You are on page 1of 10

HALI NA NYAKATI MBALIMBALI

MARANDA- BUNYORE 2013

Tambua na eefeze hali zinazojitokeza katika sentensi ulizopewa.(AIama 2)


i) Ukichelewa hutanipata
ii) Kalale mtoto wewe!
hali ya KI- masharti 'A / hu- Ukanushi 'A
hali ya Ka - amri Vi
KIBWEZI 2013

Sentensi zinaweza kuwa katika hali tatu. Kwa kila sentensi andika hali zilizokosekana.
( alama 4)
(i) Goma lililotumiwa katika sherehe zile ni zuri.
(ii) Mwizi aliyeiba alipatikana amejificha kando ya mto.

Ngoma iliyotumiwa katika sherehe zile ni nzuri


Kigoma kilichotumiwa katika sherehe zile ni kizuri.
- Jizi lililoiba lilipatikana limejificha kando ya jito.
- Kijizi kilichoiba kilipatikana kimejificha kando ya kijito.

MATUNGULU 2013

Tunga sentensi moja yenye kuonyesha hali isiyodhihirika. (alama 2 )

- Atoa maagizo tena.


- Chakula chote chaliwa 2 x 1 = 2

LAIKIPIA 2013

Andika sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu: (alama 1)


Lugha ya kiswahili ilienea Afrika kote.

Lugha ya kiswahili itakuwa imeenea Africa kote. (alama 2)

RABAI 2013
Tambua ni hali gani inayowasilishwa katika sentensi hii.
Osama auawa.
Hali isiyodhihirika (hali ya a). alama 1
RABAI 2013
Bebora alinunua pikipiki.
bebora atakuwa amenunua pikipiki (alama 2)

KIHARU 2013

Tofautisha kati ya: (alama 2)


(i) Ungesoma kwa bidii ungepita mtihani.
(ii) Ungalisoma kwa bidii ungalipita mtihani.

(i) Ungesoma kwa bidii ungepita – Kuna uwezekano kuwa akisoma


kwa bidii atapit
(ii) Hakuna uwezekano. Muda umepita na kitendo hakiwezekani. (2 x 1) = 2
SUBUKIA 2013

Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ‘a’ (alama 1)


Shule yetu imepokea walimu wengi
. Shule yetu yapokea walimu wengi al 1

NANDI YA KATI 2013

Andika sentensi ifuatayo katika hali ya -a- (alama 1)


Kibofu hupaa angani.

Kibofu chapaa angani. √1


Ondoa nusu ya alama kwa kila kosa la sarufi na hijai.

NANDI KUSINI- TINDIRET 2013

Tunga sentensi katika wakati usiodhihirika. (alama 1)


Mf Mwalimu afunza Kiswahili. (alama 1)

NANDI KUSINI –TINDIRET 2013

Eleza tofauti baina ya sentensi hii. (alama 2)


Ningekuwa na pesa ningenunua gari.
Ningalikuwa na pesa ningalinunua gari.
Kuna uwezekano – Nge
Hakuna uwezekano – Ngeli (alama 1 kwa nge, 1 kwa ngeli).
KASSU 2013
Andika katika hali ya mazoea: (alama 2)
Mtambo ambao unakarabatiwa leo utatufaa
Mtambo hukarabatiwao hutufaa

SUPAJET 2013

Eleza hali katika sentensi zifuatazo:- (al 1)


Anasimama akaimbe.
Wakulima wapanda ngano.
(i) Mfululizo wa kitenzi wakati uliopo. (al 1)
(ii) Hali isiyodhihirika. (al 1)

KCSE 2012

Tunga sentensi moja katika wakati uliopita hali timilifu (alama 2)


Watoto walikuwa wameketi ilipoanza kunyesha.
Maisha yalikuwa yamemwendea vyema 1x2=2

NANDI KATI 2012


Tofautisha matumizi ya ngali katika sentensi zifuatazo. (alama 2)
(i) Mueniangalianasoma (ii) Kerich angalisoma angalipata kazi:
(i) Hali ya kuendelea / kitenzi kishirikisha kikamilifu.
(ii) Kutowezekana / hamna matumaini. (2 x 1 = alama 2)

KISUMU KASKAZINI 2012

Tofautisha matumizi ya ngali katika sentensi zifuatazo. (alama 2)


i) Mueni angali anasoma.

ii) Kerich angalisoma angalipata kazi.

i) Mueni angali anasoma


- Hali ya kuendelea.
ii) Kerich angalisoma angalipata kazi
- Kutowezekana kwa kitendo
- Wakati uliopita.

