You are on page 1of 3

Kamusi ya Kiswahili sanifu

Kwa mujibu wa TUKI (2014) wanasema hili ni toleo la tatu la Kamusi ya Kiswahili

Sanifu. Toleo la kwanza lilitolewa mwaka 1981, uandishi wa toleo hili ni ushirikiano wa

wanaleksikografia na wataalamu wa lugha na fasihi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo

Kikuu cha Dar es Salaam. Hili ni toleo la aina yake kwani limesheheni msamiati wa nyanja

mbalimbali kama vile sayansi na teknolojia, kompyuta na maneno mengine yaliyoibuka

kutokana na lugha kuwa na matumizi mapana. Katika toleo hili picha na michoro imeboreshwa

na kuvutia. Kuingizwa kwa picha hizo kutamsaidia msomaji kuelewa vizuri zaidi maana au kile

anachokitafuta kwenye kamusi. Katika kamusi hii mambo mapya mbalimbali yameingizwa kama

vile etimolojia ya maneno, ngeli zilizoainishwa kimofolojia, kisintaksia, na rangi kubainisha

visawe, misemo, nahau na methali. Wataalam mbalimbali wametoa vigezo vikuu vitatu vya

kuzingatia katika kuhakiki kamusi ambavyo ni: Wingi wa taarifa zilizoingiwa katika kamusi.

Kigezo cha pili ni Ubora wa taarifa iliyoingizwa kwa kila kidahizo na mwisho ni namna taarifa

zilivyowasilishwa katika kamusi.

Wingi wa taarifa zilizoingiwa katika kamusi, katika kigezo hiki taarifa

zinazohakikiwa ni pamoja na idadi ya vitomeo vilivyoingizwa, idadi ya maana zilizoorodheshwa

kwa kila kidahizo, idadi ya msamiati mpya ulioingizwa katika kamusi, msimbo wenye kuashiria

mitindo ya nyanja za matumizi ya kidahizo ilioonyeshwa na taarifa ya etimolojia. Kamusi ya

Kiswahili sanifu ina maneno mengi ya lugha na hutoa taaarifa nyingi na za kimsingi.taarifa hizi

ni pamoja na vidahizo, fasili ya vidahizo hivi, asili ya maneno,jinsi ya kutamka,matumizi ya


maneno,visawe na vinyume vya maneno hayo, kategoria ya maneno, mifano ya matumizi ya

vidahizo hizo nakadhalika.

Ubora wa taarifa iliyoingizwa kwa kila kidahizo, . katika kigezo hiki huzingatia taarifa

ambazo huingizwa katika kamusi zenye usahihi, kamilifu na wazi. Ni muhimu taarifa hizo

kuelezwa kwa urahisi ili kuweza kueleweka kwa msomaji.maneno yaliyo kwenye kamusi sanifu

ya Kiwsahili yana manufaaa anuwahi kwa msomi anayejifunza

namna taarifa zilivyowasilishwa katika kamusi.Katika kigezo hiki mambo ya kuzingatia wakati

wa kuhakiki ni jinsi taarifa zilivyoingizwa katika kamusi mfano, kuorodhesha maneno kialfabeti,

jinsi etimolojia ilivyoingizwa, mpangilio wa maana za maneno zilivoorodheshwa, uchapaji na

ukubwa wa maneno wenye hadhi tofauti. Mdee (keshatajwa) anaendelea kusema kuwa vipengele

vingine ambavyo hutumiwa katika kuhakiki kamusi ni: Mwaka wa kuchapishwa kwa kamusi,

idadi na weledi wa washauri waliohusika katika kutunga kamusi, idadi ya kurasa za kamusi na

wastani wa idadi ya maneno katika kitomeo.


 Marejeleo

Massamba. D.P.B.(2004 ). Kamusi ya isimu na falsafa ya lugha. Dares salaam: TUKI

Masebo . J. A. & Nyangwine. N. (2012). Kiswahili kidato cha tatu na nne . Dares salaam: nyambari

nyangwine publishers

Matinde. R. S. (2012). Dafina ya lugha. Isimu na nadharia. Kwa sekondari, vyuo va kati na vyuo

vikuu. Mwanza : Serengeti bookshop.

TUKI (1990).kamusi sanifu ya isimu na lugha. Dares salaam: Tuki na Educational publishers and

distributors ltd.

Wamitila. K. W. (2003). Kamusi ya fasihi, istilahi na nadharia. Nairobi: Focus publishers ltd.

You might also like