Professional Documents
Culture Documents
Secret Society s01
Secret Society s01
SOCIETY
(JAMII YA SIRI)
SEASON 1
MTUNZI: PATRICK.CK
SIMULIZI ZA MAPENZI
1.MISS TANZANIA
2.SERENA
3.BEFORE I DIE
4.BEYOND PAIN
SIMULIZI ZA UPELELEZI
5.PENIELA
6.QUEEN MONICA
7.THE FOOTBALL
8.I DIED TO SAVE PRESIDENT
9.KIAPO CHA JASUSI
10.KIKOSI CHA SIRI
11.SIRI
12.SCANDAL(KASHFA)
13.CAPTURE OR KILL MISSION
MAWASILIANO
0764294499
© 2020 Masimulizi.Haki zote zimehifadhiwa
DAR ES SALAAM
Tayari ni saa kumi na mbili
za jioni Mathew Mulumbi
alipowasili Nikita hotel moja ya
hoteli maarufu jijini Dar es
salaam.Alisimamisha gari katika
maegesho na kushuka akaelekea
ndani ya hoteli.Kabla hajaingia
ndani akasikia mbinja ikipigwa
akageuka na kumuona mtu
amekaa chini ya mwavuli
akatabasamu halafu akabadili
uelekeo akamfuata.Mtu Yule
ambaye umri wake ulipata miaka
hamsini hadi sitini alisimama na
kumpa mkono Mathew Mulumbi
“Karibu sana Mathew
Mulumbi” akasema Yule mzee
“Ahsante sana Profesa
Santala.Shikamoo”
“Marahaba
Mathew.Nimefurahi kukuona
tena.Nimuda mrefu hatujaonana”
akasema mzee Santala
“Ni kweli mzee majukumu
yamekuwa mengi” akajibu
Mathew.Muhudumu akafika mara
moja na kuwahudumia vinywaji
“Samahani sana Mathew
kama kwa namna yoyote ile
nitakuwa nimekusumbua kwa
kukuita hapa kwani nafahamu
wewe ni mtu mwenye mambo
mengi”
“Usijali mzee.Unapoitwa na
mtu kama wewe lazima uache
kila unachokifanya na kwenda
kusikiliza kitu ulichoitiwa”
akasema Mathew
“Nashukuru kwa
hilo.Mathew sitaki kuchukua
muda wako mwingi.Mathew
nimelazimika kukufuata mimi
mwenyewe kuzungumza nawe
.Kwa sasa niko
Arusha.Tumefungua chuo kipya
cha mafunzo ya ujasusi kilichopo
karibu na hifadhi ya Arusha.Nina
wanafunzi hamsini ambao
wanatarajiwa kumaliza mafunzo
ndani ya miezi mitatu ijayo.Vile
vile kuna wanafunzi wengine mia
moja na sabini wakiwa katika
ngazi mbali mbali za
mafunzo”akasema Profesa
Santala
“Hongereni sana kwa hatua
hii kubwa ya kuanzisha chuo cha
kuwafundisha vijana wetu ujasusi
hapa hapa nchini.Nakumbuka
enzi zetu tulikuwa tunakwenda
kujifunza nje ya nchi.Hii ni hatua
kubwa na ya kupongezwa sana”
akasema Mathew
“Ni kweli ni hatua
kubwa.Wanafunzi hao hamsini ni
darasa la kwanza kuhitimu katika
chuo hicho.Ninajisikia fahari
kuwa mkuu wa kwanza wa chuo
hicho” akasema mzee Santala na
kunywa kinywaji chake
“Mathew wanafunzi hao
hamsini wamefundishwa mambo
mengi sana na ninaweza kusema
wameiva ila kuna kitu kimoja
bado ninahitaji wakipate”
“Kitu gani mzee
Santala?Mathew akauliza
“Si somo rasmi ila nataka
vijana hawa wafundishwe nini
maana ya uzalendo wawapo
katika kazi hii ya ujasusi.Si
kwamba hawajafundishwa
uzalendo,wamefundishwa sana
lakini nahitaji wajifunze zaidi
kwa mifano hai.Mathew
nimekufuata kukuomba unisaidie
kuwapa elimu juu ya uzalendo
wanafunzi hawa.Wewe umekuwa
ni jasusi wa kutiliwia mfano
kabisa.Umeshiriki katika misheni
nyingi ndani na nje ya nchi kwa
mafanikio makubwa na hakuna
hata misheni moja ambayo
umewahi kushindwa.Mafanikio
yako yamesababishwa na kila
wakati kuitanguliza mbele
nchi.Hukuwahi kutanguliza
maslahi binafsi katika misheni
zako,kwako ni nchi kwanza”
akasema mzee Santala
“Mzee Santala” akasema
Mathe wna mzee Santala
akamfanya ishara asubiri kwanza
“Mathew nafahamu
unachotaka kukisema.Nafahamu
umejiweka pembeni na mambo ya
ujasusi na unajishughulisha na
biashara lakini bado unaweza
kuwa na msaada mkubwa kwa
taifa.Nataka vijana hawa
wajifunze kupitia kwako nini hasa
maana ya kujitoa kwa ajili ya taifa
lao kama ulivyofanya wewe.
Tafadhali Mathew naomba
usinikatalie katika hili jambo ni
muhimu sana.Tunataka
kutengeneza akina Mathew
Mulumbi wengine ili hata kama
ikitokea Mungu akakuita leo basi
tuwe na vijana wengine ambao
taifa linawategemea katika
ujasusi” akasema mzee Santala na
kumtazama Mathew ambaye
alitafakari kwa muda halafu
akauliza
“Ni muda gani ambao
unataka nikusaidie hilo jambo?
Mathew akauliza
“Wiki mbili zinatosha”
akajibu mzee Santala.Mathew
akafikiri tena kidogo halafu
akasema
“Mzee Santala wewe ni
mmoja wa watu ambao siwezi
kuwakatalia jambo na hasa
linapokuwa jambo lenye maslahi
makubwa kwa nchi kama hili
ulilolitaja.Tatizo sifahamu
nitaanzaje kuwafundisha vijana
hao hicho unachonitaka
nikawafundishe” akasema
Mathew
“Usihofu Mathew.Huna haja
ya kufanya
maandalizi.Unachotakiwa
kufanya ni kuwaeleza ukweli
mtupu ukiwapa mifano ya
misheni ambazo umewahi
kuzifanya nataka wapate picha
namna ya kulitanguliza taifa
mbele pale wawapo kazini au
katika misheni Fulani” akasema
mzee Santala
“Lini unataka nikaanze somo
hilo? Akauliza Mathew
“Jumatatu ijayo” akajibu
mzee Santala
“Nimekuelewa mzee.Leo ni
alhamisi nitafanya maandalizi
siku ya kesho na jumamosi
nitakuja Arusha ili siku ya
jumatatu nianze kazi hiyo”
akasema Mathew
“Nakushukuru sana Mathew
Mulumbi kwa kulikubali ombi
hili”
“Usijali mzee Santala.Tupo
kwa ajili ya taifa na pale
tunapohitajika kufanya jambo
Fulani lenye maslahi kwa taifa
basi hakuna kusita unatii mara
moja.Nitaweka mambo yangu
sawa siku ya kesho na jumamosi
nitakuja Arusha kama
nilivyokueleza” akasema Mathew
Walikuwa na mazungumzo
marefu na ilipotimu saa nne za
usiku wakaagana kila mmoja
akaondoka
“Nimelipokea ombi la
kufundisha vijana kwa mikono
miwili.Ni jambo jema sana kwani
lina maslahi makubwa.Taifa letu
linahitaji sana vijana wa kulilinda
lakini vijana hao lazima wawe
wamepikwa vilivyo wafahamu
thamani yao kw ataifa na wajue
nini wanapaswa kukifanya kwa
taifa lao.Kwa sasa tuko katika
mapambano ya uchumi na tunao
maadui wengi hivyo vijana hawa
lazima wafundwe kupambana
kwa ajili ya taifa lao” akawaza
Mathew Mulumbi akiwa garini
akielekea nyumbani kwake
ARUSHA
Saa mbili asubuhi siku ya
Jumatatu,Mathew Mulumbi
akawasili katika chuo cha ujasusi
kilichojengwa pembezoni mwa
hifadhi ya Arusha.Alipokewa na
profesa Santala
“Mathew Mulumbi karibu
sana katika chuo chetu” akasema
Profesa Santala na kisha
akamzungusha Mathew katika
chuo kile kumuonesha miundo
mbinu mbali mbali ya chuo
“Mnastahili pongezi Profesa
Santala.Chuo ni kizuri
sana.Hakina tofauti na vyuo
tulivyosoma nje ya nchi.Naamini
si muda mrefu wanafunzi kutoka
nchi nyingine barani Afrika
wataanza kuja hapa kujifunza
ujasusi.Hiki ni moja ya chuo bora
kabisa Afrika” akasema Mathew
halafu akaenda kutambulishwa
kwa wahadhiri wengine wa chuo
kile.
