Professional Documents
Culture Documents
Sababu Za Kufichwa Kwa Kitabu Cha Enoch - JamiiForums
Sababu Za Kufichwa Kwa Kitabu Cha Enoch - JamiiForums
Log in Register
1 of 14 Next
Apr 2, 2021 #1
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73
iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa
Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia
lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi"
lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.
Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa
Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni
Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa
mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na
Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita
Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao
zimo.
Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa
Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini
kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama
Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI
au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo
wataalamu husema ni siri.
Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu
JamiiForums uses cookies
mweupe alipata to helpPia
wapi Ujuzi, personalise
huonyeshacontent, tailorcha
Chanzo yourMapepo
experience
naand to keep you logged in if
Wanefili.
you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti
wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna
Accept
malaika
Learn more…
kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 1/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa
wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie
tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika
wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa
kutekeleza. (Henoko 7:3-6)
Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa
katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL,
DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL,
TUREL, JOMJAEL, SARIEL.
Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu
Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA
WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio
maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha
malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6
unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa
nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni
lazima waliyaacha makao yao...
Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na
SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia
hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu
Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations"
Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba
(pharmacology).
Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa
Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka
Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na
Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.
Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza
kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani
(BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI
akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.
Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia
hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia
wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo
Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza
Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 2/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio
wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda
Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona
wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini
ya Giza wakingojea hukumu.
Lakini Mungu anajua Zaidi (An omniscient) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua
Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na
Kubakiza Wanadamu 8 tu.
keisangora
JF-Expert Member
Apr 2, 2021 #2
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 3/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
plan z
JF-Expert Member
Apr 2, 2021 #3
Hebu naomba hicho kitabu kama unacho nikisome mwenyewe. Tuma pdf yake humu
Apr 2, 2021 #4
plan z said:
Hebu naomba hicho kitabu kama unacho nikisome mwenyewe. Tuma pdf yake humu
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 4/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
mikogo mia
M Member
Apr 2, 2021 #5
plan z said:
Hebu naomba hicho kitabu kama unacho nikisome mwenyewe. Tuma pdf yake humu
Bora hivyo
Icho hapo
Anigrain
Sent using Jamii Forums mobile app
JF-Expert Member
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 5/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Apr 2, 2021 #6
"Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na
malaika duniani" kwahiyo unataka kusema bila malaika kumwambia Mungu asingejua
matendo ya hao malaika?
"Lakini Mungu anajua Zaidi (AN OMNISCIENT) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua
Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na
Kubakiza Wanadamu 8 tu"
Kupitia hizo paragraph 2 inaonekana kama kuna ukomo wa kuona au kujua mambo Kwa
Mungu, kama anajua zaidi hadi akafuta kizazi cha Nuhu nazani lengo lilikuwa ni kuondoa
kizazi kiovu cha Nuhu na kuleta kizazi kizuri Ila cha ajabu hiki kizazi ndio kibaya kuliko ata
cha Nuhu hivo sidhani kama alijua na hiki kizazi kitakuwa hivi
Kuendelea kumuacha shetani uraiani ili binadamu apambane nae mwenyewe ni Sawa na
kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe, kama Baba huwezi kuwatakia mema
watoto wako Kwa kuwaweka chumba kimoja na Nyoka, kuendelea kutuweka zizi moja na
shetani na kutegemea tutakuwa tofauti na kina Nuhu inabidi uwe na akili za Wanyonge
kuamini hili, Kamata shetani funga huko dunia iwe sehemu salama easy tu
Surya
JF-Expert Member
Apr 2, 2021 #7
Maandiko ya Biblia yanajitosheleza kabisa, na ndio Mungu kataka tusome hayo tu.
Nje na hapo hakuna hekima tena, labda ukajifunze uchawi tu huko nje ya biblia.
kopites
JF-Expert Member
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 6/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Apr 2, 2021 #8
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa
mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g
(Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano
Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakinj ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu
nyingi....
Nimekisoma chote hicho kitabu kina siri nyingi sana ambazo hazijulikani
ancillary
JF-Expert Member
Apr 2, 2021 #9
Amigoh
JF-Expert Member
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa
mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g
(Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 7/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakinj ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu
nyingi...
Niliwahi kupata dokezo kidogo wa hiki kitabu kupitia jarida moja la mashahidi wa yehova..
itabidi nikitafute nikipitie aisee.
mtu chake, MUME MASKINI and crusader_jr
Kimwakaleli
K JF-Expert Member
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa
mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g
(Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano
Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakinj ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu
nyingi....
