiyo inaeleza kuwa uharibifu huo umesababisha kubaki hekari za
hifadhi za miti 5821 kati ya 14,155 zilizopandwa wakati wa mradi sawa na asilimia 30 ya miti yote iliyopandwa.
Inaendelea kwa kusema “Asilimia 90 ya hekari zote za miti iliyopandwa wakati mradi imekatwa, ni hekari 10 tu
ambazo zimebaki kwenye kata hii, ambazo mbili zipo kwenye shule ya msingi Igobe na moja kwenye shule ya
sekondari Mwandoya, saba zinamilikiwa na watu binafsi,” anasema Malya. Chanzo ni gazeti la Mtanzania la tarehe
3/8/2017. https://mtanzania.co.tz/kasi-uharibifu-mradi-wa-hifadhi-ya-miti-yatisha/
3
utekelezaji wa andiko. Tunatarajia kupitia kampeni hii ya changizo la upandaji miti kukusanya
kiasi tasilimu cha kitanzania Milioni kumi na sita na laki tisa (16,900,000/=). Wananchi
watatozwa gharama ya kiasi cha shilingi taslimu za kitanzania elfu moja mia tano (1,000/=) kwa
kila mche wa mti wa mbao, mia tano (500/=) kwa kila mche wa mti wa matunda, na kwa kila
mwanachi atachangia mia saba (700/=) kwa kila mche wa muanzi. Tunatarajia kuuza miche zaidi
ya 1,000 ya miche ya mbao, miche zaidi ya 1,000 ya miti ya matunda na miche zaidi ya elfu
3,000 ya mianzi hivyo kukusanya fedha tasilimu za kitanzia shilingi milioni tatu na laki sita
(3,600,000/=). Katika awamu ya kwanza ya utekelezaji tunatarajia kukusanya kiasi cha shilingi
milioni nane na laki sita za kitanzania (8,600,000/=) ambazo zitatumika kwa kuendeleza mradi
katika awamu mbili zilizo salia.

MPANGO KAZI WA MRADI KATIKA KATA YA KISESA WILAYANI MEATU MKOA WA


SIMIYU.

Muhimu: Mradi una awamu tatu za utekelezaji wa mradi wa upandaji miti mpaka uvunaji kwa
miti ya muda mfupi isiyozidi miaka mitano.

Tazama Jedwali la mpango kazi (Jedwali namba 2) lililoambatanishwa.

Jedwali Na 2 (a).

AWAMU YA AINA YA SHUGHULI YA MRADI MUDA WA UTEKELEZAJI


MRADI J A S O N D J F M A M J
Awamu ya Ununuzi wa shamba na uandaaji wa
kwanza ya shamba kwa ajili kupanda mianzi
utekelezaji Kutangaza nafasi za kazi na watu wa
Mradi kujitolea kupitia Redio na luninga,
Ununuzi wa mbegu za mianzi, uandaaji
wa vitalu na upandaji wa mbegu
Maandalizi ya uchimbaji kisima (Hatua
ya kwanza) na kupokea maombi ya kazi
na Wafanyakazi wa kujitolea.
Utoaji wa elimu kwa njia ya nadharia
katika kata ya Kisesa Wilayani Meatu
Ununuzi wa Jenereta, mipira ya

4
umwagiliaji. Kutangaza majina ya
wafanyakazi wa kujitolea.
Uwekaji wa Jenereta, Mipira ya
umwagiliaji, na vifaa vya umwagiliaji
tayari kwa kilimo cha mwagiliaji
Ukamilishaji wa kuchimba kisima
(Hatua ya Mwisho). Kutangaza majina
ya waajiliwa (Nafasi mbili).
Kuandaa kitalu cha miti ya mbao,
matunda na mapambo kwa kushirikiana
na Wananchi (Hatua ya awali ya utoaji
elimu kwa vitendo)
Kutoa mwito wa wananchi kuanzisha
vitalu vya miti sawa na elimu iliyo
tolewa, na kufanya utafiti juu ya
mwitikio wa wananchi katika
utayarishaji wa shamba na uandaaji wa
vitalu
Upandaji wa miti ya mbao, matunda na
miti ya mapambo kwa kushirikiana na
Wananchi (hatua ya pili ya utoaji kwa
jamii kwa njia ya vitendo)
Ufatiliaji wa mashamba yaliyokwisha
andaliwa na Wananchi tayari kwa
upandaji miti na kushirikiana na
wananchi katika upandaji wa miti katika
mashamba yao, kutoa elimu juu ya
utengenezaji wa mkaa utokanao na
mianzi.
Kutembelea sehemu za kata ambazo
hazijafikiwa na kutoa elimu kwa
nadharia na kutoa mwaliko wa
Wananchi kutembelea shamba darasa na