Hatimaye muda wa Mathew
kuingia darasani kufundisha
kipindi chake cha kwanza
ukawadia
“Mathew ondoa
hofu.Utaweza” akasema Profesa
Santala kisha akaongozana na
Mathew kuelekea katika darasa
analotakiwa kulifundisha.Profesa
Santala akawasalimu wanafunzi
halafu akawajulisha kuwa kuna
mgeni ambaye atakuwa nao kwa
muda wa wiki mbili
akiwafundisha somo maalum la
uzalendo kwa mifano.
“Anaitwa Mathew
Mulumbi.Yawezekana wengine
mmewahi kulisikia jina hilo basi
leo mmekutana naye ana kwa
ana.Huyu ni jasusi nguli na
atawaelekeza mambo mengi
ambayo mtakwenda kukutana
nayo katika kazi yenu na zaidi
sana uzalendo kwa nchi
yenu.Mtajiuliza kwa nini Mathew
Mulumbi awafundishe uzalendo
wakati mmekuwa mkifundishwa
tangu mlipoingia hapa chuoni?
Mtanijibu pale atakapokuwa
amemaliza kuwapeni
somo.Karibu Mathew” akasema
Profesa Santala na Mathew
akasogea ubaoni
“Kama alivyonitamblisha
Profesa Santala ninaitwa Mathew
Mulumbi.Kwa nusu ya umri
wangu nilionao sasa nimeifanya
kazi hii ya ujasusi hadi
nilipoamua kupumzika na
kuendelea na mambo mengine na
kwa sasa ninajishughulisha na
biashara japo kazi hii iko damuni
na ndiyo maana niko hapa mbele
yenu.Niliingia katika ujasusi
nikiwa bado kijana mdogo sana
na nilikuwa ndiye jasusi mdogo
zaidi kiumri katika shirika la
ujasusi Tanzania.Bado
naikumbuka simu niliyopigiwa
saa sita na dakika tano siku ya
jumanne na mtu aliyejitambulisha
kama mkaguzi wa polisi Damian
Mlanza akanitaka siku inayofuata
nisitoke nyumbani polisi watafika
kuna mambo wanataka kuja
kunihoji.Sikupata usingizi
nikakesha nikijiuliza nimefanya
nini hadi polisi
wanifuate?Nilijiuliza maswali
zaidi ya elfu moja na
kulipopambazuka nikawaeleza
walezi wangu wakanitaka
nikimbie lakini nikawaeleza
sintakimbia kwa kuwa sijafanya
kosa lolote na hakuna sheria ya
nchi niliyovunja.Nilibaki
nyumbani na kweli likafika gari la
polisi wakanichukua bila maelezo
yoyote nikaondoka nao
nikapelekwa kituo cha polisi na
pale nikaingizwa katika chumba
nikakutana na mzee mmoja
ambaye akajitambulisha kuwa
anatoka idara ya ujasusi na
akaniweka wazi kuwa nisihofu
hakuna kosa nililolifanya na
kwamba nimeshinda mtihani wa
kwanza wa kujiamini kwani
ingekuwa ni mtu mwingine
amepigiwa simu kuwa atafuatwa
na polisi na hajui amefanya kosa
gani angetoweka lakini mimi
nilijiamini sikufanya kosa
nikatulia.Huo ndio ulikuwa
mwanzo wangu wa kuingia katika
masuala ya ujasusi.Walipata
taarifa zangu na kuanza
kunifuatilia kwani nikiwa kidato
cha tano niliweza kuchunguza na
kuwabaini watu waliochoma
mabweni ya shule jirani.Vile vile
nikafanikiwa kuwapata watu
walioua mifugo ya shule yetu
hivyo nikaonekana ninafaa sana
katika mambo haya na baada ya
kumaliza kidato cha sita
wakanichukua.Huo ndio ulikuwa
mwanzo wa safari ndefu hadi
hapa nilipo sasa” NdivyoMathew
Mulumbi alivyoanza somo lake
Wakati Mathew Mulumbi
akifundisha,katika chumba cha
mikutano wahadhili walikuwa
kimya wakifuatilia katika runinga
kubwa kile alichokuwa
anakifundisha.Darasa lile lilikuwa
limeunganishwa na vifaa maalum
na mhadhili aliweza kufundisha
hata akiwa ofisini kwake.
Wanafunzi walionekana
kumwelewa sana Mathew kwani
alikuwa anafundisha kwa mifano
iliyowahi kumtokea.Lilikuwa ni
somo lenye msisimko
mkubwa.Madarasa mengine nayo
yaliunganishwa kielektroniki na
kile kilichokuwa kinaendelea
katika darasa la mwaka wa
mwisho.Chuoni kila kitu
kilisimama kwa muda wote
wakimfuatiliaMathew Mulumbi
**********
Mathew Mulumbi alitumia
saa mbili na nusu katika darasa
lake la kwanza kabisa na
alipotoka akapongezwa na kila
mtu pale chuoni.Akiwa katika
mazungumzo na profesa Santala
mara simu yake ikaita.Ilikuwa ni
namba ngeni katika simu yake
akatoka nje na kupokea
“Hallo” akasema Mathew
“Hallo Mathew
Mulumbi”ikasema sauti ya
mwanamke upande wa pili
“Nani mwenzangu? Mathew
akauliza
“Naitwa Linah Mpama
unanikumbuka?akauliza Yule
mwanamke
“Linah? Mathew akashangaa
“Ndiyo.Unanikumbuka
tuliwahi kukutana Arusha japo
imepita miaka mingi? Akauliza
Linah
“Ninakukumbuka
Linah.Siwezi
kukusahau.Nimefurahi leo
umenikumbuka.Unaendeleaje?
Hawajambo wadogo zako Flora
na Jonathan? Mathew akauliza
“Wote wazima kabisa”
“Tena imekuwa vyema
umenipigia.Mimi niko hapa
Arusha kwa siku chache nitakuja
kuwatembelea bado mko Arusha?
Mathew akauliza
“Hapana Mathew hatuko tena
Arusha tumekwisha hama tuko
Dar es salaam” akasema Linah
“Basi nitakaporejea
nitakutafuta tutaonana” akasema
Mathew
“Mathew nimekutafuta nina
shida kubwa nahitajimsaada”
“Msaada upi unahitaji Linah?
“Kuna watu wanataka
kuniua.Niko katika hatari kubwa
na muda wowote naweza
kuuawa” akasema Linah
“Nani wanataka kukuua na
kwa nini?
“Mathew ni jambo kubwa
nitakueleza pale tutakapoonana
lakini kwa sasa naomba utafute
namna ya kunisaidia”
“Linah niko mbali kwa
sasa.Kwa nini usiende kutoa
taarifa katika kituo chochote cha
polisi kilicho karibu yako?
“I Can’t ! akasema Linah
“Kwa nini Linah?