KWANZA 2012
Iweke sentensi ifuatayo katika wakati uliopita hali timilifu. (Alama 1)
Aliomba msamaha kwa kuchelewa.
Alikuwa ameomba msamaha kwa kuchelewa. 1x1=1

BURETI 2012
Andika sentensi ifuatayo katika mazoea.
Ua linalomea vizuri linietiwa rnbolea. (ala.1)
Ua limealo vizuri limetiwa mbolea/huwa limetiwa mbolea

KISII KUSINI 2012


Andika sentensi ifuatayo iwe katika hali ya -ki- ya masharti (ala 2)
Tulilala sana tukachelewa kwenda shuleni.
Tukilala sana tutachelewa kwenda shuleni. 1×2 = 2

MBOONI MAGHARIBI 2012

Tambua wakati uliotumika katika sentensi zifuatazo.


(i) Mwanafunzi ameenda nyumbani. (alama1)
(ii) Sisi twala wali. (alama1)
(i) Wakati timilifu / wakati uliopita si muda mrefu.
(ii) Wakati usiodhihirika Alama 2

KURIA MASHARIKI 2012

Andika sentensi ifuatayo upya ukizingatia maagizo uliyopewa. (alama 2)


Wakulima wala kwa pupa nchini Kenya. (Geuza katika wakati ujao hali timilifu)
Wakulima watakuwa wamekula kwa pupa nchini Kenya. (alama 2)

KILUNGU 2012

Andika kwa wakati ujao hali timilifu. (alama1)


Wizi ulikwisha na usalama ukarudi
Wizi utakuwa umekwisha na usalama utakuwa umerudi.

EMBU 2012

Tambua wakati nahali katika sentensi ifuatayo:Ali amekuwa akisomatangu asubuhi (alama 2)
i) wakati - uliopita
ii) hali – timilifu (alama 2 x 1 = 2)
KASSU 2012

Tunga sentensi ukitumia vibadala vya hali na wakati uliyopewa kwa mabano. (al 2)

(a) (-takuwa - , - me - )
(b) (- takuwa -, - ki -)

(a) Mwaka ujao mitihani itakuwa imekwisha


- takuwa -, - ki – (wakati ujao timilifu)

(b) Akarani atakuwa akiandika


- takuwa, - ki – (wakati ujao hali ya kuendelea)

Kassu 2012
Bainisha nyakati na hali katika sentensi hizi (alama 3)
Walimwomba awasamehe.
Yule angekuwa mwalimu.
Nyakati – li
Hali – nge
Wakati- a- usiodhihirika. (alama 3)

MBITA- SUBA 2012

Tumia kitenzi ‘vuka’ kutunga sentensi katika hali ya kuamrisha. (alm1)


Vukeni barabara!
Usivuke mpaka huu!

MBITA- SUBA 2012


Andika sentensi katika hali isyodhihirika. (alm1)
Aliimba akioga.
Aimba akioga

KITUI MAGHARIBI 2011


Tambulisha nyakati na hali katika sentensi .
Wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi. (Alama 2)
Wakati uliopita ,hali ya kuendelea (al 2 )
Mumias 2011
Andika sentensi ifuatayo kwa udogo.
Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kiafya. (alama.2)
Kijitu kile hakiachi kuandamana na kijibwa chake kilichodhoofika kiafya
Mutomo 2011
Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa -amba (alama 2)
Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia
Mtoto alaye ndiye aliaye ( Alama 2)
Nyamira 2011
Tunga sentensi sahihi ukitumia – la- katika hali timilifu. ( ala. 2)
Tumia – Amekula (al. 2)

Sotik 2011
Tambulisha nyakati au hali za sentensi zifuatazo. (al.2)
(i) Naja
(ii) Nilikuwa nimeketi alipotembelea
(i) Wakati uliopo
(ii) Waakti uliopita hali timilifu (2x1=al. 2)