5
mashamba ya wananchi walioitikia
wito. Kufanya utafiti juu ya mwitikio
wa wananchi wa utumiaji wa mkaa wa
Mianzi.
Utoaji elimu ya miti kupitia vyombo
vya habari (luninga na redio) na
kuhamasisha jamii kushiriki katika
changizo ili kupata kiasi cha kitanzania
milioni kumi na sita, laki tisa
(16.900,000/=)
Siku ya changizo la kusaidia shughuli
nyingine za mradi na kuitisha mkutano
wa wanakijiji kujadili juu ya hatua
zinazochuliwa katika uhifadhi misitu

Jedwali Na 2(b).

AWAMU YA MRADI AINA YA SHUGHULI YA MRADI MUDA (MWAKA) WA


UTELEZAJI MRADI
2 3 4 5
Awamu ya tatu ya Ufanyaji tathmini wa miti iliyo pandwa kwa
mradi. mwaka wa kwanza (1) wa utekelezaji mradi,
kutoa fursa ya upimaji udongo katika
maeneo ambayo miti mingi haijaota,
Kutoa elimu ya sheria juu ya uhifadhi misitu,
na kuitisha mkutano wa Kijiji kuanzisha
vikundi vya vijana vya ulinzi shirikishi.
Kutoa elimu ya upandaji miti kwa nadharia
katika vijiji jirani, kuandaa njia mbadala ya
upandaji wa miti baada ya upimaji udongo
na kuitekeleza, Kufanya tathimini juu ya
ushiriki wa wananchi katika uhifadhi wa

6
mazingira, na kuitisha mkutano wa Kijiji na
kushirikisha wananchi wawakilishi kutoka
vijiji jirani kujadili juu ya matokeo ya
mpango mkakati uliowekwa wa kuhifadhi
mazingira na usalama wa raia.
Uandaaji wa Mashamba, uchimbaji visima,
kuandaa vitalu vya miti, kupanda miti, na
kuitisha mkutano wa Kijiji pendekezi
(Mwandoya).
Kufanya tathimini ya mradi katika Kijiji cha
Mwandoya, Tathimini ya jumla ya mradi
Utoaji wa elimu juu ya uvunaji wa miti, na
utafutaji masoko, Kupokea maoni kutoka
wakala wa misitu Tanzania, Wadau wa
maendeleo na Serikali kwa ujumla.
Uwasilishwaji wa Makala zote
zilizoandaliwa tangu mwanzo wa mradi,
Upangaji mikakati katika vijiji vilivyo salia
kulingana na matokeo chanya katika Kijiji
cha kisesa.

VICHOCHEO VYA MAFANIKIO

Mradi utatoa nafasi mbili (2) za ajira ambazo zitahusisha mtaalamu mmoja wa upandaji wa miti,
usimamizi, ukuaji na uvunaji wa miti na mtaalamu mmoja wa sanaa ya habari ili kuchukua video
na kutengeneza makala itakayo tolewa kila mwaka. Mradi pia utatoa nafasi kumi (10) za
kujitolea kwa wakazi wa eneo la Kisesa hasa katika kuandaa maswali ya utafiti kujua idadi ya
walioelimika, kuchukua taarifa mbali mbali na kuandaa ripoti ya kila wiki, mwezi na mwaka
ambazo zitawekwa wazi kwa wadau wetu wakuu yaani serikali, Mamlaka ya Misitu Tanzania na
Wadau mbali mbali na Kushiriki katika utoaji wa elimu ya uhifadhi misitu na usimamizi wake.

7
Changamoto tunazotarajia kukutana nazo ni upungufu wa fedha za kuendesha mradi ambapo
tumeandaa mkakati wa kufanya changizo na uuzaji wa miche ya miti itakayo tokana na kitalu
tutakacho kianzisha cha miti.