“Mathew please help me.Ni
wewe pekee ambaye ninakuamini
kwamba unaweza kunisaidia na
kuniondoa katika hatari hii
kubwa” akasema Linah
“Linah ningekuwa karibu
ningekusaidia lakini niko
mbali.Kitu gani kinakufanya
usiende kutoa taarifa polisi
kuhusu hao wanaotaka kukuua?
Akauliza Mathew
“It’s because I killed
someone”akasema Linah na
Mathew akastuka
“You killed someone?
Mathew akauliza
“Yes” akajibu Linah na
Mathew akavuta pumzi ndefu
“Mathew please help me !
akalia Linah
“Kwa sasa uko wapi?
“Nimejificha kwa rafiki
yangu” akajibu Linah
“Sawa Linah.Naomba utulie
hapo hapo wakati ninafanya
utaratibu wa kurejea Dar es
salaam leo hii hii kuja
kukusaidia.Tafadhali usiondoke
mahala hapo” akasema Mathew
“Nashukuru sana
Mathew”akasema Linah na
kukata simu.
“Is this true? Akajiuliza
Mathew na kuirejesha kichwani
picha ya msichana mdogo
aliyekutana naye miaka kumi na
tano iliyopita
“Lina Yule niliyekutana naye
miaka ile leo hii ananiambia kuwa
ameua mtu ! haya ni maajabu.I
need to help her.Lazima nirudi
Dar es salaam leo hii hii nikajue
nini kimetokea nione namna ya
kuweza kumsaidia.Hadi
amenipigia mimi simu inaonesha
hana mtu mwingine ambaye
anaweza akamsaidia” akawaza
Mathew na kumfuata Profesa
Santala akamueleza kuwa
amepata dharura na anatakiwa
kurejea Dar es slaam mara moja.
“Hakuna tatizo Mathew
Mulumbi unaweza ukaenda
kutatua tatizo hilo na ukarejea
tena au tutatumia mfumo wa
kielektroniki ili uweze kufundisha
hata ukiwa Dar es salaam”
akasema Profesa Santala
Mathew hakupoteza muda
akaondoka pale chuoni na kuanza
kushughulikia usafiri wa kurejea
Dar es salaam akafanikiwa kupata
nafasi katika ndege ya shirika la
ndege la Tanzania inayoondoka
Arusha saa kumi alasiri.Wakati
akisyubiri muda ufike akaenda
kupumzika hotelin “Angekuwa
ni mtu mwingine nisingekubali
katu kwenda kumsikiliza lakini
Linah lazima nikamsikilize nijue
nini hasa kimemsibu hadi akaua
mtu.Sura ya kimalaika ya binti
Yule bado iko kichwani kwangu
hadi leo na inaniwia ugumu
kuamini eti amemuua mtu”
akawaza Mathew akiwa
anakusanya nguo zake tayari kwa
safari ya kurejea Dar es salaam.
“She was a beautiful kid japo
mambo yake yalikuwa makubwa
kuzidi umri wake.Nilistaajabu
namna alivyofahamu mambo
makubwa ambayo kwa binti wa
umri wake hakupaswa kuyajua”
akawaza Mathew na kurejesha
kumbu kumbu nyuma
MIAKA 15 ILIYOPITA
Ilikuwa ni siku ya Jumanne
Mathew Mulumbi alipowasili
katika jijini Arusha akitokea Dar
es salaam kwa ajili ya kutekeleza
misheni muhimu aliyotumwa na
viongozi wake.Alipokewa na
mmoja wa wafanyakazi wa
shirika la ujasusi ofisi ya Arusha
na kumpeleka katika nyumba
ambako angekaa kwa muda
ambao angekuwepo hapo
Arusha.Ilikuwa ni nyumba nzuri
na kubwa.Ilikuwa na vyumba
vitatu vya kulala,jiko,chumba cha
kulia chakula,sebule
kubwa,chumba cha
maongezi,maktaba ndogo,na
chumba ambacho kingetumika
kama ofisi ya nyumbani bila
kusahau gereji ya gari.Pembeni
kidogo ya nyumba hiyo ya
Mathew kulikuwa na jumba
lingine kubwa la kifahari
Siku ya Jumatano Mathew
alianza rasmi kuifanya kazi
ilimpeleka Arusha.Aliondoka
nyumbani saa mbili za asubuhi na
kurejea nyumbani saa tatu za
usiku.Toka alipofika Arusha
hakupumzika alitoka asubuhi na
kurejea nyumbani usiku.Jumapili
aliamua kupumzika nyumbani
akachukua kitabu chake cha
hadithi akaenda kuketi kandoni
mwa bwawa la kuogelea akiwa
na chupa yake ya mvinyo
pembeni.Akiwa amezama katika
hadithi ile tamu akasikia sauti za
watoto wakimsalimu.
“Shikamoo uncle” Mathew
akageuka na kukutana na sura
zenye tabasamu za watoto wawili
wa kike na kiume ambao bila hata
ufafanuzi lazima ungegundua
kwamba ni mapacha.Walikuwa
wanafanana mno.Mathew
akatabasamu na kucheka kidogo
kwa namna watoto wale
walivyofanana.
"Marahaba hamjambo?
“Hatujambo" wakajibu kwa
pamoja watoto wale
walioonekana wachangamfu
sana.Wakamsogelea Mathew pale
katika kiti wakaa pembeni yake.
“Uncle unaitwa nani?
akauliza mmoja wao
“Ninaitwa Uncle Mathew
Mulumbi.Wewe unaitwa nani?
“Mimi naitwa Flora na huyu
anaitwa Jonathan" akasema
mmoja wao ambaye alionekana
muongeaji sana.
“Nimefurahi
kuwafahamu”akasema Mathew
huku akikifunika kitabu chake.
“Uncle Mathew watoto wako
umewaacha wapi? akauliza
Jonathan.Mathew akacheka
kidogo
"Sina mtoto..." Mathew
akajibu
“Jumba lote hili unaishi
mwenyewe? akauliza tena
Jonathan
“Ndiyo ninaishi mwenyewe"
Mathew akajibu
“Mke wako yuko wapi?
akauliza Flora.Mathew
akastaajabu maswali ya wale
watoto wadogo
“Mnapenda juisi? Akauliza
Mathew
“Ndiyo uncle” wakajibu na
Mathew akawachukua wakaenda
ndani na kuwapatia juisi na
biskuti.Aliwafurahia sana wale
watoto kwa uchangamfu
wao.Kwa muda mfupi watoto
wale walimzoea sana na wakati
akiandaa chakula cha mchana
dada yao akiwaita
“Dada anatuita" akasema
Flora.
Mathew akainuka na
kuelekea nje.Mlangoni alisimama
binti mmoja mweupe aliyevaa
fulana ya mikanda.Chini alivaa
kaptura iliyomfika
magotini.Mathew akastuka baada
ya kukutanisha macho na sura
yenye tabasamu la mstuko la binti
yule.
“Mambo kaka" akasema binti
yule ambaye kiumri yeye na
Mathew hawalingani.Mathew
akababaika kuijibu salamu ya
binti yule.Akabaki akimtazama.
“Kaka nakusalimia" akasema
tena yule binti ambaye
hakuonekana kuwa na wasiwasi
wowote
“Hujambo? Akajibu Mathew
“Sijambo.Kumbe wewe
ndiye uliyehamia humu? akauliza
yule binti huku akiona aibu kwa
mbali
“Ndiyo ni mimi" Mathew
akajibu
“Karibu sana.Mimi naitwa
Linah.Sisi tunaishi nyumba hiyo
ya pembeni.Unaitwa nani?
Akauliza Linah .
“Naitwa Mathew Mulumbi"
akajibu Mathew
“Ouh !.Jina zuri sana"
akasema Linah.