BARINGO 2013
Tunga sentensi kubainisha nyakati na hali zifuatazo.
(i) Masharti yasiyowezekana
(ii) Wakati uliopita hali ya kukanusha (alama 2)
Masharti yasiyowezekana – Ningalikuwa na pesa ningalinunua gari. (alama 2)
SIAYA UGENYA 2009

Tambua nyakati katika sentensi hizi,


(i) Nichezapo kandanda watu hunishangilia.
1x1 = 1
(ii) -Ninapocheza kandanda watu hunishangilia.
- Wakati wowote.
- wakati maalum

MSURURU WA TOP STUDENT 2009


Geuza sentensi zifuatazo katika hali ya mazoea:
(i) Mtoto unavyomlea ndivyo anavyokuwa. (alama 2)
(ii) Matunda yanayoiva ndiyo yanayotundwa. (alama 2)
(i) Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. (alama 2)
(ii) Matunda yaivayo ndiyo yatundwayo. (alama 2)
KCSE 2006
Onyesha hali katika sentensi zifuatazo:
i) Henda mvua ikanyesha leo. (alama 1)
ii) Miti hukatwa kila siku duniani. (alama 1)
(i) Uwezekano/ haliya kutenda
(ii) Mazoea/ hali ya kutendwa
Wakati Uliopita => LI
Hutumia kiambishi 'LI' na hurejelea kitendo kilichokamilika muda mrefu uliopita.
Ifuatayo ni mifano katika sentensi.
k.m: nilikwenda, tulilima, walikufukuza
1 Mama ataenda sokoni Mama alienda sokoni
2 Ndoto hiyo imenisumbua usiku kucha Ndoto hiyo ilinisumbua usiku kucha
Wakati Timilifu (Uliopita Muda Mfupi) => ME
Hutumia kiambishi 'ME' na hurejelea kitendo ambacho kimekamilika muda usio mrefu.
k.m: amepona, nimewachagua, zimechanganyika
1 Tutauona wema wake Bwana Mungu. Tumeuona wema wake Mungu wetu.
2 Dada yake alipagawa Dada yake amepagawa
Wakati Uliopo => NA
Hutumia kiambishi 'NA' kurejelea jambo linalotendeka sasa hivi.
k.m: anaugua, yanametameta, unatisha
1 Nilikupenda kwa yale uliyonitendea Ninakupenda kwa yale unayonitendea.
2 Nyumba zote zilibomolewa mwaka jana Nyumba zote zinabomelewa mwaka huu
Wakati Ujao => TA
Huchukua kiambishi 'TA' na hurejelea kitendo ambacho bado hakijafanyika lakini
kinatarajiwa kufanyika..
k.m: atakupa, kitajulikana, utapokelewa
Mtoto amelifunga dirisha lililokuwa Mtoto atalifunga dirisha litakalokuwa
1
likiingiza hewa likiingiza hewa.
2 Je, ulienda sokoni juzi? Je, utaenda sokoni kesho kutwa?
Wakati wa Mazoea => HU
Hutumia kiambishi 'HU' na hurejelea kitendo ambacho hufanyika mara kwa mara au kila
siku n.k.
k.m: hutembea, husoma, huzilinda
1 Dkt. Matumbo alitibu wagonjwa. Dkt. Matumbo hutibu wagonjwa.
2 Mchungwa ule ulizaa machungwa matamu. Mchungwa ule huzaa machungwa matamu.
Wakati Usiodhihirika => A
Hutumia kiambishi cha ngeli au nafsi pamoja na kiungo 'A' kurejelea kitendo kinachoendelea
kutendeka katika wakati usiodhihirika.
k.m: achukua, zapepea, twaangamia
1 Baba alitusubiri nyumbani. Baba atusubiri nyumbani.
2 Vitabu vyako vyote vimechomeka Vitabu vyako vyote vyachomeka
Wakati Timilifu Usiodhihirika => KA
Hutumia kiungo 'KA' kurejelea kitendo ambacho kinakamilika katika wakati usiojulika. Pia
hutumika kurejelea kitendo kifanyika baada ya kingine. Hutumiwa katika masimulizi.
k.m: ikawalemea, tukazichukua, likampendeza
Latifa aliangalia mvunguni na kumwona
1 Latifa akaangalia juu akamwona nyoka.
nyoka..
2 Aliwanyeshea mana wakiwa jangwani. Akawanyeshea mana wakiwa jangwani

You might also like