MPANGO WA UPEREMBAJI NA TATHMINI

Mradi huu kuanzia hatua za awali mpaka hatua ya mwisho ya mradi utakuwa na aina tatu za
uperembaji na kufanya tathimini. Aina hizo tatu zitakazo husishwa zitazingatia kanuni na
taratibu (sera ya miradi ya shirika) ambazo zinajadili juu ya ukweli, uwazi na uwajibikaji. Aina
hizo zinatanabaishwa hapa chini; -

a) Ushirikishaji wa Wananchi. Wananchi watahusishwa kupitia ajira, wafanyakazi wa


kujitolea, ulinzi shirikishi na kuwa na vikao vitatu kila mwaka kwa kipindi cha miaka
mitano kujadili kwa pamoja juu ya changamoto zinazoendelea katika uhifadhi wa
mazingira.
b) Ushiriki wa wadau wa maendeleo ya misitu na mazingira. Katika uekelezaji wa mradi
awamu ya kwanza mdau mkubwa atakuwa ni Mamlaka ya Misitu, Serikali za mitaa na
kata na uangalizi kutoka ofisi ya mkurugenzi Wilaya, Meatu. Wadau wengineo
watahusika mara baada ya kutoa changizo nao watachangia kwa kiasi kikubwa kwa kutoa
michango yao ya hali na mali baada ya kuona jitihada madhubuti zikichukuliwa kwa
vitendo, ivyo njia ya picha na video zitasaidia sana.
c) Ushiriki wetu yaani Tanzania Sustainable Development Implementation Organization,
(TSDIO) kama mtekelezaji mkuu wa mradi. Mchango mkubwa tuliouweka katika mradi
huu nguvu kazi ya uandaaji, utekelezaji, usimamizi na uangalizi, na ufanyaji tathimini wa
mradi. TSDIO itashirikiana na TFS kufanya tathimini ya mradi kupitia ripoti na makala
mbali mbali katika awamu ya mwisho ya mradi.

Mradi huu utathibitika kutekelezeka na kuleta mabadiliko ikiwa kama Robo tatu ya tafiti itakayo
fanyika kudhihirisha wazi badiliko la tabia ya kuharibu misitu, tafiti hii itafanyika katika mtaa
mmoja tu kama sampuli ya badiliko. Mradi pia utakaribisha watafiti watakao fanya utafiti kwa
njia ya satelaiti ambapo itatusaidia kujua ni idadi ya mashamba mangapi ya miti ambayo
yameanzishwa tayari na maendeleo yake, tafiti hii itafanyika katika kata nzima ya kisesa mwaka
mmoja kabla ya kumalizika kwa mradi. Watafiti hao ni sharti wafate sera ya shirika yaani
TSDIO inayohusu ushirikishwaji wa wadau (Collaboration and Partneship Policy of 2020/2021)

8
ambayo inaweka bayana kutoa taarifa sahihi za utafiti amabazo zimepembuliwa vizuri kwa
kushirikisha dawati la TSDIO linahusiana na ufanyaji na utoaji taarifa kuhusu tafiti mbali mbali.

MPANGO ENDELEVU WA MRADI

Mradi huu utaendelea kufanyika katika eneo la kisesa kulingana na mkakati uliopo wa
kushirikisha wadau kutoa changizo la kuendeleza mradi, pia shirika linachukua hatua za kubadili
miche kuwa fedha (miche hii itapandwa na kusimamiwa katika ofisi zetu ndogo zilizopo Meatu
kata ya Kisesa na miche baadhi iliyopo katika makao makuu yetu hapa Ubungo, Dar es salaam).
Katika mradi huu ikiwa ruzuku itakoma shirika litaanzisha mradi wa maji ya kisima ambapo kila
mwananchi atanunua maji kwa bei ya shilingi mia tatu (300/=) kwa ndoo kubwa (lita 20) na
ndoo ndogo (lita 10) kwa bei ya shilingi mia na hamsini (150/=) kwa sababu ya changamoto ya
maji tunatarajia mradi huu utatoa gharama ya kuendeleza mradi.

FAIDA ZA MRADI HUU KWA TAIFA NA JAMII KWA UJUMLA.

Mradi huu utasaidia kwa kiwango kikubwa katika viwanda vya mbao na viwanda vidogo vidogo
vya utengenezaji samani, hivyo kuunga juhudi za sera ya raisi juu ya kuanzisha, kufufua na
kuendeleza viwanda. Mradi utachangia kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuajiri
wafanyakazi wawili, kutoa nafasi kwa wafanyakazi wa kujitolea na kuanzisha na kuendeleza
ajira kwa vijana kwa njia shirikishi ambapo serikali za mitaa zitahusika katika kusimamia
masilahi ya vijana hawa.

Mfuko wa Misitu wa Tanzania utanufaika kwa kiwango kikubwa ikiwa kama mradi huu utapewa
ruzuku kwa ajili ya utekelezaji basi utapunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa misitu na
upotevu wa miti ya asili.