“Karibu ndani Linah”
akasema Mathew
“Nawahitaji akina Flora”
akasema Linah
"Wako humu ndani
wanaangalia katuni.Karibu
ujumuike nasi" akasema Mathew
“Ahsante lakini naogopa
kupigwa” akasema Linah huku
akimfuata Mathew kuelekea
sebuleni
“Upigwe na nani ? Mathew
akauliza
“Na wenye nyumba” akajibu
Linah na kumfanya Mathew
aangue kicheko akamkaribisha
Linah sebuleni
“Unatumia kinywaji gani
Linah? Akauliza Mathew.Linah
akatabasamu na kusema
“Una bia yoyote humu ndani
au mvinyo? Akauliza Linah na
kumfanya Mathew astuke akabaki
akimtazama.
“Mbona umestuka
Mathew.Unashangaa mimi
kunywa bia au mvinyo?Akauliza
tena Linah.Mathew akatabasamu
na kusema
“Ndiyo nimestuka kidogo
kwa sababu vinywaji hivyo ni
vikali na haviwezi kukufaa.Humu
nina Ice cream,juice
mbalimbali,soda na maji”
akasema Mathew.
“Watoto wadogo kama hawa
akina Jonathan ndio hawatumii
vinywaji vikali lakini mimi
ninatumia hasa mvinyo” akasema
Linah huku akicheka kichini chini
“Kwa hiyo nikupatie
kinywaji gani Linah? Akauliza
Mathew
“Nashukuru sihitaji chochote
kwa sasa.Kuwa na amani
Mathew” akajibu Linah na
kumfanya Mathew azidi
kumstaajabia binti yule mdogo.
Mathew akaenda kuketi
sofani akaendelea kumfanyia
usaili Linah.
“Anaonekana ni binti mdogo
lakini mambo yake ni tofauti
kabisa na umri wake
ulivyo.Anaongea kwa kujiamini
sana na macho yake makavu hana
aibu hata kidogo.Nilishangaa sana
aliponipa ile salamu.Anapaswa
kunisalimu shikamoo kaka lakini
badala yake akaniambia eti
mambo kaka.Amenistua zaidi
alipohitaji bia au mvinyo.Umri
huu anatumia kilevi !!
Nimeshangaa sana” Akawaza
Mathew
“Mathew sebule yako
nzuri”akasema Linah huku
akitabasamu baada ya kuona
kumekuwa kimya sebuleni.
“Ahsante Linah..” akajibu
Mathew.
“Ana sauti nzuri,sura
nzuri.Kiujumla mtoto huyu ni
mzuri kupindukia.Nasikitika si wa
umri wangu.Naogopa hata kukaa
naye humu ndani wazazi wake
wasije wakaanza kuniletea
matatizo”akawaza Mathew
Wakati Mathew akiendelea
kumtazama Linah kwa kuibia ibia
mara simu ya Linah
ikaita.Akaipokea na kuongea
kidogo kisha akasimama.
“Mathew nawachukua akina
Flora wanapelekwa saluni na
dereva.Nitakuja baada ya muda
mfupi .Au unatoka? Akauliza
Linah.
“Hapana Linah leo ni siku
yangu ya mapumziko,nitakuwepo
nyumbani muda wote.” Akajibu
Mathew.
“Basi vizuri nitarejea baada
ya muda mfupi.Ngoja niwapeleke
hawa watoto” akasema Linah na
kuwashika mikono Jonathan na
Flora akaondoka nao.
“Ama kweli leo nimepatwa
na mshangao.Anasema anarudi
baada ya muda mfupi,sijui
niondoke ili akija
asinikute?Nimemuogopa hata
kukaa karibu naye.Naogopa
iwapo wazazi wake watamkuta
akiwa huku kwangu ninaweza
kuletewa shida.Linah amenizoea
kwa haraka sana mpaka
nimeshangaa.Ninatakiwa
kutokumzoea huyu binti anaweza
akaniletea matatizo” Mathew
alizama mawazoni na mara
mlango ukafunguliwa Linah
akaingia akiwa ameshika mfuko
wa karatasi huku akitabasamu.
“Nimerudi Mathew.Jonathan
na Flora wameenda Saluni
nimebaki peke yangu.Ninahisi
upweke nikiwa peke yangu
ndani” Akasema Linah na
kuuweka ule mfuko wake wa
karatasi mezani.
“Usihofu Linah karibu.Baba
na mama wamesafiri ? akauliza
Mathew
“Unamzungumzia baba
Clemence na mama Blandina?
Akauliza Linah
“Ndiyo” akasema
Mathew.Linah akainama akafikiri
kidogo na kusema
“Wale ni walezi
wangu”akasema Linah
“Wazazi wako wanaishi
wapi? Akauliza tena
Mathew.Linah akanyamaza
kidogo halafu akajibu
“Wazazi wangu walikwisha
fariki” Mathew akastuka kidogo
na kusema
“ouh pole sana Linah.Sikujua
kama umewapoteza wazazi wote
wawili” akasema kwa masikitiko
Mathew.
“Usijali Mathew.Haya ni
mambo ya kawaida na ambayo
yanatutokea sisi sote” akasema
Linah.
“Nilipotambulishwa kwa
mzee Clemence kuwa ndiye
mmiliki wa nyumba hii nikadhani
ndiye baba yako mzazi.”
Akasema Mathew
“Hapana yule ni mlezi
wangu.Sina undugu naye
wowote.Aliwahi kuwa rafiki
mkubwa wa baba kwa hiyo baada
ya wazazi wetu kufariki
akatuchukua na kutulea” akasema
Linah.
“Ndugu zako wengine wako
wapi? akauliza Mathew
“Ndugu pekee
tunayemfahamu ni hawa
wanaotulea wengine wote hatuna
muda nao” akajibu Linah
“Kuna tatizo lolote lilitokea
kati yenu na hao ndugu zenu?
Akauliza Mathew
“Ni historia ndefu kidogo
lakini kwa ufupi tu ni kwamba
baada ya wazazi wetu kufariki
ulitokea mgogoro mkubwa wa
mali na kutuacha masikini.Kama
si huyu mzee kutuchukua na
kutulea yawezekana mimi na
wadogo zangu hivi sasa
tungekuwa watoto wa mitaani
wakati baba yetu alikuwa ni
bilionea”
“Pole sana
Linah..Umekumbana na mikasa
mizito wakati bado mdogo”
akasema Mathew
“Udogo wangu nini Mathew?
Au unanipima kwa umbo?
Akauliza Linah na kumfanya
Mathew acheke kidogo.
“Kwa kweli umbo lako
linaonyesha bado wewe ni binti
mdogo” akasema Mathew na
kumfanya Linah acheke kicheko
kikubwa.
“Usidharau reli
Mathew.Pamoja na wembamba
wake lakini inabeba vitu vizito”
akasema Linah huku akicheka.
“Sijakudharau Linah lakini ni
umbo lako ndilo linaonyesha
kwamba bado ni binti
mdogo.Unaweza ukaniambia una
miaka mingapi?
“C’mon Mathew sitaki
kuzungumzia masuala hayo ya
miaka”akasema Linah na
kumfanya Mathew
atabasamu.Linah akauchukua ule
mfuko wake wa karatasi aliokuja
nao akatoa chupa ya mvinyo na
kuiweka mezani.
“Mathew unatumia kinywaji
hiki? Akauliza Linah .Mathew
akashindwa ajibu nini akabaki
akimkodolea macho hakuyaamini
macho yake
“Mathew unatumia hiki
kinywaji? Akauliza tena
Linah.Mathew akamtazama na
kuuliza
“Linah unatumia hii pombe
kali? Akauliza Mathew
“Ndiyo.Hiki ni kinywaji
changu hasa kwa siku za mwisho
wa wiki na nyakati ambazo huwa
nina furaha.Kwa siku ya leo
ninafuraha kubwa na ndiyo maana
ninataka kunywa kinywaji
hiki.”akasema Linah.Mathew
akaichukua chupa ile akaisoma na
kuirudisha mezani akamtazama
Linah.