Lupweko
JF-Expert Member
Ndio maana ya imani. Huwezi kulazimisha watu wengine waamini katika maandiko fulani,
lakini inawezekana kwako wewe kuamini maandiko hayo. Kama ni kweli unayoyasema,
basi RC waliona hayo maandiko hayaendani na imani yao.
Lakini RC hawajamzuia mtu kuyaamini. Cha ajabu watu wanataka wengine waamini
imani fulani wakati wapo huru kuifuata, na hata katiba za nchi nyingi zinaruhusu tu
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 8/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Shadow7
JF-Expert Member
Ahsante
zitto junior
JF-Expert Member
Surya said:
Maandiko ya Biblia yanajitosheleza kabisa, na ndio Mungu kataka tusome hayo tu.
Nje na hapo hakuna hekima tena, labda ukajifunze uchawi tu huko nje ya biblia.
Hiko kitabu kinatumika na Ethiopian Orthodox ambalo ndio kanisa la Kwanza Afrika hata
kabla RC haijafikiriwa kuanza.
Je unaona nani yupo sahihi hapo? Au inakua halali pale tu mzungu akikiweka kwenye
biblia?
Mfano Wimbo ulio bora una changamoto zote kma book of Enoch ila hakijatolewa and
more so hta makanisani hakifundishwi regularly!! But kingekua nje ya Biblia kama naona
jinsi mngekikejeli.
Surya
JF-Expert Member
Hiko kitabu kinatumika na Ethiopian Orthodox ambalo ndio kanisa la Kwanza Afrika hata kabla RC
haijafikiriwa kuanza.
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 9/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Je unaona nani yupo sahihi hapo? Au inakua halali pale tu mzungu akikiweka kwenye biblia?
Mfano Wimbo ulio bora una changamoto zote kma book of Enoch ila hakijatolewa and more so hta
makanisani hakifundishwi regularly!! But kingekua nje ya Biblia kama naona jinsi mngekikejeli
Mimi naujua umuhimu wa agano la kale na muhubiri anatakiwa kulitumia vipi agano la
kale kufundisha neno la Mungu,
Agano jipya pia.
Sasa kama kuna kitu cha muhimu mwanadamu kukijua na hakipo ndani ya biblia kiseme.
Kwasababu biblia inasema laiti kama biblia ingeandika kila alilolifanya Yesu kipindi chake
isinge wezekana ?
Yohana 21:25
[25]Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani
hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
zitto junior
JF-Expert Member
Surya said:
Mimi naujua umuhimu wa agano la kale na muhubiri anatakiwa kulitumia vipi agano la kale
kufundisha neno la Mungu,
Agano jipya pia.
Sasa kama kuna kitu cha muhimu mwanadamu kukijua na hakipo ndani ya biblia kiseme.
Kasome Yuda 6 na 14-15 alafu uniambie ilikua quoted kutoka kitabu gani cha agano la
kale then ukifaham naomba ukaulize kwanini mitume walikisoma alafu sisi tukataliwe?
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 10/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Surya
JF-Expert Member
Kasome Yuda 6 na 14-15 alafu uniambie ilikua quoted kutoka kitabu gani cha agano la kale then
ukifaham naomba ukaulize kwanini mitume walikisoma alafu sisi tukataliwe?
Nikasome wapi. ?
zitto junior
JF-Expert Member
Surya said:
Nikasome wapi. ?
Agano jipya.... Yuda mstari wa 6 na 14-15 then unipe mrejesho kuendana na nlichouliza
hapo juu
Surya
JF-Expert Member
Agano jipya.... Yuda mstari wa 6 na 14-15 then unipe mrejesho kuendana na nlichouliza hapo juu
Lakini point yangu itabaki pale pale, ni mafundisho yapi ya Henoko unayoyalilia wewe
ukitaka yawekwe kwenye biblia.
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 11/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Manabii wa zamani walitoa unabii kuwaonya watu wa kipindi kile, si henoko peke yake
alifanya hivo, wapo manabii wengi tu.
Lakini swali linakuja wewe uliyesoma kitabu cha henoko unanizidi nini mimi ambae
sijakisoma. ?
Surya
JF-Expert Member
Agano jipya.... Yuda mstari wa 6 na 14-15 then unipe mrejesho kuendana na nlichouliza hapo juu
Similar Discussions
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 12/13
1/5/23, 11:09 AM Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch | JamiiForums
Jamii Intelligence
Amka Muafrika
Started by Mtuache · Oct 6, 2022 · Replies: 18
Jamii Intelligence
Share:
https://www.jamiiforums.com/threads/sababu-za-kufichwa-kwa-kitabu-cha-enoch.1854578/ 13/13