9
BAJETI YA MRADI

Jedwali Na. 3: Kiolezo cha Bajeti ya Ruzuku ya Kati/Kubwa

Shughuli Kipimo (Kizio) Kiasi Gharama ya Gharama ya


Kizio (Tsh) Jumla (Tsh)
Ununuzi wa Shamba la Heka moja (1) Heka moja na 1,500,000/= 2,250,000/=
mradi Nusu
Ununuzi wa Jenereta la Jenereta moja (1) Jenereta moja (1) 1,080,000/= 1,080,000/=
umwagiliaji
Ununuzi wa mipira ya Rola moja (Mita Rola moja na 515,000/= 515,000/=
umwagiliaji 120) nusu (Mita 180)
Upandaji Miti Mti mmoja (1) Miti 1500 4,000/= 6,000,000/=
Uchimbaji wa kisima cha Kisima 1 Kisima 1 11,000,000/= 11,000,000/=
maji hatua za awali
Kukamilisha kuchimaba Kisima 1 Kisima 1 11,000,000/= 11,000,000/=
Kisima
Ununuzi wa pampu kisima Pampu moja (1) Pampu moja (1) 1,200,000/= 1,200,000/=
kwa umwagiliaji shamba
Darasa
Usafiri kwa ujumla kwa Mtoa huduma Watoa huduma 100,000/= 2,000,000/=
watoa huduma kwa miaka mmoja (1) kwa wane (4) kwa
5 mwaka 1 miaka 5
Uandaaji makala Makala 1 ya Makala 6 za 650,000/= 19,500,000/=
dakika 15 kila dakika 15 kila
Mwaka moja kwa Miaka
5
Jumla 54,545,000/=
Kiasi kinachoombwa toka kwenye mfuko 33,545,000/=
Michango inayotegemewa kutoka kwa wadau wengine 16,900,00/=
Mchango wa mwombaji 4,100,000/=
Muhimu: Gharama zote zinazohusiana na uandaaji wa ripoti, kulipa wafanyakazi na gharama za
usafiri na chakula kwa wafanyakazi wa kujitolea zote zitagharamikiwa na shirika.

10
Jedwali Na.1 Bao la Mantiki
MAELEZO KUHUSU MRADI VIASHIRIA VYA UTEKELEZAJI NAMNA NA VYANZO VYA UTHIBITIKAJI WA MADHANIO
MRADI MRADI
LENGO LA MRADI  Wananchi kuhifadhi miti na uoto wa  Mfuko wa ruzuku wa misitu Tanzania.  Utawala bora.
Kuwa na kizazi chenye asili bila shuruti.  Utekelezaji kwa vitendo kupitia Tanzania  Utoaji wa ruzuku kwa
kutuhifadhi misitu na  Ongezeko la kipato kwa wananchi Sustainable Development Implementation wakati.
kujiongezea kipato kupitia wengi kupitia mkaa wa mianzi, mbao, Organizatio, TSDIO.  Uendelezaji Amani na
upandaji miti kuni, na matunda. Ushirikiano
 Wananchi wengi kuwa na mashamba
binafsi ya miti na kufata sheria za
uhifadhi na ukataji miti.
KUSUDI LA MRADI  Ongezeko la asilimia 10 katika  Tanzania Sustainable Development  Upatikanaji wa ruzuku
 Wakazi wa mtaa wa uhifadhi wa misitu. implementation organization, TSDIO. ili kuendesha mradi.
mwamigagani kwenye kata  Uzalishaji wa mkaa utokanao na  Mfuko wa ruzuku wa misitu Tanzania  Umwagiliaji
ya Kisesa wapate kujifunza mianzi kuanza kutumika kutoka asilimi  Serikali ya kata ya Kisesa na mitaa yake. kukabiliana na ukame.
kwa vitendo kupitia mradi 0 kufikia asilimi 20 ya wakazi wote.  Wadau mbali mbali wa maendeleo ya mazingira  Ushirikishanaji wa
huu.  Utii wa sheria ya uhifadhi mazingira na misitu. elimu kati ya wananchi
 Kueneza elimu ya uhifadhi bila shuruti  Wananchi na watakelezaji yaani
miti na elimu ya sheria dhidi TSDIO.
ya uhifadhi miti katika mitaa
ya kata ya kisesa na Kata
jirani.
 Kuongeza kipato kwa
wananchi kupitia mkaa wa
mianzi, kuvuna miti ya
mbao, matunda na kuuza
miti ya mapambo.
MATOKEO YA MRADI  Kuwepo kwa kisima cha maji kwa  Tanzania Sustainable Development  Hakuna magonjwa na
 Wananchi kuwa na tabia ya ajili ya umwagiliaji. Implementation, TSDIO. maambukizi hatari ya