“Linah unasoma darasa la
ngapi? Akauliza Mathew
“Usiulize darasa sema kidato
cha ngapi? Darasa ni kwa watoto
wadogo” akasema Linah na
kumfanya Mathew atabasamu
“Leo nimekutana na kiboko
yangu” akawaza Mathew
“Uko kidato cha ngapi?
Akauliza tena Mathew
“Mathew niwapo nyumbani
au katika sehemu za mapumziko
sipendi kuongelea sana masuala
ya shule.Kama hutajali naomba
tafadhali usiniulize masuala ya
shule au maisha binafsi kwa
sasa.Nataka nifurahi.Ila kama
huridhiki kwa mimi kukaa hapa
kwako its ok I can just leave…”
akasema Linah.
“Samahani Linah kama
umekwazika kwa maswali
niliyokuuliza.Hofu yangu mimi
ilikuwa ni kwa walezi wako
wakija na kukukuta huku kwangu
tena ukiwa na chupa ya mvinyo
wanaweza wakaniletea matatizo”
akasema Mathew kwa sauti ya
upole
“Walezi wangu wamekwenda
safari watarudi wiki ijayo"akajibu
Linah
“Kama ni hivyo basi vizuri"
akasema Mathew huku akipiga
hatua kwenda jikoni na kuchukua
glasi mbili na vipande vya
barafu.Akajimiminia mvinyo
katika glasi na kwenda kuketi
sofani.Linah naye akajimiminia
mvinyo akanywa na kukohoa
kidogo halafu akageuza kichwa
na kumtazama Mathew ambaye
alikuwa amemkodolea macho ya
mshangao.
“Mathew mbona
unaniangalia hivyo? Mimi
najisikia vibaya sana
unavyonitazama namna
hiyo.Mathew nina kitu gani cha
ajabu kinachokufanya unitazame
namna hiyo? au unashangaa kwa
mimi kunywa pombe? Sioni kama
ni kitu cha ajabu." akasema Linah
“Linah imenibidi nishangae
kidogo kwa sababu ni mara yangu
ya kwanza kumuona binti wa
umri wako akinywa kinywaji
kikali kama hiki" akasema
Mathew
"Mathew nimekwambia
usiniweke mimi katika kundi la
watoto.Mimi si mtoto mdogo
kama unavyofikiri" akasema
Linah
“Samahani Linah.Usinifikirie
vibaya lakini ninasema hivyo kwa
sababu ninakujali kama mdogo
wangu.Vinywaji vikali kama hivi
havifai kwenu ninyi wanafunzi"
akasema Mathew.Linah akainuka
pale sofani akaifunga ile chupa ya
mvinyo akairudisha katika mfuko
wake wa karatasi akazirusha
nywele zake nyuma na
kumtazama Mathew.
“Nilitegemea ningepata
kampani ya maana toka kwako
badala yake umeanza
kunikashifu.Tayari siku yangu
imeharibika.Kwa heri Mathew”
akasema Linah huku akipiga
hatua kutoka nje.
“Linah usikasirike mdogo
wangu sikuwa na maana mbaya
kukwambia vile”akasema
Mathew lakini Linah hakugeuka
akatokomea zake.
**********
Mathew alistuka saa tatu za
usiku.Alikuwa amelala sana
kutokana na uchovu wa wiki
nzima.Kwa uchovu akainuka na
kukaa kitandani.Wakati
akijinyoosha nyoosha mlio wa
ujumbe mfupi wa maandishi
ukasikika katika simu
yake.Akanyoosha mkono na
kuichukua simu akaanza kuusoma
ujumbe ule ambao ulitoka katika
namba ambazo hakuwa
akizifahamu.
" Mathew nafahamu
nilikuudhi kwa maneno
yangu.Naomba tafadhali kama
nilikuudhi kwa namna yoyote ile
unisamehe na ukubali tuwe
marafiki tena.mwisho naomba
uniruhusu nikupigie simu walau
niisikie sauti yako nzuri yenye
kunipa wazimu....Linah" Mathew
akavuta pumzi ndefu
“Amepata wapi namba zangu
huyu binti? akawaza Mathew
akainuka na kukaa kitandani.Kwa
dakika chache akawa katika
mawazo mengi.Sura ya Linah
ikamjia tena kichwani akausoma
tena ujumbe ule uliotoka kwa
Linah na kutikisa kichwa.
“Nashindwa kumuelewa
huyu mtoto.Nimemfahamu kwa
muda mfupi tu lakini mambo
yake ni makubwa na ya
kushangaza.Kitu kingine cha
kushangaza ni wapi amezipata
namba zangu za simu" akawaza
Mathew halafu akaitupa simu
pembeni akajilaza tena kitandani.
“Inanibidi niwe mwangalifu
sana na huyu mtoto.Mwelekeo
wake si mzuri .Anaweza
akanisababishia matatizo"
akawaza Mathew na kujigeuza
upande wa pili na mara
akastuliwa na sauti ya mlio wa
ujumbe mfupi katika simu
yake.Akageuka na kuichukua
akaufungua ujumbe
ule.Alipousoma akajikuta
akikunja uso.
“Its her again...Huyu binti
anataka kitu gani kwangu?
Natakiwa kumkemea ili apunguze
mazoea na mimi.Ngoja nikatolee
uvivu haka katoto ili kasiendelee
kunizoea." akasema Mathew huku
akiziandika zile namba za Linah
na kupiga.Simu ikaanza
kuita.Mathew alikuwa amekunja
uso kwa hasira
“Hallo Mathew,ahsante kwa
kupiga" ikasema sauti laini ya
Linah.Kabla Mathew hajajibu
Linah akaendelea.
“Mathew samahani kwa
kukusumbua usiku huu.Uko
kitandani? akauliza Linah kwa
sauti laini.Mathew akajikuta
akitabasamu akashindwa ajibu
nini
"Sijui nikajibu nini haka
katoto.Sijui nikafokee kaache
mazoea na mimi...Lakini ngoja
nikasikie kanataka nini" akawaza
Mathew.
Mathew nakuuliza umelala?
akauliza tena Linah
“Sijalala Linah" akajibu
Mathew na kukohoa kidogo
“Pole" akasema Linah
"Pole ya nini? Mathew
akauliza
“Nimekusikia unakohoa.Pole
sana.Kifua kinakusumbua?
akauliza Linah
“Hapana sisumbuliwi na
kifua” akajibu Mathew
“Mathew sema basi hata
ahsante.Mwenzio amekupa pole
na husemi hata ahsante" akasema
Linah kwa sauti laini.Mathew
akatabasamu na kusema
“Ahsante” Kimya kifupi
kikapita halafu Linah akasema
“Unafanya nini muda huu
Mathew?.Mathew akafikiri
kidogo na kujibu.
“Nimejilaza tu hapa
kitandani”
“Uko na nani? akauliza Linah
“Niko peke yangu" akajibu
Mathew halafu akaukunja uso
wake.
“Umevaa nini usiku huu?
akauliza Linah na kumfanya
Mathew abaki kimya akishangaa
“Haka katoto ..!!
“Nijibu basi Mathew umevaa
nini usiku huu? akauliza tena
Linah
"Nimevaa nguo za kulalia"
akajibu Linah.
“Nguo gani? suruali
,kaptura,shati,kanzu au nini?
Mathew akacheka kidogo na
kusema
“Linah naomba unisikilize"
akasema Mathew lakini kabla
hajatamka lolote Linah
akasema
“Naomba kwanza unisikilize
mimi Mathew halafu na mimi
nitakusikiliza.Mimi ndiye
niliyekuwa wa kwanza kukutumia
ujumbe.Nisikilize kwanza
ninachotaka kukwambia halafu na
mimi nitakusikiliza hata kwa
usiku kucha" akasema
Linah.Mathew akazidi kuikunja
sura yake
“Haya sema haraka
unachotaka kuniambia" akasema
kwa sauti ya ukali Mathew.
“Usikasirike Mathew.Nataka
tuongee kirafiki tu.Najua uko
mwenyewe mida hii na mimi niko
mwenyewe.Najua unahisi upweke
mkubwa kwa kuwa peke yako
mida hii na ndiyo maana
nimeamua kukupigia tuongee ili
ufurahi au nimefanya vibaya
Mathew? Akauliza Linah na
kumfanya Mathew atingishe
kichwa chake huku akitabasamu.
“Dah ! Huyu mtoto” akawaza
Mathew.
“Mathew najua unaniona
mimi kama mtoto mdogo labda
kutokana na umbo na muonekano
wangu lakini katika umbo hili hili
na muonekano huu huu ninaweza
nikawa rafiki yako mkubwa na
ambaye nikakufanya ukatabasamu
na kuifurahia dunia" akasema
Linah.
“Linah nani amekupa namba
zangu za simu? akauliza Mathew
kwa sauti ya ukali.
“Mathew kuna kitu kimoja
ambacho ninapaswa
kukukumbusha japokuwa mimi ni
mtoto mdogo kama
unavyonichukulia.Wewe ni
msomaji wa maandiko
matakatifu? akauliza Linah.
“Ndiyo ninasoma" akajibu
Mathew
“Good.Nadhani umesoma
biblia japo kidogo japokuwa
hauonekani kama ni mtu wa
kusoma maandiko.Katika biblia
takatifu agano la kale kitabu cha
mwanzo moja,mstari wa kwanza
hadi wa tano inasema kwamba
Hapo mwanzo Mungu aliziumba
mbingu na nchi.Nayo nchi
ilikuwa ukiwa,tena utupu, na giza
lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya
maji, Roho ya Mungu ikatulia juu
ya uso wa maji. Mungu akasema,
Iwe nuru; ikawa nuru.
Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni
njema; Mungu akatenga nuru na
giza. Mungu akaiita nuru Mchana,
na giza akaliita Usiku.." akasema
Linah na kunyamaza kidogo..
“Unataka kunifundisha nini?
akauliza Mathew akionesha
kuzidi kukerwa na Linah.
“Kuna jambo nataka
nikueleweshe kwa sababu
nikisema nataka kukufundisha
utasema kwamba huwezi
kufundishwa na mtoto" akajibu
Linah
“Linah nimekwisha choshwa
na wewe.Naomba useme
unachotaka kukisema ninahitaji
kupumzika” akafoka Mathew
“Usihofu Mathew
utapumzika,tena utalala usingizi
mnono sana endelea kunisikiliza"
akasema Linah na kunyamaza
kidogo halafu akaendelea.
“Mwenyezi Mungu alikuwa
na makusudi yake alipoumba
usiku.Aliuweka usiku maalum
kwa ajili ya mapumziko ya
viumbe wake wote aliowaumba
na ndiyo maana hata wanyama na
wadudu hupumzika usiku.Kwa
maana hiyo usiku si wakati wa
kukasirika wala kuongea kwa
sauti ya juu ya ukali.Ili kuupa
usiku hadhi yake unapaswa
kuongea lugha nyepesi,kwa
kutumia sauti laini hasa kama
unaongea na mtu wa jinsia ya
tofauti na yako.Kwa hiyo Mathew
nakuomba usiwe na hasira
,tabasamu na uongee na kucheka
na mimi kwa usiku huu.Mathew
nataka tuongee kama
marafiki,japokuwa hatulingani
kiumri lakini hicho si kigezo cha
mimi na wewe kushindwa kuwa
marafiki.Kuna mambo mengi
ambayo tunaweza
tukaongea,tukabadilishana
mawazo na hata kusaidiana
ikibidi" akasema Linah
“Unataka nikusaidie kitu gani
Linah? akauliza Mathew
“Sihitaji unisaidie kitu
chochote kile kwa sababu
ninajitosheleza kwa kila kitu
lakini ninachokiomba toka kwako
ni mimi na wewe kuwa marafiki"
akasema Linah.Mathew akacheka
kidogo na kusema
“Linah unanifurahisha
sana.Mimi na wewe hatuwezi
kuwa marafiki.Kwanza umri wetu
haulingani,pili mimi ni
mfanyakazi na wewe ni
mwanafunzi kwa hiyo tuko katika
dunia mbili tofauti sana.Linah
wewe ni kama mdogo wangu na
si kama rafiki yangu" akasema
Mathew na kumfanya Linah
acheke kwa nguvu.
“Mathew umenifurahisha
sana.Hatuvunji katiba ya nchi
kwa mimi na wewe kuwa
marafiki.Kuna kitu kimoja
ambacho wewe na wengine wengi
huwa
mnajichanganya.Ninapozungumzi
a urafiki sina maana ya kwamba
mimi na wewe tuwe na
mahusiano ya kimapenzi.Achana
na ile dhana kwamba kuwa na
rafiki wa jinsia tofauti basi ni
lazima mjiingize katika masuala
ya ngono" akasema Linah na
kumfanya Mathew atabasamu.
“Haka katoto kanaonekana
kamekomaa sana kiakili.Kana
zungumza mambo makubwa
tofauti na umri wake." akawaza
Mathew.
“Kwa hiyo Mathew mimi na
wewe tunaweza kuwa marafiki
wa kawaida tu japokuwa tuko
katika dunia mbili tofauti kama
ulivyosema." akasema Linah
“Najua kwa muda huu
utakuwa ukiwaza kwamba huyu
mtoto anataka nini
kwangu.Sihitaji chochote toka
kwako Mathew zaidi ya kuwa
marafiki kwa sababu nimeona
kuna vitu vinavyoweza kutufanya
tukawa marafiki wakubwa.Vile
vile ninataka kukusaidia kwa
mambo mawili matatu hivi"
akasema Linah
“Mambo gani hayo ambayo
unataka kunisaidia? akauliza
Mathew huku akitabasamu
“Ninataka kukusadia
kukuondolea upweke ulionao"
akasema Linah na Mathew
akacheka tena kwa nguvu.
“Usinivunje mbavu zangu we
mtoto.Upweke huo unawezaje
kuuondoa? akauliza Mathew
huku akicheka.
“C'mon Mathew naomba
usiniite mimi mtoto wakati hata
wewe bado ni mtoto kwa mama
yako.Naomba tuitane kwa majina
yetu Linah au Mathew.Kuhusu
upweke ninaweza kukusaidia
ukaondokana nao..Niambie
kwanza una mpenzi au huna?
..Akauliza Linah.Mathew akasita
kujibu
“Nijibu Mathew una mpenzi
au huna? akauliza tena Linah
"Ninaye" akajibu
“Yuko wapi ?
“Yuko nje ya nchi" akajibu
Mathew
“Ok Vizuri.Mara ya mwisho
umekutana naye lini? akauliza
Linah
"Miezi kadhaa iliyopita"
“Sawa.Ukimkumbuka sana
huwa unafanya nini?
"Sijakuelewa unamaanisha
nini? akauliza Mathew
“Nina maana kwamba siku
ukiwa na hamu naye,hamu ya
kufanya naye mapenzi si unajua
tena kwa binadamu aliyekamilika
hii ni hali ya kawaida kutokea na
yeye yuko mbali huwa unafanya
nini ? Be honnest with me.."
akasema Linah.Mathew akakaa
kimya.
"Haka katoto kana wazimu
nini? maswali gani haya ya
kuniuliza? akawaza Mathew na
kuikunja sura
“Mathew mbona hunijibu?
akauliza Linah na mara Mathew
akakata simu...
“Hana adabu huyu mtoto !
akasema Mathew kwa hasira na
simu yake ikaita.Akatazama
mpigaji alikuwa ni Linah.
"Ni yeye tena" akasema
Mathew kwa hasira.Akaipokea
simu ile na kusema kwa ukali
“Linah unataka nini kwangu?
Kwa nini unakuwa msumbufu
namna hiyo? akauliza Mathew
kwa ukali.Linah akacheka kidogo
na kusema kwa sauti ndogo..