11
Jedwali Na.1 Bao la Mantiki
kujali na kuthamini thamani  Uwepo wa taarifa sahihi kuhusu  Mfuko wa ruzuku wa misitu wa Tanzania, TFS. ukuaji wa miti.
ya miti. maendeleo ya mradi.  Serikali ya kata na mitaa.  Kuwepo kwa mvua
 Utii wa sheria za kuhifadhi  Uwepo wa mtaalamu wa misitu na  Ripoti za mradi na taarifa za upelembaji na zisizojitoshereza.
misitu bila shuruti mtaalamu wa makala. utathimini wa mradi.  Upandaji wa miti ya
 Ongezeko la ujuzi kwa  Kuwepo na mbegu na Miche ya miti  Muundo mbinu wa umwagiliaji. muda mfupi (Isizidi
wananchi wa kujiongezea ya kutosha. miaka mitano kufika
kipato kwa kuuza mkaa  Kuwepo na uwajibikaji, kuthamini uvunaji)
unaotokana na mti wa muanzi muda na kupendana.
na kutoa ajira kwa wakazi.
SHUGHULI ZA MRADI  Kazi zote za mradi kufanyika Mhasibu na mtoa taarifa za mradi. Inafafanuliwa na msimamizi
 Kufanya manunuzi ya  Idadi ya wafakazi, malighafi na wa mradi na mwandaaji wa
shamba, na vifaa vya uwezeshaji kifedha ili kutekeleza mradi.
umwagiliaji. mradi.
 Uchimbaji kisima.
 Uandaaji wa vitalu na
upandaji miti.
 Kufanya tafiti ya utathimini
wa mapokeo ya mradi kwa
wananchi.
 Kutoa elimu ya sheria ya
uhifadhi misitu, kuanzisha
vikundi vya ulinzi shirikishi
kwa kushirikiana na serikali
za mitaa kuhifadhi misitu na
mali za jamii na elimu ya
nadharia katika vijiji jirani
juu ya uhifadhi misitu

12
BOARD OF DIRECTORS

GENERAL ASSEMBLY
ADVISORS CHIEF EXECUTIVE OFFICER

INTERNAL
AUDITOR UNIT

COMMUNICATION AND
MANAGING DIRECTOR OPERATIONAL FINANCE DIRECTOR
DISSEMINATION DIRECTOR
(SECRETARY GENERAL) DIRECTOR (TREASURER)
(G/SECTRETARY)
(CHAIR PERSON)
FUNDRISING
MEMBERSHIP ACCOUNTANT CORDINATOR
CORDINATOR PR MANAGER

HUMAN RESOURSES
MANAGER
UNIT
PROJECT CLIMATE CHANGE AND
CORDINATOR APPLIED METEOROLOGY COMMUNICATION AND
DIRECTOR PROJECT
TECHNOLOGY CORDINATOR
DIRECTOR
PROJECT FIELD VOLUNTEER
OFFICER TEAM LEADER
VOLUNTEER PROJECT FIELD
TEAM LEADER OFFICER

PROJECT
EDUCATION
CORDINATOR
DIRECTOR PEOPLE WITH DISABILITY PROJECT
DIRECTOR CORDINATOR
PROJECT FIELD VOLUNTEER
OFFICER TEAM LEADER
VOLUNTEER PROJECT FIELD
TEAM LEADER OFFICER

PROJECT HEALTH AND WELL BEING


CORDINATOR DIRECTOR SUSTAINABLE CULTUTE PROJECT
DIRECTOR CORDINATOR
PROJECT FIELD VOLUNTEER
OFFICER TEAM LEADER
VOLUNTEER PROJECT FIELD
TEAM LEADER OFFICER

PROJECT WORK AND ECONOMIC


CORDINATOR GROWTH ENVIRONMENT AND WATER
DIRECTOR SANITATION PROJECT
DIRECTOR CORDINATOR
PROJECT FIELD VOLUNTEER
OFFICER TEAM LEADER
VOLUNTEER PROJECT FIELD
TEAM LEADER OFFICER

PROJECT
GENDER
CORDINATOR INDUSTRY, INNOVATION AND
DIRECTOR PROJECT
INFRASTRUCTURE
DIRECTOR CORDINATOR
PROJECT FIELD VOLUNTEER
OFFICER TEAM LEADER
VOLUNTEER PROJECT FIELD
TEAM LEADER OFFICER

You might also like