“Mathew nimekwisha
kueleza kwamba ukifanya hivyo
unavunja taratibu za
usiku.Usipige kelele au kuongea
kwa ukali.Ongea kwa sauti ndogo
yenye kuvutia kama
ninavyoongea mimi" akasema
Linah halafu kikapita kimya
kifupi
“Mathew nakuomba
usikasirike rafiki yangu.Nina
imani huu ni mwanzo wetu mzuri
wa kufahamiana na baada ya
muda utanizoea na utafurahia
sana kuwa na mimi karibu.Kwa
sasa nakuomba taratibu jilaze
kitandani na tuendelee na
maongezi yetu.Pretend niko
pembeni yako tunaongea kama
marafiki wakubwa" akasema
Linah na kumfanya Mathew avute
pumzi ndefu..
“Sijawahi kukutana na mtoto
kama huyu" akawaza Mathew
“Mathew hukunijibu swali
langu nililokuuliza" akasema
Linah
" Swali gani Linah? akauliza
Mathew
“Nilikuuliza kwamba ukiwa
na hamu ya kufanya mapenzi na
mpenzi wako yuko mbali huwa
unafanya nini? Mathew akakata
simu kwa hasira
DAR ES SALAAM
Mathew Mulumbi aliwasili
Dar es salaam na kumkuta dereva
wake akimsubiri uwanja wa
ndege.Akampigia simu Linah na
kumfahamisha kuwa tayari
amekwisha fika Dar es salaam na
Linah akamuelekea mahala alipo
na Mathew akamuelekeza dereva
wake kulekea mahala
alikoelekeza Linah.
“Mathew Mulumbi ! akasema
Linah na kutabasamu baada ya
Mathew Mulumbi kufika katika
nyumba alikokuwa amejificha.
“Linah ! akasema Mathew na
wakatazamana kwa muda
“Nimefurahi kukuona tena
Mathew Mulumbi baada ya miaka
kumi na tano.Ahsante sana kwa
kukubali ombi langu la kuja
kuonana nami na samahani sana
kwa kukuharibia ratiba zako”
akasema Linah na kutikisa kichwa
chake kurudisha nyuma nywele
zake ndefu.Mathew hakujibu
akaendelea kumtazama
“Linah nimelazimika
kukatisha shughuli zangu muhimu
na kurejea Dar es salaam kwa
kuwa ni wewe.Tusipoteze muda
ingia garii tuondoke” akasema
Mathew na Linah akachukua
mizigo yake ikapakiwa garini na
safari ikaanza
“Mathew kuna sehemu
nataka unipeleke lakini nataka
twende mimi na wewe pekee
sihitajimtu mwingine wa tatu”
akasema Linah
“Huyu ni dereva wangu na
hana tatizo lolote”akasema
Mathew\
“I don’t need him ! akasema
Linah na Mathew akamtaka
dereva wake kusimamisha gari
katika hoteli moja akashuka kisha
yeye na Linah wakaendelea na
safari
“Ahsante sana Mathew”
akasema Linah huku akitoa
machozi
“Linah huu si wakati wa
kulia” akasema Mathew
akiendelea kukanyaga mafuta
“Katika maisha yangu
sikutegemea kama ningekutana
tena na Linah.Amekuwa mkubwa
na mrembo sana kinachoniumiza
kichwa nini kimemuingiza katika
masuala ya mauaji? Amepataje
namba yangu ya simu? Akajiuliza
Mathew
“Mathew nataka tupite katika
duka la madawa” akasema Linah
na safari ikaendelea hadi
walipofika katika duka kubwa la
madawa.Tayari kiza kilikwisha
ingia.Linah akachukua vitu
alivyovihitaji katika lile duka la
dawa Mathew akalipa
wakaondoka
Linah akamuelekeza Mathew
mahala anakotaka
waelekee.Wakaliacha gari katika
maegesho ya baa Fulani
wakapanda pikipiki hadi mahala
ambako Linah alielekeza halafu
wakaanza kutembea kwa miguu
na kushika njia ambayo Mathew
hakujua wanaelekea wapi.
Walitembea kimya kimya Linah
akiongoza njia na mara
wakajikuta wamefika katika
makaburi
“Tumefuata nini huku?
Mathew akauliza kwa mshangao
“Relax Mathew” akasema
Linah na kumuongoza Mathew
hadi katikati kabisa mwa eneo lile
la makaburi
“Kuna nini huku Linah?
Akauliza Mathew
“Mathew kuna kitu muhimu
nataka unisaidie kukifanya”
akasema Linah wakiwa juu ya
kaburi
“Mathew Mulumbi nafahamu
wewe ni jasiri hivyo nataka
utumie ujasiri wako
kunisaidia”akasema Linah
“Kitu gani unahitaji
nikusaidie? Akauliza
Mathew.Linah akamtaka asogee
karibu
“Unaiona hii pete kidoleni
kwangu? Akauliza Linah na
kumuonesha Mathew pete katika
kidole chake
“Ndiyo nimeiona”akajibu
Mathew
“Ninataka kuitoa pete hii
katika kidole changu lakini pete
hii haitoki kirahisi hivyo basi
ninataka unisaidie kukata hiki
kidole”
“Kukata kidole? Mathew
akashangaa
“Ndiyo Mathew ninataka
kukikata hiki kidole na usiniulize
sasa hivi kwa nini.Nitakueleza
sababu baadaye.Naomba
unisikilize vizuri” akasema Linah
na kumtazama Mathew kwa
makini
“Wakati wa kukiondoa kidole
hiki kuna mambo yatatokea”
akanyamaza na kumtazama
Mathew
“Mabadiliko gani? Akauliza
Mathew
“Nitabadilika na kuwa
kiumbe wa ajabu lakini pamoja na
mabadiliko hayo naomba
tafadhali usiogope wala kukimbia
hutadhurika.Endelea na zoezi la
kukata kidole usiache” akasema
Linah na Mathew akabaki
anamshangaa
“Mathew tusipoteze muda
zoezi lianze mara moja” akasema
Linah
“Who are you? Akauliza
Mathew
“Mathew ni mimi
Linah.Najua nimekustua kwa
haya niliyokwambia na ndiyo
maana nilikuchagua wewe kwani
ni mtu ambaye utaniamini na
kunisaidia.Let’s do this Mathew!
akasema Lina na kumpatia
Mathew mkasi,akakishika kidole
kilichokuwa na pete na kukibana
kwa mkasi.Mara tu ngozi ya
kidole ilipokatwa na damu
kutoka,ghafla ukasikika upepo
mkali na sauti ya
muungurumo.Mathew akageuka
kutazama pande zote lakini
hakuona kitu chochote aliingiwa
na hofu na mara akaanza kuhisi
mabadiliko katika mkono wa
Linah.Ngozi ilianza kuwa ngumu
na kucha zikabadilika.Linah
alikuwa anaunguruma kwa sauti
nzito ambayo ilimuogopesha
Mathew akamuachia Linah
akaruka pembeni akaanza
kushuhudia mabadiliko makubwa
yakitokea.Linah alikuwa
anabadilika na kuwa kiumbe cha
ajabu chenye umbo kama la
Mamba ambacho kilitoa sauti kali
ya kutisha.Kikapanua mdomo
wake na kuanza kumsogelea
Mathew ambaye alirudi nyuma
kujinusuru
“Kuna mabadiliko
yatatokea.Nitabadilika na kuwa
kiumbe mwingine lakini pamoja
na mabadiliko hayo naomba
tafadhali usiogope wala kukimbia
hutadhurika.Endelea na zoezi la
kukata kidole usiache”Mathew
akayakumbuka maneno ya Linah
“I need to help her ! akawaza
Mathew na kukunja ngumi
akasimama huku kiumbe kile cha
kuogofya kikiendelea
kumsogelea.Japo aliingiwa na
woga lakini hakukimbia na
kiumbe kile kikasimama huku
kikitoa muungurumo.
Mathew akapata ujasiri na
kukisogelea kile kiumbe akaanza
kupambana nacho akafanikiwa
kukiangusha chini.Lilitimka
vumbi kubwa lakini Mathew
aliendelea kuushikilia mkono
wake wa kulia na kufanikiwa
kukikata kile kidole
alichoelekezwa na Linah na mara
tu alipokikata kile kidole
kukatokea vumbi kubwa na
Mathew akapigwa kikumbo
akaanguka chini kama
furushi.Baada ya dakika chache
kukawa kimya na vumbi
lilipotulia Mathew akamuona
Linah akiwa amelala juu ya
kaburi
“Linah ! akaita Mathew na
kuinuka akamfuata.Linah alikuwa
anavuja damu kidoleni huku
akigugumia kwa maumivu
“Linah ! akasema Mathew na
kufungua mfuko wa dawa
waliokwenda nao akamtibu
jeraha.Linah akapata nguvu na
kuinuka akakaa akiweweseka
“Mathew ahsante sana
tunatakiwa kukitafuta kile kidole
chenye pete ulichokikata”
akasema Linah na Mathew
akawasha tochi yake ya simu
wakaanza kukitafuta kidole kile
na wakafanikiwa kukipata kikiwa
kimeanguka pembeni kidogo ya
mahala walipokuwa.Linah
akamuelekeza Mathew
kukichukua kidole kile
akakifunga katika kitambaa
cheupe akatafuta kaburi jipya
akachimba shimo katikati na
kukifukia
“Kazi imemalizika tunaweza
kuondoka” akasema Linah
wakaanza kuondoka mahala pale
huku bado Mathew akiendelea
kumshangaa Linah
“Ama kweli dunia ina
maajabu.Kitu gani kile
kimetokea? Huyu ni Linah Yule
ninayemfahamu au ni kiumbe cha
aina gani? Akajiuliza maswali
akiendelea kumfuata Linah
wakafika katika kituo cha basi
wakachukua piki piki mbili hadi
katika baa walikoacha gari lao
wakaingia na kabla ya Mathew
kuliwasha akaegemea kiti na
kuvuta pumzi ndefu akamtazama
Linah
“Drive ! akasema Linah
“Who are you? Akauliza
Mathew
“Mathew just drive !
akasema Lina na Mathew
akawasha gari wakaondoka
“Kama kweli huyu ndiye
Linah niliyekutana naye Arusha
kitu gani kimemtokea na
kuyabadili maisha yake na kuwa
namna hii? Niliyoyashuhudia ni
mambo ya kutisha sana ambayo
hayasimuliki.Mimi ni jasiri sana
lakini katika muda wote
niliofanya kazi hii ya ujasusi
sijawahi kukutana na mambo ya
kutisha kama haya niliyokutana
nayo muda mfupi uliopita”
akawaza Mathew
**********
Walifika nyumbani kwa
Mathew,akamganga Linah jeraha
lake halafu akampeleka katika
chumba cha wageni kwa ajili ya
kupumzika.Mathew akaingia
chumbani kwake na kujitupa
kitandani
“Mambo niliyoyashuhudia
leo,nilikuwa nikiyatazama katika
filamu na sikujua kama siku moja
ningeweza kuyashuhudia kwa
macho yangu.Huyu kweli ni
Linah Yule ninayemfahamu au ni
kiumbe amechukua umbo lake na
anataka kucheza na akili yangu?
Akajiuliza Mathew na kuinuka
akaenda kuchukua chupa ya maji
akanywa
Alihakikisha kamera zote za
usalama alizozifunga nyumbani
kwake zinafanya kazi vyema
kisha akaenda jikoni kuandaa
chakula.Baada ya kuandaa
chakula Mathew akaenda katika
chumba alimolala Linah taratibu
akaufungua mlango na
kuchungulia ndani bado Linah
alikuwa amelala.
“Who are you? Akajiuliza
Mathew akimtazama Linah na
kutaka kuufunga mlango mara
akasikia Linah akikohoa halafu
akasema
“Come in Mathew” akasema
Linah
“Ouh kumbe umekwisha
amka.Unajisikiaje sasa hivi?
Mathew akauliza na kuingia ndani
“Nina maumivu lakini
nitapona.Ahsante sana Mathew”
akajibu Linah na Mathew
akamtaka wakapate
chakula,Linah akainuka
wakaenda katika chumba cha
chakula wakapata chakula kimya
kimya.Mathew hakutaka kugusia
chochote kuhusu kile kilichotokea
kule makaburini.Alikuwa
anamtazama Linah kwa kuibia
“Mathew nimefurahi sana
kukuona tena baada ya miaka
kumi na tano” Linah akaanzisha
mazungumzo baada ya kuona
kumekuwa kimya sana.
“Ni muda mrefu sana huo na
mengi yametokea” akasema
Mathew na kuendelea kula
taratibu
Baada ya kumaliza kupata
chakula Mathew akamchukua
Linah wakaenda kuketi sehemu
ya juu ya nyumba yake ambako ni
maalum kwa kupumzikia.
“Linah it’s time to talk!
Akasema Mathew
“Mathew kabla ya kukueleza
chochote kwanza nataka
nikushukuru sana kwa kile
ulichokifanya.Sikufanya makosa
kukuchagua wewe na kweli
umenifanyia jambo kubwa sana
ambalo wengine wasingeweza”
akasema Linah
“Nahitaji kufahamu kila kitu
Linah.Mambo niliyoyashuhudia
kwa macho yangu leo yamenipa
hofu na nimekuwa najiuliza
maswali mengi bila majibu je
wewe ni Yule Linah niliyekutana
naye miaka kumi na tano iliyopita
au ni kiumbe amevaa mwili wa
Linah na kutaka kuiteka akili
yangu? Akauliza Mathew
“Mathew I’m
sorry.Nafahamu kilichotokea
kimekupa hofu kubwa sana lakini
mimi ni Linah Yule Yule
unayenifahamu japo maisha
yangu yamekuwa na mabadiliko
makubwa sana na nitakueleza kila
kitu” akasema Linah
“Kabla hujanieleza chochote
nataka kwanza unieleze ukweli
kuhusu mtu ambaye umemuua.Ni
kweli umeua?Nieleze ukweli bila
kunificha” akasema Mathew
“Ni kweli nimeua Mathew”
akasema Linah na kumtazama
Mathew
“Umemuua nani na kwa nini?
Mathew akauliza
“His name was Genes.He
was a nice guy and I loved him so
much.They forced me to kill him
! akasema Linah na kuinamisha
kichwa baada ya muda
akaendelea
“Jambo hili limeniumiza sana
na ndiyo maana ninataka niweke
nukta katika maisha haya.I’m
tired and I can’t do it anymore”
akasema Linah na kuanza
kumwaga machozi.Mathew
akampa kitambaa afute machozi
“Linah naomba unieleze
kuhusu maisha yako kwa miaka
kumi na tano tangu nilipokuacha
wakati ule hadi leo hii” akasema
Mathew.Linah akafikiri kwa
muda na kusema
“Ni mambo mengi
yametokea Mathew Mulumbi
siwezi kukueleza usiku huu
nikayamaliza.Nimepitia mambo
makubwa sana katika kipindi
hiki” akasema Linah
“Nieleze tafadhali” akasema
Mathew na Linah akanywa
mvinyo na kusema
“Nilitegemea safari hii
ningeweza kuyabadili maisha
yangu na kujaribu kuingia katika
mahusiano na mwanaume
niliyempenda kumbe nilikuwa
najidanganya” akasema Linah na
kunyamaza kidogo halafu
akaanza kumueleza Mathew
kuhusu kile kilichotokea
MWAKA 1 ULIOPITA
NDUGUMSOMAJI MAMBO
YAMEANZA TENA,
MATHEW MULUMBI USO
KWA USO NA THE RED
MAMBAZ.
ATAFAULU KUMUOKOA
LINAH ASIUAWE?
ATAFANIKIWA KUMUOKOA
HAPPY NA WANAKWAYA
WENZAKE WASIUAWE ?
ENDELEA KUFUATLIA
SIMULIZI HII